JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................297-298
Sura ya: 297
Alvin na Sarah walionekana kukaribiana sana katika kila picha kana kwamba walikuwa mapacha walioungana.
Katika ukurasa wake wa facebook, Sarah aliweka picha ya keki ya ngazi tatu. Juu ya keki hiyo kulikuwa na wanasesere wawili, binti wa kifalme na mwana mfalme. Alikuwa ameandika nukuu pia: [Sikuwahi kufikiria kuwa ungesherehekea siku yangu ya kuzaliwa pamoja nami tena. Nakupenda. Yote yalianza na wewe, na yataishia na wewe!]
Picha na ujumbe wa Sarah vilizua ghasia mtandaoni!
[F*ck, nilifikiri Alvin Kimaro alikuwa mtu muungwana sana. Juzijuzi hapa aliufahamisha ulimwengu juu ya msimamo wake kwa mke wake. Muda haujapita, anatutambulisha uhusiano wake mpya wa kimapenzi sasa. Ni upuuzi gani huu?]
[Me too. I even envied the otherworldly love between The Great Kimaro and his wife.] Hii ilikuwa ni komenti kutoka Naijeria.
[Lisa is so pitiful.] Mchangiaji kutoka Afrika Kusini.
[Mwanamke huyu anaonekana kama kikongwe. What a shameless person.] Mchangiaji kutoka Kenya
[Die, you b*tch!] Mchangiaji kutoka Uganda akimkashifu Sarah.
[Kujitongozesha kwa mume wa mtu mwingine, huoni aibu?] Mchangiaji kutoka Tanzania.
Sarah hakuambulia hata komenti moja ya kumsifia, zote zilikuwa zikimponda tu!
Lisa alizima simu yake. Aliinuka na kupiga mswaki akijitahidi kupotezea kila kitu alichojionea. Alifikiri asingelia tena, lakini akiwa katikati ya kupiga mswaki, alibubujikwa na machozi. Ni kwa sababu aliuona mswaki wa Alvin kwenye sinki la kuogea.
Alipotoka nje ya chumba chake saa 8:30 asubuhi, wajakazi waliopita mara kwa mara walimtazama kwa huruma.
Alijua kwamba kila mtu alikuwa ameona habari hiyo.
Alipokaribia sebule ya chakula, sauti ya Iveta, ambaye alikuwa mkwe wa Kimaro aliyeolewa na Spencer, mtoto pekee wa kiume wa Mzee Kimaro, ilisikika kutoka ndani. “Nilidhani Alvin anampenda sana Lisa lakini alibadili moyo wake ndani ya siku chache tu. Hata alitoa Jumba la kifahari na maonyesho ya fataki kwa mwanamke mwingine. Nadhani hamjali tena Lisa.”
Spencer alisema, “Siwezi hata kushangaa. Tulijua ni kiasi gani Alvin alimpenda Sarah hapo awali, na Lisa… Uso wake umeharibika. Haonekani mrembo tena.”
“Uko sahihi. Hata kama ningekuwa mimi, nisingevumilia sura ya kutisha kama ile. Alvin naye ni mtu jamani, tusimlaumu sana!” Iveta alikandamizia.
Bibi Kimaro alisema. "Wanaosikitisha ni wale watoto wawili ambao bado hawajatoka tumboni."
Iveta alisema, “Alvin bila shaka atataka watoto, sivyo? Mimi ni mama pia. Naamini Lisa hakika hataweza kuvumilia kuwaacha watoto wake wawili kwa familia ya Kimaro.”
Mzee Kimaro alisema kwa sauti nzito, “Hata hivyo, watoto wa familia ya Kimaro lazima wakae katika familia ya Kimaro. Hakuna anayeweza kuwachukua.”
Lisa alisimamisha hatua zake bila kupenda. Aligeuka na kuondoka bila mtu yoyote kumwona.
•••
Katika ofisi za KIM International, Alvin aliona habari mbaya kwenye kompyuta yake. Uso wake ulibadilika ghafla. "Umegundua ni nani aliyesambaza habari hiyo?"
“Ni kampuni ya vyombo vya habari iliyofadhiliwa kwa siri na familia ya Campos," Hans alisema ukweli.
"Familia ya Campos?"
Alvin alikodoa macho. Alitokea hisia mbaya na hatari wakati huu. "Vema, familia ya Campos inaenda kinyume na mimi sasa."
