JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................337-338
Sura ya: 337
Akili ya Alvin ilizunguka kwa muda. Muda mfupi baadaye, alirudi kwenye fahamu zake na kumtazama Lisa kwa hasira. Hata alitoa ripoti juu ya jambo dogo kama hilo? Mwanamke mbaya kama nini!
Polisi alikohoa kidogo. "Aliripoti kwa polisi wa trafiki. Kulingana na sheria za trafiki, mmiliki wa gari atapata upungufu wa pointi mbili kwenye leseni yake na faini kwa kutupa vitu nje ya dirisha. Sawa, nyinyi watu tayari mnaweza kuondoka." Polisi walitaka tu Alvin na Lisa wapatane na kuondoka.
"Subiri, bado hajanifidia gharama zangu za matibabu." Kidole maridadi cha Lisa kilipita kwenye skrini ya simu yake na akaonyesha ujumbe kwa polisi. "Ada yangu ya kulazwa hospitalini na matibabu ilinigharimu shilingi milioni sita na laki nane."
Afisa wa polisi alihisi kuumwa na kichwa. “Kesi hii si rahisi kuhukumu. Iwapo nyote wawili bado mna mzozo, mnapaswa kuufikisha mahakamani. Hata hivyo, kuajiri wakili kutagharimu zaidi ya kiasi hicho cha fedha, kwa hiyo nashauri wote wawili msuluhishe suala hili nje ya mahakama.”
"Sawa, mradi tu Bwana Kimaro yuko tayari kunipa pesa." Lisa alimtazama Alvin huku akitabasamu. Alionekana kama mbweha mjanja mbele ya Alvin. Aliufanya moyo wake kuwasha na kutamani kumpiga makofi machache kwenye uso wake.
"Pesa ni kitu kidogo tu kwangu, lakini kwanini nikupe?" Alvin aliuliza.
"Basi, naweza tu kupakia rekodi kwenye mtandao na kuwafanya wengine wasikie kwamba sio tu kwamba hatujaachana, lakini hata ulikuwa unapanga kuniteka nyara na kunifungia. Hilo lingependeza.”
Ilikuwa ni kama Lisa angeweza kukisia jibu lake kabla. Alvin alihisi kichwa chake ambacho kilikuwa kimepona, kinaanza kumuuma tena. "Lisa, kuna kitu kingine unachojua kufanya isipokuwa kunitisha?"
“Najua mambo mengine mengi. Unataka kujaribu?" Midomo ya Lisa ya rangi ya waridi yenye majimaji ilitabasamu na macho yake ya kuchecheza yakapepesa kwa namna isiyoeleweka. Alvin alichukizwa na mbwembwe na tabia yake ya kutaniana. Uso wake uligeuka kuwa mbaya.
Punde, gari jeusi lilikaribia. Joseph alishusha kioo cha gari na kumsalimia Alvin. Baada ya hapo, aliondoka na Lisa kwenye gari lake.
Alvin karibu kuwafuata kwa hasira, lakini alisimama alipokumbuka maneno ya Lisa.
“Alvin, bado umeniweka moyoni mwako…” Sauti ya mwanamke huyo ilisikika masikioni mwake. Akatoa sigara na kuiwasha kwa hasira. Ilikuwa haiwezekani. Alikuwa na Sara tu moyoni mwake.
10:00 Usiku.
Usiku ulikuwa kimya. Alvin alikuwa akiangalia ripoti ya maendeleo ya kampuni ya kipindi cha robo mwaka akiwa kwenye chumba chake cha maktaba. Sarah alikuwa amevalia kinguo laini cha kulalia chenye kutamanisha sana na kumkumbatia Alvin taratibu kwa nyuma. “Alvinic, umeshamaliza dawa. Hebu tujaribu.”
Mwili wa Alvin ulisisimka. Aligeuka na hakuweza kukataa alipomwona Saraha akimwangalia na kumsihi. “Sawa.”
Akiongea kimantiki, Alvin alikuwa na hisia kali kwa Lisa mara ya mwisho.
Hata hivyo, alipofika karibu na Sara, hakuna chochote alichohisi mwilini mwake zaidi ya baridi kali na mwili kupooza kabisa.
"Samahani, nadhani bado sijapona." Alvin alimsukuma kwa fujo. "Subiri kidogo tu."
