JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................453-454
Sura ya: 453
Mara baada ya Logan kupelekwa kituo cha polisi, angelazwa kwa matibabu na kuhojiwa tena kulingana na utaratibu wa kawaida. Si hivyo tu, angekuwa mikononi mwa polisi, hivyo Alvin asingeweza kumfundisha Logan somo.
“Nitatoa ripoti kwa polisi pia." Alvin akashuka ngazi huku akimuelekezea Lisa. “Mwanamke huyu alimteka nyara mtoto wa ndugu yangu na anakusudia kumuumiza. Tafadhali chunguza suala hili mara moja.”
"Sawa, Bi Jones na Bw. Kimaro, tafadhali tufuateni hadi kituo cha polisi," polisi walisema. Kisha, Logan alipelekwa hospitalini kwa gari la wagonjwa.
Lisa alikaa kwenye gari la polisi huku Alvin akifuata nyuma kwa Sedan iliyopangwa na ONA.
Muda si mrefu baada ya kufika kituo cha polisi, Jack alimleta Suzie.
“Habari, Bwana Polisi,” Suzie aliwasalimia polisi kwa furaha mara tu alipoingia.
"Halo, mpenzi mdogo." Polisi alikandamiza mashavu ya Suzie kwa upole.
Alvin alimtazama Jack kwa uchungu. "Nini kimetokea? Kwanini Suzie yuko na wewe? Yuko wapi yule mtu aliyekuwa naye?”
“Unamaanisha Austin? Alikuwa anacheza na Suzie sasa hivi.” Jack akajifanya kama amechanganyikiwa.
Polisi walimtazama Alvin kwa mshangao. "“Bwana Kimaro, si ulisema kuna mtoto alitekwa nyara?” Polisi walihoji.
Jack akamuuliza Alvin, “kaka, kwanini ulisema kuwa Suzie alitekwa nyara?”
“Jack, ulikula njama na Lisa ili kunidanganya! ” Alvin alipandwa na hasira. Akashika kola ya Jack. “Mtu kama wewe anastahili kweli hata kuwa babake Suzie?”
"Anti Lisa, nini kimetokea kwenye paji la uso wako?" Sauti ya Suzie ilisikika. Alikimbia kuelekea kwa Lisa na akawa anatokwa na machozi kwa kuona paji la uso wake.
“Niliumia nilipoanguka chini kimakosa." Lisa alinyoosha mikono, akitaka kumbeba Suzie, lakini, Alvin alimuwahi haraka na kumbeba kwanza. “Huna haki ya kumbeba. Potelea mbali!”
Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Suzie kumuona Alvin akiwa na hasira sana. Alikuwa katika butwaa kutokana na mshtuko. Kisha, akaanza kulia kwa sauti kubwa. “Sipendi unamkasirikia sana Aunty
Lisa! Unatisha sana. Sitakupenda tena.”
“Suzie, huelewi. ” Alvin aliposikia kilio cha mtoto, moyo wake ulikuwa karibu kutoka kwa maumivu.
“Najua! Wewe ndiye uliyemuumiza Aunty Lisa usoni, sivyo? Wewe ni mkatili sana. Nenda zako!” Suzie aliendelea kupiga mabega yake.
Jack alipoona sura mbaya ya Alvin, aliingiwa na wasiwasi kuwa Alvin angeweza kumuumiza Suzie. Hapo hapo akamtoa Suzie kwenye kumbato la Alvin.
“Baba tuondoke na Aunty Lisa. ” Suzie aliufungua mkono wake mmoja ili kumshika Lisa.
"Sawa, twende." Lisa akakipapasa kichwa cha Suzie. Kisha akaondoka kituo cha polisi na Jack.
Alvin akawatazama kwa nyuma. Walikuwa kama familia ya watu watatu.
Moyo wake ulikuwa ukimuuma hadi kumziba. Kwanini Suzie hakumuelewa? Alitaka kumwokoa, lakini hakuweza kutambua wema wake na akasema hatampenda tena. Hah! Ilionekana kuwa kila mtu hakumpenda. Lisa pia alikuwa ameuliza kwanini hakufungiwa katika hospitali ya magonjwa ya akili na kwanini hakuwa amekufa.
Je, alikuwa anachukiwa kiasi hicho?
Wimbi la uhasama lilizidi kumpanda. Alionekana kama volkano ambayo ilikuwa karibu kulipuka. Hakuna aliyethubutu kumsogelea.
