JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................421-422
Sura ya: 421
Mara Alvin alipoingia kwenye kiti cha dereva, akawasha gari na kuondoka. "Babe, mambo yameendaje huko Ngosha Corporation leo?"
"Hakuna jipya sana. Mambo ni yaleyale tu ya ajabu.” Lisa alisema kwa uchovu. “Ngosha Corporation na Campos Corporation tayari wameamua kuanzisha ubia, na pesa nyingi zimewekezwa. Wana tamaa sana.”
Familia ya Campos ilikusudia kuanzisha kampuni kubwa zaidi ya kifedha nchini Kenya. Kama mambo yangeenda sawa, kampuni tanzu za kifedha za KIM International zingeweza kupikuliwa hivi karibuni. Familia ya Kimaro imekuwa haifanyi maendeleo yoyote katika biashara ya fedha miaka ya karibuni.
Alvin akavaa miwani yake ya jua. “Lakini… Familia ya Ngosha haina ufahamu wa kutosha wa biashara ya fedha hata kidogo. Je, huogopi kwamba familia ya Campos itakuwa tegemeo lenu ikiwa mtaingia katika sekta ya fedha kwa haraka hivyo?”
"Nilikuwa na mawazo kama hayo pia. Lakini wanahisa tayari wameonja mafanikio matamu wakati wa ushirikiano wao wa awali na Kampuni ya Campos kwenye biashara ya mtandaoni. Wameonjeshwa asali kiduchu sasa wanataka kuchonga mzinga kabisa. Wamedanganywa na kujazwa na tamaa. Melanie hata alimshawishi babu yangu arejee kazini.”
Lisa akahema. Alikuwa amepoteza nguvu nyingi sana dhidi ya Sarah kwa wiki chache zilizopita ma kuwasahau Melanie na baba yake hivyo kuwapa nafasi ya kuibuka tena.
"Ingawa Mzee Ngosha amestaafu kwa miaka mingi, bado ana heshima katika familia ya Ngosha," Alvin alisema. “Melanie ni mjanja sana.
Ikiwa Mzee Ngosha atarudi, atakuwa tegemeo lake kubwa. Kulingana na maoni ya babu yangu, Mzee Ngosha ni… mkaidi kidogo, mjinga, na mwenye majivuno. Kwa kweli, yeye ni mtu anayejiona kuwa ana uwezo mkubwa lakini hana uwezo huo katika uhalisia. Lakini, hakuna mtu anayeweza kumkosoa.”
Lisa aONA aibu. Kama ilivyotarajiwa, maoni ya Mzee Kimaro yalikuwa ya moja kwa moja na sahihi. "Unafikiri Jerome ni mtu wa aina gani?"
Alvin alipapasa usukani na kusema. "Yeye ni mwenye tamaa, na anaweza kufanya lolote ili kufikia lengo lake. Kulingana na ufahamu wangu wa mbinu za kawaida za familia ya Campos, wao si waaminifu hata kidogo. Hawapo katika kusaidia Ngosha Corporation. Wanataka ushirikiano huu kwa sababu wanafikiri wanaweza kuvuna faida kubwa kutoka kwao. Ubia huu, utainyonya Ngosha Corporation na kuineemesha familia ya Campos.
"Ni wakati tu atakapoinyonya Ngosha Corporation ndipo ataweza kushindana na familia ya Kimaro bila kujizuia."
Lisalishtuka sana na kukaa kimya kwa muda. Alipoona ukimya wake, Alvin alifikiri alikuwa na wasiwasi. Kwa hiyo, alicheka na kusema, “Usifikirie sana kuhusu hilo.
Ingawa wewe ni mrithi wa Ngosha Corporation, urithi wako utakuwa na nguvu tu wakati Ngosha Corporation iko mikononi mwako. Jina lako la mwisho ni Jones. Kwa macho ya wazee wawili wakaidi wa familia ya Ngosha, bado wewe ni tofauti ukilinganisha na Melanie na Damien, ambao wamewalea. ”
“Najua. Ndio maana sijisumbui sana juu yake. Kwa kuwa babu yangu anasisitiza kushirikiana na familia ya Campos, basi sitaingilia mambo yao, nisije nikapoteza pande zote mbili.” Lisa aliinua mabega yake bila wasiwasi. "Kusema ukweli, sina uhusiano wowote na familia ya Ngosha na kampuni ya Ngosha."
