JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................417-418
Sura ya: 417
Jessica alimtazama Rodney akiwa hoi. “Babu yuko serious. Unapaswa kufikiria hili kwa undani. Unaweza kwenda umbali gani bila usaidizi wa familia ya Shangwe?"
“Nimetafakari. Piga, ua, galagaza, sitaoa mtu ambaye simpendi,” Rodney alisema kwa hasira.
Sura ya Jessica ilibadilika, na alama ndogo ya huzuni ikaangaza machoni pake. Kisha, alitoka nje ya sebule na kuondoka pia.
Rodney alisimama hapo kwa muda kabla ya kutoka nje ya nyumba ya familia ya Shangwe kwa hasira.
Alipofika kwenye gari, alipokea simu kutoka kwa Meneja Mkuu Stevens. "Bwana Shangwe, ununuzi wa kampuni yetu ya Umoja Group ya Tanzania umeshindikana."
"Nini kimetokea? Hukuchukua miaka miwili kujiandaa kwa ununuzi wa Umoja Group?” Rodney alihisi hasira isiyoelezeka ikimwagika tena.
Hapo awali, alitaka kuchukua fursa ya kununua Umoja Group ili kuiwezesha Osher Corporation iingie katika uzalishaji wa shampoo na hata kuipanua zaidi kimataifa. Kwa njia hiyo, asingehitaji kuwa na wasiwasi na ushindani wa SE Group hata kidogo.
Ikiwa kampuni ilitaka kukua zaidi, ilibidi kupanua aina ya bidhaa. Alidhani kwamba kwa kuinyakua Umoja Group bila shaka ingekuwa mwanzo wa mafanikio.
Meneja Mkuu Stevens alicheka kwa uchungu.” Bwana Shangwe, Umoja Group awali ilikubali kampuni yetu kuinunua. Lakini baada ya habari kuwa familia ya Shangwe imeghairi haki yako ya urithi, Umoja Group ilizingatia. Waliogopa kwamba maendeleo ya siku za usoni ya Osher Corporation huenda yasiwe mazuri bila usaidizi wa Shangwe Corporation, kwa hiyo wakakubali kuiuzia kampuni nyingine kubwa nchini Tanzania.”
“Bullsh*t, kwani nilifika hapa kwa kutegemea Shangwe Corporation? Nilijitegemea.” Bahati haikuwa upande wa Rodney siku hiyo.
“Bwana Shangwe, jambo muhimu zaidi sasa ni kukuza umaarufu wa bidhaa ya Osher Corporation ya kutunza ngozi nchini Kenya.
Kuna uvumi kwamba Pamela na meneja mkuu wa SE Group wanapanga kushirikiana. Mara tu watakapounda bidhaa mpya, nafasi ya Osher Corporation itaporomoka. Tunaweza hata kuondolewa sokoni.”
Meneja Mkuu Stevens aliendelea, "Bidhaa zinaboreshwa na kubadilishwa haraka sana siku hizi. Tunahitaji mkemia bora na wa hali ya juu wa vipodozi. Kwa kuwa umepoteza usaidizi wa familia ya Shangwe, utakuwa kicheko miongoni mwa familia tajiri nchini Kenya mara tu Osher itakapoanza kuyumba.”
Rodney alishika simu yake kwa nguvu. Mishipa ya nyuma ya mkono wake ilikuwa ikipiga. Hakuwahi kufikiria kwamba yeye, aliyependelewa katika familia ya Shangwe, angekuwa katika hali kama hiyo siku moja.
Osher Corporation ilikuwa damu yake, jasho, na machozi. Ikiwa angepoteza Osher Corporation, angeachwa bila chochote.
"Bwana Shangwe, haijalishi ni nini, lazima umsihi Pamela arudi kwenye kampuni," Meneja Mkuu Stevens alisema kwa uchungu.
"Tumefikiria kila njia iwezekanavyo. Lakini mwaka huo ulikuwa ni wewe…”
"Nyamaza. Inatosha, nimekupata.” Rodney nusura aivunje simu yake.