Ndani ya gari, Suzie alilala kwenye kumbato la Lisa. Machozi yalimtoka. “Mama, inauma sana? Simpendi tena baba mchafu. Usiwe pamoja naye tena.”
“Ni sawa. Sijambo.” Lisa akagusa kichwa cha Suzie. “Suzie, umefanya kazi nzuri leo. Samahani kwa kukutumia.” Ikiwa angeweza, hakutaka watoto wake waone mambo machafu kama hayo.
“Ni sawa, ulifanya hivyo tu ili kumwokoa Anko Logan. Isitoshe, Anko Austin aliendelea kunitunza,” Suzie alinong’ona.
“Nenda ukacheze na Anko Jack baadaye. Bado nahitaji kutafuta ushahidi kuthibitisha kuwa Anko Logan hana hatia.” Lisa akambusu paji la uso la Suzie. “Nitakutafuta baada ya kumaliza kazi yangu, sawa? Mm, Suzie atakuwa msichana mzuri."
“Unahitaji msaada?” Jack aliuliza.
“Hapana, nahitaji tu unisaidie kumtunza vizuri Suzie.” Lisa akatikisa kichwa. Jambo hilo lilikuwa gumu sana. Aliogopa kwamba jambo lingetokea kwa Jack pia.
"Ni kosa langu kwa kutokuwa na maana." Jack alitabasamu kwa uchungu.
“Usiseme hivyo. Nadhani una akili sana, angalau ukilinganisha na kaka yako,” Lisa alisema kwa dhati.
“Una hoja hapo. Kwa kweli sielewi jinsi Sarah alivyomroga.” Jack akahema.
Baada ya kuachana na Jack, Lisa aliwasiliana haraka na Austin. Alimtaka Austin aende kufanya uchunguzi kwenye pango ambalo kisa hicho kilitokea. Wakati akienda huko, alipita kwenye nyumba aliyokaa Logan aliposhambuliwa.
Alipofika, aliangalia picha za usalama za nyumba hiyo. Aligundua kuwa rekodi ya mtu anayesafirisha chakula akimpelekea Logan chakula chake cha jioni ilifutwa. Hakukuwa na picha kabisa kutoka saa mbili hadi saa mbili na nusu usiku.
Alitafuta picha za usalama katika maeneo ya karibu pia lakini hakukuwa na chochote. Hatimaye, ilibidi aelekeze mawazo yake kwenye dashibodi za magari yaliyoegeshwa chini…
•••
Siku iliyofuata katika kampuni ya KIM International.
Ofisini, Alvin alikuwa akisikiliza taarifa za wasimamizi waandamizi huku akionyesha giza totoro. Hakuwa amefika kwenye kampuni hiyo kwa siku chache. Kulikuwa na mambo mengi ambayo wasimamizi wakuu walipaswa kuripoti kwake.
Hata hivyo, walikuwa wameanza kuripoti ndipo mlango wa ofisi hiyo ulipopigwa teke. Jack aliingia kwa hasira. “Alvin unamaanisha nini kusema hivyo? Unaniagiza niende Uganda kujenga kiwanda cha cement na nisirudi kabla hakijakamilika? Unatumia vibaya uwezo wako kunikomoa. Unatumia njia kama hizi za kijinga kila wakati ninapokukasirisha. Unajua wazi kuwa siwezi kuondoka Nairobi kwa muda mrefu sana. Suzie anahitaji uangalizi wangu.”
"Mwenyekiti ... Mwenyekiti Kimaro, tutarudi baadaye." Wasimamizi wakuu walihisi kuwa kuna kitu kibaya katika hali hiyo. Walitoka nje kwa haraka huku wakiwa wameinamisha vichwa chini.
Walibaki Alvin na Jack tu kwenye ofisi kubwa.
Alvin aliikunja mikono yake kifuani. Alikuwa hana cha kujieleza. “Hustahili kuwa babake Suzie.”
“Kama sistahili, ni nani sasa awe baba yake!” Jack alicheka kwa hasira. Akasema, "Kila mtu ana haki ya kusema hivyo isipokuwa wewe."
Alvin alikodoa macho. Alimuuliza Jack kwa ukali, "Unamaanisha nini kwa hilo?"
Moyo wa Jack ulirukaruka, akasema kwa hasira. "Ikiwa una haki, kwanini mapacha wako walipotea wakati huo?"
