JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................295-296

Sura ya: 295

Ilikuwa haiwezekani.
Alvin alikunja uso. “Lisa, mwanamke ninayempenda amekuwa Sarah muda wote. Haijawahi kubadilika.” Mwili wa Lisa ulitetemeka.
Alitumia sentensi moja fupi tu kukana maisha yao yote ya nyuma. Alimaanisha nini kwake?
"Kwa hiyo yote uliyoniambia kwenye jumba la baharini yalikuwa ni uongo? Ulisema utanipenda katika maisha yako yote." Lisa alikuwa karibu kuangua kilio. “Unawezaje kunifanyia hivi? Umebadilika tu ghafla. Je, huoni kwamba wewe ni mtu wa ajabu sana?”
“Usiseme neno lingine. Naujua moyo wangu mwenyewe.” Alvin alikasirishwa na macho yake. “Nimechoshwa na wewe tangu zamani sana. Isingekuwa watoto, tungekuwa tushaachana zamani.”
Lisa alishusha pumzi. Wakati huo, alihisi moyo wake ukizidi kuwa baridi na baridi zaidi. Ilikuwa hivyo? Je, alikuwa amemvumilia muda wote huu? Je, asingeweza kusimama naye tena?
Hata hivyo, Alvin hakujali. Aliendelea kusema kikatili, “Baada ya wewe kuzaa watoto, nitakupa talaka. Usijali, nitakupa kiasi chochote cha pesa unachotaka. Kitatosha kwako kutumia maisha yako yote. Kuanzia leo na kuendelea, acha kumsumbua Sara. Ikiwa sivyo, utabeba matokeo yake."
Alipokuwa akisema maneno hayo, macho yake yalijawa na hasira kali iliyopenya mwilini mwa Lisa. Damu yake ikaingia baridi.
“Alvin, mpumbavu wewe! Wewe ni mpumbavu kweli!” Hakuweza kuvumilia tena. Alilia na kuchukua kikombe mezani na kumrushia.
Alvin alikwepa kwa kutikisa kichwa. Alipoona anapandisha hasira kiasi cha kukaribia kupoteza akili yake, alijidhibiti ili asiweze kumuumiza. Akabonyeza intercom. "Waite walinzi ndani na kumtoa mtu huyu."
“Bwana Kimaro…” Shangazi Yasmine alisema huku akiwa na hofu, “Bwana Mkubwa, huwezi kufanya hivi.”
“Anti Yasmine, unahitaji kukumbuka ni nani anayekulipa mshahara,” Alvin alionya kwa ukari.
“Usiseme tena, Alvin. Ikiwa unataka kunipa talaka, unaweza kunipa wakati wowote unaotaka. Lakini sitawahi kutoa watoto wangu kwa mtu yeyote. Si hivyo tu, sitawahi kumwacha Sarah awe mama yao wa kambo.” Baada ya Lisa kumfokea kana kwamba amerukwa na akili, aligeuka na kuondoka huku akiwa amechanganyikiwa.
Alvin alipata maumivu ya kichwa kutokana na kelele hizo. Haukupita muda mrefu, Hans aligonga mlango na kuingia. "Bwana Mkubwa, nilipata matokeo baada ya kuchunguza kaburi..."
"Kaburi gani?" Alvin aliinua kichwa na kuuliza.
Hans alipigwa na butwaa. Je, Sarah hakuwa anatibu ugonjwa wa Alvin? Kwanini kumbukumbu yake haikuwa bora lakini badala yake ilizidi kuzorota? Hata hivyo, alipofikiria kuhusu matokeo ya uchunguzi, alihisi baridi moyoni mwake. Alisema kwa haraka, “Wakati fulani uliopita, ulinitaka nichunguze kaburi la Jennifer. Nilishirikiana na mlinzi wa makaburi hayo kufanya uchunguzi. Kwa kweli kilichomo kwenye jeneza si mwili wa binadamu, ni mwili wa mbwa!”
“Unataka kusema nini?” Alvin alizidi kuchanganyikiwa huku akimsikiliza, hivyo akamkatisha kwa kuudhika.
“Bi. Njau alisema angemzika Boris karibu na kaburi la Jennifer, lakini mwili kwenye uliomo kwenye jeneza la Jennifer si wa binadamu…”
“Unashuku kwamba Sarah hakuuzika mwili wa Jennifer kulipiza kisasi kwake?”
