JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................335-336

Sura ya: 335

"Alvin, kwa nini umekuja?" Wakati Sam, ambaye alikwenda kujaza sahani nyingine ya nyama, aliporudi, macho yake karibu yadondoke kutoka kwenye soketi zake alipoona tukio hilo. Alitazama huku na kule kwa pupa na kushusha pumzi baada ya kuona yupo Alvin tu. Hakutaka kugongana na Rodney, Sarah, na wengine. Kulikuwa na kejeli zisizoisha kila walipokutana.
“Si nyie mlikuwa mkienda clubhouse? Si unaandamana na Sarah?” Sama aliongeza aliongeza maswali mawili zaidi.

Hilo lilifanya uso wa Alvin kuwa mweusi. “Kwanini uniulize hivyo? Ina maana Lisa hajakwambia japo mmekuwa kwenye ‘hangout’ kwa muda mrefu tayari?” Akageuza kichwa kuelekea kwa Lisa na kuinua macho yake. “Cheti chako cha ndoa kiko wapi? Si huwa unatembea nacho kila mahali ili kunitishia? Kitoe na uwaonyeshe."

Lisa kidogo akose la kusema. “Huoni hata aibu unaposema hivi kwa sauti? Huoni aibu kwa kutamba na kuringa na mwanamke mwingine wakati kumbe unajua bado kwenye ndoa! Mbaya zaidi unafanya kazi pamoja naye ili kuniangamiza mimi na kampuni yangu. Aibu kwako."

“Unajua wazi kwamba sina hisia na wewe. Ni wewe ndiye unayening'ang'ania. Ulijaribu hata kumuumiza Sarah. Unastahili hayo yote! " Alvin hakuonyesha kujali maneno yake hata kidogo.

Sam alikuwa amemzoea, lakini Joseph alishangaa kusikia maneno yake. "Sikujua kwamba maneno ya mtu tajiri zaidi wa Kenya, Bwana Kimaro ambaye kila mtu anamheshimu, yangekuwa ya ajabu kiasi hiki."

“Unafikiri wewe ni nani wa kuninyooshea kidole?” Midomo myembamba ya Alvin ilionyesha tabasamu la kejeli. "Au unampenda?"

Joseph alisema kwa upole, “Kwani kuna shida gani nikimpenda? Lisa ni mzuri na mrembo. Maadamu yuko tayari na yuko huru kuolewa nami, ninaweza kumkubali wakati wowote, tofauti na mtu fulani ambaye ni kama mbwa kwenye hori.”

Lisa alishangaa, lakini alielewa mara moja alipomwona Joseph akipepesa macho kwa siri. Moyo wake ukapata joto.

Alvin alikunja ngumi. Hasira yake ilimfanya Sam ashuku kwamba angemrukia mtu sekunde yoyote.

Sam ilikwenda kati ya watu hao wawili haraka. “Alvin, tulia. Joseph anatania tu.”

"Sikuwa na mzaha hata kidogo." Joseph alifoka.

Alvin, ambaye alikuwa akichokozwa tena, alipunguza macho yake. Alidhihaki, “Mimi sina shida naye, ila ni yeye ndiye hataki. Ni yeye ambaye sasa anakataa kuachwa.” Baada ya kuongea alimvuta Lisa kwake na kumtazama kwa ukali. “Sema mawazo yako. Uko tayari kunitaliki?”

Lisa alitabasamu. “Niko tayari!”

Uso wa Alvin ukawa mgumu ghafla. Macho yake makali yalionekana kana kwamba alitaka kumla akiwa hai. Alikuwa amekataa kabisa kutiasaini hati za talaka siku chache zilizopita. Hata hivyo, kwa kuwa sasa alikuwa na mwanamume mwingine, alitaka kumwacha mara moja.

“Lakini si sasa,” Lisa aliendelea kusema, “Wewe na Sarah mlinitesa na kuyafanya maisha yangu kuwa magumu. Nimeirudi baada ya miaka mitatu, lakini bado Sarah ananifanyia mambo mengi ya kijinga. Mwambie aendelee kuota ikiwa anafikiri nitasalimisha cheo cha Bi Kimaro kwa urahisi hivyo.”

