JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................355-356

Sura ya: 355

Alvin na Sarah walipoingia, mara wakawaona Jack na Lisa wakiwa katikati ya ukumbi wa ngoma. Walikuwa wakicheza pamoja kama wanandoa waliokuwa na ‘chemistry’ nyingi. Mmoja alikuwa mrembo kama binti wa kifalme, wakati mwingine alikuwa amevaa suti nyeupe kama mtoto wa mfalme.
Chini ya mwanga, walizungumza na kucheka. Mara kwa mara, Lisa alikuwa akisema jambo ambalo lililomfanya Jack acheke kwa sauti. Pia alikuwa na tabasamu la kupendeza na tulivu usoni mwake. Tukio lile liliuumiza sana moyo wa Alvin. Wakati huo, alikuwa na hamu ya kukimbilia na kuwatenganisha wote wawili.

Kile Alvin alichohisi kilimfanya amkaze kwa nguvu mkono Sarah. Sarah akashusha pumzi na kugugumia kwa sauti ya chini. "Alvinic, unaniumiza ..."

“Samahani.” Alvin aliachia mshiko wake kwa maneno ya kuomba msamaha, lakini macho yake hayakutoka katikati ya sakafu ya dansi.
Sarah alikunja ngumi kwa hasira.

Harusi yake na Alvin ilipaswa kuzungumziwa zaidi wakati huu, lakini Lisa alionekana kutawala kila mahali na kuiba umaarufu wake. Si hivyo tu, watu wengi walikuwa wakimlinganisha na Lisa kwenye mitandao. Ingawa alikuwa ameitangaza harusi yake hadi kwenye mabngo ya barabarani, bado alishindwa kabisa kupambana na Lisa.

Hatimaye alipata kuhudhuria hafla hiyo na Alvin, lakini Lisa alionekana kama mzimu unaowasumbua. Kilichomfanya azidi kuchanganyikiwa ni kuona wivu machoni mwa Alvin. Ilikuwa ni aina ya wivu ambayo mwanaume angekuwa nayo kwa mwanaume mwingine.

“Alvinic, Aunty Lea yuko pale. Twende tukasalimie,” Sarah alisema kwa sauti nyororo ili kumpotezea mawazo ya Lisa.

“Sawa.” Walikuwa familia, baada ya yote, kwa hiyo walipaswa kutendeana vizuri hadharani.

Wote wawili walitembea kuelekea kwa Lea. Lea alikuwa akibadilishana maneno na rafiki wa zamani. Rafiki yake wa zamani alimtania, “Binti-mkwe wako na mwana wako wako hapa.”

“Habari yako, Aunty Lea,” Sarah aliwasalimia wale wanawake wawili.
"Ah, ana tabia nzuri sana." Rafiki wa zamani wa Lea alipoona kwamba familia ya Lea imeingia, alipata kisingizio na akaondoka kwenda kuzungumza na watu wengine.

Lea alimpa Sarah mtazamo wa chuki. Alimchukia sana Sarah, hasa pale kila Mzee Kimaro na Bibi Kimaro walipotaja kuharibika kwa mimba ya Lisa enzi hizo alipokuwa amebeba mapacha. Wanandoa hao wazee wangeizungumzia kila alipoenda kuwasalimia katika miaka hii michache. Kama si Sarah, Lisa asingepoteza ujauzito wake na angekuwa ni Bi. Kimaro zamani sana.

Ingawa Lea hakumpenda sana Lisa hapo awali, alifikiri kwamba Sarah alikuwa mkatili sana. Sarah aliweza hata kujihusisha na mwanaume ambaye alikuwa ameoa na alikuwa akitarajia kupata watoto. Mwishowe, alisababisha mke halali apoteze mimba. Ilikuwa wazi kwamba Sara hakuwa na hisia zozote za maadili.

Sarah alionekana kuwa na huzuni baada ya kuona Lea anampuuza.
Alvin aliona ni vigumu sana kuvumilia na akasema, “Mama, salamu ya Sarah.”

“Najua. Mimi si kiziwi,” Lea alijibu bila kujali.

Sarah alilazimisha tabasamu na kusema, “Aunty Lea, nitakuletea chakula.” Hakutaka kujaribu kupata kibali cha Lea ili tu kukwepa asikutane na karipio kali.

Alipoona Sarah anaondoka kwa huzuni, Alvin alikasirika. “Inaonekana sikupaswa kuja kukusalimia. Na kwanini hukumtupia jicho kali kama hilo Jack na kumwacha acheze na Lisa? Shemeji wa zamani na shemeji yake, ni aibu sana.”

