JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................451-452

Sura ya: 451

Alvin aligeuka nyuma na kuelekeza mgongo wake kwa Lisa. Lisa alipotazama kivuli chake kwa nyuma, kulikuwa na uchungu unaozunguka machoni mwake.

Shani alipiga magoti chini. “Bwana Mkubwa Kimaro, Sidhani kama Bi Jones anaweza kuwa anahusika na hili— ”

Alvin alimpiga jicho kali kabla hajamaliza sentensi yake. "Shani, wewe ni sawa na Maya. Nyote wawili mlifanya makosa sawa. Ninyi nyote ni wanachama wa ONA, lakini mnaruhusu hisia zenu kutawala matendo yenu.”

"Ninaelewa. Ndiyo maana Bwana Mkubwa ulinihamisha mwaka huo.”
Shani alitabasamu kwa uchungu. "Hata hivyo, nilikuwa nikimlinda Bi. Jones kando yake kama ulivyoagiza zamani. Kwa kweli yeye si mtu mbaya. Bwana Mkubwa, ninafanya hivi kwa ajili yako pia. Hatimaye uliweza kurudiana pamoja naye. Kama utakuwa mkatili sana na kukata hisia za pekee ulizo nazo kwake, unaweza usipate wakati mwingine baada ya hili."

“Unadhani najali kuhusu hilo? Je, aliwahi kufikiria kuhusu hisia zangu alipofanya mambo hayo? Anajua wazi Sarah ndiye mfadhili wangu. Tayari nina deni kubwa la Sarah, akidhurika Sarah ni sawa na kudhurika mimi, lakini anaendelea kunilfanya nijihisi hatia kwake tena na tena. Labda… hajawahi kunipenda hata kidogo.” Alvin akacheka vibaya.

“Bwana Mkubwa, naamini si yeye… “

Shani akakatishwa kwa ukali. "Peleka hii hospitalini." Alvin aliinua mkono wake na kumtupia Shani begi mkononi.

Shani aliangalia. Uso wake ulibadilika mara moja. " Hii ni…"
"Kidole cha Logan. Ni ahadi yangu kwa Sarah, aliniomba nimkate mkono, lakini kidole kinatosha. Hiyo ndiyo huruma ya pekee kwangu kwake.” Alvin alisema.

Shani alifungua kinywa chake na kusema kwa kusitasita, “Nilipokutana na Miss Jones mlangoni, alisema kwamba ingawa Logan ni mlinzi wake, anamchukulia kama familia yake. Nawaza tu, Bwana Mkubwa, ungejisikiaje ikiwa mtu angekata kidole cha mtu wa familia yako?"

Moyo wa Alvin ulitetemeka. Akafinya macho. " Unamaanisha nini?"

“Namaanisha huenda Lisa asikusamehe tena baada ya hili, hasa utakapogundua ukweli kuwa si yeye aliyehusika na kumteka Sarah.” Shani alitabasamu kwa uchungu. Akainama na kuokota kidole pale sakafuni na kwenda nacho hospitali.

Alvin alisimama palepale, huku akiwa hana wasiwasi. Majira ya joto yalikuwa yanakaribia, lakini alihisi ndani yake kuwa baridi. Hapana, haiwezi kuwa. Alikuwa ni mlinzi tu. Isitoshe, ilimbidi kumfundisha Lisa somo. Kama sivyo, asingeweza kumpa Sarah maelezo.

Lisa aliletwa ndani baada ya mlango kufunguliwa na mara akasikia harufu ya damu. Kisha, akaona Logan ametupwa sakafuni kama gunia. Tayari alikuwa amepoteza fahamu. Uso wake, ambao ulikuwa na kiburi na msimamo, ulikuwa na majeraha makubwa. Mwili wake wote ulikuwa umejaa majeraha yaliyotokana na mjeledi.

Lisa alipitisha macho juu ya mwili wake wote. Hatimaye, macho yake yakatua kwenye mkono wake. Macho yake yalipungua ghafla.

“Kidole chake…”

"Bwana Kimaro alikikata sasa hivi," mlinzi wa ONA alisema. Baada ya hapo, alifunga mlango na kuondoka.

“Sasa hivi?” Akili ya Lisa ililipuka. Sasa hivi, Alvin alikuwa humo alipokuwa akisubiri nje? Alikunja ngumi hadi kucha zikachimba kwenye nyama yake. Alvin anawezaje kuwa mkatili hivyo? Ilikuwa ni ukatili kupita kiasi! Hakuwa binadamu hata kidogo! Chozi lilidondoka kutoka kwenye jicho lake. Wakati huo, macho yake hayakuwa na joto na yalijaa chuki tu.