Hakuwahi kufikiria kuwa ipo siku ambapo ingembidi kumsihi Pamela. Zaidi ya yote, mwanamke huyo hata aliharibu sifa yake siku chache zilizopita, lakini bado alionekana kuwa tegemeo lake. F*ck.
•••
Usiku, Lisa alikula chakula na Joel na Lucas kwenye nyumba ya familia ya Ngosha. Joel na Lucas walipojua kwamba Lisa angekaa usiku kucha, walisisimka. Jumba hilo kubwa lilikuwa tupu sana kwa wao wawili tu na watumishi wachache.
Saa 8:00 usiku, Lisa alipokuwa karibu kujaza sinki la bafuni kwa ajili ya kumuogesha Lucas, wasimamizi wa jengo iliyomo nyumba yake huko Karen Estate walimpigia simu ghafla.
“Bi. Jones, kwa mujibu wa jirani yako, kuna mwanaume amekuwa akikungoja mlangoni kwako tangu jioni hii na bado hajaondoka. Inaonekana ni… mpenzi wako wa zamani. Tuna wasiwasi kwa kuzingatia kuwa juzijuzi hapa ulivamiwa nyumbani kwako.”
“Mpenzi wa zamani?” Pembe za mdomo wa Lisa zilitetemeka. Jirani yake alikuwa amemwona Alvin akiingia na kutoka nje ya mlango wake mara chache kabla. Hata hivyo, hakuwa amejitokeza kwa muda sasa. Jirani yake lazima alihisi Alvin kama mpenzi wake wa zamani, ambaye waliachana naye.
"Ndiyo," wasimamizi walisema, "bila shaka, tunakutaarifu tu. Hatuwezi kuelewa kinachoendelea. Ikiwa kuna mzozo au usumbufu wowote, kati yenu, unaweza kuchagua kuripoti hili kwa polisi. ” Baada ya kukata simu, Lisa alipiga simu mara moja polisi.
•••
9:30 pm
Alvin aliuegemea mlango wa nyumba ya Lisa na kuitazama simu yake mara kwa mara. Kwanini mwanamke huyo alikuwa bado hajarudi wakati tayari ilikuwa usiku sana? Je, anaweza kuwa kwenye miadi na mwanamume mwingine tena? Laiti Alvin asingefuatilia mahali alipo Erick kabla na kugundua kuwa anafanya kazi kwa saa za ziada kwenye kampuni yake usiku huo, asingesubiri hapo kipumbavu kwa saa saba. Hakuwahi kumngoja mwanamke kwa muda mrefu hivyo awali.
Ding. Sauti ilitoka kwenye lifti. Polisi wachache walimwendea wakiwa wamekunja uso. "Unafanya nini hapa?” Alvin alipigwa na butwaa.
“Ondoka sasa hivi au tutakupeleka kituo cha polisi.” Polisi walisema kwa uthabitii, “Mmiliki wa hii nyumba tayari imetoa taarifa polisi. Alisema wewe ni mume wake wa zamani ambaye umekuwa ukimsumbua sana hata baada ya talaka hata hathubutu kurudi nyumbani.”
“Alipiga simu polisi?” Uso mzuri wa Alvin ulitetemeka, na akatoa sura ya kutisha. Bila kujua, iliwafanya polisi wahisi kwamba alikuwa mtu mkatili na mwenye tabia mbaya.
“Acha kuongea upuuzi. Kwa hiyo asipige simu polisi na akuache umsumbue?” Polisi mmoja alianza kumsomesha Alvin. “Nimeona wanaume wengi kama wewe ambao bado wanawanyanyasa wake zao hata baada ya kuachwa. Ngoja nikushauri jambo moja. Kwa kuwa tayari mmeachana, ishi maisha yako mwenyewe. Bado wewe utajiita ni mwanamume utaendelea kumng'ang'ania mwanamke?"
"Vizuri sana." Alvin alikunja ngumi na kuelekea kwenye lifti kwa hatua ndefu.
Wakati anaingia kwenye lifti, alisikia polisi wakizungumza.
