JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................393-394

Sura ya: 393

Rodney alitilia shaka ikiwa alikuwa katika ndoto mbaya hadi mwanamke kutoka upande wa pili alipokuja na kumshikilia. “Handsome, kwa nini usilale muda mrefu zaidi? Bado ni mapema.”

Alishtuka na kuelekeza macho yake upande wa pili, ambapo alimuona mwanamke mwingine mnene, mwenye nywele zilizosongamana. Mdomo wake ulitoa harufu mbaya sana. Kisha, wanawake wengine kitandani waliamka pia. Kila mmoja alikuwa na sifa zake za kipekee, lakini za kutisha.

Rodney alijipiga makofi mawili kwa nguvu. Baada ya hapo, alipiga kelele na kuruka kwa mshtuko. Mbaya zaidi, aligundua kuwa alikuwa uchi wa mnyama. Aliogopa sana na akatumia blanketi kujifunika. Isingekuwa maumivu makali usoni mwake, asingeamini kuwa kila kitu kilikuwa kweli.

“Nyie nyote ni akina nani? Kwanini mko hapa? Mmenifanyia nini?” Maswali dabodabo ya mshangao yalimtoka Rodney.

“Una shida gani, handsome? Ulitupigia simu jana usiku, ukaishia kulala kama gogo. Tumejaribu kukubembeleza kwa muda mrefu, lakini haukuonyesha dalili za kutaka kufanya chochote, kwa hivyo tulilala tu na wewe usiku wote bila kufanya chochote. Kwa kuwa umetulipia, hebu tukusaidie sasa hivi.”

Ikizingatiwa kuwa wanawake hao walikuwa hawajawahi kumuona mwanaume mwenye sura nzuri kiasi hicho, walikuwa wakimbembeleza, lakini mbembelezwaji sasa ndiye hakuwepo.

“Usinikaribie.” Akiwa amechoka, Rodney alipoteza stepu na akaanguka kitandani.

Kwa wakati huu, mlango wa chumba ulifunguliwa kwa nguvu. Hapo ndipo umati wa waandishi wa habari ulipoingia.

“Jamani. Kweli ni Rodney Shangwe."

“Bwana Shangwe, unatisha sana Umelala wanawake wote hawa kwa usiku mmoja?”

"Bwana Shangwe, wewe ni noma."

"Bwana Shangwe, una nguvu sana."

Kundi la kamera zilimwangazia Rodney. Wakati huo huo, alihisi kana kwamba alikuwa amenaswa katika ndoto mbaya. Alihisi kama alitaka kuvunjika na kufa vibaya sana.
•••
Huko Karen Estate, nyumbani kwa Lisa, Pamela aliitazama simu yake na kuzidisha kicheko maradufu huku akipiga piga kitandani. Ni furaha iliyoje.

Lisa, ambaye alikuwa ametoka tu kuamka, alipita kwenye chumba cha Pamela na kusikia kicheko chake, alikosa la kusema. Alifungua mlango, na kumuona Pamela akiwa amelala kitandani huku akicheka na machozi ya furaha. Lisa alishindwa kuvumilia kuuliza. “Unatazama nini ambacho kinachekesha sana?”

"Acha nikuonyeshe kitu muhimu." Pamela akampa Lisa simu yake.
Kwa mtazamo wa harakaraka kufuatia habari zilizovuma sana asubuhi na mapema, Lisa alifikiri itakuwa juu ya ndoa ya Alvin na Sarah. Lakini, hakutarajia kuona; "Rodney Alala na Wanawake Watano".

Alibonyeza picha hiyo, iliyomwonyesha Rodney akiwa amechoka na kujifunika blanketi akiwa ameketi kwenye kitanda cha chumba cha hoteli. Pia kulikuwa na wanawake watano ndani wenye maumbo na ukubwa mbalimbali wamelala kitandani. Bila shaka, alichomaanisha kwa maumbo na saizi mbalimbali ilimaanisha kuwa walikuwa wanene na wembamba wenye sura mbaya.

Kulikuwa na, bila shaka, zaidi ya picha moja, na pia kulikuwa na video iliyoonyesha Rodney akiwafukuza waandishi. Tukio hilo mara moja lilizua tafrani miongoni mwa wanamtandao.
[Nimefungua habari zinazotrend leo, nikadhani ni kuhusu ndoa ya Alvin na Sarah. Katika ndoto zangu za ajabu sikuwahi kutarajia iwe kuhusu rafiki wa Alvin, Rodney Shangwe.]