"Logan ... Logan." Aliita jina lake kwa upole.

Hakuna aliyejua jinsi Logan alikuwa muhimu kwake. Alikuwa mdogo tu kwake kwa miaka mitano. Alianza kumchukulia kama kaka yake zamani.

“Bosi…” Logan alijitahidi kufumbua macho. “Kwanini uko hapa? Alvin… Alvin alikufunga wewe pia?”

"Mimi ... nimekuja kukutoa hapa," Lisa alisema kwa macho mekundu, "Lakini kidole chako ..."

“Ni sawa. Si… Si ni kidole tu?” Logan alivuta pumzi kutokana na maumivu. Baada ya muda, mwili wake ulianza kutetemeka huku macho yake yakirudi nyuma.

"Una tatizo gani?" Lisa alishtuka sana.
“Mimi… nilidungwa dawa za kulevya. ” Logan alihema kwa pumzi kubwa.


"Alvin ndiye aliyefanya hivi?" Lisa aliuliza kwa sauti ya kutetemeka.

“Hapana…Si yeye.” Logan alipiga chini ngumi kwa uchungu. "Uliponimbia kuwa nisionekane hadharani baada ya paparazi kutupiga picha kule baa, nilikuwa nikijificha ... kulingana na maagizo yako. Nilikuwa mwangalifu, lakini sikuwahi kutarajia kwamba mtu aliyekuwa akiniletea chakula angetia dawa za kulevya kwenye chakula changu. Nilipokula ndipo nikapoteza fahamu. Nilipoamka… nilijikuta nimetupwa pangoni.

“Sarah alikuwa pembeni pia. Nilianza kujitahidi kujiondoa wakati huo, lakini sikuweza, sikuwa na nguvu hata kidogo. Baada ya hapo… Alvin na wengine wakaja. Ulikuwa ni mpango."

Lisa aliogopa sana. Alijua kuwa kuna mtu alikuwa akijaribu kuwatengenezea kesi nzito ya utekaji nyara na ubakaji. Hata hivyo, kulingana na maneno ya Logan, ilikuwa ni kana kwamba kuna mtu alikuwa amefuatilia mambo yote ya Logan na mienendo yake.

“Haya yote… lazima yaunganishwe na Sarah. Lakini… kinachotisha zaidi ni mtu anayejificha nyuma ya Sarah. ” Logan alihangaika na kusema, "Tayari ... anatulenga."

Lisa alitetemeka. "Ulimwambia Alvin kuhusu hili?"

"Nilimwambia, lakini hakuamini hata kidogo... wanafikiri ninadanganya." Logan alicheka kwa uchungu. “Bosi, wewe… Una jicho baya, ni mtu gani huyu ulichagua kwenye maisha yako?”

"Samahani. Unaweza kustahimili?” Lisa alimtazama kwa wasiwasi.

"Jambo la muhimu zaidi ni njia za kujiokoa." Logan alikuwa akihema. "Lakini maumivu katika mwili wangu hunisaidia kukaa macho na kujidhibiti mwenyewe. Isitoshe, kifo si kitu. Nina deni kwako maisha yangu hata hivyo.”

“Usiseme zaidi. Nitakutoa hapa.” Lisa alishika mikono yake na kuapa kwa macho mekundu.

Milango ya chuma ilifunguliwa ghafla. Alvin alisimama mlangoni. Alipoona mikono yao yote miwili imefungwa pamoja, uhasama ulitanda machoni pake.

"Inaonekana hujaridhika na kukatwa kidole chako, labda tuukate kabisa mkono wako tena." Alvin alitembea kwa hatua ndefu. Akamtoa Lisa na kumkanyaga Logan kwa nguvu.

"Acha!" Lisa alishindwa kuvumilia tena akampiga ngumi Alvin.

Alvin alishikwa na butwaa na kujikongoja nyuma baada ya kupigwa. Alihisi damu yake ikichemka kifuani. Hata hivyo, uchungu aliokuwa nao haukuweza kulinganishwa na uchungu uliokuwa moyoni mwake.

“Umenipiga kwa ajili ya mwanaume mwingine?” Alvin alimkazia macho Lisa kwa hasira mithili ya simba anayetaka kwenda kumrarua adui.
"Kwa kuwa unamjali sana, nitamuua."

“Alvin, ukithubutu kumuua, nitakufa mbele yako,” Lisa alimtishia kwa hasira.

