JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................353-354
Sura ya: 353
Siku iliyofuata baada ya Nina kuhukumiwa, Joel alitangaza hadharani kwamba amemfanya Lisa kikamilifu kama mrithi wake na mrithi wa urithi wake. Zaidi ya hayo, Lisa angekuwa msimamizi wa kila jambo, liwe kubwa au dogo, alipokuwa amelazwa hospitalini.
Hapo ndipo watumiaji wa mtandao walipogundua kwamba utajiri wa Joel ulifikia kiasi cha dola za Marekani bilioni tatu. Pamoja na thamani ya soko la kampuni ya Mawenzi Investments, ilimaanisha kwamba Lisa angekuwa mwanamke tajiri zaidi nchini Kenya.
Si hivyo tu, lakini mitandao pia ilisheheni picha mbalimbali za urembo wake na sifa zake za elimu ya juu. Mamia ya maoni yalitiririka kufuatia habari hiyo kusambaa kama upepo mitamdaoni;
[Nimekuwa mmoja wa mashabiki wake. Ni mwanamume gani atastahili mwanamke tajiri, mrembo, na mwenye kipaji kama yeye?]
[Hivi, hata anahitaji mwanaume kweli? Si bora kwake kuwa single? Anaweza hata kubadili kati ya wavulana wachache na wazuri wakati wowote anaotaka.]
[Ni ukumbusho tu kwamba yeye ndiye mke wa zamani wa Alvin Kimaro.]
[Hivi Alvin Kimaro ni kipofu? Lisa ni dhahiri kuwa ni bora kuliko Sarah kwa sura, thamani halisi na urembo.]
Mashabiki wa Sarah ambao hawakuridhika walionekana kumtetea pia.
[Sarah ana shida gani? Yeye ni mwanasaikolojia maarufu. Ana kipaji na mzuri pia. Kando na hilo, yeye ndiye mmiliki wa New Era Advertisings.]
[Kwani ni nini ikiwa yeye ni mwanasaikolojia? Lisa pia ni miongozi mwa wabunifu bora wa Kilimani Group, na mkurugenzi mkuu wa ubunifu wa kampuni hiyo]
[Kilimani Group ni nini? Sijawahi kusikia.]
[Jibu mbele yangu. Ni sawa kama hujui, lakini tafadhali usifichue ujinga wako. Utaiona mara tu unapotafuta kwenye mtandao. Kilimani Group ni kampuni ya ujenzi maarufu na yenye mapato ya juu zaidi Afrika. Watu wengi wenye vipaji katika Kilimani Group ni wasanifu mashuhuri wa kimataifa ambao wamepokea tuzo nyingi, na mapato yao ya kila mwaka yanazidi makumi ya mabilioni kwa urahisi. Ili kuwa afisa mkuu wa kubuni wa Kilimani Group, lazima awe mmoja wa wasanifu watano bora Afrika, angalau. Lisa alishinda tuzo kadhaa huko Tanzania na hapa Kenya kama vile Grand-Prix award ya Lexus Crowns]
[Hiyo haiwezekani. Lisa bado mdogo sana. Acha kukuza mambo.]
[Naweza kuthibitisha hilo. Siyo ya kujisemea tu. Baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu, nilipata fursa ya kufanya mafunzo yangu katika Kilimani Group mwaka jana. Nilitokea kukutana na Lisa, na wakati huo, hata Lorenzo alikuwa akimheshimu.]
[Lorenzo. Unazungumza juu ya mbunifu, Lorenzo, ambaye alichukua Tuzo la ‘AAK Duracoat Awards of Excellence in Architecture’ mwaka jana?]
[Ndiyo, huyo ni yeye.]
Huku kukiwa na mjadala mzito kwenye mtandao, Kilimani Group ilichapisha kimataifa picha ya Lisa: [Bi Lisa Jones, afisa mtendaji mkuu wa kampuni yetu, ambaye alichukua nafasi hiyo mwaka jana.]
Habari hizo zilishangaza Kenya nzima.
Watu wengi walitoa maoni kwenye akaunti ya Facebook ya KIM International.
