JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................455-456

Sura ya: 455

Alvin aliporudi kwenye jumba lake la kifahari, Aunty Yasmine alimkaribisha kwa tabasamu. “Bwana Mkubwa Kimaro, utamrudisha lini Bibi Jones?"

Uso wa Alvin ulibadilika ghafla, lakini Aunty Yasmine hakugundua na aliendelea na tabasamu, "Nilitazama habari siku hiyo. Uliandamana na Miss Jones nje ya nchi. Nyinyi wawili mmerudiana pamoja? Nina furaha sana nikiwaona mkiwa pamoja.”

"Tumeachana tena," Alvin alisema bila kufafanua.

Aunty Yasmine aliganda. "Kivipi…"

“Usirudie kumtaja tena huyo mwanamke siku zijazo,” Alvin alisema na kupanda ghorofani.

Baada ya Alvin kuingia chumbani, alifunga mlango kwa kishindo. Akawasha sigara na kukumbuka maneno ya Suzie. Je, ni kweli Lisa alimtumia Suzie kumtishia? Vipi ikiwa angemdhuru Suzie? Athari ya kuchanganyikiwa ilionekana machoni pake.

Kisha, Hans akaingia. “Bwana Mkubwa Kimaro, hii ndiyo taarifa kuhusu kesi ya Logan Law.”
Alvin aliduwaa na ghafla akakumbuka kuwa aliamua kuchukua kesi ya Sarah. Ikabidi apokee taarifa husika.

Wakati huo, Lisa na yeye wangekutana mahakamani.
Kwa kuwa Lisa alimjali sana Logan Law, yeye binafsi angempeleka mtu huyo jela.
Baada ya yote, neno 'kushindwa' halikuwepo katika kamusi yake.

“Bwana Mkubwa, hujasimamia kesi mahakamani kwa miaka mingi. Mbona imekuwa ghafla? Kwa heshima zote, haijalishi ni nani atashinda kesi hii, Bi Jones na wewe mtakuwa maadui kabisa mwisho wake,” Hans alisema kwa ujasiri.

Alvin alipigwa na butwaa kidogo. Ilikuwa ni kweli kwamba ilikuwa imepita miaka mingi tangu achukue kesi ya mwisho. Ikiwa Thomas asingezungumza hospitalini siku hiyo, labda asingechagua kwenda kortini kibinafsi. Ilibidi akiri maneno ya Thomas yalimsukuma sana kuchukua uamuzi huo.

Ndani ya moyo wake, kulikuwa na mlipuko mkali wa kuwashwa na kuudhika. Hata hivyo, alipotafakari kwa makini, alijua Lisa tayari ameshakatisha penzi lao la mwisho pale alipomtumia Suzie kumtishia.

“Inatosha, najua ninachofanya. Nenda nje,” Alvin alisema kwa ukali.
Hans alifunga mlango nyuma yake na kuhema.
•••
Nyumbani kwa Lisa huko Karen Estate.


Katika siku mbili zilizopita, Lisa alikuwa ametingwa nyumbani na kutazama video za dashcam hadi macho yake yakawa ukungu ili kutafuta ushahidi. Kwa bahati nzuri, Pamela alikuwepo kumsaidia. Hata hivyo, iliwachosha sana hivi kwamba walikosa usingizi.

Mchana, Hans aliwapelekea makaratasi husika kwa kesi ya Logan. “Kesi imepangwa kufanyika Jumatano ijayo.
Wakili wa upande mwingine ni Alvin Kimaro.”

"Alvin Kimaro?" Pamela nusura aigeuze laptop mbele yake. “Amedhamiria kumsaidia Sarah tena, sivyo? Kila mtu nchini anajua kuwa Alvin hajawahi kupoteza kesi yoyote hapo awali. Haijalishi ni ushahidi gani uliopo, anaweza kupindua meza.”

Pamela alikumbuka jinsi Alvin alivyosimamia kesi ya Lisa kumuokoa hapo awali, kwa hivyo hakutarajia angeenda kinyume na kumpeleka gerezani mlinzi wake aliyeaminika zaidi.

“Hatuwezi kukata tamaa,” Lisa alisema, “Kwa uso wa ushahidi kamili, wakili yeyote mwenye nguvu ana uwezekano wa kushinda. Kwa kuwa hajawahi kushindwa, safari hii ataonja machungu ya kupoteza kesi katika vita dhidi yangu.”