“Hilo linawezekana,” Hans aligugumia kujibu. Baada ya yote, Alvin ghafla alikuwa akimthamini sana Sarah wakati huo.
Alvin akatazama juu. Hasira usoni mwake ilikuwa imefurika. “Inatosha. Sarah hayuko hivyo.”
Ilikuwa haiwezekani kwa yeye kuamini.
“Lakini…”
“Hans, naona kwamba umekuwa ukielewana vizuri na Lisa hivi karibuni. Una nia ya kumsaidia. Ngoja nikuambie, hakuna anayemuelewa Sarah zaidi yangu. Yeye ndiye mwanamke ninayempenda. Sitamruhusu mtu yeyote kumhoji,” Alvin alisema kwa hasira, “Jambo hili linaishia hapa.”
Hans alishangaa. "Bwana Mkubwa, sijawahi-"
"Toka nje." Alvin alifungua laptop yake na kutoa amri ya kuondoka.
Hans alihisi kuchanganyikiwa na akaona ni ajabu. Ushahidi ulikuwa mbele yake, lakini Bwana Mkubwa alionekana kana kwamba hakuweza kutofautisha kati ya mema na mabaya hata kidogo. Alvin aligeuka kuwa kuwa wa ajabu sana. Ni kana kwamba alikuwa amegeuka kuwa mtu mwingine.

Ndiyo, Hans alikiri kwamba Alvin alimpenda Sarah hapo awali, lakini aliweza kuona kwamba alikuwa na Lisa moyoni mwake pia. Hans alihisi kuwa kuna kitu hakikuwa sawa kadiri alivyofikiria zaidi juu yake.
Hans alienda kwa Mzee Kimaro baada ya kutoka kazini siku hiyo. Tangu Lisa aliporudi kutoka ofisini kwake asubuhi, aliendelea kukaa kwenye kibaraza chake na kutazama nje bila kusema neno.
Hans alipofika, alimtazama kwa huzuni. “Alvin anataka uniambie nini? Au hana uwezo tena wa kuvumilia hivyo kakuambia ulete hati za talaka?”
“Bibi mdogo, umeelewa vibaya. Bwana Mkubwa hajui kwamba nimekuja kukutafuta.” Hans alisema kwa kusitasita, “Ninajua kwamba Bwana Mkubwa amekuwa akichukulia mambo tofauti sana siku hizi. Nadhani hii sio dhamira yake. Amekuwa wa ajabu…”
“Unashuku kwamba Sarah alimfanyia kitu wakati wa matibabu?” Lisa aliuliza kwa sauti ya chini.
Hans alifungua kinywa chake. Muda mfupi baadaye, alisema kwa hali ya kuchanganyikiwa, “Siwezi kueleza kwa kweli, lakini ninahisi kama Bwana Mkubwa amevurugwa akili. Kweli, hapo awali aliniomba nichunguze kaburi la Jennifer. Kuzungumza kimantiki, alipaswa kuwa na shaka kidogo na Sarah. Lakini matokeo yalipotoka, hakujali kabisa. Hii si kawaida yake ya kufanya mambo. Hata alipokuwa akimpenda Sarah siku za nyuma, hakuwahi kuwa mtu wa namna hii. Kando na hilo… Kabla ya hili, Bwana Mkubwa alikuwa akimkwepa Sarah kadri iwezekanavyo isipokuwa wakati wa vipindi vya matibabu. Hivi majuzi, alikwepa hata tafrija zilizofanywa na Rodney na wengine. Sasa, cha kushangaza, ghala akawa karibu sana na Sarah. Hii ni ajabu sana.”
Uso wa Lisa ulikuwa umepauka na kujawa huzuni. "Nilihisi pia. Aunty Yasmine aliniambia kuwa ni kana kwamba Alvin amegeuka kuwa mtu tofauti baada ya kipindi chake cha juzi cha matibabu na Sarah. Ndiyo maana nilijikaza na kwenda kumtafuta kwenye kampuni.”
Moyo wa Hans uliruka. Ilionekana kana kwamba alikuwa amekisia kwa usahihi. “Bibi Mdogo, Bwana Mkubwa lazima awe amechezewa kisaikolojia. Usimchukulie maneno yake ya kuumiza kwa uzito. Hakika ana wewe moyoni mwake. Mimi ni msaidizi wake binafsi, naweza kuhisi kitu.”
