JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................307-308

Sura ya: 307

Sam alimtazama Rodney, kisha akawatazama Chester na Alvin waliokuwa kimya. Hakuweza kuelewa ni kwanini walionekana kana kwamba wamevurugwa akili. Ilianza lini? Ilionekana kama kila kitu kilibadilika tangu Sarah atokee.
“Chester, Rodney, ni sawa kwa vile Alvin ni mgonjwa, lakini nyinyi wawili ni watu wa kawaida. Ugonjwa wa Alvin ulipoanza, Lisa alikataa kumuacha. Unajua jinsi alivyoharibika na kufungwa kwenye jela ya Kimaro, na nyinyi wawili hata mlimsifu hapo awali. Ndiyo, hujamfahamu kwa muda mrefu, lakini unapaswa kumuelewa kidogo.” Sam alinguruma kwa hasira. "Wakati huo, ni yeye aliyemchukua Alvin na kuzuia familia ya Kimaro kumtupa katika hospitali ya magonjwa ya akili. Bado sasa, mnamtumpa yeye moja kwa moja. Bado nyinyi ni wanaume?"
Alvin alikunja uso sana. Maneno ya Sam yalionekana kufahamika kwake kidogo. Alijaribu kukumbuka kumbukumbu hizo, lakini kichwa kilimvurugika ghafla, na hakukumbuka chochote tena.
Rodney naye alikunja uso. Sam alimfokea. “Rodney, najua unamlaumu Lisa kwa kumchukua Alvin, lakini alipokutana na Alvin, hakujua kama Alvin aliwahi kuwa na Sarah. Alipojua, aliamini pia kwamba Sara alikuwa amekufa. Ni mke wa Alvin, lakini baada ya kurudi kwa Sarah ulidai aondoke kwa sababu nyie mna uhusiano mzuri na Sarah. Lakini umewahi kujiweka katika viatu vyake? Alipoteza watoto wake na mumewe. Yeye hana chochote alichobakiza. Vipi kuhusu Sarah? Ana wewe. Ana Alvin. Ana wakati ujao mkamilifu.”
Rodney alishangazwa na maneno yake. Macho ya Chester yaliganda kidogo huku akiwasha sigara. Ndiyo, wakati fulani alifikiri kwamba Lisa alikuwa anastahili kuwa na Alvin, lakini, Lisa alipokutana na Charity mara kwa mara alimuudhi sana. Kisha, ni baada ya kifo cha Maurine na kurudi kwa Sarah ambako kulimfanya asahau kwamba alikuwa amemsifu Lisa hapo awali.
“Sam, kwa kawaida sitamruhusu atoke hadi atakapopata nafuu,” Alvin alieleza. Kwa kweli, alikuwa amechanganyikiwa sana.
Sam alipokuwa anataka kuzungumza, mara ghafla simu ya Chester ikaita. Aliijibu, na muda mfupi baadaye, sigara mdomoni ikaanguka kwenye suruali yake na kuchoma tundu ndani yake bila yeye kutambua.
Ni hadi Cindy alipomfagilia sigara hiyo kwa haraka ndipo alipoweka simu yake chini na kusema kwa sauti nzito, “Hospitalini wananitafuta. Lisa Jones amekufa...”
Chumba kilikaa kimya kwa zaidi ya sekunde kumi. Alvin alimtazama Chester na kupata shida kupumua. Ni kana kwamba kilindi cha moyo wake kilichomwa na kisu kikali. "Umesema nini?"
Macho yake yalimtazama Chester. Chester alifungua kinywa chake kwa uso mgumu. "Wauguzi hospitalini walipoenda kumchoma sindano, waligundua kuwa alikuwa amepasua shuka vipande vipande na kujinyonga."
Alvin kichwa kilimshtuka. Kila kitu kilichomzunguka kiligeuka kuwa cheusi. Lisa alikuwa amekufa? Hiyo ingewezaje kutokea?
