JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................347-348
Sura ya: 347
Mara baada ya kula, Pamela alimpigia simu kutoka Marekani. “Mpango wako unaendeleaje?”
“Kila kitu kipo sawa. Ninachukua hatua moja baada ya nyingine, lakini ninahisi kama nimekuwa nikiforce sana mambo hivi karibuni. Sarah amekuwa kimya sana hivi karibuni, na Damien na Melanie wamekuwa kimya sana kwa sasa.” Lisa alijimiminia kikombe cha mtindi, akaongeza matunda na kukoroga kwa kijiko.
"Bado sijaridhika na wazo la kuwa peke yako huko." Pamela alilalamika.
"Logan yuko hapa pia."
"Hiyo ni kweli. Pia kuna Kelvin Joseph, na Jack. Una mashujaa wengi sana." Pamela alicheka na ghafla akanong'ona, "Osher Corporation imenitumia barua ya kuajiriwa. Walinipa dola milioni 30 kwa ajili ya ile proposal yangu ya kutengeneza bidhaa ya kuzuia kuzeeka niliyoiandaa kabla hawajanitimua.”
Lisa alitabasamu kwa kucheza. “Hilo linavutia. Forrest alikuwa sahihi aliposema Rodney hataweza kukufungia utakapokuwa na nguvu. Sema, ikiwa wangegundua kwamba mgunduzi wa vipodozi vya ‘farasi mweusi’ ndiye waliyempiga marufuku na kumdharau hapo awali, maneno yao yangependeza.”
"Nimekuwa nikitarajia siku hii kwa muda mrefu," Pamela alisema katika hali nzuri.
“Uko tayari kurudi Osher?” Lisa aliuliza.
“Hapana, nimekataa ofa yao, lakini nimekubali kufanya mazungumzo kwa ajili ya SE Group ya Tanzania na nitarudi mwishoni mwa mwezi. Unataka nikuletee watoto wako wawili? Wanakukumbuka sana.”
“Hakika. Nimewamiss pia, lakini hawataweza kukaa pamoja na mimi. Itabidi ukae nao wewe na useme tu kwamba hao ni watoto wa kaka yako.”
“Sawa.” Pamela aliafiki.
•••
Saa 8:00 usiku, Alvin alikuwa amerudi kwenye jumba lake la kifahari, lakini Sarah alikuwa bado hajarudi. Kwa hiyo, alimpigia simu, na akasema kwamba alikuwa akinunua vitu na marafiki.
Saa 11:00 usiku, Alvin alipokuwa akifanya kazi katika chumba chake cha kusomea, ghafla akapigiwa simu na Rodney.
“Alvin, njoo haraka. Sarah alilewa. Njoo umchukue.”
"Si alienda shopping na marafiki?" Alvin alikunja uso.
Rodney akamrukia kwa hasira. “Shopping ya mat*ko yako? Aliogopa kwamba ungekuwa katika hali mbaya, kwa hiyo akaenda kunywa na Joan Halua na wengine. Sijui alikunywa kiasi gani, lakini Joan alinipigia simu, na mimi nikaja hapa fasta.”
“Sawa, nitamfuata mara moja.” Alvin alikimbia haraka kwenye baa, ambapo Joanne, Rodney, na Maya walikuwapo. Sarah alikuwa amezidiwa na ulevi kwenye sofa, akiwa bado ameshika chupa ya whisky mikononi mwake. Aliendelea kuipeleka mdomoni japo alikuwa amelewa kabisa.
"Nini kimetokea?" Macho makali ya Alvin yalipita kwa Joan na Maya.
Joan alishindwa cha kusema. “Hata mimi sifahamu sana. Alisema tu kwamba alikuwa katika hali mbaya na akaniita tunywe. Alikunywa na kunywa hadi akazima, na amekuwa akilia tangu wakati huo.”