“Mm, huna haja ya kujali sana Ngosha Corporation. Kwa kuwa utakuwa mke wangu siku zijazo, na KIM International yote itakuwa yako. ” Alvin alimshika mkono ghafla. "Una mtu tajiri zaidi wa Kenya mikononi mwako."
"Sahau. Baada ya yote, wanawake wanapaswa kujitegemea wenyewe. Labda… utaniacha tena. ” Lisa alitoa mkono wake. Macho yake yalikuwa chini kuficha aibu machoni mwake.
“Ni sawa kama huniamini. Nina muda mwingi wa kukuthibitishia hilo.” Alvin alitabasamu kwa utulivu.
Lisa alimtazama kwa pembeni na kumuuliza. "Huna wasiwasi kwamba familia ya Campos itakuwa familia tajiri zaidi Kenya baada ya kuichukua Ngosha Corporation?"
"Hapana. KIM International tayari imewekeza fedha nyingi katika utafiti na maendeleo kwa miaka michache iliyopita. Tayari tumepata mafanikio muhimu pia. Tutapanda juu zaidi katika siku zijazo." Alvin alitabasamu kwa kujiamini. "Familia ya Campos inapata pesa kutoka kwa soko la ndani, wakati KIM International inalenga soko la kimataifa. Hawawezi kamwe kutuzidi.”
Lisa alipigwa na butwaa. Bado alikuwa na sura ile ile ya kupendeza, lakini mng'aro wa kujiamini machoni mwake wakati huo kwa kushangaza ulimfanya kupoteza sauti yake. Ingawa kijana huyo alikuwa mpuuzi, ilimbidi akubali kwamba alikuwa mfanyabiashara mahiri. Hakuna mwanamke ambaye angeweza kupinga kuvutiwa naye.
Dakika arobaini baadaye, gari lilienda kwenye mgahawa mashuhuri katikati ya jiji. Mambo ya ndani ya mgahawa yalikuwa ya kigeni sana.
Alvin alikuwa tayari ameweka oda mapema na kukuta meza yao imeshaandaliwa. Kulikuwa na hata mtu anayecheza gita karibu na meza yao.
Lisa alifurahia sana chakula hicho. “Nimeona nyie ni wastadi sana wa kuchagua mahali pa kula. Mgahawa ambao Sam na Joseph walinipeleka mara ya mwisho ulikuwa mzuri pia.
Moyo wa Alvin uliingia uchungu mara moja. “Wakati ujao, huruhusiwi kwenda kula chakula peke yako na watu wa jinsia tofauti, hasa Joseph. ”
“Kuna nini kuhusu Joseph? Ni rafiki yangu mkubwa.” Lisa alicheka. "Kama si yeye, Mawenzi Investiments ingekufa kwa sababu yako."
Alvin aONA aibu. Sawa, angeweza kujilaumu tu kwa kufanya mambo mengi ya kihuni na kujipa shida mwenyewe bila kujua. “Ahem. Nilichomaanisha ni wakati mwingine Joseph atakapokuja… tunaweza kwenda kula naye pamoja. Nitamfanyia chakula ili kumshukuru kwa kuokoa kampuni ya babe wangu mzuri.”
“Mradi unalijua hilo." Lisa alimsukumia sahani nzima ya samaki amchambulie miiba. “Unajua kwanini wanawake wana wapenzi? Ni kuwafanya wafanye mambo ya aina hii.”
Alvin aliumwa na kichwa akiitazama ile sahani. Kwa kawaida, yeye mwenyewe alimmega samaki mara moja tu kila upande kwa uvivu wa kuchambua miiba.
Hata hivyo, alikuwa tayari kufanya hivyo ili kumfurahisha Lisa.
Wakati wa mchakato huo, hata alijichoma kidole chake na kikavuja damu.
“Wewe ni kweli… mzembe.” Lisa alikishika kidole chake na kukitazama kwa muda kabla hajakiweka mdomoni.
