JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................299-300

Sura ya: 299

Baada ya Lisa kuoga, Pamela alimtumia ujumbe akimkaribisha waende baa kufanya party ya kumfariji kwa matatizo yake. Lisa alijua kwamba Pamela alihofia yeye kuwa peke yake na mawazo yake, kwa hiyo alikubali kwa furaha.
Lisa alipokuwa tayari, alimpigia simu Pamela ili kumwambia kuwa angempitia nyumbani kwake. Lakini badala ya kujibu, Pamela alipiga kelele, "Fanya haraka unisaidie. Nimevamiwa! Siwezi kutoka.”
“Umevamiwa na nani…” Lisa alichanganyikiwa na ghafla akamsikia Pamela akisema, “Kuna watu wanagonga mlango kwa fujo ... hawasemi hata wao ni kina nani…”
“Bam!”Ghafla, kulikuwa na sauti kubwa za harakati kwenye upande wa pili wa simu. Kisha, ikawa kimya!
Lisa kwa haraka akarudia kupiga namba ya simu ya Pamela lakini simu haikuweza kupokelewa. Hisia mbaya ilimtawala. Umbali kutoka nyumbani kwa Mzee Kimaro mpaka nyumbani kwa Pamela ulikuwa angalau saa moja kwa gari. Kwa vyovyote vile asingeweza kufika kwa wakati na kumuokoa Pamela.
Baada ya kutafakari, alimpigia simu Kelvin kwa haraka. Kelvin aliishi karibu sana na Pamela. "Kelvin, kuna mtu alivamia nyumba ya Pamela. Unaweza kuharakisha huko na kunisaidia kuangalia? Ninaogopa kuna kitu kibaya kimemtokea. Piga namba hii kujua anuani yake."
“Sawa, nitaenda huko sasa hivi.”
Baada ya kukata simu, Lisa alipiga simu polisi na mara moja akaendesha gari hadi getini.
Mlinzi wa getini hakumruhusu atoke, lakini, kwa kuwa alikuwa na wasiwasi sana, aligonga geti kwa gari. Geti bado lilikuwa limefungwa na halikuweza kuachia njia, lakini mlinzi aliogopa na kumfungulia geti haraka. Baada ya kumruhusu atoke, mlinzi alimpigia mfanyakazi wa nyumbani.
Lisa aliendesha gari kwa kasi kama siku ile alipopata ajali. Speed meter ilisoma 150kph. Umbali wa saa moja kwa mwendo wa kawaida ulipunguzwa hadi dakika 20 tu. Hatimaye alifika kwenye nyumba ya Pamela.
Alipoingia, mlango wa ghorofa ulikuwa tayari umefunguliwa. Sebuleni kulikuwa vululuvululu na sauti za mapambano zilisikika kutokea chumbani.
Aliingia ndani kwa haraka. Pamela alikuwa amelala kitandani, macho yake yakiwa yameduwaa. Nguo za sehemu ya juu ya mwili wake zilikuwa zimechanika na matiti yakiwa wazi huku uso na mwili ukiwa na michubuko.
Kelvin alikuwa akipambana na wanaume watatu peke yake, wawili ambao walikuwa warefu na wenye misuli, na waziwazi walionekana kuwa majambazi. Kelvin alikuwa tayari amejeruhiwa katika sehemu nyingi. Mtu wa tatu hakuwa mwingine bali Thomas Njau. Alichukua fursa hiyo kushughulika na Pamela, akimalizia kumvua suruali yake.
“Wewe mjinga!” Lisa alimkemea kwa hasira. Tukio hili lilimtoboa macho Lisa bila huruma. Bila kujali alishika pipa la taka lililokuwa pembeni na kumponda Thomas.
Thomas alipandwa na hasira na kumfuata, akamshika na kumtupia mbali.
“Lisaa…” Kelvin alimkimbilia na kumdaka kbal hajaanguka chini. vinginevyo angefikia tumbo, na sijui ingekuweje kwa mapacha wake.
Hata hivyo, wale majambazi wawili waliokuwa nyuma yake waliona hivyo na mara moja wakamchoma Kelvin kisu begani.
