JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................395-396
Sura ya: 395
Mzee Shangwe alisema kwa hasira, “Usifikirie kuwa sijui kwanini ulikunywa hadi kuzima jana usiku. Je, si kwa sababu Sarah anaolewa leo? Familia ya Shangwe ni familia maarufu pia. Kwanini tunakatishwa tamaa na kijana kama wewe? Kwani, Nairobi ina uhaba wa wanawake hadi unalazimika kumfukuzia Sarah siku nzima? Mjukuu wangu, unachukuliwa kama tairi la akiba katika uhusiano. Hata kama huoni aibu, mimi na wazazi wako tunaona hivyo.”
“Babu, maneno yako ni mengi sana. Mimi si mpenzi wake. Mimi na Sarah ni marafiki wazuri,” Rodney alieleza bila raha.
Wendy alisema kwa hasira, “Kama nyinyi ni marafiki wazuri tu, kwanini unaenda kwake popote na wakati wowote anapokuhitaji? Zamani ulipokuwa ukisoma, shajara yako ilijazwa na jina la Sarah pia.”
“Mama, unazidi sana. Hata ulichunguza shajara yangu.” Rodney alikasirika.
“Wewe ni mwanangu. Sitaki uchukuliwe kama mpumbavu na wengine,” Wendy alisema kwa hasira. "Nililifumbia macho hapo awali, lakini Alvin tayari anamuoa sasa. Wewe pia sio kijana mdogo tena, lakini hata umesababisha tukio la aibu kama hilo sasa. Ninachukuliwa kama kituko kila ninapoenda nje. Wale wasiojua vizuri zaidi watafikiri kwamba sikumfundisha mwanangu vizuri.”
Mzee Shangwe alisumbua. “Usifikiri kuwa sifahamu suala la Pamela pia. Miaka mitatu iliyopita, alikuwa mkemia mwenye kipaji cha vipodozi katika kampuni yako ya Osher. Kwa sababu tu ya chuki yake binafsi na Sarah, ulimshutumu kwa wizi na hata kumfanya asiajiriwe kwenye tasnia hiyo. Ninaweza kuwa mzee, lakini bado sijachanganyikiwa. Kwanini alilipiza kisasi kwako jana usiku? Wewe ndiye uliyejilsababishia. Ulistahili!”
“Babu…” Rodney alichanganyikiwa kabisa. Hakutarajia kwamba familia yake mwenyewe ingechukua upande wa Pamela. “Tafadhali, hivi mimi ni mjukuu wako kweli?”
"Mimi, Derek Shangwe, pia ningependa kujua kwanini nina mjukuu kama wewe licha ya kuwa nimeishi kwa heshima na uadilifu maisha yangu yote." Mzee Shangwe aligonga meza kwa hasira na kusimama. “Angalia baba zako, shangazi zako, kaka zako na dada zako. Wote ni watu wa heshima. Ni nani kati yao anayefanana nawe?”
“Baba usikasirike sana kwani itakuathiri tu afya yako.” Jason alipapasa mgongo wa Mzee Shangwe.
“Wewe ni aibu kwa familia. ” Mzee Shangwe alishusha pumzi ndefu. Kisha, ghafla akasema, "Ulisema kwamba ni Pamela aliyekufanyia njama. Kwa kuwa tayari amekuharibia sifa nzuri, basi itabidi akufidie hilo.”
“Fidia… atanifidia nini?” Rodney aliguswa. Alijua kuwa yeye ndiye mjukuu kipenzi wa babu yake, hata hivyo. Familia yake bila shaka ingemsaidia.
“Atakufidia kwa ndoa. Itabidi aolewe na wewe.” Mzee Shangwe alihema. "Ingawa hali ya familia ya Masanja iko chini sana, hili ndilo chaguo pekee ambalo tumesalia nalo."
Rodney alipigwa na butwaa kabisa. Amuoe Pamela? Hapana, hapana, hapana! "Babu, unafanya utani wa aina gani huu?"
“Ninaonekana kama ninatania?” Mzee Shangwe alimkazia macho. "Familia ya Masanja ni moja ya familia tajiri zaidi huko Da es Salaam. Nimeichunguza muda mrefu. Kaka wa Pamela, Forrest Masanja, ana uwezo pia. Katika miaka hii miwili, kampuni ya familia yetu, Shangwe Corporation ilikuwa na ushirikiano mdogo na familia ya Masanja pia. Dada yako alisema Forrest ni mtu wa kushangaza sana. Tangu achukue kampuni ya familia yao, amekuwa akiiendesha kwa kasi na hata kupanua masoko kuingia Kenya. Sifa ya familia yao pia si mbaya, ukiondoa suala la Pamela na Thomas Njau la miaka mitatu iliyopita… Lakini tayari nilichunguza hilo. Yeye hakuwa na hatia. Wewe na Alvin ndio mlimsababishia matatizo na kumharibia sifa. Kwa njia hii, itakuzuia kumfikiria mwanamke huyo, Sarah.”