Alitazama saa yake kujua kama ilikuwa ni Aprili ya Wajinga na kuna mtu alikuwa akimchezea. Lisa alikuwa bado mdogo sana. Kwanini alijinyonga? Hakuamini. Hakuamini kuwa Lisa amekufa.
Alvin alitoka haraka chumbani. Alikimbia hadi hospitali na kumshika mmoja wa madaktari wa idara ya magonjwa ya akili. "Wadi ya Lisa Jones ni chumba gani?"
"Amepelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti."
“Chumba cha kuhifadhia maiti?” Alvin alishusha pumzi, na mng'aro wa hasira ukamtoka machoni. “Kwanini ulimpeleka kwenye chumba cha kuhifadhia maiti?”
Daktari aliogopa sana kwa sura yake ya ukali kiasi kwamba miguu yake ilitetemeka. “Yeye… Alikufa. Ni utaratibu wa kawaida wa hospitali kumpeleka mtu aliyekufa katika chumba cha kuhifadhi maiti.”
Alvin alimtupa pembeni na kukimbilia chumba cha maiti. Alvin aliinua kitambaa cheupe huku mikono yake ikitetemeka, na kumuona Lisa akiwa amelala kimya kimya. Kama asingekuwa na jeraha la kijani kibichi kwenye shingo yake, angeonekana kama alikuwa amelala tu.
Aliweka mkono wake unaotetemeka kwenye pua yake ili kuona kama alikuwa akipumua. Kulikuwa na barafu. Je, alikuwa amekufa kweli? Kisha akapiga kichwa chake kwa nguvu. Ilibidi awe anaota. Hii haikuwa kweli. Mara ya mwisho walipokutana, hata alikuwa akiwakosoa na kuwauma watu. Alikufaje ghafla hivyo?

“Potelea mbali, Alvin.” Nguvu kali ilimvuta kwa nyuma na kumsukumia mbali. Pamela alikimbia kando ya kitanda. Baada ya kuona maiti ya Lisa, alimtazama Alvin kwa hasira. “Yote ni sababu yako, b*star! Wewe ndiye ulimnyanyasa Lisa hadi kifo chake, muuaji wewe!”
“Sikufanya hivyo. Yeye… alikuwa mgonjwa.” Alvin hakutupa hata macho yake yake meusi kwa Pamela. Alibaki palepale huku akimtazama Lisa. Bado hakuweza kukubali kilichokuwa mbele yake.
Hakuweza kujielewa. Hakumpenda Lisa hata kidogo. Hata hivyo, kwanini alihisi kana kwamba nafsi yake ilikuwa imetolewa? Ni kana kwamba alikuwa amepoteza mtu muhimu katika maisha yake? Machozi hata yalimtoka bila kujizuia na kumfanya asione vizuri.
"Wewe ndiye mgonjwa." Huku akiwa na kwikwi, Pamela alimfokea na kumkosoa, "Lisa alikuwa sawa. Wewe ndiye uliyekuwa ukimtesa na kumnyanyasa bila sababu. Ulimsukuma kwa makusudi na kumfanya apoteze watoto wake. Ulimfunga hata katika hospitali ya magonjwa ya akili na kumwondolea uhuru wake wote. Ni wewe na Sarah ndiyo mlimfanya aonekane kichaa. Haijalishi kama hukuwa na hisia kwake. Ungeweza tu kuachana naye. Lakini kwanini ulilazimika kumtelekezana ujauzito wa watoto wako na kisha wewe ukarudi kwa Sara? Kwanini hukumwacha aende zake? Hata hivyo ni sawa. Sasa kwa kuwa amekufa, hatimaye ameachiliwa. Ameachiliwa kutokana na kuteswa na nyie. Nitamchukua. Sitawaruhusu ninyi wanandoa wasio na aibu kuhifadhi maiti yake.” Pamela akashusha pumzi ndefu na kumuomba muuguzi amsogeze Lisa.
