JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................339-340

Sura ya: 339

Usiku wa manane, gari lilitembea kwa kasi barabarani. Alvin alishusha madirisha yote. Upepo wa usiku wa baridi ulivuma, lakini haukutawanya joto katika mwili wake. Badala yake, alikuwa katika hatihati ya kuanguka.
Hapana. Hii haikuwa nzuri. Uso wa Lisa uliangaza kwenye akili yake yenye giza. Alizidi kukanyaga moto.

Gari lilienda kwa kasi kuelekea Karen Estate. Akiwa ndani ya chumba chake cha kulala, Lisa hakujua kuwa kuna mtu alikuwa akimfikiria.
Alikuwa kwenye simu ya video na Suzie na Lucas. Kwa sababu ya tofauti ya wakati, bado ilikuwa mchana huko Marekani.

"Mama, kazi zako zimeendaje leo?" Suzie aliuliza kwa furaha, “Nilikusikia ukiita jina la Alvin, nikajua huyo ni baba yangu mchafu. Bila shaka, nisingemwambia mimi ni mwanao. Sitaki anirudishe na kumwacha mwanamke mbaya awe mama yangu wa kambo.”

“Koohkooohkoh…” Lisa nusura apaliwe na maji aliyokuwa akinywa. Binti yake alivyokuwa akiongea haikuwa kawaida. Ikiwa ni watoto wengine, wangekuwa na huzuni kwa nusu ya siku.

Hakuweza kujizuia kumkazia macho Lucas usoni mwake. "Mwanangu mpendwa, unaonaje?"

“Simpendi. Sitaki kuwa na baba asiyempenda mama yangu, usije ukamsamehe hata siku moja.” Lucas alifika moja kwa moja kwenye uhakika.

"... Pole, una hoja hapo." Lisa alishangazwa kwa siri na msamiati mpana wa mapacha hao.

“Mama, mimi pia simpendi. Hataniruhusu nile chokoleti,” Suzie alisema, “Tayari inatosha kuwa na mtu mmoja katika familia ambaye haniruhusu kula chokoleti. Ikiwa kuna mwingine, basi sitaweza kula chokoleti hata kidogo.

“… Ha, wewe ni mtoto mdogo mwenye akili sana.” Lisa alimsifia huku akihisi kuumwa na kichwa.

Wakati huo sauti ya mtu akigonga mlango ilisikika kutoka nje.
"Lisa, fungua mlango haraka." Alikuwa Alvin tena.

“Wanangu, kuna jambo la dharura limetokea. Tuzungumze kesho.”

"Mama, ni baba yangu mchafu alikuja kukutafuta tena?" Lucas alisema haraka,

“Hapana, byee…kesho!” Lisa akakata simu ya video. Aliuendea mlango lakini hakuwa na haraka ya kuufungua. “Alvin, unataka kufanya nini?”

“Acha kuropoka. Usipofungua mlango nitaupiga teke mpaka uvunjike.” Alvin alianza kuupiga mlango kwa mateke bila kukoma.

Lisa aliogopa kwamba angesumbua majirani saa za usiku sana, kwa hivyo alifungua mlango. Mara mlango ukafunguliwa, Alvin aliingia na kumfakamia. Midomo yake ilitua juu ya midomo ya Lisa kwa bidii.

Lisa alikuwa ametoka kuoga muda si mrefu uliopita na harufu hafifu mwilini mwake ikaingia puani mwake. Mawazo yaliyobaki ambayo Alvin alikuwa nayo yaliharibiwa kabisa. Wakati huo, Lisa alionekana kama kipande cha keki yenye ladha tamu kwake. Alikuwa anajaribu sana kujinasua lakini wapi.
“Alvin, unafanya nini?! Niache niende!” Lisa alishtuka sana. Aliweza tu kumsukuma mbali kidogo licha ya kutumia nguvu zake zote.

Uso wake mzuri ulikuwa umebadilika rangi na mwili wake ulikuwa joto kama mtu mwenye homa kali. Hakuhitaji maelezao. Aliwahi kujionea tukio kama hilo yeye mwenyewe na alikuwa akijua sana hali yake.

"Nakutaka." Alvin alimtazama kwa macho ya hamu.

“Umekuja mahali pasipofaa. Nenda kamtafute Sarah. Mimi—ah!”