[Rodney Shangwe anajaribu kushindana na Alvin Kimaro kwa vichwa vya habari leo? Kwa kweli ametumia juhudi kubwa katika kufanya hivyo.]

[Mbona Rodney ana mambo ya ajabu namna hii? Wanawake hao wanaonekana kana kwamba wanaweza kuwa mama yake.]

[Kama ningejua mapema kwamba Rodney Shangwe anapenda mambo kama hayo, ningekuwa na nafasi ya kuolewa na familia yake tajiri. Angalau ningeonekana bora kidogo kuliko wanawake hao.]

[Rodney Shangwe anaupiga mwingi sana. Mimi siwezi kulala na wanawake watano kwa mpigo. Afadhali nipate parachichi zaidi ili kuongeza bguvu zangu.]

[Si ajabu Bwana Rodney Shangwe amekuwa single. Kumbe huwa anavutiwa na aina hii ya wanawake? Je! Familia ya Shangwe inajua juu yake? Wanapaswa kumuozesha tu Bwana Shangwe kulingana na viwango vya wanawake hawa watano.]

Lisa alifurahi kutokana na kutazama maoni. “Wewe ndiye uliyefanya hivi?” Alirudisha simu kwa Pamela. Watu wengine wanaweza wasijue, lakini alielewa kila kitu. Rodney alikuwa amejitolea kabisa kwa Sarah. Hakika huo ulikuwa ni mzaha kwake.

“Haha, ni kweli. Nilikutana naye kwenye baa jana usiku. Alikuwa amelewa kabisa hajitambui, kwa hiyo nilimpeleka chumbani na kumletea wanawake wachache.” Pamela alikuwa akitabasamu. "Wanawake hao ni bora kuliko Sarah, sawa?"

Lisa alimtazama bila kuonesha dalili za kufurahishwa. “Unaweza kumfanyia chochote unachotaka, lakini hukupaswa kuwaita waandishi. Nilisikia Baba mdogo wa Rodney atagombea urais hivi karibuni. Ikiwa suala hili litakuwa kubwa, hakika litaikasirisha sana familia ya Shangwe."
“… Huu.” Pamela alihisi hofu kidogo kutokana na kusikiliza maneno yake. “Ni… pengine sivyo? Sijawahi kusikia kuhusu familia ya Shangwe kuwa na mgombea urais.”

"Sina uhakika pia, lakini unaweza kuwa umeharibu sifa ya Rodney. Kuwa makini tu.” Lisa alimtupia jicho la tahadhari kisha akageuka na kutoka nje.

Pamela alimfuata kwa wasiwasi. Ghafla, aliona kadi ya mwaliko kwenye meza. Aliifungua na kutazama. Ilikuwa ni mwaliko wa harusi ya Alvin na Sarah. “Nani alikutuma hivi?”

“Nani mwingine we unadhani anayeshindana nami?”

"Huyu mwanamke hana aibu kabisa."” Pamela alisema baaa ya kugundua kuwa ni Sarah. “Ni wazi alikualika kwenye harusi ili kukuaibisha na kujionyesha. Unakwenda.?"

“Bila shaka, sina budi kwenda. Baba yangu pia amealikwa. Nitaenda naye.” Lisa alitabasamu kwa unyonge. "Harusi hii inaweza isiweze kuendelea vizuri hata hivyo."

"Una hoja hapo." Pamela alipiga miayo. "Nitaendelea kulala."
•••
Hotelini. Baada ya Rodney hatimaye kupata watu wa kuwafukuza waandishi na wale wanawake, akawasha simu yake. Alipoona maoni ya kejeli yaliyoachwa na wanamtandao, nusura ashikwe wazimu. Ilikuwa ni nani? Ni b*tch gani alikuwa akimchezea mzaha?

Alikumbuka kuwa alikuwa amelewa sana usiku, na alikuwa peke yake. Mwishowe aliota ndoto isiyoeleweka. Kulikuwa na mwanamke kama Sarah ambaye alikuwa na harufu ya kupendeza. Alinukia vizuri na alikuwa laini kiasi kwamba alikaribia kupoteza fahamu.