“Kelvin...” Lisa alishtuka na kumshika kwa hofu.
"Usijali, ni ... jeraha dogo." Kelvin alikunja uso wake kwa maumivu, lakini bado alijilazimisha kumtoa wasiwasi Lisa.
Moyo wa Lisa ulitetemeka huku macho yake yakimtoka machozi. Hiyo ilikuwa mara ya pili kwa Kelvin kuchomwa kisu ili kumuokoa. Lakini, Lisa aliishia kuhisi hatia tu juu yake na hakuweza kumlipa chochote kingine.
"Huyu ni mpenzi wako au wa Pamela?" Thomas hakuelewa somo hapo. "Lisa Jones, inaonekana umekuwa ukimsaliti mume wa dada yangu."
“Thomas Njau, mnyama wewe! Tayari nimewaita polisi. Utajuta kuzaliwa safari hii. Tuone kama Alvin atakutetea tena.” Lisa hakuwahi kumchukia mtu kama alivyokuwa akimchukia Thomas wakati huo.
“Hehe, endelea kuota. Alvin ni mume wa dada yangu, wakili maarufu. Hakika atanisaidia.” Thomas alionyesha kujigamba kwa jazba na dharau. "Baada ya yote, nimefanya mambo kama haya mara nyingi hapo awali. Sikuzote amenisaidia.”
Aliendelea kusema 'mume wa dada yangu', lakini Alvin alikuwa mume wa Lisa. Maneno hayo yalimkera sana Lisa hadi mwili ukamtetemeka.

Kwa bahati nzuri, polisi waliingia ndani wakati huo na kuwakamata haraka Thomas na wenzake.
Kelvin na Pamela walipelekwa hospitalini haraka. Akiwa amekaa kwenye gari la wagonjwa akielekea hospitali, simu ya Lisa iliita bila kukoma. Zote zilikuwa simu kutoka kwa familia ya Kimaro, akiwemo Alvin.
Aliitikia wito wake na mara akasikia kishindo cha Alvin chenye hasira. "Lisa Jones, uliendesha gari usiku tena kwa kasi ya kuhatarisha maisha. Ulithubutu hata kugonga geti la uzio. Ninakwambia, ikiwa chochote kitatokea kwa watoto wangu, nitaondoa maisha yako.”
"Alvin, kwa hivyo bado unakumbuka kuwa una watoto, huh?" Lisa alishindwa kujizuia na kumfokea mtu huyo, “unajuwa kwanini nilitoka nje? Ni kwa sababu Thomas Njau alivamia katika nyumba ya rafiki yangu mkubwa na kutaka kumbaka. Yote ni makosa yako. Ni kwa sababu yako huyo fisadi amekuwa na kiburi na ukosefu wa maadili. Alvin Kimaro, nakuchukia. Ninakuchukia sana!” Baada ya kutoa hisia zake, machozi yake yalidondoka kama mkufu wa lulu uliovunjika. Alifunika uso wake na kuruhusu kububujikwa na machozi.
Kelvin ambaye alikuwa amelala kiunyonge kwenye machela, aliushika mkono wake kwa macho yaliyojaa wasiwasi. Lisa akakata simu na kuruhusu kilio chake kirindime ndani ya gari la wagonjwa. Hakuwahi kuwa na majuto zaidi ya siku hiyo. Hakupaswa kamwe kuwa na moyo mpole na mwanaume huyo. Hakupaswa kamwe kumruhusu amtawale.
•••
Usiku sana hospitalini. Baada ya dakika 40 katika Emergency Room, daktari alitoka. "Mgonjwa wa kike hakushambuliwa kabisa lakini bado alipata majeraha katika maeneo mengi. Ana mshtuko wa moyo, na kwa vile alikuwa amelewa dawa, huenda ikamchukua zaidi ya saa kumi kupata fahamu.”
Hatimaye Lisa alishusha pumzi. Asante Mungu… Asante Mungu Thomas hakufanikiwa kumwingilia Pamela. Vinginevyo, hakujua jinsi Pamela angeikabili habari ya kubwakwa na Thomas.
