JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................345-346
Sura ya: 345
Saa tano usiku.
Gari jeusi lilisimama kwenye maegesho ya magari nje ya jengo kubwa la makazi kwenye eneo la maarufu la Karen Estate.
Alvin alitazama kiti cha nyuma. Lisa alikuwa amelala kuegemea kwenye dirisha, huku nywele zake zenye mawimbi zikiwa zimetanda kwenye mabega yake, mwanamke huyo alifinya macho yake pale Alvin alipowasha taa kwenye gari. Mwanga hafifu wa uso wake mdogo ulitoa haiba ambayo hakuna mwanaume angeweza kupinga.
Suti yake kubwa iliyofunika mwili wake mdogo ilimfanya aonekane kupendeza zaidi. Alvin aliegemeza kichwa chake kwenye usukani akiwaza kwa muda. Ikiwa dawa ziliathiri uamuzi wake wa kuja na kumwingia Lisa jana yake usiku, basi vipi usiku huo? Usiku huo alikuwa mzima kabisa. Mwanzoni, alikasirika na alitaka kumfundisha somo la kumtisha, lakini kwa namna fulani alipoteza udhibiti wa hisia zake njiani na kujikuta akimwingilia tena.
Wakati wawili hao walipokutana, kitu mapenzi kilikuwa na mvuto wa kiasili sana hivi kwamba Alvin hakuweza kujizuia kujiingiza ndani yake. Hakujua kwanini ilikuwa hivyo.
Mchana, alishikwa hatia waziwazi na kuumia moyoni alipomwona Sarah akiwa amefunikwa na majeraha. Hata aliapa kukaa mbali na Lisa.
Lakini, alihisi kama amepoteza busara yake mara tu baada ya kumuona tena Lisa. Ni kana kwamba aliwekewa dawa ya mapenzi na mwanamke huyu.
Akiwa amekasirika, alichukua sigara lakini akaiweka chini haraka alipofikiria kwamba kulikuwa na mwanamke nyuma yake. Baada ya kusubiri kwa dakika tano, bado mwanamke huyo hakuonyesha dalili za kuamka. Kwa hiyo, alishuka kwenye gari, akaenda siti ya nyuma na kumbeba Lisa kumtoa nje.
Hakuona wakati alipomnyanyua, lakini alipombemba aligundua kuwa alikuwa mwepesi sana. Midomo yake iliyovimba kidogo ilikuwa imelegea, ikionekana laini na ya kuvutia. Alionekana kupendeza.
Kwa bahati mbaya, alipombeba juu, midomo ya Lisa ikagusa kwenye kifua chake na kusuguasugua kidogo juu yake. Wakati huo Alvin alihisi ghafla moyo wake umelainika kama mafuta. Hisia za msisimko zikaanza kufurika tena mwilini mwake.
Alvin akambeba Lisa juu juu na kuchukua ufunguo kutoka kwenye begi lake ili kufungua mlango. Alipoingia ndani, akamweka taratibu kwenye kitanda kikubwa kilichokuwa chumbani humo. Mwanamke huyo mara moja alianza kujigeuzageuza juu ya kitanda. Alikumbatia mto na kurusha viatu vyake, akifunua miguu yake ya kupendeza. Rangi yangozi ya mapaja laini ya Lisa chini ya mng’aro wa taa ilikuwa inaroga.
Alvin nusura apate hamu ya kumbusu juu ya mapaja yake.
Lakini, wakati wazo hilo lilipopita, alishtuka. Jamani. Alikuwa anawaza nini? Alikuwa anafanya kama mpuuzi asiyejielewa. Mara aseme hamtaki, mara tena amtamani! Alvin akaamua kumfunika kwa blanketi kwa upole kabla ya kufunga mlango nyuma yake na kuondoka.
Alvin alipotoka, aliwasha simu yake na kuona missed call kadhaa.
