JINA LA SIMULIZI............................LISA

AUTHOR...........................JOMBA WAJO

SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY

WHATSAPP...........................0628924768

SEHEMU YA................................343-344


Sura ya: 343


Logan alilalamika. “Bosi, Sarah amekuwa na wanaume wengi sana. Sidhani kama ningeweza kustahimili ikiwa mimi ningekuwa mwanamume wake, kwa hivyo inashangaza sana kwamba Alvin Kimaro anaweza kumchukua. Lakini Sarah ni mjanja sana. Siku hizi muda wake mwingi anautumia kujivinjari na Hisan kwa upande mmoja na anajua pia kudili na Alvin kwa upande mwingine. Lazima atakuwa na akili nyingi sana."


“Sawa. Inatosha." Lisa alikunja uso.


“Usikasirike sana. Ni mpuuzi tu wa kuchukiza.” Logan alifikiri kwamba Lisa alikuwa amekasirika.


“Unawaza kupita kiasi. Ulichosema kilinifanya nichukie tangu yule fisadi aliponibusu jana usiku. Nenda uninunulie vidonge vya kuzuia mimba…”

Lisa akamtupia pesa taslimu mara moja. Logan akapepesa macho na kujiweka mbali naye.


"Unafanya nini?" Lisa aliuliza.


“Hapana… Bosi, nilisikia kwamba maisha ya faragha ya Hisan ni ya fujo sana. Ana wanawake wengi wagonjwa huko. Hisan analala na Sarah, Sarah analala na Alvin, na Alvin anafuatana nawe…” Logan alikuwa na mchanganyiko wa hisia. “Unapaswa kuwa makini.”


Lisa karibu akose nguvu. Ikiwa sio kwa sababu alikuwa na wasiwasi juu ya Joel kumngojea, angeenda hospitalini mara moja kuchunguzwa.

“Utanipeleka hospitali nikachunguzwe baada ya kumaliza kazi yetu.”


Dakika arobaini baadaye, gari likafika kwenye jumba la kifahari la Ngosha. Lisa alipoingia, katibu wa Joel, Walter Maliga, alikuwa akiripoti hali ya kampuni kwa Joel.


"Sifa ya kampuni imekuwa ikishuka hivi karibuni, na Kampuni ya Campos imesitisha miradi mingi na Kampuni ya Ngosha. Wanahisa wana wasiwasi sana na wanasitasita ikiwa wamrejeshe Damien na binti yake kwenye kampuni.”


Joel alidhihaki. "Je, baba na binti huyo wanawezaje kujitokeza kwenye kampuni. Hawaogopi wengine kuwakosoa na kuwacheka?”


Walter alitabasamu vibaya. “Sifahamu kwa kweli. Mimi ni katibu tu.”


"Ndio hivyo? Sidhani kama wewe ni katibu tu.” Lisa aliingia huku akiwa na tabasamu la hasira na macho makali sana kiasi cha kuwafanya watu waogope. Hata Joel alishangaa kidogo. Ilikuwa ni siku chache tu tangu walipokutana mara ya mwisho, lakini binti yake sasa alikuwa na utisho wa hali ya juu zaidi.


"Binti mkubwa, sielewi unachosema." Walter alitabasamu huku akimtazama kijana aliyekuwa nyuma ya Lisa.


“Hellow!” Logan aliita na papo hapo akamzuia Walter kwa kumfunga kamba.


"Wewe ni nani? Niache.” Akiwa mwishoni mwa akili yake, Walter alijitahidi kwa nguvu zake zote. "Binti mkubwa, unafanya nini?"


Joel alikohoa kwenye ngumi yake na kusema kwa kukata tamaa, “Walter, ni jinsi gani ulivyo mkarimu? Umekuwa ukiniwekea sumu kwenye milo yangu kila siku. Na kwa miaka hii miwili iliyopita, umevujisha ratiba yangu yote ya kibinafsi, kwa hivyo haijalishi ni hospitali gani ninaenda kwa uchunguzi, umeweza kumlipa daktari mapema. Niambie, ni nani aliyekuhonga?”