“Thubutu kusema hivyo tena.” Alvin alisimama ghafla. Sauti na macho yake yalionekana ya kutisha kabisa.
Jack alihisi hofu ikimpiga moyoni. Alihisi kwamba Alvin alikuwa akitoa harufu ya umwagaji damu, kama mwendawazimu. Na muda wowote kingenuka!
Jack alikunja ngumi na kusema bila kuridhika, “Siwezi kuondoka sasa. Suzie ni mdogo sana. Unaweza kuagiza watu wengine kufanya hivi…”
“Kuna watu wengi wa kumtunza Suzie. Isitoshe, uko karibu sana na mwanamke huyo katili, Lisa. Sina imani kama unafaa kumlea Suzie. Ni shaka huenda kutakuwa na siku nyingine Suzie atakapokuwa mateka tena. Yeye ni mchanga na hajui chochote. Wewe ni baba yake, lakini uliungana mkono na mtu mwingine na kumtumia Suzie kunitisha. Je, umewahi kufikiria kama Lisa angefanya uzembe, huenda Suzie angekufa wakati wowote?”
Alvin alimkodolea macho Jack. “Mimi ndiye mkuu wa familia ya Kimaro na Suzie ni sehemu ya familia ya Kimaro. Nina haki ya kuamua kila jambo linalohusiana na nyinyi nyote.”
“Wewe ni mtu wa kiburi na jeuri kweli. ” Jack alikasirika. “Kwanini unamuwazia vibaya Lisa? Kupendana naye kweli ni bahati yake mbaya.”
“Upendo?” Alvin alicheka. “Mtu kama yeye hastahili upendo wangu. Nilikuwa kipofu wakati huo. Kuanzia sasa sitaki kumuona Suzie akiwa karibu naye.”
"Ninakuambia, sitaenda Uganda" Jack akatikisa kichwa. Hakuweza kumuacha Suzie peke yake kwenye nyumba ile. Pia alikuwa amemuahidi Lisa atamlinda Suzie na kuwaruhusu wakutane mara kwa mara.”
“Kama hutaki kwenda, basi usiwe meneja mkuu tena. Nenda ukafanye kazi kwenye madaraja ya chini,” Alvin alisema kwa ukali.
"Sawa, amua lolote unalotaka kuamua." Jack alihisi chuki na fedheha zikiendelea ndani ya moyo wake. Akageuka na kuondoka kwa hatua ndefu.
Alipofika mlangoni, alisimama na kugeuka. "Alvin, ninamchukulia Lisa kama rafiki mzuri na ninaweza kumwamini bila masharti. Lakini wewe? Yeye hulala kando yako kila usiku, lakini imani yako kwake haiwezi kulinganishwa na yangu. Si hivyo tu, hata polisi wanachunguza kesi ya Logan kwa utaratibu wa kawaida. Wewe ndiye pekee ambaye hauko tayari kumpa nafasi ya kudhibitisha kuwa hana hatia. Wewe ni mkatili sana. Utakuja kujuta siku moja." Baada ya kuongea aliufunga mlango kwa nguvu na kuondoka bila kuangalia nyuma.
Sura ya: 454
Ofisini, Alvin alipiga meza kwa ngumi. Macho yake yalionekana kuduwaa. Je, alikuwa mkatili? Si yeye ndiye aliyemlazimisha? Alimtumia hata Suzie kumtishia safari hii. Alikuwa amemchochea kabisa.
Wakati huo simu yake iliita. Thomas alikuwa akimpigia simu kutoka hospitali. “Shemeji Kimaro, unakuja lini? Baada ya kuondoka asubuhi, Sarah hajala kabisa. Hana hata hamu ya kula. Kwa kawaida, Rodney angekuja, lakini hatujaona hata kivuli chake siku hizi.”
"Nilikuwa na kazi katika kampuni. Nitakuja mara moja."
Alvin harakaharaka akakimbilia hospitali. Sarah alipomwona, roho yake ilipata nafuu na hata akala chakula. "Alvinic, nilisikia ... Logan alipelekwa kituo cha polisi."
“Mmh!” Mtazamo wa Alvin ukiwa mkali. “Polisi tayari wamefungua kesi. Muda ukifika, kutakuwa na kesi mahakamani.”
“Ni vizuri…” Sarah alitoa tabasamu la faraja. "Baada ya yote, haifai kutoa adhabu isiyo ya kisheria. Ni bora kesi hii ipelekwe polisi.”