Akafungua WhatsApp. Nusu saa iliyopita, alikuwa ametuma ujumbe kwa Sarah. [Nina safari ya haraka ya kikazi jioni na sitarudi. Lala mapema.]
Alishika kichwa chake kwa maumivu na kumpigia Chester. “Umelala? Njoo tupate kinywaji.”
“Sina nafasi. Nilifanya zamu ya ziada jana usiku, na nimechoka sana.” Chester alikataa.
“Basi, nitakuja kwako,” Alvin alisema kwa huzuni.
Alipofika katika nyumba ya kifahari ya Chester, Chester alikuwa bado amelala huku akikoroma. Alvin alimvuta pale kitandani. “Amka tunywe.”
Chester akauma meno na kusema, “Una nini muda huu? Hukurudi nyumbani kwako jana usiku, lakini uko hapa usiku wa leo pia. Huogopi Sarah atakuwa akikuwazia vibaya?… Subiri, ni harufu gani hiyo kwako?”
Chester alikosa la kusema. “Ni harufu ya mwanamke. Ni Lisa?”
“Umejuaje kuwa ni yake?” Macho ya Alvin yalimkazia.
“Nilisikia harufu yake alipofungua mlango asubuhi ya leo. Ilikuwa ni harufu nzuri, kwa hivyo nimeikumbuka."
"Umbea huo." Alvin alimpiga onyo kwa macho yake baridi mara Chester aliposema hivyo.
Chester hakujua la kusema. “Una mpango gani na hawa wanawake? Nilizungumza na wewe juu ya hii asubuhi tu. Kwa nini…”
“Vaa nguo.” Alvin akamtupia nguo zake na kutoka nje.
Chester alipanda juu kwa maumivu. Hata hivyo, alipotoka tu, alimuona Alvin akifungua chupa ya Lafite, mvinyo wa kifahari zaidi ambao Chester aliutunza kwa miaka kumi. “Alvin, fungua pombe nyingine yoyote lakini hivyo iweke chini!”
Kilichomjibu ni sauti ya 'pop' ya kufunguka kwa chupa. “Kuna maana gani kuendelea kuuhifadhi? Mvinyo umekufa, lakini sisi tuko hai."
Moyo wa Chester ulikuwa karibu kupasuka. “Jamani, kwa nini hukuenda kwa Rodney badala yake?”
"Ikiwa nitamwambia Rodney kwamba nililala na Lisa siku mbili mfululizo, bila shaka tutagombana." Alvin akammiminia glasi ya mvinyo.
Chester akajipapasa paji la uso na kushusha midomo miwili ya mvinyo harakaharaka, Alvin asije akamaliza yote. “Kwa hiyo ulikuwa unafikiria nini? Kuishi na wanawake wote wawili?"
"Sijui." Alvin akatikisa kichwa. “Siku zote nilifikiri ninampenda Sarah, lakini ninapomwona Lisa tu natamani kumlaza kitandani. Unajua maana hisia hizo?"
Chester akamtazama. “Hilo si jambo geni. Ulikuwa na hisia kwa Lisa zamani.
"Ni lini nilipata hisia kwake?" Alvin alikosa la kusema.
"Kumbukumbu zako za miaka mitatu iliyopita zinazidi kuwa mbaya siku hadi siku. Pengine umesahau mambo mengi.” Chester hakuweza kujizuia kukumbuka mambo fulani ya zamani.
Akiwa mtazamaji, alikiri kwamba Alvin alimpenda zaidi Sarah, lakini Sarah alipokuwa hayupo, Lisa alikuwa na nafasi muhimu sana katika moyo wa Alvin. Hata hivyo, aligundua kuwa Alvin alikuwa amesahau baadhi ya mambo.
Alvin alipigwa na butwaa. “Nimesahau nini?”
Chester akamtazama. "Unakumbuka kwenda Coco Beach na Lisa kipindi mnaishi Dar?"
"Nilienda Coco Beach?" Alvin alionekana kama amesikia mzaha. “Haiwezekani.”
