JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................333-334
Sura ya: 333
Wakati wa ukaguzi jioni, Lisa alipofika tu katika Idara ya Masoko, alimwona mwanamume akigeuka na kuondoka alipomwona.
"Meneja Halua, si vizuri kumkwepa mwenyekiti wa kampuni unapomuona, sawa?" Lisa alimwita kwa tabasamu la uwongo.
“Mwenyekiti… Mwenyekiti Jones, samahani. Kwa kweli sikukuona.” Meneja Halua alijikaza na kurudi nyuma kuomba msamaha.
"Macho yangu hayako vizuri sana."
"Nadhani sio macho yako tu ambayo hayako vizuri sana lakini mdomo wako pia." Lisa alitabasamu kwa kucheza na kusema, “Kwa mfano…
unajua sana kusema mambo ambayo ni ya uzushi.”
Miguu ya Meneja Halua ilikuwa ikitetemeka kidogo. Alikuwa amefikiria kweli kwamba Mawenzi Investments ingesambaratika au Lisa angefukuzwa nje ya kampuni. Lakini ikatokea ndivyo sivyo.
“Meneja Halua, umefukuzwa kazi. Ondoka mara moja. Ninaamini hutatilia shaka uamuzi wangu kwani tayari umeshapata mtu wa kukuunga mkono. Kampuni inayofuata hakika itakukaribisha." Baada ya Lisa kumnong'oneza sikioni, alipiga hatua za kifahari na kuendelea kuelekea Idara ya Masoko.
Meneja Halua aliuma meno. Aligeuka nyuma na kusema kwa sauti kubwa, “Kuna shida gani hata kama nikiondoka? Bi. Njau anakaribia kuwa mke wa mtu tajiri zaidi nchini Kenya. Baada ya kuondoka mahali hapa, atanipanga kuingia KIM International.”
Wakati msaidizi wa Lisa, Amba alipokuwa karibu kumkemea, Lisa alimgonga begani na kumzuia. "Usipoteze nguvu na muda wako!"
Baada ya wao kuondoka, Amba alisema kwa hasira, “Mwenyekiti Jones, kwanini hukumfundisha somo?”
“Hakuna haja, nimeshafanya hivyo,” Lisa alisema kwa utulivu.
Nusu saa baadaye. Meneja Halua alikuwa karibu kuondoka baada ya kufunga. Hata hivyo, alipofika kwenye milango, kulikuwa na polisi wa kumkamata. “Kampuni yako imetoa ripoti polisi. Unashukiwa kufanya ubadhirifu. Tufuate kituo cha polisi.”
“Sikufanya hivyo! sitaki!” Meneja Halua alipiga kelele. Hapo awali wakati Sarah akiwa ni mwenyekiti, wale ambao walikuwa na msimamo kama wake wangeiba pesa, na kila mtu alifumbia macho. Katika kipindi hicho alipochukua upande wa Sarah, alikuwa ametapeli pesa nyingi sana kwa jina la kampuni. Baada ya Lisa kuingia iliripotiwa kama kesi ya uchunguzi. Angelazimika kwenda jela.
“Acha kukurupuka. Tayari tuna ushahidi thabiti. Twende zetu.”
Meneja Halua alichukuliwa na polisi. Habari zilienea katika kampuni.
Amba alipojua jambo hilo, alikumbuka lile somo alilomaanisha Lisa.
•••
Jioni, gari la kifahari la lilisimama mbele ya jengo la kampuni ya Mawenzi. Lisa akaingia kwenye gari. Alipouona uso wa Joseph Ruta, ambao hakuwa ameuona kwa muda mrefu, alitoa tabasamu la kirafiki.
"Joseph, muda umepita."
Asingesahau kamwe kwamba alikuwa ni Joseph ambaye alimpa kazi wakati alipofungiwa na tasnia ya usanifu wa majengo huko Dar es Salaam wakati huo kutokana na hila za Jones Masawe. Hakutarajia kwamba wangefanya kazi pamoja tena baada ya miaka mitatu.
