JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................391-392
Sura ya: 391
Pamela alipoinua macho yake kumwangalia kwa hasira, Thomas aliogopa sana hivi kwamba alijificha nyuma ya Sarah.
Sarah aliinua mkono wake na kuweka nywele zake nyuma ya sikio lake. Wakati huo huo, alifunua pete ya almasi inayometa kwenye kidole chake cha shahada. "Kesho itakuwa sikukuu ya harusi yangu na Alvin. Itahudhuriwa na familia zote mashuhuri hapa Nairobi. Ukithubutu kunipiga, utakuwa umeichokoza tu familia ya Kimaro, na Alvin hakika atafanya jambo kuhusu hilo. Nawashauri mfikirie kwa makini.”
Alipouona uso wa Lisa, Sarah alishindwa kujizuia kutabasamu kwa hasira. “Hii ndiyo pete ya almasi ambayo Alvin alinipa jana. Ina uzito wa gramu 13.14. Ni ya gharama sana. Mtu fulani asitegemee kabisa kama kidole chake kinaweza kuwa na bahati ya kuvaa pete kama hii.
Lisa alisonya tu kwa dharau. Jana yake alitoka kuitupa pete hiyo kwenye pipa la taka aliporudishiwa na Alvin wakati anaingia ofisini. Kumbe Alvin alienda kuiokota tena na kumpelekea Sarah?
“Hizo ni zilipendwa, nilikuambia kuwa wewe ni wa kuambulia makombo tu.” Lisa alimwambia bila kufafanua.
Pamela aliingilia kati. "Ni ndogo sana ukilinganisha na zawadi ambazo Alvin alimpa Lisa wakati huo. Alvin hata alimpa Lisa Mkufu wa almasi wenye thamani ya shilingi bilioni tatu. Unaitwa Mkufu wa Malkia.
Umewahi kusikia juu yake? Ni mkufu ambao wapenzi wakipeana hawawezi kuachana tena."
Tabasamu la Sarah likawa gumu. Hakika alikuwa amesikia kuhusu Mkufu wa Malkia. Baada ya yote, wanawake wengi wa Kenya kutoka familia za kifahari walikuwa wamesikia kuhusu hilo. Ni nani asiyependa kupokea Mkufu wa Malkia, ambao uliashiria mapenzi ya milele, kutoka kwa wanaume wao wapendwa?
Kwa mawazo kwamba Alvin alimpa Lisa mkufu ule, alikasirika sana kiasi kwamba uso wake ulikaribia kugeuka kuwa kama msukule.
"Acha, Pamela. Yote ni ya zamani.” Lisa akahamishia macho yake kwa Sarah. "Hata hivyo, niliurudisha Mkufu wa Malkia tulipoachana. Nilimpa Sam amrudishie Alvin. Nadhani amempa.”
Sarah alikasirika sana. Alikuwa hajawahi hata kuuona mkufu ule. Aidha, Lisa alimaanisha nini kwa kuurudisha? Hata kama Alvin angempa Sarah, ingefanya ionekane kama Sarah amekubali makombo yake.
Pamela alienda sambamba na maelezo ya Lisa. “Bi. Njau, huoni hata kinyaa kuchukua makombo ya watu wengine?”
“Sawa. Nitamjulisha Alvin kuwa mmemwita takataka leo.” Sarah aliwaambia kwa jeuri. Watu hao wangekuwa takataka kwake baada ya kesho.
“Utajua mwenyewe.” Lisa alimjibu na kumpuuza kisha pamoja na Pamela wakaweka maua mbele ya kaburi. Kisha, walitoa heshima zao kwa Boris na Jennifer.
Sarah aliinua kichwa chake. "Mnaweza kutoa heshima zenu kwa baba yangu, lakini hakuna haja ya kutoa heshima zako kwa mbwa aliye kando yake."
Sura ya kutisha iliangaza machoni mwa Lisa. Boris na Jennifer walizikwa pamoja, lakini Sarah alikuwa amebadilisha mwili wa Jennifer na kuweka mbwa.
"Sarah Langa, wewe ni mbaya kuliko mbwa," Pamela alimshambulia kwa hasira.
"Angalau Lisa bado anaweza kushindana nami. Wewe kwangu ni kituko tu. ” Sarah alimpiga Pamela jicho la dharau.