[Bwana Kimaro, hadhi ya mke wako wa zamani imekuwa juu sana. Unajuta?]
[Haha, Alvin Kimaro, asante kwa kumtaliki Lisa wetu. La sivyo, asingekuwa hapa alipo leo.]
[Bwana Kimaro, tafadhali usijute na uje kumtafuta Lisa wetu siku zijazo.]
Kwa siku moja nzima, mratibu wa ukurasa wa Facebook wa KIM International alikuwa na kazi ya kufuta ujumbe mmoja baada ya mwingine, lakini maoni hayakuwa na mwisho, kadri alivyoyafuta ndivyo yalivyozidi kuingia. Jambo hilo lilimfanya aingiwe na wasiwasi kiasi cha kutokwa na jasho.
Wakati huo, mkutano wa ndani wa ngazi ya juu wa KIM International ulikuwa ukiendelea. Jack alikuwa akitazama chini kwenye simu yake wakati ghafla alifoka. Chumba cha mikutano, ambacho kilisikika sauti ya Alvin pekee, kilikuwa kimya sana. Kila mtu alitazama kuelekea Jack.
Umbo la Alvin la kifahari liliegemea nyuma, na kalamu iliyokuwa mikononi mwake akaitupa mezani. Macho yake makali yalikuwa ya hasira kali. “Meneja Mkuu Kimaro unajishughulisha na nini? Kwanini haupo pamoja nasi kwenye mkutano?”
Jack aligusa pua yake. “Unataka kujua kweli?” Wasimamizi wakuu walishusha pumzi zao. Waliweza kuhisi hali ya hewa ikiwa imeanza kuchafuka. Wawili hao walipokaa pamoja haikupita hata dakika tano bila chumba kugeuka kama Urusi na Ukraine.
“Ninaangalia akaunti rasmi ya Facebook ya kampuni. Inakaribia kulipuka.” Jack alitabasamu bila kufafanua. "Inahusiana na wewe, Mkurugenzi Kimaro."
Meneja mmoja alicheka na kusema, “Lazima ni watu wanaompongeza Mkurugenzi Kimaro na Bi. Njau kwa harusi yao.”
"Hiyo ni sawa. Hivi majuzi, watu wengi walikuja kwenye kampuni kutoa baraka zao. Mkurugenzi Kimaro ndiye mtu tajiri zaidi wa Kenya.”
Alvin alibaki kutojali, lakini alikubaliana na kile wasimamizi wakuu walisema. Hata hivyo, hakupendezwa na mambo hayo hata kidogo. "Kwa hivyo ... hiyo ndiyo sababu umakini wako ulizunguka kwenye simu yako katika mkutano muhimu wa kampuni?"
“Hapana, umeelewa vibaya. Inahusu… mke wako wa zamani.” Jack aliinua mabega yake. "Huenda hujui kuhusu hilo bado, lakini Joel tayari amemfanya Lisa kuwa mrithi wake. Wanamtandao wanajadili thamani halisi ya Lisa, na kuna mtu hata akafichua madili yake yaliyofichwa. Kumbe yeye ni mkurugenzi wa ubunifu wa Kilimani Group. Kilimani Group tayari imethibitisha hilo.”
"Kilimani Group?" Baadhi ya wasimamizi wakuu walishangaa. "Ni ukweli? Hiyo ndiyo kampuni ya juu zaidi ya ujenzi Afrika. Wanaofanya kazi huko wote ni magwiji katika uwanja wao. Ni lazima awe gwiji kwa kuwa na cheo kama hicho.”
“Sisemi uongo. Unaweza kujiangalia mwenyewe ikiwa huniamini.” Jack alimtazama Alvin kwa kuchekacheka. “Kaka, ulijua hilo? Hata hukuniambia.”
Alvin alikosa la kusema. Hakujua jambo lolote kati ya hayo. Haishangazi Kilimani Group ilikuwa ya kwanza kushirikiana na Lisa. Mwanamke huyo… alikuwa na uwezo mkubwa, jambo ambalo hakulitarajia.
Tayari alishangazwa na kazi nzuri aliyoifanya kuwaondoa wanahisa wasiotii wa Mawenzi Investments mara ya mwisho, lakini, hakutarajia kwamba angemshangaza tena.