“Niambie, ninaweza kufanya nini? Ananidharau sasa.” Lisa alitabasamu kwa huzuni. "Nilienda ofisini kwake lakini nikafedheheshwa. Sasa ananichukia.”
Hans alisema kwa wasiwasi, “Bibi mdogo, ingawa sielewi ni kwa nini Bwana Mkubwa amekuwa hivi ghafla, wewe ni mke wake na yeye ni baba wa watoto. Hakika hutaki aendelee kuwa hivi, sivyo?”
Lisa akatikisa kichwa. Alikuwa katika kuchanganyikiwa. “Ni kweli sitaki hilo, lakini uelewe kuwa Alvin ndiye anatawala familia ya Kimaro sasa. Hata kama wanafamilia wa Kimaro wananiamini, hakuna tunachoweza kubadilisha ikiwa Alvin mwenyewe hataniamini. Ana nguvu zote na ushawishi. Mzee Kimaro na Bibi Kimaro ni wazee, huku Rodney na Chester wanamwamini Sarah sana. Hawatanisaidia chochote.”
Moyo wa Hans ulizama. Ilibidi akubali kwamba alichosema Lisa kilikuwa ukweli. "Bibi mdogo, kusema kweli, sikuwahi kufikiria kuwa Bi Njau angetisha vile vile. Ikiwa tutamwacha mtu kama huyo abaki kando ya Bwana Mkubwa, fikiria jinsi atakavyowatendea watoto wawili ulio na ujauzito wao sasa katika siku zijazo.”
Lisa aliumia sana. Hilo ndilo alilokuwa na wasiwasi nalo. Aliinamisha kichwa chini na kugusa tumbo lake. Macho yake yalishika alama ya uchungu mwingi. 'Watoto, nifanye nini ili kuwalinda?'
"Hans, unaweza kutafuta mwanasaikolojia mzuri? Usiruhusu Chester ajue. Nataka kujifunza kuhusu hali ya jumla ya Alvin.”

Sura ya: 296

"Sawa." Hans akashusha pumzi ya furaha. Kwa bahati nzuri, Lisa alikuwa hajakata tamaa.
Kama msaidizi wa mtu tajiri zaidi wa Kenya, Hans alikuwa na uhusiano mzuri pia na watu mashuhuri. Harakaharaka akampata daktari anayeitwa Dr Mauki. Ingawa Dk. Mauki alikuwa amestaafu kwa miaka mingi, alikuwa na uzoefu mkubwa katika utafiti wa kisaikolojia.
Jioni hiyo, Hans aliongozana na Lisa kukutana na Dk Mauki.
Baada ya Dk. Mauki kusikia kuhusu mabadiliko ya Alvin, alirekebisha miwani yake ya kusomea. Alisema, “Nilipokuwa na majadiliano ya kitaalamu na wanasaikolojia wakuu kutoka Ulaya na Marekani, niliwasikia wakitaja ujuzi wa kale wa kisaikolojia ujulikanao kama ‘Hypnotic Mind Control’ ambao ungeweza kuharibu hisia na kumbukumbu za mtu na kumtengenezea hisia tofauti. Dalili za rafiki yako zinafanana kabisa na hizo.”
Lisa alishtuka. Aliuliza kwa hamaki, “Je, inaweza kuponywa?”
Dk Mauki alicheka kwa uchungu. "Tayari nimesema kwamba ujuzi huu wa hypnotic ni wa kale sana. Marafiki zangu wanasaikolojia kutoka sehemu mbalimbali duniani walisema hivyo tu kwa msingi wa uvumi. Hakuna hata anayejua jinsi ya kufanya. Ustadi huu mbaya umepigwa marufuku katika taaluma ya kisaikolojia. Inavyoonekana, hakuna hata mmoja atakayethubutu kujaribu katika hali ya kawaida kwa sababu kudhibiti ubongo na hisia za binadamu ni jambo lisiloweza kutabirika. Mara nyingi hufanyika bila idhini ya mhusika ili matokeo yawe bora. Kwa sababu ni kinyume cha maadali ya taaluma yetu kubadili akili ya mtu bila idhini yake, ujuzi huu hutumiwa na watu wenye nia mbaya tu hivyo ulianza kusahaulika polepole.”