“Wewe si mwanasaikolojia tu? Naam, na mimi ni mwanakemia wa vipodozi maarufu. Je, unadhani una hadhi ya juu kwa sababu tu uko na Alvin? Labda ningeolewa na mwanamume tajiri zaidi duniani katika siku zijazo, na wewe usingekuwa kitu kwangu.” Pamela alidhihaki, “Jiangalie. Ukiweza kuolewa na Alvin licha ya kuwa mkubwa na mbaya kuliko mimi, nina uhakika nitaweza kuolewa na mwanaume bora.”
“Wewe…” Akiwa ameudhishwa na shutuma zake, Sarah alihisi kutaka kupiga kelele. Alichukia zaidi watu waliposema kwamba alikuwa mkubwa kuliko wao. Ilikuwa kama mwiba kwake, hasa ikilinganishwa na mwanamke mrembo kama Lisa.
Kabla Sarah hajapandwa na hasira, ghafla sauti ya ngurumo ikasikika.
"Pamela Masanja, muombe msamaha Sarah sasa hivi." Rodney alitembea kando ya makaburi na kumsogelea akiwa na sura mbaya usoni mwake.
Thomas alimtazama Rodney kana kwamba ndiye mwokozi wa maisha yake na mara moja akamsogelea. “Bwana Shangwe niokoe. Mwanamke huyu ni mkatili sana. Alinipiga mara tu aliponiona. Alitaka hata kumpiga dada yangu, lakini kwa bahati nzuri, ulikuja kwa wakati.”
"Rodney, hatimaye umefika." Macho ya Sarah yalikuwa mekundu, na alionekana mwenye huzuni.
Kwa kuona hali hiyo, Rodney alishindwa kujizuia. Alimtazama sana Pamela machoni kana kwamba atamla. "Mwanamke katili kama wewe anataka kuolewa na mwanamume tajiri zaidi duniani, eh? Endelea kuota. Msifikirie kuondoka mahali hapa ikiwa nyinyi hamtapiga magoti na kuwaomba msamaha.”
Pamela alikosa la kusema. “Subiri, una uhusiano gani na Sarah? Kwanini anapenda kukutafuta wewe badala ya Alvin anapoonewa? Mnaweza kuwa na uhusiano wa kimapenzi, eeh?"
“Usiwe mjinga. Sarah ni rafiki yangu.” Damu ya Rodney ilichemka. Aligundua kuwa alikuwa na hamu ya kumpasua mdomo mwanamke huyo kila anapojibizana naye.
"Wewe una rafiki mzuri sana aliye tayari kukusaidia muda wowote zaidi hata ya mumeo mtarajiwa." Pamela alimtazama Sarah kwa mshangao. "Nakutamani. Sio tu kuwa una mpenzi tajiri, lakini pia una rafiki wa karibu ambaye anaweza kukulinda kila wakati. Lakini, kwa yeyote mwenye akili timamu, anaweza kusema kwamba Rodney anakupenda, sivyo?”
"Pamela Masanja, unazungumza upuuzi gani?" Hali ya hofu ilitanda usoni mwa Rodney huku akimvuta Pamela haraka. "Nyamaza."
Sarah hakuwa mtulivu pia. Kwa muda mrefu alikuwa amejua kwamba Rodney alikuwa akipendezwa naye. Hata hivyo, hawakuwahi kuzungumzia jambo hilo waziwazi. Sasa baada ya Pamela kufichua jambo hilo mbele ya Sarah na Rodney, wote wawili walikuwa wamefedheheka sana.
“Pamela yuko sahihi. Nimeliona hilo zamani pia,” Lisa aliongeza. “Hata ulinilazimisha niachane na Alvin enzi hizo. Nadhani inafaa kukuita Romeo kwa kuwaleta Sarah na Alvin pamoja kwa siri.”
“Ndio hivyo. Nilisikia kuwa hujawahi kuwa kwenye uhusiano kabla.” Pamela alitoa mtazamo wa ajabu kwa Rodney. “Wewe… Unapohitaji kukidhi mahitaji yako, huwa unamfikiria Sarah?”
