JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................351-352
Sura ya: 351
Baada ya Joel kujionea ‘live’ usaliti wa Nina, alishindwa kuvumilia na kupata mshtuko wa moyo. Lisa alimpeleka baba yake haraka hospitali kuingiziwa dripu ya IV. Ingawa kuona Nina akikamatwa kulimfanya Joel kupumua, afya yake ilidhoofika tena kwa sababu alikuwa amechanganyikiwa.
Haikuchukua muda Mzee Ngosha na Bibi Ngosha wakakimbilia hospitali. Mara baada ya Bibi Ngosha kuiona hali ya Joel, machozi yakaanza kumlenga lenga. "Nina hana akili. Tulimtendea vizuri sana kwa miaka mingi. Ajali uliyokutana nayo miaka mitatu iliyopita lazima inahusiana naye. Kwa bahati nzuri, mimi na baba yako tulimwomba Lisa akutunze. Vinginevyo…”
Maneno hayo yalipelekea mtetemo kwenye uti wa mgongo wa Mzee Ngosha. Sasa alipofikiria jambo hilo, alitoa shukrani zake za dhati kwa Lisa. "Tuna deni kubwa kwako, mjukuu wangu..."
Lisa alitabasamu na kukaa kimya kwa muda. “Usijali kuhusu hilo, babu. Sikuwahi kutarajia mengi kutoka kwa familia ya Ngosha, kwa hiyo sijavunjika moyo.”
“Wewe...” Mzee Ngosha aliona aibu ghafla.
Bibi Ngosha akamvuta. “Lisa yuko sahihi. Kwa kweli tabia yetu ilimkatisha tamaa tangu mwanzo. Ni kosa langu. Sikupaswa kumzuia Joel kumuoa mama yako. Samahani sana."
Mzee Ngosha alikunja ngumi na kukohoa kwa aibu. “Nakubaliana na bibi yako. Kuanzia sasa jisikie huru kabisa. Unakaribishwa nyumbani muda wowote utakao. Baada ya yote, hiyo ni nyumba yako."
Lisa alipigwa na butwaa kwa muda na kujawa na hisia mseto. Kwa kweli, alitamani kwamba babu na bibi yake wangemwambia hivyo alipofika Nairobi kwa mara ya kwanza. Hata hivyo, walimzingua pindi tu walipomuona. Siku zote alilazimika kupambana peke yake ndani ya jiji hilo, jambo ambalo lilimfanya ajisikie kama mgeni.
Wakati huo, kuna mtu aligonga mlango, ambapo Melanie aliingia akimsukuma Damien, ambaye alikuwa ameketi kwenye kiti cha magurudumu.
“Mnatafuta nini hapa?” Joeli alipowaona, alianza kupandwa na hasira na kukohoa kwa nguvu.
“Joel, usifadhaike. Ni mbaya kwa afya yako.” Mzee Ngosha kisha akawanyooshea kidole Damien na Melanie, na kusema, “Tokeni nje.”
“Babu tumekuja kukuomba msamaha. Kwa kweli sikujua kwamba Mama alifanya mambo hayo.” Melanie aliinua kichwa chake na kujibu kwa uchungu. Macho yake yalikuwa mekundu.
“Ulikuwa hujui kweli?” Lisa alidhihaki, “Wewe ndiye uliyempeleka Baba kwa uchunguzi wa kimatibabu kila mara. Wewe na Nina mlipanga njama hizi zote pamoja, lakini una bahati kwamba mama yako ndiye aliyebeba lawama zote.”
Baada ya ukimya wa muda, Lisa alihamishia macho yake kwa Damien. “Baba mdogo, ninazungumza na wewe hivi kwa sababu mimi ni mtu mstaarabu sana. Kama ningekuwa wewe, ningeona aibu kujitokeza hapa. Ikiwa baba yangu angekufa kwa sumu, Kampuni ya Ngosha ingeenda kwako na Melanie. Nyote wawili mngefaidika zaidi, na Nina aliyeenda gerezani kwa niaba yenu.”
Uso mzuri wa Damien ulilegea kabla ya kujibu, “Siku zote nimemchukulia kaka yangu kama baba yangu, kwa hiyo ningewezaje kujaribu kumuua kaka yangu? Kaka nitapiga magoti nakuomba msamaha sasa. Kwa miaka hii yote, nilipumbazwa na Nina na nimefanya mambo mengi mabaya dhidi yako, lakini sikupanga kukuua hata kidogo.”