Joseph mara moja akammiminia glasi ya mvinyo na kumpa kwa hisia ya upendo. “Nitakuunga mkono hata ufanye nini, nitakusubiri."

"Asante." Lisa alikuwa karibu kupokea glasi ya mvinyo. Hata hivyo, alishushwa kutoka kwenye kiti na Alvin kabla hata hajaigusa.

“Tunaondoka sasa hivi.” Alvin aliamuru.

“Hilo halitawezekana. Maisha ya usiku ndiyo kwanza yanaanza." Joseph akamshika mkono mwingine Lisa.

“Muachie twende. Ukinisumbua, bado ninaweza kusababisha madhara kwa Ruta Design hata kama siwezi kuiharibu. Haijalishi uko katika biashara tofauti,” Alvin alionya.

Macho ya watu hao wawili yaligongana. Lisa alimgeukia Joseph kinyonge na kusema kwa sauti nyororo, “Joseph samahani. Nitakuhudumia kwa chakula kingine wakati ujao.”

“Hauruhusiwi kula naye tena,” Alvin alitamka onyo lingine.

Joseph alicheka na kupuuza maneno ya Alvin. “Sawa, wakati ujao. Kuwa mwangalifu na unipigie ikiwa chochote kitatokea. Nitakuwa kando yako daima.”

“Asante—” Lisa alikuwa bado hajamaliza kuongea aliponyanyuliwa na kuwekwa kwenye mabega ya Alvin na kutoka nje.

Sam alimpa Joseph ishara ya dole gumba. “Unashangaza. Unathubutu kwenda kinyume na Alvin waziwazi. Huna hofu naye?”

“Niko kwenye biashara ya huduma na yeye yuko kwenye biashara za bidhaa. Hata kama anataka kuniangamiza, itachukua mipango fulani na muda mrefu. Haitakuwa rahisi hivyo.” Joseph aliinua mabega yake kwa utulivu.

"Ni mbaya sana kama utakuwa unamwigizia tu?" Sam alionyesha wasiwasi.

“Kwanini unasema naigiza? Sionekani kuwa serious kuhusu hilo?” Joseph aliinua nyusi zake kwa namna ya kutania.

Sam alishikwa na butwaa. “Hapana… Ina maana uko serious kabisa?”

"Wanaume siku zote hutamani wanawake warembo," Joseph alisema huku akitabasamu, "Ingawa najua kuwa siwezi kuwa naye, haibadilishi ukweli kwamba anaweza kuwa mpenzi wangu."
•••
Lisa alitupwa ndani ya gari na Alvin. Alipoanguka, ni kana kwamba viungo vyake vilikuwa karibu kuvunjika pia. Kiatu kimoja kwenye mguu wake kilianguka nje ya gari alipotupwa kama furushi.

“Kiatu changu…” Lisa alinyanyuka kukichukua lakini alimsikia tu Alvin akifunga mlango kwa nguvu. Mlango ulifungwa haraka, na hakuweza kuufungua hata alipojaribu kiasi gani.

Alvin akaketi kwenye kiti cha dereva. Akakanyaga moto na kuondoka kwa kasi.

“Alvin, simamisha gari. Kiatu changu kilianguka." Lisa alimsogelea na kumvuta.

“Usijaribu kunihadaa. Najua unataka tu kurudi kumtafuta Joseph, sivyo?” Alvin alikuwa na moto mkali ndani yake."Lisa Jones, kwanini wewe ni mtu mbaya hivi? Nilikuwa nikishangaa jinsi ulivyoweza kusaini ushirikiano na Kilimani Group na Ruta Design, na ikawa kwamba ulitegemea sura na mwili wako. Huna aibu?”

"Unasema nini?" Lisa alikodoa macho.

Alvin alidhihaki, “Unahitaji maelezo ya wazi kutoka kwangu? Kwa uwezo wako ninaoujua mimi, Kilimani Group ingeweza kufikiria hata Mawenzi Investments ikiwa hukuwa na maelewano yaliyo kinyume na maadili? Kweli una ujanja fulani juu ya mkono wako. Umemfanya Joseph akuangukie na hata hafikirii kuwa wewe ni mchafu.”