Mwishowe, alipoamka, lilikuwa ni kundi lile la wanawake wa kutisha.
Kulikuwa na hisia ya kichefuchefu tumboni mwake. Hakuweza kuvumilia tena na kukimbilia bafuni kutapita.
Baada ya kutoka, mara moja alimtafuta meneja wa hoteli ili kuangalia kamera za usalama. Alipokagua picha za usalama kuanzia usiku wa manane, alimuona mwanamke akimsaidia kuingia ndani ya hoteli hiyo.
Alipomtazama vizuri yule mwanamke usoni, nusura azimie kwa hasira.
Alikuwa ni Pamela Masanja!

Alikuwa ni b*tch huyo, Pamela Masanja? Aliharibu sifa na picha ambayo alikuwa ametumia maisha yake yote kuilinda. Ilibidi amlipe kwa hilo.

Wakati huo simu ya Rodney ikaita. Alikuwa Chester akimpigia. Chester alituliza koo lake mara mbili na kusema huku akizuia kicheko chake, “Hivyo ndivyo ulivyomaanisha uliposema una jambo la kufanya jana usiku? Wow, Rodney. Kwa kawaida hukaa mbali na wanawake, lakini ulifanya kila mtu ashangae ulipowagusa. Siwezi kujilinganisha na wewe hata kidogo. Lakini staili yako ni ya kipekee.”

"Nyamaza!" Rodney alifoka kwa aibu. "Niliundiwa njama na yule b*tch, Pamela."

"Sikuwahi kujua kuwa alikuwa mbunifu hivi." Chester alikuwa akifurahi. "Kwahiyo ulipoteza ubikira wako jana usiku?"

“Bado wewe ni rafiki yangu?” Rodney aliuma mdomo. “Ikiwa ndivyo, unapaswa kunisaidia kuzima habari hizi zisienee zaidi.”

“Sawa, njoo haraka. Ni harusi ya Alvin leo. Usisahau, wewe ni mtu wa heshima." Chester alimkumbusha vizuri. Hapo ndipo Rodney alipokumbuka kuwa ilikuwa ni harusi ya Sarah na Alvin siku hiyo.

Alihisi huzuni na kufadhaika jana yake usiku. Lakini, baada ya shida aliyomletea Pamela, alihisi hasira tena kusikia Sarah anaolewa. Hakutaka hata kuhudhuria harusi hiyo. Alitaka tu kumtafuta mwanamke huyo na kumalizana naye.

Sura ya: 394

“Tafuta mtu mwingine awe mtu wa heshima. Nitakuja kwenye sherehe alasiri. Nina deni la kumalizana na Pamela kwanza, kabla hajatoroka." Rodney alifikiria kati ya pande zote mbili kwa muda, lakini mwishowe, alimkataa Chester.

“Sawa, usichelewe.” Baada ya simu kukatika, mara moja Rodney alimtaka mtu fulani kujua anwani ya sehemu alipo Pamela. Kisha, alienda kwa kasi hadi eneo lile.

Alipofika nyumbani kwa Lisa, Karen Estate, hakuna aliyejibu mlango licha ya yeye kubisha hodi kwa muda mrefu. Lisa alikuwa ameshaenda kazini muda huo na ndani alibaki Pamela peke yake akiwa amelala.

Alipojaribu kuufungua mlango ulimwitikia, akaingia sebuleni. Lakini hakujua chumba cha Pamela ni kipi, kati ya vyumba viwili vya nyumba ile.

Baadaye Pamela alitoka baada ya kusikia purukushani ya mtu hapo sebuleni. Alipofungua mlango wa chumba chake na kuchungulia, alishangaa kumuona Rodney.

“Rodney, labda hujui kuwa tulivamiwa hapa juzijuzi na majambazi. Nikipiga simu polisi sasa hivi hakika utakuwa kwenye matatizo. Nakusihi uondoke kabla sijafanya uamuzi mbaya,” alipomaliza kuongea hayo, Pamela alimpuuza na kurudi kulala.

Punde, Rodney aliupiga teke mlango wa chumba cha kulala cha Pamela. Alipomwona yule mwanamke pale kitandani amelala bila kujali, wimbi la hasira lilimtoka moyoni hadi juu ya kichwa chake.

