JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................331-332

Sura ya: 331

Lisa alichokonoa masikio yake kwa vidole na kuhema. "Ninasikitika sana kwa kila mtu pia. Sikujua kwamba kurudi kwangu kungedhuru watu wengi, nitarudi na kufikiria njia zingine."

“Potelea mbali. Usirudi tena.” Mkurugenzi Gumbo alikasirika sana hata hakutaka kumuonyesha adabu yoyote. "Bila shaka, tunaweza kukupa nafasi ikiwa utapiga magoti na kuomba msamaha wa Bwana Kimaro na Bi. Njau."

"Hiyo haiwezekani. Ni afadhali kampuni isambaratike kuliko kuinamisha kichwa changu kwa wapenzi hao wasio na haya.” Lisa kwa ukaidi alisema hivyo na kuondoka huku kukiwa na shutuma za kila mtu.

Alipofika nyumbani, polepole alianza kutengeneza kikombe cha kahawa. Amba alikuwa kwenye hatihati ya kupiga magoti na kumlilia kumsihi ili akamwombe Alvin msamaha.

"Mwenyekiti Jones, makampuni ambayo yalikuwa yanaendelea kufanya kazi pamoja na kampuni yetu yanatishia kuvunja ushirikiano wao. Tafadhali fikiria kumuomba msamaha Bwana Kimaro…”

“Usiwe na haraka.” Lisa alikoroga kahawa yake. "Amba, ninakupa nafasi ya kuruka hadi kileleni sasa."

“Nafasi gani? Una uhakika haitanifanya niporomoke badala yake?” Amba alikuwa karibu kuachia machozi.

Lisa alimpiga jicho kali. Akatoa kadi nyeusi kwenye pochi yake na kumtupia. "Kuna shilingi bilioni sabini ndani yake. Baada ya siku mbili, nunua hisa zote kutoka kwa wanahisa wa Mawenzi Investments.”

Amba karibu adondoke magotini. "Mwenyekiti Jones, kwanini una pesa nyingi kiasi hiki?" Ilikuwa ya ajabu. Ni nini hasa kilikuwa kimempata katika miaka hiyo mitatu?

“Unataka kuchukua nafasi hii, au unataka kuniuliza maswali tu?” Lisa aliuliza.

"Ndio ndio ndio..." Amba alivutiwa kabisa.

"Kwa wakati huu, wanahisa lazima wawe na hofu. Ikiwa kuna mtu aliye tayari kununua hisa, bila shaka ataziuza kwa bei ya chini. Shilingi bilioni sabini za Kenya ni zaidi ya pesa za kutosha.” Lisa alimfafanulia.

“Lakini Bi. Jones, tukinunua hisa, utakuwa mwenye hisa pekee kwenye kampuni. Utakuwa na udhibiti kamili, ndiyo, lakini pindi Kimaro akikandamiza kampuni, Mawenzi Investments haitakuwa na mustakabali. Kwanini unataka kupoteza pesa hizi?”

“Nani alisema hakutakuwa na mustakabali?” Lisa alimtazama kwa pembeni. “Tayari nimewasiliana na kampuni za ujenzi. Ninachukua tu fursa hii kubadilisha muundo wa kampuni. Kuanzia sasa na kuendelea, sitaki kumsikiliza mtu yeyote ambaye anataka kwenda kinyume na mimi katika kampuni.”

Amba alishangaa. Hii ilikuwa mara ya kwanza kuhisi kwamba Lisa alikuwa tofauti na hapo awali.
•••
Usiku, wanaume kadhaa walikusanyika kucheza poker kwenye chumba cha hoteli ya nyota tano. Rodney alicheza kadi ya Mfalme, kisha akaanzisha mada. "Nilisikia kwamba wanahisa wa Mawenzi Investments wanauza hisa zao kwa bei ya kutupa."

Alvin alikuwa akigonga meza bila kujali. "Kuziuza ndio njia pekee ya wao kuzuia hasara zao zaidi. Kampuni hiyo ni lazima ifilisike kabisa. Hakuna mtu anayeweza kumuokoa Lisa wakati huu.

