JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................423-424
Sura ya: 423
Gari liliegeshwa kwenye eneo la maegesho lambele ya nyumba ya Lisa huko Karen Estate. Lisa alifungua mkanda wake wa kiti. Wakati anakaribia kuteremka kwenye gari, ghafla Alvin alimshika.
Koo lake likamtoka, lakini hakujua la kusema. Walikuwa na wakati mzuri wakati wa chakula. Hata hivyo walinyamaza baada ya Cindy kuja na kuvuruga mambo.
“Lisa, samahani…” Alvin alijawa na majuto. Ikiwa angejua kwamba alimpenda, asingeweza kamwe kuwa mkatili wakati huo. “Bado unanichukia?”
“Itakuwa uwongo ikiwa nitasema sikuchukii.” Macho ya Lisa yalitetemeka. Kulikuwa na dalili ya uchungu machoni pake. “Kila nikifikiria wale watoto wawili nilipokuwa ng’ambo, nilitamani kukutafuna ukiwa hai. Niliporudi, nilidhamiria kuwafanya wewe na Sarah mteseke. Lakini uliponilazimisha kupata talaka, niligundua bado sikuwa na uwezo wa kwenda kinyume na nyinyi. Na sasa uko hapa, unanibembeleza. Ninahisi mgongano na wasiwasi. Wakati mwingine nataka kurudiana pamoja nawe tena, lakini wakati mwingine ninaogopa sana…”
Alvin alimvuta kwenye kumbato lake kabla hajamaliza sentensi yake. Akamkumbatia kwa nguvu. “Haitatokea tena. Niamini. Sitakuumiza tena. Nilikasirika mara ya mwisho, Lisa. Hebu tuwe na mapacha tena katika siku zijazo, sawa?"
Lisa alicheka huku macho yake yakiwa chini. Alisikika akiwa hoi. “Unafikiri bahati inaweza kujirudia? Unadhani ni rahisi hivyo kuwa na mapacha?”
'Basi, tutakuwa na watoto wawili. Binti yetu hakika atakuwa mrembo kama Suzie. ” Kwa namna fulani, Alvin aliposema hivyo, ghafla alitamani kupata mtoto wa wao wawili.
“Suzie…” Lisa alitamani kuchekai. Suzie alikuwa binti yake tangu mwanzo.
Hata hivyo, hangeweza kamwe kumruhusu Alvin ajue. Mtu kama yeye hakustahili kuwa baba wa mtoto. "Tutazungumza juu ya hili tena siku nyingine." Alitazama juu. “Usiku wa leo hukula sana. Una njaa? Ninaweza kwenda ghorofani na kukutengenezea rchakula cha fasta.”
Macho ya Alvin yakaangaza. Alifikiri kukumbuka yaliyopita kungeweza kumkasirisha. Yeye, pia, alikuwa na wasiwasi sana, lakini hakutarajia bado angejali tumbo lake. Hasa alipomwalika kwa chakula usiku kama huo, hakutaka kuipiga teke bahati hiyo.
Mara walipofika ghorofani, Lisa alitumia mchele uliobaki jana yake na kumtengenezea Alvin mseto wa wali na njegere. Pia kulikuwa na karoti, hoho, na nyama ndani yake. Chumba kizima kilijaa harufu ya chakula. Alvin alifuta sahani nzima ya mseto.
“Babe, mbona upishi wako ni mtamu sana?” Alvin alilalamika tena. "Nataka kula chakula chako tu kwa maisha yangu yote."
“Ndio. Wakati fulani ulipata nafasi hiyo, lakini ukanifukuza.” Lisa aliinuka na kukusanya sahani. "Rudi nyumbani, usiku umeenda.”
Alipogeuka, Alvin alikuja kwa nyuma na kukaza mikono yake kiunoni.
“Sitaki kurudi nyumbani. Nataka kubaki hapa. Naweza kulala kwenye sofa.”
"Alvin, mimi sio mwanamke mwingine yeyote," Lisa alisema kwa upole. “Nilipolala na wewe hapo awali, nilichoambulia ni kufedheheshwa na vidonge vya kupanga uzazi. Wakati huu, nataka kujipenda zaidi. Sitaki kujitoa kirahisi hivyo.”
Alvin alikosa la kusema. Ilikuwa ni kosa lake kwa kufanya mambo mengi ya kihuni. Ikiwa angejua kuwa siku kama hiyo ipo, angerudi nyuma na kujipiga mara kadhaa.
“Sawa, nitaenda. Lakini nataka busu." Alvin bila aibu akamgeuza na kumbusu midomo yake.