Lisa akashusha pumzi ndefu. Ingawa alijua kwamba hakuna maneno mazuri yanayoweza kutoka katika kinywa chake kibaya, alitaka kumpiga na kiatu chake hadi kufa kwa kumfikiria kwa mawazo hayo machafu.

Kwa kweli, alifanya hivyo. Haraka akavua kiatu kilichobaki kwenye mguu wake na kumpiga usoni bila kusita.


Alvin, ambaye hakufikiria kwamba Lisa angethubutu kufanya hivyo, aligongwa moja kwa moja usoni na soli ya kiatu chake. Gari hata lilitikisika kidogo kwa kukosa udhibiti kwa muda

"Lisa, nadhani lazima uwe umechoka kuishi." Alinyakua kiatu na kukitupa nje ya dirisha kwa hasira. Ikiwa asingekuwa akiendesha gari wakati huo, bila shaka angemfundisha somo.

"Nani alikuambia uniambie maneno machafu kama hayo?" Lisa alijisikia kuridhika ajabu alipoona alama ya kiatu kwenye uso wake mzuri. “Alvin, umepoteza viatu vyangu. Lazima unifidie kwa jozi nyingine."

Alvin alidhihaki, “Kwanini? Unataka nikufidie pea ya viatu uvae mbele ya Sarah na kusema nimekununulia ili umuumize? Lisa, una mipango mzuri sana ya kuudhi."

"Ikiwa hutaki kumuumiza, unapaswa kuniacha niende na usisumbuane nami hapa katikati ya usiku." Lisa alitazama mbele, na haikuonekana kama ilikuwa njia ya kurudi nyumbani kwake.

"Alvin, unanipeleka wapi?"

"Wanawake wasiofaa kama wewe ni afadhali wafungiwe tu ili usiniaibishe na kunidanganya." Lisa alihisi baridi ikifika kwenye mifupa yake. “Unanifungia tena?”

"Umejitakia hili," Alvin alijibu.

Sura ya: 336

Akikumbuka siku ambazo alikuwa amefungwa miaka mitatu iliyopita, Lisa alikimbia mbele na kushika usukani kana kwamba alikuwa mwendawazimu.

“Lisa, wewe ni kichaa! Achia usukani haraka…!” Alvin aliufungua mkono kumsukuma.

Lakini, Lisa wa sasa hakuweza kuzuiliwa kwa urahisi ikilinganishwa na miaka mitatu iliyopita. Usukani ulinyongwa bila mpangilio. Mmoja akinyonga kushoto na mwingine kulia. Hatimaye, Lisa aliuma sikio lake. Alvin aligeuza usukani ghafla na karibu kugonga kitalu cha maua kando ya barabara. Mguu wake ukaubana ili kukanyaga moto kwa nguvu.

"Lisa, acha haraka!" Alvin alishtuka baada ya kuona gari likipita juu ya vitalu vya maua, likielekea ukutani. Alvin, ambaye alikuwa amepagawa kwa maumivu baada ya kung’atwa, alishtuka. Haraka akakanyaga breki.

Lisa kwa siri alishika sehemu zake nyeti. Hilo lilimfanya Alvin alie kwa uchungu. “Alvin, sitaki tena kufungiwa na wewe. Wakati huu, tutakufa pamoja." Lisa alimtazama kwa macho ya kichaa na ya kizembe.

Alvin alishikwa na butwaa. Mshindo mkubwa ukasikika hatimaye! Kulikuwa na sauti kubwa ya mshtuko baada ya gari kugonga ukutani. Madirisha yalivunjwavunjwa. Mifuko ya hewa ya usalama ilitanuka na kubana pande zote mbili kwenye kiti cha dereva na abiria.