Damien alipokuwa akizungumza, alijilazimisha kutoka kwenye kiti cha magurudumu na kupiga magoti sakafuni. Hata hivyo, miguu yake ilikuwa dhaifu sana kuweza kusimama. Mara miguu yake ikageuka kuwa mlenda, alianguka sakafuni vibaya.
“Baba.” Melanie alilia na kwenda kumshika kwa haraka.
“Melanie, nishike nipige magoti.” Damien aliendelea.
Kwa kuwa Damien alikuwa mwanae wa kumzaa, Bibi Ngosha alishindwa kuvumilia kumuona akipiga magoti. “Miguu yako imelemaa. Utapiga magoti vipi? Fanya haraka ukae kwenye kiti chako.”
"Ndio, miguu yangu imelemaa." Damien aliinamisha kichwa chini na kububujikwa na machozi. “Tangu nilipozaliwa, watu wengi wamekuwa wakinidharau kwa sababu tu ya ulemavu wangu. Ninamshukuru Kaka, lakini wakati huo huo, ninamwonea wivu. Nampenda Nina, lakini hakuwa anavutiwa nami. Zaidi ya miaka ishirini iliyopita, sijawahi kumpenda mtu mwingine yeyote isipokuwa yeye. Nilimfanyia kila kitu bila kulalamika. Nilidhani angeniangukia hatimaye baada ya kupata Ngosha Corporation, lakini nilikosea. Ni sasa tu ndio nimeelewa utu wake. Baba, Mama, Kaka, ni kosa langu…”
Bibi Ngosha alikuwa kwenye hatihati ya kulia. Hakuweza kupinga kusema, “Yote ni makosa yangu. Sikupaswa kukuzaa na kukufanya uteseke sana na kujidharau.”
“Baba, Mama, mnaweza kunilaumu mimi. Ni sawa. Lakini natumaini hamtamchukia Melanie.” Damien aliinua kichwa chake na kuomba. "Melanie hana hatia. Sijawahi kuoa, na yeye ni binti yangu wa pekee. Yeye pia ni mjukuu wako wa damu.”
“Babu, Bibi, samahani. Nimekuwa mbali nanyi kwa muda mrefu, na imenisikitisha sana. Bado mnakumbuka jinsi mlivyokuwa mkinijali?" Melanie mara moja akapiga magoti karibu na Damien. Alitazama juu na kugeuza nywele zake kuelekea nyuma, akionyesha uso uliopigwa na kuvimba.
"Ni nini kilitokea kwenye uso wako?" Mzee Ngosha aliuliza kwa sauti nzito.
Melanie akasonga na kuuma mdomo. Kisha, Damien akasema kwa huzuni, “Ni Jerome aliyempiga.”
"Ni mpuuzi sana huyo mwanamume." Mzee Ngosha alipandwa na hasira. "Familia ya Campos ina kiburi sana. Nitakutana na babu yake.
Familia yetu imewanyanyua sana mafukara wale wasio na shukrani, hawakuwa na kitu chochote!”
“Ni sawa, babu. Tayari wewe ni mzee. Hakuna haja ya kusimama kwa ajili yangu, na sitaki wewe kuwa upset kwa sababu yangu. Familia ya Campos sio sawa na ilivyokuwa hapo awali. Jerome alisema kwamba alinioa kwa sababu tu alifikiri nilikuwa…Binti wa Joel. Alichagua kuwa nami kwa sababu ya familia ya Ngosha.” Tabasamu la uchungu likapita usoni mwa Melanie.
“Ni dharau kiasi gani?” Damien alisema kwa uchungu huku akimpapasa Melanie sehemu ya nyuma ya mkono wake. “Ni kosa langu, sio lako. Ananidharau kwa sababu mimi ni mlemavu na siwezi kumsaidia chochote”
“Inatosha!” Bibi Ngosha hakuweza kuvumilia tena kusikia hivyo. "Sasa kwa kuwa Nina yuko jela, acha yaliyopita yawe yamepita. Damien, bora usiishi peke yako huko nje. Rudi nyumbani. Uwe mtu mzuri na ulete sifa njema kwa familia ya Ngosha pamoja na kaka yako.”
“Naweza kweli kufanya hivyo?” Damien kwa tahadhari akahamishia macho yake kwa Joel aliyekuwa amejilaza kitandani. “Baba, ni sawa. Sitaki Kaka anielewe vibaya.”
Midomo ya Joel ilicheza, lakini kabla hajazungumza, Melanie alisema, “Baba, msikilize babu. Mimi nakaa katika nyumba ya familia ya Campos. Nina wasiwasi kuhusu wewe kuwa peke yako katika hali yako. Je, ukianguka? Hata iweje, mtumishi wako si sehemu ya familia yetu kamwe.”