Lisa na Hans waliogopa sana. Hawakutarajia kwamba Sarah angekuwa mkatili kiasi kwamba angetumia ustadi wa hypnotic ambao umepigwa marufuku, kubadili akili ya Alvin. Alikuwa mtu aliyempenda, kwa ajili ya wema.
Ilikuwa ni bahati kwamba Alvin alikuwa sehemu ya asilimia ambayo haikua nyuma ya kurekebishwa.
"Kwa hiyo hakuna nafasi kabisa?" Lisa aliuliza huku akikataa kukata tamaa.
“Hiyo ni kweli, Bw. Mauki. Tafadhali fikiri juu yake,” Hans alisema kwa haraka, “Ingawa umestaafu, najua kwamba una ujuzi zaidi kuhusu hili kati ya wanasaikolojia wote nchini Kenya.”
Dk Mauki alipumua. "Kwa hakika siwezi kumponya, na kuna madaktari wachache sana wanaoweza kutibu ugonjwa huu. Hata ukipata daktari anayeweza kufanya hivyo, nitakushauri usifanye hivyo kwa sababu mchakato wa matibabu ni hatari zaidi. Nafasi za kupona ni asilimia moja tu, kwa hivyo sijawahi kusikia kesi zilizofaulu. Nadhani waliopata matibabu bado ni walemavu."
Akili ya Lisa ilikuwa tupu, na ni kana kwamba moyo wake pia ulikuwa umeacha kupiga.
Sebule ilikuwa kimya kwa dakika nzima. Kisha, Lisa akauliza. "Kwa hivyo njia bora ni kumwacha aendelee kuwa hivi?"
“Ndiyo, ndivyo ninavyomaanisha.” Dk. Mauki akanywa kahawa.
Hans aliuliza kwa wasiwasi, “Vipi kuhusu baadaye? Je, kutakuwa na madhara yoyote?"
"Mbali na hisia zake kudhibitiwa na mtu mwingine, hakuna kitu kikubwa. Itakuwa kama anaishi ndotoni.” Dr Mauki alimtazama Lisa kwa huruma. "Ni wale tu aliowapenda hapo awali ndiyo watakuwa hawana bahati."
Midomo ya Lisa ilitetemeka. Yeye hakuwa na bahati mbaya tu. Alikuwa katika kuzimu pia.
"Asante, Dk. Mauki." Alisimama na kutoka nje ya nyumba ya Dokta Mauki akiwa kama hana roho.
Hans alimfuata kwa wasiwasi. “Bibi mdogo. ..”
“Acha kuniita ‘Bibi Mdogo’. Labda sitakuwapo tena hivi karibuni.” Lisa aliyatazama yale magari yaliyokuwa yakitembea barabarani huku akijisikia mnyonge.
Ilikuwa ni ndoa kamilifu. Hakujua kwanini alikuwa akipitia mambo hayo sasa. Lisa pia hakuelewa ni kosa gani alilofanya.
“Sikuwahi kufikiria kwamba Sarah angetisha sana. Bwana Mkubwa hawatarajii kama haya yanafanyaika pia," Hans alisema kwa wasiwasi.
“Hans, hatuwezi kufanya lolote. Ikiwa tutammshughulikia Alvin kwa nguvu, tutaweza hata kumuumiza. Mwache tu, Mungu atasaidia.”
Hata kama hakumpenda tena, bado angekuwa wa kawaida kwa sehemu kubwa. Ilikuwa tu kwamba hisia zake zilikuwa chini ya udhibiti wa mtu mwingine. Bado alikuwa mtu tajiri zaidi nchini Kenya ambaye kila mtu alimheshimu.
"Na wewe je?" Hans alimuhurumia kweli.

"Mimi?" Lisa alitazama chini na kugusa tumbo lake. “Hans, kama kweli unamjali Alvin, lazima unisaidie. Sarah yuko tayari kumuumiza hata Alvin. Ikiwa watoto wangu wote wawili wataangukia mikononi mwake wakati ujao, bila shaka watateseka sana.”
“Usijali Bibi Mdogo. Ilimradi ni kwa manufaa ya watoto wa Bwana Mkubwa, nitakuunga mkono kwa nguvu zangu zote bila kujali utakachochagua kufanya—”
Hans hakuwa amemaliza kuzungumza Alvin alipompigia. "Ulienda wapi? Leo ni siku ya kuzaliwa ya Sarah. Nenda kClub yoyote maarufu na ukodi ukumbi na kuupamba. Nataka kumfanyia suprise! Umesikia nilichosema?” Sauti ya Alvin ilikuwa kali.