“Hasira za huyu jamaa zinaonekana ni mbaya sana. Ndiyo maana alitalikiwa na mwanamke.”
Baada ya kutoka kwenye lifti, Alvin alitembea hadi sehemu ya maegesho. Akaufunga mlango wa gari kwa nguvu na kupiga simu kwa jamaa mmoja wa ONA.
“Nitafutie eneo alilopo Lisa. Nataka kujua yuko wapi.”
Muda mfupi baadaye, alitumiwa anwani: [Lisa yuko kwenye jumba la kifahari la familia ya Ngosha.]
Uso wa Alvin ulilegea kidogo. Bahati nzuri Lisa hakuwa kwenye uchumba na mwanaume mwingine. Kama sivyo ... angeweza kumuua mtu huyo.
•••
Lisa alilala vizuri na Lucas. Asubuhi iliyofuata walipoamka ili kupata kifungua kinywa, mtumishi aliingia na kusema, “Bwana Ngosha, gari moja lilifika mlangoni mwendo wa saa nne usiku jana na limeegeshwa hapo tangu wakati huo. Mlinzi alisema taa kwenye gari ziliwashwa mara kadhaa usiku, hivyo kuna mtu ndani. Gari hilo ni toleo la kipekee.
Kwa sasa… ni Alvin pekee aliye nayo katika Kenya yote.”
Uso wa Joel ukabadilika ghafla. “Mbona anasubiri mlangoni kwetu? Sijawahi kuona mtu asiye na haya kama huyu maishani mwangu.”
Lucas alimtazama Lisa kwa woga. “Mama…”
“Usijali. Hebu tupate kifungua kinywa chetu kwanza. Nitakutana naye mara baada ya kula.” Kwa hayo, Lisa alijaza sahani za Joel na Lucas.
“Lisa, nisikilize. Kaa mbali na huyo jamaa. Erick ni mzuri pia. Unaweza kumfahamu zaidi,” Joel alimshauri kwa dhati. “Alvin ni fisadi asiyebadilika. Sarah asingepata matatizo, hata asingegeuka na kukutafuta.”
“Najua. Baba, acha Uncle Sheldon ampeleke Lucas shule, na usiruhusu mtu yeyote kujua,” Lisa alikumbusha.
Sura ya: 418
Baada ya kiamsha kinywa, Lisa alitoka kwenye lango kuu la jumba la kifahari la familia ya Ngosha.
Mara Alvin akafungua mlango wa gari na kuelekea kwake. Kwa kuwa hakuwa nyumbani kwa usiku mbili mfululizo, shati alilovaa lilikuwa limekunjamana, na kulikuwa na tongotongo usoni. Hata hivyo, hilo halikuathiri sura yake nzuri hata kidogo.
“Ulipiga simu polisi jana usiku?” Alvin alimkazia macho Lisa kwa mtazamo wa kutisha.
"Ndiyo.” Lisa alijibu kwa jeuri bila hisia yoyote ya hatia. “Uliendelea kusimama mlangoni kwangu, hukutaka kuondoka. Ulikuwa ni usumbufu mkubwa kwangu. Majirani wananiona mimi ni mtu wa ajabu sana.”
“Wewe…” kifua cha Alvin kilimtoka. Akiwa mwanamume aliyeheshimiwa sana, hakuwahi kudhalilishwa na mwanamke namna hiyo hapo awali.
“Mimi nini? Mimi si mtu ambaye umeniweka kwenye kiganja chako kama simu yako. Kwamba muda wowote ukitaka kuitumia, unaitumia tu” Lisa alimkemea kwa ukali. "Nakumbuka nilikuambia waziwazi usiku uliopita, kwamba ikiwa utaenda kwa Sarah, hupaswi kujisumbua tena kunirudia."
Lisa alipokumbuka kuwa alimtumia selfie nyumbani kwake lakini akaenda kumtafuta Sarah dakika iliyofuata, alichukizwa naye sana.