"Pamela Masanja, unatamani kifo?" Kichwani mwa Redney kilisikika kishindo cha hasira, na mwale wa hasira ukaangaza usoni mwake. Hakuweza kupinga kunyoosha mkono wake kumpiga Pamela usoni.
Lakini, Pamela hakuwa mjinga. Alimkwepa mara moja na kukimbia huku akimshika mkono Lisa.
Nusu ya kukimbia kwake, aligeuka na kupiga kelele, “Sarah Langa, wewe ni mbaya sana. Utaolewa kesho, bado una mwanamume mwingine wa kumpigia simu. Huna aibu? Pia, nakuonea huruma Rodney.”
Kila neno la Pamela lilikuwa kama kofi kwenye nyuso za Rodney na Sarah. Sarah alikuwa na aibu, huku Rodney akiwa mwendawazimu na mwenye huzuni isiyo na kifani.
"Subiri hapo hapo, Pamela Masanja." Wakati huo, Rodney hakuwa na jinsi ya kukabiliana na Sarah, kwa hiyo kitu pekee alichoweza kufanya ni kumfuata Pamela badala yake.
“Jamani. Anakuja nyuma yetu. Haraka tukimbie, sina mood ya kupigana na mtu tena. ” Pamela hakutarajia hilo. Aliogopa sana hivi kwamba alishika mkono wa Lisa na kukimbia kwa nguvu huku akimkokota Lisa.
Hatimaye walipoingia ndani ya gari, Lisa alifunga mlango haraka na kuwasha gari. Pamela aligeuka nyuma na kumkoromea Rodney, ambaye alikuwa bado akiwakimbilia. “Unataka kunipiga kwa sababuya Sarah? Hutaki fomula?”
Rodney alishusha pumzi ndefu huku akihema. Kuangalia macho yake ya kuvutia, alitamani kumuua mara moja. "Kwa hiyo unanitisha kwa sababu ya fomula?"
"Ukithubutu kunigusa, unaweza kusahau," Pamela alijibu huku akivaa miwani yake ya jua kwa ujasiri.
Sura ya: 392
Huko nyuma, Thomas alisema, “Angalia jinsi Bwana Shangwe anavyokupenda. Sarah, wewe ni wa ajabu. Baada ya miaka mingi, si tu kwamba ulimpata Alvin kuwa mpenzi wako tena, lakini pia una Rodney Shangwe kama mbadala wake.”
Ingawa familia ya Shangwe haikuwa na ushawishi mkubwa kama familia ya Kimaro, ilikuwa moja ya familia tano bora nchini Kenya. Mbali na hilo, watoto wa familia ya Shangwe walihusika katika siasa na biashara, tofauti na Kimaro, ambao walikuwa na nguvu kwenye biashara pekee na Alvin ndiye alikuwa mtu mkubwa nyuma yake.
Uvumi ulikuwa umeendea kwamba Baba mdogo wa Rodney ndiye angekuwa mgombea wa Urais katika uchaguzi mkuu wa Kenya wa mwaka uliopita. Miongoni mwa wagombea wote, aliaminika kuwa na nafasi nzuri ya kushinda. Wanawake wengi matajiri walipendezwa na Rodney, lakini alikuwa akimpenda tu Sarah ambaye alimchukulia kama kaka yake.
"Kweli, mtu hatakiwi kuchoma madaraja yoyote." Sarah akahema. "Ikiwa Alvin atanitupa siku moja, bado ninaweza kwenda kwa Rodney."
“Hilo litawezekanaje? Unafunga ndoa kesho.” Kadiri Thomas alivyozidi kuwaza juu ya jambo hilo, ndivyo alivyokuwa akiingia kwenye mkanganyiko. "Hata hivyo, Bwana Kimaro ni bora kuzingatia uwezo wake. Kwa maana hiyo, Bwana Shangwe hana uwezo kama yeye.”
“Ndio, lakini pia siwezi kumpoteza Rodney. Anaweza kuniunga mkono kila wakati.” Sarah alicheza na vidole vyake. Rodney alikuwa mjinga wa kudanganyika kirahisi kuliko Alvin. Alimpenda sana Sarah hivi kwamba angefanya chochote kwa ajili yake.