“Bwana Ngosha, sijui unazungumzia nini.” Walter alijifanya mtulivu na kusema kwa uso wa uchungu, “Nimekuwa nawe kwa miaka kumi, na nimekuwa mwaminifu kwako kila wakati.”


"Hiyo ni sawa. Miaka kumi imepita.” Lisa aliitikia kwa kichwa.

"Ingawa mshahara wa katibu ni shilingi za Kenya elfu thelathini tu kwa mwezi, baba yangu huwa anakupa mara tatu zaidi pamoja na milioni kama bonasi yako ya mwisho wa mwaka. Pia alikupa nyumba, gari, na kuwapeleka watoto wako wawili katika shule bora zaidi, lakini hivi ndivyo unavyomlipa? Walter, unaweza kukataa, lakini tunazo kumbukumbu za wewe kumpa baba sumu. Labda hujui, lakini tumeweka kamera zilizofichwa kila kona ya nyumba.”


Joel kisha akatoa kamera ndogo ya uchunguzi kutoka kwenye sanduku la kurekodia lililokuwa sebuleni. Uso wa Walter ulipauka mara moja kwa kukosa la kusema.


“Nitakupa nafasi nyingine. Nani alikuelekeza?” Macho mazuri ya Lisa yalikuwa makali.


“Hapana… hakuna aliyeniagiza. Nilifanya mwenyewe,” Walter aliguna na kutikisa kichwa. “Namchukia Mwenyekiti Ngosha. Mimi… nachukia kwamba yeye ni mbahili sana na mshahara wake ni mdogo.”


“Huna elimu yoyote, na ninakulipa mshahara sawa na mtu mwenye degree, na bado unasema ni kidogo sana?” Joel alikasirika sana hadi akakohoa huku akijishika kifua.


“Baba usihangaike naye.” Lisa alimtuliza baba yake. “Lazima uelewe kwamba watu wengine watakuwa na njaa zaidi kadri unavyowalisha. Ni kawaida tu kwamba mwanaume hawezi kuridhika kamwe.”


Lisa aligeuka na kumwambia Logan, “Mlete ndani. Nitamuacha mikononi mwako.”


“Wewe… utanifanya nini?” Walter alimtazama Logan aliyekuwa akimkaribia na kulalamika sana, lakini, Logan alimvutia tu chumbani, akimpuuza. Kwa muda mfupi, vilio vya huzuni na vya kikatili vilisikika.


Joel alitetemeka huku akisikiliza. “Lisa, wewe…”


“Baba, usipomfundisha somo, atakutumia vibaya kila wakati.” Kwa tabasamu, Lisa alimsaidia kuketi.


“Hapana, itabidi apelekwe kituo cha polisi baadaye, naogopa…”


“Usijali. Hakuna atakayejua kuhusu hilo,” Lisa alisema. "Nilimwambia Logan tu atumie mbinu rahisi lakini hatari. Atahisi kama amechomwa na sindano elfu moja, na maumivu yake ni mabaya zaidi kuliko kifo, lakini hawezi kufa. Kadiri anavyohangaika ndivyo sindano zinavyopenya ndani zaidi, na ndivyo itakavyokuwa chungu zaidi.”


Joel alishindwa kujizuia kutetemeka. “Umejifunzia wapi ukatili wa aina hii? Na yule kijana…”


“Baba, hatimaye nimeelewa baada ya miaka hii yote. Tunaweza tu kujilinda ikiwa hatuna huruma.” Lisa alitabasamu na kumtazama. "Tunaweza kuwalipa watu mema kwa mema, lakini hakuna haja ya kuwa na huruma kwa watu wasio na shukrani."


“Uko sawa.” Joel alipoona jinsi alivyokuwa, alisikitika tena kwa jinsi alivyobadilika. Hata hivyo, hilo lilieleweka. Alikuwa ameteseka sana, na kama baba yake, alipaswa kuwa kama yeye pia.


Nusu saa baadaye, Logan alimkokota Walter aliyekuwa kachoka sana.