Hapo awali Lea alifikiri kwamba haikuwa sawa pia, lakini kwa silika alienda kinyume na maneno ya Alvin aliposikia sauti yake. “Wewe na Lisa tayari mmeachana. Ni muziki tu wanacheza na sio mapenzi. Watu wengine hata hawasemi chochote. Ni wewe tu unayenyoosha vidole hapa. Unajiingiza sana katika mambo ya wengine.”
“Hata ikiwa watu wengine wanasema jambo fulani, hawatalisema mbele yako,” Alvin alijibu kwa ukali.

“Umekosea. Wanafikiria tu njia za kufahamiana na Lisa sasa. Yeye ndiye mrithi wa Ngosha Corporation na mkurugenzi mkuu wa muundo wa Kilimani Group. Kwa utambulisho huu, hakuna mtu atakayetaka kupitisha nafasi hii ili kumjua. Kutakuwa na manufaa na hakuna hasara iwapo Jack atajenga uhusiano mzuri na Lisa.” Lea alisema kwa hisia ngumu, “Alvin, lazima uelewe kwamba Lisa si Lisa tena wa zamani. Ana uwezo wa kuongeza thamani ya soko la Mawenzi Investments kwa urahisi na kuifanya iingie kwenye orodha 100 bora za Kenya.

"Mbali na hilo, yeye ndiye binti pekee wa Joel Ngosha na mwanamke wa kweli wa familia ya Ngosha. Ingawa alikuwa ameolewa hapo awali, bado kuna wanaume wengi bora kutoka kwa familia tajiri ambao wanataka kumuoa na kufahamiana naye. Ikiwa huamini, jionee mwenyewe.”

Alvin alitazama tena ulingo wa muziki. Lisa alikuwa tayari amemaliza kucheza wimbo na Jack. Baada ya hapo, alialikwa kwa nyimbo nyingine na Erick Malugu mwenye uwezo na mwonekano mzuri, aliyekuwa mkurugenzi wa S.E Group. Alvin alikunja ngumi bila fahamu.

Lea akahema. "Wakati mwingine, huwezi kuwadharau wengine. Wewe unajiona ndiyo mwenye kujua kila kitu? Uvumi niliousikia zaidi leo haukuwa juu ya watu kumcheka Jack, lakini wanazungumza juu ya jinsi ulivyoachana na Lisa na kumuoa na Sarah! Atakuletea kitu gani kizuri? Kila mtu katika jamii ya juu anamuepuka Thomas Njau. Ikiwa sio wewe kuisaidia New Era Advertisings, hakuna mtu ambaye angekuwa tayari kushirikiana nao.”

“Imetosha, usiseme tena.” Alvin tayari alihisi kuudhika, na alizidi kukosa raha kusikiliza maneno ya Lea. “Nilipona kutokana na ugonjwa wangu kutokana na matibabu ya Sarah. Kama si kutiwa moyo na Sarah wakati huo katika hospitali ya magonjwa ya akili, ningekuwa tayari nimekufa.”

“Lisa aliwahi kukutia moyo pia. Ungeniua wakati ule isingekuwa yeye,” Lea alifoka.
Alvin alipigwa na butwaa, akahisi uvimbe kooni. "Je! kitu kama hicho kilitokea hapo awali?"

Lea alikosa la kusema. “Hivi ndivyo Sarah alivyoutibu ugonjwa wako? Umesahau kila kitu kizuri kuhusu Lisa."

Alvin alikuwa ameduwaa kutokana na maneno yake. Hata hivyo, alipojaribu kutafakari kwa kina, ghafla kichwa kilianza kumuuma. Aliegemeza kichwa chake kwenye mikono yake.

Alvin alipoona kwamba Mason na Jerome walikuwa katika mazungumzo ya kina si mbali naye, alisema kwa upole, “Mtazame Mason. Alisema hakuwa na hatia, lakini bado ana uhusiano wa karibu na familia ya Campos. Bado unamwamini?”

Lea akatazama juu, na sura yake ikageuka kuwa mbaya mara moja.
Aligeuka na kuelekea kwa Mason. "Mason, njoo hapa kwa sekunde."

Lakini, alingoja kwa dakika tatu kamili kabla ya Mason kumjia na tabasamu usoni mwake. “Lea, kuna nini?”