Lisa alikuwa na upinzani kidogo mwanzoni, lakini polepole, alishika kiuno chake. Busu la Alvin lilikuwa refu na la moto. Busu lilipoisha, alisukumwa nje ya mlango huku macho yake yakiwa yamejawa na matamanio. “Babe, nitakuletea kifungua kinywa kesho, sawa?”
“Sawa.” Lisa kisha akafunga mlango, akakimbilia bafuni na kupiga mswaki na kujisafisha vizuri.
Wazo tu la mdomo wake kumbusu Sarah kabla lilimjaza karaha.
Alvin alikuwa kinyume chake. Mdomo wake ulikuwa mtamu kana kwamba anakula asali tu.
Hata baada ya Hans kuendesha gari ili kumchukua, aliendelea kufurahia ladha kinywani mwake.
Kwa bahati mbaya, busu ilikuwa fupi sana. Ilikuwa ni dakika tano au sita tu. Ingekuwa bora kama ingedumu kwa muda mrefu zaidi.
"Bwana Kimaro, unaonekana kama uko katika hali nzuri." Hans alijua, kwa hiyo alitania kwa ujasiri, “Kama kijana ambaye ametoka tu kukutana na mpenzi wake wa kwanza.”
“Kama?” Alvin alikunja uso kwa kutoridhika. "Kwani mimi si kijana?"
Kama mwanamume katika mapenzi, alijali sana umri wake, haswa kwani Lisa alikuwa mdogo kwake kwa miaka mitano au sita.
“Aha, nilikosea.” Hans aliomba msamaha kwa haraka. “Ninachomaanisha… umebadilika kidogo, Bwana Mkubwa. Hakukuwa na hisia za aina hii ulipokuwa ukichumbiana na Bi. Njau.”
“Uko sawa.” Alvin naye alitambua hilo, lakini hakuweza kuelewa. Siku zote alikuwa akikumbuka kwamba alimpenda Sarah. Ingawa alipokuwa naye, hakuwa na furaha kila wakati.
Midomo ya Hans ikasogea. Hapo awali alitaka kumwambia kwamba Alvin alifanyiwa Hypnosis na Sarah, lakini alighairi alipofikiria juu yake. Mwanasaikolojia alisema iwapo angejaribu kupata nafuu huenda ingeharibu ubongo wake na kumfanya awe mpumbavu. Aliamua kuacha tu. Angalau kila kitu kilikuwa kikienda vizuri.
Wakati huo Chester alimpigia simu Alvin. “Miadi imekwisha? Njoo tuzungumze.”
Alvin alitazama muda akakubali kabla hajampeleka Hans kwenye baa aliyokuwepo Chester. Alipofika, Chester pekee ndiye aliyekuwepo.
"Yule mwanamke aliondoka?" Alvin aliketi kando ya Chester. “Chester, utaendelea kumvumilia huyo mwanamke? Sijawahi kuwa na hisia nyingi za Cindy, lakini baada ya usiku wa leo, niligundua kuwa yeye sio mzuri. Hastahili kuwa na wewe.”
"Kuna mambo ambayo hayawezi kusaidiwa." Chester akanywa mvinyo. Macho yake yalikuwa ya kina. " Na wewe je? Unarudiana na Lisa kweli?"
“Ndiyo.” Alvin alikuwa katika hali nzuri usiku huo. Kwa kweli, ingeweza kuwa bora zaidi ikiwa hakukutana na Cindy katikati.
Chester alimtazama kwa wasiwasi. “Umewahi kufikiria ikiwa Lisaanataka kwa dhati kuwa na wewe au ... kulipiza kisasi kwako?”
Uso wenye furaha na mzuri wa Alvin uliganda mara moja. Alvin akaweka glasi yake ya divai, na ukali wa kutisha ukaangaza machoni pake.
Ikiwa ni mtu mwingine yeyote, angeweza kuwa na hofu. Hata hivyo, Chester alimfahamu tangu wakiwa watoto, hivyo alimuelewa.
Chester aliendelea na uso ulionyooka, “Fikiria ulichomfanyia siku za nyuma kwa sababu ya Sara. Ulimweka kwenye kizuizi cha nyumbani, ulimlazimisha talaka, ulimsukuma chini, ulisababisha kupoteza watoto wake, ulimpeleka hospitali ya magonjwa ya akili kwa matibabu, na orodha inaendelea. Unafikiri anaweza kuweka kando kabisa kinyongo moyoni mwake hadi kusiwe na chuki iliyobaki?”
Kope za Alvin zililegea kwa kila jambo Chester alisema. Kifua chake kilihisi kama kinapigwa. Ikiwa Chester asingemdokezea, asingethubutu kukumbuka kwamba alifanya mambo mengi ya kumuumiza.