Alvin alikodoa macho. Hakuweza kujizuia kupendezwa na mwanamke huyo kwa mara nyingine tena.
Akivunga hamu ya kuitoa simu yake na kutazama umbea, Alvin alisema kwa ukali, “Tuko katikati ya mkutano. Ondoka kama unataka kujadili mambo mengine."
Kila mtu katika chumba cha mkutano akanyamaza. Jack aliinamisha kichwa chake na hakuongea zaidi.
Mkutano ulipelekwa haraka haraka huku mada zikipitiwa juujuu tu. Takriban dakika 10 baadaye, mkutano ulikuwa umekamilika. Kitu cha kwanza alichofanya Alvin ni kuitazama simu yake. Alipoona habari kuhusu Lisa, karibu apige namba yake, bila kujua lengo lake ni kumpongeza au kumdhihaki, lakini sekunde moja baadaye, akakumbuka kwamba alikuwa mwanamume aliyeoa.
Alijizuia na kuwasha sigara. Alipitia kila habari hadi mwishowe, macho yake yakatua kwenye picha nzuri ya Lisa. Alipigwa na butwaa kwa muda na hakuweza kupinga kuhifadhi picha hiyo.
•••
Mawenzi Investments.
Wakati Lisa alipopita kuelekea ofisini kwake, nusura azime kwa kelele za pongezi kutoka kwa wafanyakazi wake.
"Mkurugenzi Jones, wewe ni wa kushangaza sana."
Kwa kustaajabishwa, Amba alikuwa akihaha kwa kugonga mikono na magoti yake. "Vyombo vya habari vingi vimepiga simu kuomba mahojiano ya kipekee na wewe asubuhi ya leo. Ulifanya nini hasa kubadilisha hali yako katika miaka mitatu?"
'Nilitegemea kitu pekee cha thamani alichonipa Mungu, akili, bila shaka.” Lisa alisema kwa utulivu. “Tafadhali kataa mahojiano yote ya kipekee. Niko busy,”
“Sawa, lakini umealikwa kuhudhuria Starlight Gala na Times Media kesho usiku. Bwana Ngosha awali alitakiwa kuhudhuria, lakini amelazwa, kwa hiyo mwaliko ulikuja kwako.”
Sura ya: 354
Lisa alipokea kadi ya mwaliko na kuichezea mikononi mwake. "Je, kuna maana yoyote kwa aina hii ya mialiko?"
"Watu mashuhuri kutoka kila tasnia watakuwepo. Nilisikia kwamba Cindy, mwimbaji mashuhuri wa kike unayemchukia zaidi, atatumbuiza pia.” Amba alimchombeza Lisa kwani aliogopa asingehudhuria mwaliko huo. “Ikiwa huna shughuli nyingi, unaweza kwenda kumpa wakati mgumu kidogo, si unakumbuka wakati ule alivyokuwa anachonga sana akiwa na Sarah?”
Sekunde chache baadaye, Lisa alicheka. “Wow, Msaidizi wa miye, unazidi kuwa mkorofi zaidi kama bosi wako. Cindy ni mpenzi wa Chester. Huogopi kwamba nitaingia kwenye matatizo?”
Amba alisema huku akitabasamu, “Wewe ni mrithi wa kampuni ya Ngosha na mbunifu mkuu wa Kilimani Group sasa. Thamani ya kampuni ya Mawenzi Investments imepanda hata maradufu. Watu wengi sana wanajaribu kukufahamu. Ingawa familia ya Chokaina nguvu, wewe pia si haba. Ni lazima wajiulize mara mbili kwa sasa kabla ya kukufanyia ujinga wowote.”
“Una hoja hapo. Kwa bahati nzuri, nina jambo langu na Chester pia.” Lisa alifunga kadi ya mwaliko. Lisa alikuwa bado na kinyongo kwamba hospitali ya familia ya Choka ilimfukuza Joel mara ya mwisho.