Thomas alifoka, "Lakini kesi za utekaji nyara kama hizi zitapokea tu kifungo cha miaka michache jela."
“Naamini atatubu kwa moyo wote jela. Tunapaswa kutii sheria pia,” Sarah alisema kwa kujieleza kwa dhati.
Thomas akahema. "Wewe ni mkarimu sana."
Alvin alishusha macho yake chini, akiitazama sura laini na ya upole ya Sarah. Hakuweza kujizuia kufikiria sura mbaya ya Lisa.
Hakuweza kujizuia kuomboleza. Je, kweli alimpenda mtu asiyefaa? Huenda hakumpenda Sara tena, lakini angalau alikuwa mtu mwenye fadhili. Hata hivyo, alikuwa amemuumiza tena na tena kwa ajili ya mtu kama Lisa.
"Shemeji Kimaro, utakuwa wakili wa Sarah kwa kesi yake, sivyo?" Thomas alisema ghafla, “ Nina wasiwasi kwamba Lisa ataajiri wakili stadi. Itakuwa shida ikiwa Logan ataachiliwa huru."
“Hilo halitatokea. Nitaisimamia kesi mwenyewe,” Alvin alisema kwa sauti ya chini.
“Hapo sawa. Hakuna kesi ambayo Alvinic hawezi kushinda.” Sarah aliinua kichwa chake na kutabasamu kumtazama.
•••
Usiku, katika makazi ya familia ya Kimaro.
Alvin alirudi, ingawa ilikuwa nadra kwake. Bibi Kimaro hakujisikia raha baada ya kumtazama. “Je, jua limechomoza kutoka magharibi leo? Leo umerudi? Ni nini hicho mkononi mwako?”
"Mdoli mpya zaidi wa Barbie. ” Alvin alimletea Suzie ambaye alikuwa akipata vitafunwa. "Ninakupa hii, sawa?"
Hakuwa mtu wa kujali hisia za mtoto, lakini maneno ya Suzie jana yake yaliuumiza moyo wake. Hakuweza kulala kwa usiku mzima. Hakuelewa kwa nini alikuwa na wasiwasi juu ya binti wa Jack. Ilikuwa ni ajabu sana.
"Hapana." Suzie alimkwepa. Alikimbia hadi upande wa Bibi Kimaro na kuinamisha kichwa chake.
Bibi Kimaro alimkodolea macho Alvin na kufoka, “Ulimpokonya umeneja baba yake na kumpa kazi za chini na kumfanya kuwa kicheko, lakini bado unathubutu kuja kumfurahisha Suzie?”
"Jack alikwambia hivyo?" Uso wa Alvin ulisinyaa.
“Hapana kabisa.” Bibi Kimaro aliinua kichwa chake, akasema kwa sauti, “Suzie aliwasikia Jack na Lisa wakijadili jambo hili. Baba yake alikukosea nini hata ukamtendea hivyo?”
Alvin alishindwa cha kusema. Hakuweza kumwambia ukweli.
"Najua, lazima iwe kama vile Aunty Sarah alisema Anko Alvin na baba yangu wana baba tofauti, hivyo Anko Alvin hampendi baba yangu,” Suzie alisema kwa uchungu huku macho yakiwa na machozi.
"Sarah alikuambia hivyo?" Maneno ya Bibi Kimaro yalibadilika papo hapo. “Ni mwanamke wa aina gani? Angewezaje kusema hivyo mbele ya mtoto? Amezidi sana.”
“Bibi…” Alvin alionekana kutoridhika.
Bibi Kimaro alisema kwa ukali, “Nilisikia kwamba umekuwa ukikaa karibu na Sarah kila siku hospitalini hivi majuzi. Je, hukuwa na mwanamke katika maisha yako ya nyuma? Tayari amekusaliti. Kila mtu hapa mjini anazungumza juu yake. Mbona wewe ni mjinga sana?”
Alvin aliweka uso mrefu. Hakusema neno.
Mzee Kimaro aliingia kwa msaada wa fimbo yake. “Acha kuongea. Huyu mjukuu wako hawezi kuishi bila wanawake hata hivyo. Afanye chochote anachotaka. Yeye ndiye mkuu wa familia ya Kimaro sasa. Haifai mtu kusema lolote.”
“Nifanye nini tena? Ikiwa unataka kumuoa Sarah, nenda kafunge naye ndoa nje ya nchi.