"... Sawa, nitaenda mara moja." Hans alimtazama Lisa kwa huruma. “Bibi Kijana—”
“Kuwa upande wa Alvin na ufanye chochote anachokuomba ufanye.” Lisa akamkumbusha, “Kama unatakakunisaidia, mfanye Alvin na wanafamilia wa Kimaro wafikiri kwamba mimba yangu imeharibika. Ni hapo tu ndipo ninaweza kuondoka.”
“Unataka kuondoka?” Hans alishangaa.
"Ndiyo, hiyo ndiyo njia pekee kwa watoto wangu wawili kuweza kuishi." Macho ya Lisa yalijawa na uchovu.
Hans alitikisa kichwa bila kusita. Alikuwa na deni kubwa kwa Alvin. Maadamu angeweza kuwasaidia watoto wake, alikuwa tayari kusaidia kwa njia yoyote aliyoweza.
Baada ya Hans kuondoka, familia ya Kimaro ilituma gari kumrudisha Lisa kwenye nyumba ya kifahari. Usiku akiwa amelala kwenye kitanda kikubwa tupu, alipokea simu kutoka kwa Kelvin. “Lisa kuna nini kati yako na Alvin? Nilisikia kuwa wewe ni mjamzito. Anawezaje kukufanyia hivi?”
Lisa alikaa kimya kwa muda na kukunja blanketi. Kisha, alijifanya kama hakuna kitu kibaya na akacheka. “Umesikia nini?”
'Sikusikia chochote. Niliona kwa macho yangu mwenyewe." Sauti ya Kelvin ilijaa hasira. "Alvin amekodiukumbi mzima kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Sarah usiku wa leo. Aliajiri na mtu kwenda kununua mauwaridi safi kutoka nje na kuajiri mpishi mkuu wa vyakula vya Kizungu kutoka Dubai. Hata alilipua fataki kando ya bahari kwa saa mbili mfululizo na kumzawadia jumba la kifahari la dola milioni 5. Kila mtu katika Nairobi anajua kuhusu hilo sasa…”
"Kwa hiyo?" Lisa alitamka maneno hayo mawili kwa sauti kali.
Alijkuwa amejitahidi sana kupotezea mambo fulani, lakini aliposikia kwamba Alvin alikuwa akimthamini sana Sarah, alihisi maumivu makali kana kwamba kuna kisu kinampasua kipande kwa kipande. Alikuwa karibu kupandwa kichaa kutokana na wivu, lakini angeweza kufanya nini? Alvin alikuwa amelazwa akili.
“Lisa, nilikuzuia sana wakati ule. Alisema anakupenda. Lakini muda haujapita na tayari ameshakutupa wewe na mimba yako!” Kelvin alikasirika.
“Kelvin, usiseme tena. Nimechoka. Nataka kupumzika.”
“Lisa, usiogope. Haijalishi nini kitatokea, nitakuwa… daima kuwa rafiki yako. Unaweza kunitafuta kwa msaada. Ninaendelea vizuri sasa. Mimi si yule mnyonge tena ambaye ninaweza kukanyagwa tu na Alvin,” Kelvin alisema kwa upole.
“Sawa, asante.” Baada ya Lisa kukata simu, hakulala kwa usiku mzima.
Siku iliyofuata, alitazama simu yake. Habari ya mjini kwenye mitandao ilikuwa inamhusu Alvin. [Alvin Kimaro ls Having An Affair],
[Alvin Kimaro Amkabidhi Mpenzi Wake Mpya Jumba la kifahari la Dola Milioni 5]
[Alvin Kimaro sasa Ambwaga Rasmi Mke Wake Aliyeharibika Sura: Aibuka Na Chombo Safi!]
[Alvin Kimaro Alitumia Usiku Huo Pamoja Na Mpenzi Wake Mpya Hotelini]
[Utambulisho wa Mpenzi Mpya wa Kimaro Wavunja Rekodi!].
Lisa alichukua tu picha chache na kuzitazama. Picha ya Alvin akiwa amemshika Sarah mkono huku wakiingia kwenye jumba hilo la klabu ilizunguka mtandaoni. Pia kulikuwa na picha walipoingia ndani ya hoteli hiyo wakiwa wamekumbatiana na video za fataki hizo za kupindukia.....ITAENDELEA...

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.