•••
Usiku. Kwenye lango kuu la ukumbi wa mikusanyiko, Ssafu na safu za magari ya kifahari yaliingia. Kwenye zulia jekundu refu, Lisa alishuka kutoka kwenye gari nyeusi aina ya Rolls-Royce Ghost. Alivalia mavazi ya nguva yenye matundu ya almasi, ambayo yalionyesha kikamilifu mikunjo yake yenye umbo la S. Iliyolingana na sifa zake maridadi na rangi ya korosho iliyokoza, alionekana kama binti wa kifalme moja kwa moja kutoka kwenye jumba la malikia. Alikuwa wa kisasa, wakifahari, mzuri, na asiye na mbwembwe. Angeweza kuelezewa kwa kila kivumishi cha sifa.
Wanawake wasomi na watu mashuhuri waliovalia mavazi ya kifahari usiku huo walipauka kwa kulinganisha na Lisa. Si nyuma ya Lisa, Cindy alishuka kutoka kwenye gari aina ya Bentley Bentayga. na kumshika mkono Chester. Hata hivyo, Lisa alivutia macho sana hivi kwamba hakuna mtu aliyemwona Cindy pindi anaingia.
Cindy akasaga meno kwa chuki. Times Media ilikuwa moja ya makampuni makubwa ya Kenya, kwa hivyo hapo awali alikuwa amepanga kuwa bora usiku huo. Hata vazi alilovaa lilibuniwa na mbunifu wa hali ya juu, ambaye alikuwa ameombwa na Chester kwa muda mrefu. Kamwe hakutarajia kwamba Lisa angemwibia umaarufu tena. Hata alipata nafasi ya kusaini mkataba na Mawenzi Investments kama balozi wao, lakini Lisa aliuvunja.
Kwanini hakufa miaka mitatu iliyopita? Ikiwa angefanya hivyo, Cindy asingekuwa mtu wa kudharauliwa sana. Ilisikitisha zaidi kwamba Lisa alikuwa sasa mrithi wa Ngosha Corporation. Hakuna kinachomkera mwanadamu zaidi ya mafanikio ya mwanadamu mwingine.
"Chester, sikuwahi kufikiria kwamba Lisa angezingatiwa sana. Ulikuwa unaangaziwa popote ulipoenda." Cindy alificha wivu wake na kumtania yule mtu mashuhuri kando yake.
Chester akarekebisha miwani yake yenye fremu ya dhahabu na kumtazama kwa mawazo. “Kwanini? Unamwonea wivu?”
Cindy alishangaa, lakini hakuthubutu kufsema ujinga wowote mbele ya Chester. “Hilo ni hakika. Ni nani hapa ambaye hatamuonea wivu? Ana bahati sana.”
“Una bahati pia. Unapaswa kujifunza kuridhika na ulicho nacho.” Sauti ya Chester ilikuwa ya kubembeleza, lakini ilikuwa ya kutisha.
Cindy alitabasamu huku akisema, “Nimeridhika sana kukutana na wewe. Lakini… Alvin Kimaro na Sarah watakuwa hapa usiku wa leo pia. nina wasiwasi sana…”
“Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu watu wengine. Kila mtu yuko ndani ya jumuiya moja nchini Kenya na hatimaye tutagongana tu. Sarah lazima azoee.”
Baada ya Chester kusema kwa utulivu, Cindy aliweza tu kuinamisha kichwa chake na kunyamaza.
Lisa alipoingia kwenye jumba la karamu, aligundua kuwa kulikuwa na watu wengi waliofahamiana naye usiku huo, kama vile Jerome na Melanie, Lea na Mason. Pia kulikuwa na Jack, Kelvin, Rodney…
Lisa akacheka. Hata damu katika mwili wake alihisi ikikimbia kwa kasi.
Usiku huo ulikuwa unaenda kuwa wa kuvutia. Baada ya miaka mitatu, watu waliofahamiana wote walikusanyika mahali pamoja.
Kelvin aliinua glasi yake kuelekea kwake kutoka mbali. Punde, alipokea ujumbe wa WhatsApp kutoka kwake: [Ninajua unalenga nini, kwa hivyo sikukukaribia. Lakini nitakuwa nikikutazama.] Moyo wa Lisa ukapata joto.