"Unampenda?" Macho ya Alvin yalikuwa kama macho ya pepo.

"Nampenda kwa kuwa yeye ni mtu muhimu wa familia yangu." Lisa alifumbua macho yake mekundu. “Katika miaka hiyo mitatu, mimi na Pamela tulipitia magumu mengi tulipokuwa Marekani. Kama isingekuwa ulinzi wa Logan, ningekuwa tayari nimekufa. Nilimwokoa na hatari fulani hapo awali, na aliahidi kunilinda kwa miaka kumi. Katika miaka hii kumi, siwezi kumwacha afe.”

Macho ya Alvin yalipoa, lakini bado yalikuwa ya kutisha. “Kama ndivyo, kwanini ulikuwa unamshika mkono sasa hivi? Wewe ni mwanamke wangu. Sikuruhusu kushika mkono wa mwanaume mwingine yeyote.”

"Mke wako? ” Lisa alicheka, lakini tabasamu lake lilionekana kuwa baya kuliko mtu aliyekuwa akilia. "Sahau. Sikuwahi kuwa mwanamke wako tangu mwanzo. Ni Sarah ndiye mwanamke wako. Sitakuwa na ndoto za aina hiyo tena.”

Uso wa Alvin ulibadilika. “Inatosha. Kama usingemuumiza Sarah, nisingekuwa nakutendea hivi. Wewe ndiye uliye katika makosa. Hujawahi hata siku moja kujiweka katika viatu vyangu. Hata ninashuku ... uliingia tu kwenye uhusiano na mimi ili kulipiza visasi. Kwanza ilikuwa ni kisasi kwa Lina na Ethan na sasa ni kisasi kwa Sarah na mimi.”

“Ndiyo, ninalipiza kisasi kwako. Nilikuhudumia hadi ukaridhika kila usiku.” Lisa alicheka kwa uchungu. “Sikuwahi kutaka ulinzi wako wala mali yako. Hata nilikupikia na kukipasha moto kitanda chako. Alvin Kimaro, niambie, unaweza kupata wapi mwanamke kama mimi?"

Alvin alikosa la kusema kutokana na maneno yake, lakini alichohisi zaidi ni majuto. “Maadamu unatubu kwa dhati, omba msamaha kwa Sarah, na ukishakuomba msamaha, ninaweza kukusamehe.”

“Haha.” Logan, ambaye alikuwa amejilaza sakafuni, alicheka ghafla. “Bosi, huyu ndiye mwanaume uliyempenda? Yeye ni rundo gani la takataka?”

"Inaonekana nimekuwa mpole sana kwako." Alvin alikodoa macho kwa kutisha.

Uso mzuri wa Lisa haukuonyesha hisia. “Alvin, huna haja ya kunisamehe tena.”

"Unamaanisha nini?" Alvin alishikwa na butwaa.

“Anamaanisha nini? Bado hujaelewa?” Logan alicheka kwa kejeli. “Inamaanisha kwamba… hahitaji kuwa na wewe tena. Je, unafikiri wewe ndiwe… mwanamume pekee duniani?”

Sura ya: 452

Uso wa Alvin ulibadilika. Akamtazama Lisa bila kuyumba.
Macho ya Lisa yalikuwa kama maji ya ziwa yaliyotuama- tulivu bila mawimbi yoyote.

“Alichosema ni sawa. Ikiwa tulikuwa wapenzi rasmi hapo awali, basi ninasema hivi rasmi, Alvin, tuachane. Haiwezekani niwe na wewe tena. Haitawezekana tena. Kwa hiyo, si muhimu kama unisamehe au la.”

Alvin alimtazama mwanamke aliyekuwa mbele yake ambaye alikuwa ametulia na kujieleza. Moyo wake wenye nguvu ulitetemeka sana. Hali ya unyonge isiyoelezeka ilimfunika.

Lisa alikuwa karibu naye wakati huo, lakini ilikuwa kana kwamba kulikuwa na milima na mito kati yao. Kwenye akili yake hakufikiria tena kutengana na Lisa. Hata Rodney alipopiga magoti mbele yake na kumsihi amwoe Sarah… Hata alipojua kuwa yeye ndiye aliyemwagiza Logan, hakuwa tayari kumuacha Lisa. alitaka tu kumtumia Logan mbuzi wa kafara.

Baada ya muda mrefu, alizungumza kwa sauti ya ukali. “Usithubutu.”

