JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................293-294
Sura ya: 293
Alvin alihisi wasiwasi na hofu moyoni mwake.
“Si ajabu hukuungana na Rodney na wengine hata walipokualika. Samahani, labda sikupaswa kwenda. Mwishowe, urafiki wako na Rodney na wengine umekuwa mbaya,” Sarah alisema kwa hatia.
“Sio kosa lako. Cindy ndiye wa kulaumiwa,” Alvin alisema kwa huzuni, “Hivi dunia nzima hakuna wanawake wengine wazuri? Kwanini Chester ameamua kuwa na mwanamke huyu mwenye sifa mbaya kwenye tasnia ya muziki?”
"Kwani humjui Chester? Daima amekuwa na tabia ya kuchezea wanawake, hasa wenye umaarufu fulani. Labda anatoka naye tu kwa kujifurahisha. Anaweza kuachana naye baada ya muda mfupi.” Sarah alitazama wakati. "Wacha tuanze matibabu."
“Sawa.” Alvin akasimama.
Katika chumba cha matibabu, Sarah alicheza wimbo wa ajabu kwenye simu yake. Wimbo huo haukuwa wa Kiswahili na ulisikika kuwa wa zamani sana. Alvin alikuwa hajawahi kusikia kabla. "Kwanini unacheza wimbo leo?"
"Ndiyo, tunabadilisha hisia zako kwa njia nyingine leo. Huu sio wimbo in such, wahindi wanaitaga ‘mantra’." Sarah akatoa sarafu ya zamani. "Baadaye, utaangalia sarafu hii kwa umakini."
Dakika tatu baadaye. Alvin alisikia sauti kubwa ya kutetemeka masikioni mwake. Ni kana kwamba alikuwa amepoteza fahamu mara moja, na macho yake meusi yalionekana kuwa matupu.
Baada ya Sarah kuendelea kuuliza maswali machache na kuthibitisha kuwa kweli amepoteza fahamu, aliinama chini na kumnong’oneza sikioni, “Alvin, mtu unayempenda ni Sarah. Mtu unayempenda ni Sarah. Unamchukia Lisa zaidi na zaidi …”
Jioni mida ya saa kumi, Lisa alikuwa amepumzika kwenye bustani ya Bibi Kimaro.
Hapo hapo, Shangazi Yasmine alikuja na kumshauri kwa msisitizo, “Bibi mdogo, unapaswa kurudi kwenye chumba sasa. Bwana Kimaro alikuwa akipiga kelele alipokuja kukutazama na kukukosa.”
“Nirudi ili akanikasirikie?” Lisa aliinamisha kichwa chini ili kunusa harufu ya maua aliyokuwa ameshikiria. “Sirudi nyuma. Tutaishia kwenye vita kila ninapomwona Sarah. Sitaki kuathiri hisia zangu.”
"Lakini ikiwa hujali, huogopi kwamba Bwana Mkubwa atanyakuliwa na Sarah?" Aunty Yasmine akahema. “Bibi mdogo, nitakuwa mkali kwa maneno yangu. Ikiwa nyinyi wawili mnataka kuachana, hakuna mtu katika familia ya Kimaro ambaye atakuruhusu uchukue watoto. Wewe ndio unapata tabu sana kuwa mjamzito wa watoto sasa. Unaweza kuvumilia kuwaona wakimwita Sarah mama yao katika siku zijazo?”
"Hiyo ni kweli." Shani akaitikia kwa kichwa. “Hata kama Sara atawalea watoto vizuri, lakini utajisikiaje wewe kama mama yao kuwa mbali nao? Bwana Kimaro alikua akinyanyaswa alipokuwa mdogo pia. Bibi Kimaro ni mzee. Hataweza kushugulika na watoto."
Utulivu machoni mwa Lisa ukatanda taratibu. Asingeweza kamwe kuruhusu Sarah kuwa mama wa kambo wa watoto wake. Mwanamke mwovu kama Sarah angewanyanyasa.
Alikuwa amechoka sana kwa siku za karibuni, hivyo aliendelea kuepuka tatizo hilo. Shangazi Yasmine na Shani walikuwa wamempa ukumbusho wakati huo wa muhimu.
“Sawa, nitarudi.” Kujificha na kutokabiliana na tatizo isingemsaidia hata hivyo. Alishikilia maua yake na kurudi chumbani kwake.