Chester aliendelea, “Zamani, wakati Sarah hakuwepo, Lisa alikupeleka tukashangaa unakula hadi miguu ya kuku ya kukaangwa uswahilini.”
Alvin alishangaa. Je, hilo lilitokea kweli?
Chester aliongeza, "Wakati mwingine, ulimuumiza Lisa na kumpeleka hospitali katikati ya usiku."
Alvin akapigwa na mshtuko tena. Ni kweli hapo awali alikuwa amefanya jambo kama hilo kwa Lisa? Ikiwa mtu mwingine angesema hivyo, bila shaka asingeamini, lakini Chester alikuwa kama ndugu ambaye alikuwa amepitia mazuri na mabaya pamoja naye. Maneno mengi aliyosema yanapaswa kuwa ya kweli.
“Chester, mimi ni mhuni? Nimekuwaje hivi?” Alvin alishika kichwa chake mikononi mwake. Mwenendo wake wa sasa ulimpa hisia zisizojulikana.
Chester alimtazama tu na kumwambia, “Mimi nimekuwa na uhusiano na wasichana wengi siku za nyuma, na watu wa nje wananijua kama mtu asiyetulia, malaya! Kila mara nilianzisha uhusiano mpya kabla ya kukatisha mwingine. Naweza kukusaidia”
"Nipe mawazo." Alvin siku zote alikuwa mtu wa maamuzi, kwa hiyo mara chache alikuwa na mkanganyiko kama huu.
Chester alimkumbusha, “Usifanye mambo kuwa magumu. Ninamfikiria Sarah kama dada mdogo na ninamtakia furaha. Lakini kusema ukweli, ukikataa kumgusa, hiyo ni shida pia kwa sababu huwezi kuishi nao wote wawili. Isitoshe, Sarah amekuwa na wewe kwa muda mrefu, na haujamgusa hadi sasa. Lisa ni rahisi kumwacha, Sarah ni ngumu."
Alvin alikunja uso. Mwishowe, alichukua glasi ya mvinyo na kuigonganisha na ya Chester tena. Maskini Chester aliongozana naye kunywa usiku kucha.
Sura ya: 346
Alvin alilala kwa Chester hadi mchana siku iliyofuata, akaamka akiwa na kizunguzungu. Baada ya kumfwagiza Hans kupeleka nguo zake, alioga kabla ya kuelekea kwenye kampuni. Alipoona duka la madawa njiani alifikiria kitu. Kwa hiyo, alimsimamisha Hans ili aweze kushuka na kununua dawa fulani yeye mwenyewe.
Alipofika kwenye kampuni, alimuona Sarah akimsubiri ofisini kwa muda. Pia kulikuwa na kontena maridadi la chakula cha mchana lililowekwa maboksi kwenye meza.
“Alvin, nimekusubiri kwa saa moja. Nilidhani haurudi tena." Mara Sarah akamsalimia huku akitabasamu. Uso wake bado ulikuwa mwekundu na umevimba baada ya usiku mmoja, lakini aliufunika kwa kuweka nywele zake chini.
Alvin alijisikia vibaya. Alitaka kumfundisha Lisa somo jana yake usiku, lakini aliishia kulala naye badala yake. Alikuwa mpuuzi sana. “Sarah, hukuhitaji kufanya hivi. Unapaswa kupumzika nyumbani kwani wewe ni mgonjwa."
“Lakini hukurudi nyumbani jana usiku. Nilikukumbuka sana.” Sarah alimtolea macho ya kimahaba na kumuegemea kifuani.
Alvin alitazama chini usoni mwake, na ghafla, alikumbuka hisia za Lisa akiwa amejiegemeza kwenye kifua chake jana yake usiku. Moyo wake ulikuwa umejaa wakati huo, tofauti na sasa, ambapo hakuhisi chochote zaidi ya hatia. “Samahani…” Alitazama chini kwa hisia tofauti.