Chester aliwasha sigara. “Hebu fikiria, si umekuwa ukihisi hatia tangu alipokufa kwa miaka hii mitatu? Amefanya nini tena kukukasirisha?”

Vidole vya Alvin vikawa ngumu. Baada ya muda, alisema, “Alinitishia kwa kutumia cheti cha ndoa. Ana hamu ya kifo."

“Huogopi kwamba akikutishia tena, Sarah ata…”

“Haina maana. Hakika ninampa somo muda huu,” Alvin alisema. “Na hana pa kutokea ila kwa kunidondokea na kuniomba msaada wangu.”

"Nilisikia kwamba maeneo muhimu ya ujenzi chini ya Mawenzi Investments yameacha kufanya kazi kwa siku tano. Wamepoteza zaidi ya dola bilioni. Watu wengi walionunua nyumba hizo wanadai kurejeshewa fedha.” Rodney alicheka na kucheza karata yake ya mwisho. "Nimeshinda. Lipa."

Wakati Alvin akitoa pesa zake nje, alitazama simu yake iliyokuwa kando yake bila fahamu. Je, mwanamke huyo hakuwa tayari kupiga simu kuomba msamaha na kukubali makosa yake bado? Hata hivyo, kuomba msamaha ingekuwa bure sasa. Lisa hakupaswa kamwe kumuumiza Sarah.
•••
Kesho yake asubuhi, nyumbani kwa Alvin, wajakazi walitoa kifungua kinywa kwenye meza. Sarah alimimina glasi ya maziwa ya moto kwa Alvin kwa furaha, kisha akasema kwa kusitasita, “Tayari ni siku ya sita. Nadhani Mawenzi Investments inapaswa tu uisamehe Hubby.”

Macho meusi ya Alvin yalimtazama. "Wewe ni mtu mpole sana."

Sarah alicheka kwa uchungu. "Nimefanya kazi huko kwa miaka miwili, baada ya yote."

"Wacha tupate kifungua kinywa." Alvin alimenya yai lililochemshwa kwa ajili yake.

“Alvinic,” Sarah alisema kwa hisia tofauti, “Je, kweli huna hisia na Lisa? Hujawahi kunisindikiza kwenda kununua chupi hapo awali. Nimekuwa nikijaribu kujishawishi siku hizi lakini bado ni ngumu kwangu kukubali. Kila nikifikiria jambo hilo, moyo wangu unauma sana hivi kwamba nashindwa kupumua.”

“Hapana.” Alvin alikanusha waziwazi. "Samahani. Sitafanya tena jambo lolote la kukuudhi.”

“Sawa,” Sarah alijibu huku akitabasamu kwa lazima.

Alvin alikuwa na hisia za huzuni moyoni mwake. Aliapa kumpa adhabu kali zaidi Lisa na kumtendea vyema Sarah.

"Bwana Kimaro, Hisa za Mawenzi Investments zilifikia kikomo mara tu soko la hisa lilipofunguliwa asubuhi ya leo," Hans aliingia ghafla na kusema kwa sauti ya chini.

“Ni nini kinaendelea?” Alvin alimtupia jicho kali.

Hans akapepesa macho. "Saa 7:00 asubuhi ya leo, Kilimani Group ilitangaza ushirikiano na Mawenzi Investments kwenye tovuti yake ya kimataifa."

Sarah alikuwa na hisia mbaya. "Kampuni ya Kilimani Group ni maarufu sana?"

Hans alielezea, "Kilimani Group sio maarufu tu, historia yao inarudi nyuma zaidi. Zaidi ya wasanifu mia moja wa juu kutoka kote Afrika Mashariki wamekusanyika hapo. Kampuni hii ndiyo kampuni ya ujenzi yenye mapato makubwa zaidi Afrika Mashariki na wana sifa kubwa. Kilimani Group imeshiriki katika takriban kila mradi wa kitambo ambao umesifiwa na watu kote hapa nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla. Wakati huo huo, wasanifu wa Kilimani Group wamepokea tuzo zote za kimataifa kwa miaka kumi mfululizo.”

Mkono wa Sarah uliokuwa umeshika uma ulikaza, na yeye mwenyewe hakujitambua. "Kwanini kampuni kama hiyo ifanye kazi na Lisa? Hawaiogopi KIM International?"