Alipofika mlangoni mwa jengo lililokuwa na vyumba vyao, alimuona Alvin na Sarah wakitoka ndani. "Sarah, ngoja nikurudishe." Alvin ghafla akamshika mkono Sarah.
“Alvinic…” Sarah alipigwa na butwaa. Aliutoa mkono wake mara baada ya kumuona Lisa pembeni. Alisema kwa wasiwasi, "Bibi mdogo, usielewe vibaya."
Lisa alijisikia vibaya sana alipomuona Alvin akiushika mkono wa Sarah kwa macho yake. “Alvin, wewe—”
“Kwanini umekuja?” Alvin alimkatisha na kumpa jicho la kuudhi.
Kulikuwa na jua kali la kiangazi Nairobi siku hiyo, lakini Lisa alihisi ubaridi hewani ghafla.
Hata kama alikuwa amemkamata kwa bahati mbaya, sio tu kwamba hakujielezea, lakini pia hakuficha karaha aliyokuwa nayo baada tu kumuona Lisa akitokea. Angewezaje kufanya hivyo?
"Alvinic, usiwe hivyo," Sarah alisema kwa haraka, "Yeye ni mke wako, hata hivyo."
Alvin alishtuka. “Kama sikuamini kuwa umekufa hapo awali, asingekuwa mke wangu. Twende, Sarah. nitakurudisha.” Baada ya kuongea alimshika Sarah mkono na kuondoka zake.
Lisa alihisi kana kwamba damu mwilini mwake ilikuwa imepoa. Machozi yalimtoka huku akisema, “Alvin, unathubutu kuondoka? Ukiondoka, sitakusamehe tena.”
Alvin alitazama nyuma. Mwanamke nyuma yake alikuwa amevaa mavazi mapana ya ujauzito. Alikuwa na ujauzito wa miezi miwili, lakini umbo lake lilikuwa dhaifu kana kwamba upepo ungeweza kumpeperusha wakati wowote.
Wakati huo, moyo wake ulipiga kwa uchungu. Alitaka kurudi, lakini akakumbuka sauti kichwani mwake iliyosema, “Mtu unayempenda ni Sarah…Lisa si mwanamke unayempenda.”
“Sihitaji msamaha wako hata kidogo.” Alvin akaripuka kwa ukali. “Najisikia vibaya sana kukaa mahali pamoja na wewe.” Alimshika Sarah mkono na kuondoka bila kuangalia nyuma.
Hakuona uso wa Lisa ukibadilika na kuwa kama mfu kwa muda ule. Angewezaje kuwa hivyo… bila huruma? Yule Alvin aliyeapa kumpenda milele alikuwa wapi? Yule Alvin aliyesema hampendi Sarah alikuwa wapi? Ghafla, Lisa aliona tu mbele yake!
Shangazi Yasmine alimshikilia mara moja. Shani alimwita daktari wa familia kwa haraka.
Bibi Kimaro na Mzee Kimaro walisikia habari hiyo na mara moja wakakimbia. Waliposikia kuwa Alvin amemshika mkono Sarah na kuondoka naye, Bibi Kimaro alipandwa na hasira. “Huu ni ujinga. Mkewe ni mjamzito lakini bado anashikana na mwanamke mwingine kutoka nje. Mwambieni arudi mara moja."
“Tayari nimejaribu kupiga simu lakini Bwana Mkubwa hapokei simu zangu," Aunty Yasmine alisema bila msaada.
“Mjinga huyo! Nipe simu." Mzee Kimaro alichukua simu na kupiga namba ya Alvin.
"Ni nini, babu?"
“Alvin mkeo amezimia. Rudi hapa sasa hivi!” Mzee Kimaro alifoka, “Sijali kilichotokea kati yako na Sarah siku za nyuma, lakini wewe ni mwanamume uliyeoa sasa. Wewe ndiye uliyemuoa kwa hiari. Unapaswa kuchukua jukumu sasa kwa kuwa yeye ni mjamzito. Mwanaume anapaswa kuwajibika kwa matendo yake mwenyewe.”
Alvin alinyamaza upande wa pili wa simu. Alipotaka kuongea tu, sauti ya mwanamke aliyekuwa akipiga kelele kwa maumivu ilisikika.
