JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................415-416
Sura ya: 415
Kesho yake asubuhi, nyumbani kwa Lisa.
Lisa alipokuwa akiwaandalia Suzie na Pamela kiamsha kinywa jikoni, Pamela alipiga kelele kutoka nje ghafla.
Kisha, akaingia jikoni na simu yake. “Lisa, nitakuonyesha kitu. Usiwe na wazimu.”
Lisa alishika simu na kuitazama. Kichwa cha habari cha stori hiyo kilikuwa 'Sarah Ajeruhiwa, Bwana Kimaro Mara Moja Amkimbiza Hospitali. Kuvunjika Kwa Ndoa Yao-Tetesi Zilikoma.'
Alipobofya kufungua video hiyo, mwandishi alitoa maelezo ya kina ya habari hiyo. “Harusi ya Alvin Kimaro na Sarah Njau ilighairishwa ghafla hapo awali, na hakukuwa na habari kuhusu ndoa hiyo kufanyika tena baadaye. Uvumi juu ya kutengana kwao umekuwa ukienea kama moto wa nyika. Hata hivyo, mwanahabari wetu aliyekuwa akifuatilia habari hizi kwa karibu usiku na mchana, alipata taarifa kuwa Sarah alikuwa amelazwa hospitalini jana usiku. Muda mfupi baadaye, Bwana Kimaro alikimbilia hospitalini huku akiwa na sura ya huzuni, pengine kwa sababu alikuwa na wasiwasi kuhusu hali ya Sarah. Hadi saa saba usiku mwanahabari wetu alimuona Bwana Kimaro akitoka hospitalini hapo kwa uchovu.”
Lisa alizima habari hiyo moja kwa moja. Kisha, akarudisha simu kwa Pamela. Uso wake ulikuwa shwari na usio na wasiwasi kana kwamba hakuwa ameguswa na chochote kwenye habari hiyo.
"Uko sawa?" Pamela alimtazama Lisa kwa wasiwasi. Jana yake usiku, Alvin alikuwa amempa hata nyumba ya kuishi kumfanya atoke nje kumpisha Lisa, hivyo alifikiri alikuwa akisisitiza kurudiana na Lisa. Hata hivyo, bado aliishia kwenda kumtafuta Sarah. Hata mgeni kama yeye angekasirika juu yake.
"Bila shaka, sina cha kunifanya nichukie. Lakini nimemdharau mtu huyu asiye na aibu.” Lisa alicheka sana. Jana yake usiku, Alvin hata alimtumia selfie ambayo alipiga nyumbani, na kweli alimuamini.
'Wa Kwako Pekee'? Nenda kuzimu!
Naam, ilikuwa ni kofi usoni kwake. Ilimfanya atulie na kuwa macho zaidi.
“Wacha tupate kifungua kinywa. Baada ya hapo, nitampeleka Suzie shule.”
Lisa alitenga kifungua kinywa mezani. Baada ya kifungua kinywa, alimkimbiza Suzie hadi shule. Alipomshusha Suzie alikutana na Sheldon aliyekuwa akimshusha Lucas getini.
"Asante tena, Anko Sheldon." Lisa alimshukuru. Ili kumzuia Lucas asishukiwe, Joel alimwomba Sheldon ajifanye kuwa babake Lucas. Kwa bahati nzuri, Sheldon alionekana kama Joel, kwa hivyo hakuna mtu aliyemshuku.
“Unakaribishwa sana. Ni kwa sababu ya baba yako kwamba nilifanikiwa kurudi Ngosha Corporation na kuwa meneja,” Sheldon alijibu huku akitabasamu.
Lisa alitabasamu. Akainama na kumbusu Lucas kwenye paji la uso. "Lucas, hujani’miss?"
“Mimi sio Suzie.” Sura ya kiburi ilivuka uso wa Lucas. Hata hivyo, alinyoosha mikono yake kumkumbatia Lisa ili kupata upendo wa mama yake.
“Nitaongozana na wewe kula chakula cha jioni kwa babu yako usiku wa leo,” Lisa alisema kwa upole.
“Mama, nataka kwenda na mimi kwa babu” Suzie alifoka.