“Alvin, nini kinaendelea?” Rodney alimvuta Alvin pembeni. “Sijawahi kumuona Sarah akiwa na maumivu makali hivyo. Tayari ana huzuni sana kwa kuwapoteza wazazi wake. Ni sisi tu ambao tumebaki kama ndugu wake. Ikiwa umemkosea, sitakuacha.”
“Sawa, ngoja nimpeleke nyumbani.” Alvin alimbeba Sarah, na Maya akafuatana pamoja nao.
Alipotaka kumweka Sarah kwenye gari, ghafla akanyoosha mikono yake na kuizungusha shingoni mwake. Akiwa katika kilio chake, alisema, “Usiniache, Alvinic. Usiniache. Najua mimi ni mchafu, na ndiyo maana hutaki kunigusa.”
"Hapana. Sio vile unavyofikiria.” Moyo wa Alvin ulishituka.
“Si lazima ueleze. Naelewa." Aliziba mdomo wake. “Kwa kweli, najua umelala kwa Lisa kwa muda wa siku mbili zilizopita. Ulinidanganya, ukisema kwamba ulienda kwa safari ya kikazi, lakini ni sawa. Ni kosa langu kwa sababu siwezi kukuridhisha. Sijali kuwa mpenzi wa aibu milele maadamu una furaha. Haijalishi ilimradi nibaki pembeni yako na kukuona kila siku nikifumbua macho yangu. Nakupenda. Ninawezaje kukupenda zaidi? Nilipokutana nawe kwa mara ya kwanza wakati huo, nilikupenda sana. Kama hutanioa, naweza kufa kwa majuto.”
Sarah alilala huku akigugumia mikononi mwake.
Maya hakuweza kujizuia kusema, “Bwana Mkubwa, ulipomdanganya Bi Njau kwamba ulikuwa na safari ya kikazi jana usiku, kwa kweli alianguka na kulia. Lakini aliniambia nisikufahamishe. Alikuwa tayari kuvumilia kila kitu peke yake. Hata alisema kwamba hajali Lisa kukaa karibu nawe.”
"Inatosha." Alvin alikunja ngumi. Kulikuwa na dokezo la dhamira kuu machoni pake. "Nitapanga harusi yetu mwezi ujao."
"Hiyo ni sawa, lakini ... bado hamjaachana na Lisa, sawa?"
“Nitapata uthibitisho wa talaka kesho,” Alvin alijibu bila kujali.
•••
Siku inayofuata. 8:00 asubuhi. Karen Estate.
Lisa alikuwa akiandaa kifungua kinywa aliposikia mlango ukigongwa kwa haraka. Alipofungua mlango, aliona watu kadhaa wamesimama pale. Kulikuwa na Alvin, Hans, Maya, na washiriki wawili wa ONA ambao alikuwa amekutana nao hapo awali.
“Niwasaidie nini?” Lisa alishusha pumzi ndefu na kuvua apron yake. Macho yake yalikuwa yamemtoka mpaka kiwango cha mwisho kabisa.
Maya alimtazama Lisa bila huruma kabla ya kusema kwa ujasiri, "Bwana Mkubwa yuko hapa kukutaka utie sahihi hati za talaka."
Lisa alikodoa macho na kuhamishia macho yake ya kukata tamaa kwa Alvin. "Bado umeamua kunitaliki, huh?"
“Kwani nimewahi kusema kwamba sitakupa talaka?” Alvin alimwambia kijeuri na kumgeuzia Hans macho.
Akiwa hoi, Hans akatoa makubaliano ya talaka na kumkabidhi. "Tafadhali saini hii Bi. Jones."
Lisa alizirarua zile karatasi baada ya kuzipokea. “Sitatia saini hii. Alvin, ukithubutu kunilazimisha, nitamuweka wazi Sarah na rangi zako halisi.”
"Kachukueni cheti cha ndoa!" Alvin aliwatazama wale wanachama wa ONA, na baadaye wakaingia ndani kupekua droo.
“Alvin, unafanya nini?” Lisa akaruka kwa hasira.