“Rudi tu.” Maneno ya Melanie yalimfanya Bibi Ngosha kukosa raha. "Hamia nyumbani leo."
Joel akafumba macho. Muda si mrefu, Mzee Ngosha na Bibi Ngosha waliondoka wakiwa na Damien na Melanie. Lisa alikuwa akitazama tukio zima kimyakimya. Hakuwahi kufikiria kwamba Damien na Melanie bado wangepokea hisani nzuri kwa wazee hao baada ya Nina kufungwa gerezani. Ukiachana na Melanie, Damien hakuwa na haya kama mwanaume.
“Unawaza nini baba?” Macho ya Lisa yakatua kwa baba yake. Ikiwa baba yake naye alifikiria sawa na babu na bibi yake, Lisa angejuta kujiingiza kwenye sakata hilo.
“Unafikiri kwamba mimi bado ni mjinga kama hapo awali? Baada ya kupitia mengi, nimeshajifunza somo langu.” Joel alilalamika. "Damien anatisha zaidi kuliko hata Nina. Anajua kabisa kwamba babu na bibi yako watamhurumia na kumbembeleza.”
“Najua." Lisa akahema. Babu na bibi yake walionekana kuwa wazee, lakini walikuwa na mali nyingi. Ingawa Mzee Ngosha alikuwa amestaafu kufanya kazi, bado alikuwa na nguvu katika Ngosha Corporation na ushawishi katika jiji la Nairobi. Mara baada ya Melanie na Damien kupata kampuni ya Ngosha Corporation, wangemtumia tena.
Sura ya: 352
“Lisa, kwa kuwa niko hospitalini, nitakuomba unishughulikie mambo fulani kwa sasa.” Joel ghafla akampiga piga Lisa nyuma ya mkono wake. "Nitamwambia msaidizi wangu kuripoti kwako mambo yote ya kampuni kuanzia sasa."
Kichwa cha Lisa kilianza kumuuma. "Baba, unanilazimisha kijanja kusimamia Kampuni ya Ngosha?"
“Ninakulazimisha vipi?” Joel alimkazia macho. "Kama binti yangu na mrithi wa Ngosha Corporation, hutaitwa tena binti haramu. Unastahili kuwa na mwanmke bora kabisa katika Kenya nzima. Hata Sarah pia hawezi kufananishwa na wewe.”
Nia ya Joel hatimaye ikamwingia Lisa. Hisia ya joto ikaenena ndani yake. Bila kusema, Joel lazima aligundua kuwa Alvin alikuwa akienda kufunga ndoa na Sarah, hivyo alitaka asihizunike. Kwa kuzingatia kwamba Lisa alikuwa mmiliki wa Mawenzi Investments, binti pekee na mrithi wa Ngosha Corporation, Sarah asingeweza kumshinda kwa heshima na hadhi. Haidhuru Sarah alikuwa na jeuri kiasi gani, yeye alikuwa mwanasaikolojia tu. New Era Advertisings, kampuni ya familia yao, ingekuwa imeanguka kwa muda mrefu bila usaidizi wa Alvin, na Thomas angekuwa jela kama si kukingiwa kifua na Alvin.
“Usijisumbue na mambo hayo mwanangu. Utaweza kupata mtu bora zaidi anayekustahili. Binti yangu ni mrembo sana, mwenye uwezo, na tajiri. Hakuna mtu yeyote katika Kenya anayeweza kukuzidi,” Joel alimtia moyo huku akitabasamu.
“Asante, Baba. Ninajiamini kila wakati. Kwa wale ambao hawakunichagua, ni hasara yao.”
"Safi sana." Joel alitabasamu.
Saa kumi jioni, Lisa alipanga foleni kwenye chumba cha pharmacy kilichokuwa chini ili kuchukua dawa. Alipomaliza, alirudi juu na kumuona Maya akitoka nje ya kitengo cha uzazi na magonjwa ya uzazi ya wanawake akiwa na Sarah.
Akiwa amevalia nguo nyeupe, Sarah alionekana kama malaika kiasi kwamba kila mtu hospitalini alimtazama mara mbili mbili. Kwa upande mwingine, Lisa alikuwa rafu kidogo kwani siku nzima tangu jana yake alikuwa akimuuguza Joel hospitalini. Hakuwa hata na chembe ya kipodozi usoni na nywele zake zilikuwa zimetimka kidogo, na alionekana amechoka.