Usitualike. Hatutahudhuria harusi. Inatia aibu,” Bibi Kimaro alisema kwa hasira.
“Naenda chumbani kwangu.” Alvin aliweka mdoli wa Barbie juu ya meza kabla ya kugeuka na kuondoka.
Wakati anakaribia kupanda ngazi, alisikia sauti ya Suzie kwa nyuma. "Anko Alvin, subiri."
“Suzie, nilifikiri hunipendi tena?” Alvin akageuka nyuma. Dokezo la uchungu likaangaza machoni pake.
Suzie aliuma mdomo wake, na macho yake safi yalikuwa mekundu. “Nataka tu kukuambia hivi. Siku hiyo, Aunty Lisa hakuniteka nyara. Kabla sijaenda, Aunty Lisa alikuwa ameshanieleza kila kitu. Alisema alitaka kumuokoa rafiki kwani rafiki huyo alitekwa na wewe. Hakuwa na chaguo ila kukufanya ufikiri kwamba nilitekwa nyara. Hapo ndipo ungemruhusu huyo Anko aende zake.”
"Ulijua tangu mwanzo." Alvin alishtuka. Alidhani Suzie asiye na hatia alikuwa amefichwa ukweli wa mambo.
Suzie alisema kwa umakini, “Mm, baba alisema Anko Logan ni mtu mzuri pia. Alimsaidia sana Aunty Lisa hapo awali, kwa hiyo nilitaka kumsaidia. Samahani nilikudanganya. Nataka tu kukuambia kuwa Aunty Lisa hakuwahi kuniumiza. Yeye pia hakuwahi kunidanganya. Ninampenda sana, na nitaendelea kumpenda katika siku zijazo. Ingawa mimi ni mdogo, bado ninaweza kuwatofautisha watu wazuri.”
Alvin alipigwa na butwaa. "Mtoto mdogo kama wewe anaweza kutofautisha nini?"
"Bila shaka, naweza." Suzie aliweka mikono yake kwenye kiuno chake kidogo. “Katika nyumba hii kubwa, Anko, Grand’ma, Grand’pa, Bibi mkubwa, Babu mkubwa, na maanti wote wananipenda kikweli, lakini Babu, Babu mkubwa na Bibi yangu, na maanko na maanti kutoka upande wa baba yangu hawanipendi.”
Alvin alishtuka na kujibu baada ya muda mrefu. "Ina maana babu yako na bibi, Aunt zako na Uncle zako kutoka kwa familia ya Campos hawakupendi?"
"Ndio, Baba aliponipeleka kwa familia ya Campos, wote hawakunipenda. Kaka mwingine mkubwa hata alininyanyasa. Aliponichokoza, lakini babu aliniambia nimuombe msamaha.” Suzie aliinamisha kichwa chini na kukunja ngumi zake ndogo. “Nililelewa na Mama tangu nilipokuwa mdogo, kwa hiyo nina uwezo wa kusoma maneno ya watu.”
Moyo wa Alvin uliinama kwa uchungu, lakini hakuweza kujua ni kwanini. “Usiende kwa familia ya Campos tena. Ikiwa umechoka, njoo unitafute.”
"Hapana. Simpendi Aunty Sarah, na najua hata mimi pia hanipendi.” Suzie alitikisa kichwa na kupunga mkono. “Kwaheri, Anko.”
Kisha, alikimbia kurudi ndani ya nyumba.
Alvin alimtazama mgongoni kwa muda mrefu na kuchukua simu yake kupiga idara ya Human Resources. "Wacha Jack aendelee kuhudumu kama meneja mkuu wa kampuni."
Meneja wa idara ya Human Resources alikosa la kusema. "Bado anahitaji kwenda Uganda kujenga kiwanda?"
"Hakuna haja. Nitapanga mtu mwingine aende.”
Alvin akahema. Kwa nini Jack alikuwa na binti ambaye angeweza kumfanya Alvin afadhaike hivyo? Iwapo angemvua Jack umeneja na kumtupa kwenye vyeo vya chini katika kampuni, Suzie angedharauliwa kama binti yake. Alvin asingeruhusu mtu yeyote kumdharau Suzie.
Hata hivyo… hakutarajia kwamba Mason Campos angemchukia sana Suzie. Suzie alikuwa ni mjukuu wake. Ni babu yupi hawakupenda wajukuu zake? Watu wa familia ya Campos walikuwa wa ajabu sana.....ITAENDELEA...
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA..