“Ni ... ni sawa. Labda niilikuwa na haraka sana,” Sarah aliuma mdomo wake kwa kukerwa na kusema kwa sauti ya kutojiamini, “Ninaendelea kuhisi kukosa amani sana siku hizi tangu arudi Lisa. Nataka tu kwenda pamoja nawe ili moyo wangu uhisi raha.”
Alvin aliwasha sigara na kuivuta kwa kuchanganyikiwa. “Sarah, sielewi kwanini mimi pia niko hivi. Nikibaki hivi milele…”
“Hapana, hutafbaki hivi siku zote. Hata ukikaa hivi maisha yako yote, bado niko tayari kuwa nawe. Ninakupenda; mambo mengine si muhimu.” Japo aliongea maneno hayo ya kufariji, ubongo wa Sarah ulihisi kuchanganyikiwa. Mambo yasingeweza kuendelea kuwa hivyo yalivyo. Ilibidi atafute haraka njia ya kuwa na mwanaume huyu peke yake.
"Samahani, Sarah." Alvin alijawa na hatia. Aliweza kuwa na hisia kali za mapenzi alipokuwa na Lisa, lakini kwa nini hakuweza kuhisi hivyo alipokuwa na Sarah? Ingekuwa hiivyohivyo na kwa wanawake wengine pia au na ni Sarah tu ambaye hakuweza kumkubali?
Siku iliyofuata, akiwa njiani kuelekea kwenye kampuni, Alvin alimwambia Hans, "Niletee wanawake wachache na warembo hotelini leo usiku."
Miguu ya Hans karibu itetemeke, na akakanyaga breki. "Bwana Mkubwa, wewe-"
"Usiniulize chochote." Alvin alimkatisha.
Hapana, Hans alitaka kusema ni wanawake wangapi alitakiwa kumpelekea? Je, Alvin angeweza kumudu wanawake wengi hivyo?
8:00 usiku.
Hans alileta wanawake watatu ambao alikuwa amewachagua maalum.
Katika muda usiozidi dakika tano, wanawake hao watatu walifukuzwa nje kama mbwa. “Potelea mbali. Poteeeni nyote!” kishindo cha hasira cha Alvin kilisikika nje.
Hans aliwaondoa wanawake hao kwa haraka. Aliingia ndani na kumuona Alvin ameinama kichwa chini huku akiwa amekaa pembeni ya kitanda, mikono yake ikiwa hoi kwenye nywele zake. Alvin alikuwa akinung'unika, “Mbona iko hivi? Kwanini iko hivi…”
“Bwana Mkubwa, wewe… Uko sawa?” Hans aliuliza kwa wasiwasi.
Alvin alimpuuza na kumpita kwa hatua ndefu. Akaufunga mlango kwa nguvu na kutoka nje ya chumba cha hoteli.
Aliendesha gari kando ya barabara bila kujua alikuwa anaelekea wapi. Aliporudi kwenye fahamu zake, tayari alikuwa kwenye lango la jengo la nyumba ya Lisa, Karen Estate. Alisita kwa muda kabla ya kuegesha gari na kushuka.
Baada ya kuvuta sigara mbili, alimwona Lisa akitembea kutoka upande wake wa kulia. Alikuwa amevaa suruali nyeupe ya michezo na tisheti ya kawaida. Lilikuwa vazi la kawaida, lakini liliangaza mitetemo ya vijana. Alikuwa ameshika mifuko miwili ya shopping mikononi mwake na amevaa earphone za Bluetooth. Labda kwa sababu alikuwa akisikiliza muziki mtamu kwenye simu ndo maana alikuwa akitabasamu kwa furaha. Lakini alichoongea hasa ndicho kilionekana kumfurahisha zaidi. Alvin aliweza kudaka maneno ya mwishomwisho kwa mbali;
“Mpenzi, pia nakukumbuka sana. Muah, ngoja nikubusu.”
Lisa alipomaliza kuzungumza, aliona kivuli kikimjia.
Alvin alikuwa akimwangalia kwa sura ngumu, na macho yake yalikuwa yakiwaka.
“Uko kwenye simu na nani? Joseph?” Alvin aliuliza kwa kuchanganyikiwa Hasa aliposikia akisema neno 'mpenzi' na akambusu mtu huyo upande wa pili wa simu. Alipofikiria kuhusu Lisa kuwa karibu sana na mwanamume mwingine, alikuwa na hamu ya kumnyonga.
