JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................413-414

Sura ya: 413

Alvin alitikisa kichwa chake kwa kuudhika. Alijilaumu kwa kumuudhi kwa maneno yake ya kijinga. Alipogeuka tu, akamuona Pamela akitoka kwenye lifti huku akipiga kelele.
 Macho yao yalipokutana, Pamela alishikwa na butwaa. "Alvin, kwanini uko hapa tena?"

Alivin alishangaa. Alimaanisha nini aliposema 'tena'? Hata hivyo, hakupenda kumuona Pamela kwani alikuwa ameharibu nafasi yake ya kukaa na Lisa.
 “Ofisi yako si ipo Marekani? Unaondoka lini?” Alvin aliuliza bila huruma.

“Kuondoka?” Pamela alipigwa na butwaa. “Sina mpango wa kuondoka. Nitabaki Nairobi kufanya kazi."

Kichwa cha Alvin kilimuuma kwa kuwaza gurudumu hilo la tatu ambalo lingeendelea kubaki hapo. Alivuta uso mrefu na kuuliza, "Kwa hiyo, utaendelea kukaa na Lisa?"

“Bila shaka. Sisi ni marafiki, na tunategemeana. Lisa yupo single na mimi nipo single, kwa hiyo hatuna wasiwasi.”

Alvin akafikiria kwa muda na ghafla akatoa simu yake kutoka mfukoni mwake. Alibofyabofya kidogo na kumwambia Pamela. "Hii hapa ni virtual card ya nyumba ya ghorofa mbili yenye ukubwa wa mita za mraba 40, iliyopo kwenye mtaa wa Brighton Gardens. Ghorofa hii ina kila kitu ndani. Kadi hii ya kieletroniki ina maelezo yote ya umiliki wa nyumba. Nitawaambia watu wangu wabadilishe jina na kuweka lako. Namba za siri za kufungua kila mlango zimo kwenye hii virtual card. Hamia huko na ni yako kuanzia leo na kuendelea.”

Pamela alipigwa na butwaa. Ingawa hakuwa amekaa Nairobi kwa miaka mingi, alijua kwamba Brighton Gardens ulikuwa ni mtaa mmoja wapo wenye nyumba za gharama kubwa zaidi huko Nairobi. Kwa kuzingatia kwamba ilikuwa katikati mwa jiji, kila senti mita moja ya mraba ya ardhi ilikuwa na thamani kubwa mno.
 Kweli Alvin alimpa nyumba kama hiyo bure?

“Unaitaka?” Alvin alimuuliza.

“Ndiyo!” Pamela alikubali haraka haraka, akifikiri kwamba ingekuwa ni kupoteza fursa adimu kukataa ofa kama hiyo. "Nitaondoka kesho."

“Mm. Alvin aliitikia kwa kuridhika. Alimtumia hiyo virtual card iliyokuwa na maelezo yote ya nyumba kwenye simu yake. Baada ya hapo, aliingia kwenye lifti na kuondoka. Hatimaye, aliweza kulitoa gurudumu hili la tatu nje.

Baada ya Pamela kufungua mlango na kuingia ndani ya nyumba, haraka akamkimbilia Lisa. Alionyesha kadi kwenye simu yake, akisema, "Jamani.
 Sasa hivi, Alvin amenipa nyumba yenye ghorofa mbili kwenye mtaa wa Brighton Gardens. Alisema ni mita za mraba 40.”

Lisa alikuwa anakunywa maji na akayatema mara moja. Akiwa ameduwaa, Lisa alikazia macho kwenye kadi ya kieletroniki iliyoonyesha anuani ya nyumba. Alihisi kukosa la kusema. "Kwa hiyo umemwambia kuwa utahama?"

"Ndiyo, najua uhusiano wenu unaendelea vizuri hivi karibuni, kwa hivyo sitakaa hapa na kuwasumbua nyinyi… Hehehe." Pamela alicheka kwa furaha. "Zaidi ya hayo, ninaweza kukupa nyumba hiyo baadaye."

“Ni sawa. Mimi ni tajiri na sitamani nyumba. ” Lisa aONA ni ujinga. Labda Alvin alivaa kofia ya dola kumi kwenye kichwa cha senti tano. Walipoachana kabla ya hii, hakupokea nyumba kutoka kwake, lakini alikuwa tayari kutumia dola milioni 10 ili tu kumfukuza Pamela, ambaye alikuwa gurudumu la tatu machoni pake. Ilikuwa ni kama anajaribu kuua mbu kwa bunduki.

Lisa hakuweza kuwa na wasiwasi kuhusu Pamela. Aligeuka na kwenda kuoga.

Baada ya kuoga, alirudi kitandani kwake na kufungua WhatsApp. Aligundua kuwa mtu aliyekwenda kwa jina 'Ni Wako Pekee' alikuwa amemfikia.

Lisa alihisi kukosa raha na akajitenga kimawazo kwa muda. Wakati Alvin na Lisa walikuwa wakipendana kwa sana hapo awali, Alvin alikuwa amebadilisha jina lake la WhatsApp kuwa hilo.

Muda mfupi baadaye, Alvin alimtumia ujumbe wa WhatsApp. [Uliblock namba yangu ya mwisho, kwa hivyo nilipata namba mpya.]

Lisa hakujibu. Kisha, Alvin akamtumia selfie. Alikuwa amevaa vazi la kuogea ambalo lilikuwa limefungwa ovyo. Mbali na uso wake mzuri, tumbo lake la misuli lililofunikwa na matone ya maji ya kumeta pia lilikuwa likionekana. Japokuwa Lisa aliwahi kumuona mwanaume huyo kuanzia utosini hadi unyayoni, hakuweza kujizuia kuona haya usoni kwa kuuona mwili wake uchi. Alvin alikuwa akijaribu kufanya nini?

Kwa wakati huo, alicheza ujumbe wa sauti ambao alikuwa amepokea. Sauti nzito ya kiume ya mwanaume huyo ilimfanya ajisikie kana kwamba umeme unapita mwilini mwake na kumfanya aishiwe nguvu.

“Mpenzi, nipo nyumbani. sikwenda popote.”

Mpenzi? Upuuzi ulioje! Uso wa Lisa ulimtoka. Mtu huyu alikuwa hana aibu kweli.

Hata hivyo, Sarah lazima angekuwa na wazimu kwamba Alvin hakwenda kumuona usiku huo.
 Baada ya kufikiria kidogo, Lisa alimtumia emoji ya busu. Baada ya kutuma emoji, uso wake ukabadilika na kujawa aibu tena. Alitaka tu kumpagawisha mwanaume huyo na kumchokoza Sarah kwa makusudi.

Mara Alvin alipoona emoji ya busu, alihisi msisimko mkubwa ndani yake. Mjeledi wake uliamka, na kumsababishia usumbufu kwa sababu isiyoelezeka. Akajilaza huku akimwazia Lisa akimbusu.

Wakati huo, ghafla aliketi kitandani na kumtumia Lisa ujumbe maneno mawili tu: [Nataka kesho.] Kisha, akakimbilia bafuni kuoga maji baridi.

Hakuwahi kusisimka na Sarah licha ya kuwa naye kwa muda mrefu. Kamwe katika ndoto zake kali hakufikiri kwamba emoji rahisi kutoka kwa Lisa ingemfanya awake kwa msisimko. Akatoa kicheko cha uchungu.

Alipotoka bafuni, simu yake ikaita tena. Maya alimpigia. “Bwana Mkubwa, si ulisema unakuja? Bi Njau analia hospitalini. Anakataa kufungwa bandeji.”

Alvin alikasirika kwa namna fulani. "Ni mwili wake, sio wangu! ”

Maya aliogopa alipomfokea. “Lakini Bi Njau anakuhitaji sana sasa, Bwana Mkubwa. Siku zote hizi ukiwa haupo, hajaweza kula wala kulala vizuri. Kwa sababu hiyo, hakuwa na nguvu ndiyo maana akaanguka kutoka kwenye ngazi wakati wa kukatika kwa umeme usiku wa leo. Daktari alisema kuwa miguu yake imejeruhiwa. Ikiwa hatatibiwa mara moja, anaweza kuwa mlemavu katika siku zijazo.”

Maneno ya Maya yalionekana kama uzito mkubwa kwenye akili ya Alvin.
 Kwa mara ya kwanza, hakuhisi hatia. Badala yake, alihisi kuishiwa nguvu.
 Kama Lisa alivyosema, alikuwa tu katika uhusiano na Sarah.
Kwanini ilionekana kana kwamba alipaswa kuwajibika kwa maisha yake yote?

“Sawa, nitakuja,” alinong’ona baada ya muda fulani.


Katika hospitali, Maya mara moja alimwambia Sarah kuhusu hilo. Sarah alisisimka. Alijua kwamba Alvin angeenda hatimaye. Sarah alikuwa amekasirika baada ya Alvin kutokwenda alipopigiwa simu na Maya mara ya kwanza. Lakini, alifurahi kwamba Maya alifanikiwa kumshawishi mwishowe.

Alikuwa amepanga wakati wa Alvin kuonekana tu, kungekuwa na waandishi wa habari wakiwapiga picha. Kisha, kila mtu katika Kenya angejua kwamba jambo fulani lilikuwa limempata Sarah na Alvin ndiye aliyekuwa wa kwanza kukimbilia hospitalini kumwona kwa wasiwasi. Ha! Tayari angeweza kufikiria kulalamika kwa Lisa kwa hasira kesho yake. Lisa alikuwa akijaribu kumpokonya mtu wake. Lakini, mara Sarah alipotoa agizo, Alvin angemmwaga Lisa bila huruma.


Dakika 20 baadaye.
 Sarah alipomwona Alvin hospitalini, haraka akajilaza kitandani na kujifanya kutoa machozi ya kukata tamaa. Ili kupata huruma ya Alvin, Sarah alikuwa amejiangusha bila huruma kutoka kwenye ngazi siku hiyo. Paji la uso, miguu na mikono yake vilijeruhiwa.
 Alionekana mwenye huzuni sana.

“Alvinic, hatimaye umefika. Nilifikiri sitaweza kukuona tena.” Sara alipomwona, alianza kulia kwa uchungu. Alinyoosha mikono yake na kuanguka katika mikono yake. Alvin alishindwa kujizuia kumshika, au angeanguka kutoka kitandani.

Sura ya: 414

"Alvinic, nimekukumbuka sana." Sarah akajiegemeza kwenye mikono ya Alvin, machozi yake yakilowanisha shati lake. “Siku hizi nimekuwa nikijitafakari. Nilikuwa mjinga sana na mpumbavu. Ninaapa kwamba sitakukosea tena. Rudi kwangu. Nimekukumbuka sana.”

Alvin alikaza macho na kumweka kitandani. Baada ya hapo, aligeuka na kumwambia daktari nje, "Ingia ndani umtibu."

"Hapana. Usiponiahidi, sitatibiwa. ” Sarah alijitahidi kwa fadhaa.

Alipoiona sura yake, macho ya Alvin yalimtoka kwa hasira. Uso wake mzuri ulidhihirisha polepole hali ya ukali.
 “Inatosha. Acha kutumia mwili wako kunitisha.”

Hakujua ni kwanini Sarah amekuwa msumbufu na asiye na akili. Hata sasa alikuwa akimtishia, hiyo ndiyo mbinu ambayo alikuwa akiichukia zaidi. Ilikuwa mara yake ya kwanza kutumia sauti ya kutisha hivyo kuzungumza na Sarah.

Baada ya kupigwa na butwaa kwa muda, Sarah alianza kulia zaidi. "Sipendi kuwa na tabia kama hii pia lakini ninaweza kufanya nini? Siwezi kujizuia kufanya hivyo.”

"Sarah, kwanini tusitengane bila kuwa na kinyongo?" Alvin hakuguswa na kilio chake hata kidogo. Badala yake, alihisi wimbi la uchovu likimuandama. “Miguu yako ni yako. Hata ukiwa kilema siku za usoni, sitawajibikia kwa sababu si mimi niliyekuangusha kwenye ngazi.”

Sarah aliutazama uso wake mzuri bila kuamini. Siku zote alikuwa mpole na mvumilivu kwake. Lakini siku hiyo, alikuwa na mawazo tofauti kabisa juu yake.

“Bwana Mkubwa, tafadhari usimkasirishe Bi. Njau tena. ” Maya akawa na wasiwasi. “Umesahau kuwa Bi Njau ndiye aliyekutibu ugonjwa wako? Kama isingekuwa kwa Bi Njau kukutana na wewe katika hospitali moja ya wagonjwa wa akili kama wewe, usingekuwa na ujasiri wa kutosha kusimama hapa leo ukiwa mzima hivi."

“Hiyo ndiyo sababu niliamua kumuoa, lakini yeye ndiye aliyefanya mambo ya hovyo,” Alvin alisema kwa uchungu, “Sasa, nimekuwa kicheko miongoni mwa kila mtu kwenye jiji hili. Wakati polisi walipofunua uozo wako wakati wa harusi yetu, nilivumilia na kukusamehe. Lakini kwa nini usiniruhusu niende? Kama si kifo cha Hisan, ungeendelea kufanya naye matendo hayo mabaya. Sarah, usinichukulie kama mjinga.”

Uso wa Sarah ukageuka kuwa na huzuni. "Nisingefanya, Alvinic. Usinifikirie vibaya sana.” Ghafla alitupa blanketi sakafuni kama mwanamke mwendawazimu na kulia kwa uchungu. “Kwanini wewe
kunifanyia hivi? Hisan alinilazimisha kufanya hivy. Si kwamba nilifanya kwa sababu nampenda. Hata mimi ilikuwa ikiniumiza pia.”

“Bi Njau, usihangaike. Miguu yako imejeruhiwa.” Maya alimwambia Sarah na kumsihi Alvin bila utulivu, “Bwana Mkubwa, punguza sauti yako na umsikilize. Ikiwa ataendelea kuwa na tabia kama hii, miguu yake inaweza kuwa na ulemavu."

Kumtazama Sarah alivyokuwa mjeuri, Alvin alijihisi kuishiwa nguvu hadi kichwa kikaanza kumuuma. Aligeuka na kuwaambia wahudumu wa hospitali, "Mkandamizeni tu chini na mumfunge majeraha yake kwanza."

Wahudumu wa hospitali hiyo walitazamana kwa muda. Kisha, walifuata maagizo yake na kumkandamiza Sarah kitandani. Sarah, ambaye alikuwa amejifanya kushindwa kujizuia, hakuwahi kutarajia Alvin kuwa mkatili kiasi kile. Alifikiri kwamba angembembeleza. Sasa alipokuwa akiomba wafanyakazi wamfunge, alikasirika sana hivi kwamba aliendelea kupiga mateke. Hata alimjeruhi mfanyakazi wa hospitali kwa teke lake.

Alvin alimwendea na kumshika mguu wake mmoja ili daktari ampake dawa kwenye majeraha yake.
 Hata hivyo, daktari alipomaliza kumpaka dawa, Sarah aliivua bandeji. Alisema katikati ya kilio chake, "Hapana. Bila wewe, bora niwe kilema. ”

Baada ya kuchokozwa tena na tena, Alvin alipandwa na hasira. “Basi, endelea na uwe kiwete. Sihitaji kuwajibika kwa maisha yako.”

"Alvin, hivi ndivyo unavyomjibu Sarah leo?" Rodney ambaye alikuwa ameingia ghafla, alitokea kusikia maneno ya Alvin na akashindwa kujizuia mara moja. “Ni mwanamke wako! Yeye ni mchumba wako! Unapaswa kuchukua jukumu kwa ajili yake." Rodney alimvuta Alvin pembeni. Huku akiwa amekata tamaa, alimuelekeza Sarah pale kitandani ambaye alikuwa ameumia sana. “Umesahau kuwa uliahidi kumtunza? Na hivi ndivyo ulivyomuumiza?”

“Nimemuumiza vipi?” Papara za Alvin zilikuwa zimefikia kikomo. "Rodney Shangwe, wewe si mimi. Hujui lolote.”

“Ninachojua ni kwamba ikiwa hutamuoa Sarah, sifa yake itaharibika milele,” Rodney alijibu kwa hasira, “Anakupenda. Unadhani alifanya mambo hayo yote makusudi? Yeye ni mwathirika. Zaidi ya hayo, bado unajihusisha na Lisa, lakini Sarah hakusema lolote. Ni nini kinakupa haki ya kumkosoa?”

“Umemaliza?” Alvin alishindwa kujizuia. “Nimesema mimi na yeye hatuwezikuendelea tena. Sina mjadala kwa hilo.”

“Umekuwa naye kwa zaidi ya miaka kumi. Ikiwa sio wewe, basi ni nani anayepaswa kuwajibika kwa hilo?" Rodney aliuliza kwa hasira.


Kwa mara ya kwanza maishani mwake, Alvin alihisi kuwa uhusiano wake na Sarah ulimfanya ajisikie kuchoka kabisa. Hakutaka tu kumuoa tena Sara. Ni nini kilmpa Sarah haki ya kumlaumu? Je, yeye ndiye aliyekuwa ametuma mtu wa kumteka nyara Sarah huko Garisa? Je, yeye ndiye aliyewafanya Sarah na Hisan walale pamoja? Hapana.!
"Rodney, ikiwa unampenda sana, muoe wewe. Usije kwangu kila wakati ili kunilazimisha niwajibike kwake.” Alvin alipiga hatua kuelekea mlangoni huku akihisi kuvuta sigara.

Baada ya kuutazama uso wa Sarah uliopauka, Rodney alishindwa kujizuia kumfuata Alvin nje. Akamshika mkono Alvin na kumnong'oneza, “Unadhani sitaki kumuoa? Jambo ni kwamba anakupenda wewe tu.
 Wewe ndiye anayetaka kuwa naye. Alvin, huwezi kumsukumia Sarah kwa mtu mwingine kwa sababu tu hutaki kuwa naye.
 Yeye ni binadamu, na anakupenda kwa moyo wake wote.”

“Simpendi tena.” Alvin aliinua kichwa chake ghafla. Huku mikondo ya hasira ikitiririka katika macho yake yaliyozama ndani, alionekana kama simba aliyekasirishwa.

"Umesema nini?" Rodney alipigwa na butwaa.


“Unaweza kunichukulia kama mpuuzi. Hata hivyo, haiwezekani nimuoe tena,” Alvin alisema kwa uthabiti.

“Wewe ni mtu wa ajabu kiasi gani!” Rodney alikasirika sana hadi akampiga Alvin usoni. “Lazima Lisa ndiye aliyekujaza upepo tena, sivyo? Nitamuua.”

Rodney aligeuka na kuwa karibu kuondoka. Hata hivyo, Alvin alimzuia na kumwonya bila huruma, “Huruhusiwi kumtafuta Lisa. Haina uhusiano wowote naye. Hata bila yeye, bado sitamuoa Sarah.”

“Usifikirie kunidanganya. Kila kitu kilikuwa sawa kabla ya Lisa kurudi. Nitahakikisha atalipia mateso ya Sarah.” Rodney hakuweza kuwa na wasiwasi kuhusu Alvin.

Wale watu wawili walisukumana na kusukumana kwenye korido.
Hatimaye, Rodney alimpiga ngumi kwani hakuweza tena kumvumilia.
 Hasira za Alvin zilikuwa zimefika kileleni pia. Wawili hao walianza kupigana kwenye korido.

“Acheni kupigana! ” Chester, ambaye alikimbilia hapo baada ya kusikia habari hizo, aliwaamua haraka. “Nyinyi nyote ni watu mashuhuri. Hamuoni aibu kutazamwa kana kwamba ninyi ni wanyama?”

Wawili hao walishtuka. Hapo ndipo walipogundua kuwa kulikuwa na watazamaji wengi karibu nao.
 Kwa bahati nzuri, Ghorofa hiyo ilikuwa ya wagonjwa wa VIP, kwa hiyo hapakuwa na watu wengi. Wengi wao walikuwa madaktari.


“Endeleeni na kazi zenu. Ikiwa yeyote kati yenu atathubutu kueneza tukio la usiku wa leo, atafukuzwa kazi moja kwa moja,” Chester aliwaonya kabla hajautawanya umati.

Rodney, ambaye uso wake ulijeruhiwa, alitoa maneno ya kikatili kwa Alvin. "Ukithubutu kumwacha Sarah, hatutakuwa marafiki tena."

“Utajua mwenyewe.” Alvin alidumisha uso usio na huruma, jambo ambalo lilimfanya Rodney apate wazimu tena.

“Inatosha, Rodney. Haya ni mambo ya Alvin na Sarah. Kwanini unaendelea kujiingiza?” Chester alimwonya bila aibu, “Zaidi ya hayo, Sarah yuko wodini. Akijua kuwa nyinyi wawili mnampigania, lazima atavunjika moyo.”

Kwa mawazo ya Sarah, Rodney alishindwa hata kusema lolote. Vile vile, Alvin alikaa kimya huku akiwa amesimama upande mmoja.

Wakiwa wodini Sarah alisaga meno aliposikia wawili hao wakipigana.
Hakuwahi kufikiria kuwa Alvin angesema bila huruma kwamba hatamuoa...ITAENDELEA....

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.