“Lisa, umekuwa mrembo zaidi. Ninakuona kwa mtazamo mpya.” Joseph alicheka. “Twende. Ili kusherehekea ushirikiano wetu, nitakuandalia chakula.”
“Joseph, mimi ndiye ninayepaswa kukuhudumia. Kampuni yako ndiyo pekee nchini Kenya ambayo ingejitokeza kuniunga mkono,” Lisa alisema kwa unyoofu, “Wewe ndiye mfadhili wangu.”
"Watu wa nje hawajui utambulisho wako kama mkurugenzi wa muundo wa Kilimani Group." Joseph alitania.
"Tuendelee kuweka wasifu wa chini tu." Lisa alisukuma kidole kwenye midomo yake na kufanya sura ya kushangaza. Vicheko vilisikika ndani ya gari.
Saa moja baadaye, gari liliingia uani kwenye hoteli kubwa. Magari machache ya kifahari yalikuwa yameegeshwa uani. Lisa alifahamu hoteli chache zilizotoa huduma nzuri za chakula kama ile. Japo ilikuwa katika eneo lililojitenga, chakula chake kilikuwa na ladha nzuri.
Waliposhuka kwenye gari, kuna mtu alikuja kuwapokea. Alikuwa ni Sam Harrison. Lisa alishangaa kumuona pale maana kumuona Sam maeneo hayo pia ilimaanisha kuwa Alvin na genge lake wangekuwepo pia. Alijikuta anakosa raha ghafla maana kila alipokuwa na wakati mzuri basi Alvin angekuwepo tu ili kumharibia.
“Lisa nilikukumbuka sana. Njoo, nikukumbatie.” Sam alimlaki kwa furaha.
“Bwana Harrison…” Lisa alikunja uso kuonyesha kutofurahishwa kwake.
“Usinifikirie sana Lisa. Najua unahofia kukutana na Alvin na wengine,” Sam akaeleza haraka ili kusafisha hali ya hewa, “nilikuja Nairobi nna Bwana Joseph na hivyo nilimwalika kwa chakula hapa na marafiki zangu. Sikuwa naelewa kama nyie tayati mmekutana na angekuja na wewe hapa!”
“Basi itabidi niondoke, wewe mwenyewe unajua namna mambo yanavyokuwaga nikikutana na genge la Alvin.” Lisa alitoa wasiwasi wake.
“Usijali, mimi nipo nitasuluhisha hilo.” Sama alimtoa wasiwasi.
“Kwani….” Joseph alitaka kuongea kitu lakini kabla hata hajamaliza usemi wake, sauti kali ilisikika.
“Nyie…” Alvin akageuka. Alishangaa kumuona Lisa akitoka na kijana mtanashati. Mwanaume huyo alikuwa amevaa suruali ya jeans na shati la khaki. Nywele zake fupi zilikuwa zimekunjamana kidogo, na alionekana kama mtu mashuhuri—aliyekuwa na mvuto mzuri!
Kwenye mkono wa kijana huyo kulikuwa na mkoba wa wanawake wa rangi ya zambarau, na ni wazi ulikuwa wa Lisa.
Mwanamke huyo… Hawakuwa wametalikiana bado lakini tayari alikuwa akishirikiana na wanaume wengine. Ubaridi ulitanda kwenye macho meusi ya Alvin. Wakati huo, Lisa aliona kundi la watu pia. Alipepesa macho na kumtazama Sam bila la kusema neno. Sama aligusa pua yake kwa unyonge.
Sarah ghafla akasema, “Sam, marafiki uliosema unakuja kuwapokea sasa hivi walikuwa… ndo hawa?”
“Ndiyo.” Sam aliitikia kwa kichwa tu. "Lisa anafahamiana na Bwana Joseph Ruta. Nilikuwa nimepanga nikutane naye kwa chakula. Lakini najua wewe na Lisa hamna maelewano mazuri, kwa hiyo tutaondoka sehemu nyingine.” Akapunga mkono na kuelekea upande wa Lisa.