"Unafikiri anajaribu kunirudia kwa ajili ya kulipiza kisasi?" Alvin aliuliza kwa sauti kubwa baada ya muda mrefu.
“Siyo jambo lisilowezekana.” Chester akampiga bega. “Nakukumbusha tu kuwa makini. Usizame ndani sana hadi ukajisahau. Ninahisi ana nia ya kulipiza kisasi kwako.”
Sura ya: 424
Glasi iliyokuwa mkononi mwake ilipasuka ghafla, na damu nyekundu nyangavu ikatoka na kuchanganyikana pamoja na ile pombe. Uso mzuri wa Alvin ulikuwa na huzuni. “Haiwezekani. Ananipenda. Naweza kuhisi. Sikumpenda mara ya mwisho na ndiyo maana nilienda mbali zaidi, lakini nitampenda kuanzia sasa. Nitampa kila la kheri kwa moyo wangu wote.”
"Vema, ikiwa ndivyo unavyofikiria, basi hakuna ninachoweza kufanya. Nimesema kinachopaswa kusemwa. ” Chester alipomuona hivyo alikoroma na kumpa kitambaa. "Sema, kwanini wewe na Rodney mligombana kwa sababu ya mwanamke? Kuna maana gani? Kwa bahati nzuri, mimi sipo kama nyinyi wawili."
“Ha! Kweli, ni nani aliyetuita tuende kunywa pombe usiku kucha alipogundua kuwa Charity alikuwa akitoka na mwanaume mwingine?"
“Usinitajie jinala huyo mwanamke.” Macho ya kina Chester yaliangaza kwa karaha.
“Sawa. Hata hivyo, tayari amekufa. Hakuna maana hata kumjadili." Alvin alichukua kitambaa na kufuta damu mikononi mwake.
“Umesikia kuhusu lolote kuhusu Rodney? Anaendeleaje sasa?”
“Kushindwa kuinunua Umoja Group imekuwa pigo kwake, lakini hatujui mengi kuhusu mambo ya vipodozi, kwa hivyo hatuwezi kumsaidia lolote." Chester akahema. “Kama angesikiliza ushauri wangu, ningemwambia akubali tu ndoa ambayo Babu Derek amepanga, lakini anakataa. Pengine ni kwa sababu anataka kumuoa Sarah kwa vile wewe umemtema.”
Alvin hakuchangia lolote kwenye hilo, badala yake aliinuka na kuaga, “Naondoka. ”
Ndani ya gari, akainama kwenye siti akiwaza. Je, kweli Lisa atalipiza kisasi kwake? Je, iliwezekana?
•••
Siku iliyofuata, Alvin alipeleka kifungua kinywa asubuhi na mapema. Lisa alipokuja kufungua mlango, alikuwa bado amevaa pajama ya hariri na uso wake ulikuwa wa kusinzia.
“Alvin, ni saa kumi na mbili asubuhi. Mbona umefika hapa mapema hivi?” Lisa alishangaa.
“Sio mapema. Niliamka saa kumi na moja asubuhi” Alvin alimtazama kifuani, na mashetani yake yakaruka, na mara moja akamsukumia Lisa ndani, akaingia na kufunga mlango.
“Mbona unanisukumia ndani kwa nguvu?” Lisa alishangaa kwa msukumo ule.
“Sitaki mwanamume mwingine atokee akuone ukiwa hivi. Mwili wako unavutia sana.” Hakutaka wanaume wengine wamuone akiwa amevaa kinguo cha kulalia.
“Leo hii unaona wivu mwili wangu kutazamwa na wanaume wengine, lakini ulipokuja kudai talaka kwa nguvu ulimwacha Maya anivue nguo mbele ya wanaume wa ONA.” Lisa alisimama na kumtazama kwa mshangao.
“Haiwezekani kitu kama hicho.” Alvin alibisha.
“Kweli kabisa Alvin, wewe ni wa kunifanya mimi nidhalilishwe na mlinzi kabisa? Halafu leo hii unasimama mbele yangu na kusema hutaki wanaume wengine wauone mwili wangu?”
“Babe, nimeleta kifungua kinywa. Kwanini usikae ule kwanza kwa amani?” Alvin alimsihi. “Maya ni mtu mdogo sana, kama kweli alifanya hivyo, nitamshughulikia baadaye.”
“Lazima nione unamshughulikia vinginevyo sitaamini kama kweli mapenzi yako kwangu ni ya kweli.”
Asubuhi na mapema, kulikuwa na kijibaridi sana ambacho kilitamanisha mambo fulani. “Nenda ukabadili nguo. Usijaribu uvumilivu wangu.”
