JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................305-306
Sura ya: 305
"Lisa Jones, bora uendelee kukaa. Hakuna kinachopaswa kutokea kwa watoto." Alvin alimnyanyua na kukimbilia hospitalini. Mwanamke mikononi mwake alikuwa na mimba ya miezi mitatu, lakini alikuwa mwepesi kama manyoya. Ni kana kwamba angeweza kuelea wakati wowote.
Moyo wake ulihisi kama kuna kitu kinaubana. Hakuweza kujua ni nini, lakini ilionekana kama hofu na kwamba alikuwa akipoteza kitu chake cha tahamani zaidi. Hata hivyo, Lisa alifumba taratibu macho yake yaliyochoka kana kwamba hakumsikia.
Punde si punde, Lisa alisukumwa kuingia Emergrncy Room. Alvin alitembea huku na kule nje ya mlango huku damu zikimtiririka kwenye paji la uso wake.
Hans alionekana kukosa amani. "Bwana Mkubwa, kwanini usifunge paji la uso wako kwanza?"
"Achana nao tu." Mikono ya Alvin iliyotapakaa damu ilikuwa ikitetemeka bila kukoma. Alionyesha uwepo wa hasira na kuchanganyikiwa.
Haikuchukua muda mlango wa chumba cha upasuaji kufunguliwa. Daktari akatoka. “Bwana Alvin, watoto wawili wa mgonjwa hawawezi kuokolewa. Ni lazima utie sahihi hii mara moja ili atoe mimba. Vinginevyo, hata maisha ya mama yatakuwa hatarini.”
"Unasema nini?” Alvin alishikwa na bumbuwazi. “Watoto hawawezi kuokolewa? Wewe ni bure kabisa. Umesomea wapi udaktari wako?" Alvin alimshika dokta kola kwa hasira huku macho yakiwa mekundu.
Hao walikuwa watoto wake. Laiti si kwa wakati huu, asingejua ni kiasi gani aliwajali wale watoto wawili.
“Bwana Kimaro, kwa kweli hata kama angepelekwa wapi bado haitakuwa na masaada wowote. Itakuwa sawa na daktari yeyote,” daktari alieleza kwa woga. “Vitoto tumboni mwa mama yao vilikuwa tayari vimeyumba sana alipokuwa na ujauzito wa mwezi mmoja, na hajawa katika hali nzuri siku hizi pia kutokana na kiwewe. Tayari kulikuwa na dalili za kuharibika kwa mimba hapo awali, na alikuwa amebeba mapacha. Kwa kweli nimejaribu niwezavyo.”
Mapacha! Mapacha wake walikuwa wamekwenda. Alikuwa amewasukuma kwa mikono yake mwenyewe. Alvin kwa unyonge akamuachia daktari. Uso wake mzuri ulionekana kuvunjika moyo katika mwanga uliofifia. Tayari alikuwa amepoteza damu nyingi, na wakati huo, alihisi kizunguzungu cha ghafla ambacho kilimuumiza sana kichwa.
"Alvinic, umepoteza damu nyingi." Sarah alimkimbilia ghafla na kumnyanyua kwa haraka. “Wacha nikufunge jeraha lako.” Alvin kwa hali ya kawaida alitaka kukataa, lakini maneno ya Sarah yalikuwa kama kamba iliyomvuta kwa nguvu. Akili yake ilikwenda tupu, na akamfuata bila kujua.
Daktari alisema kwa wasiwasi, “Bwana Kimaro, hii saini ya…”
“Hans, nitakuachia hili.” Alvin akamwambia Hans. Sarah akamvuta Alvin harakaharaka hadi kwenye chumba cha matibabu.
Akiwa amekunja uso, Hans alitia sahihi haraka karatasi za daktari. “Si lazima useme… Kuwaokoa mama na watoto ni muhimu zaidi."
“Bila shaka.” Daktari alikimbia tena ndani ya ER ili kumuokoa Lisa.