Cindy alisema kwa kusitasita, “Kwa kuwa kila mtu anamjua mwenzake, hakutakuwa na shida. Kwanini tusiende pamoja kwenye jumba la klabu? Tukiwa wengi zaidi ndivyo inavyopendeza zaidi.”
Macho ya kila mtu mara moja yalitua kwake. Chester alikunja uso huku Alvin akitabasamu. “Siyo jambo lisilowezekana. Inatokea kwamba nina kitu nataka kujifunza kutoka kwa Mkurugenzi Jones. Ulianza lini kupanga hila hiyo ya biashara ili kufufua kampuni licha ya kuwa katika hali isiyo na matumaini? Nadhani tukijumuika pamoja itakuwa vizuri zaidi.”
Lisa aliinua macho yake kwa uvivu. Alipotaka kuongea, ghafla alifoka. “Samahani, sikukusikia vizuri, ulikuwa unasema?"
Wakati kila mtu alipofikiri kwamba Alvin alikuwa karibu kuachia hasira yake kwa Lisa, ghafla alitabasamu. "Unafikiri kwamba hali yako itabadilika kwa sababu tu thamani ya soko ya Mawenzi Investments imeongezeka? Lisa, kukuangamiza ni rahisi kama vile kumkanyaga sisimizi chini ya miguu yangu.”
Lisa alisafisha sikio lake kwa kidole. "Nadhani sasa nimeelewa maneno yako, na ninakushukuru sana kwa kweli. Bila wewe kunipa changamoto nisingepata akili hii. Ningekuandalia chakula cha jioni ukipendacho kama shukrani lakini naogopa kundi hili la watu ulilofuatana nalo. Je, ninahitaji kuwahudumia pia? Hata nikiwa na pesa nyingi, hazikuanguka kutoka angani.”
Sarah, Chester, Rodney, na Cindy walichukulia maneno ya Lisa kama dhihaka kwao. Nyuso zao zilibadilika.
Chester alisema kwa sauti isiyo ya kirafiki kabisa. “Lisa, ni miaka mitatu imepita bado haujaonyesha maboresho. Umeuchoka ulimi wako?”
“Kwa kweli siwezi kuthubutu kuwaudhi nyie. Kazi yenu ni kuharibu tu makampuni ya watu wengine na kutishia kukata ndimi zao." Lisa alishtuka na kutikisa kichwa. Akamgeukia Joseph na kusema, “Joseph, twende zetu.”
Joseph? Alvin alimtazama kwa ujeuri. "Wewe ni Mkurugenzi wa Ruta Design?"
Joseph alitabasamu kwa unyonge. Hakukubali wala kukanusha.
Alvin alitikisa kichwa na kusema kwa ukali, “Vema sana, wewe ndiye mtu pekee ambaye unathubutu kwenda kinyume na mimi katika Kenya yote.”
“Lisa nimetoka naye mbali. Kwake, siogopi vitisho vyovyote.” Joseph alitabasamu na kumgeukia Lisa ambaye alishikwa na butwaa. “Twende zetu.”
“Sawa.” Lisa aliondoka naye wakitembea sambamba.
Sura ya: 334
Wakiwa wanatembea kuelekea kwenye gari, mwanga wa mwezi uliwaangazia kana kwamba walikuwa wanandoa wakamilifu. Kifua cha Alvin kilihisi kana kwamba kuna mtu amewasha moto ndani yake. Alikasirika. Sarah alimtazama na kukunja ngumi kwa siri.
“Um…mimi naondoka pia. Tuliahidina na Joseph kuwa na chakula cha jioni pamoja.” Sam aliondoka haraka baada ya kusema.
"Sam hasomeki kabisa siku hizi," Rodney alisema kwa hasira na kuwageukia wenzake, "Bado tunaenda kwenye jumba la klabu kujiburudisha?"
"Inachosha kwenda kwenye jumba la kilabu kila wakati. Sarah, twende zetu nyumbani.” Alvin alifoka na kuingia ndani ya gari.
Muda mfupi baadaye, gari lilisimama mbele ya jumba la kifahari. “Unaweza kutangulia ndani. Nina miadi na mtu mwingine kujadili mambo kadhaa ya kikazi sasa hivi."