Alvin alihisi ubongo wake kupigwa na kusababisha mtikisiko. Alikuwa anahisi kizunguzungu. Wakati huo, aliona macho ya Lisa yenye kung'aa lakini meusi yakiwa yamejawa na furaha, kama fataki za rangi zikichanua kwenye anga la usiku lenye nyota. Alipotabasamu, mchiriziko wa damu ulitiririka kwenye paji la uso wake. Macho ya Alvin yalimtoka.

Kwa namna fulani, alihisi kama kitu kifuani kilikuwa karibu kupasuka kwa maumivu. Alihisi uchungu sana hadi hakuweza kupumua kawaida. Maumivu yalikuwa makali sana. Alihisi hata macho yake yakimsisimka kana kwamba kulikuwa na majimaji yanayokaribia kutoka ndani yake. Ilionekana kama ... alitamani sana afe. Alikuwa amedhamiria sana kumfanya afe.

Alisikia watu wakipiga kelele kutoka nje ya gari.

"Ajali imetokea!"

“Pigia gari la wagonjwa!”

•••
“Beep, beep!” Sauti ya kidhibiti moyo ilisikika mfululizo. Alvin aliweza kusikia sauti ya kilio tu pembeni ya masikio yake.Alijitahidi kufumbua macho na kuuona uso wa Sarah uliokuwa na michirizi ya machozi.

"Alvinic, umeamka." Sarah akasimama mara moja.

Rodney na Chester waliingia kwa wakati mmoja.

Wakati akiwatazama, tukio la mwisho kabla hajapoteza fahamu lilimjia kichwani. Akafoka kwa silika, "Lisa yuko wapi?"

Uso wa Sarah wenye michirizi ya machozi ukakakamaa. Rodney alisema kwa hasira, “Bado una ujasiri wa kuuliza juu yake? Alvin, ulimdanganya Sarah eti una kikao lakini ulienda kumtafuta Lisa badala yake. Ulikuwa unajaribu kufanya nini? Polisi walikagua kamera za uchunguzi. Walisema nyinyi wawili mmegombana kwenye gari na ndio maana mlishindwa kulidhibiti gari, na kugonga ukuta. Ukweli kwamba alijaribu kukupokonya usukani ulipokuwa ukiendesha alimaanisha kwamba alitaka ufe. Polisi watamchunguza. Atahukumiwa atakapopata nafuu.”

Alvin alikuwa amebana midomo. Kwa namna fulani, tukio kabla ya kupoteza fahamu liliendelea kujirudia kichwani mwake. Macho ya Lisa yalikuwa yamechongwa sana akilini mwake.

"Alvinic," Sarah alimwita kwa sauti ya chini kwa koo kali.

Alirudi kwenye fahamu zake haraka. “Sarah, samahani…”

“Alvinic, kwanini ulinidanganya?” Machozi yalimtoka Sarah. “Alvinic, tumekuwa pamoja kwa zaidi ya miaka kumi. Ikiwa huwezi kumwacha Lisa, unapaswa… Unapaswa tu kurudi upande wake.”

"Sarah, unawezaje kusema hivyo?" Rodney alifoka. "Ukiniuliza mimi, nitasema wema wako unakuponza sana, Alvin. Je! unajua kwamba Sarah alikaribia kuzirai alipojua kwamba ulipata ajali? Amekuwa akikutunza bila kula wala kunywa. Amekungoja kwa muda mrefu sana. Ukimsaliti, nitakuwa mtu wa kwanza kuvunja urafiki na wewe.”

"Alvin, kwanini ulikwenda kumtafuta Lisa?" Chester alikuwa akimwangalia Alvin pia.

“Usimwulize maswali zaidi. Mwache apumzike vizuri,” Sarah alisema huku akimshika mkono Alvin. Macho yake yalijawa na dhiki.

Hatia ndani ya moyo wa Alvin ilizidi kuwa nzito. “Samahani, Sarah. Nitafikiria njia ya kupata talaka haraka iwezekanavyo. Hakika nitakuoa mwaka huu.”

“Sawa, nitakusubiri.” Sarah alishusha macho yake.

Alikuwa karibu kwenda wazimu kutokana na wivu. Kwanini Lisa aliendelea kumsumbua? Je, Lisa alilazimika kumlazimisha kufanya jambo la kutisha tena?