"Pamela Masanja, unawezaje kulala wakati umeniona kabisa?" Rodney akavuta blanketi lake. Mwanamke yule chini ya blanketi alivaa tu nightdress ya pink, fupi iliyokataa kabisa kuyahifadhi mapaja yake manono. Hata kifuani kwake pia kuliacha hali ya taabani kwa mwanamume kumuangalia. Ngozi ya uso wake ilikuwa imejikunja kutoka usingizini.

Kuonekana kwa ngozi yake nzuri kulijaza mtazamo wa Rodney. Kupumua kwake kukawa kwa shida.
Wanawake wale aliowaona asubuhi walikuwa wamevaa nguo za kuvutia, lakini hawakuweza kulinganisha na sura ya Pamela. Alikuwa na kiuno chembamba na miguu mirefu minen. Kifua chake kilikuwa zaidi ...oooh! Mungu wangu!

Pamela alipiga kelele. Alichukua sweta kutoka upande wake na kuivaa kwa wasiwasi. “Rodney, toka nje! ” Alichukua mto na kumpiga usoni wakati anavaa.

Rodney, ambaye alipigwa usoni na mto, alikuwa na hasira. “Unathubutu vipi kunipiga? Pamela Masanja, usifikiri sijui wewe ndiye uliyewapigia simu wale wanawake jana usiku. Wewe ndiye uliyewafahamisha waandishi pia, sivyo? Umefanya sifa yangu kuharibika. Jina langu la mwisho sio Shangwe ikiwa sitakufundisha somo linalofaa wakati huu.”

“Nilijua kwamba ungenilaumu, kwa bahati nzuri, niliweka ushahidi. ” Pamela akatoa simu yake kwa haraka. “Nilirekodi yote. Ni wewe uliyesema unataka jana usiku, na mimi nikafanya kama kukusaidia.”
Alicheza rekodi ya sauti baada ya kusema. Sauti ya Rodney ya kilevi ilisikika.

“Nataka…”

“Sawa, nitakusaidia kama unataka. Hutmwambia mtu sawa?”

"Hapana, siwezi kumwambia mtu yoyote."

Uso mzuri wa Rodney ulibadilika huku akikasirika. Hakuamini kwamba angeweza kusema maneno kama hayo jana usiku.

"Kwa hiyo mimi na wewe nani anayepaswa kulaumiwa?" Pamela alisema huku akilia, "Uliendelea kunishikashika huku ukinikumbatia jana usiku. Kwanza ulinidhania mimi ni Sarah, lakini bado ulitaka kufanya hivyo. Sikuweza kuchukua faida ya wewe kuwa umelewa ili nilale na wewe kwa sababu najua kuwa mimi sio aina yako kwa hivyo, sikuwa na jinsi zaidi ya kupiga simu. Una mtarimbo mkubwa na mwili mzuri, kwa hivyo nilikuwa na wasiwasi kuwa mwanamke mmoja asingeweza kukuridhisha. Kwa hiyo, niliwaita wanawake watano.”

"Nyamaza!" Kichwa cha Rodney nusura kiripuke kwa hasira. Angekuwa na shimo kwenye ubongo wake ikiwa angeamini maneno yake.

"Kwa kweli sikujua ... kwamba wanawake hao wangekuwa wabaya sana. Sikufanya kwa makusudi,” Pamela alisema kwa uchungu, “Labda kwa sababu walikuwa nafuu sana. Ilikuwa dola 100 kwa kila mwanamke.”

"Dola 100 ...?" Rodney karibu ateme damu. “Pamela Masanja! Ulienda mbali zaidi kufanya kitu kama hicho.”

"Hiyo ni sawa. Sikuweza kupata wale wanawake ambao walitoza dola 1,000. Ingenigharimu dola elfu tano kwa usiku mmoja. Ungenikana na usinilipe baadaye, ningepata hasara kubwa.” Pamela alikuwa na sura isiyo na hatia usoni mwake. "Kwa hiyo, mimi ndiye nililipa pesa yote jana usiku. Una deni langu la dola 500 kwa ajili ya wanawake na dola 50 kwa ajili ya chumba cha hoteli."

“Sawa, nitakupa dola 550 lakini utazitumia ukiwa ahera." Rodney aliushika mguu mmoja wa Pamela na kumburuta. Wakati anakaribia kufika mlangoni, simu yake ikaita.

