AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP...........................0628924768
SEHEMU YA................................291-292
Sura ya: 291
Sarah alishika glasi yake kwa nguvu. Kisha ghafla aliinamisha kichwa chake na kukohoa.
"Uko salama? Koo lako bado halijatulia?" Rodney aliuliza mara moja kwa wasiwasi.
Lisa akasema, “Kidonda chako bado hakijapona? Ni bora kupumzika nyumbani ikiwa hujisikii vizuri.”
"Lisa, umesema vya kutosha?" Rodney hakuweza kumvumilia tena. Alionya, "Unapaswa kuelewa hili vizuri. Sarah alinyongwa na Alvin kwa sababu alikuwa anatibu ugonjwa wake. Kama mke wake, sio tu kwamba huna shukrani, lakini hata unakosa huruma.”
Lisa alihisi uchungu na kupiga kelele. "Bwana Shangwe, unawezaje kusema hivyo? Siku ile si wewe uliyeniambia kwamba Alvin na Sarah bado wana hisia kwa kila mmoja na kuniambia niachane nao. Katika hali hiyo, nimshukuru kwa lipi wakati aliumia akiwa anamtibu mpenzi wake?”
Lisa aliposema hivyo hofu ilitanda machoni mwa Rodney. Kwa jinsi alivyokuwa akimtizama ni kana kwamba alitaka kumla akiwa hai.
Sura za Sam na Alvin zilibadilika kwa kusikia maneno hayo, hasa hasa Alvin. Kifua chake kilikuwa kikitokota kwa hasira. "Rodney, ulimtafuta lini na kumwambia maneno hayo?"
"Rodney, haukupaswa kufanya hivyo." Sarah alipumua kwa wasiwasi. “Nilishawahi kukuambia, mimi na Alvinic tayari tumesonga mbele.”
“Sawa, yote ni makosa yangu.” Rodney akapiga teke kiti kusafisha njia Alisimama na kuelekea uani.
“Naenda kuzungumza naye.” Sarah alimfuata kwa haraka.
Uso wa Alvin ulijawa na mfadhaiko. Alijuta kumleta Lisa. “Jamani mbona hukuniambia kuwa Rodney kakuambia maneno hayo? Kama ningelijua hilo, ningekusaidia kumpa somo kali.”
“Lisa. Rodney huwa ni mropokaji tu. Usiweke maneno yake moyoni.” Sam alisema kisha akabadilisha mada. "Unaonaje tukienda kucheza pool?"
Lisa aliitikia kwa kichwa. “Sawa.”
Alitembea kuelekea kwenye pool table akiwa na Sam. Alvin alisema kwa wasiwasi, “Una mimba. Haifai kwako kucheza pool. Kwanini nisicheze huku wewe unatazama pembeni?”
Lisa alikunja uso, na Sam akasema kwa haraka, "Alvin, jaribu kuzuia hisia zako mbaya. Hata hatuchezi soka. Ulimwita Lisa ili tu aketi hapo na kufanya drama na Sarah?”
“Drama?” Lisa nusura aanguke kicheko. “Sawa, nitakuwa makini. Unaweza kukaa pembeni, usitusumbue.” Sauti ya Lisa ilikuwa shwari.
Alvin alichanganyikiwa kupita kiasi. Mtazamo wake kwake ulikuwa mbaya zaidi kuliko mtazamo wake kwa Sam.
“Mpenzi wangu, unataka kula nini? nitakuagizia.”
“Chochote.”
Baada ya Alvin kuondoka hatimaye, Sam alimwangalia Lisa na kusema kwa upole, “Pole, lazima ulikuwa na wakati mgumu siku za karibuni, sivyo?”
Machozi yalimtoka Lisa na nusura kulia, lakini, aliyazuia na hakuonyesha hisia zake. “Hunilaumu mimi? Nilidhani ungekuwa upande wa Sarah pia.”