Pamela akampa dole gumba. “Wewe unajiamini sana!”

Hans alisema, "Kila wakili ambaye alikuwa ameenda mahakamani dhidi ya Alvin Kimaro alisema hivyo pia, lakini wote walishindwa kabisa. Hakuna uwezekano wa kushinda hata kidogo ikiwa Alvin ataenda mahakamani kwa ajili ya Sarah.”

Lisa aliinamisha macho yake. Kope zake nyeusi na nzito zilizuia mwanga hafifu machoni pake. "Haijalishi Alvin anashangaza kiasi gani, au yeye ndiye mwenye nguvu zaidi hapa nchini. Siku zote kutakuwa na mtu mwenye nguvu zaidi yake huko nje. Ilimradi mtu huyo anaweza kupatikana na kuwa tayari kuja, niko tayari kutumia kiasi chochote cha pesa.”

“Kweli…” Hans alisita na kusema, “Alvin Kimaro aliwahi kushindana na wakili aliyeshika nafasi ya pili hapa nchini na wawili hao wakafungana. Kwa sasa, mwanasheria anayeweza kupambana naye ana zaidi ya miaka 60 na amestaafu kwa zaidi ya miaka kumi. Hataonekana hata mtu tajiri zaidi duniani atamwomba afanye hivyo.”

Lisa, akaguna. Pamela alikosa la kusema. "Kwa maneno mengine, Alvin Kimaro hashikiki kwenye uwanja wa sheria?"

"Kitu kama hicho." Hans aliitikia kwa kichwa kwa kusisitiza.

Pamela naye akanyamaza ghafla. Kwa maoni yake aliamini kwamba hata kama Alvin angefahamu kuwa Suzie na Lucas ni watoto wake na Lisa, ilionekana kwamba daima angempendelea Sarah bila masharti. Hata angekua anampenda Lisa, hakuna kitu ambachokingebadilika. Ulinzi wake juu ya Sara ulichongwa ndani ya mifupa yake.

Siku chache zilizofuata, Lisa na Austin walikuwa wanahangaika kutafuta ushahidi. Ilikuwa ni Jumanne, na siku ya kesi ilikuwa imekaribia katika kupepesa macho. Kelvin alipokuja kumtembelea, aliona macho yake yakiwa yametapakaa damu na uso wake ulionekana kuwa umepungua. Moyo wake ulikunjamana.

“Unaenda mahakamani kesho. Umepata ushahidi wowote?"

“Ndiyo.” Lisa aliyapapasa macho yake yaliyochoka. "Tulipata ushahidi fulani. Kuna nafasi ya kushinda, lakini sio kubwa."

“Oh?” Macho ya Kelvin yaliangaza kumaanisha. “Ni nini? Nina hamu sana ya kujua.”

“Sitasema sasa. Utajua kesho,” Lisa alisema kwa wasiwasi, “Lakini uwezekano wa kushinda ni mdogo sana. Baada ya yote… wakili wa upande unaopingana ni Alvin Kimaro, ambaye hajawahi kushindwa hapo awali. Kesho, badala ya kumtegemea hakimu kutamka kwamba Logan hana hatia, tunajaribu kumshawishi Alvin. Alimradi afahamu kuwa Logan alichezewa mchezo mchafu, kuna nafasi tunaweza kushinda."

"Sio lazima," Kelvin alimkumbusha, "Hata kama atatambua kuwa Logan kachezewa mchezo mchafu, itakuwa ni kushindwa kwake kwa mara ya kwanza katika taaluma yake kama wakili ikiwa atakubali. Hata akijua amekosea, kwa kuangalia tabia yake ya kiburi, ataendelea kupambana ili kushinda.”

Lisa alipigwa na butwaa na kutabasamu kwa uchungu. “Uko sahihi. Watu kama yeye wanajali sana hadhi zao machoni kwa watu, hata kama hali halisi inapingana na ukweli.”

"Lakini ... utashinda." Kelvin ghafla alimkandamiza begani mwake. “Najua umekuwa na shughuli nyingi na umechoka sana, kwa hivyo pia sijakaa bure bila kufanya kazi. Nilipata gari ambalo lilitumika kumteka Sarah. Hakukuwa na alama yoyote ya Logan ndani yake.

