JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................303-304
Sura ya: 303
Lisa alikimbia, lakini alisikia sauti ya mlango ukifungwa kwa nje. Alijaribu kuvuta mlango, lakini haijalishi aliuvuta vipi, haukutikisika hata kidogo. Alikuwa mfungwa kwa mara nyingine tena. Hakuweza kwenda popote. Alikaa chini kama mdoli aliyevunjika.
Zamani, hata kama Alvin alimtendea ukatili kiasi gani, hakuwahi kumchukia kabisa. Ni kwa sababu alijiambia kuwa hakukusudia kufanya hivyo. Alilemazwa tu na Sarah. Lakini, sasa alimchukia sana.
Alimchukia Thomas Njau. Alimchukia Sarah Njau. Alimchukia Alvin Kimaro. Alimchukia Rodney Shangwe na kila mtu mwingine aliyekuwa karibu naye.
Ikiwa si kwa Alvin na ujinga wao, je Sarah angewadanganya? Mwisho wa siku, Alvin alistahili. Mapenzi yake yasiyoisha kwa Sarah ndiyo yaliyomfikisha hadi hapo.
Ni yeye pia aliyemruhusu Thomas kuwaumiza Pamela na Kelvin. Sasa, Thomaso hakulazimika kuteseka na vikwazo vya sheria. Na yeye, alikuwa amefungwa. Hakupata picha jinsi Thomas, ambaye aliruhusiwa kutoka katika kituo cha polisi, angezidisha jitihada zake za kuwaumiza marafiki zake hata zaidi. Alimchukia Alvin Kimaro. Kwenye mawazo yake, alimwinua hadi juu angani kisha akamrusha na kumkanyaga vibaya sana ardhini. Siku moja, angewafanya wateseke kwa ajili ya maumivu waliyowasababisha kina Pamela, Charity, Kelvin na yeye.
Mchana. Mwanamke asiyemfahamu alitumwa kwenda kumhudumia. Aunty Yasmine na Shani, watu wawili waliomtunza hapo awali, walihamishwa.
Lisa alifungiwa katika nyumba hiyo ya ghorofa mbili kila siku bila mahali popote ambapo angeweza kwenda. Ilikuwa inachosha sana. Angeweza tu kutazama televisheni au kupata hewa safi kwenye kibaraza. Wakati mwingine alipotazama chini kutokea kwenye kibaraza, alikuwa na hamu ya kujirusha. Hata hivyo, kwa mawazo ya watoto tumboni mwake, aliamua kuwa mgumu.
Aliendelea kukaa humo kwa wiki nzima bila kutoka hadi Hans alipokuja kumchukua ili kumpeleka hospitali kwa uchunguzi wa uzazi.
“Alvin yuko wapi?” Lisa aliuliza. Hans alikuwa kimya sana.
Lisa alicheka. “Najua. Lazima awe pamoja na Sara. Hakuna kitu muhimu zaidi kwake kuliko Sarah kwa sasa."
"Bibi mdogo, usiwe hivyo." Macho ya Hans yalikuwa yamejaa huruma. "Nitaongozana na wewe hadi hospitali." Lisa alikuwa anataka kusema kitu, lakini alipowaona walinzi wawili wasiowafahamu, alinyamaza.
Njiani kuelekea hospitali, Hans aliendesha gari huku Lisa akiwa amekaa kwenye siti ya nyuma. Hans alisema, “Siku hizi, nimekuwa makini hasa kwa Sarah Njau. Ni kwa hilo tu ndipo Bwana Mkubwa ameanza kuamini kwamba mimi ni mwaminifu kwake kabisa.”
"Lazima iwe ngumu kwako." Lisa hakutarajia kwamba Alvin angekuwa mwangalifu na Hans.
"Inaweza kuwa ni kwa sababu nilikutetea mara ka mara sana mbele ya Bwana Mkubwa hapo awali, kwa hivyo hakuniamini sana," Hans alisema kwa sauti ya chini. "Hapo awali uliniomba nikusaidie kutafuta mtu akutengenezee mchongo ili kufanya mimba ionekane kama imeharibika ..."