"Hapana. Sasa kwa kuwa wewe ni wa familia ya Kimaro, watu watakushuku ikiwa utaendelea kukaa nami kila wakati,” Lisa alimuonya.
Baada ya kuwaacha Suzie na Lucas shuleni, alipokea ujumbe wa WhatsApp kutoka kwa 'Ni Wako Pekee. [ Darling, umempeleka Suzie shule?]
Lisa aliinamisha kichwa na kuutazama. Baada ya hapo, alimblock tena.
Alvin aliendesha gari hadi ofisini baada ya kutuma ujumbe. Akiwa njiani kwenda huko, aliiangalia WhatsApp yake mara kwa mara. Hakupata jibu kutoka kwa Lisa hata baada ya kufika ofisini.
Kwa hasira, akamtumia ujumbe mwingine. [Uko bize na nini? Kwanini hujibu ujumbe wangu?]
Lakini, ujumbe wake ulionyesha tiki moja tu kwa muda mrefu, kwa maana kwamba haujaenda. Wakati huo, aligundua kuwa hakuweza kuona picha yake ya profile tena.
Alvin alikosa la kusema.
Hii ilimaanisha nini? Jana yake usiku, aliweza kuona picha yake ya profile na meseji zake zilionyesha kupe mbili. Je, alikuwa kamblock tena? Kwa namna fulani, alipata hisia inayowaka katika kifua chake, ambayo pia ilibeba dokezo la utusitusi, manung'uniko, na kuudhika.
Wakati huo huo, Hans aliingia. "Bwana Kimaro, tafadhali saini hati hii haraka iwezekanavyo."
Alvin alimkodolea macho Hans kwa huzuni. Hans alikosa la kusema.
Alikuwa amefanya kosa gani? Alichokuwa anaomba ni saini tu. Hakika, kuwa Msaidizi Mkubwa wa Alvin Kimaro ilikuwa inazidi kuwa ngumu.
"Nipe hati." Alvin alifungua mdomo wake taratibu huku akimwangalia kwa jicho la kifo.
Hans akamkabidhi. Ilikuwa tu baada ya Alvin kusaini ndipo Hans alisema, "Halafu, kuna jambo moja zaidi, Bwana Mkubwa. Umetoa habari kuwa ulimtembelea Sarah hospitalini jana usiku?” Hans akabofya habari ile na kumuonyesha Alvin. "Sasa kwa kuwa unamfuatilia Bi. Jones, nadhani akiona kipande hiki cha habari, anaweza kuhisi… kukatishwa tamaa."
“Mbona hukuniambia mapema?” Baada ya Alvin kuitazama video hiyo, uso wake uligeuka kuwa na huzuni moja kwa moja. "Ni mwandishi gani?"
“Ni ripota kutoka Udaku Live. Mtandao huu wa habari kila mara huripoti mambo madogo madogo yanayotokea katika jamii. Kila mara kuna wanahabari wanaokesha kwenye majumba ya umma, kama hospitalini, klabu, madukani, polisi na kwingineko wakiwinda habari za udaku.”
Alvin akauma meno. “Ninakupa nusu ya siku ili kufanya mtandao huu wa habari kutoweka. Wakati huo huo, hakikisha habari zote za jana usiku zinafutwa. Pia, waonye makampuni mengine ya habari kwamba yatakabiliwa na matokeo mabaya ikiwa yatathubutu kuripoti habari zinazonihusu bila ridhaa yangu.”
“Sawa.” Hans pia alihisi kuwa Udaku Live ilikuwa imejitakia kifo.
Baada ya Hans kuondoka, mara moja Alvin aliendesha gari hadi Mawenzi Investments, na kukuta Lisa alikuwa bado hajafika.
Amba alikerwa na jinsi Alvin alivyokuwa akitamba kwenye ofisi ya Lisa. Hata hivyo, kutokana na utambulisho wa Alvin, hakuwa na jinsi zaidi ya kummiminia kikombe cha kahawa ya moto. " Mwenyekiti Jones huwa haji ofisini kila siku. Yeye hufuata ratiba yake binafsi wakati mwingine." Amba alimwambia.