"Unafanya nini?" Alvin bila fahamu alishika mkono wake. “Ni mke wangu, kwa hiyo nitashughulikia mazishi yake. Hili halikuhusu.”
“Umewahi kumchukulia kama mke wako? Ni nini kinakupa haki ya kumzika? Mpuuzi wewe!” Pamela akatoa kitambaa kilichokuwa na damu na kukiweka kifuani mwake. “Itazame kwa makini. Lisa aliandika maneno yake ya mwisho juu yake kwa kutumia damu yake mwenyewe. Hataki umzike, na hataki kuzikwa chini ya familia ya Kimaro pia. Anataka tu kukaa mbali nawe.”
Alvin aliduwaa baada ya kuona maneno yale yaliyoandikwa kwa damu. Ina maana, alimchukia sana? Labda ingembidi amwache aende zake. Hata hivyo, hakuweza kufanya hivyo alipomtazama usoni. Hakuweza kuzuia macho yake kutoka kwake. Hakuweza kukubali ukweli kwamba asingemuona tena katika maisha yake.
"Hapana. Huwezi kumuondoa.” Alvin alimzuia Pamela kwa dhamira.
"Alvin, acha tu amchukue Lisa." Ghafla, Bibi Kimaro ilisikika mlangoni.
Ghafla Alvin akageuza kichwa chake na kumuona Mzee Kimaro, Bibi Kimaro, na Jack wamesimama pale. Hakujua walipotokea. Jack alipomuona Lisa alishindwa kujizuia kumpiga Alvin usoni. “Jinsi gani huna aibu kufikiria hata kumzika binti wa watu. Hukumchukulia kama binadamu alipokuwa hai, kwa kuwa sasa amekufa, kwanini usimwachie?”

“Kwa sababu tu sikuingilia mambo yako, uliishia kumsukuma Lisa na kuwaua mapacha. Niligundua tukio hili siku mbili tu zilizopita,” Mzee Kimaro alisema kwa hasira. “Unawezaje kuwa mkatili hivyo? Unaweza kuwa mpenzi kigeugeu, lakini huwezi kumtendea mke wako na watoto kwa njia hii. Hata mama yako hakufika hatua kama hii.”

Sura ya: 308

"Kweli," Bibi Kimaro alisema kwa kukata tamaa. “Mkeo alipokuwa mjamzito, ulimsumbua Sara mchana kutwa na usiku kucha. Sio tu kwamba ulimpuuza, lakini pia ulimfunga na kumsababishia kuishia katika hospitali ya magonjwa ya akili. Umepitia hospitali ya magonjwa ya akili ulipokuwa mdogo pia. Unawezaje kufanya jambo lisilo la moyo kama hilo? Tayari amekufa, lakini unakataa kumwachilia. Unapanga kumwonyesha jinsi unavyopendana na Sarah kwenye mazishi yake mwenyewe?"
“Tafadhali, nakuomba, mwache aende zake." Pamela ghafla alipiga magoti na kulia kwa uchungu. "Hakuwa na furaha na wakati wake wote hapa Nairobi. Ningependa kumrudisha Dar es Salaam, kule alikotoka.”
“Mwondoe.” Mzee Kimaro alitikisa mkono wake. Huenda hakumpenda Lisa hapo mwanzo, lakini wakati wa muda wao pamoja siku za mwishoni mwishoni, alianza kumpenda kwa utii wake. “Ulimtesa sana binti wa watu alipokuwa hai. Kwa kuwa sasa amekufa, mwacheni tu, mwache aende kwa amani.”
Bibi Kimaro alisema kwa uchungu, "Alvin, sielewi kwanini umekuwa mkatili hivi siku za karibuni."
Hapo hapo, kifua cha Alvin kikamshikana. Je, alikuwa mkatili? Je, alikosea?Hakuwa na maana ya kumfungia Lisa. Alikuwa chini ya hisia kwamba alikuwa na huzuni.
