JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................375-376

Sura ya: 375

Alipozinduka, ni kwa sababu kuna mtu alikuwa akivuta kope zake. Alimsikia mtoto akicheka kitoto pia. Akafumbua macho. Alipigwa na butwaa kwa muda alipoona Suzie amekaa na makorokoro mengi kitandani.

“Anko Alvin, hii ni ya nani?” Suzie ghafla akamuonyesha pete.

Alvin alishikwa na butwaa. Alipotazama vizuri aliona ni pete ya almasi ya waridi ya bei ghali, yenye uzito wa gramu 13.14. Alifikiri ilionekana kuwa ya kawaida, lakini hakuweza kukumbuka. "Umeipata wapi hii?"

“Kuna kisanduku kidogo kabatini. Kuna namba nyingi juu yake. Nilicheza nayo tu na ikafunguka.”

Suzie alikuwa anadanganya. Kwa kweli, aliweka namba za siku ya kuzaliwa ya mama yake. Lakini, hakujua kwamba ingefungua. Walipokuwa wakiishi Marekani, mama yao aliwaelekeza kufungua kila kitu kilichohitaji namba ya siri kwa kutumia namba za tarehe yake ya kuzaliwa. Lucas na Suzy walikuwa wamekariri namba hizo, na Suzie alifanya tu kama kujaribu kwenye kisanduku hicho. Hiyo ilithibitisha kwamba Mama yake aliwahi kuishi katika chumba hicho hapo awali.

Alvin alikosa la kusema. Alijua kuwa Suzie alikuwa anazungumza juu ya sanduku la usalama. Lisa alikuwa amekaa katika chumba hicho miaka mitatu iliyopita. Yeye ndiye aliyeweka namba za siri pia. Baada ya Lisa kuondoka, vitu vyake vingi vilivyokuwa ndani ya chumba hicho viliondolewa, isipokuwa sanduku la usalama. Hakuna mtu aliyelifungua kwa sababu hawakujua namba za siri.

Kabla ya hili, Alvin hakujali hata kidogo na hakuwahi hata kufikiria kuifungua. Hakutarajia kwamba yule mtoto mdogo angefungua kwa bahati mbaya.

“Ni…pete, tu” Alvin alisema kwa sauti ya hovyo.

“Ni yako, Anko Alvin?" Suzie aliuliza kwa udadisi.

“Siyo yangu Lakini nadhani najua ni wa nani. Nitamrudishia.” Pamoja na kumbukumbu zake dhaifu, Alvin alikumbuka aliwahi kumnunulia pete hiyo Lisa kwenye duka la ‘The Only Love In Life’ kipindi kile mara baada mapenzi yake ya siri na Lisa kubumburuka.

“Sawa.” Suzie aliweka pete kwenye kasha lake na kwenda kuosha uso wake.

Wakati wa kifungua kinywa, Jack alikuwa wa kwanza kufika kwenye meza ya chakula akiwa na Suzie. Alikunja sura na kusema kwa sauti ya chini, “Suzie, mama yako akigundua kuwa unamganda sana Alvin, atakasirika sana, unajua hilo?” Jack alikuwa karibu kulia, lakini machozi hayakutoka.

"Baba, kwani utamwambia?"

"Kwa hiyo bado unakumbuka kuwa kwa sasa mimi ndiye baba yako? Akili zako zote zimeishia kwa Alvin baada ya kurudi jana. Uliniacha baada ya kulala katikati ya usiku. Mtoto wewe, usiharibu mipango.”

“Anko Jack, umenielewa vibaya. Natumia sura yangu tu kama mtego.” Suzie alinong’ona. “Ninamsaidia Mama kumfundisha somo mama yangu wa kambo mkatili.”

Kichwa cha Jack kilikuwa karibu kulipuka. “We mtoto hebu nenda ukavae. Mama yako aliniambia nikupeleke chekechea moja na Lucas.”

“Hiyo ni nzuri. Nina kadi ya pesa ambayo nataka kumpa Lucas,” Suzie alisema kwa sauti ya dhati. Jack alihisi kuwa ilikuwa kazi sana kudili na mtoto.

Muda mfupi baadaye, watu wengine wa familia ya Kimaro walikuja kupata kifungua kinywa pia. Alvin alitoka chumbani kwake akiwa na kisanduku cha kung’aa. Queenie alipoona kisanduku hicho kizuri hakuweza kupinga kukifungua ili kutazama. Alishangaa, "Hii si pete ya almasi?"

Alvin aliinua kichwa chake na kumtazama huku akikunja uso. "Unashangaa nini kuhusu pete?"