Macho ya Lisa yalikuwa na uchungu sana hata hakuweza kuyafungua. Hata hivyo, hakuwa amepoteza fahamu kabisa. Masikio yake yangeweza kusikiliza mazungumzo ya madaktari.
“Nilisikia Bwana Kimaro amepata penzi jipya, lakini sikuamini mpaka nilipojionea leo. Nimeshtushwa sana."
“Ndiyo, inasikitisha sana. Mkewe yuko hatarini, lakini hakutia sahihi hata karatasi. Hajali iwapo mke wake ataishi au kufa.”
“Je, hiyo ni kweli?"
“Nawezaje kusema uongo? Ikiwa Msaidizi wake hakutia saini, sidhani kama kuna mtu angemjali.”
“Pia nilimwona Bwana Kimaro na yule mwanamke wakiondoka wakiwa wamekumbatiana."
Lisa alipumua kwa nguvu! Chozi lilidondoka kwenye kona ya macho yake. Ha! Alvin Kimaro, wewe ni mkatili sana! Ilibainika kuwa alikataa hata kusaini jina lake wakati maisha yake yalikuwa hatarini. Kwake, thamani ya maisha yake kwa Alvin ilikuwa ndogo kuliko hata ya ombaomba wa mitaani. Hata wakati huo, kulikuwa na Sara tu moyoni mwake. Mapenzi yoyote aliyokuwa nayo kwake yalionekana kugeuka mavumbi na kutoweka kabisa. Kuanzia muda huo na kuendelea, maadamu bado alikuwa hai na anapumua, alikuwa na chuki tu na wapenzi hao wadanganyifu.
Katika wodi, Lisa alifungua macho yake. Sarah alikuwa amesimama wodini peke yake, akitabasamu na kucheza na ufunguo wa gari mkononi mwake. “Unaona hii? Hili ndilo gari la kifahari la kipee nchini ambalo Alvinic alikupa mara ya mwisho, lakini pleti namba yake imebadilishwa hadi AKLSN. ‘Alvin Kimaro Loves Sarah Njau’. Imekaa vizuri, eeh?"
Lisa aliitambua kwa haraka. Alvin aliwahi kumpa funguo hizo za gari, na plate namba ya kipekee ya gari wakati huo ikawa mada moto kwenye Mtandao. Iliwafanya wanawake wengi kuwa na wivu.
Lisa alitabasamu kwa utulivu. “Unapenda tu kuokota mabaki ya watu. Magari, majengo ya kifahari, wanaume. Hakika, wachukue wote. hata hivyo sijali.”
"Kwa hivyo ikiwa unajali? Mimi ndiye pekee katika moyo wa Alvin.” Sarah akasogea hadi kitandani na kumtazama kwa unyonge kutoka juu. “Angalia. Nilichofanya ni kusema neno moja tu. Kwa hivyo vipi ikiwa rafiki yako wa karibu angebakwa? Ndugu yangu alitoka bila dhamana, lakini rafiki yako wa karibu hakuwa na bahati. Amedhalilishwa na kuwa kama panya wa mitaani. Sifa yake imeharibiwa, lakini anastahili. Ni kosa lake kunitukana hospitali hapo awali.”
"Ulijua kuwa Thomas atamdhuru?" Macho mekundu ya Lisa yalimtoka.
“Duh.” Sarah akainama huku tabasamu likiwa limejikunja kwenye kona za mdomo wake. "Ni aibu iliyoje kwamba hatua ya mwisho haikufaulu, lakini haijalishi. Hata hivyo hakuna mwanaume atakayemtaka tena.”
Lisa alikasirika sana hadi kifua kilimvimba. Akiwa ametoka tu kwenye upasuaji, alitetemeka kwa maumivu. “Wewe b*tch…”
Sarah alitazama sura yake ya uchungu na kutabasamu kwa ushindi zaidi. “Nilisahau kukuambia, lakini nilimuua Jennifer Musyoka pia. Ni huruma kwamba polisi hawatawahi kupata ushahidi.”