Alvin alimwambia kisha, akageuza uso wake na kutazama pembeni.
Lisa alitazama chini, na pembe za mdomo wake zikainua. Ingawa anapaswa kuona haya, alikuwa ametumia hila hii hapo awali walipokuwa wakiishi pamoja huko Dar es Salaam ili kumshawishi Alvin. Heh. Alvin alipagawa kana kwamba hajawahi kuona mwanamke hapo awali.
Aliingia chumbani kwake na kupitiliza bafuni kunawa uso, kisha akatoka nje baada ya kubadilisha nguo zake.
Alvin aliketi kwenye meza ya chakula pamoja na kifungua kinywa alichonunua kutoka kwa mgahawa maarufu wa kifungua kinywa.
"Nimefurahishwa na mpishi bora zaidi katika mgahawa wa ‘Wasp & Sprout’ aliyeniandalia kiamsha kinywa hiki. Kuna ‘ricotta pancakes’, toast ya parachichi, baby spinach bacon salad, double cappuccino, hot chocolate…” Alvin aliziorodhesha moja baada ya nyingine.
“Mh! Kifungua kinywa cha kizembe kama nini!” Lisa aliweza kuhisi kwamba kilikuwa kitamu kwa kunusa tu harufu yake tu. Kwa hiyo, akachukua uma na kuanza kula. Baada ya kula kwa muda, aligundua kuwa Alvin hakuwa amegusa chochote.
“Mbona huli?”
“Sina hamu ya kula. ” Alvin alikuwa anasema ukweli. Hakupendezwa na kitu chochote zaidi ya chakula chake cha nyumbani.
“Hiyo si sawa. Unapaswa kula kifungua kinywa. Nitakulisha.” Lisa aliinua uso wake, kisha, akaweka kipande cha pancake mdomoni mwake na kumwelekea.
Alvin alishusha pumzi. Alikuwa karibu naye kiasi kwamba aliweza kuona kope zake ndefu. Alikuwa akitumia mdomo wake kumlisha.
Alvin awali hakuwa na hamu ya kifungua kinywa kile, lakini koromeo lake likacheza ghafla. Aliinamisha kichwa chake na kuuma kwenye nusu nyingine ya keki ile.
“Sasa ni kitamu?” Lisa alimtazama kwa tabasamu. Ni kana kwamba mwanga wa jua wa asubuhi ulikuwa unamulika machoni pake.
"Ni kitamu sana." Hakuweza kupinga, Alvin kisha akamvuta kwenye mapaja yake na kuuzika uso wake ndani kabisa ya bega lake. Alihisi kama Lisa alimfanyia limbwata. Walikuwa wakigombana kila siku, lakini bado alivutiwa naye kihisia kuliko mwanamke mwingine yoyote. Hata hivyo, sasa alitambua kwamba mwanamke huyo alikuwa hodari sana katika kuteka hisia zake. Ni wazi alianza kumpenda tena siku chache zilizopita. Lakini sasa, alimpenda hata zaidi.
"Lisa hata kama unataka kulipiza kisasi kwangu, bado nataka kuwa na wewe." Alvin alijizika kwenye shingo yake na kunung'unika.
Mwili wa Lisa ukakakamaa, akamtazama tena. "Unasema nini?"
"Ninahisi kama nimefanya mambo mengi mabaya na ya kihuni hapo awali." Alvin aliukunja uso wake mdogo. "Lisa, hata ukinichukia na kutaka kulipiza kisasi kwangu, sitakuacha uende."
"Alvin Kimaro, sikiliza. Ninakuchukia kweli kwa mambo uliyonifanyia, lakini moyo wangu ni mwepesi kusamehe. Sina nia ya kulipiza kisasi kwako. Ninataka tu kukurudisha kwangu. Ninataka kukuchukua na kukushikilia kwa nguvu mkononi mwangu. Sitajali hata kama Sarah atakuwa mnyonge na asiye na furaha. Wewe ndiye furaha yangu ya pekee duniani.” Lisa alimchombeza. Asingekuwa mwendawazimu kumweka wazi nia yake ya kumlipiza kisasi. Alitaka tu kumlevya kwa mahaba motomoto, akishakolea ndipo baadaye amteme ili na yeye aonje uchungu wa kuachwa na mtu anayempenda sana.
Lisa kisha akakumbatia shingo yake na kuuliza kwa macho tulivu, “Una wasiwasi kwamba ninakupenda kwa nia ya kulipiza kisasi?"