Alvin alishtuka. Wakati huo, ilikuwa ni kama volkano ilikuwa karibu kulipuka mwili wake. Pumzi zake zikawa nzito huku akiutazama uso wake mzuri, mdogo kwa macho ya joto.
Alishuku kwamba alikuwa akimtania kimakusudi.
Midomo ya Lisa iliacha kidole chake tarataibu. Hakusahau kumtazama kwa jicho la uchochezi. Hata hivyo, wanaume walipaswa kuchezewa mara kwa mara na kupewa mahaba fulani. Ikiwa sivyo, angeachaje hisia nzito kwake?
Alvin alitazama bila kujali kidole chake kilichoacha kuvuja damu. Baada ya muda kidogo, akainua mwiba wa samaki na kujichoma kidole chake kingine. Kisha, akampa kidole chake. "Kinatoka damu tena."
Je, alifikiri alikuwa kipofu? Alikuwa amenogewa, eeh? “Mhudumu.” Lisa aliinua mkono wake na kumpungia mkono mhudumu. “Tafadhali niletee chumvi.”
Alvin alikunja uso. Kwanini ilikuwa tofauti na vile alivyofikiria? “Mbona hunyonyi? Damu inazidi kutoka.”
“Ni sawa. Itakata tukinyunyiza chumvi juu yake baadaye. ” Lisa alitabasamu kama mbweha mjanja.
Alvin aliuliza kwa kukata tamaa. "Kwanini mwanzo ulininyonya na sasa unakataa?"
“Mimi ni kichaa? Watu watafikiri mimi ni kichaa nikiendelea kukunyonya vidole unavyojitoboa makusudi. Isitoshe, huna vijidudu mikononi mwako?” Lisa alishindwa kujizuia kucheka.
Mara Alvin akanyamaza kimya kutokana na kuzodolewa.
Kwa kuwa hakuweza kunyonywa tena, aliweza tu kuizuia damu kwa kitambaa.
"Sahau. Acha nifanye mwenyewe. Mpenzi wangu hana maana tena. Hawezi hata kutoa miiba kwenye samaki.” Lisa alipumua na kuanza kujichambulia samaki mwenyewe.
“Acha, nitakuchambulia.” Baada ya kupata kipigo kingine cha maneno, Alvin aliendelea kuwachambua samaki kwa utiifu. Alijiona anazidi kuwa mnyenyekevu mbele ya Lisa.
Hata hivyo, alipokumbuka tukio la mwanamke huyo kunyonya damu kutoka kwenye kidole chake, moyo wake ulipiga kwa kasi.
Sura ya: 422
Muda si mrefu Chester akaingia na Cindy. “Alvin, ni wewe kweli. Nilidhani nimekosea. ” Chester alikuwa ameweka mikono mfukoni. Uso wake wa kiungwana ulijawa na mshangao.
Mara nyingi walipokuwa wakila pamoja siku za nyuma, Sarah mara zote alikuwa pamoja na Alvin, na Chester hakuwahi kumwona Alvin hata akimsogezea tu Sarah sahani ya chakula. Alishangaa kumuona Alvin kaatamia sahani ya samaki akichambua mifupa na kumlisha Lisa minofu kama vile angefanya kwa Suzie.
Cindy alizidi kushangaa. Alijua jinsi Alvin alivyokuwa kauzu wakati wa mikusanyiko ya kawaida, hivyo hakuwahi kutarajia kwamba angeweza kumtendea Lisa vizuri. Cindy aliuma meno kwa siri kwa wivu. Aliamini Alvin hakika angemwacha Lisa. Hata hivyo, mwishowe, ni Sara ambaye hakuwa na maana tena, na alikuwa amepoteza miaka mitatu ya wakati wake kujipendekeza kwa Sarah bure kabisa.
“Bwana Kimaro…” Cindy alijifanya kana kwamba yuko kwenye hali ngumu. “Sikuamini nilipokuwa nikitazama kwa mbali, lakini wewe. ..
Unaongozana na Lisa. Je! Sarah anajua kuhusu hili? Bado amelazwa hospitalini. Hii ni sawa kweli?”