Hapo awali alikuwa amefikiria kumpa kiasi cha pesa ambacho kilimtosha kutumia maishani mwake na kumfanya aondoke baada ya kujifungua watoto. Lakini, kwanini alikufa vibaya hivyo? Alvin alikuwa ameganda palepale. Mwishowe, Pamela alimchukua Lisa.
Tukio la kukutana kwa mara ya kwanza na Lisa lilimpita akilini na kuendelea kujirudia kichwani mwa Alvin.
“Kweli mimi ni mgonjwa, nina kichaa. Ninaumwa kichaa cha mapenzi!”
"Mvulana mzuri, unaonekana kupendeza sana huku macho yako yakiwa yamefumbwa hivi kwamba unawafanya wanawake washindwe kujizuia."
"Nataka kukuoa."
“Naapa kuanzia sasa nitakutendea mema tu, na nitakuahidi kila nilichosema. ..
Kwa kweli, aliwahi kuwa mrembo sana na mrembo kama vixen mdogo. Kwa hiyo alianza lini kumchukia, hasa alipomwona? Je, yeye ndiye aliyemsababisha ajinyonge? Wakati huo, Alvin alichanganyikiwa mpaka mwisho wa akili zake. Hakukumbuka hata jinsi alivyotoka hospitalini.
Hapo ndipo Sara alipotokea mbele yake, na macho yake mekundu yakajawa na hatia. "Ni kosa langu. Nilifikiri alikuwa anaugua mshuko wa moyo kidogo. Sikujua kuwa hali yake ilikuwa mbaya sana. Asilimia 15 ya watu wanaopatikana na unyogovu wa moyo huishia kujiua. Nilipaswa kumtendea vyema. Samahani."
Hata hivyo, Alvin moja kwa moja alimpita Sarah kana kwamba hakumsikia. Alichokuwa nacho akilini mwake ni sura ya Lisa iliyokufa huku macho yake yakiwa yamefumba. Alikuwa akifanya nini alipokufa?
“Alvinic…” Sarah alinyoosha mkono wake kumshika.
Alvin aliinua mkono wake kwa nguvu ili kujinasua kutoka kwenye mshiko wake. Alimtazama kwa hasira na kusema, “Imetosha. Baada ya yote, yote yamesababishwa na Thomas. Ikiwa asingefanya hivyo, Pamela asingejiingiza kwenye matatizo, na nisingemfunga Lisa. Ugonjwa wa Lisa usingekuwa mbaya zaidi, na asingefikiria kuniua. Watoto wasingepoteza maisha yao pia. Sikupaswa kumsaidia.”
Ilikuwa ni kwa sababu ya Thomas kwamba alipoteza mapacha pamoja na Lisa. Ghafla, alianza kutilia shaka. Je, Mungu alikuwa akimuadhibu Alvin kwa kumsaidia Thomas?
“Samahani. Sikutarajia ingekuwa hivi.” Sarah aliogopa kuona sura yake ya hasira. Hakuwahi kumuona Alvin akionekana kutisha kiasi hicho.
Ikiwa hilo lingetokea kabla ya hapo, angehisi hatia mara moja kwa kuwa mkali kwake. Lakini, hakuweza kuvumilia kifo cha Lisa. “Ndio. Hukutarajia kwa sababu unachofikiria ni kumwendekeza Thomas tu. Ameua watu wangapi kwa miaka yote?"
Lisa alikuwa sahihi. Alvin aliona maisha ya kila mtu hayana thamani isipokuwa ya Sarah. Hata alivuka msingi wake wa maadili kwa ajili yake tena na tena.
"Alvinic, mimi ndiye wa kulaumiwa kwa hilo. Ni kosa langu." Sarah alipiga magoti na kulia kwa jazba. "Kwa kweli sikutarajia mambo kuwa hivi."