“Kweli?” Lisa akaketi ghafla, macho yake yakiwa yamejawa na mwanga.

“Ndiyo.” Kelvin akamkabidhi faili. “Nimeziomba mamlaka husika kulikagua gari na hata kutafuta alama za vidole. Ni bodi la gari pekee ndilo lenye alama za vidole za Logan.”

"Hiyo ni safi sana." Lisa alichukua faili na kuhisi mlipuko wa furaha. "Kwa hili, tutashinda kabisa. Kelvin asante sana. Siwezi kamwe kulipa—”

“Usiongee kuhusu kunilipa. Hisia zangu kwako zinanifanya niwe tayari kufanya lolote kwa ajili yako wewe.” Kelvin alishika mikono yake kwa upole. Macho yake yalijawa na upendo aliposema, “Ikiwa unataka kumlinda Logan, nitamlinda pamoja nawe.”

Moyo wa Lisa ulitetemeka sana.
Muda wote huo, alifahamu hisia za Kelvin kwake, lakini siku zote alikuwa amemkataa.
Wakati huo, aliguswa kabisa. Kwa kweli, alipaswa kutambua zamani kwamba alikuwa mtu ambaye alimtendea vyema zaidi. Miaka hii yote, alikuwa ameandamana naye bila malalamiko. Angeweza kumsaidia kila alipohitaji, na aliwatendea vizuri Suzie na Lucas pia.

Kwa upande wa Alvin, alimuumiza tu bila kikomo.
Alijuta ghafla. Alijuta kwamba alitambua kuwa amechelewa. "Samahani, Kelvin. Ninatambua kwamba nimefanya makosa,” Lisa alisema kwa uchungu, “Sikupaswa kumwendea Alvin tena na kurudiana naye. Ninaendelea kukuumiza mara kwa mara, lakini sitarudia tena.”

"Unamaanisha…?" Kelvin alitazama juu kwa mshangao.

"Zamani, nilifikiria tu kumrudia Alvin na kumwacha baadaye ili aonje uchungu wa kuachwa na mpendwa wake." Lisa alisema kwa uchungu, “Lakini sikujua kwamba uhusiano kati yake na Sarah hauwezi kuvunjwa na mtu yeyote. Kwa kweli, hata kama Sarah asingemsaliti Alvin, asingeweza kuvunja uhusiano wake naye. Kwa muda mrefu, tungekuwa tumetalikiana hata hivyo. Ni sasa tu ndipo hatimaye ninaelewa kwamba mimi na Alvin tuliachana wakati huo si kwa sababu ya Sarah kuilaza akili yake bali kwa sababu anampenda sana na Sarah. Katika maisha haya, Sarah daima atakuwa kipenzi cha kwanza cha moyo wake.”

"Ni vizuri unajua," Kelvin alisema huku akitabasamu. “Ni kama vile nilivyo na wewe moyoni mwangu. Hata nikijua hutanikubali, bado nitaweka mstari wazi moja kwa moja na wanawake wengine. Kwa maoni yangu, upendo wa kweli na uaminifu unapaswa kuwa hivi.”

"Ndio, najua ni nani anayestahili kuthaminiwa sasa." Lisa alimshika mkono Kelvin. “Asante kwa kunisubiri kila wakati. sitaki kukuangusha tena.”

“Hiyo ni nzuri.” Uso mpole na maridadi wa Kelvin uliingiwa na furaha.
Alimkumbatia Lisa kwa furaha na kumzungusha huku na kule. “Lisa, nimeisubiri sana siku hii. Hii siyo ndoto tu, sivyo? Hutaniacha kwa Alvin tena baadaye, sivyo?”

“Hapana, lakini sitawaacha Sarah na kaka yake. Lazima nilipize kisasi kwa niaba ya familia ya Charity,” Lisa aliuma meno na kusema.

“Sawa, nitakusaidia siku zote. ” Kelvin alinyoosha mkono kumshika kwa nguvu, uso wake ukiwa umejaa furaha na kuridhika.

Sura ya: 456

Saa mbili asubuhi siku iliyofuata.
Bentley nyeusi ya Alvin ilikuwa ya gari ya kwanza kufika mahakamani. Baada ya gari kuegeshwa, Alvin alishuka na kumfungulia mlango wa gari Sarah. Wakati huo huo, Thomas alishuka kutoka kwenye kiti cha nyuma.