"Vipi kuhusu mgonjwa wa kiume?" Lisa aliuliza kwa haraka.
“Kisu kilichomwa kwenye mkono wake, na tatizo ni kwamba kilijeruhi mishipa karibu na jeraha la awali. Anahitaji kufanyiwa upasuaji. Baada ya operesheni,Itachukua angalau miezi sita kupona kabisa."
"Tafadhali umfanyie upasuaji mara moja." Lisa alilipa pesa kabisa. na kulala pamoja na Pamela wodini. Pamela alikuwa bado amepoteza fahamu. Uso wakewote ulikuwa umevimba.
Baadaye, polisi pia walifika kukusanya ushahidi wa tukio lile kwenye jeraha la mwathirika. Lisa alipomaliza kutoa maelezo yake, tayari ilikuwa saa nane usiku. Alikuwa na shughuli nyingi na uchovu hata kichwa kilikuwa kikimdunda. Hakuweza kuvumilia tena hivyo akajilaza pembeni ya Pamela ili apumzike.
Ghafla Alvin akaingia. Uso wake ulikuwa umeumuka kwa hasira. Macho yake yalikuwa meusi sana kama anga la usiku.
Alimtazama Lisa chini-uu kwa dharau. Katika akili yake, maneno, 'Ninakuchukia. I really hate you' yalitawala.

Sura ya: 300

Alvin hakuelewa ni kwa nini, lakini moyo wake ulikosa raha aliposikia maneno hayo.
“Twende nyumbani.” Alvin akamtazama, sauti yake ikiwa chini kana kwamba ana amrisha mtu asiye na thamani kwake.
Lisa hakutetereka na hakuweza kuwa na wasiwasi hata kumtazama. Kusikia sauti yake tu kulifanya damu yake ichemke kwa hasira.
“Umesikia nilichosema? Una mimba sasa. Huwezi kukaa hapa namna hii.” Alvin akamvuta juu.
Hata hivyo, Lisa alimsukuma na kutabasamu kwa huzuni. “Unadhani nimependa kukaa hapa saa hizi? Marafiki zangu wawili bado hawana fahamu. Unafikiri nitakuwa na hamu ya kwenda kulala nyumbani? Bila shaka, mtu kama wewe ambaye hana moyo kwa mtu yoyote isipokuwa kwa Sarah Njau anaweza kufanya hivyo.”
Alvin aliutazama uso wake uliopauka na kusitasita kabla ya kuvua koti lake na kumvisha, kisha akasema, “Usiwaue watoto wangu kwa baridi.” Nuru ya macho yake ikafifia tena. Lisa alitabasamu kwa dhihaka yake.
Muda si mrefu akakaa, Lakini ghafla simu yake ikaita. Aliitazama na kuona jina la 'Sarah' likiangaza kwenye skrini alipotoa simu yake. Alvin akainuka na kwenda pembeni kuipokea.
Akiwa kwenye korido ile tulivu, Sauti ya Sarah iliweza kusikika kutoka kwenye simu hadi kwa Lisa aliyekuwa kitandani ndani ya wodi..
Wakati huo taa za chumba cha upasuaji zilizimika. Kisha daktari akamsukuma Kelvin nje. Kelvin alikuwa macho, na mara tu alipomwona Lisa, alitabasamu kwa unyonge. “Lazima utakuwa umechoka. Rudi ukapumzike. Sijambo…”
Alvin ambaye alitoka kupokea simu yake, akageuka na kuliona tukio la Kelvin na Lisa wakitazamana. macho yake yakamtoka kwa hasira. “Umetoka wodini kuja kumpokea Kelvin akitoka kwenye upasuaji?”.
"Kama asingewahi mapema ili kumuokoa Pamela, Pamela angekuwa amebakwa na shemeji yako mpendwa." Lisa alimtazama Alvin kwa hasira. “Alichomwa kisu mkononi na watu wa Thomas, palepale alipochomwa na Zigi kipindi kile alipomsababisha apoteze figo. Wakati huu, nitahakikisha anapelekwa jela na kuozea huko milele, hata kama utamtetea.”