Lea akamtazama. Alihisi kwamba alikuwa akizidi kumsoma vizuri. "Mason, si nilikuambia toka mwanzo kuweka umbali kati yako na familia ya Campos? Hasa Jerome—”

“Lea, jina langu la mwisho ni Campos. Pia ni familia ya wazazi wangu. Siwezi… kutowasiliana na familia ya Campos kwa sababu tu ya mpasuko kati ya familia ya Campos na familia ya Kimaro.” Mason alinyoosha mikono yake. "Mbali na hilo, maendeleo ya familia ya Campos miaka hii hayajazuia familia ya Kimaro kwa njia yoyote ile. Huoni kwamba familia hizo mbili zinaendelea kukua pamoja katika miaka ya hivi karibuni?”

Baada ya mshangao wa muda, Lea alisema kwa hasira, “Haijaizuiaje familia ya Kimaro? Baadhi ya kampuni tanzu za KIM International zilinyonywa faida mara kwa mara na kampuni ya Campos. Si hivyo tu, kama isingekuwa msaada wa KIM International wakati huo, familia ya Campos—”

”Kwamba Familia ya Campos ingekuwa kama ilivyo leo? Nilijua ungesema hivyo tena,” Mason alimkatisha. "Familia ya Campos ipo kama ilivyo leo kupitia umoja wa wafanyikazi wote katika kampuni ya Campos. Isitoshe, kwani hatuendelei vizuri hata bila msaada wa KIM International miaka hii mitatu?”

"Kama nisingekupa makumi ya mabilioni hapo awali, unafikiri siku hii ingefika kwa Campos Corporation-"

“Sitaki kugombana na wewe, Lea.” Mason alimkatisha. “Siku zote ni sisi, familia ya Campos, ambao tunashutumiwa kwa kupanga njama na kula njama kila tunapopambana kutoka kwenye dhiki. Ni kana kwamba familia ya Campos inapaswa kuwa na shukrani kwa familia ya Kimaro milele,” Mason alisema kwa kuudhika. Akageuka na kuondoka.

Lea alihisi ubaridi moyoni mwake. Mason hakuwa hivyo hapo zamani. Hata hivyo, alikuwa akizidi kukosa subira naye kadiri muda ulivyopita.

Sura ya: 356

Baada ya Mason kuondoka, alienda moja kwa moja kwenye bustani iliyokuwa nje. Nyuma ya kitalu cha maua gizani, mwanamke alionekana na kushika mikono yake shingoni mwake. "Kwanini ulitoka peke yako na kumwacha yule mwanamke mzee, Lea?"

“Kwa sababu nilikukumbuka. Hakika Lea ni mzee ukilinganisha na wewe." Mason alizunguka kiuno cha mwanamke huyo. Walianza kubusuana na kubadilishana joto.
“Mpenzi, hapa tutakutwa, ninapafahamu mahali ambapo pamejificha zaidi. Twende huko.” mwanamke alisema kwa utamu.

"Sweety babe, twende huko sasa.” Mason alitembea kuelekea nyuma huku akiwa amemkumbatia yule mwanamke. Walipeana peksi kadhaa huku wakitembea.

Hata hivyo, hawakutambua kwamba Lisa alikuwa ametoka nyuma ya mti wa kijani kibichi ili kuongea na wanaye kwa njia ya video. Aliwafumania wakati wanaondoka. Simu ambayo aliishika ilikuwa ikirekodi video. Alipotaka tu kuwafuata, mkono ukatoka nyuma na kumpokonya simu yake. Aligeuka nyuma kutazama. Alimuona Alvin akiwa ameshika simu yake na kuitazama ile video. Mara moja naye akaishiwa pozi.

"Huoni aibu kama mwanamke kwa kurekodi mambo haya?" Alvin alivunga. Baada ya muda, alimtazama Lisa kwa sura isiyo na furaha.

Lisa hakuwa na la kusema. Alifikiri kwamba Alvin hakuwa na furaha kwa sababu aliona tu video ya baba yake wa kambo akiwa na uhusiano wa kimapenzi na kibinti kidogo, lakini hakutarajia angezungumza naye.

“Kwanini nione aibu? Wewe ndo wa kuona aibu.” Lisa alitabasamu huku akisema. “Angalia jinsi baba yako wa kambo alivyo wa ajabu. Ana zaidi ya miaka 50 lakini bado anaweza kujihusisha kimapenzi na mwanamke huyo mdogo sawa na binti yake.”

"Futa video hiyo kutoka kwenye simu yako." Alvin alihisi kuudhika ajabu.