"Alvin, haukupaswa kamwe kumkata Logan kidole. Macho ya Lisa yalijawa na dharau. “Yeye ni familia yangu. Ninamchukulia kama kaka yangu. Je, umewahi kufikiria utakavyojisikia kuona mtu wa familia yako anakatwa kidole? Bora kidonda cha nyama au mfupa uliovunjika kinaweza kupona. Hata hivyo, kidole hakiwezi kuota tena! Wewe ni pepo mkatili na mtu wa ajabu. Mtu kama wewe anapaswa kuwa pamoja na Sarah maisha yako yote!”

"Katika ndoto zako!" Alvin alimfokea kama mwendawazimu. “Hata nikioana na Sarah, bado itabidi uwe mwanamke wangu. Ikiwa unataka nikuache uende, hakuna nafasi isipokuwa nife."

“Basi unaweza kufa. Mwanamume katili na mbaya kama wewe hustahili kuishi katika ulimwengu huu hata hivyo,” Lisa alianza kupiga kelele, “Familia ya Kimaro ilifanya jambo sahihi hapo awali. Ni sawa kwa mtu kama wewe kufungiwa katika hospitali ya magonjwa ya akili na kukaa humo milele. Kwanini nilikukingia kifua? Kwanini nisingekuacha tu ukafie huko?!"

Alvin alimkazia macho Lisa. Macho yake yaliyokuwa yakiwaka moto wa damu yalikuwa yakimtoka machozi. Uso wake mzuri ulikuwa umejikunja na kumfanya aonekane kichaa. Hakuwahi kufikiria kuwa ipo siku mwanamke aliyempenda atamlaani hivyo. Alikuwa mkali sana hivi kwamba alitamani kifo chake.

Alihisi kana kwamba moyo wake ulikuwa ukivunjwa kwa nguvu na kusema, "Utathubutu kusema hivyo wakati mwingine?" Alitembea kuelekea kwake hatua kwa hatua kama mwendawazimu aliyekata tamaa.

“Nimesema kitu kibaya? Nilisema Logan alishtakiwa kimakosa na alifanyiwa njama na mtu mwingine. Kwanini hukuchunguza ipasavyo?! Tangu nilipokutana nawe, umekuwa ukinilaumu mimi kila mara na kumuomba msamaha Sarah. Sikufanya hata jambo lolote la f*cking. Acha kusema kwamba unanipenda! Nakuomba, kaa mbali nami siku zijazo. Siwezi kumudu kuishi na wewe, Alvin Kimaro!”

Baada ya kuongea hayo, Lisa alimsaidia Logan kunyanyuka.

“Unajaribu kufanya nini?” Alvin alimtolea macho ya kejeli. "Ikiwa unataka kumwondoa, endelea kuota! Lisa Jones, kuanzia sasa mtakaa hapa milele. Ukija kwangu na kuniomba nifanye mapenzi na wewe, labda nitakuruhusu ulione jua la nje.”

"Kwa kuwa nilithubutu kuja, basi hakika nina ujasiri wa kutoka.” Lisa alicheka. “Alvin, mbona hutambui ni yupi kati ya wanafamilia wako amepotea?”

Uso wa Alvin ulikunjamana kwa mshangao. "Umefanya nini?"


“Unaweza kumpigia simu Suzie kumuuliza yuko wapi sasa hivi?” Lisa aliinua uso wake na kumkumbusha Alvin.


Moyo wa Alvin ulitetemeka. Suzie alikuwa na simu ndogo ya saa. Akaipata namba ya Suzie na kuipiga kwa haraka, lakini haikupatikana.
“Ulimfanya nini Suzie?” Macho yake yalikuwa yamejaa nia ya kuua kana kwamba anataka kumuua.

"Ninaweza kukuonyesha mahali alipo, lakini itabidi unirudishie simu yangu ili nimpigie mtu mmoja simu ya video." Lisa alinyoosha mkono wake kuelekea kwake.

Mara moja Alvin akaomba mtu alete simu yake. Lisa alimpigia Austin. Mwanamume aliyevaa kinyago usoni mwake alionekana kwenye skrini.
“Bi Jones…”

“Muache amuone mtoto,” Lisa aliamuru. Muda si muda, Austin akampa simu Suzie.

“Anko Alvin…” Suzie aliinua kichwa chake kwa tabasamu angavu. Alvin alitazama pia. Aliona haikuwa Karen Estate bali ni sehemu isiyojulikana kabisa.

“Suzie, kwanini haukwenda shule leo?” Aliuliza kwa haraka.

“Aunty Lisa alisema ananileta nicheze leo. Alimwomba Anko huyu anichukue. Anko Alvin, unaweza kumuuliza Aunty Lisa ataniijia saa ngapi? Suzie alisema kwa sauti ya kitoto, "Nimechoka sana."