Alvin akakuna kichwa chake. Hakutarajia Thomas angefanya jambo kama hilo tena. Kusema kweli naye alikasirika sana, lakini alipomuona Lisa anakasirika kwa niaba ya Kelvin, aliona inakera. "Lisa Jones, unamuonea huruma?"
"Ninachojua ni kwamba kama si yeye, Pamela angebakwa leo. Kama si yeye, ningekuwa tayari nimepoteza watoto wangu.” Lisa alimtazama kwa chuki machoni mwake. “Ukithubutu kwenda mahakamani kwa ajili ya Thomas tena wakati huu, tutapambana mahakamani.”
Alvin alijikuta katika hali mbaya zaidi, na akamtazama tena kwa ukali. “Jipange.” Kisha akageuka na kumwambia Hans, "Kaa hapa na kumwangalia." Baada ya hapo, aliondoka bila kuangalia nyuma.
Lisa alimtazama hadi kivuli chake kilipopotea. Alichanganyikiwa. Alimaanisha nini aliposema ajipange? Je, ni kweli angemtetea Thomas hata iweje? Lisa aliogopa. Alikuwa akimtishia tu Alvin. Ikiwa angeenda kinyume na Alvin, asingeweza kushinda hata kama angeajiri wakili bora.
“Lisa.” Sauti ya upole ya Kelvin ilisikika kando yake ghafla.
Aligeuka, na Kelvin akatabasamu kwa unyonge. “Mfuate.”
"Hakuna haja." Lisa akatikisa kichwa. Ingekuwa na faida gani? Kwa wakati huo, Alvin lazima angekuwa anaenda kituo cha polisi kumtoa Thomas au Mombasa kumfuata Sarah.
Kwa kweli, alikisia kwa usahihi. Dakika ishirini baadaye, alisikia mungurumo wa helkopta. Sarah alifika kituo cha polisi na muda mfupi baadaye Alvin alifika pia. Sarah alionekana mwenye huzuni na macho yake yakiwa yamevimba.
“Alvinic…” Sarah alijitupa mikononi mwake mara moja alipomwona na kuanza kulia. “Samahani kwa matatizo yaliyotokea tena kwa kaka yangu. Sikutarajia angekukatisha tamaa hivyo.”
“Ni kwa sababu nimekuwa nikimsaidia kila wakati ndiyo maana anazidi kuwa jeuri, sivyo?” Uso wa Alvin ulikuwa umejaa hasira. “Hata alidiriki kuingia katika nyumba ya mtu na kumchoma kisu na kumtia dawa za kulevya. Anafikiri yeye ndiye bosi wa Nairobi? Kwanini asichukue bunduki na kwenda kuiba benki, basi?”
Sarah alieleza kwa haraka, “Anampenda sana Pamela Masanja. Ni sawa ikiwa Pamela hampendi, lakini alimtukana tena na tena. Kwa hiyo, broo akakasirika babe..”

“Kwa hiyo? Hana makosa?" Alvin aliuliza kwa hasira.
“Siyo hivyo…” Sarah hakutarajia Alvin angekuwa mkali. Akijua kwamba angezidi kumchukiza, machozi yake yalizidi kumdondoka aliposema kwa huzuni, “Hilo silo ninalomaanisha. Amekosea, na pia nimekatishwa tamaa sana. Yote ni makosa yangu…”
“Sawa, haina uhusiano wowote na wewe. Thomas ndiye mjinga.” Alvin akampigapiga mgongoni mwake taratibu.
“Alvinic, niliwauliza polisi. Walisema tayari wamefungua kesi. Ikiwa upande wa walalamikaji watakaza zaidi, anaweza kwenda jela kwa miaka kumi." Sarah alisihi huku machozi yakimlenga lenga. “Nina kaka mmoja tu. Wazazi wangu wamekwenda. Akienda jela, basi nitapoteza familia yangu yote.”
"Lakini bado una mimi," Alvin alisema kwa upole. Kwa kweli hakutaka kumuokoa Thomas wakati huo.