“Baba, Mama, semeni maneno machache kwa ajili yangu. Babu anazidi kuchanganyikiwa na uzee.” Rodney aliweza tu kuwatazama wazazi wake bila msaada.
Wendy alisita kwa muda na kumtazama Mzee Shangwe. "Pamela labda hatakuwa tayari kuolewa naye."
“Nafikiri hivyo pia.” Jason aliitikia kwa kichwa.
Hapana, hiyo ndiyo ilikuwa maana yao? Hoja ilikuwa kwamba hatamuoa, Pamela, sawa?! "Mnaweza kufanya chochote mnachopenda. Hata hivyo sitamuoa. Ni afadhali kuwa mtawa kuliko kuoa mwanamke huyo,” Rodney alisema kwa hasira na kuondoka.
Mbaya zaidi ilikuja kujulikana kuwa mbaya zaidi, angekataa hata kurudi nyumbani tena.
“Mtoto huyu…” Wendy alitikisa kichwa huku akitazama Rodney akiondoka.
"Hajui watu wa Nairobi wanazungumza nini juu yake? Haijalishi ingekuwa ni mtu mwingine, lakini ana mpango gani na familia ya Njau?"
“Mama, usiwe na haraka. Kutakuwa na njia." Jessica alimfariji.
•••
Pavilion Intercontinental Hotel.
Katika hoteli ya nyota saba kando ya bahari, huko Mombasa, harusi ya karne ilikuwa inafanyika. Ilikuwa sita kasoro mida ya mchana mchana hivi wakati Lisa na Joel walionekana pamoja wakielekea kwenye hoteli hiyo.
Watu wakaanza kuulizana punde walipowaona wakiingia.
“Siyo Lisa na Joel wale? Kwa nini baba na binti wamekuja?"
"Familia ya Ngosha na familia ya Kimaro ni marafiki wa zamani, kwa hivyo ni kawaida kwamba Joel alialikwa. Lakini haikutarajiwa kwamba Lisa angekuja.”
“ Yeye ni mke wa zamani wa Alvin, hata hivyo.”
“Tsk tsk, mke wa zamani anayehudhuria harusi ya mume wake wa zamani. Hili linavutia.”
Minong'ono ya wageni iliinua anga hadi kiwango cha juu. Alvin, ambaye alikuwa akikutana na wageni kwenye bustani, alisikia minong'ono ya kila mtu na akageuka nyuma kutazama.
Lisa alikuwa akitembea akiwa amevaa mavazi ya kawaida. Kulikuwa na maua mepesi ya kijani yaliyopambwa kwenye gauni lake. Mwangaza wa jua ulipoangaza kwenye mavazi yake, uliangaza rangi ya dhahabu yenye kuvutia. Pia ilikazia umbo lake lililopinda. Alikuwa na mwendo wa kifahari kana kwamba alikuwa Miss Tanzania wa zamani.
Alvin alikuwa ameduwaa kwa muda. Alijua kwamba alikuwa mrembo, lakini hakujua kamwe kwamba angeweza kuonekana mzuri sana wakati anavaa nguo kama hizo.
Chester, bestman wa heshima aliyekuwa kando yake, alisafisha koo lake na kumuuliza, “Kwanini Lisa yuko hapa?”
“Sina uhakika."
Joel alikuwa mkubwa, baada ya yote, hivyo Alvin ilibidi kwenda mbele na kumkaribisha. “Anko Joel—”
“Mm. ” Joel alimtazama bila kujali. "Nipo hapa kwa sababu ya babu na bibi yako."
Lisa alipunga kadi ya mwaliko mkononi mwake. “Nimealikwa. Kusema kweli, sikufikiri kwamba mimi, mke wako wa zamani, ningeweza kupokea mwaliko wako.”
Uso mzuri wa Alvin ukakakamaa. Hakuwa na mawazo ya kumtumia Lisa mwaliko, hivyo ni nani aliyemtumia?