Sarah alilinganisha sura yake ya nje na ya Lisa, akafurahi sana, na akapata nguvu ya kuongea mbele yake. "Hi, Lisa. Nini kinakuleta hapa? Nini tatizo? Hujisikii vizuri?”
Lisa akatoa macho yake na kuendelea kwenda mbele bila kumjali Sarah. Alihisi kuchoka sana baada ya kumtunza Joel kwa siku moja. Hakuwa na nguvu ya kupoteza kuongea upuuzi na mwanamke yule.
“We mwanamke, mbona huna adabu hivyo?” Maya alipiga kelele, “Bi Njau alikuwa anakusemesha, ina maana hujamsikia?”
“Bi Njau ni nani na kwanini nijibu swali lake?” Lisa aliwageukia kwa jazba na kusimama kwenye korido. Aliwatupia macho wawili hao kwa hasira.
“Wewe…” Maya alikuwa amekasirika kwa hasira.
Sarah alimsimamisha Maya na kusema kwa upole, “Lisa, najua unanichukia, lakini nimejitayarisha kukukubali. Kwa kweli ninampenda Alvin sana, na wewe najua unampenda, kwa hivyo tunaweza tu kushea. Naweza kukubali hilo.”
Lisa alichukizwa. “Oh, asante. Lakini sina mpango wa kushea mume na mtu yeyote. Ninaogopa kuambukizwa maradhi.”
Sura ya Sarah ilibadilika kidogo, kisha akainamisha kichwa chake. “Unathubutuje kutoa maneno ya dharau hivyo? Unapolala naye kila siku haimaanishi kwamba unampenda?” Aligusa tumbo lake huku akisema, “Sawa, unaweza kukaa kando basi uniachie mume wangu. Nimepanga kuzaa watoto wengi kwa Alvinic. Nilikuja hospitalini leo kuangalia jinsi ya kupata mapacha au mapacha watatu kwa njia ya urutubishaji katika mfumo wa uzazi.”
Maya alitabasamu na kusema, “Ni Bw. Kimaro ambaye alipendekeza kufanya urutubishaji kwa vitro aliposikia kwamba Sarah alitaka kupata angalau watoto wawili. Aliogopa kwamba angekuwa na wakati mgumu kuwa mjamzito mara mbili. Tayari amemuomba Dokta Choka kuajiri timu bora zaidi ya madaktari wa uzazi nchini kwa ajili yake.”
“Maya…” Sarah alimtazama kwa aibu na kudhihaki.
Macho ya Lisa yalitangatanga na kutua kwenye tumbo la Sarah kabla ya kucheka ghafla. "Ni bora kuwa mwanaume. Ni rahisi kwao kusema kwa vile wana kazi ya kutoa manii tu kwa ajili ya kuingizwa kwenye hiyo ‘artificial insemination’. Lakini wanawake wana kazi kubwa ya kupitia kila aina ya shida. Katika hatua za mwanzo, wanawake wanatakiwa kuchukua sindano na madawa. Nilisikia kwamba mchakato wa kuingizwa mbegu ni mchungu sana pia. Nakushangaa sana. Upendo wangu kwa Alvin si kama wako.”
Uso wa Sarah ukabadilika ghafla. Kwa kweli, alijua kila kitu ambacho Lisa alikuwa ametaja. Yeye pia alikuwa hataki, lakini hakuwa na jinsi kwa sababu Alvin hakuweza kumgusa hata kidogo.
“Umemaliza? Una wivu tu.” Maya alimshutumu Lisa kwa hasira.
"Nina wivu?" Lisa aliinua mabega yake. “Nina wivu gani? Nimepata mimba ya mapacha hapo awali, kwa hivyo sihitaji kupitia shida hizi zote. Inaonekana nimeweka kiwango cha juu sana kwa Alvin kwamba mtoto mmoja hawezi kumtosha tena.”
“Umezidi sasa Lisa.” Sarah aliuma mdomo wake kwa huzuni, na machozi yakaanza kumlenga lenga.
Lisa alitazama pembeni, na hakika Alvin alikuwa akielekea kwao. Kulikuwa na viongozi wachache wa hospitali pamoja naye.
Alipofika juu na kumuona Sarah analia, alimwangalia Lisa mara moja. “Ulimfanya nini tena? Si tayari tumeachana, kwanini unaendelea kutusumbua?”