'Hiyo ni tofauti. Ni yeye pekee ambaye bado nina uhusiano wa damu naye.” Sarah alilia kwa uchungu kifuani mwake.
Alvin akampapasa mgongoni, macho yake yakiwa yanamulika kwa mng'ao usioeleweka. Sarah alipoona anasitasita kujibu kwa muda, akauma mdomo na kutabasamu kwa uchungu. “Basi sawa, kama unaona ni ngumu kumsaidia kaka yangu. Nitafikiria njia mwenyewe."
“Unafikiria nini?” Alvin aliuliza kinyonge.
'Nitamwomba Pamela msamaha. Kusudi amsamehe kaka yangu, nitakubali chochote atakachosema. Ninaweza hata kupiga magoti mbele yake.” Sarah akatoka kwenye kumbatio lake. “Naenda hospitali sasa hivi.”
Hata hivyo, Alvin alimzuia. “Pamela bado hajaamka. Hakuna maana kwenda."
“Basi… basi nitasubiri hadi atakapoamka. Nitamwomba msamaha kuonyesha uaminfu wangu kwake. Pia nitamlipia gharama zake zote za matibabu.” Sarah alimsukuma Alvin mbali kwa ukaidi. “Alvinic, lazima niende. Ndugu yangu yuko kwenye matatizo."
Bila kungoja jibu lake, aliondoka kuelekea hospitali. Alvin alijikuta akimfuata bila kujijua.
•••
Lisa alirudi kwenye wodi ya Pamela baada ya kuachana na Kelvin. Pamela alikuwa akiota ndoto mbaya. Alitingisha kichwa chake kwa hofu na kusema, “Hapana, usinipige. Inauma."
“Pamela, Pamela, nyamaza. Niko hapa!" Lisa alimshika mkono haraka huku machozi yakimdondoka.
Kwa kuwa Pamela alikuwa mtoto pekee wa kike na pia mtoto wa mwsiho, familia ya Masanja ilimlea kama binti wa kifalme, na hakuwahi kupigwa hata na chelewa tu. Lakini sasa, hata ndoto iliweza kumfanya aogope sana. Ilikuwa wazi kuwa aliteswa sana kabla ya kuzimia.
“Lisa…” Kwa kupigwa na butwaa, Pamela alifumbua macho yake ya woga na kumkazia macho. “Ninaota?”
“Hapana, huoti ndoto. Uko sawa sasa. Thomas hakufanikiwa. Bado wewe ni bikra.” Lisa alimkumbatia. "Kwa bahati nzuri, Kelvin alifika kwa wakati na kukuokoa."
Pamela alinung'unika, "Lisa, hunidanganyi? Kweli haku…”
“Hakufanya hivyo. Kama nasema uwongo, basi nikatwe radi." Lisa aliapa.
Macho ya Pamela yalikuwa mepesi kwa muda. Kisha, kana kwamba anakumbuka jambo fulani, machozi yalimtoka. “Lisa, niliogopa sana, niliogopa sana. Huyo kichaa Thomas alileta watu wake na kuingia ndani ya nyumba yangu kwa nguvu. Nilikataa, lakini walinipiga, na wakasema wangenibaka kwa zamu. Walininywesha dawa kwa nguvu. Asante Kelvin kwa kuniokoa.”
“Namchukia sana Thomas. Mnyama huyo, anathubutu vipi…” Hasira moyoni mwa Lisa iliwaka alipokuwa akimsikiliza Pamela. Hakuwahi kutarajia kuwa genge la Thomas lingekuwa la kikatili kiasi hicho.
Kama asingemjulisha Kelvin, Pamela angekuwa amebakwa au kufa kabisa.
“Usijali shosti, yamepita. Shukuru Mungu upo salama.” Lisa alizuia hasira yake ili kumfariji Pamela.
Pamela aliendelea kulia mikononi mwake. Hata hivyo, kwa kuwa alilemewa na dawa za kulevya, haikuchukua muda kabla ya kuhisi kizunguzungu tena na kuzimia.....ITAENDELEA...

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.