Lisa alikuwa bado hajamaliza kusema wakati Alvin alimvamia kumbusu tena bila kumpa nafasi ya kuongea.

Usiku ukapita! Jua la asubuhi liliangaza kupitia madirisha. Lisa alifumbua macho kutokana na mwanga wa jua. Aligeuza kichwa na kumuona Alvin akiwa amelala fofofo. Alimwamsha kwa hasira.

Alvin ambaye alikuwa amelala fofofo, alikunja uso. Hata hivyo, hakufungua macho yake. Lisa alijitahidi kuinuka. Akaingia bafuni.
Alioga kwa maji ya moto kwa muda mrefu na akatoka baada ya nusu saa.

Alipofungua mlango wa bafuni, alimuona yule jamaa akiwa amekaa kitandani baada ya kuamka. Macho yao yakakutana. Alvin mara moja aliona michubuko kwenye shingo ya Lisa na sehemu ya kifua chake. Akashusha macho na kuona kitanda kikiwa kimevurugwa. Bado aliweza kukumbuka kwa uwazi kilichotokea jana yake usiku.

Alikuwa amewekewa kitu na Sara kwenye mazima, kitu ambacho kililiamsha dude lake. Lakini alishindwa kabisa kumalizia mihemko yake kwa Sarah! Alikuwa mpenzi wake na mchumba wake. Ingawa alikuwa amefanya kosa, bado alimpenda na alikuwa tayari kumsamehe. Ni vile tu alihisi kichefuchefu kila alipomshika Sarah kwa nia ya kushiriki tendo.

Mwishowe alitoka nje na kuja kumtafuta Lisa bila kujizuia. OOh! Jamani, kwa nini imekuwa hivi? Sio tu kwamba alimkosea Sarah, bali hata alijirusha na Lisa?

Lisa aliutazama uso wake ambao ulionekana kuwa na maumivu kwa muda na kumuona akiuma meno muda uliofuata. Alimsonya kwa dharau na kumtupia taulo alilolishika mikononi mwake.

“Alvin, kwa hiyo haya ndiyo mapenzi uliyonayo kwa Sarah? Naweza kuhisi kinachoendelea.”

“Lisa acha kejeli zako.” Alvin alijibu. “Unafikiri nilitaka kufanya hivyo? niliwekwa dawa”

"Ha" Lisa alicheka. Kwa mara nyingine tena alidhihirisha upuuzi wake.
Yaani dawa awekewe na mwingine halafu zikapozwe na mwingine?

"Kwanini unacheka? Utakuwa ulifurahia sana janausiku, huh?” Alvin alikumbuka jinsi alivyokuwa akimpagawisha sana usiku wa jana. Alikuwaaa….aibu!

“Nimefurahi?” Lisa alikunuja mikono yake. Alionyesha alama za michubuko kwenye mikono yake iliyosababishwa na mtu huyo aliyemshika kwa nguvu nyingi. “Tafadhali, tazama hili. Nina michubuko mwili mzima. Ndugu, hujui hata kumpetipeti mwanamke kimahaba, yaani ulnachojua ni kuvamiana tu ngo’ombe? Pengine hata ngo’mbe ana nafuu. Usiku hukunitendea kama binadamu kwa kweli. Ninaweza kukushtaki kwa hili!”

Kuangalia michubuko hiyo, Alvin alibana midomo. Athari za kuomba msamaha zikamjaa.

“Una chuki gani na mimi hadi unifanyie hivi?” Lisa alizidi kulalamika. “Kwanini hukwenda kumtafuta Sarah?” Lisa alijizuia kuonesha chuki machoni mwake.
Alvin alinyamaza kimya.

“Hauwezi… huna hamu na Sarah sasa?” Lisa akamsogelea hatua kwa hatua, akitabasamu. Baada ya jana yake usiku, alikuwa na alihisi hisia za ziada ya kuvutia kwake.

Utamu usiosahaulika wa usiku wa jana yake ulipita kichwani mwa Alvin. Hakuweza kusahau hisia hiyo hata wakati huo.

“Nimeelewa sawa?” Alipoona amenyamaza, tabasamu la Lisa likazidi kuongezeka.