"Unafikiri mimi ni kompyuta ambapo unaweza kufuta chochote upendavyo?" Lisa akairudisha simu yake. Aligeuka, akitaka kuondoka.

Alvin alimshika huku macho yake yakionekana kuwa makali. "Nitumie video hiyo."

Lisa alimnyooshea mkono. Chini ya mwanga wa mwezi, mikono yake midogo midogo ilionekana mizuri sana. Alivaa bangili ya almasi mkononi mwake. Ilikuwa rahisi, lakini ngozi yake nzuri ilifanya ionekane ya kifahari.

Moyo wa Alvin ulirukaruka. "Unataka nini?"

"Nilipe kwa uhamisho wa hakimiliki." Lisa alipepesa macho yake mazuri kana kwamba ni jambo la kawaida. "Video ya Mason itakuwa na thamani kubwa. Ni mkwe wa familia ya Kimaro na mtoto wa kiume mkubwa wa familia ya Campos. Taarifa hizi lazima ziwe na thamani ya angalau milioni 80."

Alvin alimpiga jicho kali. “Milioni 80? Kwanini usiibe benki tu?”

“Alvin Kimaro, usinifikirie kuwa mimi ni mtu asiye na uzoefu na asiyeelewa soko. Paparazi yeyote anaweza kupata makumi ya mamilioni ya shilingi kwa urahisi kwa kashfa ya mtu Mashuhuri. Ikiwa hauko tayari kulipa, ninaweza tu kuuza video kwa vyombo vya habari. Lazima kuna watu watapigania kulipia, haswa familia ya Campos. Hata wataizika kwa mabilioni ya shilingi, nadhani.” Lisa aligeuka na kuondoka kwa utulivu.

Alvin alihisi anaumwa na tumbo kutokana na kumkasirikia Lisa. Alitakiwa kuhamisha video hiyo kwenye simu yake wakati alikuwa amempokonya simu mapema. “Sawa, nitalipia. Nihamishie video hiyo.”

“Nipe pesa kwanza ndo nikuhamishie video. Wakati wa kufanya biashara, mimi huwa mwaminifu kwa wateja wakubwa na wadogo.” Lisa aliinua nyusi zake.

Mdomo wa Alvin ulitetemeka. Akatoa simu yake na kumhamishia pesa mara moja. Macho ya Lisa yalikuwa yamepinda huku akitabasamu alipoona kiasi hicho cha pesa. Tabasamu lile tamu liliujaza moyo wa Alvin hadi ukingoni.

Bado alikuwa na hasira kidogo mwanzoni, lakini ilikuwa ni kana kwamba hasira yake ilitulizwa kwa ghafula. Milioni 80 tu? Angeweza kuirejesha kwa sekunde chache tu. Kwa thamani ya biashara zake kama mtu tajiri kabisa, alikuwa akiingiza angalau milioni 500 kwa saa, awe mamcho au amelala! Milioni 80 ilikuwa psa ndogo tu. Akiwa na huzuni, alipokea video hiyo kwenye simu yake.

“Kwaheri. Ilikuwa ni furaha kufanya biashara na wewe wakati huu." Lisa akageuka na kuondoka. Alikuwa ametoka nje kwa muda tu na kupata milioni 80. Jamani, alitaka kuhudhuria karamu nyingi zaidi kama hiyo.

“Subiri…” Alvin alifoka bila fahamu alipomuona akiondoka.

“Kuna kitu kingine chochote?” Lisa alitazama nyuma. Sehemu ya nywele zake ndefu za rangi ya korosho zilipeperushwa na upepo wa usiku, ukifichua uso wake wenye kustaajabisha na shingo yake kama ya swala.
Koo la Alvin likamkauka. Hakuweza kujizuia kusema, “Usicheze na Jack tena kuanzia sasa. Inatia aibu.”

"Nicheze naye, nisicheze naye, hiyo haikuhusu. Wewe povu linakutoka la nini? Mwanamume hapendezi kuwa mbea"

Alvin alikunja uso. "Kwa hiyo mimi ni mmbea?"

“Kwa sababu unaendelea kujiingiza katika mambo ya watu wengine,” Lisa alijibu kwa kejeli.

Alvin alicheka. “Wewe ni mke wangu wa zamani. Jack ni kaka yangu. Je, watu watasema nini ikiwa nyinyi mtakuwa pamoja? Nyinyi wawili hamna aibu, lakini mimi najali heshima yangu.”