Hans akatikisa kichwa. "Kilimani Group mara nyingi hufanya kazi na serikali kwenye nchi hizi za Afrika Mashariki. Hawaogopi mtu wala kampuni yoyote.” Alisita na kusema tena, “Zaidi ya hayo, kampuni ya Ruta Design, inayoongoza huko Uganda na yenye tawi lake Tanzania na hapa Kenya pia imetangaza kuwa wametia saini ushirikiano wa miaka kumi na Mawenzi Investments. Timu ya ujenzi ya Ruta Design iliwekwa kwenye saiti ya ujenzi ya Mawenzi Investments jana usiku.

“Ruta Design?” Sarah alishikwa na hamu ya kupiga kelele. "Hiyo ni kampuni gani ya uwongo? Sijawahi kusikia kabla.”

Hans alimtazama kwa kina. "Ingawa mkurugenzi wa Ruta Design, Joseph Ruta, ni kijana, aliwahi kuwa mmoja wa wasanifu watatu bora huko Uganda. Yeye binafsi alibuni hoteli moja na pekee ya nyota saba huko Uganda. Baada ya hapo, alianzisha kampuni ya usanifu. matawi ya kampuni yake yanaweza kupatikana karibu miji yote mikubwa nchini Uganda, Tanzania na Kenya, na yanaendelea kwa kasi miaka hii. Lazima uwe umesikia kuhusu Mradi wa Kigamboni Satelite City huko Tanzania miaka miwili iliyopita. Ilifanyika kwa ushirikiano na Ruta Design, na likawa eneo la makazi lenye gharama kubwa zaidi nchini Tanzania. Bei yake ni shilingi 140,000 kwa kila futi ya mraba, na watu hata waliingia wazimu kuinunua.”

"Joseph Ruta ... Inaonekana hanifikii kwa chochote." Alvin alicheka, lakini sauti yake ilikuwa ya kujilazimisha kana kwamba chuki ilikuwa ikipita ndani yake. Wale waliokuwa wanamfahamu walijua ni ishara kwamba alikuwa na hasira.

Hans alimkumbusha kwa kuchanganyikiwa, “Bwana Mkubwa, hukumbuki huyu jamaa?”

“Unakumbuka nini?” Alvin aliuliza kwa ukali.

Hans alipumua. “Bi. Lisa alikuwa mfanyakazi katika Ruta Design hapo awali. Joseph alikuwa mwandamizi wake.”

Sura ya: 332

Alvin alipigwa na butwaa. Hakuwa na kumbukumbu yake hata kidogo.
Hata hivyo, kutokana na ugonjwa wake mara ya mwisho, alikuwa amesahau mambo mengi. Ilikuwa kawaida kwamba hakuweza kukumbuka.

"Sijawahi kujua ... Lisa alikuwa na mwandamizi kama huyo." Sarah alikasirika kiasi cha kutaka kutema damu. Hapo awali alifikiria kuwa angeweza kumwangamiza kabisa Lisa wakati huu. Hakutarajia kamwe Lisa kuhusishwa na kampuni kubwa kama hizo za ujenzi.

Mwangaza ulipita machoni pa Sarah. Alifanya kama alikuwa na wasiwasi na akasema, "Hata kama Joseph alikuwa mkuu wa Lisa ... hana uwezo wa kwenda kinyume na Alvinic. Angalia hadhi ya Alvinic.”

Uso wa Alvin ulibadilika sana. Hiyo ilikuwa sawa. Kwanini mtu asiyefahamika kama huyo aende kinyume naye kwa ajili ya Lisa?

“Lisa asingeweza kuuza mwili wake, sivyo?” Sarha alichombeza. Alvin alipomfikiria Lisa kuwa karibu na mwanaume mwingine, alihisi wimbi la hasira isiyoelezeka.

Hans alikosa la kusema. Sarah alikuwa amebobea kabisa katika ustadi wa kuchomekea uchochezi kati ya watu. Hakupaswa kusema chochote.

“Chunguza ni nani hasa alinunua hisa za Mawenzi Investments kwa bei ya chini." Alvin ghafla akakumbuka kitu na kumuamuru Hans.