“Babu, nina jambo la kufanya hapa. Siwezi kuzungumza nawe sasa hivi. Hata mimi si daktari. Unaweza kumpeleka kwa daktari ikiwa amezimia. Nitawalea watoto. Kuhusu Lisa, ninaweza tu kumtaliki na kumpa kiasi cha pesa.” Alvin alikata simu baada ya kumaliza kuongea.
Mzee Kimaro karibu ateme damu. Je, hayo ndiyo maneno ambayo mtu kama Alvin angesema? Kwanini alikuwa na mjukuu asiye na moyo na asiye na shukrani?
Aligeuka nyuma na kumuona Lisa ambaye alikuwa amezinduka. Hakuna aliyejua alipoamka. Alimtazama kwa macho yaliyojaa na tabasamu la huzuni.
"Babu, Alvin anataka kunitaliki na kunilipa pesa?" Lisa alikuwa na sura ya huzuni.
Mzee Kimaro alijikaza. Alikumbuka kuwa kila mara ilibidi aweke loud speaker kwa sababu alikuwa mzee na hasikii vizuri. Lisa alikuwa amesikia kila kitu.
Bibi Kimaro naye aliingiwa na hofu. Aliogopa kwamba Lisa atakuwa katika mshtuko. Zaidi ya hayo, alikuwa na mimba ya mapacha sasa. "Tulia. Maadamu mimi na babu yako tuko hapa, hatutamruhusu akutaliki. Kuhusu Sarah, hatutakubali Alvin kuwa naye pamoja.”
"Hukukubali Alvin kuwa pamoja nami hapo awali, lakini bado alinioa mwishowe, utawezaje kumzuia asimuoe Sarah?" Lisa alisema.
Sura ya: 294
Alvin alikuwa akitawala familia ya Kimaro. Ikiwa alitaka kufanya jambo lolote kwa njia yake, hakuhitaji hata kuwasikiliza wale wazee wawili.
Sura ya Bibi Kimaro ikabadilika. “Ni nini kinaendelea kati yenu nyie wawili? Tuligundua kuwa hamkuwa mkizungumza hapo awali. Lakini tulifikiri kwamba ni mambo ya kawaida ya wapenzi hivyo tukajua mtarekebisha tofauti zenu.”
Lisa alihisi baridi kali kwenye kifua chake. Yeye pia hakujua. Je, Alvin alikuwa amechoshwa na yeye kwa kutozungumza naye kwa muda, hivyo alitaka kurudiana na Sarah? Kwa kweli hakutarajia Alvin kuwa mkatili kiasi kile.
“Usijali. Tutakaa naye na kuongea naye. Unapaswa tu kuzingatia kuwatunza watoto kwa sasa." Huu ulikuwa wakati adimu wakati Mzee Kimaro alipokuwa akimfariji mtu kwa upole sana. Lisa alifumba macho na hakusema neno lolote.
Chumba kilipotulia tena, Aunty Yasmine alileta bakuli la mtori na kumsihi anywe. “Bibi mdogo, lazima uwe na chochote. Hata kama huna njaa, watoto walio tumboni mwako wanahitaji pia kula.”
“Shangazi Yasmine, siwezi kumuacha Sarah awe mama yao wa kambo. Ninahisi kukosa raha,” Lisa alinong’ona.
“Usilie Bibi Mdogo. Kusema kweli, nadhani Bwana Kimaro bado ana wewe moyoni mwake. Jioni hii tu kabla ya Sarah kuja, alikuwa akikutafuta kila mahali. Maneno yake yanatofautiana na hisia zake, lakini ninaona kwamba anataka kupatana na wewe. Si hivyo tu, amekuwa akirudi nyumbani kila siku sasa hivi. Jana usiku alikuwa hata akirandaranda kwenye mlango wako.” Aunty Yasmine alisema kwa kusitasita, “Au ni kwa sababu umempuuza kwa muda mrefu sana hivyo sasa anajaribu kukuchokoza?”
"Asingetumia njia hiyo ya kikatili kunichokoza, itakuwa moyo wake umebadilika sana." Lisa alitabasamu kwa uchungu na kutikisa kichwa. “Hapana, moyo wake haujawahi kubadilika. Amekuwa akimpenda Sara muda wote.”