Alvin alimpiga jicho kali kama mwiba. Cindy alishtuka kana kwamba kisu chepesi kimepita usoni mwake. "Samahani. Mimi…ninaweza kuwa naingilia sana mambo yako. Labda ni kwa sababu nina uhusiano mzuri na Sarah. Anatia huruma sana sasa. ”
Lisa akachukua maji taratibu. “Ninaona uhusiano wako na Sarah umekuwa mzuri sana siku zote. Vinginevyo, ulijuaje kwamba Alvin alirudi nyumbani kwa Sara baada ya kutoka kula bata kila siku miaka mitatu iliyopita? UONA hata kikwaruzo kwenye shingo ya Sarah siku iliyofuata.
Uso wa kila mtu ulibadilika. Macho ya kina Chester yalikuwa yakimtazama Cindy, na sura nzuri ya Alvin nayo ilikuwa imebadilika kuwa ngumu. “Ni lini… niliacha mikwaruzo kwenye shingo ya Sarah?”
Alvin hakuwahi hata kumgusa Sarah kabisa. Angewezaje kuacha alama za mabusu shingoni mwake?
Cindy alijilazimisha kutulia na kusema, “Lisa, sijui unazungumza nini.”
“Kwa kweli, ninakushukuru sana,” Lisa alisema. "Kipindi hicho, nilikuwa mjamzito na niliwekwa kizuizini na Alvin hadi nilipolazimika kwenda kufanyiwa uchunguzi wa ujauzito. Isingekuwa wewe, nisingejua kuwa vyombo vya habari vilisambaza habari za Pamela kuzagaa mtandaoni. Na hata nisingejua kuwa Thomas alitangaza hadharani kuwa Pamela ndiye aliyemtongoza. Hilo lilinikasirisha sana hivi kwamba nilirudi na kuvunja kila kitu nyumbani. Niligombana na Alvin, jambo ambalo lilisababisha anisukume chini, nikatokwa damu nyingi na kisha mimba ikaharibika.”
Huo ndio wakati alipoteza mapacha. Alvin alikumbuka na sura yake ilibadilika sana. Lisa alionekana kana kwamba alikuwa na kichaa siku hiyo. Alichukua hata kisu na kujaribu kumchoma. Hilo lilimfanya ashangae jinsi gani Lisa alikuwa amegundua mambo hayo yote ikiwa alimyanganya hadi simu. Ikawa kumbe ni Cindy ndiye aliyemwambia. Kama si mdomo wake mkubwa, huenda asingepoteza watoto wake wote wawili.
"Kwa hiyo ilikuwa ni wewe?" Alvin alisimama ghafla. Akauvuta mkono wa Cindy na kumkandamiza kwenye meza kwa nguvu. “Nani alikuruhusu kuongea hivyo? Ulimi wako unakusumbua? Ikiwa ndivyo, nitaukatilia mbali.”
Baada ya kuongea, alichukua kisu kutoka mezani.
Macho ya Cindy yalimtoka kwa woga, mwili mzima ukamtetemeka. “Sikufanya hivyo. Mimi sina hatia. Chester, niokoe.”
“Alvin.” Chester akamshika mkono Alvin. “Tafadhali nifanyie upendeleo.”
“Unajua ni mdomo wake ulinifanya nipoteze watoto wangu?” Macho ya Alvin yalikuwa makali.
"Achana naye. Usisukumie lawama kwa wengine." Lisa alijifuta mdomo kwa kitambaa kabla hajamuombea kwa ghafla Cindy. “Cindy alikuwa ananiambia ukweli tu. Wakati huo, nilishukuru sana. La sivyo, ningewekwa gizani kama mjinga. Kwa kuwa sasa watoto wamekwenda, si kosa la mtu mwingine bali letu.”
Mwili wa Alvin ukakakamaa kwa aibu. Alijua alitaka kusema kwamba kupoteza watoto wao lilikuwa kosa lake hasa. Thomas ndiye aliyekuwa kichochezi, na ndiye aliyeongeza chumvi kwa jeraha.
Chester alichukua kisu kutoka kwa Alvin na kumtoa Cindy mikononi mwake.