“Mimi sikuwa na chaguo. Sarah alianguka chini kutoka kwenye ngazi siku hiyo, na akaumiza mguu wake. Ikiwa nisingeenda, angekataa kutibiwa.
Mwishowe, nilienda na kumweleza mambo wazi. Unaona? Rodney hata alipigana nami kuhusu jambo hili.” Alvin alimnyooshea kidonda mdomoni. Alichoweza kufanya ni kujionea huruma huku akihema kwa maumivu. "Bado inauma sana."
"Nimekuvumilia sana Alvin, lakini hubadiliki. Wewe ni yule yule tu." Lisa alisema maneno hayo na kudharau.
Alvin alijikaza kwa muda kabla ya kusema kwa ujasiri, “Ndiyo, najua nimekuudhi babe. Uliniambia nisiende na mimi nikaenda. Lakini sikwenda kwa nia mbaya...”
“Nani babe wako? Angalia mdomo wako." Kichwa cha Lisa kilimsisimka kumuita babe wake,
Macho yake makubwa, ngozi laini, na midomo ya waridi yenye majimaji iliufanya moyo wa Alvin kuyeyuka. Iliyeyuka zaidi alipokumbuka emoji ya busu ambayo alimtumia. Alidhamiria kumfanya amsamehe siku hiyo, hata ikiwa ni lazima awe na uso wa jazba. Kisha, polepole angeonja ladha ya kumbusu. “Lisa, tayari nimeshamalizana na Sarah. Simpendi tena, na haiwezekani nirudiane naye na kumuoa.”
Alvin alishika mikono ya Lisa na kuikamata kwa nguvu. Mtazamo wake wa kina ulikuwa mzito.
Akili ya Lisa ilizunguka kwa muda.
Alikumbuka siku za nyuma aliwahi kumtazama kwa dharau na kusema kwamba aliyempenda ni Sara. Kwa hiyo, alipomsikia akisema hivyo kutoka kwa midomo yake myembamba tena, hakuhisi kuguswa. Badala yake, alifikiri ni kejeli.
“Babe, unaweza kunipa nafasi nyingine?” Alvin alifikiri kukaa kwake kimya kunamaanisha kuwa ameguswa. Kwa hiyo, alinyoosha mikono yake na kutaka kumvuta kwenye kumbato lake.
Lakini, Lisa aliweka mikono yake kifuani mwake. “Alvin, sijui nikuamini tena au nisikuamini. Nimeumizwa na wewe mara nyingi sana sasa. Ninaogopa kwamba nikianza kuwa na matarajio na wewe kwa mara nyingine, Sarah atakupigia simu tena au kukutishia maisha yake. Sijakaa nawe kwa muda mrefu, lakini wewe na Sarah mmefahamiana kwa zaidi ya miaka 10…”
“Hapana Lisa. Sitakuangusha tena.” Alvin akamkumbatia kwa nguvu. “Si unajua mimi ni mtu wa aina gani kwa sasa? Sitasema maneno kama hayo ikiwa sina uhakika wa hisia zangu.”
Uso wa Lisa ulizikwa kwenye kumbatio lake. Mahali ambapo hakuweza kuona, kulikuwa na dhihaka machoni pake. Alimfahamu vizuri sana. Aliweza kutamka maneno yoyote matamu akiwa katika mapenzi. Ndiyo maana alimwangukia tena licha ya kuumizwa naye mara kwa mara. Hata hivyo, wakati hakuwa katika upendo, alikuwa jeuri, asiye na moyo, na mkatili.
“Babe…” Alvin alipomwona Lisa bado yuko mikononi mwake, wimbi la shauku lilimpanda. "Unadaiwa kunibusu." Baada ya hapo, aliinamisha kichwa chake na kumbusu.
Mkono ulifunika midomo ya Alvin kabla hajambusu Lisa. "Nilikubusu lini?" Lisa alishangaa. Alikuwa karibu kushindwa na ukosefu wake wa aibu.
“Usiku wa kuamkia jana. ” Alvin akatoa simu yake na kumuonyesha emoji ya busu ambayo alimtumia.