"Samahani zako zimetosha. Umekula? Nimetengeneza nyama choma ya nguruwe kwa ajili yako. Unataka kujaribu?" Sarah akamkabidhi vyombo.
Alvin alikuwa hajala, lakini baada ya kuonja vipande viwili tu, hakuweza kula tena. Ilikuwa ni nyama choma ya nguruwe, lakini nyama ambayo Lisa alitengeneza ilikuwa tamu na yenye harufu nzuri zaidi.
"Sarah, samahani." Alvin alichukua vipande viwili zaidi kwa kujilazimisha na kuweka uma pembeni.
Sarah alipepesa macho na kutabasamu kwa upole. “Alvin, una nini? Unaendelea kuniomba msamaha tu kila muda, kwanini?”
Alvin akaminya midomo yake myembamba. Mikono yake ilikunjamana taratibu hadi mishipa yake ikasisimka, kisha akalegea taratibu. "Si chochote."
Hakuona kwamba machoni mwake, Sarah alikuwa akitetemeka hadi seli ya mwisho. Mtazamo wa macho ya Alvin sasa hivi ulimtia hofu. Hapo ndipo alipokumbuka maneno ya Lisa. Alikuwa ametumia usingizi na hypnosis ili kuathiri akili na hisia za Alvin na kuharibu kumbukumbu zake, lakini Lisa alikuwa amemkumbusha kwamba hisia za watu zinaweza kubadilika. Ikiwa Alvin angekuwa na mabadiliko ya moyo, yote yangekwisha.
Hapana, asingeruhusu Lisa kufanikiwa. Sasa, njia nzuri ilikuwa ni kulala na Alvin haraka iwezekanavyo na kupata ujauzito wa mtoto wake.
Asingeweza kukaa tu na kungoja hivi.
•••
Jioni, Lisa alitoka kwenye lifti akiwa na vyakula alivyonunua kwenye duka kubwa na mara akasikia harufu ya moshi wa sigara. Baada ya hapo, aliona sura ndefu na nzuri kwenye mlango wake. Mwanaume huyo alikuwa amevalia suti nyeusi iliyomficha kwenye mwanga. Lisa aliduwaa macho yake yalipokutana na yake.
Wakati huo, mvulana mdogo katika nyumba ya jirani alifungua mlango ili kutoa takataka. Aliinua kichwa chake na kumkonyeza Lisa huku akitabasamu. “Dada, hatimaye umerudi. Mpenzi wako amekuwa akikungoja hapa kwa saa moja. Nilimwona niliporudi kutoka shuleni.”
“Yeye si mpenzi wangu, uwe na adabu kijana.” Lisa alisema kwa aibu.
“Hakuna haja ya kuwa na aibu. Niliwaona nyinyi mkilala koridoni mara ya mwisho.” Kijana alicheka na kufunga mlango haraka baada ya kumaliza kuongea.
Kupitia mlangoni, Lisa alimsikia mama akimkemea mwanae. “Mtoto wewe, nilikuambia utoe takataka au ukachunguze wakubwa zako? ujinga gani?”
“Mama, wewe hujui. Nilipokuwa naenda shule jana asubuhi, nilishuka na yule mtu kwenye lifti. Kuna Aunty alisema yeye ndiye mtu tajiri kabisa Kenya nzima. Lakini kwanini anakuwa na uhusiano kama huu?”
Uso wa Alvin ulishuka. Mashavu ya Lisa nayo yalikuwa na joto kidogo huku akiutoa ufunguo na kuufungua mlango. "Unafanya nini hapa? Kazi kuja kuniaibisha tu"
Alvin akafoka, “Hutaki kunikaribisha?”
Lisa alimtazama na kumdharau. “Siku hizi umezua mtindo mbaya sana. Kila unapokuja hapa, unataka nilale na wewe. Samahani, lakini nimechoka sana, na sitaki tena hata kuguswa na wewe.”