Lisa alishtuka. Alikuwa akiongea na Suzie na Lucas. Asingeweza kamwe kuruhusu Alvin kugundua kuwepo kwao. Angemsumbua mpaka mwisho wa dunia kama angejua uwepo wa watoto hao mapema vile.
“Ina uhusiano gani na wewe?” Lisa alitoa earphone kwa haraka na kutaka kukata simu. Hata hivyo, hakujua kwamba vitendo vyake vya kuhangaika vilimfanya Alvin ajisikie kuwa anajaribu kuficha kitu.
Alvin alimpokonya simu yake kwa hasira na kuweka simu kwenye spika.
“Joseph?”
“Alvin…” Moyo wa Lisa ulikuwa karibu kutoka kooni mwake.
Alitumaini kwamba Suzie na Lucas walikuwa na akili za haraka.
"Mjomba, Jotheph ni nani?" Sauti ya kitoto ilisikika kutoka kwenye simu.
Alvin alishikwa na butwaa. Hakutarajia kamwe kwamba ingekuwa sauti ya msichana mdogo. Zaidi ya hayo, sauti hiyo ilikuwa ikizungumza katika lafudhi ya kitoto. Inaweza kufanya mioyo ya watu kuwa laini.
Lakini, swali likamjia ghafla, kwanini Lisa alikuwa karibu sana na mtoto?
"Samahani toto. Wewe ni nani? Una uhusiano gani na Lisa?" Alvin alijaribu kupunguza sauti yake ili kuepusha kumuogopesha binti huyo.
Sura ya: 338
“Mjomba, mbona una mathwali meeengi kwani wewe polithi?” Suzie alisema bila furaha.
Alvin alikuna kichwa. Katika umri huo hakujua jinsi ya kuwasiliana na watoto hata kidogo.
“Alvin, nirudishie simu yangu.” Lisa alinyoosha mkono wake kumpokonya. Hapo hapo Alvin aliishika simu kwa mkono wake mwingine na kuinyanyua juu.
“Mjomba kwanini umeiba thimu ya Aunty Litha?” Suzie alisema kwa hasira.
"Shangazi?" Alvin alipigwa na butwaa. Kwa sababu fulani, ilionekana kana kwamba uzito fulani ulipunguzwa kutoka kifuani mwake. Alijisikia nafuu hadi rohoni. Alidhani Lisa tayari alikuwa ana mtoto na mwanaume mwingine.
"Hiyo ni thawa. Ulifikiri yeye ni mama yangu? Lakini yeye ni thawa na mama yangu pia." Suzie alianza kulia baada ya kusema hivyo.
Midomo ya Lisa ilitetemeka. Alishangaa sana hapo awali hata akasahau kwamba, ingawa Suzie alikuwa mvivu, alikuwa na akili ya haraka na malkia wa maigizo.
Alvin kwa kawaida alichukia sana watoto walipolia, lakini kwa namna fulani, alisikiliza kwa moyo mpole wakati msichana mdogo kwenye simu alilia. “Huna mama?”
“Thio hivyo. Mama yangu ni mkali thana kwangu. Yeye hunigombesha kila mara na hunikathirikia. Hanipi hata chokoleti. Shangadhi Litha ni tofauti. Yeye huninunulia chokoleti nyingi kila wakati. Nampenda thana. Lakini baada ya kwenda Afrika, hakuna mtu anayeninunulia chokoleti tena. Boo-hoo…”
“Mtoto mdogo, kula chokoleti nyingi ni mbaya kwa meno yako," Alvin alisema kwa upole.
Lisa alikosa la kusema. Je, Suzie alikuwa akimaanisha kwamba ampelekee chokoleti? Yule mtoto alikuwa na akili kweli.
“Meno yangu bado yapo vidhuri thana. Mjomba, una uhuthiano gani na Aunty Litha? Mbona unamthumbua?” Suzie aliuliza kwa hasira.
Alvin hakupata neno lolote la kumjibu. Ilionekana kana kwamba mazungumzo hayangeweza kuendelea tena.
“Mbona hujibu thwali langu?” Suzie alisema kitoto, "Yeye ni nani kwako?"