“Sio hivyo. Bwana Kimaro anakupenda kweli." Shangazi Yasmine aliona ni vigumu kueleza kwa maneno. "Kwanini ghafla akawa hivi? Ni ajabu sana.”
Lisa alipigwa na butwaa kwa muda. “Anti Yasmine, una uhakika kwamba Alvin alikuwa akinitafuta kabla Sarah hajafika?”
"Hakika. Alisema hata wewe ndiye uliyependekeza kuwa Dokta Nyasia aje kwa Kimaro kwa ajili ya matibabu yake, lakini ukatoweka muda ulipofika. Alikuwa anakulaumu kwa kutokuwa naye.”
Lisa alishangaa. Hakika, ilionekana kwamba Alvin alikuwa amegeuka kuwa mnyonge ghafla. Alikumbuka kwamba baada ya Sarah kukutana na Jennifer mara ya mwisho, Jennifer alifariki muda mfupi baadaye. Je, inawezekana kwamba Sarah alikuwa amemchanganya Alvin na kitu cha ajabu? Lisa aliingiwa na wasiwasi mkubwa kuhusu hilo.
Alilala kitandani akiutafuta usingizi usiku mzima, lakini hakuweza kulala hata kidogo. Siku iliyofuata, mwili wake haukujisikia vizurii. Aliamka na kuuliza kwenye chumba alichokuwa analala Alvin. Alipogundua kuwa hakuwa amerudi kwa usiku mzima, moyo wake ulipata simanzi sana.
Alikuwa ameondoka na Sarah jana yake. Je, walitumia usiku pamoja? Je! kuna kitu kilitokea? Kichefuchefu kilimjia.
Alijitupa kwenye kochi kwa uchovu wa mwili na akili.
"Bibi mdogo, nikupe maji?" Shangazi Yasmine alimpigapiga mgongoni, akiwa na wasiwasi mwingi.
“Niko sawa. Tayarisha gari. Naenda kumtafuta kwenye kampuni yake,” Lisa alisema kwa unyonge.
Shangazi Yasmine alikuwa na wasiwasi. “Lakini uko katika hali hii…”
“Nataka kurekebisha mambo fulani,” Lisa alisema kwa msisitizo.
"Basi, tayarisha gari," Shani alisema, "Hatuwezi kuruhusu Bwana Kimaro aendelee kuwa hivi."
Aunty Yasmine akahema kwa nguvu. Alienda kuandaa gari la kumpeleka Lisa KIM International.
Lisa alipofika, mhudumu wa mapokezi alimtambua mara moja. Alama ya huruma iliangaza machoni pake. "Bibi mdogo, Bosi... Hayuko huru kwa sasa.”
Lisa alimtazama mhudumu yule machoni na kumuona ana wasiwasi mwingi. Alisema kwa kusisitiza, "Bado nitaapanda hata kama ana shughuli nyingi." Alielekea moja kwa moja juu.
Alipousukuma mlango wa ofisi kufunguka, sauti ya Alvin ya kukasirika ilisikika kutoka ndani. "Ni nani aliyekuruhusu kuingia bila kubisha hodi"
Kabla hajamaliza sentensi yake, alisimama ghafla alipomuona Lisa.
Lisa aliona kilichokuwa kikiendelea ofisini. Sarah alikuwa amekaa kwenye mapaja ya Alvin. Tukio lile lilikuwa la kuchukiza sana hata akatamani kujirusha kutoka juu ya ghorofa ile hadi chini.
“Bibi mdogo…” Sarah alisimama mbali na mapaja ya Alvin kwa hamaki. "Samahani…"
“Acha kujifanya Sarah. Huoni hata aibu kujirahisisha kwa mwanaume aliyeoa?” Lisa hakuweza kuvumilia tena. Alikimbia na kuinua mkono wake na kumpiga Sarah kofi la usoni. Hata hivyo, Alvin alishika kifundo cha mkono wake kabla hajarudisha kofi jingine.
Alvin akamtazama kwa ukali. “Lisa, unafikiri wewe ni nani? Unathubutu vipi kumpiga Sarah? Potelea mbali.” Kisha akautupa mkono wake kwa nguvu. Kama Shani asingemshikilia Lisa, angeanguka chini moja kwa moja.