"Sitakuacha uharibu sifa ya Sarah." Yale maneno yaliyotoka kwenye midomo maridadi ya Alvin yalimkatisha tamaa. "Nipe cheti cha ndoa kwa hiari yako."
"Sitakupa." Lisa akarudi nyuma.
Alvin alishika mkono wake na kumpiga Maya macho. “Mchape.”
Baada ya kungoja wakati huu kwa muda mrefu, Maya alikimbia mara moja kuelekea Lisa. Lisa alimpiga teke, lakini Alvin kisha akawaamuru wanachama wote wa ONA wamkandamize Lisa sakafuni.
“Alvin, wewe si binadamu. Mimi ni nani kwako? Unaponihitaji, unanitumia. Usiponihitaji unanitupa kana kwamba mimi ni tambala la deki?”
Haijalishi Lisa alikuwa na nguvu kiasi gani, asingeweza kuwashinda mabwana hao peke yake. Alitetemeka kwa hasira, na macho yake yakawa mekundu kwa hasira.
Alvin aligeuza macho yake bila kuhangaika kumwangalia Lisa. Aligeuka na kumwambia Maya, “Kitafute cheti na umlazimishe kutia sahihi. Nitasubiri nje.” Pamoja na hayo, akatoka nje.
“Sawa.” Maya alifurahi. Alikuwa ameshikilia kinyongo dhidi ya Lisa kwa muda mrefu.
Alinyoosha mkono wake na kujifanya kumpiga ngumi. Alivuta hata sweta ya Lisa iliyofumwa, akifunua nyuzi zake nyembamba. Kwa kuwa Lisa alibanwa sakafuni, sehemu kubwa ya mwili wake ilifunuliwa.
Kwa kuwa pembeni yake kulikuwa na wanaume wachache, Lisa hakuwa na jeuri yoyote ya kumfanyia Maya. Aliishia kuinua kichwa chake kwa unyonge na kukaripia, “wewe…”
Kabla hajamaliza sentensi yake, Maya alifunika mdomo wake. Milio ya makofi tu ndiyo ilisikika.
Sura ya: 348
Maya alikuwa na wasiwasi kwamba Alvin angeingia, kwa hiyo alitabasamu haraka na kusema, “Bi Jones, usipoteze pumzi yako kwa kunikaripia. Nahitaji tu kupata cheti cha ndoa.”
Maya alipokuwa akizungumza, alipeleka mkono wake kwenye suruali ya jeans ya Lisa na kusema, “Utatoa, hutoi?”
Mara baada ya kusema hivyo, alivuta suruali ya Lisa chini, na wanaume wawili wa ONA wakafungua macho yao. Baada ya yote, mikunjo ya Lisa ilionekana kuvutia sana.
Macho ya Lisa yalikuwa mekundu kwa hasira. Alijitahidi kumwondoa Maya, lakini mikono ya watu hao ilikuwa na nguvu kama chuma.
Kadiri Lisa alivyokuwa na aibu, ndivyo Maya alivyozidi kuridhika. Maya kisha akamnong’oneza Lisa sikioni, “Usiogope. Nitakuvua nguo zako zote. Unafurahia kujionyesha kwa wanaume, sivyo? Nitawaruhusu waangalie vizuri mwili wako, basi.” Maya alikuwa karibu kumvua nguo.
Hans hakuweza kustahimili tabia ya Maya tena, alisema, "Maya, umetumwa kumvua nguo au kupekua cheti?"
Maya alimkasirikia Hans alipogundua mpango wake wa kushughulika na Lisa ulikatizwa. Alijifanya kuhisi uchungu na kujibu, “Anaweza kuwa ameficha cheti ndani ya mwili wake. Ikiwa unafikiri ninafanya kazi mbaya, unaweza kuja kuchukua nafasi, Bosi uchwara wewe!”