“Mtoto mdogo, nani kakufundisha maneno hayo? Wewe ni mdogo sana. Huelewi ulimwengu wa watu wazima.” Alvin alihisi kukereka na haraka akakata simu. Hii ilikuwa mara ya kwanza alihisi uchovu kwa kuzungumza na mtoto.
Lisa alichukua tena simu yake. Alvin aliuliza kwa hasira, “Ni mtoto wa nani huyo? Wazazi wake wanamlea vipi? Malezi yake ni mabovu sana.”
“Ndiyo, wazazi wake hawamfunzi kuhusu mambo haya.” Lisa alidanganya tabasamu na kusema, “Hasa baba yake. Ana mwanamke mwingine nje na mara nyingi hayupo nyumbani.”
"Baba yake si mwajibikaji kabisa." Alvin alimuonea huruma ajabu binti huyo.
“Ndiyo, kama wewe,” Lisa alisema, “Nilipokuwa ng’ambo, sikuweza kujizuia kukumbuka watoto tuliowapoteza kila nilipowaona watoto wa jirani yangu.”
Alvin alihisi kujaa ghadhabu. Alidhihaki, “Unajaribu tu kudokeza jambo fulani kunihusu. Kwanini tulifunga ndoa wakati huo? Ni wewe uliyekuwa umesisitiza kwa ujasiri kuolewa na mimi. Isingekuwa wewe kupanda kitandani kwangu, ningekupa nafasi ya kupata mimba?”
Lisa alitabasamu huku akimwangalia. “Niambie basi. Nilianzaje kupanda kitandani kwako?”
“Vipi bado unathubutu kunibishia? Hukunilazimisha kwa sababu uliongeza kitu kwenye kinywaji changu huko Dar es Salaam?” Alvin alimshutumu kwa ukali.
Lisa alitambua mara moja. Hali ya akili ya Sarah ilikuwa na nguvu sana hata kumbukumbu za Alvin ziliandikwa upya kiasi kwamba yeye mwenyewe hakuweza kuziona.
“Kwa nini? Je, ulifikiri kwamba ningeisahau baada ya miaka mitatu?” Alvin alimdhihaki.
"Ndio, kumbukumbu yako ni nzuri sana. Nimechelewa, nataka kwenda kupumzika. Unataka kunifuata? Nani anajua, ninaweza kukuwekea kitu kwenye divai tena na kukulazimisha kupanda kitandani kwangu.” Lisa alitingisha mfuko wa plastiki alioushika. “Nimebeba mvinyo mwekundu humu ndani. Unataka kupata glasi pamoja na mimi?"
"Ni chafu." Alvin alimtazama kwa hasira. Kisha akageuka na kuondoka.
Lisa akatikisa kichwa bila kuongea. Alizunguka eneo lake kila siku wakati alikuwa na mwanamke nyumbani. Sarah lazima awe na wasiwasi.
Lakini, Lisa alipenda iwe hivyo. Kama sivyo, mpango wake usingewezaje kutekelezwa.
Baada ya Alvin kupanda gari, hakuwa na haraka ya kuwasha gari.
Alikumbuka sauti ya msichana mdogo kwenye simu. Ghafla alihisi hisia za kuumiza moyo.
Ikiwa watoto wao wawili wangekuwa bado hai, wangekuwa na sura gani? Hakika zingekuwa za kupendeza. Hata daktari alisema kwamba walikuwa mapacha. Katika miaka hiyo, hakuwahi kufikiria jambo hilo hapo awali. Hata hivyo, moyo wake ulikuwa na maumivu ghafla usiku huo.
•••
Akiwa kwenye jumba la kifahari la Alvin, Sarah alipokea picha chache kutoka kwa mpelelezi wake binafsi kwenye simu yake. Katika picha hizo, Alvin na Lisa walikuwa pamoja kwenye lango la jengo la makazi ya Lisa, kwenye eneo maarufu la Karen Estate.
Uso mzuri wa Sarah ulipinda kutokana na hasira na wivu. Asingeweza kuendelea hivyo. Ilibidi amshinde haraka Alvin.
Saa moja baadaye, Alvin alifika nyumbani kwa gari lake. Alipokuwa karibu kuoga, Sarah alimpelekea glasi ya maziwa juu ya ghorofa. "Alvinic, nimekutengenezea hii."