“Mbona sikusikia kuwa ulikuwa na miadi hapo awali?” Sarah aliuliza, nusu-utani.
"Nilisahau kukuambia kuhusu hilo hapo awali." Alvin aliwasha sigara. Alionekana kutokuwa na raha kabisa. “Usinisubiri usiku huu. Lala mapema.”
Sarah akauma meno na kujilazimisha kushuka kwenye gari. Alitaka kusema maneno machache zaidi lakini alichosikia ni exhaust ya gari tu.
Alikanyaga miguu kwa kufadhaika. Hakujua ni kwanini, lakini alikuwa na hisia kali kwamba Alvin alikuwa anaenda kumtafuta Lisa.
Nusu saa baadaye, gari la Alvin lilifika kwenye Hoteli ya Silverland.
Sam ndiye aliyependekeza waende hapo. Sam aliipenda baa hii zaidi katika Nairobi nzima ndiyo maana Alvin alijua kulikuwa na nafasi kubwa sana ya kuwakuta hapo.
Alipousukuma mlango na kuingia ndani, sauti ya kupasua anga ilisikika ikiimba.
🎶'"Ingawa rohoni nimekwisha….
Namuomba Mola anisaidie…
Niweze kukusahau kabisaaa …
Nipate mwingine kushinda weweee "🎵🎵
Alvin akatazama katikati ya ukumbi wa baa. Mwanamke kijana mwenye nywele ndefu zilizomwagika alikuwa ameketi kwenye kiti kirefu. Kichwa chake kilikuwa chini na alikuwa akiimba kwenye kipaza sauti. Alikuwa amevaa suruali ya jeans ya buluu. Mguu wake mmoja uliegemea kwenye kiti kirefu huku mguu wake mwingine ukigusa chini. Alikuwa amevaa jozi ya viatu vya turubai vyenye rangi nyeusi na nyeupe ambavyo vilifichua sehemu ya vifundo vyake vya mguu vilivyo maridadi.
Mwangaza hafifu wa taa za rangi ulioanguka juu yake ulikuwa kama maua ya waridi yaliyochanua usiku. Alishika gitaa la acoustic na kutekenya nyuzi zake kwa vidole vyake vyembamba.
Wanaume walivutiwa na uzuri wake.
Wanawake walipiga mayowe kwa sauti nzuri iliyomtoka.
"Kila mtu, wacha tuimbe pamoja." Lisa alisimama kutoka kwenye kiti kirefu. Kasi aliyokuwa akiipiga gitaa ilikuwa inaendana na kasi ya wimbo. Ujuzi wake haukuwa mkubwa sana na wala si duni sana, lakini wimbo ulivutia sana.
Banio la nywele lilitoka nyuma ya sikio lake na nywele zikasambaa kufunika uso wake mzima. Alizirudisha nyuma kwa kutingisha kichwa chake, akifunua uso wake wa kushangaza na wa kuvutia. Uso huo mdogo uling'aa chini ya mwanga hafifu wa rangi, na ilikuwa kana kwamba nyota bilioni zilikuwa zikimulika machoni pake.
Miguu ya Alvin ilikuwa imekwama palepale. Lisa alionekana kama amesimama kwenye jukwaa la tamasha. Mwili wake mzima ulionekana kung'aa. Hakujua kuwa uimbaji wake ulikuwa wa sauti na ustadi zaidi kuliko hata baadhi ya wasanii maarufu. Hakujua kuwa Lisa ndiye alikuwa mwalimu wa Cindy enzi hizo wakiwa shule ya sekondari, akimfundisha kuimba na kumtungia nyimbo pia. Hakujua kuwa angeweza kucheza gitaa pia. Hakuwahi kugundua kuwa anaonekana mrembo sana alipotkuwa akiimba na kucheza jukwaani huku akitabasamu.
Moyo wake ulipiga kwa nguvu. Wimbo ulipoisha, akabaki akitamani zaidi. Sio yeye tu, bali watazamaji wote walihisi vivyo hivyo.