“Ni wewe?...” Lisa hakuweza kujizuia kunyakua kikombe cha maji ya moto pembeni na kumwagia Sarah.
Mara Sarah akapiga kelele na kukwepa haraka, Alvin akaingia ndani kwa kasi, alikasirika sana baada ya kuona maji kwenye nguo za Sarah.
“Wewe kichaa. Sara alikutunza kutokana na wema wa moyo wake lakini bado huthamini wema wake. Nadhani unapaswa kupelekwa katika hospitali ya magonjwa ya akili." Sauti na macho ya Alvin yalikuwa yamejaa chuki.
“Nakushukuru sana kwa wema wako. Unapaswa kumruhusu akutunze badala yake. Sitaki kamwe kuwaona nyinyi wawili maishani mwangu.” Lisa alifunga macho yake. Alikuwa na wasiwasi kwamba kweli angepandwa na hasira ikiwa angewatazama kwa muda mrefu zaidi.
"Alvinic, kulingana na uzoefu wangu wa miaka mingi, nadhani anaweza kuwa amepata unyogovu wa moyo. La sivyo, asingetuumiza mimi na wewe. Haijalishi ataniumiza, lakini ninaogopa kwamba kwa hali yake ya sasa, anaweza kuwaumiza wengine pia,” Sarah alisema kwa wasiwasi.
Alvin aliganda. Kikumbusho hicho kilimfanya atambue kwamba kweli Lisa alikuwa akipatwa na kichaa sana tangu alivyoonekana siku za karibuni. Kwanza, alijaribu kumchoma kisu na kumpiga kwa chupa ya glasi. Sasa, hata alimmwagia Sarah maji ya moto. Kwa kuzingatia hayo, pamoja na ukweli kwamba Sarah alikuwa mwanasaikolojia maarufu, vilimfanya awe na shaka pia.
Sura ya 306
“Sarah Njau, usifanye mzaha. Mimi si mgonjwa. Hali yangu ya akili ni timamu sana.” Lisa alipoona jinsi Alvin alivyokuwa kimya, ghafla alihisi kukosa amani. Kwa hiyo, alieleza kwa haraka, “Msitake kuniudhi zaidi.”
Sarah alimtazama kwa macho ya huruma. “Hakuna kichaa yoyote ambaye amewahi kukubali ugonjwa wake. Isitoshe, ulipata mimba pia ukiwa na hali hiyo. Nakushauri upate matibabu haraka iwezekanavyo.”
Lisa hakutaka kitu zaidi ya kuinuka na kumpasua Sarah usoni kwa pumzi yake ya mwisho. Hata hivyo, alijua kwamba Alvin angemwamini zaidi Sarah ikiwa angepandisha hasira zaidi. “Sarah Njau, Alvin tayari ni wako, na unaweza kuchukua nafasi ya Bibi Kimaro pia. Lakini kwanini huwezi kuniacha niende? Ninawaomba nyote wawili mniruhusu niende, sawa? Ninaahidi kwamba nitakuepuka kila wakati nikikuona katika siku zijazo.”
Alvin alikunja uso bila fahamu. Kimantiki, alimchukia Lisa, lakini wazo la kumkwepa lilimfanya akose furaha isiyoelezeka.
Sarah alitabasamu kwa uchungu. “Nawezaje kukufanya uelewe hili? Huenda usijitambue, lakini itaharibu maisha yako yote ikiwa hautatibiwa. Mbali na hilo, wewe bado ni mke wa zamani wa Alvinic. Ikiwa habari itaenea, wengine wangemwonaje?”
Uso wa Alvin ullilegea ghafla. “Inatosha. Kwanini hutaki kuamini kama wewe ni mgonjwa?”
Lisa karibu kupasuka kwa hasira kwa sababu ya Sarah. Alilia kwa uchungu. “Nini nilikukosea katika maisha yangu ya nyuma? Kupoteza watoto wangu tayari kumenisikitisha sana, lakini sasa unataka kuniweka katika hospitali ya magonjwa ya akili? Alvin Kimaro, sijali kama hunipendi, lakini tafadhali nichukulie kama binadamu.”