Alvin hakujua la kusema. Kwa kweli alikubali kuachana na Sarah kwa ajili ya Lisa, lakini maneno ya Chester jana yake yalimtia wasiwasi. Asingeweza kumwambia hivyo Lisa. Vinginevyo, angejisikia vibaya nakumchukia zaidi Chester.
"Najua kwamba Sara amekuwa nawe kwa miaka ishirini. Siwezi kujilinganisha naye." Lisa ghafla akainamia mikononi mwake. Nywele zake zikamsugua Alvin kwenye shingo yake, akifanya kama nyoka. “Ni kweli, kama si Sarah, ugonjwa wako usingepona. Ni kawaida kwako kuhisi hatia juu yake.”
“Mmhm. ” Koo la Alvin lilikuwa likiwashwa vibaya na nywele zake. Sasa angeweza kuelewa vizuri ni kwanini watu wengi katika nyakati za kale walichanganyikiwa na kumwaga siri zao wakati mwanamke alipokuwa mikononi mwao.
“Lakini…” Lisa alibadilisha mada. “Kuna mtu nataka kumfundisha somo. Usiponiruhusu nitoe hasira yangu, nitakuwa na shaka kuhusu hisia zako.”
“Nani tena?”
"Maya Chande." Lisa aliyatema maneno hayo mawili taratibu. Sauti yake ilisikika kana kwamba alikuwa akiuma meno.
Alvin alishtuka, lakini mara akakunja uso. “Leo umeamka na Maya? Ni kwa sababu ya maneno uliyosema mwanzoni?”
"Ndiyo." Lisa alimtazama kwa chuki. “Siku hiyo alinidhalilisha sana. Kama Hans asingemkaripia, basi angenivua suruali. Sitasahau aibu hii.”
Macho meusi ya Alvin yalikuwa baridi kidogo. Siku hiyo mambo yalikuwa yamechafuka sana. Alichokumbuka ni kwamba alikuwa ametoka baada ya kuwaamuru watafute cheti cha ndoa na aliingia tu baada ya kusikia sauti za Hans na Maya wakirumbana. Hata hivyo, aliona kwamba Lisa alikuwa mzima na amevaa kikamilifu wakati huo.
“Mbona nilikukuta umevaa kawaida tu?”
"Unamaanisha nini? Huniamini?” Lisa alitoka mikononi mwake kwa hasira. "Sina chochote dhidi ya Maya, kwanini nimsingizie mlinzi yule masikini kwa uwongo? Ikiwa huniamini, unaweza kumuuliza Hans na wale wanaume wengine wa ONA waliokuwepo siku hiyo.
Ikiwa mimi, Lisa Jones, ninakudanganya, sitakufa kifo kirahisi.”
"Sitakuruhusu kuapa juu ya jambo baya kama hilo." Sura ya Alvin ilibadilika huku akionya.
"Nina dhamiri safi kwa sababu sisemi uwongo, kwa hivyo siogopi." Baada ya Lisa kuongea, alipoteza hamu ya kupata kifungua kinywa kilichokuwa mezani. “Alvin wewe ndio unasema unanipenda na hutaki kuniacha. Lakini unapenda nini kwangu? Kulala na mimi? Huna imani nami hata kidogo. Angelikuwa ni Sarah ndiyo kafanyiwa hivi ungejisikia hatia juu yake, lakini mimi? Sistahili hilo.” Lisa alianza kukata tamaa.
“Siyo kwamba sikuamini…” Ingawa ndivyo kinywa chake kilitamka, moyo wake haukuwa na uhakika. Maya alikuwa akimhofia Lisa kwa sababu ya Sarah, kwa hivyo alihisi kwamba Lisa alikuwa akifanya hivi kwa sababu ya chuki yake binafsi.
Lakini, kwa Lisa, kusita kwake kuliongeza mafuta kwenye moto.
“Alvin, kwa nini usiende kuchunguza. Sitaki kuamini maneno yangu moja kwa moja.” Lisa aligeuka ghafla na akakunja ngumi kwa nguvu. Alikuwa na sura ya kujizuia usoni mwake. “Sitaki pia unibembeleze. Mlete tu Maya baada ya kufanya uchunguzi na kuujua ukweli." Kisha, akamvuta kutoka kwenye kiti na kumsukuma nje.
Alvin kichwa kilimuuma. Alikuwa mtamu muda mfupi uliopita, na hata alimlisha keki kwa mdomo wake.
Aliwezaje kumfukuza kwa kupepesa macho?
Alvin aliingia kwenye gari huku akifikiria sababu ya ugomvi huo. Macho yake yakawa na huzuni, na mara moja akawaita wanachama wawili wa ONA waliokuwa pale siku hiyo ofisini kwake....ITAENDELEA...
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