"Msichana mzuri, uimbaji wako ni mzuri sana. Imba wimbo mmoja zaidi!”
"Ni kweli, unaimba vizuri zaidi kuliko hata wale waimbaji kwenye matamasha ya moja kwa moja."
“Msichana mzuri, mimi ni meneja katika kampuni ya muziki. Unataka kusaini mkataba na sisi?"
“Hakuna haja, naimba kwa ajili ya kujifurahisha tu. Nimechoka, hivyo nitapumzika kwanza.” Lisa alishuka kutoka jukwaani. Ngazi za jukwaa zilikuwa za juu sana, na Joseph akaenda mara moja ili kumsaidia kushuka.
Tukio hilo lilimchoma macho vibaya sana Alvin. Watu waliokuwa karibu nao walianza kunong'ona.
“Huyo lazima awe mpenzi wake. Ninamuonea wivu sana kwa kuwa na pisi kali kama hii, utasema ni mungu wa kike!”
"Ndio, sura yake inaonekana nzuri sijawahi kuona! Kwanini sina bahati kama hiyo?"
Alvin akakunja uso. Alitembea kwa hatua ndefu. Wakati Lisa, ambaye ndo kwanza alikuwa ameketi tu anainua glasi yake ili kunywa mvinyo wake, nguvu kali ilimrudisha nyuma kwa ghafla. Mvinyo mwekundu kwenye glasi ulimwagika kote kwenye fulana nyeupe kifuani mwake.
Sehemu ya shati lake iliyolowa sana ilinasa kifuani mwake, ikionyesha mikunjo yake ya kuvutia na mistari iliyofifia chini.
Lisa alipiga kelele. Aligeuka nyuma kwa hasira na kumuona Alvin akiwa na sura yenye hasira na nyororo. "Alvin, una wazimu?"
Baada ya kumkazia macho, kwa haraka Lisa alichukua kitambaa ili kufuta madoa kwenye shati lake. Hata hivyo, haijalishi aliifuta kwa bidii kiasi gani, bado ilishikamana na kifua chake kwa nguvu. Ilifanya hata matiti yake kuonekana kwa mbali kupitia kitambaa laini cha fulana kilicholowa.
"Vaa hii." Mara moja Joseph alivua shati lake la khaki na yeye akabaki kwenye fulana ya ndani. Alitaka kumfunika Lisa, lakini mikono mikubwa ya Alvin ilimzuia kufanya hivyo. Macho ya kina Alvin yalikuwa yakimtazama kwa onyo.
“Bwana Kimaro, si tayari una mpenzi wako? Unaingilia mambo mengine ambayo hayakuhusu kwanin?” Joseph alitabasamu kwa utulivu.
"Unapaswa kumuuliza Lisa kwanini ninaingilia mambo yake." Alvin akalishika lile shati la Joseph na kulitupa huko. "Tuondoke!"
Alipokuwa akiongea, macho yalimtoka Lisa na kuyafanya macho ya Alvin yakawa na joto. Hakuwahi kutarajia kuwa Lisa angekuwa mrembo kiasi hicho. Akikumbuka kuwa ni yeye ndiye aliyenunua nguo za ndani alizovaa chini, hisia zisizoelezeka zilijaa moyoni mwake.
"Ni bahati mbaya gani niliyopata katika maisha yangu ya mwisho kwamba nililazimika kukutana nawe katika maisha haya?" Sauti yake ya kiburi ilimfanya Lisa kuhisi hasira kali.
"Hilo ndilo ninalotamani pia kujua." Alvin aligundua kuwa mikunjo ya kifua cha Lisa bado inaweza kuonekana kwani fulana yake ilikuwa bado imeshikama na mwili.
Alivua shati lake badala yake na kumlazimisha alivae. Lisa aligoma. Ghafla Alvin alihisi kukasirika na kumsaidia kumvalisha kwa nguvu. Ulaini aliouhisi chini ya mkono wake ulikuwa kama unyoya unaoufurahisha moyo wake......ITAENDELEA....
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