Punde, Lisa na Joel walikwenda upande wa pili wa bustani ile ya kifahari kando ya bahari. Ilikuwa pale ambapo watu wa familia ya Kimaro walisimama. Suzie alikuwa amevaa kama binti wa kifalme. Lea alikuwa
Akitembea na Suzie pamoja naye pembeni yake.
“Aunty Lisa. ” Suzie alimkimbilia Lisa kwa furaha baada ya kumuona.
Lisa alimbeba Suzie kawaida. Akawa hayupo kimawazo alipolitazama lile gauni la flower girl alilovaa Suzie.
Hakutarajia kuwa binti aliyemzaa naye angekuwa msichana wa maua kwa harusi ya Alvin na Sarah. Kulikuwa na kila aina ya mambo ya ujinga ambayo yangetokea maishani.
“Lisa, sijakuona muda mrefu,” Bibi Kimaro alimsalimia kwa utulivu.
"Babu, Bibi." Lisa aliwaitikia kwa tabasamu. Hakuwapenda wala kuchukia wanafamilia wa Kimaro. Aliwachukulia kawaida tu.
Valerie pekee ndiye aliyecheka huku ameziba mdomo alipomuona Lisa. "Lisa, Alvin tayari anaoa. Hujapata mchumba bado? Ah, hata nilifikiria kuhudhuria harusi yako na ya Alvin. Sikuwahi kutarajia kwamba, ingawa wewe na Alvin mlifunga ndoa zamani, hamkuwa na harusi sawa?”
Joel hakuonyesha kufurahishwa. "Wacha kuzungumza juu ya yaliyopita."
“Oh, niangalie. Ni kosa langu kuwa na shobo nyingi.” Valerie aligonga mdomo wake kwa upole. “Ninamhurumia tu Lisa. Ingawa aliweza kuishi katika nyumba ya familia ya Kimaro kwa muda kidogo, hajaweza kuwa bibi mdogo wa familia ya Kimaro mwishowe.
"Funga mdomo wako." Mzee Kimaro alimpiga jicho kali. "Nenda ukaropokee huko ikiwa huna mambo yoyote mazuri ya kusema."
“Babu, ni sawa. Nimekuja leo maana yake ni kwamba tayari nimeachana na yale yaliyopita.” Lisa alitabasamu kwa unyonge. “Nitafikiria kupata mchumba, lakini bado najipa muda. Sina haraka, na kuna wachumba wengi sana karibu nami. Macho yangu yanakuwa na ukungu kwa sababu ya kuchagua mmoja tu atakayenifaa.”
Alipomaliza kusema tu, mara akasikia sauti ya Erick Malugu. “Bi. Jones, Anko Joel.” Erick, ambaye alionekana kustaajabisha, alitembea
Joel alitabasamu alipoeleza, “Tayari nimezungumza na baba wa Erick ili kuwaruhusu watoto wetu wote wawili kuwa na mahusiano zaidi.”
kuelekea kwao. Akawapungia mkono kuwasalimia huku akitabasamu. “Bi. Jones, kama ningejua unakuja, ningekuja kuwachukua wewe na baba yako."
"Hakuna haja ya shida kama hiyo," Lisa alisema kwa upole huku akitabasamu.
“Siyo shida hata kidogo.”
Erick aliguna kwa shauku. "Nyinyi wawili ni..." Mzee Kimaro alikuwa na sura ngumu usoni mwake.
Sura ya: 396
Wanafamilia wa Kimaro walinyamaza papo hapo. Ingawa familia ya Malugu haikuweza kulinganishwa na familia ya Kimaro, bado walikuwa familia ya wasomi. Kwa kuongezea, utambulisho wa Lisa ulikuwa tofauti sasa. Ilikuwa kawaida tu kwamba familia ya Malugu ingemtaka aolewe katika familia yao.
Hata Valerie alibaki kimya, lakini alihisi kuchanganyikiwa. Hakutarajia kuwa Lisa bado angekuwa maarufu hata baada ya kuachwa.
Kwa upande mwingine, ingawa Alvin alikuwa akipiga toast na wageni, aliendelea kutazama kile kinachotokea upande wa Lisa. Erick alipopita, mikono yake kwenye glasi yake ya divai ilikaza bila hiari.
"Alvin, Chester." Ghafla, Rodney akatokea kwa haraka. Bado alikuwa amevaa nguo zake za jana. Alikuwa amelewa pombe, na shati lake lilikuwa limekunjwa.
Chester alimtazama kwa dharau. “Angalia mwonekano wako. Angalau ulipaswa kubadilisha nguo zako kabla ya kuja."