Hans alichomwa na maneno yake ya kejeli. Alijua wazi kuwa Lisa ni mwanamke wa Alvin, na Alvin asingemruhusu amguse. Wakati huo, sauti za nyayo zilitoka nje ya mlango. Maya alifunga zipu ya jeans ya Lisa kwa haraka huku Alvin akiingia na kumuuliza kwa sauti nzito, “Kuna nini?”
Maya alisimama kwa haraka na kujibu mara moja, “Bwana Mkubwa, nilipokuwa nikimsachi Lisa, nilivua jeans yake ili kuangalia kama cheti cha ndoa kilikuwa ndani. Lakini Hans alinirukia kwa kuvua sweta yake.”
Lisa alidhihaki, “Si ulikuwa unapanga kunivua nguo? Umenifunika hata mdomo wangu.”
Maya alikunja uso wake na kusema kwa hasira, “Bi Jones, najua hunipendi kwa sababu namlinda Bi Njau, lakini kila mara mimi hufanya maamuzi yangu kwa haki. Ninatekeleza tu maagizo ya Bwana Mkubwa. Baada ya yote, wewe ni mke wake. Sitakuwa na ujasiri wa kukuchukiza kamwe.”
Lisa alichukizwa sana na maneno yake ya kinafiki kiasi kwamba alihisi kutaka kuropoka. “Umejidhihirisha kweli kuwa wewe ni mlinzi wa Sarah.
Umemudu unafiki wake.”
"Nyamaza. Usithubutu kumtukana Sarah tena. Vinginevyo, nitamwambia kweli akuvue nguo.” Alvin alifoka.
Lisa aliganda na macho yake kuingiwa giza taratibu. Ni kana kwamba mwanga machoni mwake ulikuwa umetoweka na akaingia katika hali ya kukata tamaa.
Hans hakuweza tena kuvumilia hali hiyo. “Bwana Mkubwa, umeelewa vibaya…”
“Inatosha. Kuna faida gani ya mimi kuwaleta nyie hapa? Mmebaki kubishana tu. Hamjasuluhisha chochote tangu mlipoingia.” Moyoni, Alvin alichanganyikiwa na jinsi Lisa alivyokuwa mkorofi, lakini wakati huohuo aliguswa na unyonge wake pale sakafuni.
Uso wa Hans uligeuka baada ya kukosolewa.
Lisa alilala sakafuni, akionekana kuchoka. “Sawa. Niachie basi. Nitatia sahihi hati za talaka na kukupa cheti cha ndoa. Siwezi kukushinda hata hivyo. Mimi sio mkatili kama wewe, Alvin. Sikuwezi hata kidogo.”
"Nawezaje kuamini maneno yako?" Alvin alikuwa na shaka. "Ulinidanganya mara ya mwisho pia, na ukaishia kunipiga teke."
“Sitakupiga teke muda huu. Kwa kuwa umekuja na jeshi kubwa, nitawezaje kuwapiga ninyi nyote kwa mikono yangu miwili?” Lisa alitoa kicheko cha huzuni. “Cheti cha ndoa kiko kwenye droo kwenye kabati la kushoto.”
Hans mara moja akaenda kukitafuta. Hakika, alikipata kwa muda mfupi. "Bwana Mkubwa, ni kweli."
Alvin alikodoa macho na kutoa amri. “Achana naye.”
Sura ya chuki iliangaza macho ya Maya huku wanaume wawili kutoka ONA wakimuacha Lisa bila huruma.
Lisa alijaribu kusimama, lakini miguu yake ilikuwa inamuuma na kufa ganzi kutokana na kubanwa kwa muda mrefu. Miguu yake ikageuka kuwa kama mlenda, na akaanguka.
Miguu ya Alvin ilimtetemeka huku akipata hamu ya kutaka kwenda kumsaidia. Muda mfupi baadaye, hata hivyo, alimtupia karatasi za talaka bila huruma. “Isaini na acha kuniita mkatili. Hapa kuna dola milioni 200 kwa ajili yako mara tu tunapoachana."
“Dola milioni 200? Hiyo ni mahari ama?" Lisa alidhihaki.