Mlangoni, mwandishi wa habari mwenye macho makali akaenda mara moja. "Alvin Kimaro, umerudiana pamoja na Bi.
Njau? Nilisikia kwamba ulisafiri hadi Johannesburg siku chache tu zilizopita pamoja na Miss Jones. Wewe unawamiliki wote sasa…?”

“Usichukue video…” Sarah aliuzuia uso wake kwa mkono wake na kujificha kwenye mikono ya Alvin kwa woga.

Alvin alimkodolea macho mwandishi. "Endelea kurekodi video ikiwa haujali kampuni yako kupotea kabisa kwenye uso wa dunia."

Mwanahabari huyo alikumbuka ghafla kwamba kampuni ya vyombo vya habari iliyoripoti kuhusu kurudiana kwa Alvin na Lisa siku chache zilizopita ilifungwa ghafla. Miguu yake ilitetemeka na kuondoka kwa haraka kutafuta habari nyingine za kuripoti.

"Alvin, kesi ya leo inapaswa kuwa faragha, sawa?" Sarah alisema kwa woga na wasiwasi, “Sitaki habari za kutekwa nyara kwangu zienee…”

“Ni kesi ya faragha hata hivyo, haitakuwa na watazamaji baki. Usijali, habari zake hazitaenea.” Alvin akampiga bega taratibu.

Wakati huo, gari jingine lilipita na kuegesha karibu na Bentley la Alvin. Kisha, Lisa, Pamela, na Austin wakatoka nje ya gari. Sarah alipomuona Lisa, aliogopa sana na mara moja akajificha mikononi mwa Alvin akiwa na uso uliopauka.

Alvin alifikiri kwamba alikuwa akikumbuka mambo yale ya kutisha tena na hakuweza kujizuia kumtazama Lisa. “Nilifikiri usingethubutu kuja.”

“Kwanini nisingethubutu? Nina dhamiri safi.” Lisa alimtazama Sarah aliyekuwa amebebwa mikononi mwake bila viwimbi machoni mwake. Alikuwa amepitia baadhi ya mambo baada ya kuyatafakari.

"Ni aibu kwamba hakika utapoteza ingawa uko hapa." Thomas alicheka kwa ujeuri. “Alvin Kimaro ndiye anayeshughulikia kesi ya Sarah leo. Yeye ndiye wakili bora zaidi nchini na hajawahi kushindwa.”

“Hiyo si lazima iwe kweli. Labda leo ndio siku ambayo rekodi yake ya unbeaten inakwenda kuvunjwa kama Yanga na Ihefu?" Lisa alitabasamu kwa utulivu.


Thomas alikoroma kwa kicheko. "Ni wakili gani anayekusimamia mpaka unajiamini sana kisi hicho?"

Lisa alitazama nyuma yake na ghafla akatabasamu. "Bwana Nelly, nitakutegemea."

Alvin na wengine waligeuka kutazama na kumwona mzee wa makamo mwenye kichwa kinachong'aa akitoka kwenye gari aina ya Santana.

“Unamaanisha yeye…?” Pembe za mdomo wa Thomas zilitetemeka. Alifikiri kwamba Lisa angetafuta wakili wa angalau kiwango cha Alvin huko Nairobi au nje ya nchi, lakini aliishia kupata wakili asiyejulikana ambaye alikuwa mfupi na alionekana maskini. Jamani, mtu huyo hata alikuwa akiendesha Santana ambayo ilikuwa na thamani ndogo sana. Je, hakuwa na uwezo kiasi gani?

“Ndiyo, huyu ni Bw. Nelly.” Lisa alipeana mkono na mwanasheria kwa shauku.

Tabasamu la Bw. Nelly lilikuwa la kujilazimisha sana. Wakati mstari mkali wa macho wa Alvin ulipompita, miguu yake ilianza kutetemeka pia.

"Mungu wangu! Umempata wapi wakili takataka kama huyo?" Thomas alishindwa kujizuia kuangua kicheko. “Alvin Kimaro, angalia nguo zake. Nadhani ni mitumba iliyotumika Ulaya. Hata soli za viatu vyake vya ngozi zimechubuka. Tumbo langu litauma kutokana na kucheka huku.”