“Sikuwa hata na hamu ya kubadilika. Ninakaribia kufa kutokana na hasira,” Rodney alifoka. “Mimi-”
“Ni wakati wa kujiandaa kwa sherehe. Bibi arusi anaweza kutokea muda wowote kuanzia sasa hivi.” Msimamizi wa sherehe alikuja na kukatiza maneno ya Rodney.
Rodney alionekana kuhuzunika, lakini hakuna aliyemjali. “Sawa.”
Alvin aliitikia kwa kichwa, na macho yake yalikuwa chini. Aliwaambia Chester na Rodney waende kumchukua Sarah.
Sherehe ya harusi ilianza kwa wakati mwendo wa saa sita na nusu mchana. Sarah alivalia vazi maridadi la harusi lililomfanya aonekane kama binti wa kifalme. Alitembea polepole akiburuta shera refu jeupe. Alivaa kishada kichwani, na kilipambwa kwa almasi nyingi. Iliwafanya wanawake waliohudhuria harusi kuwa na wivu.
Aliingia kwenye gazebo nyeupe na kusimama uso kwa uso na Alvin, aliyekuwa amevalia suti nyeupe. Alikuwa na mwonekanoa kipekee uliyomfanya awe na sura nzuri.
Moyo wa Sarah ulianza kwenda kasi. Alikuwa akingoja kwa muda mrefu sana siku hii, na hatimaye ikafika. Akamtazama kwa haraka Lisa aliyekuwa kwenye bustani. 'Ha, mwishowe, Alvin ananioa!' Alijiwazia kwa furaha.
Katika siku zijazo, angekuwa na watoto na Alvin. Kila alichokuwa nacho kingekuwa chake.
“Alvini…” Sarah alimtazama Alvin kwa upendo.
Alvin alikuwa na hisia tofauti. Tayari alikuwa ameamua kumuoa Sarah muda mrefu uliopita. Aliamua tu kufanya harusi kwa sababu alikuwa na deni la Sara. Hata hivyo, kwa kuwa sasa wakati huo ulikuwa umefika, alihisi kana kwamba kuna jiwe kubwa linaloukandamiza moyo wake.
Msimamizi wa sherehe alishika kipaza sauti na kuanza kuuliza, “Mr. Alvin Kimaro, unamchukua Bi. Sarah Langa Njau kama mke wako wa ndoa? Je, unaahidi kuwa mwaminifu kwake pekee, kumlinda, na kumthamini, kwa utajiri au umaskini zaidi, katika ugonjwa na afya?”
“Nina…” Alvin alikunja ngumi. Alipokuwa karibu kusema neno la mwisho, kundi la polisi liliingia ndani.
"Samahani, tuko hapa kwa shughuli za kipolisi." Mkaguzi mmoja alimsogelea Sarah na kusema, “Bi.
Njau, polisi waligundua mwili wa mtu mgeni kando ya mto siku mbili zilizopita. Tunashuku kuwa unahusiana na kifo chake. Tafadhali twende kituo cha polisi pamoja nasi kwa uchunguzi."
Wageni wote walishtuka. Sara alihisi kana kwamba alikuwa akianguka kutoka mbinguni hadi kuzimu. Alisema kwa sura ya kusikitisha, “Sijui unazungumzia nini. Sijui mtu yoyote wa kigeni mimi.”
“Una uhakika humtambui?” Inspekta alimwonyesha picha ya Hisan Gadaffi. “Baada ya uchunguzi wetu, tunaweza kuthibitisha kwamba mwanamume huyu amekuwa akiishi katika nyumba iliyo chini ya jina lako. Si hivyo tu, ulikuwa ukiingia na kutoka katika nyumba hiyo mara kwa mara siku chache zilizopita. Tunashuku kwamba ulishiriki naye uhusiano usiofaa.”
Uso wa Alvin uligeuka kuwa mbaya sana. Ni nini kinachoweza kuwa aibu zaidi kuliko kundi la polisi linalomshutumu bibi arusi wake kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi usiofaa wakati wa sherehe ya harusi yake?
Wageni pia walizusha kelele. Hakuna mtu aliyetarajia kwamba wangeshuhudia tukio hilo la kushangaza wakati wa kuhudhuria sherehe ya harusi ya Bwana Kimaro.
“Ni ukweli?”
“Je, polisi wanasema Sarah alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume huyo wa kigeni?”
"Hicho ndicho hasa alichomaanisha."