Uso mzuri wa Lisa ulishtuka alipoona emoji ya busu kwenye simu. Alifanya hivyo kwa kukurupuka tu kwa nia ya kumfanya mtu huyu amtamani. Hata hivyo, hakutarajia angekumbuka vizuri hivyo.
“Oh, nakumbuka. Lakini... ulienda kumtafuta Sarah mara baada ya kupokea emoji yangu?” Aliuliza huku akitoa tabasamu bandia.
"Hapana." Sura ya Alvin ilikakamaa, na akasema isivyo kawaida, “Nilienda kuoga maji baridi baada ya kuipokea.”
Kwa kuwa walikuwa watu wazima, Lisa alijikuta akielewa maneno yake mara moja. Macho yalimtoka kwa kutoamini kabla ya moyo wake kujawa na msisimko. Hakuwa na la kusema.
Je! haikuwa emoji tu ambayo kila mtu alikuwa akitumia? Kwanini alikuwa na hisia nayo sana?
Lisa akageuza macho yake. "Ina maana kwamba utakuwa na deni langu nikikutumia emoji ya kukuchapa wakati ujao?"
“Hakika.” Alvin alitazama midomo yake kwa tamaa. Muda mrefu alikuwa akitamani kumbusu.
“Nadhani bado unaota. Siwezi kuendelea kupoteza wakati wangu na wewe. Naenda kwenye kampuni.” Lisa hakujali tena juu yake na akageuka moja kwa moja.
"Subiri, nitakupeleka ofisini kwako." Alvin akamshika mkono na kufungua mlango wa siti ya abiria.
Lisa alitupia macho kwenye kiti cha abiria. "Hapana. Sitaki kuketi mahali ambapo wanawake wengine wameketi hapo awali.” Baada ya hapo, alitembea kuelekea lango kuu la nyumba. Mlinzi tayari alikuwa amelisogeza gari lake getini.
Lisa alifungua mlango wa gari na kuingia kwenye kiti cha dereva. Hata hivyo, mara moja Alvin aliketi kwenye kiti cha abiria na kufunga mikanda yake ya usalama.
“Kaka mbona unanifuata? Lazima niende kazini.” Lisa alifoka.
“Nitakusindikiza kazini. Nataka kutumia wakati mwingi zaidi na wewe njiani." Midomo myembamba ya Alvin ilifunuliwa kwa tabasamu. "Nimegundua hata hewa ni tamu ninapokuwa na wewe."
Lisa alitetemeka. "Nyamaza."
Alvin alikunja uso huku akionekana kuwa na huzuni. Hakulala ndani ya gari usiku kucha ili tu aweze kusema maneno haya yenye mguso, ya kimahaba aliyokuwa akijifunza kwenye simu yake.
“Sawa, nitanyamaza. Lakini akili yangu imejaa sauti yako, kwa hiyo haijalishi tunazungumza au la.” Alitabasamu kwa upendo.
Kona za mdomo wa Lisa zilimtetemeka huku akiweka mkono wake kwenye paji la uso. “Vipi kuhusu gari lako la thamani? Utaliacha tu hapa?"
“Umesema hutaki kulipanda, kwa hiyo silitaki tena. Nitanunua gari jipya.” Alvin akatoa simu yake na kumpigia Hans. Alitazama nembo kwenye usukani wa Lisa na kusema, “Nipatie Aston Martin.”
"Lakini umenunua gari lako muda si mrefu uliopita." Hans alishangaa.
“Siendesha gari hilo tena. Lisa halipendi, kwa hiyo hakuna haja ya kuwa nalo.”
Hans aONA ajabu. "Lakini Aston Martin itakuwa nafuu sana? Hailingani kabisa na hadhi yako.”
"Usijali. Lisa anaendesha Aston Martin pia. Kwa kuwa anaendesha gari nyeupe, unaweza kuninunulia nyeusi. Tutakuwa na magari yanayofanana.” Alvin alikata simu baada ya kusema hivyo. Kubadilishia gari kwake ilikuwa rahisi kama vile kubadilisha mboga tu...ITAENDELEA...
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