"Unafikiria sana." Alvin alimpiga jicho kali ghafla. Maneno yake yalikuwa mabaya, kana kwamba yametiwa sumu. “Niliogopa kwamba ningepoteza akili jana usiku na kufanya jambo la kumuumiza Sarah. Anapaswa kutendewa vizuri na kutunzwa. Kwa upande wako, sijali unaumia kiasi gani."

"Ooh! Kumbe?" Tabasamu la Lisa taratibu likaganda.
Hakika huyu ndiye Alvin aliyekuwa anamfahamu. Siku zote alikuwa na njia ya kugeuza uhalisia wa mambo ili tu kumfanya achukie.

“Wewe ni mke wangu wa jina tu. Kwa vile unakataa kuachia nafasi yako, basi inafaa utimize wajibu wako kama mke.” Baada ya Alvin kusema hivyo kana kwamba ni jambo la kawaida, alijisikia faraja. Hakuwa na chochote cha kuhisi hatia tena kwa Lisa.

“Unaweza kuthubutu kumwambia Sarah maneno haya?” Lisa aliuliza kwa kejeli.

Uso wa Alvin ulibadilika. Akamkazia macho. "Lisa, ikiwa utathubutu kufichua chochote kilichotokea jana usiku, nitakufanya ulipe."

"Alvin, katika hadithi ya 'Mkulima na Nyoka', wewe ni yule nyoka mwenye sumu." Lisa alijilaumu kwa kuwa mpole na kumhurumia Alvin jana yake usiku. Alipaswa kumfukuza na kumwacha ateseke na kufa.

Alvin alijiona kama amejidharaulisha, lakini hakuwa na jinsi. "Maadamu hausemi chochote, Sarah hatajua."

“Hakuna kinachoweza kubaki siri milele. Sarah atakaposikia kuhusu hili, mimi ndiye nitaonekana mbaya tena. Itakuwa kama mara ya mwisho uliponinunulia chupi. Sikusema neno lolote, lakini hukumwamini mwishowe?” Lisa alicheka na kuelekea mlangoni.

Alvin alishikwa na butwaa. Alikunja uso na kuuliza, “Bado unataka kukataa kuhusu hilo? Ikiwa hukusema lolote, Sarah alijuaje? Una maanisha Sarah alishirikiana pamoja na meneja huyo kunidanganya?”

“Nikisema ndiyo, utaniamini? Kati yangu na Sarah, hautawahi kuwa upande wangu.” Alisema hivyo bila kugeuka nyuma.

Sura ya: 340

Alvin alikuwa ametokwa na jasho jingi kwa shughuli aliyofanya usiku wa kuamkia jana yake, kwa hiyo alikuwa anajisikia vibaya mwili mzima sasa. Alitaka kuoga baada ya kuingia bafuni lakini hakuwa na taulo. Aliwaza na kuchukua taulo la Lisa tu.

Alikuwa kituko mbele zake mwenyewe. Hakuweza hata kuvumilia kutumia taulo la Sarah kujifuta usoni. Hata hivyo, alipotumia taulo la Lisa, hakuhisi kuchukizwa hata kidogo. Kitambaa chake kilikuwa na harufu ya kupendeza, sawa na mwili wake.

Alipotoka bafuni, Lisa alikuwa amekaa kwenye sehemu ya kulia chakula, akiwa na pasta. Kulikuwa na yai la kukaanga pia kwenye pasta. Ilionekana kupendeza kwa kutazama mara moja tu.

Alvin, ambaye alikuwa amechoka jana yake usiku, mara moja alihisi njaa. “Kifungua kinywa changu kiko wapi?” Moja kwa moja akaketi kwenye kiti kilichokuwa kando yake na kuonekana kama alikuwa akisubiri mtu wa kumpatia kifungua kinywa.

Lisa alimtazama kwa uvivu. "Cha kwako? Ni nyumbani kwako hapa?" Hakuna mjakazi wa kukuhudumia kifungua kinywa hata ukisubiri milele hapa."

Matarajio usoni mwa Alvin yalionekana kupungua kwa kasi, badala ya hasira. “Lisa, nipo kwako sasa, sijali. Nina njaa, lazima unipikie kifungua kinywa sasa hivi.”