"Mpigie simu na umwombe aje hapa," Alvin alisema kwa sauti ya ukali.
Amba alimpigia Lisa mbele yake. "Mwenyekiti Jones, Bwana Kimaro yuko hapa na anasema kwamba anataka kukutana nawe."
“Nina shughuli nyingi sana siwezi kumsikiliza. Mwambie aende kuzimu.” Lisa alikata simu mara baada ya kumaliza sentensi yake.
Uso wa Alvin ukageuka kwa huzuni mara moja. Amba hakuthubutu kucheka kwa sauti kubwa. Kwa bahati, Alvin aliondoka muda mfupi baadaye ndipo alipoachia kicheko chake hadi mwisho.
Mchana, Alvin alikwenda hospitali tena wakati Rodney akiwa hayupo.
"Alvinic, uko hapa." Mara Sara alipomwona, macho yake yaling'aa.
Wakati habari hiyo ilipotolewa asubuhi, wale wasichana matajiri huko Nairobi ambao walimkwepa Sarah baada ya kusikia ameachana na Alvin, walianza kumpigia simu mara moja kutuma salamu zao. Wengi wao walikuja kumtembelea Sarah asubuhi, na kulikuwa na aina tofauti za vyakula na vinywaji kwenye meza.
Wakati huo, Sarah alikuwa ameridhika sana. Kwa hivyo, hakuweza kuruhusu kumwacha Alvin aende.
"Unajisikiaje?" Alvin aliuliza kwa sauti ya chini.
"Miguu yangu bado inauma. Daktari alisema mishipa yangu imejeruhiwa.” Sarah alilitazama jeraha lililo pembeni ya mdomo wake. “Samahani, Alvinic. Kwa sababu yangu, uligombana na Rodney. Hukuumia? Ngoja nikuwekee dawa.”
"Hakuna haja." Alvin akatoa hati. “Sarah, nimekuja hapa leo kukuwekea jambo bayana. Mimi…”
“Alvinic, sijisikii vizuri. Hebu tuzungumze kuhusu hilo wakati fulani baadaye.” Mara Sarah alipoona hati miliki kwenye folda, alihisi kuzama ndani kabisa. Haraka akajifanya kujisikia vibaya na kujilaza.
Sura ya: 416
"Sarah, acha kukwepa jambo hili." Alvin hakujisikia tena kuliburuza jambo lile, kwa hiyo alitenda bila huruma. "Hii ni hati miliki ya jumba la Oasis, ni lako kuanzia leo. Hapa kuna kadi yenye dola milioni 50 ndani, ambazo zinatosha kwako kuishi maisha ya anasa mpaka utakapotoweka duniani. Kwa hayo, naomba uniache huru!”
"Hapana. Sitaachana na wewe. ” Sarah alimwaga thermos ya maji ya moto kando yake kwa fadhaa na hivyo kuunguza mkono wake.
“Bi Njau…” Maya alishtuka sana hivi kwamba mara moja akabonyeza kengele kumwita daktari.
“Mkono wangu unauma. Unauma sana.” Sarah alianza kulia kwa uchungu.
Maya alimshauri Alvin, “Bwana Mkubwa, Bi Njau bado hajapata nafuu. Kwanini usisubiri hadi apone ndiyo umwingizie mambo mengine?”
Kama hili lingetokea wakati ule, Alvin angevumilia. Hata hivyo, Sarah alikataa kuukubali ukweli huo na aliendelea kuzua fujo tangu jana yake usiku. Zaidi ya hayo, Alvin alikuwa amekaa usiku kucha akifanya kazi jana yake na hakupata usingizi. Huku hisia za kila aina zikimtawala, hakuwa na subira.
“Sarah, usiende mbali sana. Hatuwezi kurudiana pamoja kamwe." Alvin aliiweka ile hati kabla hajageuka na kuondoka. Kila alipomuona Sarah akifanya vituko sasa, kwa namna fulani alikuwa na hamu kubwa ya kukimbia. Pia ilichochea nia yake ya kumaliza uhusiano wake na Sarah.
Wakati analia, Sarah alivunja vitu vingi.