•••
Usiku wa manane kwenye baa. Rodney alilala kwenye kaunta ya baa, akishusha glasi kadhaa za pombe. Kwa sababu asizoweza kuzijua, alijikuta moyo wake ulimuuma sana alipofikiria ndoa ya Sarah na Alvin kesho yake. Juu ya kukata tamaa, pia alivunjika moyo.
Wakati huo simu ya Rodney ilitetemeka. Chester alikuwa amemtumia ujumbe wa sauti wa WhatsApp. [Uko wapi Rodney? Alvin anafunga ndoa kesho. Tukutane kwenye jumba la klabu na kumshangilia akiingia kwenye kaburi la mapenzi.]
Aliinamisha kichwa chake na kujibu ujumbe wake: [Kuna kitu kimenitinga ghafla, kwa hivyo sitaweza kujiunga. Hii si mara yake ya kwanza kuingia kwenye kaburi la mapenzi hata hivyo.]
Baada ya hapo, aligonga meza. "Nipe chupa chache zaidi."
Aliendelea kunywa hadi saa saba usiku. Alipotoka nje ya baa ile, aligongana na mtu kwa bahati mbaya kwa sababu alikuwa akiyumbayumba sana. Alikuwa amelewa sana hivi kwamba alipoteza stepu na kuanguka chini.
Mwanamke ambaye aligongana naye alimtazama kwa uchungu. Mara tu alipomtazama usoni kwa karibu, alishtuka.
“Nina bahati mbaya kiasi gani kukutana na huyu fala mara mbili kwa siku moja? Mara ya kwanza kwenye makaburi leo mchana, na sasa kwenye baa?” Pamela alishangaa moyoni mwake.
Pamela alikuwa pale usiku huo kukutana na wafanyabiashara kadhaa wa tasnia ya vipodozi kujadili madili fulani ya biashara. Maongezi yalipoisha waliendelea kujipongeza kwa vinywaji hadi usiku wa manane.
"Ah, Pamela. Una bahati. Umegongana na mwanamume mwenye kuvutia,” Mmoja kati ya washirika wake kibiashara alimtania.
“Yeye?” Pamela alikosa la kusema. “Oh kumbe ni yeye? Nimemfahamu. Ni bosi wangu wa zamani. Kwanini nyie msiondoke tu? Nataka kumsaidia. Siwezi kumuacha katika hali hii.”
“Ooh, ni Rodney Shangwe? Anaonekana mzuri sana ingawa.” Binti mmoja ambaye ni model wa bidhaa za vipodozi, alimtania kwa kumnong’oneza. “Unaweza kuchukua fursa hii kufanya naye kwa vile amelewa.”
Akiwa ameumizwa na kejeli yake, Pamela alipunga mkono wake. "Kama unamtaka nitawakodishia chumba hapa niwaache ukifurahi naye."
“Ooh! Hapana, nilikuwa natania tu. Wewe msaidie tu.” Wale watu wakaondoka na kumuacha.
Mara wale washirika zake walipoondoka, alienda kwa Rodney na kumpiga teke. "Hey, unajua mimi ni nani?"
Rodney aliinua kichwa chake na kukodoa macho kabla hajazungusha mikono yake kwenye mapaja yake. “Sarah? Wewe ni Sarah?"
“Jamani!” Pamela alijiuliza ni sehemu gani kati ya mwili wake inafanana na yule b*tch.
“Sarah. Sarah, nimekasirika kwamba kesho utafunga ndoa. Sarah, nakupenda. Unajua kwamba nakupenda?" Rodney aliendelea kugugumia huku akikumbatia mapaja ya Pamela.
Pamela hakuguswa hata kidogo na tabia yake ya Romeo. Badala yake, alichukizwa zaidi na maneno yake, na alihisi kuwa sura yake nzuri ilikuwa bure. Alikuwa na sura nzuri sana, lakini kulikuwa na kitu kibaya sana mfano wa matope tu kwenye ubongo wake.
Kwanini awe na mapenzi na Sara? Si alikuwa mpenzi wa rafiki yake? Hilo halimkuhusu sana Pamela, lakini kwa kuwa alikuwa amempania Rodney muda mrefu, ilimpa hamu ya kumfundisha somo huyo boya, au asingekuwa binti wa Masanja.