“Kwanini nikupikie? Unaweza kunishukuru ikiwa ningefanya hivyo? Sioni hata ukinishukuru kwa kukuokoa jana usiku.” Hasira ya ndani ya Lisa hatimaye ililipuka. "Unakula na kunywa vitu vyangu kila unapokuja hapa. Sio tu kwamba hulipii chochote, hata unaniingiza kwenye matatizo kila baada ya muda fulani. Potelea mbali!”

“Unathubutu kuniambia nipotee?” Mwale wa hasira ulitoka kwa Alvin.

“Nini tena? Unataka nikuambieje ili ujue namaanisha uondoke? Tatizo hujui hata lugha.”

Uso wa Alvin ulizidi kujawa na hasira. Kwanini hapo awali hakugundua kuwa Lisa alikuwa na mdomo mchafu? "Lisa, unatamani kifo?"

“Kwanini? Unataka kuniua? Niue basi. Nina maumivu mwili mzima hata hivyo.” Lisa akasimama. Macho yake mazuri, safi yalikuwa yakiangaza machozi. Alionekana mwenye huzuni.

Hasira kwa Alvin ilipungua ghafla. Hakuweza kustahimili kumuona akihuzunika namna hiyo. Alikiri kuwa kweli alikuwa amevuka bahari jana yake usiku.

“Usilie. Si pesa tu…” Akatoa kadi ya benki kutoka mfukoni mwake na kumkabidhi. “Kanunue chochote unachotaka. Nataka tu nile sahani hii ya tambi."

“Sitaki. naumwa.” Lisa hakumtazama kabisa aliendelea kula pasta yake.
Alvin alitazama nyuma ya kichwa chake kwa muda. Alichukua uma kutoka jikoni na kula pasta pamoja naye.

"Alvin, huruhusiwi kula tambi zangu." Lisa alizuia uma wake. Macho yake mazuri yalikuwa yametoka kwa kung'aa. Midomo yake iliyovimba kidogo ilitiwa mafuta, lakini ilifanya tu midomo yake ionekane maridadi zaidi kama jeli.

Muonekano wake asubuhi hiyo uliufanya moyo wa Alvin kuwasha. Alijua kwanini midomo yake ilikuwa imevimba. Ni kwa sababu alikuwa ameibusu kwa vurugu jana usiku. Bado aliweza kukumbuka ladha ya midomo yake.

“'Nataka kula." Alvin alianza kumpokonya chakula.

Wale watu wazima wawili walikuwa kama watoto wanaopigana wao kwa wao. Yai liligawanyika nusu kwa nusu.
Wakati kulikuwa na ntambi chache zilizobaki, Lisa aliinamisha kichwa chake na kuzibugia zote. Baada ya kufaulu, aliinua kichwa chake kwa hasira, kana kwamba alikuwa mtoto aliyeshinda pambano.

Alvin alimtazama Lisa. Sura yake ya kitoto ilifanya moyo wake uende mbio. Aliguna na kusonga mbele bila fahamu, ambapo aliuma tambi iliyobaki ikining'inia mdomoni mwake. Alipoinama chini, midomo yake ikagusa midomo yake.

Macho ya Lisa yakamtoka. Kope zake nene zilipita kwenye ngozi ya mashavu yake, na macho yake safi yalikuwa yanawaka kama nyota angavu zaidi angani. Wakati huo, Alvin alihisi kitu kwenye ubongo wake.
Alitaka kushika nyuma ya kichwa cha Lisa na kumsogeza kupata ladha ya kile walichokuwa nacho jana yake usiku kwa mara nyingine tena.

Ghafla, kengele ya mlango ililia. Lisa alishtuka na kumsukuma Alvin pembeni. Uso wake ulitia haya kidogo huku akimkazia macho Alvin kabla ya kwenda kuufungua mlango.

Umbo la Chester refu na la kibabe lilisimama mlangoni. Mara macho yake makali yalipotua kwenye midomo ya Lisa, ghafla alihisi maumivu ya kichwa yakiongezeka. Baada ya yote, alikuwa na uzoefu pia.

“Ni kwa ajili yako. Tafadhali fanya haraka na uondoke. Sitaki kutuhumiwa kukutongoza tena.” Lisa aligeuza kichwa na kumwambia Alvin kwa madaha. Kisha, alichukua hatua hadi jikoni.