“Unamchukulia Jack kama kaka yako? Ulimpiga upendavyo katika kampuni na kumfanya awe kicheko Nairobi nzima,” Lisa alimkaripia, “Sijawahi kuona mtu mbabe na mbinafsi kama wewe.”

"Kwa hivyo unajisikia vibaya kwa Jack sasa?" Alvin alikodoa macho. Hasira ilimtoka machoni pake.

“Aliokoa maisha yangu. Kwa hivyo ni lazima niwe upande wake?” Lisa alitabasamu aliposema, “Hata hivyo sisi sote tupo single. Kuna tatizo gani hata tukiamua kuwa wapenzi? Jack pia ni handsome kuzidi hata mtu fulani.”

“Thubutu!” Macho ya hasira ya Alvin yalionekana kana kwamba yanataka kumrukia. "Familia ya Kimaro haitakubali hili."

“Haijalishi hata kama hukubaliani, kwa sababu Jack ametelekezwa katika Kampuni ya KIM. Anyway, hata mkimtimua kabisa, anaweza tu kufanya kazi katika kampuni yangu. Inaweza kutokea kwamba nina kampuni nyingi sana ambazo siwezi kuzisimamia zote. Nani anajua? Huenda utaniita 'shemeji' siku zijazo." Lisa alimtazama. "Hujui kwamba maisha yamejaa mshangao?"

Kifua cha Alvin kilidunda hadi kichwa kilimuuma. Aligundua kuwa asingeweza kufanya mazungumzo na Lisa. Kila mara alikuwa akikasirika sana hivi kwamba alihisi kama alikuwa karibu kupata mshtuko wa moyo.
"Lisa, ningependa kukuangamiza kuliko kukuacha wewe na Jack kuniingiza katika aibu."

“Usijali, nilikuwa najisemea tu hata hivyo. Kuna watu wengi sana wanajaribu kunitongoza sasa. Jack ni chaguo moja wapo tu. Bado sijachagua mmoja.” Lisa aliondoka huku akionyesha dharau baada ya kusema hivyo.

Alvin aliupiga mti kwa hasira. Walikuwa wametalikiana, lakini kwa nini hisia zake bado zingeweza kutawaliwa na mwanamke huyo? Alitamani hata kumficha alipomwona akicheza na mwanaume mwingine.

Aliporudi kwenye jumba la karamu, Cindy alikuwa akicheza piano.
Sauti tamu na laini ya kuimba kucheza kwake ilisikika katika jumba la karamu. Wageni walifurahia onyesho hilo kwa kuwa watu wengi katika familia za matawi ya juu walikuwa na mapenzi fulani na piano na muziki.

Watu walikuwa wakizungumza kumsifia;

"Cindy sio diva wa tasnia ya muziki bure. Anaweza kuimba noti za chini na za juu huku akicheza piano bila kuhitaji kuvuta pumzi.”

"Hiyo ni kweli. Uwezo wake sio wa maonyesho tu. Si ajabu Dokta Choka amekuwa akimsaidia miaka hii michache.”

"Sio tu kwamba anamuunga mkono, lakini pia anamdekeza sana. Chester humpa chochote anachotaka. Hata alimsaidia alipofanya mabadiliko kutoka kuwa mwimbaji hadi kuwa nyota wa filamu.”

"Ulienda wapi? Nilikutafuta kila mahali. Jack alikimbilia upande wa Lisa kwa haraka na kusema. “Unafuata baada ya Cindy…”

"Nimetoka tu kutafuta pesa kidogo." Lisa alimwonyesha milioni 80 ambazo alipata.

Jack alishtuka. "Ni nini, umepata wapi?"

"Ndugu yako." Lisa alimn”yooshea kidole Alvin ambaye aliingia kwa nyuma huku akionyesha giza totoro.
Jack alimpa dole gumba. “Nimevutiwa. Ninunulie dinner ya laki baadaye.”

“Siwezi. Bwana Malugu alisema atanirudisha nyumbani baadaye.” Lisa alipofikiria jinsi alivyokuwa amepata pesa hizo kupitia video ya baba yake, hakuweza kujizuia kumuonea huruma Jack. Ilimsumbua kwa muda na kujikuta anashikwa na hatia. "Ili kufidia masikitiko yako ya kunikosa, nitahamisha milioni 40 kwako."

Jack alikuwa ameduwaa kutokana na mshtuko. "Wewe ... wewe ni mkarimu sana?"

“Sisi ni marafiki! Ni milioni 40 tu.” Lisa alimhamisha zile pesa bila mpangilio na kuondoka zake......ITAENDELEA.......

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.