"Si lazima uende kwenye hospitali ya wagonjwa wa akili, lakini huwezi kuondoka kwa sasa. Itabidi unywe dawa kila siku,” Sarah alimfariji kwa upole.
“Mimi ni mzima wa afya. Sihitaji dawa hata kidogo.” Lisa alijitetea.
“Ni kupoteza muda kujaribu kuzungumza na wewe.” Sarah kisha akamgeukia Alvin. "Alvinic, tunapaswa kuchukua hatua kabla hali yake haijawa mbaya. Tunapaswa kumsaidia. Wewe pia umewahi kuwa na ugonjwa huu hapo awali. Unapaswa kujua jinsi ugonjwa wa akili unavyoweza kuwa na madhara.”
Lisa aliitazama sura ya mwanaume huyo na ghafla aliingiwa na hali ya kutokuwa na utulivu.
“Basi, hebu tumtendee wema kwa sasa. Mkabidhi kwa wataalam wa magonjwa ya akili kwa muda. Ikiwa hali itakuwa mbaya, tutamhamisha hadi hospitali ya magonjwa ya akili." Baada ya hapo, Alvin aliondoka.
“Alvin Kimaro, simama hapo ulipo…” Lisa hakuweza kukubaliana na hali hiyo, hivyo akainuka haraka kitandani. Hata hivyo, mara tu miguu yake ilipotua chini, maumivu makali kwenye sehemu ya chini ya mwili wake yalimfanya aanguke tena. Alitazama juu tu na kuona mwonekano wa Alvin ukiondoka.
Sarah akainama na kunong’ona, “Nitazungumza na madaktari hapa. Ugonjwa wako utakuwa mbaya zaidi na hatari zaidi. Hatima yako itakuwa tu kwenda hospitali ya magonjwa ya akili."
"Sarah Njau, nenda kuzimu ukafe." Wakati huo, kuna kitu katika akili ya Lisa kikaingia. Kwa vile hakuweza kuinuka, alirukwa na akili na kumng'ata Sarah paja.
Hata hivyo, alimuacha baada ya kusikia sauti ya Sarah. Ni wakati huo Alvin aliporudi na kujiona tukio hilo. Kwa hivyo, mara moja alimkimbilia na kumpiga teke. Mguu wake ukampiga begani.
Kichwa cha Lisa kisha kikagonga fremu ya kitanda cha chuma nyuma yake. Ilikuwa inamuma sana kiasi kwamba karibu hakuweza kuvumilia. Ilionekana kana kwamba alikuwa karibu kuzimia wakati wowote.
Aliuma meno na kutazama juu huku akihangaika, ila alichokiona ni Alvin akiuangalia mguu wa Sarah kwa huruma. "Uko salama?"
“Sijambo. Asante Mungu umewahi kurudi." Sarah akaikumbatia shingo yake kwa nguvu.
“Usijali, nipo hapa kwa ajli yako." Alvin alimbusu paji la uso wake kwa upole. Alipomtazama Lisa, mara moja sura yake nzuri ikabadilishwa na sura ya kuchukizwa.
“Ulisema huumwi wewe? Nadhani ugonjwa wako ni mbaya ya tunavyofikiria. Usipopona, utafungiwa ndani milele. Kwa njia hiyo, huwezi kumuumiza yeyote.” Baada ya Alvin kumuonya, alimbeba Sarah kuelekea mlangoni na kuondoka bila kuangalia nyuma.
“Mimi si mgonjwa. Mimi si mgonjwa…” Lisa alitambaa hadi mlangoni, akijaribu kutoroka, lakini, mlinzi aliingia haraka na kumpeleka kwenye wodi ya wagonjwa wa akili.