“Umefikiria vizuri na upo tayari kusema?” Lisa alimuuliza wakati akipitia kitu kwenye laptop ya baba yake. “Nimeangalia akaunti yako ya benki. Tangu miaka miwili iliyopita, akaunti yako imekuwa ikiongezeka kwa milioni 10 za ziada kila mwaka. Si hivyo tu lakini kabla ya hapo, akaunti yako imekuwa na ziada ya elfu 100, na kisha elfu 200, na kisha elfu 300… Namba inazidi kuwa kubwa zaidi. Kama nipo sahihi, ningesema umekuwa ukifuja pesa, lakini kuna mtu aligundua na kukuamuru kumpa baba yangu sumu ili akufichie siri hii. Niko sahihi?” Lisa aliinama chini na kumshangaa.


"Y-ndiyo." Walter alimtazama kama shetani. "Ilikuwa Nina Mahewa. Hakutarajia Bwana Ngosha kama angenusurika kwenye ajali ya gari, hivyo aliniambia niweke sumu ya kumuua polepole kwenye milo yake. Maadamu Bwana Ngosha angekuwa amekufa, Bi… Bi. Ngosha angeweza kuchukua kampuni ya Ngosha kwa haki.”


“Huyo b*tch. Mwanamke mkatili huyo.” Mwili wa Joel ulitetemeka kwa hasira. “Nimeishi kwa miaka mingi na kuona watu wengi waovu, lakini sijawahi kuona mtu katili kama yeye.”


"Baba, wewe tulia." Lisa akatikisa kichwa kwa utulivu na kumtazama Walter, akisema, “Nina kazi kwa ajili yako. Kutana na Nina faragha na upate ushahidi kwamba alikuambia umtilie baba yangu sumu.”


Walter alinyauka mara moja.


“Najua Nina ana ushahidi wa ubadhirifu wako, lakini uliibia kampuni ya Ngosha. Ilimradi Mwenyekiti Ngosha hatafuatilia, ushahidi utakuwa hauna maana.”


Lisa akainama mbele yake. Ingawa sauti yake ilikuwa ya upole, ilikuwa ni ile ambayo inaweza kuwafanya watu waogope.


“Ikiwa hutashirikiana nasi, tutakushitaki moja kwa moja polisi na kukagua akaunti haramu za kampuni kwa miaka mingi. Kwa kuwa utashtakiwa kwa sumu na ubadhirifu, ninahofia hutaweza kutoka jela maisha yako yote. Fikiria mke wako na watoto wako wawili.”


Macho ya Walter yalitetemeka kidogo.


Lisa aliendelea kusukuma maneno magumu. “Ngoja nikukumbushe kuwa mkeo ana miaka thelathini. Ikiwa utaenda gerezani kwa muda mrefu sana, anaweza kuchukua pesa zako na kuolewa tena. Kufikia wakati huo, watoto hawatakuwa wako tena. Huoni kwamba hiyo ni sawa na kupoteza maisha yako?”


Sura ya: 344


“Sawa, nitakusaidia kupata ushahidi,” Walter alisema huku akiwa amezidiwa na majuto.


"Kweli, lakini lazima ule kitu." Lisa akatoa kidonge. “Ni lazima tuwe waangalifu iwapo utatusaliti. Nitakupa dawa mara tu utakapomaliza kazi yako.”


Logan alizungumza, “Dawa hii ina sumu kali, na itakuua ikiwa hautapata dawa ya kuipindua ndani ya wiki moja. Bila shaka, daktari anaweza kutibu, lakini itachukua miezi. Hutadumu kwa muda mrefu hivyo.”


Walter aliitazama sura nzuri ya Lisa ambayo ilikuwa ya kutisha kwa wakati huo. “Sitakusaliti. Wiki moja inatosha kwangu kupata ushahidi.” Walter alikaza mishipa yake na kumeza dawa hiyo.


Baada ya zoezi hilo kuisha, Lisa aliongozana na Joel kwenye chakula cha jioni kana kwamba hakuna kilichotokea.