Kwa siku tatu zilizofuata, Sarah alimtunza Alvin bila kuondoka upande wake. Siku aliporuhusiwa, alimuona Lisa akishushwa na polisi wawili alipokuwa akishuka. Macho yao yakakutana.

Lisa alimkazia macho. "Alvin, unataka niende jela? Vibaya hivyo!"

Alvin alishikwa na butwaa. Sarah ambaye alirudi kutoka kuchukua dawa alifika na kusema huku akikunja uso, “Sio kwamba tunataka uende jela, lakini umevuka bahari safari hii. Alvinic karibu afe. Mbali na hilo, polisi wanafanya kazi zao kwa mujibu wa itifaki. Ulikiuka sheria kwa kumzuia dereva wakati akiendesha gari.”

"Hujui kwanini nilikuzuia?" Lisa alicheka. Macho yake mazuri yalikuwa tulivu na baridi.

Alvin alikunja uso, huku Sarah akiuzunguka mkono wake. “Alvinic, twende. Mpuuze.”

Kwa pembeni ya macho yake, Alvin alimuona Lisa akiingia kwenye gari la polisi. Alihisi kuudhika.

"Samahani. Lazima ufikiri kwamba mimi ni mbaya sana,” Sarah alisema kwa kujidharau, “ninaogopa sana. Tusipompa somo, ninaogopa kwamba atakuondoa wakati mwingine.”

“Usiongee ujinga.” Alvin akatikisa kichwa.

"Alvinic, kaa mbali naye. Siwezi kuvumilia maumivu ya kukupoteza,” Sarah alisema kwa huzuni.

"Hutanipoteza." Alvin alihema moyoni.

Baada ya dereva kumrudisha Sarah nyumbani, Alvin alienda kwenye kampuni. Alikuwa amechelewesha kazi nyingi sana siku alizolazwa. Alipoingia tu kwenye gari, alipokea simu kutoka kwa polisi. “Bwana Kimaro, samahani, lakini kuna mabadiliko katika kesi ya Bi. Lisa. Tafadhali njoo kituo cha polisi.”

Saa moja baadaye, Alvin alitokea kituo cha polisi. Kwenye kiti kilichokuwa nje ya kituo cha polisi, Lisa alikuwa tayari ameshamaliza duru yake ya mahojiano. Hakuwa na vipodozi vyovyote na alikuwa mtupu kabisa usoni. Nywele zake zilikuwa zimefungwa kwenye fundo moja, zikifunua uso wake mzuri na safi. Alionekana kama mwanafunzi wa chuo kikuu.

Hata hivyo, Alvin bado alikumbuka jinsi alivyoshika usukani na sehemu zake nyeti pia… F*ck, alikuwa na maumivu makali kwa siku chache.

“Habari! Tunakutana tena hivi karibuni." Lisa alimpungia mkono huku akitabasamu.

"Kuna nini?" Alvin alitembea kwa hatua kubwa.

Polisi walicheza rekodi. Sehemu ya mazungumzo yao kutoka walipoanza kurumbana ndani ya baa ya hoteli hadi kwenye gari ilichezwa.

Uso wa Alvin ukawa mkali. Mwanamke huyo alikuwa ameenda mbali na kurekodi wakati huo?

Polisi walisema, “Samahani, Bwana Kimaro. Ningependa tu kukuambia kwamba rekodi hii inajumuisha ushahidi kwamba ulikuwa unakusudia kumteka nyara na kumfunga Bi Jones. Ukweli kwamba Bi Jones alinyakua usukani unaweza kuhesabiwa kama jitihada za kujilinda na sio uhalifu.”

"Badala yake, ninaweza kukushtaki kwa kujaribu kuniteka nyara." Lisa alitabasamu, akionyesha meno yake meupe. "Oh, hata nilikuripoti kwa kutupa vitu nje ya dirisha wakati unaendesha gari."

"Nilitupa nini?" Alvin alishangaa.

“Kiatu changu.” Lisa alimkumbusha.....ITAENDELEA....

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.