Jack, ambaye alivalia suti nyeupe, alimwendea kwa furaha na kumpa glasi ya mvinyo. “Sikutaka kuhudhuria mara ya kwanza, lakini niliamua kuja mara moja niliposikia kwamba na wewe ungehudhuria. Usiku wa leo utapendeza sana.”
“Pamechangamka kweli kweli. Nimependa sana.” Lisa alikunywa mvinyo kabla ya mdomo wake kuinua tabasamu la kuvutia.
Mwangaza uliangaza machoni pa Jack. Ghafla akahema kwa majuto. “Usingeolewa na Alvin kwanza, hakika ningekuoa. Lakini nikikutongoza sasa hivi, wanafamilia wa Kimaro bila shaka watanisema vibaya. Hakuna mtu ambaye angeweza kukubali ndugu wawili kuoa mwanamke mmoja.”
“Kwa bahati nzuri, hukunitongoza. ningekubali.”
“Kwa nini?”
"Kwa sababu nina wachumba wengi sana." Lisa aliwatupia macho wanaume waliokuwa wakimtazama kwa pembeni. "Angalia, kuna watu wengi ambao wanajaribu kumrithi kaka yako."
“Ni kawaida. Sasa wewe ndiye mwanamke mrembo, mwenye kipaji, na mwenye thamani ya juu nchini Kenya.” Jack alinyoosha mkono wake kwake. "Unaweza kucheza na mimi? Ninataka kuwa mtu anayeonewa wivu sana usiku wa leo. Nipe furaha hii."
“Sawa.” Lisa aliweka mkono wake kwenye kiganja chake kikubwa, na wote wawili wakatembea kwenye uwanja wa muziki.
Walichukua nafasi kama wanandoa wakamilifu. Mara moja walivutia wivu na porojo za watu wengi, lakini wote wawili walipuuza yote na badala yake wakaanza mazungumzo.
“Sema, kwa nini umekuja leo? Kuharibu sherehe?" Jack aliuliza kwa utani.
Lisa akatumbua macho. "Ni tamasha la Times Media, kwanini niharibu? Nimekuja tu kucheza gitaa na kufurahi na kujumuika na marafiki.”
"Unajua kucheza gitaa?" Jack akakohoa. “Walimwalika Cindy kutumbuiza usiku wa leo. Yeye ni mtaalamu.”
“Ni vizuri. Nataka kutumbuiza baada yake.” Lisa alidhamiria. "Niliandika wimbo mpya, na nahisi watu wataupenda sana. Unaweza kuusikiliza kidogo?”
Jack nusura apoteze stepbaada ya Lisa kumwimbia sikiono kipande cha wimbo huo. “Lisa, unataka kumchokoza Cindy? Huu wimbo ameuachia hivi karibuni na unafanya vizuri…”
“Ni wimbo wangu.” Lisa alimnong’oneza huku akitabasamu.
“Toka lini umekuwa mwanamuziki?"
“Huniamini?” Lisa alimkazia macho. “Mimi ndiye niliyeandika nyimbo maarufu za Cindy. Nilikuwa nikicheza gitaa na piano kabla hata Cindy hajajifunza kuimba. Ndoto yangu ya kwanza ilikuwa kuwa mwanamuziki lakini mazingira yalinibadilisha kuwa injinia. In fact ni kwamba Cindy alivutika kuwa muimbaji kupitia mimi.”
Mshangao ulikuwa umeandikwa usoni mwa Jack. “Kwa hiyo huu wimbo mpya ni wewe pia uliuandika?”
“Sio huo tu, hata ule uliomtoa kwenye gemu niliuandika mimi. Ni vile tu kwamba amesahau kushukuru. Ni lazima nimfundishe hilo leo.” Lisa alilalamika.
"Una ujuzi gani mwingine ambao siujui?" Jack alikosa la kusema.
“Mimi ni hazina. Maisha yangu ya utotoni yalikuwa magumu sana hapo awali, na kipaji changu kilizuiwa na wengine. Sasa, ni wakati wangu wa kuangaza.” Lisa aliongea kwa kujiamini. Jack hakuweza kujizuia kuangua kicheko....ITAENDELEA.....
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