Kulikuwa na kitanda kimoja tu kwenye kona na dirisha dogo na la juu sana hivi kwamba mtu asingeweza kupanda kutoka humo. Mlango wa chuma nje pia ulikuwa umefungwa. Lisa alibisha mlango kwa muda mrefu, lakini hakuna mtu aliyeufungua. Baadaye, alichoka sana na akalala kwenye kitanda cha hospitali, akijipinda na kujikunja kama mapira.
Hali ya hewa ilibadilika na kuwa joto kali. Ni kana kwamba joto liliongezwa makusudi. Punde, alianguka kwenye joto kutokana na joto kuzidi. Akiwa amepoteza fahamu, kuna mtu aliingia kumchoma sindano. Alitumia nguvu zake zote kumzuia. Hata hivyo, mtu huyo aalikuwa amemkandamiza kwa nguvu kitandani. Sindano ililazimishwa kupenya kwenye ngozi yake. Machozi ya moto yalitiririka kwenye kona za macho yake.
Kwa muda mfupi tu, alihisi kizunguzungu. Alihisi kwamba alikuwa akipandisha wazimu kweli. Alichukia sana. Je, alikosea nini katika maisha yake ya nyuma hadi kumfanya anyanyaswe hivyo na Alvin Kimaro, shetani? Ha! Aliwahi kutaka kubaki na kumsaidia Alvin ili apate nafuu ili asipelekwe hospitali ya wagonjwa wa akili. Alimpigania Alvin asipelekwe huko, lakini yeye ndiye aliyempeleka huko badala yake!
'Alvin Kimaro. Sarah Njau. Hata kama nitakuwa mzimu, sitawaacha kamwe'. Lisa alijipiza.
•••
Usiku sana. Katika Jumba la Klabu, Alvin alikuwa amekaa kwenye sofa la ngozi akiwa na glasi ya mvinyo mwekundu mkononi mwake. Alikuwa amevalia shati jeusi lenye mistari na vifungo vichache vya juu vikiwa vimefunguliwa. Uso wake uliokuwa umekunjamana ulionekana hatari sana.
Sarah, ambaye alikuwa akiimba na Cindy, alinyamaza na kumtazama tena. Midomo yake ikakunjua tabasamu zito. Kuanzia wakati huo na kuendelea, mwanamume huyu angekuwa wake na wake peke yake!
Kisha, mlango ukafunguliwa kwa nguvu. Sam akaingia ndani akiwa na hasira machoni pake. “Alvin, unawezaje kumfungia Lisa kama mgonjwa wa akili? Unajaribu kumfanya awe kichaa?”
“Sam, huelewi. Lisa ana wazimu kweli.” Rodney alisimama kivivu na kuweka mkono wake begani kwa Sam.
Lakini, Sam alitupa mkono wake mbali. “Bullsh*t. Alikuwa sawa kabisa nilipomwona mara ya mwisho. Ninamjua. Amepitia vikwazo vingi huko Dar es Salaam, kwa hivyo yeye si mtu ambaye atashindwa kirahisi hivyo.”
“Unamfahamu? Je, unamfahamu kuliko mimi?” Alvin alikodoa macho na kusimama taratibu.
“Alvin, unamfahamu pia, lakini umesahau mambo mengi.” Sam hakuelewa kwanini Alvin alionekana kuwa mtu tofauti sasa. “Mruhusu atoke. Ikiwa humpendi tena, basi mwache aende zake. Yeye hatakusumbua. Ukimweka mahali kama humo, hata mtu wa kawaida atarukwa na akili, achilia mbali mwanamke aliyefiwa na watoto wake.”
Sarah alisema kimya kimya, “Bwana Harrison, Lisa kweli alipatwa na wazimu. Ikiwa huniamini, karibu amchome Alvin na kisu. Yeye pia ndiye aliyemjeruhi Alvinic kichwani…”
“Funga mdomo wako.” Sam hakuwahi kumpenda Sarah, lakini sasa alikuwa na chuki isiyoeleweka.
"Sam Harrison, ndivyo unavyozungumza na Sarah?" Rodney alikunja uso bila furaha. "Sarah ana nia nzuri tu."....ITAENDELEA....
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