Kwa haraka Pamela akachukua fursa hiyo na kumpiga teke la uso. Kisha, alikimbia kwa haraka.

“Simama hapo hapo!” Rodney alimfuata, lakini simu yake iliendelea kuita. Alipokea simu kwa hasira. “Temea mate. Niko katikati ya jambo fulani.”

“Lo, inaonekana bado hujamaliza mambo yako, Bro? Kulala na wanawake watano usiku hukuridhika, kwa hiyo hata mchana unaendelea kukutana na wanawake wengine?” Sauti ya kejeli ilisikika.

Rodney akatazama jina la mpigaji. Alikuwa Jessica Shangwe, dada yake. Rodney alitetemeka kwa hofu. "Big Sis, sikujua ni wewe."

"Inatosha. Mimi ni mvivu sana kuzungumza upuuzi na wewe. Njoo nyumbani haraka. Babu anakutafuta,” Jessica alisema kwa ukali.

Rodney alikuwa karibu kulia. "Big Sis, jana usiku ilikuwa-"

“Babu ana hasira sana,” Jessica alimkumbusha. “Ni bora ukawahi.”

Rodney alitetemeka. “Nakuja sasa hivi.”

“Kuwa makini tu.” Jessica akakata simu.

Rodney alitaka kulia, lakini hakuwa na machozi. Kwa kweli alifanywa kuwa kituko cha mwaka na Pamela.

Saa moja baadaye, Rodney aliingia kwenye jumba la kifahari la familia ya Shangwe. Alipoingia ndani, alimuona tu Mzee Shangwe, wazazi wake, dada yake Jessica, na mdogo wake Carson sebuleni. Alijisikia aibu.

Ilikuwa ni jambo zuri kwamba shangazi zake na wajomba zake hawakuwepo hapo. Vinginevyo, wangemhoji kabisa na angejisikia kufa kutokana na hilo.

"Kaka, umerudi." Mdogo wa Rodney, Carson, alimtania huku akitabasamu. "Nikupatie tonic ya kupunguza uchovu? Ninahofia kwamba wanawake wale watakuwa wamekukamua kila kitu mwilini.”
Rodney alimtazama kwa hasira. Haraka akaenda kumimina kikombe cha kahawa kwa Mzee Shangwe katika harakati za kujipendekeza.

“Sikilizeni maelezo yangu. Nilifanyiwa njama na mtu jana usiku—”

"Piga magoti," Mzee Shangwe alisema kwa ukali huku akishikilia kikombe cha kahawa.

Babake Rodney, Jason, alimuonya, “Piga magoti haraka. Babu yako amekuamuru na bado unajishauri?” Rodney hakuwa na la kufanya zaidi ya kupiga magoti chini.

Mzee Shangwe aliweka kikombe chake chini kwa kishindo. "Kwanini familia ya Shangwe ina kijana mwenye aibu kama wewe? Uchaguzi wa Rais ni mwaka ujao, baba mdogo wako anafanya jitihada kulinyanyua jina la Shangwe, lakini wewe uko busy kulididimiza. Kwanini unakuwa kikwazo kwa familia ya Shangwe? Umekuwa kicheko cha Nairobi nzima mapema asubuhi sana.”

Mamake Rodney, Wendy, alipumua na kusema, “Juzi, shangazi yako alinuia hata kukuoza kwa bintiye Mkurugenzi Lawson. Walisikia kuhusu suala hilo asubuhi ya leo na kukataa binti yao kuolewa na wewe bila kusema neno lingine. Niambie, ni binti gani kutoka kwa familia zinazofaa atathubutu kuolewa na wewe katika siku zijazo?"

"Hilo sio jambo kubwa hata kidogo." Rodney aliinamisha kichwa chini. Hata hivyo hakutaka kuoa. Kila mwaka, alikasirika zaidi wakati familia yake ilipanga wachumba kwa ajili yake.

"Nyamaza." Sauti ya Mzee Shangwe ilikuwa ya moto.

Rodney alisema kwa uchungu, “Babu, nilikuwa nimelewa jana usiku. Kwa kweli sikujua chochote. Alikuwa ni mwanamke anayeitwa Pamela Masanja ambaye aliwaita wanawake hao. Sikuwagusa.”

"Tayari tumelichunguza.".......ITAENDELEA.....

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.