Hans alitetemeka kidogo, lakini alijipa ujasiri na kusema, “Bwana Mkubwa, kwanini usiujulishe umma kwamba wewe hauna uhusiano wa kimapenzi na Sarah bali ni marafiki? Umeoa sasa, kwa hivyo si vizuri kwa sifa ya Kampuni ikiwa hii itaenea.”
Alvin alikaa kimya kwa muda. Kabla hajamjibu, Thomas akampigia simu. “Bwana Kimaro, kuna kitu kimetokea. Sarah aliumia baada ya kugongwa na mtu alipotoka asubuhi ya leo.”
Nusu saa baadaye, Alvin alifika hospitalini. Thomas alikuwa amesubiri kwa muda mrefu mlangoni. “Bwana Kimaro, hatimaye umefika. Sarah bado amelala kitandani. Daktari alisema ana mshtuko wa ubongo.”
Alvin alikunja uso. Akausukuma mlango wa wodi ile kwa nguvu. Paji la uso la Sarah lilikuwa limefungwa bandeji. Uso wake mzuri, mdogo, ulikuwa na hali dhaifu.
“Mbona hukuniambia?” Alvin aligusa jeraha kwenye paji la uso wake.
Sarah aligugumia kwa maumivu na kulazimisha tabasamu. "Hakuna shida, ni mkwaruzo mdogo tu."
Thomas, ambaye alikuwa pembeni, mara moja alisema, “dada, kwanini usiseme ukweli?” Alimgeukia Alvin kwa sauti ya huzuni, “Dada yangu alivuja damu nyingi sana Bwana Kimaro. Nakusihi ufuatilie hili kwa ajili ya Sarah. Sijui ni mtu gani aliyefichua picha zenu mkisherehekea siku yake ya kuzaliwa, lakini sasa kila mtu kwenye mitandao anamkaripia dada yangu na kumwita majina ya ajabu. Hata wengine wanamwita malaya. Kwa vyovyote vile, wanatumia kila aina ya maneno machafu kumzungumzia. Wengine hata wanadiriki kumfuatilia mpaka nyumbani kwake. Ni hatari sana kwake.”
Alvin alitafakari kwa muda na kusema, “Kwa hali hiyo, itabidi ahamie kwenye nyumba yangu sasa.”
“Ndiyo.” Macho ya Thomas yakaangaza. "Nilisikia kwamba ulinunua nyumba ya kifahari karibu na bahari miaka michache iliyopita. Sarah anapenda kuishi kando ya bahari. Twende huko.”
Alvin aliganda. Kweli alikuwa na jumba la kifahari kando ya bahari huko Mombasa, lakini… aliwahi kuishi huko na Lisa. Alikuwa chini ya maamuzi tata. Akubali ama akatae!
“Kaka…” Sarah alimkazia macho Thomas lakini kwa haraka akamgeukia Alvin. Kwa sura nzuri, alisema, "Alvin, ulinunua jumba la kifahari ufukweni mwa bahari kwa sababu ulikumbuka niliwahi kusema napenda kuishi kando ya bahari?"
Akiwa amekabiliana na macho ya mwanamke huyo yanayometameta, Alvin alitazama pembeni na kutabasamu. “Ni kweli mpenzi!”
'Basi nitahamia huko,” Sarah aliuma mdomo wake uliopauka na kusema kwa tabasamu tamu.
Alvin alikuwa hoi na aliishia tu kutikisa kichwa.
Thomas aliongeza, “Lakini hiyo siyo solution. Huwezi kujificha milele katika jumba la Alvin Kimaro. Huwezi hata kwenda kazini kwa sasa kwa sababu ya maneno ya watu. Kila mtu anakuita wewe ni mchepuko tu. Hii si haki kwako dada yangu. Ni wazi nyinyi wawili mlipendana kabla ya Lisa. Kwanini wakuseme vibaya?”
“Kaka achana nao. Tayari nimeridhika kwamba nimerudiana na Alvin.” Macho ya Sarah yakarembua kwa deko. "Niko tayari kuitwa mchepuko milele ikiwa ni kwa ajili yake."
Alvin alikipapasa kichwa chake na kuhisi hisia za hatia nyingi moyoni mwake. "Usijali, sitakuacha uwe mchepuko milele." Dokezo la chuki likaangaza machoni pake. "Naenda kwa Mzee Kimaro sasa hivi kushughulikia suala lako."