"Kaka mkubwa, unapanga kumpa Sarah?" Queenie aliuliza kwa sauti ya uchungu. "Ni pete ya gharama sana. Nimeipenda kweli. Niliiona kwenye duka la ‘The Only Love In Life’ nikatamani sana ningevaa siku moja.”

Alvin alishika mdomo. "Ikiwa uliipenda sana, kwa nini hukununua yako mwenyewe?"

“Ni mwanamke gani angejinunulia? Ni mwanamume ndiye anayemnunulia mwanamke.” Queenie alipiga kelele.

Baada ya kifungua kinywa, Alvin aliingia kwenye gari yake aina ya Sedan. Baada ya gari kuondoka Sherman Mountain, alimwagiza dereva, "Nipeleke Mawenzi Investments."
•••
9:30 asubuhi, Lisa alikuwa anaingia ofisini kwake baada ya kumpeleka Lucas shule ya chekechea. Alipokaribia kupanda juu kutoka sehemu ya maegesho, aliona sedan nyeusi ikiwa imeegeshwa mbele ya lango la kuingilia kwenye lifti. Umbo refu la Alvin lilikuwa limeegemea Sedan.

“Mbona uko hapa tena?” Lisa alimfuata kwa hatua ndefu. "Bwana Kimaro, huwezi kuegesha gari hapa."

Alvin akafungua kifungo kimoja cha shati lake sehemu ya kifua chake. Alichukua kisanduku kidogo cha kung’aa kutoka kwenye gari lake. Akakifungua na kutoa pete ya almasi iliyokuwa ndani yake. “Hii… ni yako.”

Lisa alipigwa na butwaa. Pete hiyo ilikuwa imenunuliwa naye kwa ajili yake hapo awali kwa gharama kubwa. Ilikuwa pia ushahidi wa upendo wao. Alikuwa akiitunza kwa uangalifu hadi miaka minne iliyopita alipokata tamaa. Hakukumbuka hata alipokuwa ameitelekezea. Ilikuwa ni zawadi ya pili ya gharama ambayo Alvin alimnunulia ukiacha ile ya Mkufu wa Malkia. Kwa bahati mbaya vyote havikuwa na maana kwake tena.

"Ilikuwa yangu, lakini sasa sio yangu tena." Lisa alitabasamu, lakini macho yake yalikuwa chini. Alificha hisia hizo ngumu machoni pake.

"Unamaanisha nini?" Alvin alikunja uso.

"Ulinipa kama zawadi hapo awali, lakini labda haukumbuki," Lisa alisema kwa utulivu.

Macho ya Alvin yalisinyaa. "Lazima ni wewe ndiye ulinilazimisha nikununulie."

Lisa alicheka. “Fikiria vyovyote unavyotaka, lakini tambua kwamba tumeachana sasa. Unaweza kumpa Sarah.” Alipita mbele yake baada ya kusema.

Alvin alishika mkono wake na kumzuia. Akaweka kisanduku cha pete mikononi mwake. “Sarah hatataka kitu ambacho umevaa hapo awali. Chukua."

Lisa alitazama chini kwenye sanduku. Alihisi hali ya kujidharau. Kumbe alikuwa akimpa tu kwa sababu Sarah hakutaka? “Sawa.” Alichukua kisanduku na kuondoka.

Baada ya kuingia ndani ya ukumbi ambapo lifti zilikuwepo, kulikuwa na pipa la taka kwenye kona. Lisa akakitupa kisanduku cha pete ndani yake.

Macho ya Alvin yakachomoka. Alisema kwa ukali, “Unatupa kitu cha bei ghali namna hiyo?”

"Kwa kuwa ulitaka niichukue, nina haki ya kuamua wapi pa kuipeleka."
Lisa alibonyeza kitufe cha lifti ya kibinafsi ya VIP. Aliingia kwenye lifti, akafunga milango na kuondoka.

Alvin alitembea hadi kwenye pipa la takataka. Alitoa kile kisanduku cha pete. Kuangalia pete ya almasi mle ndani, alianza kuwaza kwa umakini kwa mara ya kwanza. Alikuwa amepoteza kumbukumbu nyingi sana, lakini zilikuwa kumbukumbu gani? Alifikiri alikuwa akimchukia Lisa muda wote. Hata hivyo, kwa nini ampe pete ya almasi ikiwa anamchukia? Je, angekubali kwenda Coco Beach na Lisa, sawa na alivyosema Chester, ikiwa alimchukia sana?

Sura ya: 376

Ilikuwa karibu saa sita mchana aliporejea KIM International. Sarah alimpelekea chakula cha mchana.