"Lisa, ulipata wapi dawa kama hiyo?" Joel aliuliza huku akiwa amechanganyikiwa. "Umepitia nini katika miaka yako nje ya nchi?" "Baba, nimekutana na marafiki wapya wachache tu na kujifunza ujuzi mpya." Lisa alicheza.


Alipoona binti yake hataki kumwambia, pia hakuuliza sana. “Lisa, unafanya kazi nzuri na Mawenzi. Ungependa kuchukua pia nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Ngosha? Nadhani uwezo unao.”


“Baba, wewe bado kijana. Una miaka hamsini tu. Ni bora ukiisimamia. Sitaki kusimamia makampuni mengi sana. Inachosha sana akili.” Lisa alikataa.



“Basi, kwanini usirudi nyumbani? Baba yuko… mpweke akiishi hapa peke yake.” Joel akahema.


“Ni mbali sana hapa, hivyo pia si rahisi. Kwanini usirudi kwenye makazi ya zamani na kuishi na Bibi na Babu? Lisa alimkumbusha. "Lazima wahisi kuchoka kwa kukaa katika nyumba kubwa kama hiyo pia."


"Hiyo ni kweli." Joel alishawishiwa.


Baada ya chakula cha jioni, Joel hakufurahi alipojua kwamba Lisa alikuwa karibu kuondoka. "Unakuja mara moja tu kwa wiki, na unaondoka mara tu baada ya chakula cha jioni. Hapana, ondoka kesho badala yake.”


“Baba, bado nina jambo la kufanya baadaye. Nitarudi kesho kukuweka sawa.”


Mara baada ya Lisa kuondoka kwa ngosha, Logan alimpeleka hospitalini. Baada ya kumuacha Lisa hospitali, Logan aliondoka kwenda kuendelea kumchunguza Hisan.

•••

8:30 Usiku.


Baada ya majeraha ya Alvin kuvishwa, alitoka nje ya idara ya andrology kwa wakati na kumuona Lisa akishuka kutoka kwenye escalator.


"Lisa Jones, simama hapo hapo." Hasira iliyokuwa ikimfukuta kwa muda mrefu ikampanda tena. Alvin alipuuza kabisa maumivu hayo huku akipiga hatua kwenda kumshika. “Umefika kwa wakati tu. Nilitaka kukufuata.”


Lisa akapigwa na butwaa. Mtu huyo aligeuka kuwa mzimu unaomsumbua? Alimwona kila mahali alipoenda. "Umekuja hapa kwa andrologist tena?"


"Nyamaza." Alvin alikasirika hadi akalaani. Hakukuwa tena na ule utulivu wake wa kawaida. Aligundua kuwa tangu Lisa arudi, alikuwa akipandwa na hasira kila siku. Alitilia shaka kama angeweza kuishi zaidi ya miaka arobaini.


"Umeniumiza sana mchana."


"Kwa hiyo?" Lisa alimtazama. "Nani angefikiria? Unaonekana mkubwa na mrefu. Sikutarajia kwamba eneo lako fulani lingekuwa dhaifu sana. Ni tabu tu.”


Alvin alikasirika. “Unataka nife bila mtoto?”


Lisa alikcheka kama mazuri. “Usijali. Iwapo utaishia kukosa mtoto, nitawajibika.”


Alvin alicheka kwa kejeli. “Unaonekana unalazimisha kuwa na majukumu kwangu, sivyo? Nikikaa na mwanamke mbaya kama wewe, nitakosa furaha tu."


Lisa alipepesa macho na kusema kwa uso usio na furaha wala huzuni, “Nadhani umenielewa vibaya. Niliposema nitawajibika, simaanishi kwamba nitatunza furaha yako ya maisha yote. Ninachomaanisha ni… Nitampatia Sarah mwanamume tajiri na wa kipekee wa kumfurahisha maisha yake yote. Nadhani ikiwa huwezi kupata watoto, mtu ambaye utamsumbua zaidi atakuwa yeye, sivyo?”