"Asante." Alvin alishusha yote ya maziwa tumboni mwake bila kufikiria tena. Hata hivyo, alipokuwa akioga, alihisi mwili wake ukizidi kukosa raha. Hata kuoga tena hakukuwa na maana.
Wakati huo, aligundua kinachoendelea. Mara moja alivaa na kutoka nje kwa kasi. Sarah akajitupa mikononi mwake. "Alvinic, nakupenda."
"Uliweka nini katika maziwa uliyonipa?" Alvin alimshika mkono huku macho yake yakiwa yamejaa hasira na kukata tamaa.
"Samahani, Alvinic. Sikutaka kufanya hivi.” Sarah akatikisa kichwa na kuanza kulia. “Lakini kwa kweli siwezi kukupoteza. Tangu Lisa aliporudi, unaendelea kurudi nyumbani usiku sana. Nataka tu kuwa na wewe. Ninaogopa sana kwamba atakuiba na kukuweka mbali nami. Alvinic, usiniache, nakuomba.”
Sarah alikuwa na taswira nzuri na ya kuvutia moyoni mwa Alvin muda wote. Huku akilia mbele yake, Alvin hakuweza kuelezea hisia aliyokuwa nayo ndani ya moyo wake.
Kulikuwa na hasira, ingawa. Huenda watu wengine hawakujua kuhusu hilo, lakini Sarah alikuwa anajua fika kwamba tukio hilo lilichukuliwa kuwa mwiko kabisa kwa Alvin, lakini, bado alifanya hivyo. Sababu kuu ikiwa hakumfanya ajisikie salama vya kutosha.
Alipokuwa akifikiria jambo hilo, ni kweli kwamba baada ya Lisa kurudi, Sarah alianza kumjali sana Alvin. Mbali na hilo, Sarah alikuwa amevumilia siku nyingi kwa sababu hakuweza kutosheleza hitaji lake la msingi. Kama binadamu, Alvin alisikitika, na moyo wake ukashuka. Hakuweza kujizuia kukataa ombi la unyenyekevu la Sara.
Alipoona kwamba alikuwa kimya, Sara alichukua hatua zaidi kuliko hapo awali. Japokuwa mwili wa Alvin ulikuwa unawaka moto, bado alihisi kuchukizwa na kuguswa na Sarah. Hakuweza kuvumilia tena na kumsukuma kwa nguvu. Sarah alianguka kwenye zulia kwa fujo.
“Sarah, samahani…” Alvin alipoona uso wake ukibadilika, alitikisa kichwa kwa kukosa raha. Aligeuka na kutoka nje ya chumba cha kusoma.
"Alvinic, subiri." Sarah alijitahidi kumfuata akiwa amevaa nguo zilizochafuka, lakini aliona tu mwonekano wa gari lake ukiondoka.
“Ah, Alvin, huna maana!” Sarah alikanyaga miguu yake kwa mshangao. Hakuweza kuamini. Tayari alikuwa katika hali hiyo isiyopendeza, lakini mwili wake bado haukuweza kumkubali. Kwanini? Ilikuweje akamfanya ahisi kuchukizwa hivyo? Hypnosis yake ilienda vibaya wapi?
Hata hivyo, mwili wake ukiwa katika hali hiyo, hangeweza kwenda nje kutafuta wanawake wengine, sivyo? Hapana, haiwezi kuwa. Hakuwa na uwezo wa kufanya ngono. Kutafuta wanawake wengine ingekuwa bure kwake pia.
Wimbi la wasiwasi lilimfunika. Hata hivyo… Vipi kama Alvin angeenda kumtafuta Lisa? Sarah alimpigia simu Rodney kwa haraka. Alimueleza kila kitu huku akilia.
Rodney alishtuka. "Nini? Alvin hawezi kufanya ngono?”
“Rodney, hayo tuyaweke pembeni. Haraka fikiria njia ya kumpata. Ninahofia kwamba kuna jambo litamtokea,” Sarah alisema kwa wasiwasi.
"Jambo ni kwamba, niko mbali na safari ya kikazi leo. Nitamwomba Chester amtafute haraka iwezekanavyo.”
“Haupo karibu?” Sarah karibu alitaka kutema damu. Huyo Rodney mjinga hakuwa na manufaa yoyote ilipofikia wakati muhimu.....ITAENDELEA....
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