Baada ya kutoka hospitali, Alvin aliingia kwenye gari. Saa moja baadaye, alifunga breki mbele ya makazi ya familia ya Kimaro
Jua lilikuwa linaangaza sana, na Lisa alikuwa ameketi kwenye bustani ya Bibi Kimaro akila zabibu huku akisoma kitabu cha riwaya za Jomba Wajo. Sekunde kadhaa baadaye, hisia za ajabu zikamjia ndani ya moyo wake. Alihisi kama Alvin alikuwa karibu yake, lakini zilitoweka ghafla baada ya kugeuza kichwa chake na kuona mimea tu na upepo.
Aliporudisha tena mawazo yake kwenye kitabu, alisikia tambo za mtu zikitembea kwa hatua kubwa. Aliinua kichwa chake baada ya kusikia sauti ya nyayo hizo. Alvin alijitokeza akiwa amevalia suruali ya kawaida ya rangi ya kijivu iliyokoza na shati la bluu juu yake. Mikono yake ilikuwa imekunjwa. Mwonekano wake mzuri uliweza kuufanya moyo wa mwanamke yeyote kupepesuka, lakini ilisikitisha kwamba macho yake yalikuwa yamejawa na mapenzi sifuri.
Macho yake yalitisha zaidi kuliko walipokutana mara ya kwanza. Lisa alijipa moyo kwamba alikuwa amezoea ujeuri wa mwanamume huyo, lakini kwa wakati huo hakuweza kuwa na ujasiri wa kukabilana naye hata kidogo. Mwanaume aliyempenda sana alionekana kuwa hatari zaidi ya mtu yoyote aliyemfahamu kwa wakati huo.
“Unataka nini?” Lisa aliuliza huku akiinamisha macho yake kana kwamba anaficha huzuni ndani yake.
“Wewe ni mke wangu. Chochote ninachokitaka kwako nitachukua muda wowote ninapohitaji.” Alvin alifoka na kumfanya Lisa kupigwa na butwaa kwa jinsi alivyosema maneno hayo.
“Kwa hiyo bado unajua kuwa mimi ni mkeo? Nilidhani umesahau zamani,” Lisa alisema kwa dhihaka.
Alvin alikasirika. “Usinisumbue. Nahitaji ufanye kitu kimoja tu kwa sasa. Nitaitisha mkutano wa vyombo vya habari. Unatakiwa kutoa taarifa kwa umma kwamba mimi na wewe tuliachana mwezi uliopita. Kuhusu ndoa yetu, ilikuwa ni ndoa ya mkataba tangu mwanzo na mktaba wetu umekwisha rasmi.”
Lisa alimtazama kwa mshtuko. Macho yake yalionyesha kutokuamini.
Sura ya: 298
Alvin hakufurahishwa na macho yake na hakuweza kujizuia kuwasha sigara. Baada ya kuvuta pumzi, kadhaa aliufanya moyo wake kuwa mgumu. “Umenisikia? Nilikuoa tu kwa sababu nilikuwa nakerwa na familia ya Kimaro kuwa wananilazimisha kuoa. Na wewe ulitaka nikuoe tu kwa sababu ulinidhania kuwa mimi ni mjomba wa Ethan Zakaria Lowe.”
Lisa alishindwa kuvumilia tena. "Ndio, sikatai, tulifunga ndoa mwanzoni tu kwa sababu ya mkataba, lakini baadaye, sote wawili tulikubali kukaa kwenye uhusiano. sikukulazimisha.”
"Nyamaza." Alvin alijikuta maneno yake yakimchoma. “Ni kwa sababu wewe ndiye ulianza kunitongoza. Unafikiri mwanamke mwenye ujasiri wa kumtongoza mwanamume huyo ni mwanamke wa muoa kweli?”
Ingawa moyo wake ulikuwa tayari umejawa na matundu, macho ya Lisa bado yalikuwa mekundu kwa kukata tamaa. "Alvlisa, ni wewe kweli? Au Sarah ameshakufanya kuwa msukule? Ili tu Sarah asionekane mbaya kwa wengine, unataka niseme uongo na kutangaza kuwa tayari tumeachana. Ulimwengu wa nje utafikiri kwamba nilikuja kwako kwa sababu ya pesa za familia ya Kimaro. Ndiyo, jina la Sarah litatakaswa, lakini vipi kuhusu jina langu? Nitalaaniwa mpaka kwenye kaburi langu. Umewahi kufikiria hisia zangu kweli?"
“Kwanini nizingatie hisia zako? Sikupendi na sikuhitaji.” Alvin alikunja uso bila kujali, maneno yake yalizidi kuwa makali na ya kuchoma moyo.