Rodney alipofika, aliumia sana kuona mikono yake ikiwa imevimba.
“Rodney, Alvinic ameamua kuniacha. Alinipa vitu hivi na kuniacha.” Sarah alianguka mikononi mwake na kutokwa na machozi. “Mimi ni nani kwake? Mimi ndiye mtu ninayemjali zaidi. Sijali hata utambulisho wake wala utajiri wake.”
"Ameenda mbali sana." Kuangalia nyaraka hizo, Rodney alihisi kwamba Alvin alistahili kufa. Angewezaje kumchukulia Sarah kama jinsi Chester alivyocheza na wale wanawake huko nje? “Sarah acha kulia. Nitashughulika naye kwa niaba yako.” Rodney alikunja ngumi. “Kama Alvin atakuacha, nitakuoa. Sitakuacha uwe kicheko. Ninatoka kwa familia ya Shangwe. Ingawa sina ushawishi mkubwa kama Alvin, familia yangu ina hadhi ya juu pia.”
“Rodney…” Sarah aliduwaa kwa muda. Kisha akatikisa kichwa bila kuamini. "Hapana. Ninawezaje kukuumiza hivi? Zaidi ya hayo, familia yako haitakubali.”
"Mradi nimeamua mimi, familia yangu haiwezi kufanya chochote." Rodney alimfuta machozi yake. "Sarah, nitakuwa karibu nawe kila wakati. Ikiwa unamtaka Alvin, nitafanya chochote ninachoweza kumfanya awe wako tena. Ukiamua kuachana naye, nitakuoa.”
“Asante Rodney.” Sarah akajishikashika mikononi mwake na kulia kwa uchungu.
Sarah alitabasamu kidogo bila Rodney kutambua. Alijiona mwenye bahati kuwa na Rodney kama hifadhi yake. Rodney angeweza asiwe mkuu kama Alvin, lakini mara tu Baba mdogo wake angechaguliwa kuwa Rais anayefuata, Shangwe ingekuwa kwenye kilele cha mamlaka yao.
Wakati huohuo, msaidizi wa Rodney akaingia. “Oh hapana, Bwana Shangwe!”
“Kuna nini?” Rodney alimtazama kwa hasira.
"Angalia, Bwana Shangwe." Akiwa na uso ulioduwaa, msaidizi wake alichukua simu na kumuonyesha. "Mzee Shangwe alihojiwa kwenye ofisi za Shangwe Corporation hivi sasa."
Rodney alibofya kufungua video na kumtazama babu yake akisema, “Takriban miaka 20 iliyopita, niliamua kugawanya mali ya familia ya Shangwe miongoni mwa watoto wangu. Kwa bahati nzuri, watoto hawa hawajanikatisha tamaa kwa miaka mingi. Sasa kwa kuwa Jason anasimamia Shangwe Corporation, sina wasiwasi. Bado ninamiliki 30% ya hisa za kampuni, ambazo zitapitishwa kwa wajukuu zangu Jessica na Carson katika siku zijazo.”
Mwandishi aliuliza kwa mshangao, "Lakini huna mjukuu anayeitwa Rodney?"
Mzee Shangwe alijibu kwa mkoromo, “Rodney ameniangusha. Hisa za Shangwe Corporation hazitakuwa na uhusiano wowote naye. Ikiwa anapanga kurithi mali ya familia ya Shangwe anaweza kuendelea na ndoto yake.”
Simu ya Rodney ilidondoka chini. Uso wake mzuri ulibadilika. Kisha, akasimama ghafla. "Sarah, nahitaji kwenda nyumbani sasa kwani kuna jambo limetokea."
Akili ya Sarah pia ilikuwa imechanganyikiwa. Hakuwa na hali ya kumshawishi Rodney abaki kabisa. Muda mfupi uliopita, alifikiri angeolewa na Rodney ikiwa asingeweza kumrudisha Alvin.