“Sawa.” Hans akaitikia kwa kichwa. Ilikuwa kazi rahisi. Alitakiwa tu apige simu idara husika ili kupata taarifa hizo. Muda mfupi baadaye, alirudi kwenye chumba cha kulia akiwa na habari kamili. "Watu waliokuwa nyuma ya pazia ambao walikuwa wakinunua hisa walikuwa Lisa na Chris Masunga."

“Ah!” Sarah akatoa macho. Haraka akawa ameelewa kitu. "Lisa alikuwa amepanga tangu mwanzo. Kwa makusudi aliwafanya wanahisa wa Mawenzi Investments kuingiwa na hofu na kisha akanunua hisa zao kwa bei ya chini. Sasa, Mawenzi Investments ni mali ya Chris na yeye. Chris anafanya kazi chini yake."

Mshindo ukasikika! Kijiko kilitupwa kwenye sahani na kikatoa sauti ya wazi na ya kutoboa masikio. Alvin alisimama mara moja na kukipiga teke kiti kilichokuwa mbele yake. Hah! Alikuwa amemchukulia poa kabisa mwanamke huyo. Hapo awali alikusudia kumwangusha bila huruma. Alvin hakuwahi kufikiria kwamba njia zake alizokuwa akizitumia kumwangusha Lisa ndizo zilizomnyanyua mwishowe.

Kabla ya hili, Alvin alikuwa amepoteza mabilioni kadhaa kuwahonga wanahisa wa Mawenzi ili wawe upande wake. Lakini, iliibuka kuwa Lisa alikuwa akinunua hisa za wanahisa hao wasimotii kimya kimya. Aliwaondoa watu kwenye kampuni hiyo ambao hawakufuata maagizo yake na akafanikiwa kuwa mtu pekee aliye madarakani. Thamani ya soko ya kampuni ingepaa kwa urahisi hadi kufikia makumi ya mabilioni kwa kuweza pia kupata ushirikiano wa makampuni yenye sifa nzuri. Lisa, oh Lisa! Alimshangaza sana!

Sarah alikasirika kwa siri kiasi kwamba alikaribia kusaga meno hadi yakavunjika. Hapo awali, alidhani angeweza tu kumfanya Lisa afe, kama miaka mitatu iliyopita. Hata hivyo, hakuthubutu tena kumdharau Lisa.
•••
10:00 asubuhi, Ofisi ya mwenyekiti wa Mawenzi Investments ilikuwa katika machafuko. Mkurugenzi Gumbo alivunja chombo kwa hasira. "Lisa Jones, unacheza na sisi? Kwanini hukutuambia kuwa tayari ulikuwa kwenye mazungumzo na Kilimani Group na Ruta Design tangu mwanzo? Umetutia hofu bila sababu na hata hisa zetu tukauza kwa bei ndogo. Matokeo yake, ulinunua hisa kwa bei nafuu. Wewe ni mkatili sana! Je, Sheryl alizaaje binti mpuuzi kama wewe?”

“Lazima uturudishe hisa zetu. Kama sivyo, haya hayatakuwa na mwisho.” Mkurugenzi Williams alipiga meza kwa nguvu.

“Nimeona sehemu yangu ya watu waovu, lakini sijawahi kukutana na mtu mbaya kama wewe. Mawenzi Investments ilianzishwa na sisi sote.
Badala yake, unafanya chochote kinachohitajika ili kutuhadaa. Kama mtu, unapaswa kuwa na mapungufu fulani ya kimaadili.”

“Bibi mdogo, wewe bado kijana. Usiwe mkatili sana na usichome madaraja yako. La sivyo, ungekuwa umekufa kabla hujajua.”

Akiwa amekabiliwa na karipio na ukosoaji wa wanahisa wale waroho waliouza hisa zao, Lisa alikunywa kahawa polepole kabla ya kukiweka kikombe mezani kwa kishindo kikubwa.