Hatimaye Lisa aliachia kicheko cha uchungu, machozi yote yakimtoka. Hakujua ilikuwa ni kwa sababu njama za Sarah zilikuwa na nguvu sana, au ni kwa sababu Alvin hakuwahi kumsahau Sarah tangu mwanzo.
Alvin alijikuta akicheka bila raha. “Umesikia nilichosema?”
“Kwanza, hujali kuwa umemsaliti mke wako, lakini unataka nijishushe ili kulinda heshima ya Sarah na sifa zako! Endelea kuota. Watu kwenye mtandao hawana makosa. Sarah atabaki kuwa mchepuko tu." Lisa alishindwa kujizuia na kumfokea.
"Nyamaza!" Alvin alimpiga kofi usoni bila huruma. Lisa aliganda na kufunika uso wake, machozi makubwa yakitiririka mashavuni mwake.
"Lisa Jones, nakuonya, nisikusikie tena ukimtukana Sarah." Alvin alikodoa macho na kuonya neno kwa neno. "Ninakushauri ufanye kama ninavyosema, au nitamwambia Chester amwambie Daktari Angelo aache kutibu ugonjwa wa baba yako."
"Alvin, nyoko wewe." Lisa alilazimishwa kulia na kulia kwa kukata tamaa.
“Namaanisha.” Kwa sababu fulani, Alvin hakutaka kuona sura yake ya kulia na akageuka kuondoka.
“Alvin Kimaro, nitadili na wewe hatua kwa hatua” Lisa akasema kwa ghafula, “sijali hata kama utanitaliki, sitakuachia watoto wangu na nitafuta uhusiano wote na wewe.”
"Endelea kuota. Watoto ni wangu.” Alvin alimtishia. “Lisa Jones, kama unataka Mawenzi ikufilie mbali, endelea kucheza na mimi. Najua pia Joel ndiye ndugu yako pekee aliyebaki duniani. Jitafakari!” Alvin alimaliza na kuondoka bila kuangalia nyuma. Lisa aliitazama sura yake isiyo na huruma iliyoonekana kugubikwa na giza.
Katika muda usiozidi dakika 20, Lisa alipokea simu kutoka kwa Daktari Angelo akisema kuwa asingeweza kuendelea kumtibu tena Joel.
Lisa alichanganyikiwa. Ikiwa angekosa mtu wa kumtibu Joel, Nina Mahewa na binti yake wasingemjali pia. Familia ya Ngosha iliongozwa na Damien sasa. Joel angekufa muda si mrefu.
Hakuwa na chaguo tena, na suluhisho pekee ilikuwa ni kukubali mkutano wa vyombo vya habari ili kukiri kwa dhati kuwa yeye na Alvin hawakuwa mke na mume tangu kitambo.
[Natamka kwa dhati kwamba Alvin Kimaro si mume wangu tangu mwezi jana. Natamani apate mpenzi wake wa kuendelea kumtunza kwenye hali yake. Sasa kwa kuwa mambo yamefikia hatua hii, sina budi kusema ukweli. Mimi na Alvin Kimaro tuliachana mwezi uliopita. Tulioana tu kwa sababu Alvin alilazimishwa na familia yake, na kila mmoja wetu alichukua kile alichohitaji katika ndoa yetu. Hakukuwa na hisia za kimapenzi kati yetu.]
[Sarah Boris Langa Njau ni mpenzi wa Alvin wa utotoni ambaye alitengana naye kwa sababu ya zisizozuilika. Yeye si mchepuko. Kwa dhati ninawatakia wawili hao kila la heri.]
Baada ya chapisho hilo kupakiwa…Wanamtandao wengi walimkaripia Lisa kwenye profile yake.
[Unamaanisha nini kusema kila mmoja alichukua kile alichohitaji? Alvin Kimaro lazima awe amekupa pesa nyingi basi!]
[What the f*ck, kwa kweli niliamini katika uhusiano wako hapo awali. I feel like a fool now.]
[How much money did you receive?]
[Nafikiri unapaswa kuacha kuwa Mkurugenzi wa Kampuni na kuingia katika uigizaji. Uigizaji unakufaa.]
Mara tu baada ya hapo, Sarah alianza kuchapisha picha mbalimbali za Alvin na yeye wakati wa miaka yao ya shule. Wanamtandao wengi walianza kusifia upendo wao wa muda mrefu.
Lisa hakuzingatia hilo. Ali’delete kabisa app ya Facebook kwenye simu yake na hakusoma tena habari hizo.