Baada ya yote, aliamini alikuwa mrithi wa Shangwe Corporation na mtoto wa Rais wa nchi wa baadaye. Haikuwa heshima kidogo kuliko kuolewa na Alvin. Lakini, kwa muda mfupi tu, Rodney aliondolewa na familia ya Shangwe kutoka kurithi hisa za kampuni ya familia yao. Bila msaada wa familia yake, Rodney, ambaye alikuwa na Osher Corporation tu, hakuwa chochote. Angekuwa na ndoa mbaya kuliko Cindy. Sarah alikuwa karibu kupata kichaa. Kwanini alikuwa na bahati mbaya?
Rodney alikimbia kurudi nyumbani mara moja.
Kufika nyumbani, Mzee Shangwe na Jessica walikuwa wakizungumza juu ya mambo ya kampuni.
“Jessica, laiti ungekuwa mwanamume?! Una uwezo zaidi ya Rodney.” Wakati wowote Mzee Shangwe alipomsikiliza mjukuu wake akizungumza kuhusu kazi, alipata hisia.
“Babu, unasikika kana kwamba unatubagua sisi wanawake,” Jessica alisema kwa mzaha.
Wakati tu Mzee Shangwe alipokuwa karibu kuongea, Rodney aliinua mapazia na kuingia ndani. “Babu, je, sina haki ya urithi wa Shangwe Corporation pia? Kwanini ulininyima sifa?”
"Kwa sababu wewe ni mjinga sana." Ilikuwa kana kwamba Mzee Shangwe alitarajia kuonekana kwake, na akaongeza kahawa kwenye kikombe.
Alikuwa mjinga sana? Damu ya Rodney ilichemka kwa hasira. “Mimi ni mjinga vipi? Tangu nilipozaliwa, nimekuwa mwanafunzi wa haraka zaidi kati ya kila mtu katika familia ya Shangwe kwa chochote ninachojifunza. Mwaka niliofanya mtihani wangu wa mwisho, matokeo yangu yalishika nafasi ya tatu kati ya nchi nzima. Nilisoma hata katika chuo kikuu cha juu zaidi ulimwenguni, Havard. Ulisema hata mimi nina akili kuliko Uncle wangu."
Mzee Shangwe alicheka kijeuri. “Ndio maana nikasema wewe ni mjinga. Bado hujatambua sababu ya kukukemea.
Hakika ulikuwa mwerevu ulipokuwa mdogo, lakini unakuwa mjinga kadri unavyokua mkubwa. Sijisikii raha kukupa hisa za Shangwe Corporation. Isipokuwa ... kama utaoa kulingana na mpango wangu.”
Hapo ndipo Rodney alipogundua. "Kwa kusema wazi, hii ni mbinu yako tu ya kunilazimisha kuoa."
“Hapana, hii si mbinu. Ni nafasi yako pekee.” Mzee Shangwe alikunywa kahawa huku akisema kwa utulivu.
"Sitafuata mipango yako na kuoa mwanamke ambaye simpendi." Rodney alifikiria kwa muda na ghafla akasema, "Lakini ninaweza kuoa mke na kukufanya kupata vitukuu hivi karibuni."
“Humaanishi kwamba unamuoa Sarah, sivyo?” Jessica aliuliza.
“Sarah ni mwanamke mzuri. ”…
Mzee Shangwe alitupa kikombe chake sakafuni kabla Rodney hajamaliza kusema. "Ukithubutu kumuoa Sarah, usiwahi kukanyaga kwenye familia ya Shangwe.”
“Babu.” Rodney alishtuka na kukasirika. “Ulisikiliza maneno ya watu, sivyo? Je, si wewe uliyesema kwamba tuamini tunachokiona na sio tunasikia nini? Sarah hajawahi kunichukulia kama mbadala.”
Jessica alidhihaki. “Ikiwa hajakuchukua kama mbadala, kwanini atataka umuoe baada ya Alvin kumkataa?” Hakuweza kuelewa ni kwanini alikuwa na kaka mjinga namna hiyo.
"Mimi ndiye niliyempendekeza ..."
"Nyamaza na upotee." Mzee Shangwe aliogopa kwamba hasira yake ingeweka afya yake hatarini ikiwa angemtazama Rodney zaidi.
“Usiongee nami, nimeamua.” Baada ya hapo, Mzee Shangwe aliondoka....ITAENDELEA...
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