Alvin alipomwona Chester akiingia ndani, sura yake ikazama ghafla.
Hakuwahi kumuangalia Chester akiwa na macho kama hayo hapo awali. Ikiwa Chester asingegonga mlango muda huo, labda angekuwa kwenye sayari nyingine muda huo.

"Inaonekana nimekuja kuchelewa sana." Chester alikunja uso kidogo.

“Kwa nini uko hapa?” Alvin alishtuka ghafla. “Sarah…”

“Bado hajui. Twende zetu.” Chester akageuka na kutoka nje.
Alvin alimtazama Lisa aliyekuwa anaosha vyombo jikoni. Alitaka kusema kitu, lakini alipomfikiria Sarah, kichwa kilimuuma. Kwa hivyo, alitoka na Chester.
•••
Chini.
Alvin aliegemea ubavu wa gari huku Chester akimpa sigara. “Vema, kama Sarah asingelazimika kumpigia simu Rodney jana usiku, nisingejua kwamba hujawahi kumgusa Sarah kwa miaka mitatu iliyopita… Lakini hauonekani kama huwezi kufanya hivyo. ”

Alimzidisha ukubwa Alvin kwa sura ya ajabu machoni mwake, na Alvin akampiga jicho la onyo. “Unamaanisha nini siwezi? Naweza sana.”

"Basi, kwanini ulikuja kwa Lisa jana usiku? Humpendi Sarah?” Chester alishangazwa naye.

“Hata mimi sijui.” Alvin aliwasha sigara na kuivuta kwa muda mrefu. Alionekana mwenye huzuni kiasi fulani. “Ni ajabu. Kila ninapomgusa Sarah, ninahisi kukarahika moyoni. Ni sawa na wanawake wengine pia. Lisa pekee ndiye tofauti.”

“Inawezekanaje?” Chester aliinua kichwa chake na kuvuta pumzi ya moshi. “Najua una mysophobia. Unaogopa kwa sababu Sarah alikuwa…”

“Hapana, hapana.” Alvin alisema kwa kutatanisha, “Nimemwona daktari, na daktari amesema mimi ni mzima pia. Kwa kweli nilitaka kuwa na Sarah jana usiku. Nilijaribu, lakini sikuweza.”

Chester alirusha majivu ya sigara. “Hii ni mara yangu ya kwanza kusikia kitu kama hicho. Vipi kuhusu Sarah? Anakupenda sana. Ikiwa atagundua kuwa ulikuwa na Lisa jana usiku, atalia hadi kufa. Na wewe mbona hukukimbilia hospitali?”

Alvin alikuwa kimya. Kiukweli swali lile pia alilifikiria pindi akiwa ametulia, lakini kwa wakati huo jambo lililokuwa akilini mwake lilikuwa ni Lisa. Hakufikiria hata hospitali.

"Inaweza kuwa hivyo ... haujamsahau Lisa?" Maneno ya Chester yaliufanya moyo wake kurukaruka.

“Haiwezekani. Ninayempenda ni Sarah."

“Unampenda Sarah, lakini huwezi kumgusa.” Chester aliuliza kwa mashaka. “Alvin huoni ajabu sana? Kabla ya ajali hiyo ya gari, ulionekana kuwa na wivu ulipowaona Lisa na Joseph Ruta wakiwa pamoja.”

"Mimi, wivu?" Alvin aliitikia kana kwamba nafsi yake imepondwa. “Mimi sina wivu. Sikutaka tu kudharauliwa.”

“Una uhakika kweli huna Lisa moyoni mwako? Ulikuwa unamfikiria nani ulipokuwa naye jana usiku?” Chester aliuliza kwa ukali.

Alvin alihisi kuridhika alipokumbuka kilichotokea jana usiku. Ilikuwa ni hisia ambayo hakuwahi kuwa nayo na Sarah. Alitamani hata kumbusu Lisa wakati anakula muda mfupi kabla.

"Chester, sijui nina shida gani." Alvin alikuwa na migogoro na huzuni.
Siku zote alikuwa wazi sana juu ya hisia zake. Alimpenda Sara, na alimchukia Lisa. Hata hivyo, sasa alikuwa amechanganyikiwa.

Kuona sura yake, Chester naye alikunja uso kwa wasiwasi. “Fikiria. Ingawa simpendi Lisa, hupaswi kuwaumiza wanawake wote wawili.”......ITAENDELEA....

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.