“Alvinic sijakuona tangu jana. Nimeku’miss sana. Nilikuandalia chakula cha mchana maalum kwa ajili yako.” Sarah alifungua vyombo vya chakula.

“Sawa.” Alvin alichukua uma. Alipotaka kula, mlango ukasukumwa. Kichwa kidogo cha mtoto kilitokea nyuma ya mlango. Alvin alipotazama, Suzie alikimbia mara moja huku akirukaruka.

“Nilikukumbuka sana.” Alijitupa kwenye kumbatio la Alvin.

Sarah alipoteza utulivu alipomuona Suzie. "Huyu mtoto... hawezi kuwa binti yako, sawa ..."

“Hapana, huyu ni binti wa Jack. ” Alvin alimbeba Suzie kwenye mapaja yake. Aligundua kuwa kamwe hawezi kuwa mkali mbele ya Suzie. “Si ulikuwa kwa bibi yako? Kwa nini umekuja hapa?”

"Nilikuja kwenye kampuni na Daddy, lakini yeye ana shughuli nyingi za kufanya. Nimechoka kukaa peke yangu, kwa hiyo nilikuja kukutafuta wewe, Anko Alvin.” Suzie aligeuza macho yake kwa Sarah. “Huyu Aunty pia ni mfanyakazi wa kampuni?”

Moyo wa Sarah uliopata nafuu ulipata mshtuko mwingine. Ni kwa jinsi gani hasa alionekana kama mfanyakazi?

“Hapana, yeye ni mchumba wangu,” Alvin alieleza.

“Habari, Aunty,” Suzie alimsalimia Sarah kwa uchangamfu.

“Hujambo.” Sarah alitabasamu kwa unyonge. "Alvinic, sikuwahi kujua unapenda watoto. Inaonekana tunatakiwa kuwa na wa kwetu haraka.

"Ndio," Alvin alijibu kwa utulivu, "Labda ni kwa sababu mtoto huyu anafanana sana na mimi."

"Ni sawa. Mtoto wetu wa baadaye atafanana na wewe zaidi.” Sarah alitabasamu huku mikono yake ikiwa imeziba mdomo wake.

Macho ya Suzie yalikuwa chini. Alionyesha sura ya kukata tamaa na kuushika mkono wa Alvin kwa nguvu. "Anko Alvin, si utanipenda tena wakati utakuwa na mtoto wako mwenyewe?" Macho yake meusi yalijawa na hofu na kukata tamaa. Uso wake ulikuwa umepauka, na paji la uso bado lilikuwa limefungwa bandeji.

Alvin alihisi kubanwa moyoni. Alimbembeleza kwa sauti ya chini, akisema, “Usijali mtoto mzuri. Hata nikiwa na mtoto siku za usoni, bado nitakupenda wewe Suzie.”

"Asante, Anko Alvin." Suzie akampa kiss shavuni.

Uso wa Sarah ukawa mgumu. Ingawa Suzie alikuwa na umri wa zaidi ya miaka mitatu tu, alimchukia haswaa msichana huyo mdogo. Zaidi ya hayo, Alvin alimfurahia sana Suzie na kumtendea kwa upole sana.

"Alvinic, leo sisi-"

“Anko, hiki ndicho chakula chako?” Suzie aliuliza ghafla na kumkatisha Sara.

“Ndiyo.” Alvin aliona matarajio katika macho ya binti mdogo. "Una njaa? Unataka kula?”

“Sawa. ” Suzie alichukua kijiko na kuanza kuchota chakula. Alikunja uso baada ya kutafuna kidogo. "Wow, kina ladha mbaya sana. Sio kitamu kama cha kupikwa kwa mama yangu."

Uso wa Sarah ulikaribia kubadilika kutokana na hasira. Suzie alionja tu chakula alichotengeneza na kusema kwamba kilikuwa na ladha mbaya.

Alvin hakugundua kwani alijisikia sawa na Suzie. Alifikiri kwamba chakula hicho kilikuwa na ladha mbaya pia. "Mama yako alikuwa akipika chakula kitamu sana?"

“Ndiyo, mama yangu alitengeneza chakula kitamu sana, nyama choma ya nguruwe, kababu, kachori sambusa...”

Kwa namna fulani, Alvin ghafla alikumbuka vyakula ambavyo Lisa alikuwa amemtengenezea. Ingawa ulikuwa umepita mudi, bado aliweza kukumbuka ladha yake. Alikuwa na uhakika kwamba Suzie angeipenda pia.