“Suzie, unajua ulipo?”

“Hapana, hii ni mara yangu ya kwanza kuja hapa—”

“Mtoto mdogo, ni wakati wa kurudisha simu kwa Anko. ” Austin alimpokonya simu Suzie. Kisha akatazama kwenye kamera huku akitabasamu.


“Bi Jones, rudi haraka. Mtoto mdogo anakuhitaji. Sijawahi kulea mtoto hapo awali, kwa hiyo sina subira sana.” Alikata simu baada ya kusema hivyo.

Alvin akamtupia simu Lisa. "B*tch, unadiriki hata kumdhuru mtoto anayekuamini kabisa! Bado wewe ni binadamu? Lazima nimekuwa kipofu kwa kuanguka katika mapenzi na wewe. ”

Simu ile nzito ikampiga kwa nguvu Lisa kwenye paji la uso. Wakati huo, kichwa chake kilikuwa kikiunguruma kwa maumivu na karibu azimie. Alishindwa hata kusimama ikabidi akae chini. Aligusa paji la uso wake, na hapo ndipo alipogundua kuwa paji lake la uso lilikuwa limevimba vibaya.

“Si ulisema mimi ni mkorofi? Kwa vile mimi ni mtu mkorofi, usipotutoa ndani ya dakika kumi siwezi kukuahidi kuwa Suzie atakuwa sawa,” Lisa alimtishia Alvin kwa ujeuri.

“Unathubutu kunitishia?” Umbo kubwa la Alvin lilimsogelea hatua kwa hatua. Uso wake mzuri ulijaa nia ya kuua.

"Ungependa kujaribu?" Lisa alimkumbusha kwa tabasamu, “Umesahau jinsi Suzie anavyokupenda na jinsi anavyopendeza anapotabasamu?”

Mwili wa Alvin ulitulia. Kwa namna fulani, alipofikiria jinsi ambavyo asingeweza kukutana tena na msichana huyo mdogo, alihisi kama mtu anaupeleka mbali moyo wake.

"Lisa Jones, kosa langu kubwa katika maisha haya ni kukupenda? Potelea mbali! Mchukue mtu wako na mpotee!” Alvin alimzomea kwa dharau, "Lakini ngoja nikuambie hivi, baada ya kutoka nje ya mlango huu, nina njia milioni moja za kufanya maisha yako kuwa kuzimu hai."

“Kwani umeshayafanya maisha yangu kuwa kuzimu hai mara ngapi? Sioni hata kipya utakachonifanya.” Lisa alimsaidia Logan kunyanyuka, ambaye alikuwa na damu nyingi juu yake, na kutoka nje ya chumba cha chini hatua kwa hatua.

Wanachama wa ONA waliwazunguka, lakini Lisa akawafumbia macho. Alipomsaidia Logan kutoka nje ya ONA, mara polisi walifika.

“Tulipokea ripoti ya polisi saa moja iliyopita, na maelekezo ya GPS ya eneo hili kwamba kuna mtu anashikiliwa isivyo halali. Ni nani aliyetoa taarifa?” Polisi walipofika na kuona eneo hilo, walikuwa na maumivu ya kichwa. Baada ya yote, ONA walikuwa ni watu ambao hata polisi wenyewe hawakuthubutu kuwaudhi.

"Mimi ndiye niliyewaita polisi," Lisa alisema, akiinua mkono wake. “Siku mbili zilizopita, Bi Sarah Langa Njau alitekwa nyara. Alvin alipoenda kumuokoa alimuona mtu huyu pale pangoni na Bi Njau. Alihitimisha kuwa mtu huyu ndiye mtekaji nyara mwenyewe, wakamchukua na kumleta humu kumtesa, kwa hivyo nikapiga simu polisi. Baada ya yote, kila mtu anapaswa kuhojiwa na kutolewa hukumu na mahakama ili kuhukumiwa, sivyo?”

"Uko sahihi, na umefanya jambo sahihi." Polisi alitikisa kichwa. Akamtazama Logan aliyekuwa ametapakaa damu. Alionya, "Hakuna mtu anayepaswa kutoa adhabu isiyo ya kisheria kwa mwingine. Ingekuwa hivyo, ulimwengu si ungekuwa katika machafuko?”

Uso wa Alvin ulizidi kukunjamana kutokana na hasira. Hakutarajia kamwe Lisa angekuwa mjanja kiasi hicho. Kweli aliita polisi kabla?.......ITAENDELEA.....

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA..