JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................411-412

Sura ya: 411

“Mbona umeduwaa? Unawaza nini” Alvin aliushika mkono wa Lisa ghafla na kumtazama kwa makini. "Mnataka kula nini tena? Twendeni tukanunue."

“Nataka… nataka popcorn,” Suzie alisema kwanza.

"Unadhani mimi ni mlaji kama nyinyi?" Lisa aligugumia, lakini Alvin alijisikia hovyo.

Alvin akajibu kwa umakini, “Mimi sio mla hovyo. Ninapenda tu upishi wako."

"Na mimi pia. Upikaji wa Aunty Lisa ni bora zaidi ya wa mama wote." Suzie akaenda pamoja nao.

Kwa kuona jinsi Alvin na Suzie walivyofanana kimuonekano, macho ya Lisa yakawa ya upole. "Nataka juisi ya zabibu."

Baada ya kumkabidhi Suzie kwa Lisa, Alvin aligeuka na kwenda kununua juisi ya zabibu. Akiwa amekaa mikononi mwa Lisa, Suzie alinong'ona kwa ghafla, "Mama, baba yangu mchafu... anajaribu kukurudisha kwake?"

"Hujui chochote we mtoto, nyamaza." Lisa alibana ncha ya pua ya Suzie.

"Mama, nahisi ... Baba mchafu ni mzuri sana." Suzie alimkazia macho ya huruma. “Kwanini usifanye hivyo? Nyie tu… mnapendeza mkiwa pamoja.”

Lisa alipigwa na butwaa kwa muda. Kwa kweli, aligundua mapema kwamba Suzie alikuwa na nia ya kumuunganisha na Alvin. Japokuwa Suzie alitarajia hilo lingetokea, Je, Lisa angeweza kusahau madhara aliyosababishiwa na Alvin kwa ajili ya Suzie? "Siyo rahisi kama unavyofikiri. Aunty Sarah hataweza kumuachia baba yako kiurahisi, na baba yako mchafu anaweza kututupa wakati wowote kwa ajili yake.”

“Kweli? Ikiwa ndivyo alivyo, sitamsamehe tena,” Suzie alijibu kwa kufoka.

Suzie hakujua kwamba kama isingekuwa msaada wa Jack na Hans, yeye na Lucas wangepoteza maisha. Lisa asingeweza kusahau mateso na unyonge huo.

Muda si mrefu Alvin alirudi na popcorn na juisi. Kisha, wote watatu wakaingia kwenye ukumbi wa sinema pamoja. Suzie alikuwa ameketi kati ya Alvin na Lisa. Hata hivyo, Alvin alihisi yuko mbali sana na Lisa, hivyo akamuweka Suzie kwenye mapaja yake na badala yake akaketi na kugusana kabisa na Lisa. “Suzie, nitakuruhusu ukae kwenye mapaja yangu, sawa? Mtu mrefu aliye mbele yako anaweza kukuzuia, kwa hivyo hutaweza kuona skrini. ”

Suzie aliitikia kwa kichwa akidhani kuwa alichokisema Alvin ni kweli.
Lisa alikosa la kusema. Mara akagundua mkono wa Alvin umewekwa nyuma ya mgongo wake.

Lisa alimkazia macho, lakini Alvin alisema kwa uso ulionyooka, "Bega langu linauma, kwa hivyo ninanyoosha mkono wangu."

Lisa aligeuza macho yake kwenye skrini kwani hakuweza kuwa na wasiwasi juu yake. Lakini, sinema za katuni za watoto zilikuwa za kuchosha sana. Suzie pekee ndiye alikuwa amezama kwenye sinema.
Lisa aliinamisha kichwa chini. Aliwasha simu yake ili kucheza baadhi ya michezo.

Mkono wa Alvin ukatua begani mwake. Alikuwa amevaa vazi jepesi la hariri, hivyo aliweza kuhisi mkono wake laini ukipenya kabisa kwenye ngozi yake.

“Alvin...” Lisa alitazama juu na kumkazia macho.

Alvin aliondoa mkono wake kwa aibu. Kisha, akachukua chupa ya juisi ya zabibu iliyowekwa kati yao na kuinywa.

“Hiyo ni yangu.” Lisa kwa hasira akashusha pumzi ndefu.

“Haijalishi,” Alvin alimsogelea na kumnong’oneza sikioni. Kupumua kwake kwa jinsi ya kiume kulimfanya Lisa awe na mwasho moyoni na kitetemeshi kwenye uti wake wa mgongo. "Tumeshea mate mara nyingi sana hivyo hakuna ajabu tukishea juisi."

Lisa alibana paja lake bila huruma. Huyu mhuni anathubutu vipi kutoa maneno yasiyo na aibu? Ikiwa ukumbi wa sinema haukuwa na giza vile, bila shaka angeweza kumuona uso wake ukiwa umekunjamana kwa wakati huo.

Hakujisikia tena kuinywa ile juisi kwa vile Alvin alikuwa amekunywa. Hata hivyo, alihitaji kukata kiu yake vibaya sana. Hakuwa na jinsi zaidi ya kuinywa tu hiyo juisi.

Katikati ya sinema hiyo, Alvin aliinuka na kuelekea chooni. Lisa alipomuuliza Suzie kama angependa kwenda chooni, Suzie akatikisa kichwa na kusema hapana. Hata hivyo, Lisa alipombeba, alihisi mkojo wa joto ukitoka kwa Suzie ambao ulilowesha suruali yake. Uso wa Lisa ukaganda. Kama wangekuwa nje muda huo, angemchapa.

“Samahani mama. ” Suzie alifahamu jambo baya alilokuwa ametoka kufanya. Huku machozi yakimtoka, nusura aanze kulia.
"Kwanini ulisema hapana nilipokuuliza unataka kukojoa?"
“Sikutaka kukosa sinema hiyo, na nilifikiri ningeweza kuvumilia!” Suzie alijibu kwa unyonge.

Lisa alishindwa kusema chochote, akashusha pumzi. “Sawa. Acha kutazama filamu. Lazima ubadilishwe. Vinginevyo, utapata homa."

Alimbeba Suzie na kutoka nje. Alvin, ambaye alikuwa akitoka nje ya choo, alitokea kuona unyevunyevu kwenye nguo ya Lisa sehemu ya mapajani.

“Suzie alinikojolea. Ni lazima nimtafutie seti mpya ya nguo ili asipate homa.” Lisa alieleza.

Kwa bahati nzuri, kulikuwa na maduka chini ya ukumbi wa sinema. Muda si muda Lisa alinunua seti mpya ya nguo ili Suzie abadilishwe. Alijinunulia nguo mpya kwenye duka la nguo za wanawake na kubadilisha pia. Kwa kuwa alikuwa na sura nzuri, suruali yoyote ingempendeza.

Msaidizi wa duka kando yake alimsifu, “Bwana, mke wako ana sura nzuri sana, na pia anaonekana mrembo. Ni kama mwanamitindo bila kujali anavaa nguo gani.”

Alvin akatabasamu. Neno 'mke' halikuwahi kusikika la ajabu sana kwake. "Mpatie nguo zote za saizi yake." Alvin alitoa kadi ya malipo kwa msaidizi wa duka moja kwa moja. Msaidizi wa duka alipigwa na butwaa. Alikuwa tajiri kiasi gani?

Wakati Lisa anatoka akiwa amevalia suruali mpya ya jeans, muuza duka alikuwa tayari ameshapakia furushi la nguo. “Bibi, mumeo amenunua nguo zote za duka hili zenye saizi yako. Umebarikiwa sana!”

Lisa akahamishia macho yake kwa Alvin huku midomo ikicheza. "Mbona unanunua nguo nyingi hivi?"

"Muuzaji amesema unaonekana mzuri ukizivaa." Alvin akatabasamu.
Lisa alipapasa paji la uso wake. "Hakuna nafasi ya kutosha nyumbani kwangu kuweka nguo hizi zote ..."

“Utaziweka katika nyumba yangu ya Zion Residence, basi. Unapokuja kukaa, hutalazimika kubeba nguo zako,” Alvin alijibu kwa namna ya kujihesabia haki kana kwamba… wawili hao walikuwa kwenye uhusiano rasmi.

Lisa alikosa la kusema kabisa baada ya kuona sura yake isiyo na aibu. "Naweza kujua kwanini nije kukaa huko?"

“Usipokuja na kukaa kwangu, unapanga kukaa sehemu ya nani? Sitakuruhusu kukaa katika nyumba za wanaume wengine,” Alvin alisema kwa njia ya ubabe na ya uchochezi.

Lakini, Lisa hakuwa na nguvu ya kubishana naye tena. Kwa kuwa alitaka kutumia pesa, angemruhusu. Kwa vyovyote vile, yeye ndiye angeamua kukaa au kutokaa mahali pake.

Alvin aliishia kumnunulia zaidi ya seti 100 za nguo Lisa, ambaye mwanzoni alitaka tu kununua suruali moja ya jeans.
 Alvin aliandika anwani ya Zion Residence katika fomu ili kutuma baadhi ya nguo huko. Kisha, alimsaidia Lisa kubeba zingine kurudi nyumbani.

Wakati wote watatu waliposhuka kwenye lifti, Joan Halua, rafiki wa Sarah, ambaye alikuwa akinunua vitu, aliwaona. Hapo hapo akawapiga picha na kumtumia Sarah kwa njia ya WhatsApp. [Sarah, nini kinaendelea kati yako na Alvin? Nilimwona tena akinunua nguo na Lisa. Wamenunua nguo nyingi mno.]

Kusema kweli, Joan hapo awali alikuwa amempenda Sarah kwa kuwa mchumba wa Alvin. Alikuwa ametumia muda mwingi na juhudi kujikombakomba kwa Sarah kwa sababu hiyo. Hakutarajia hilo mwishowe…

Kila mtu alijua kuwa Sarah asingekuwa mtu wa matawi ya juu bila kumtegemea Alvin, ikizingatiwa kuwa alikuwa mwanasaikolojia tu. Angehitajika tu wakati kulikuwa na mgonjwa wa akili.


Sarah alipoona picha, aliruka kwa hasira. Kipindi hicho, Alvin alikuwa akipotezeasimu na meseji zake. Hata mlinzi wa ofisi yake angemzuia kuingia. Ilionekana kana kwamba alikuwa ametupwa kabisa.

Sarah alihisi kuwa Alvin bado ana kinyongo naye, lakini hakutegemea kwamba angeenda kumtafuta Lisa. Hata alikuwa akimsindikiza kwenda kufanya manunuzi ya nguo. Pamoja na wote wawili kuambatana na mtoto, walionekana kama familia. Mbaya zaidi aliweza kuhesabu nguo ambazo Alvin alimnunulia kwa kutumia vidole vya mkono mmoja. Sarah karibu akaenda wazimu.

Hapana! Ilibidi amzuie Alvin kuwa na tabia hii! Dokezo la chuki lilimwangazia machoni pake. Alifungua mlango na kumwita Maya.

Sura ya: 412

Wakiwa njiani kurejea Karen Estate, simu ya Alvin iliita ghafla. Alipoitoa na kuitazama, akagundua kuwa ilikuwa ni simu inayoingia kutoka kwa Sarah.
 Akakunja uso, akabonyeza kitufe cha kuzima sauti kabla hajaitupa simu pembeni.

Lisa aliyekuwa amembeba Suzie kwenye kiti cha nyuma, alibaki akihema huku akitazama tu. Muda mfupi baadaye, simu yake iliita tena. Ni Maya ndiye aliyempigia simu wakati huo. Maya kawaida hakumpigia simu. Kwa hiyo, Alvin aliitikia simu haraka. " Kuna nini?"

“Oh hapana, Bwana Kimaro! Umeme katika jumba ghafla ulizima ghafla. Bi Njau aliposhuka chini, alikosea kukanyaga na kuteleza kwenye ngazi kwa bahati mbaya. Amejeruhiwa, na anavuja damu nyingi,” Maya alisema kwa wasiwasi.


Uso wa Alvin ulibadilika. “Nenda ukaite gari la wagonjwa limpeleke Sarah hospitali. Narudi sasa hivi.”

Alipokata simu hiyo, alikanyaga moto mpaka gari likakaribia kupaa na mara akafika kwenye lango la kuingilia kwenye jengo la nyumba ya Lisa.
 “Nitamwacha Suzie na wewe hapa usiku wa leo. Kesho nitakuja kumchukua asubuhi.”

Wakati huo, Suzie alikuwa tayari amelala mikononi mwa Lisa.
 Lisa alikodoa macho. Alipotazama sura safi na tamu ya Suzie, moyo wake ulimuuma ghafla. Muda si mrefu, mtoto huyu mdogo alikuwa amesema kwamba babake mchafu alikuwa mzuri sana, kwa hiyo alitaka Lisa warudiane naye. Hata hivyo, muda mfupi baadaye alikuwa akiwatelekeza bila kusita na kwenda kukutana na mwanamke mwingine.

“Sasa kwa kuwa yeye ni mzito sana, unafikiri ninaweza kumbeba juu mpaka kwenye lifti peke yangu?” Lisa alitoa kicheko cha kejeli.

Alvin alipigwa na butwaa na akajibu bila kufikiria tena, “Basi nitambeba.”

“Alvin, mbona unakimbilia kuondoka? Huna hata wasiwasi kuhusu mtoto wa mdogo wako. Hii ni kwa sababu tu kuna jambo limempata Sarah?” Ghafla, Lisa alimkazia macho. Kwa kweli, alikuwa amesikia sehemu fulani za mazungumzo alipokuwa kwenye simu.

Alvin aliguna, akitaka kumdanganya. Hata hivyo, baada ya kuona macho yake meusi lakini angavu, alishindwa kusema lolote. Muda mfupi baadaye, hakuweza kujizuia kueleza, “Kulikuwa na giza ndani ya jumba. Sarah hakuweza kuona gizani, hivyo akaanguka alipokuwa akishuka ngazi…”
"Si kuna mtu aliyepiga simu kwa gari la wagonjwa kumpeleka hospitali?" Lisa aliuliza kwa ukali.
 "Maya ameita gari la wagonjwa. Sasa mbona unakimbilia huko? Wewe ni daktari? Au bado ni mpenzi wake? Mume wake?”

Baada ya kusikia maneno ya Lisa, Alvin alianza kuonekana mnyonge.
“Yeye… Amejeruhiwa vibaya sana…” Baada ya muda fulani ndipo alipolazimisha sentensi hiyo kutoka kinywani mwake.


Lisa alicheka tu kwa kebehi. "Alvin, mwishowe, bado una wasiwasi juu yake. Unahisi una jukumu kwake. Bado una hisia kwake, bila kujali kama unamtendea kama mwanafamilia, mpenzi, au mtu unayemuhurumia.
Kwa kawaida na bila kujua umemfanya kuwa kipaumbele chako cha juu."

“Usinielewe vibaya, Lisa. ” Mikono ya Alvin iliyokuwa imeshikilia usukani iliganda.

"Kuna mtu karibu naye sasa, na zaidi ya hayo, uliniambia kuwa haiwezekani tena nyinyi kuoana. Kwa hivyo kwanini unataka kuharakisha huko?" Lisa alilazimisha tabasamu. “Alvin, ukisisitiza kuwa na tabia hii, ningekushauri uache kunifuatafuata.
 Ni bora ubaki kuwa na Sarah. Kwa kweli sitaki unifanye niteseke na kunitendea isivyo haki.”

“Ninaenda kumtazama tu mara moja. Wewe unazidisha mambo. ” Uso wa Alvin ulijikunja. "Nina hakika kuwa wewe ndiye ninayekupenda."

“Unanipenda, lakini utaenda kwa Sarah mara tu jambo litakapomtokea. Lakini mimi? Nilivamiwa na ndugu yake na hakuna lolote ulilolifanya. Unanipendaje kwa mfano?” Lisa alijua kwamba Sarah alifanya mambo kama hayo makusudi. Alijua kuwa Sarah angejiumiza ili tu apate huruma ya Alvin.

Ni wazi, Sarah alikuwa ameanguka kutoka kwenye ngazi wakati wa giza kwa nia moja tu ya kumfanya Alvin aende huko.
 Lakini, Lisa hakumruhusu Alvin kuingia kwenye mtego wa Sarah. Hakumruhusu Alvin aelekee huko usiku huo.
"Alvin, ikiwa bado unajiona kuwa na hatia kwa yaliyompata, basi endelea kubeba jukumu lake, lakini uachane kabisa na mimi. Huwezi kuwa na uhusiano na mimi na kuendelea kumjali Sarah kwa wakati mmoja. Ingawa amefanya jambo baya, bado unamvumilia. Ukiendelea kufanya hivi, nitaanza kukudharau.” Lisa aliinua kichwa chake kama twiga mwenye majivuno, macho yake yalikuwa mazito kwa kumaanisha. “Nataka ujue kwamba usipomwacha Sarah aendelee na maisha yake, atafikiri ana nafasi ya kurudiana na wewe. Ikiwa hali ndiyo hii, mwanamume yeyote ambaye anavutiwa naye hataweza kumkaribia na kumfuatilia. Huwezi kumzuia kuolewa na mwanaume mwingine wakati hutaki kumuoa, sivyo?”

Midomo myembamba ya Alvin ilitetemeka. "Bila shaka hapana. Natumai kuwa atafurahi pia. ”

“Basi sio lazima ujisikie hatia kwake, kwa kweli. Baada ya yote, ulikuwa tu kwenye uhusiano na Sarah. Hujazaa naye mtoto wala hujawahi kumpa mimba. Umemsaidia hata Thomas kwa kumzuia kupelekwa jela mara kadhaa, na pia umeitetea sana New Era Advertisings kila wakati. Juu ya kwanini nyie hamkuishia kuoana, nadhani mnajua jibu kuliko mtu mwingine yeyote.”


Maneno ya Lisa yalimfanya Alvin ahisi raha ghafla. Licha ya kujua kwamba alikuwa na badiliko la moyo wake, bado alihisi kuwa amejawa na hatia kwa sababu ya ahadi yake ya wakati huo kwa Sarah.
 Baada ya Sarah kurejea, aliweza kutibu ugonjwa wake, lakini hakuweza kufanya naye mapenzi.

Lisa alikuwa sahihi. Alvin na Sarah walikuwa kwenye uhusiano tu na hawakuwahi kulala pamoja. Hapo awali, Alvin alitamani kwa dhati kumuoa Sarah. Isingekuwa kuonekana kwa Hisan, angeishia kumuoa Sarah. Alikiri kwamba Sarah alihuzunika, lakini si yeye aliyechangia maisha yake ya zamani yenye kuhuzunisha.

Lisa kisha akaendelea, “Mimi si mtu asiye na huruma hata hivyo. Ikiwa kusingekuwa na mtu kando ya Sarah, ingekuwa sawa kwangu ikiwa ungetaka kwenda kumsaidia kwa kuwa wewe ni mpenzi wake wa zamani. Lakini kuna mtu yuko naye sasa na kakake Sarah yuko hapahapa Nairobi. Ukitaka kwenda huko, sitakupa nafasi ya pili.” Kwa hayo, akafungua mlango wa gari na moja kwa moja akatoka huku akiwa amembeba Suzie.

“Sawa, siendi huko.” Alipoona anatoka, Alvin haraka akafungua mkanda wake na kumfuata. Akamchukua Suzie kutoka mikononi mwake huku macho yake yakimetameta. “Kwa hiyo unaweza kunipa nafasi nyingine usiku wa leo?” Alvin alianza kusukuma bahati yake. "Baada ya yote, ulikuwa unajaribu kunidhibiti sasa hivi."

“Nilikudhibiti lini? Nilikuwa nasema ukweli tu.” Lisa alianza kushindwa kujizuia. Kama asingetumia muda mrefu kumfundisha Alvin, angeenda kumtafuta Sarah. Anathubutu vipi kuuliza swali kama hilo.

"Unawazimu? Una wivu?” Mdomo wa Alvin ulijipinda na kuwa tabasamu mbaya.
 Ingawa alizuga kuwa na uso mkali, alijua kwamba alikuwa na wasiwasi juu yake.

“Unawaza kupita kiasi. Sitaki mambo yawe kama hapo awali uliponipiga teke na kunitaliki mara baada ya kulala pamoja. Alvin, ninachotaka ni hali ya usalama. Sitaki kuwa siku zote nitakayetupwa wakati wowote.”
Lisa alipomaliza kuongea, alitangulia mbele bila kuangalia nyuma.

Baada ya kuona nywele zake nyeusi zikipeperushwa na upepo wa usiku na mikunjo yake mizuri, moyo wa Alvin uliumia kwa namna fulani. Alvin alimfuata na kuingia ndani ya nyumba. Kisha, akamweka Suzie juu ya kitanda katika chumba chake cha kulala.

“Kesho, nitampeleka Suzie shule ya chekechea. Sio lazima uje kumchukua. ” Lisa alimlaza Suzie kitandani.

“Oh!” Macho ya Alvin yalipita ndani ya nyumba ile. Aliinua uso wake kwa hisia ya kukata tamaa “Nilifikiri ningelala hapa usiku huu. Naweza hata kulala kwenye kochi.”

“Unaota ndoto?” Baada ya kutumbua macho, Lisa alimtoa chumbani kwa ukali. "Pamela atarudi muda si mrefu. Itakuwa shida ukilala hapa."

"Katika hali hiyo, ... naweza kulala kwenye kochi katika chumba chako cha kulala." Alvin alimtishia kwa sauti ya chini, “Huogopi kwamba nitaenda hospitali kumtafuta Sarah ikiwa utaniruhusu niende?” Hakutarajia maneno hayo yangemkera Lisa.

Lisa alimjibu kwa kuchukia sana. “Kama unataka kumtafuta, hiyo ni biashara yako. Sio kama nimekufunga miguu yako hata hivyo."

Safari hii, moja kwa moja alimsukuma nje ya mlango mkuu na kuufunga kwa nguvu....ITAENDELEA...

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.