“Haiwezekani sasa. Alvin alisema kwamba ikiwa watoto wake watapata madhara yoyote, hatawaacha Pamela na baba yangu. Nina wasiwasi sana kuhusu Pamela sasa.” Lisa alisema, “Thomas Njau bila shaka atalipiza kisasi kwa Pamela, lakini Pamela hataondoka Nairobi ikiwa hawezi kuwasiliana nami. Unaweza kumtumia ujumbe ili aondoke nchini mara moja?”
“Bila shaka, lakini wewe…”
“Nisaidie kuwasiliana na mtu. Jack Kimaro," Lisa alisema ghafla.
Hans alishtuka. "Jack atakusaidia?"
"Sina hakika, lakini katika Nairobi yote, ni nyinyi wawili tu mnaoweza kunisaidia kutoroka." Lisa hakuwahi kutarajia kwamba angetafuta msaada wa Jack siku moja. Ingawa alimnyanyasa mara kwa mara, alikuwa na hisia kwamba Jack angemsaidia. Aliweza kuhisi msamaha machoni pake kila alipomkabili…
“Sawa.”
Wakati gari lilipopita kwenye makutano ya barabara iliyochangamka na yenye hekaheka na shughuli nyingi, skrini kubwa iliyokuwa kando ya duka kubwa ilikuwa ikitangaza harusi ya Melanie na Jerome.
Alitazama skrini. Melanie alionekana mrembo kama binti wa kifalme. Hapo awali, Lisa alipanga kufichua utambulisho wa Melanie siku ya harusi yao. Kwa bahati mbaya, alikuwa chini ya kizuizi cha nyumbani.
Hans alipumua. “Sasa kwa vile familia za Campos na Ngosha zimeunganishwa kwa ndoa, thamani ya Melanie Ngosha imepanda sana. Sio tu kwamba yeye ni makamu wa Mkurugenzi wa Ngosha Corporation, lakini pia ni mke wa Jerome Campos. Familia za Campos na Ngosha zimeshirikiana kwenye mradi mkubwa. Sasa, thamani ya Jerome ni karibu juu kama ya Bwana Mkubwa Alvin.”
Lisa alifunga macho yake na kuzuia chuki chini ya macho yake. Melanie Ngosha hakuwa binti wa Joel hata kidogo, hata hivyo alirithi kila kitu kutoka kwa Joel, vyote vilipaswa kuwa vya Lisa. Kwa upande wa Lisa, sasa alikuwa kama panya wa mitaani. Melanie Ngosha, Nina Mahewa. Walikuwa wanasubiri muda wao tu! Alimradi bado alikuwa anapumua, angefichua rangi zao halisi kwa walimwengu!
Walifika katika hospitali binafsi ya Dokta Choka. Lisa alitazamwa na walinzi kadhaa wakati akipanda juu kwa uchunguzi wake wa uzazi.
Njiani, alimwona Cindy Tambwe, ambaye alikuwa amevaa vazi la kipepeo la manjano lililofichua nusu ya mapaja yake. Alishikilia mkoba wa kifahari mkononi mwake, na mkufu wa almasi wa karati kumi ukining'inia shingoni mwake.
Lisa alikuwa mfuatiliaji mzuri wa mambo ya mitindo, kwa hiyo aliweza kusema kwa jicho moja kwamba vazi hilo lilikuwa na thamani ya pesa nyingi, ambapo bei yake ingeweza kuwa ya juu hadi tarakimu nane. Cindy Tambwe aliyepita bila shaka hakuwa na pesa, lakini mambo yalikuwa tofauti tangu alipopatana na Chester.
“Lisa, ni bahati mbaya hapa tunakutana tena. Nimemaliza kurekodi kipindi leo na nimekuja hapa kumtafuta Chester.” Cindy alitazama juu na kuinua pete ya almasi kwenye kidole chake huku akitabasamu. “Inaonekana vizuri? Chester alinipa.”
“Inaonekana vizuri, lakini Dokta Choka ni malaya maarufu. Kila mwanamke aliyelala naye lazima awe nazo angalau kumi au ishirini kati ya hizo,” Lisa alisema kwa unyonge. "Ni kawaida yake kuwanunulia wanawake pete kama hizo, lakini pia lazima wavumilie unyanyasaji mkubwa kitandani. Hapo ulipo sijui kama una marinda..."