“Naomba uondoke sasa. Nataka kutumia muda wangu peke yangu.” Alvin aliingia kwenye gari mara moja bila hata kumtazama. Hii ilikuwa mara yake ya kwanza kumtendea Sarah bila kujali tangu arudi.

Sarah aliinua kichwa chake taratibu na kulitazama gari hilo likitokomea kwa mbali. Akasaga meno na kukunja ngumi. Hakuwahi kufikiria kwamba Alvin angepoteza utulivu wake kwa sababu ya kifo cha Lisa. Ikizingatiwa kuwa alimlawiti Alvin kisaikolojia, hakupaswa kuwa na hisia na Lisa. Kwa mwonekano wake, alikuwa amedharau upendo wa Lisa kwake. Kwa bahati nzuri, Lisa alikuwa amekufa. Kusingekuwa na mtu ambaye angeweza kuchukua nafasi yake tena!
Ghafla, Thomas akampigia simu. "Sarah, kweli Lisa amekufa?"
“Ndiyo.”
“Hiyo ni ajabu. Kwa hiyo hivi karibuni, utakuwa Bi Kimaro halali?” Thomas alifurahi. Huku Sarah akiwa tegemeo lake, angeweza kuomba na kupewa chochote katika siku zijazo.
"Afadhali ujiangalie mwenyewe," Sarah alijibu kwa ukali, "Alvinic anakulaumu kwa kifo cha Lisa. Nadhani hatajisumbua kuhusu wewe tena.”
"Nini? Lazima utakuwa unatania.” Baada ya kuhisi wasiwasi kwa muda, Thomas alitabasamu na kusema, “Bwana Kimaro anakujali zaidi. Jitahidi tu kumpa mahaba mazito, na muda si muda atasahau jambo hilo.”
Sarah kichwa kilimuuma. Kwanini alikuwa na kaka asiyejitambua kiasi hicho? Kama si kaka yake wa tumbo moja, asingemjali. "Ninakuonya, chunga tabia yako kuanzia sasa. Siku moja utajikuta huna msaada."
Baada ya kukata simu, Sarah aliendesha gari hadi jela moja kwa moja.
Punde, Charity akatoka nje. Sarah alikuwa amewaomba baadhi ya watu waliokuwa jela kumshughulikia Charity, lakini alikuwa mgumu na mcheza karate mzuri kiasi kwamba hawakuweza kumfanya chochote. Kwa hivyo, alikuwa akiishi maisha mazuri gerezani. Ingawa alikuwa amekonda, alionekana bora zaidi.
Ndani ya moyo wake, Sarah alikuwa akihema kwa hasira. Hata hivyo, alipompiga picha Charity na kuhisi kuwa alikuwa amegundua mawazo yake, alitabasamu. "Inaonekana umekuwa ukiishi vizuri gerezani."
"Unajaribu kufanya nini tena?" Sura ya Charity ikaonekana kukasirika. Kama angejua ni Sara, asingetoka nje.
“Hakuna aliyekutembelea hivi karibuni, sivyo? Kwa hiyo nimekuja kukuambia jambo fulani kutokana na wema wa moyo wangu.” Sarah alitabasamu na kusema, “Rafiki yako mkubwa, Lisa, amefariki leo.
Charity alitetemeka, lakini muda mfupi baadaye, alicheka na kusema, “Acha kuongea upuuzi. Lisa yuko sawa. Alikuja tu na kunitembelea muda si mrefu uliopita.”
“Sisemi uongo. Amekufa kweli. Alijiua.” Sarah alikuwa akichezea kucha zake, ambazo zilikuwa zimetoka kubandikwa. "Hivi karibuni nitakuwa mke mpya wa Alvin."
“Sitakuamini.” Charity akatikisa kichwa. Lisa alikuwa mwanamke mzuri na mwenye afya njemaI, kwanini angejiua? Alichosema Sarah kilionekana ni ujinga tu kwake....ITAENDELEA.....

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.