Alvin alikasirika zaidi, na sauti yake ikasikika kuwa ya ukali. “Unawaza ujinga kupita kiasi. Sitaki unisumbue katika siku zijazo. Haraka na utie saini. Sina wakati wote duniani.”
“Sawa.” Lisa alichukua kalamu na kusaini karatasi.
Alvin alijitenga huku akimwangalia mkono wake. Tangu alipojua kwamba bado yu hai, alikuwa akizungumza kuhusu kutaka kumtaliki. Sasa kwa kuwa wakati huu ulikuwa umefika, hakuhisi raha hata kidogo. Badala yake, alikuwa na huzuni kwa kiasi fulani. Ilionekana kana kwamba alikuwa amepoteza kitu ambacho alikuwa amekipata tena.
"Haya nenda." Baada ya kumkabidhi zile karatasi, Lisa alipata utulivu.
"Utapokea uthibitisho wa talaka mchana huu." Baada ya kukusanya karatasi za talaka, Alvin aligeuka na kuondoka.
Maya alimtazama Lisa kwa fahari kabla ya kutoka na wengine. Nyumba ikawa kimya tena. Akiwa ameegemea nyuma ya mlango, Lisa alicheka na kalamu mkononi. Hatimaye alikuwa ameachana na Alvin.
Halikuwa jambo baya. Baada ya yote, kusudi lake la kurudi lilikuwa kulipiza kisasi. Hakuwahi kufikiria kuokoa uhusiano wake na Alvin hapo kwanza.
Alvin alishuka ngazi na kumpa Hans karatasi za talaka. “Nenda ukamalizie hili.”
“Sawa.” Hans alimtupia jicho Maya kabla hajageuka na kuondoka. Alijisikia furaha kwa Lisa. Hatimaye hakuwa na uhusiano wowote na Alvin, na Alvin kipofu hakustahili kuwa na Lisa hata hivyo. Zaidi ya hayo, pamoja na wanafiki hawa karibu na Alvin, Hans alihisi kama kucheka.
Muda mfupi baadaye, Alvin alifanikiwa kupokea hati ya uthibitisho wa talaka. Alipoifungua aliitazama ile picha mle ndani na ghafla akajihisi mtupu.
Maya alimkumbusha, “Bwana Mkubwa, unataka kuchukua picha ya uthibitisho wa talaka na kuituma kwa Miss Njau? Atafurahi sana.”
"Unaweza kupiga picha yake." Alvin akamtupia. Baada ya hapo, akawasha laptop yake na kuendelea na kazi yake. Hata hivyo, hakuwa ameandika neno hata moja licha ya kuitazama kwa muda mrefu.
•••
Katika siku chache zilizofuata, mara nyingi Lisa alisikia kuhusu mapenzi ya hadharani ya Alvin na Sarah kwenye mitandao. Mbwembwe zilikuwa nyingi sana! Leo, wamechukua pete pamoja. Siku iliyofuata, walichagua kitanda pamoja. Kesho yake, walikuwa wamechagua hoteli kwa ajili ya harusi yao.
Siku moja, Sarah alihojiwa na waandishi wa habari. Alikuwa akiangaza kwa furaha kwenye habari hiyo. “Ndiyo. Baada ya kuwa katika uhusiano na Alvinic kwa zaidi ya miaka kumi, hatimaye tunafunga ndoa.”
"Umepanga tarehe?"
"Itakuwa siku ya kwanza ya mwezi ujao, ambayo ni siku yangu ya kuzaliwa."
“Oh. Hilo linamfikiria sana Mheshimiwa Kimaro.”
"Ndio. Sasa ninahisi kuwa mwanamke mwenye furaha zaidi ulimwenguni.”
Lisa alitabasamu kwa unyonge na kuzima televisheni.
'Una furaha sasa, lakini subiri siku utakapofunga ndoa. Nitakutumia zawadi nzuri na kukufanya uhisi kuanguka kutoka mbinguni hadi kuzimu!'......ITAENDELEA....
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