“Hilo haliwezekani, sivyo? Nilisikia wamependana kwa zaidi ya miaka kumi. Mbali na hilo, kwa mwonekano wa nguvu wa Alvin, je Sarah anahitaji hata kutafuta mwanaume mwingine?”
"Haha, labda hawezi kumridhisha."
Majadiliano ya wageni yalifika masikioni mwa Alvin. Alionya kwa uso wa wasiwasi, “Sarah ni mke wangu. Tafadhali zingatieni maneno yenu mnapozungumza." Alitoa sura ya kutisha ambayo ilisababisha hata mkaguzi mzoefu wa polisi kutetemeka.
Hata hivyo, muda mfupi baadaye, Inspekta alijipa ujasiri na kusema tena, “Ni kweli kwamba marehemu alishiriki uhusiano wa kimapenzi na Bi Njau. Tunafanya hivi kwa ajili yako pia, Bwana Kimaro. Unataka kuoa katika mazingira ya kutiliwa shaka, Bwana Kimaro? Au una uhakika kwamba unamuelewa kabisa yule mwanamke aliye karibu nawe?”
"Inatosha. Ingawa wewe ni polisi, kuna wageni wengi hapa leo. Inabidi uwajibike kwa maneno yako. Nilikutana na mtu huyo wa kigeni unayemzungumzia hapo awali kwa sababu alikodisha nyumba yangu. Nilikuwa tu nikiwasiliana naye kuhusu nyumba, lakini wewe unageuza ionekane kuwa tulikuwa na uhusiano usiofaa. Hii ni kashfa kubwa mno. ” Sarah alishikwa na kiwewe cha hofu.
"Hiyo ni sawa. Sarah si mtu wa aina hiyo.” Rodney hakuweza kujizuia tena akajitokeza kuwavaa polisi. “Unafikiri unaweza kumharibia mwanamke sifa kwa sababu tu wewe ni polisi? Hamzingatii hata kuwa hii ni siku ya harusi yake?”
Inspekta alikunja uso na kusema kwa unyenyekevu, “Jeshi la polisi halikurupuki tu, linafanya kazi kwa weledi. Mpaka tunakuja hapa, ina maana kwamba tuna ushahidi mwingi mikononi mwetu. Una uhakika unataka niwaorodheshe mmoja baada ya mwingine hadharani kabla hujaniruhusu nimtoe mtu huyu?”
Sarah alianza kuingiwa na hofu baada ya kusikia hivyo. Aliambiwa kazi ilikuwa imefanywa kikamilifu, na mtu huyo hata alisema mwili wa Hisan ulizikwa kwenye milima isiyo na watu. Kwanini ilionekana kando ya mto ambapo iligunduliwa na polisi?
Polisi walikuja ghafla na kumkamata. Hakujua ni kiasi gani polisi walijua kutokana na uchunguzi wao katika siku hizi mbili.
Alvin alimtazama Sarah kimya kimya. Bado hakuamini kuwa Sarah angekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine. Hata hivyo, macho ya polisi yaliyojaa uhakika yalimfanya anyamaze wakati huo.
"Alvin, waache polisi wampeleke kwenye kituo cha polisi kwa uchunguzi," Mzee Kimaro alisema kwa sauti kubwa, "Harusi ya leo imeahirishwa kwa muda."
Mzee Kimaro aliposema hivyo, kila mtu pale ukumbini alishtuka. Hakuna aliyetarajia kwamba harusi hiyo ya karne ingefutwa ghafla. Uso mzuri wa Sarah chini ya vipodozi maridadi ulipauka papo hapo. Alikuwa amesubiri kwa muda mrefu sana hadi siku hiyo ifike. Alikuwa karibu kuwa Bi Mdogo wa familia ya Kimaro. Alikuwa akiingoja siku hii kwa muda mrefu sana.
"Alvinic." Aliushika mkono wa Alvin kwa nguvu.
Ikiwa arusi ingeghairiwa, angeukosa ubibi-arusi na kila mtu aliyemwonea wivu hapo awali angemwona kuwa kicheko cha taifa zima. Zaidi ya hayo, sifa yake ingeharibiwa.
Alimtazama inspekta kwa kusihi. “Unaweza kuturuhusu tumalizie harusi kabla sijaenda na wewe kituo cha polisi? Itachukua muda kidogo tu. Tafadhali, hii ndiyo siku muhimu zaidi maishani mwangu.”
Macho ya mkaguzi hayakuyumba. Kama asingegundua baadhi ya mambo, angevumilia na asingesitisha harusi yake....ITAENDELEA...
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