Ofisi ilinyamaza kimya. Lisa aliinua kichwa chake. “Kila mtu anielewe, sikutaka kuwa mtu asiye na huruma lakini wakati wa mkutano wa kwanza niliporudi, niliwaambia nyote kwamba kampuni hii haikupewa jina la familia ya Kimaro. Hata hivyo, nyie bado mliwaabudu Alvin na Sarah kana kwamba ni mababu zenu. Siku chache zilizopita, Alvin na Sarah walikuwa wakinitusi kwenye ukumbi wa kampuni. Ninyi nyote wenye hisa mlikuwa kama mbwa wanaolamba miguuni mwao ili kuwafurahisha. Mliniambia hata nipotee. Kwa kuwa nyote mnapenda kuwalambalamba hao wawili, nendeni mkawatafute basi.”

“Tulifanya hivyo kwa sababu hatukutaka kuwaudhi na kupoteza nguvu ya kampuni. Ilikuwa ni kwa ajili ya kampuni,” Mkurugenzi Gumbo alisema kwa unyonge, “Kama ningejua kwamba tayari ulikuwa umepata kampuni za ujenzi, je, ningekosa aibu hivyo? Nilifanya hivyo kwa ajili ya kampuni."

"Hiyo ni sawa. Tumeifanyia kampuni mengi miaka hii mitatu. Ulikuwa wapi wakati huo?”

"Ikiwa hautaturudishia hisa zetu leo, usifikirie hata kutoka nje ya mlango huu."

“Kweli? Nataka kuona jinsi utakavyonizuia kuondoka.” Lisa alicheka. Ghafla, walinzi zaidi ya 20 waliingia na kuwazunguka wanahisa. Walipoona hali hii, zaidi ya nusu ya kiburi chao kilipungua.
Mkurugenzi Wande alifikiria kitu na kupiga magoti mara moja. "Lisa, tupe wanahisa huruma yako. Sisi ni wazee, tunataka tu kupata bonasi ili kujikimu.”

"Ndio, tutakusikiliza kuanzia leo."

"Tunapaswa kila mmoja kuchukua hatua nyuma na kuweka kipaumbele katika kuleta amani."

Lisa akasugua macho yake. Ilionekana kana kwamba walikuwa wakifanya hivyo kwa njia laini kwa sababu njia ngumu haikufanya kazi.

“Inatosha. Mkurugenzi Wande, ulienda hata kumpa Sarah zawadi jana. Na Mkurugenzi Williams, tayari wewe ni mzee sana, lakini hukuchoka kumfuatafuata nyuma Sarah kama mkia. Sijawahi hata kukusikia ukiiombea kampuni. Ulikuwa ukinifokea tu mbele ya Sarah muda mwingi.

“Si hivyo tu. Mkurugenzi Gumbo, nilikuwa nimeshachukua nafasi hii lakini kwa nini bado ulikuwa unaripoti mambo ya kampuni kwa Alvin kila siku bila kuacha chochote?” Lisa alimfichua kila mmoja wao. Nyuso zao zilikuwa na rangi nyekundu kwa aibu.Hakuna aliyetarajia Lisa kujua kuhusu mienendo yao waziwazi.

“Nimewafukuza nyinyi kutoka kwa bodi ya wakurugenzi kwa sababu mioyo yenu haipo hapa tena. Unataka tu kupata samaki wakubwa kama Alvin na Sarah. Unafikiri kila kitu kitaenda sawa mradi tu unawategemea, sivyo?" Lisa alisema kwa huzuni, "Kwenu, mimi ni mtu asiye na uaminifu wowote. Mnafanya jambo moja mbele yangu na jingine nyuma ya mgongo wangu. Sitaki kuwa na sauti nyingi katika kampuni. Nataka tu sauti yangu mwenyewe isikike. Kuanzia leo na kuendelea, nyinyi hamtakuwa na uhusiano wowote na Mawenzi Investments. Usalama, wafukuzeni wote na msiwaruhusu tena katika siku zijazo."

Walinzi hao walichukua hatua haraka na kuwafukuza wanahisa wote.
Ofisi ikawa tupu mara moja. Chris alisema kwa hisia, “Lisa, unazidi kuwa mwenyekiti sasa. Una nguvu zaidi kuliko mama yako alivyokuwa wakati huo. Najiona duni ikilinganishwa na wewe sasa.”

"Mjomba Chris, kampuni itategemea mimi na wewe kuanzia sasa." Lisa alitabasamu......ITAENDELEA....

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.