“Siko hapa kwa ajili hiyo leo.” Alvin alikasirishwa na maneno yake tena. "Inatosha. Usinifanye nijisikie kuwa mimi ni mkorofi.”
"Lakini wewe ni mkrofi kweli." Lisa alimtazama kwa macho ya hasira, na mashavu yake yalitoka kidogo. Alikasirika waziwazi, lakini alionekana mrembo pia.
Alvin moyo ulimsisimka tena, akashusha sauti yake. “Unajua kuna mtu aliniweka dawa siku hiyo. Kuhusu jana… Jana ni kwa sababu ulinikasirisha.”
Lisa alijibu huku akitabasamu. “Hivyo ndivyo unavyofanya ninapokukera. Kwa hiyo huwa unafanya vivyo hivyo kwa wanawake wengine wanapokukasirisha?”
“Unafikiri mimi ni mpuuzi?” Alvin alisikika kuwa na hasira kidogo.
Lisa alijiwazia kitu lakini hakusema. Midomo yake ilijikunja kidogo, na macho yake mazuri yalifichua mng'ao wa ajabu na matarajio kana kwamba kulikuwa na sababu zingine. Hata sauti yake ikawa ya kutaniana kidogo. "Basi, kwa nini unifanyie hivyo mimi tu?"
Alvin alimvutia macho yake, na moyo wake ukapata kigugumizi. Ghafla akapata hamu ya kumkumbatia tena. Hata hivyo, sura ya upole ya Sarah ikamtokea ghafla akilini mwake. Akatoa boksi mbili za dawa mfukoni na kumpatia Lisa. "Boksi moja ni la dawa za maumivu, na lingine ni la uzazi wa mpango. Kumbuka kunywa kwa wakati."
Lisa akatazama juu. Macho yake mazuri yalitetemeka kabla ya machozi kumtoka kwa hasira. “Alvin Kimaro, nini maana ya hili? Ina maana unaogopa kwamba nitapata mimba na kuharibu uhusiano wako na Sarah? Kama ni hivyo, ulikuwa unategemea nini uliponilazimisha kulala na wewe?”
Alvin aliufanya moyo wake kuwa mgumu na kusema. “Sitakugusa tena. Chukua dawa. Jana na juzi ilikuwa ajali tu, haitakaa ijirudie tena.”
“Alvin Kimaro, wewe si mwanaume. Ondoka mbele yangu.” Lisa alimsukuma nje huku machozi yakimtoka kwenye kona za macho yake.
Alvin alipomuona analia alijisikia vibaya. Tangu aliporudi, alikuwa mkali na jeuri isipokuwa kitandani, lakini hakuwahi kumuona akilia. Mdomo wake ulisogea bila kujijua na kusema, “Lisa, sikuchukii tena.”
Lisa alicheka na kudhihirisha sura ya huzuni na kejeli. “Hiyo ina maana gani? Hunichukii, ila sasa unanidharau?"
“Hapana, lakini kunywa dawa haraka. Nitaondoka baada ya wewe kunywa.” Alvin alijua kuwa alijilazimisha kufanya hivyo, lakini Sarah alikuwa amemngoja kwa zaidi ya miaka kumi. Hakuweza kumwangusha tena.
“Sawa, nitakunywa. Nitakunywa sasa hivi.” Lisa aligeuka huku na kule kwa mshangao. Alifungua kidonge na kubugia ndani ya mdomo wake, na kuvirusha vingine kwenye uso wa Alvin. Alipiga kelele, "Haya nimemeza, nadhani ulisharidhika. Unaweza kupotea sasa?" Alimsukuma nje na kuufunga mlango kwa nguvu.
Alvin alijisikia vibaya, akasimama mlangoni kwa muda mrefu kabla ya kuondoka akiwa amekata tamaa.
Bila kujua, Lisa alikuwa ameshakausha machozi yake na kuandaa chakula cha jioni muda si mrefu baada ya Alvin kuondoka.....ITAENDELEA....
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