“Sawa. Sawa. Najua. Sasa inuka.” Pamela alimtuliza kama atakavyokuwa na Suzie na kumuinua Rodney. Magoti yake yaligongana. Wakati huo, alikosa stepu tena na akaanguka juu ya Pamela. "Sarah, mwili wako ni laini sana ...harufu yako nzuri sana. Nakupenda.”
Pamela, ambaye alikuwa akibebishwa hadharani, aliingiwa na aibu. Akashusha pumzi ndefu. Sasa kwa kuwa alikuwa ametoa mwili wake, angeshughulika naye baadaye. Alijikongoja na kumpeleka kwenye hoteli iliyo mkabala.
Hoteli hiyo ilikuwa imezungukwa na baa. Mhudumu wa mapokezi wa hoteli, ambaye alikuwa amekumbana na hali kama hiyo mara nyingi, aliwapa kadi ya chumba bila mashariti.
Pamela alipotaka kumweka Rodney kitandani baada ya kumuingiza chumbani, Rodney alimshika mikono yake kwa nguvu hadi akamvuta kwake. “Usiondoke…”
“Sawa, sitaondoka.” Sauti ya mvuto wa Pamela ilisikika kando ya sikio la Rodney. “Sasa kwanini ulichelewa kuniambia kuwa unanipenda hadi sasa naolewa na Alvin?”
“Nilikuwa namuogopa kaka mkubwa.” Rodney aliongea kilevi. “Lakini nakupenda kuliko hata Alvin.”
“Kweli? Kwa hiyo tunaweza kufanya?” Pamela alitembeza mikono yake kwenye kifua cha Rodney taratibu ili kufanya asiweze kujizuia.
“Ndiyo…”
“Sawa. Nitafanya kwa sababu umetaka. Iwe siri yako, sawa?”
“Ndiyo. Sitawahi kumwambia mtu.” Rodney alihisi kama yuko kwenye ndoto ambapo alikutana na mrembo wa warembo ambaye alikuwa akiukonga moyo wake.
Baada ya kubonyeza kitufe cha kusitisha kurekodi, Pamela alipigapiga kifua chake. Ilibidi akubali kwamba wakati mwingine wanaume walikuwa kama watoto. Alimtendea Rodney kama ambavyo angemtendea Suzie, alimbembeleza taratibu hadi akalala.
Ni wakati tu hatimaye alikuwa na usingizi mzito ndipo alipojitahidi kujinasua kutoka kwenye kumbato lake. Kisha akapiga namba fulani. “Una wanawake? Naweza kupata baadhi? Nataka watano.”
“Watano?” Mtu wa upande mwingine alishtuka.
"Ndio, lakini sipendi wale wa bei. Nipatie wa bei nafuu… Asante. Fanya haraka uwalete hapa.”
Baada ya simu kukatika, Pamela alimsogelea Rodney na kumvua nguo huku akitabasamu. Alipokaribia kuvua nguo zake zote, uso wake ukamtoka, na vipepeo wakapeperuka tumboni mwake.
Hakutarajia kuwa mwanaume huyu angekuwa na rungu kubwa vile. Alikuwa na bonge la BBC, tena likiwa limesimama wima. Lakini, yeye hakulihitaji hata hivyo. Angepata wanawake wazuri wa kulitumia ipasavyo.
Dakika kumi baadaye, wanawake watano wenye sura zisizo za kawaida walitokea mlangoni. Pamela aliwapa maelezo kadhaa kabla ya kuondoka kwa furaha.
Mara tu aliporudi Karen Estate, alimpigia mwandishi wa udaku. “Haya, unatoka kwenye mtandao wa Udaku Live? Nina habari motomoto…”
•••
6:00 asubuhi siku iliyofuata, Rodney aliamshwa kutoka kwenye hangover alipohisi harufu kali ya manukato, ambayo ilisumbua tumbo lake.
Alifumbua macho kwa kuduwaa na kutazama dari tupu kwa sekunde kadhaa. Kisha, mwanamke akaweka mkono wake juu ya kifua chake na kusema kwa upole kando ya sikio lake, "Umeamka, mpenzi."
Rodney aligeuza kichwa chake kigumu na kumkuta mwanamke mwenye mdomo mkubwa, macho madogo madogo na meno kama ngiri, akitabasamu kwa kupendeza........ITAENDELEA.....
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