“Bwana Kimaro, huwezi kufanya hivi. Bibi Mdogo ni mjamzito,” Shani alimkumbusha.
"Kama unalijua hilo kwanini umemruhusu kutoka nyumbani wakati nilikuambia umchunge?" Alvin alisema kwa hasira.
Lisa alionyesha tabasamu la huzuni. “Unafikiri angeweza kunizuia? Nitakubali vi[i mume wangu afuatane na mwanamke mwingine na kumkumbatia? Ningewezaje kulala ikiwa hukurudi nyumbani na bila shaka ulilala naye pia?"
Alvin aligeuza macho yake na hakumjibu. Hata hivyo, kukaa kimya kulimaanisha kwamba alikuwa akikubali kimyakimya. Wakati huo, Lisa aligubikwa na kukata tamaa na huzuni. Uso wake ulikuwa mweupe kama karatasi.
Alvin akakaa kimya. Kwa sababu fulani, alihisi maumivu moyoni mwake.
Wakati huo, Sarah alisema ghafla, “Samahani, Lisa. Jana nilikuwa sijisikii vizuri…”
“Kwahiyo ukaamua kuondoka na mume wangu na kwenda kulala naye kwa vile tu ulikuwa haujisikii vizuri? Ha, Sarah Langa Njau, bila shaka huna haya. Unaweza kuacha kujifanya kuwa huna hatia?”
Lisa alishindwa kuvumilia kusikiliza neno lingine. Alishusha pumzi ndefu huku akihofia kwamba angeweza kushindwa kujizuia. “Unaweza kuniruhusu niongee na mume wangu faraghani? Ikiwa una ujasiri wa kutosha kubaki hapa, basi ninaweza tu kuwaita waandishi wa habari. Tunaweza kufanya mazungumzo pamoja.”
Hasira ilitanda machoni mwa Alvin. “Hili ni suala langu binafsi. Watamfikiriaje Sarah ukiwaita waandishi hapa?”
Lisa alicheka kwa kejeli. Wasiwasi wake pekee ulikuwa sura ya Sarah. Vipi kuhusu yeye? Ina maana yeye alikuwa mtu wa kumfanyia tu dharau jinsi anavyopenda?
"Kwanini unacheka?" Alvin alihisi kukosa raha na kukerwa na tabasamu lake.
“Alvinic, acha kurumbana naye. Ninapaswa kuondoka.” Sarah akachukua mkoba wake pembeni yake kisha akasema, "Mtandao umeendelea siku hizi. Waandishi wa habari wakijua kuhusu hili, bila shaka watu watakukosoa kwa maneno makali.”
“Sarah…” Alvin aliyumba kidogo. Kama ilivyotazamiwa, ni Sarah aliyekuwa akimjali sana. "Nitamwambia dereva akurudishe."
“Sawa, nitakusubiri.” Baada ya kusema hivyo kwa upendo, Sarah aligeuka na kumtupia jicho Lisa huku mgongo wake ukiwa umemtazama Alvin. Aliondoka kwa fujo.
Lisa alikunja ngumi. Aliogopa kwamba asingeweza kujizuia na kumnyonga Sara hadi kufa.
"Lisa, ikiwa utathubutu kumuumiza Sarah, sitakuacha kamwe." Alvin alipomwona na kumuonya huku akikunja uso.
Lisa akayasogeza macho yake pembeni na kumtazama mwanamume huyo mwenye sura nzuri na ya kupendeza lakini asiye na moyo. Ni wazi bado alikuwa mwanaume aliyempenda, lakini macho yake hayakuwa ya kawaida kiasi kwamba yalimfanya aogope. Alikuwa tayari kuamini kwamba Alvin alikuwa amebadilishwa moyo na Sarah na kuwa mkatili.
"Alvin, mbona umebadilika ghafla?" Alitazama moja kwa moja machoni mwa mwanaume huyo. Macho yake yalikuwa mekundu na yamevimba. “Ulisema wazi kwamba una mimi tu moyoni mwako hivi sasa na hujawahi kufikiria kurudiana na Sarah. Ulikuwa ukinidanganya muda wote?”
Alvin alishikwa na butwaa. Alionekana kusahau kila kitu. Ni lini alimtakia maneno hayo?....ITAENDELEA....
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