Pamela akampigia simu kwa hasira. "Lisa Jones, umekuwa kichaa? Unamaanisha nini kusema uliachana na Alvin Kimaro mwezi uliopita? Hujaachika hata kidogo! Ana uhusiano wa kimapenzi na yule malaya Sarah Njau. Wanawezaje kukufanyia uhuni kama huu? mbona unafosi kuwa mpole kiasi hicho? Ningekuwa mimi, heeeh! Sijui tu. Umesikia watu hao wanavyokuita? Hapana, sikubali. Nataka kuwafunza adabu mbwa hao wawili, hawanijui eeh?!”
“Pamela, sikuwa na chaguo. Alvin alinitishia baba yangu. Nisingetoa kauli hiyo, angesimamisha matibabu ya baba yangu,” Lisa alisema akiwa hoi.
“Bado unasema Alvin ni binadamu? Kweli ni!@#$%^&. Fanya haraka uachane naye! Mbwa huyo!” Pamela alikasirika.
"Nadhani atanitaliki tu baada ya kuzaa watoto."
"Anataka kuiba watoto wako pia?" Pamela karibu kutapika damu. “Si ana Sarah? Mwache azae na Sarah. Beba watoto wako mama!”
"Familia ya Kimaro inawezaje kuruhusu watoto wao kulelewa nje?" Lisa alitabasamu kwa uchungu. “Usijali, nitafikiria njia.”
“Kweli sikubali. Huwezi kumruhusu Sarah awe mama wa kambo wa watoto wako.” Pamela alionya.
“Bila shaka.” Lisa alikata simu huku akiwa na uso wa huzuni.
•••
Sarah alihamia kwenye jumba la kifahari la ufukweni mwa bahari huko Mombasa.
Thomas alitazama huku na huko na kusema, “Sarah, mahali hapa ni pa anasa sana. Haishangazi ulikuwa unasumbua ubongo wako kujaribu kupata njia ya kuingia humu. Nilisikia kwamba huu ndio ufukwe wa bei ghali zaidi huku Mombasa.”
"Sikutaka kuhamia hapa kwa sababu ni ghali." Sarah alitabasamu na kuketi kwenye sofa.
“Najua. Ni kwa sababu hapa ndipo Lisa Jones na Alvin walikuwa wakikaa. Hehe, Lisa akigundua, labda atatapika damu kwa hasira." Thomas alimtazama dada yake kwa mshangao. “Alikuwa akijifanya kana kwamba ni Bibi Kimaro, lakini sidhani kama anaweza kulinganishwa hata na thamani ya kinyesi cha Bibi Kimaro kwa sasa. Hujui ni familia ngapi za kitajiri huko Nairobi zinajikombakomba kwangu sasa. Kila mtu anajua kuwa wewe ndiye Bibi Kimaro wa siku zijazo.”
"Hakuna haraka. Nitakapoolewa na Alvin, kutakuwa na watu wengi zaidi ambao watakusujudia,” Sarah alisema kwa kiburi. "Kwa jinsi mambo yanavyoenda, utakuwa mfalme hivi karibuni."
Simu ya Thomas iliita ghafla na akaenda pembeni kuipokea. Ghafla alianza kucheka. Kisha, akarudi na kusema, “Natoka.”
"Wapi?" Sarah akamtazama kwa wasiwasi. “Usiende kufanya ujinga wako tena. Japo Alvin ananipenda, hatakubaliana na ujinga wako, usiniharibir.”.”
"Usijali, naenda kumpa Pamela Masanja somo dogo tu la namna ya kuishi jijini Nairobi." Thomas alifoka.
Sarah akacheka kidogo. "Rafiki ya Lisa Jones?"
“Ndiyo. Anaonekana mrembo sana, lakini ana kiburi sana. Nilipomfuata hapo awali, alinikataa na kunitukana. inaniuma sana kukataliwa na msichana mimi.”
“Hah, bado nakumbuka aliponitukana hospitalini." Sarah aliongea kwa sauti ya kisasi.
Thomas alikoroma. “Nilimwekea mtu wa kumfuatilia kwa siku kadhaa sasa. Niliapa, nisipomf*** labda mimi si Thomas Njau.”
Sarah aliikunjua uso wake kwa tabasamu. Ingekuwa ni mtu mwingine yeyote, asingemkubalia. Lakini kwa Pamela Masanja, hakuwa na pingamizi. Hakumpenda kwa kuwa ni rafiki wa Lisa.
"Sawa broo. Nenda kafurahie, ila usimwue tu. Kula kabisa huo mk***”
“Usijali. Najua ninachofanya.” Thomas alivimba kichwa....ITAENDELEA..
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