Lisa aliongea kwanza kabla Sarah hajafungua mdomo wake. "Nilikuwa nashangaa tu kusikia kwamba umemwambia Sarah akuzalie watoto kwa njia ya upandikizi wa bandia. Kwanini usimruhusu apate mimba kwa njia ya kawaida? Unajua kwamba ni lazima atumie sindano na dawa kila siku kabla ya kuingizwa mimba kwa njia ya bandia? Bi. Njau, sisemi uwongo, sivyo?”
Sarah, ambaye mwanzoni alitaka kulalamika huku akitokwa na machozi, alipigwa na butwaa. Lisa hapo awali alikuwa akimnanga Sarah, lakini sauti yake mbele ya Alvin ilimfanya aonekane kana kwamba alimwonea huruma Sarah. Sarah alipoona hali ya kutofurahi ya Alvin, alieleza upesi, “Alvinic ana wasiwasi kwamba nitakuwa nimechoka sana ikiwa nitaendelea kubeba mimba mara kwa mara.”
"Ikiwa una wasiwasi kuhusu kumchosha, basi inatosha tu hata kubeba mimba mara moja. Hakuna haja ya kuwachukulia wanawake kama mashine za kutengeneza watoto,” Lisa alisema huku akiachia tabasamu.
“Kawaida wanandoa wanapoenda kwa ajili ya upandishaji mbegu kwa njia ya bandia, ni aidha hawana uwezo wa kuzaa au hawawezi kufanya ngono. Lakini ninafahamu wazi kama una uwezo au la. Haiwezekani kuwa ni Bi. Njau ambaye hana uwezo wa kuzaa…” Aliziba mdomo kwa mshangao. “Nakumbuka sasa. Nyote wawili mmekuwa pamoja kwa muda mrefu, lakini bado hana ujauzito.”
Uso mdogo wa Sarah ulibadilika rangi kwa hasira. Kwa hakika angeweza kupata mimba, lakini Alvin ndiye ambaye hakutaka kumgusa. Lakini, hakuweza kusema hivyo waziwazi, kwa hivyo aliweza kukubali tu macho ya kushangaza kutoka kwa viongozi wa hospitali. Alifadhaika sana hadi machozi yakaanza kumdondoka.
"Lisa, nitakuchana mdomo ikiwa utaendelea kuongea upuuzi." Alvin alimvuta Sarah kwenye kumbatio lake. Kisha, akasema kwa hasira kwa viongozi wa hospitali, “Mfukuzeni hapa. Sitaki kumuona.”
Akiwekwa katika hali ngumu, mkurugenzi wa hospitali alisema, “Bwana Kimaro, Lisa ni binti wa Bwana Ngosha. Bwana Ngosha kwa sasa amelazwa katika hospitali yetu…”
“Nataka familia ya Ngosha ihamie hospitali nyingine. Sitaki kumuona hapa,” Alvin alifoka na kuondoka huku akiwa amemkumbatia Sarah.
"Alvinic, yote ni makosa yangu. Nilikutia aibu.” Sarah alinung'unika mikononi mwake.
“Sio tatizo lako. Mimi ndiye nina makosa kukuacha uende kupandishwa mbegu kwa njia ya bandia.” Alvin alichanganyikiwa pia. Maneno ya Lisa yaligusa udhaifu wake, na kumfanya ajisikie fedheha.
“Ni sawa. Ilimradi niweze kuzaa mtoto wako, niko tayari kufanya hivyo,” Sarah alisema kwa utulivu. Alvin akahema. Alijisikia vibaya kwa ajili ya unyonge wa Sarah.
Dakika 15 baadaye, Lisa alipokea taarifa kutoka hospitalini kuwaamuru wabadili hospitali. Joel alikuwa katikati ya matibabu yake, lakini alikasirika aliposikia kuhusu hilo. “Alvin ana kiburi sana. Kwani familia yetu ilikuwa na chuki dhidi yake katika maisha yetu ya zamani? Au, matibabu yangu yalimsumbua kwa namna yoyote?”
“Baba si wewe uliyemsumbua, ni mimi.” Mapigo ya moyo wa Lisa yalikuwa chini. Angekumbuka kila kitu ambacho Alvin alikuwa amewafanyia.
“Lisa, usiwe na huzuni. Ni tatizo langu. Sikupaswa kuja katika hospitali ya familia ya Choka. Familia ya Choka na familia ya Kimaro zimetiwa lami kwa brashi sawa. Hebu tuondoke. Nitakumbuka ukatili huu wa leo. Sisi akina Ngosha tutarudisha walichotufanyia huko mbeleni,” Joel alisema huku akitulia.
“Ndiyo. Tutarudisha walichotufanyia.” Lisa aliitikia kwa kichwa.....ITAENDELEA...
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