Midomo ya Cindy iliganda kabla hajadhihaki. "Huenda na wewe alishakufumua eti, ungejuaje yote hayo?”
Lisa alicheka. “Labda hujui kila msichana anachangua pale anapotaka kuwekeza thamani yake. Thamani yangu niliwekeza kichwani, ndiyo maana hutaniona nikidhalilika. Wewe umechagua kuwekeza katikati ya mapaja yako ili uweze kupata maisha unayoyataka. Kwa hiyo mimi na wewe tupo anga mbili tofauti kabisa.”
Cindy akacheka kwa dharau. “Bado mimi ni bora zaidi kuliko wewe! Tizama jinsi unavyotia huruma! Mume wako alikudanganya wakati wa ndoa yako. Halooo! Nilikuwa nakuonea wivu, lakini haikuchukua muda Alvin Kimaro akakutelekeza. Sasa, anaongozana na Sarah tu popote anapoenda…” Cindy alinyamaza na kumtazama Lisa. "Ulikuwa unalijua hilo? Sasa, kila wakati Chester ananipeleka kwenye bata zao na marafiki zake, Sarah huwa yuko pamoja na Alvin kila mara. Sitataja jinsi walivyo karibu sana, lakini siku zote atalala kwa Sarah baada ya kula bata.”
“Bi. Tambwe…” Hans alionya.
"Kaka, kwani nasema uongo? Si hata wewe pia huwa unakuwepo?” Cindy akapepesa macho yake makubwa na kusema. "Hata niliona lovebites nyingi kwenye shingo ya Sarah mara ya mwisho. Teh…teh..teh…."
Uso wa Lisa ulikuwa umepoa sana. "Kumbe ndio hivyo? Basi wanapendezana. Yeye ni kipande tu cha takataka ambacho sitaki kukiona tena. Nadhani anafaa kabisa kuwa hata marafaiki na mtu kama wewe.”
“Haya, acha kujifanya. Najua imekuuma sana.” Cindy akatoa kioo na kupaka lipstick nyekundu kwenye midomo yake. "Hata hivyo, Sarah alinialika kwenda kwenye jumba lake la baharini huko Mombasa siku chache zilizopita. Ni kipande ghali zaidi cha ardhi ya pwani huko Mombasa. Unaweza kuona bahari ya bluu mara tu unaposukuma mlango wa chumba cha kulala.”
Sura ya: 304
Uso wa Lisa hatimaye ulizama. Yeye, bila shaka, alikumbuka jumba hilo la baharini. Ilikuwa ni nyumba ambayo aliwahi kuishi na Alvin, alikokuwa ameongozana na Alvin kwenda kuuguza ugonjwa wake na kupata nafuu. Pia ndipo walipoweka nadhiri zao nyingi za maisha, wakaishi kwa mapenzi mazito na hata kutunga mimba ya watoto wao. Lakini sasa, alimpa Sara? Mwanaume huyo angewezaje kuwa mkatili kiasi hicho? Kwa kweli alikuwa ... hana moyo.
Alipomwona akiwa ameduwaa, Cindy alicheka. Alimkaribia Lisa na kushusha sauti yake. "Wewe na Pamela Masanja mlikuwa mabinti wenye fahari sana. Nani angefikiria kwamba Pamela angevunjwa na kuharibiwa sifa yake, na wewe? Mumeo alikutupa. Kwa kweli, nyakati zimebadilika sana.”
"Umesema nini?" Lisa alinyanyuka ghafla na kumkazia macho kwa macho. “Pamela hakufanywa lolote na Thomas…”
“Ina maana hujaona jinsi habari za Pamela zilivyoenea kila kona mtandaoni? Koneksheni yake imevuja akifanyiwa vitendo vibaya na Thomas. Binti wa thamani wa familia ya Masanja kutoka Dar es Salaam ametiwa unajisi. Haha, kila mtu anasema kwamba anastahili kwa sababu alijitongozesha kimakusudi kwa Thomas Njau. Nani atamtaka katika siku zijazo? Hata mimi siwezi kuvumilia kuwatazama nyinyi wawili tena.” Cindy alimuangalia kwa mbwembwe kisha akageuka.