Alvin alishusha pumzi ndefu huku uso wake ukibadilika na kuwa mweusi kisha kwa hasira. Hans, ambaye alikuwa akisikiliza kando, karibu apige magoti mbele ya Lisa na kumsihi aache mara moja kumkasirisha bosi wake. Alikuwa amekaa na Alvin kwa muda mrefu, lakini ilikuwa ni mara ya kwanza kumuona Alvin akiwa na hasira kiasi kile.


"Kwani nimesema chochote kibaya?" Kuangalia sura yake ya hatari, Lisa kwa woga alipiga hatua mbili nyuma. “Oh, ni kweli, nilisahau. Hisia za Sarah kwako ni za kina kama bahari. Hata ukipungukiwa na nguvu, hatajali.”


"Funga mdomo wako," Alvin alimfokea. Hakuweza kujizuia tena.

Vurugu hizo ghafla zilivutia watu wengi kwenye hospitali yenye shughuli nyingi, ambapo watu walikuwa wakiingia na kutoka.


“Tunaondoka sasa hivi!” Alimshika na kuusukuma mlango mzito wa escalator kabla hawajaingia ndani.


“Unafanya nini? bado nasubiri majibu yangu hapa.” Lisa alimfokea.


“Majibu gani? Kwani wewe ni mgonjwa?” Hapo ndipo Alvin alipoona karatasi mikononi mwake. Aliinyakua na kuona maneno ya 'HIV Screening Test' juu yake, na masikio yake yakasisimka.


“Kwanini unaangalia HIV? Wewe… Je, umewahi kujihusisha na wagonjwa wa VVU?” Ubongo wa Alvin ulikuwa karibu kulipuka. “Hii ilikuwa lini? Usiniambie ilikuwa kabla ya leo.”


"Ndio, ilikuwa kabla ya leo." Lisa alitikisa kichwa huku akitazama kwa hasira.

"Lisa Jones, unawezaje kuwa mchafu kiasi hiki?" Alvin aliutupa mkono wake kwa nguvu na kumfokea Hans nje. “Fanya haraka

uniletee dawa ya kuua vijidudu.”


"Hakuna haja ya hilo," Lisa alisema kwa sura isiyo ya kawaida. “Mtu aliyenifanya nipime ni wewe. Ulifanya hivyo pamoja nami jana usiku, na nilipata wasiwasi. Niliogopa kuambukizwa kitu, kwa hivyo nilikuja hapa ili kuchunguzwa."


Vidole vya Alvin vilitetemeka, na kichwani kwake akahisi kupandisha mashetani. Alimtazama kwa macho yenye hasira kali na kumuuliza neno baada ya neno, “Unamaanisha… Unaogopa nitakuambukiza ugonjwa?”


"Najua ... kusema hii inaweza kukuumiza, lakini ... ni kwa amani yangu ya akili." Lisa alipiga hatua moja baada ya kuona kuwa hasira yake ilikuwa karibu kulipuka.


“Haha.” Alvin alicheka. Uso wake mzuri uligeuka kuwa kama shetani mbaya. "Lisa Jones, umenikera sana wakati huu." Kisha, akamtupa begani na kutoka nje ya hospitali.

Hans akawatazama kimya kimya kisha akatazama dawa alizotumwa na Alvin mkononi mwake. Alimuombea Lisa kimyakimya.


“Alvin Kimaro, niache.” Lisa alimpiga kofi kali la mgongoni.


Hata hivyo, Alvin alijifanya kana kwamba hakumsikia. Akambeba hadi sehemu ya maegesho ya magari, akafungua mlango wa gari na kumtupa ndani.


“Alvin, unafanya nini?” Lisa aliinuka, lakini Alvin alimkandamiza begani kwa mkono mmoja na kumpasua shati lake kwa mkono mwingine.


Lisa alipigwa na butwaa. “Alvin, huna akili. Je, humpendi Sarah? Una uhakika unataka kumsaliti tena?"

Wakati huo Alvin alikuwa amekasirika sana na hakumsikiliza hata kidogo. “Si ulisema unanichukia kwa kuwa mchafu? Unahisi nimekuambukiza maradhi, sivyo? Basi acha nikuambukize zaidi.”........ITAENDELEA.....

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.