"Ah, ghafla nimekumbuka mapisgi ya mama yangu. ” Macho ya Suzie yakawa mekundu ghafla, machozi yakaanza kumlenga lenga.

Alvin alihisi maumivu moyoni mwake. Alikumbuka Lea alimwambia jana yake kuwa mama wa msichana huyu mdogo alikuwa amefariki kutokana na saratani. “Usilie. Nitamuomba mtu akutengenezee nyama choma ya nguruwe ukitaka kula.”

“Lakini ninamkumbuka mama yangu. Nimemkumbuka sana.” Suzie alizidi kulia.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Alvin kukumbana na mtoto aliyekuwa akilia. Alikuwa katika hofu na katika hasara. Aliweza tu kumtazama Sarah ili kutafuta msaada.

Lakini, Sarah hakuwa na uzoefu na watoto pia. Si hivyo tu, bali pia alimchukia Suzie kutoka ndani ya moyo wake. Sarah alisita kwa muda na kuongea kwa kigugumizi, “Kwanini msimtafute mama yake? Watoto daima wanataka kuwa karibu na mama zao.”

Sarah alifikiri kwamba Jack alikuwa na binti wa nje na kwamba utambulisho wa mama wa mtoto haukuwa wa heshima kwa familia ya Kimaro. Kwa hivyo, familia ya Kimaro ilimrudisha mtoto, na kumzuia mama yake. Hata hivyo, Suzie alilia zaidi aliposikia maneno ya Sarah.

Alvin alimtazama Sarah kwa hasira baada ya kusikia maneno yake. Akasema, “Mama yake tayari ameshafariki! ”
Moyo wa Sarah ukapandwa hasira kutokana na kupigiwa kelele. “Ningejuaje…”

Hata hivyo, Alvin aliweza kusikia tu kilio cha Suzie wakati huo. Hakuwa na wakati wa kumjali Sara. "Unapaswa kurudi kwanza." Akambeba Suzie na kuelekea kwenye migahawa ya kampuni hiyo.

Sarah ambaye alibaki nyuma alikanyaga miguu kwa hasira. Huyo mtoto alitoka wapi? Alikuwa na chuki naye sana.

Wapishi maarufu wa migahawa iliyozunguka kampuniya KIM International waliagizwa kupika vyakula alivyopenda Suzie. Lakini, Suzie alionja mara chache tu kabla ya kulia tena. “Sipendi. Sio nzuri kama alichopika Mama. Chakula cha mama kina ladha safi na harufu nzuri,. Kwa kweli, tayari najua… kwamba siwezi tena kupata chakula kama cha Mama tena.”

Alipokuwa akiongea, vijito viwili vya machozi vilimtoka, lakini, hakutoa sauti ya kilio. Hakujua kuwa wakati analia vile, ilizidisha uchungu wa moyo wa Alvin. Mtoto huyu mdogo alikuwa mjanja sana.

Alvin pia alijua aina hiyo ya maumivu. Alipokuwa mdogo, ingawa alikuwa na mama, ilikuwa ni kana kwamba hakuwa naye.

“Suzie, twende tkwa baba yako, sawa?” Kwa kweli Alvin hakuwa na chaguo.

“Sawa, mwambie baba anipeleke kwa Aunty Lisa. Kupika kwa Aunty Lisa pia ni sawa na mama yangu. Chakula chake ni kitamu” Suzie akafuta machozi.

“Aunty Lisa?” Alvin akanyamaza. "Unamaanisha Lisa Jones?"

“Sijui, namuita tu Aunty Lisa. Yeye ni mzuri sana. Ni mrembo zaidi ambaye sijawahi kumuona, na ananitendea vizuri sana. Je, atakuwa mama yangu mpya?” Suzie ghafla akainua macho yake yasiyo na hatia na kuuliza.
Alvin akapagawa ghafla. Jack Kimaro amelaaniwa! Hata alikuwa amempeleka binti yake kukutana na Lisa? Alitaka kweli kumfanya awe mama yake? Mdomo wa Alvin ulitetemeka kwa nguvu. Lisa kuwa mke wa Jack na mama wa Suzie mpya? Kufikiria tu kulisababisha hasira kumpanda kutoka ndani kabisa ya moyo wake.

"Haiwezekani kuwa mama yako." Alvin alijikuta akimpinga yule mtoto.

“Kwanini? Nataka kila wakati kula chakula cha Aunty Lisa,” Suzie alisema huku akiinamisha kichwa.

Alvin alimtazama kwa muda na kumnyanyua. “Nitakupeleka kwake na kumwambia akupikie. ”

“Sawa! ” Suzie nusura aruke kwa furaha.....ITAENDELEA....

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.