Lisa alipigwa na butwaa. Hakuwahi kufikiria kuwa tukio la Pamela lingefichuliwa na kugeuzwa kimakusudi. Hata kama hakufanyiwa chochote, mitandao ingeeneza kana kwamba alifanyiwa mambo fulani. Hii ndiyo nguvu ya mitandao ya kijaminii bwana! Habari kama hii ilikuwa pigo kubwa kwa mwanamke. Hakuweza kuamini.
Alizunguka kumtazama Hans. "Tukio la Pamela ni la kweli kwenye mitandao?"
Hans alisita, lakini mwishowe, aliinamisha kichwa chake kwa uchungu. “Ndiyo.”
“Imekuwaje? Yeye ndiye mwathirika, lakini kwanini kila mtu anamsema vibaya kwa kujirahisha kwa Thomas Njau?” Lisa alimfokea bila kujizuia. “Ni nani aliyegeuza mambo ya kuyafanya yawe tofauti?”
"Samahani. Ni picha za sura ya Pamela ndiyo zimesambaa, zikiwa na maneno ya ‘Connection ya Mkemia Mkuu wa Zamani wa Osher yavuja. Video sijaziona lakini watu wanatumiana chini kwa chini. Lakini kwa kuwa Bi. Masanja hakufuatilia suala hilo, kila mtu alifikiri huenda ikawa ni kweli,” Hans alieleza kwa huruma.
“Nipe simu. Nataka kuona habari.” Lisa akampokonya simu mkononi.
Mlinzi aliyekuwa pembeni akamvuta mara moja. “Bi. Jones, tafadhali twende haraka kwenye uchunguzi."
"Hapana, nataka kuwasiliana na Pamela," Lisa alipiga kelele na kujitahidi kupinga. Hata hivyo, walinzi walimpuuza na kumpeleka kwa nguvu kwenye chumba cha uchunguzi wa ultrasound. Haijalishi alikuwa akifanya fujo kiasi gani, hakuna aliyemjali.
Baada ya uchunguzi kukamilika, alirudishwa tena kwenye jumba la baridi la New Metropolis Park.
Lisa alivunjavunja kila kitu ndani ya nyumba, na kumtishia mtumishi wake mpya wa ndani. Hadi jioni ndipo Alvin alipoingia pale. Aliitazama ile nyumba iliyoharibika, lakini kabla hajauliza chochote, kisu kikamjia. Akarudi nyuma na kumshika Lisa mkono ambao ulikuwa umekamata kisu, akakichukua kisu na kukitupa pembeni. Akamgeukia na kumwangalia yule mwanamke mwenye nywele ndefu na mkali aliyekuwa mbele yake. “Unataka kuniua?”
"Nilikosea. Ni afadhali uwe mpumbavu, na bado ungekuwa bora kuliko ulivyo sasa.” Lisa alimtazama kwa chuki. “Kwanini upo huru? Chizi kama wewe alipaswa kuwa umefungwa kwenye hospitali ya vichaa. Nilidanganyika kufikiria kuwa naweza kukuponya mwenyewe. Haha, lazima nilikuwa mwendawazimu."
"Nyamaza. Nadhani wewe ndiye chizi hapa." Alvin alimkokota hadi bafuni na kukiegemeza kichwa chake kwenye kioo. “Tazama sasa. Kuna tofauti gani kati yako na kichaa?”
“Mimi ni kichaa. Nimesababishwa kuwa kichaa na wewe." Uso wa Lisa ulikuwa na michirizi ya machozi. “Alvin, kwanini unamfanyia hivi rafiki yangu? Unajua kuwa Pamela alikuwa karibu kubakwa. Naweza kuachana na ukweli kwamba ulimwokoa Thomas, lakini kwanini alilidhalilisha jina la Pamela alipotoka? Je! Unajua jinsi gani sifa ilivyo ni muhimu kwa msichana? Je, wanawake wengine wote isipokuwa Sara hawana thamani machoni pako?”
Mshipa kwenye paji la uso wa Alvin ulivimba. “Umemaliza? Watu kwenye mitandao ya kijamii hawana makosa. Rafiki yako ndiye aliyejipendekeza kwa Thomas. Nasikia alikuwa anataka gari kama nililokununulia.”