Alvin naye alikunja uso na kumtazama kwa kina Lisa. “Huyu ndiye wakili anayemtetea Logan?”

Lisa alitabasamu bila kusema lolote mwanzo mwisho. Aliwatazama tu kwa utulivu.

Thomas alipomaliza kucheka, alifuta machozi machoni pake na kusema, “Bw. Nelly, nikikuuliza, alitumia kiasi gani kukuajiri?”

"Si nyingi, karibu dola 2,000," Bw.Nelly alisema, kwa aibu.

“Ajabu! ” Thomas kwa mzaha alimpa dole gumba Lisa. “Lisa, najua umekata tamaa ya kushinda kwa sababu unashughulika na wakili msomi Alvin Kimaro, lakini si unamuonea huruma Logan Law? Mbona hauko tayari kutumia pesa nyingi kidogo zaidi kuajiri wakili bora. Dola 2,000, tsk. Ikiwa unasitasita, ningekukopesha pesa, kuliko kuangukia kwa wakili wa hali ya chini kama huyo.”

“Umeelewa vibaya.” Lisa alitabasamu kwa unyonge. "Nilifikiria tu kuwa kushughulika na wakili kama Alvin Kimaro, hakuna haja ya kuajiri mtu wa gharama kubwa sana. Baada ya yote, tutashinda hata hivyo, haijalishi yeye ni nani.”

"Nini? Nasikia vitu au bado unaota? Unajiingiza katika mawazo yako.” Thomas alicheka. "Alvin Kimaro, anasema kwamba wakili mbovu kama huyu hapa anaweza kukushinda."

“Ota ndotoni,” midomo myembamba ya Alvin ilitamka maneno hayo mawili bila huruma. Machoni mwake, Lisa alikuwa tayari amekata tamaa.
Hata hivyo, alielewa hali hiyo. Ilikuwa ni kawaida kwa watu kukata tamaa wanapokuwa wanamkabili kama mpinzani wao.


"Unaweza kuridhika sasa," Pamela alidhihaki, "Kesi itakapokwisha, watu katika ulimwengu wa nje wataanguka sakafuni wakicheka wanapojua kwamba gwiji huyo mashuhuri ambaye hajawahi kushindwa alipoteza kwa wakili aliyegharimu dola 2,000."

“Kwa kweli sielewi kwanini nyie mna ndoto zisizo za kweli. ” Safari hii hata Sarah alitikisa kichwa. Alimshika mkono Alvin. “Alvin twende ndani. Tusipoteze muda tena hapa.”

“Mmh.” Alvin alitembea na kuondoka.

Nyuma yake, Thomas alimwambia Lisa kwa sauti ya chini, “Haiwezekani ushinde, lakini ukipiga magoti na kuniomba na kumuacha Pamela alale na mimi kwa usiku kadhaa, naweza nikamsihi dada yangu ampunguzie Logan. kifungo cha miaka michache.”

“F*ck off,” Lisa alitema mate pembeni kwa hasira.

Pamela alimlaani moja kwa moja, “Kipande cha takataka kama wewe unataka mwili wa thamani kama huu? Potelea mbali. Hustahili hata kushika viatu vyangu.”

"Pamela Masanja, nitakufanya ujute mapema au baadaye."
Thomas alitabasamu vibaya. "Hata hivyo, nilisahau kukuambia, kidole cha Logan kililiwa na mbwa. Ni kwa sababu Shemeji Kimaro anamjali sana Sarah. Sarah alipoomba kidole cha Logan, Bwana Kimaro alikikata na kukipeleka bila neno lolote. Mbwa alikula kana kwamba ni kipande cha soseji. ”

Lisa alitazama juu. Hali ya joto machoni mwake ilishuka ghafla hadi kiwango cha baridi, na ngumi zake zikakunjamana kwa hasira.
Thomas aliona na akacheka kabla ya kuondoka.

"Mwana wa b*tch!" Pamela alilaani. “Mapema au baadaye, nitawafanya ndugu hao waishi maisha mabaya zaidi kuliko kifo.”

"Ndio," Lisaalijibu kwa sauti ya chini. Alikuwa na mawazo sawa....ITAENDELEA...

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.