“Alvin, tutapanda juu kula chakula chetu. Hatutakusumbua.” Chester alimshika mkono Cindy na kuondoka. Cindy bado alikuwa amedhoofika magotini. Hakuwahi kufikiria kuwa Alvin angekuwa wa kutisha namna ile.
Hata hivyo, hakuwa na shukrani hata kidogo kwa Lisa kwa kumuokoa muda huo. Kama Lisa asingesema maneno hayo, Alvin asingechukia na kumshikia kisu. Kwa siri aliutazama uso wa Chester mzuri, lakini usio tabirika, na hisia za chuki zikaongezeka ndani yake.
Walipoingia kwenye chumba cha faragha, Chester alifunga mlango kwa nguvu na kuwasha sigara. Kulikuwa na athari ya uhasama kwenye uso wake wa kiungwana. “Cindy, huo mdomo wako utaniletea shida siku moja.”
“Chester, samahani. Lisa, Pamela, na mimi ni marafiki wazuri. Nilifikiri kwamba wakati huo alikuwa anasikitisha sana, kwa hiyo sikuweza kujizuia kusema ukweli,” Cindy alieleza huku machozi yakimtoka.
"Acha uongo wako. Usinichukulie kama mjinga.” Chester aligonga uso wake kwa upole. Alitoa dokezo la ukali na uadui. “Ikiwa unawajali sana, kwanini umekuwa karibu sana na Sara katika miaka mitatu iliyopita? Kwa upande mmoja, unamhurumia Sarah, na upande mwingine, unasema Lisa na Pamela ni marafiki zako. Naam, moyo wako unawahurumia watu wengi sana?” Sauti yake ilikuwa tulivu, lakini kwa Cindy, ilisikika kama mawimbi ya dhoruba. Ilimfanya ahisi wasiwasi.
“Ukiendelea kunizingua, nitaachana na wewe mara moja, nadhani unanijua vizuri.” Chester alimwonya kwa ukali, “Afadhali ukae kimya kuanzia sasa na ufunge mdomo wako. Ikiwa sivyo, usifikirie hata juu ya kuigiza kwenye filamu niliyokuunganisha.”
Akiwa na uso uliopauka, Cindy alitikisa kichwa kwa utii. Lisa alikuwa ameharibu kabisa sifa yake kwenye muziki mara ya mwisho. Kando na kushindwa kuonekana katika maonyesho kadhaa katika miezi michache iliyopita, bado alikuwa amepokea ofa ya kuigiza kwenye filamu mpya. Kwa hivyo, alikuwa akimtegemea Chester.
“Chester, nina jambo la kusema… Lakini sijui niseme au nisiseme…” Alisitasita.
"Ikiwa unafikiri halifai, basi funga mdomo wako," Chester alifoka.
"Hapana. Naona inanishangaza tu.” Cindy akauma meno. Ilibidi amalize sentensi yake. “Alvin alimuumiza Lisa kikatili sana siku za nyuma. Alimweka kwenye kizuizi cha nyumbani na kumfanya apoteze mimba. Hata alimpeleka hospitali ya magonjwa ya akili. Ningekuwa mwanamke nisingemsamehe hata kidogo. Lakini kwa nini yeye ghafla karudiana pamoja naye tena? Anajiskia vizuri kweli?”
“Unajaribu kusema nini?” Macho ya Chester yaliganda.
Cindy alishtuka. "Ninaogopa kwamba Lisa sasa anajaribu kulipiza kisasi kwa Alvin. Hii ni silika yangu kama mwanamke. Sijaribu kumsema vibaya kwa makusudi. Ninahofia kwamba Alvin Kimaro ataumia mara tu atakapozama sana kwenye uhusiano."
“Nenda kaagize chakula.” Chester alimpiga jicho kali. “Achana na mambo ya watu wengine.”
“Sawa.” Cindy aliitikia kwa kichwa na kutoka nje kwa haraka kwenda kumuita mhudumu.
Chester akavuta sigara yake. AONA ni ajabu pia kwa kile Cindy aliongea. Kimsingi alikubaliana na mashaka ya Cindy ila hakutaka kuyajadili mambo hayo pamoja naye.....ITAENDELEA....
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