"Ulisema nini?" Lisa alimkazia macho huku akimtumbulia macho kana kwamba haamini alichotoka kukisikia.
“Ni Pamela Masanja aliyeokuwa akimsumbua Thomas na kujaribu kila njia kumtongoza. Baada ya kukubaliana naye, aligundua kwamba sifa yake ilikuwa mbaya, hivyo alitaka kujiepusha naye. Hakuna kitu katika ulimwengu huu kinachokuja bila gharama." Sarah alisema kwa uso mkavu.
“Nani kakuambia ufanye hivyo? Sarah?” Lisa alimgeukia na kumuuliza Alvin, “Unaamini kila kitu anachosema?"
“Ningemwamini nani nisipomuamini Sarah? Wewe?” Alvin alikoroma na kusema kwa dharau, “Pamela Masanja na wewe ni watu wa aina moja. Ndege wenye kufanana huruka pamoja. Familia ya Masanja ina ushawishi huko Dar es Salaam, lakini hawana thamani huku Nairobi. Bila shaka, alitaka kulazimisha kuolewa na Thomas kwa sababu familia ya Njau ina ushawishi hapa.”
Uso safi wa Lisa ulibadilika rangi kama karatasi. Aliitazama midomo myembamba ya Alvin, ambayo alikuwa ameibusu mara nyingi hapo awali. Kiasi kwamba alisahau kwamba jinsi midomo hiyo ilivyokuwa myembamba, ndivyo mwanaume huyo alivyokuwa jeuri na mkatili zaidi.
Je, angemuamini nani kama si Sarah? Kila kitu ambacho Sarah alisema kilikuwa sawa. Hakukuwa na haja ya kuchunguza na kamwe haja ya kuwa na shaka. Lisa aliumia sana hata asijue la kusema.
Maneno yote yaliyokuwa yakimtoka Alvin kooni yalikuwa ni fimbo ya kumuadhibu. Hakuweza hata kusogea kwa sababu alikuwa ameshikwa na kukandamizwa kwa nguvu na Alvin.
Wakati huo Alvin alihisi yule mwanamke aliyekuwa chini yake amepatwa na kichaa ghafla. Alikuwa kama mnyama mdogo aliyejeruhiwa. Alipopotea katika mawazo kwa sekunde kadhaa, mkono wake ukalegea.
Lisa alijifungua na kunyakua chupa ya losheni kwenye sehemu ya kuoshea uso kabla ya kuipasulia kichwani mwa Alvin. Damu safi mara moja ilidondoka kutoka kwenye paji la uso wake.
Alvin alipatwa na wazimu, na yeye alinyoosha mkono kumsukuma. Lisa alijigonga ukutani mara moja, na damu ikaanza kutoka mapajani mwake. Aliteleza ukutani taratibu huku akiwa ameshika tumbo lake huku akilia kwa uchungu asiweze kuongea.
Alvin aliingiwa na hofu tena. Hakujali jeraha lililokuwa kichwani mwake, alimnyanyua kwa haraka na kutoka nje ya chumba kile. Kwa mwendo wa dakika ishirini, Lisa alikuwa amezidiwa na maumivu kiasi kwamba hakuweza kuongea kabisa. Alishika tu upindo wa sketi yake iliyotapakaa damu.
Milipuko ya maumivu ilimpata Lisa tumboni. Alijiwazia kwa huzuni, jinsi Alvin na yeye waliwahi kutazamia kupata watoto. Kwa kuwa wote wawili walitoka katika malezi ya bahati mbaya, walitamani kwamba watoto hao wangewapa familia kamili. Aliwahi kumshukuru Mungu kwa kumpa mapacha.
Hata hivyo, baadaye, kila siku alikuwa na wasiwasi kuhusu jinsi angeweza kuwalinda watoto wake akiwa kama mama. Ingemlazimu kufanya nini ili kuwazuia wasiumizwe na Sara? Labda pengine ingekuwa afadhari kwamba watoto walikuwa wameamua kwenda. Angalau wasingeteseka. Labda hiyo ndiyo ingekuwa ahueni kwao.....ITAENDELEA.....
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