“Sina ukaribu kiasi hicho na Sarah. Wewe ndiye unatoka jiji mmoja na mimi, hata hivyo, "Sam alisema kwa furaha, "Watazamaji ndiyo wanaaona mchezo vizuri. Niliona sasa hivi kwamba Sarah si mtu wa kawaida hivyo.”
Lisa alimtazama kwa mshangao.
“Rodney anampenda Sarah kupita kiasi. Imekuwa hivi kila wakati. Machoni mwake, Sarah ni binti wa kifalme mzuri huku Chester akimchukulia kama dada. Kuhusu Alvin, moyo wake umebeba hatia kwa Sarah, lakini nina hakika kwamba hampendi Sarah kivile,” Sam alisema kwa umakini.
“Haijalishi.” Lisa alitabasamu kwa unyonge. “Ataamua mwenyewe.”
Sam alikunja uso. “Wewe…”
“Nimechoka. Nataka tu kujipenda mimi na watoto wangu zaidi,” Lisa alijibu. Chembe ya wasiwasi iliangaza machoni pa Sam.
"Mpenzi wangu, kula matunda." Alvin alimpelekea sinia la matunda.
Mlango wa chumba cha faragha ulifunguliwa tena. Chester aliingia huku mkono wake ukiwa umemzunguka mwanamke mmoja mwenye umbo refu. Mwanamke huyo alikuwa na nywele nyeusi ndefu na zilizotambaa kuanzia kichwani na kuangukia mabegani mwake. Alikuwa amevaa shati la maua na mikono ya mikunjo, lililomechishwa na sketi fupi ya denim nyeupe.
Hata hivyo, Lisa alipoutazama vizuri uso wa mwanamke huyo, alikosa la kusema. F*ck! Ilikuwa siku mbaya kama nini! Mwanamke huyo alikuwa Cindy Tambwe, mwanamuziki maarufu, ambaye alikuwa hajakutana naye kwa muda mrefu.
Tangu alipojitenga na familia ya Jones, Lisa hakukutana na Cindy kwa muda mrefu, lakini mara nyingi aliona habari za burudani zinazohusiana naye kwenye mitandano. Ilionekana kana kwamba Cindy alikuwa anakuwa maarufu zaidi. Lakini, Lisa hakuwa na uhusiano na Cindy, kwa hivyo hakumjali. Jambo la kushangaza ni kwamba Cindy sasa alikuwa akishirikiana na Chester. Lisa alikumbuka Pamela alishawahi kumdokeza kwamba Cindy alipata bwana tajiri jijini Nairobi, akili yake sasa ikafunguka baada ya kumwona akiwa na Chester.
Hivi Alvin na marafiki zake walikuwa na matatizo gani? Chester hakutaka mwanamke mzuri kama Charity bali alimchagua Cindy ambaye alikuwa na sura ya kuchongesha.
Kumbukumbu ya Alvin sasa haikuwa nzuri, hivyo hakumkumbuka Cindy, lakini, Sam alimtambua mara moja.
“Lisa, nilisikia kilichotokea kwenye uso wako, hatujaonana kwa muda mrefu. Nimekukumbuka sana." Macho ya Cindy yalimtoka alipomuona Lisa. Alikwenda kwa Lisa kwa furaha.
"Samahani, lakini sijisikii kuwa karibu na wewe." Lisa aliinua mkono kuashiria asisogee karibu.
Chester alikunja uso na kumuuliza Cindy, “Nyie mnajuana?”
“Hatufahamiani tu. Lisa na mimi tulisoma shule moja ya msingi na sekondari. Uhusiano wetu ulikuwa mzuri wakati wote, lakini aliwasiliana nami mara chache baada ya kuja Nairobi.” Cindy akatabasamu vibaya.
Chester aliinua macho yake. Uso wake ulionekana wenye mawazo ghafla. Alikumbuka kuwa Lisa alikuja tu Nairobi baada ya Joel kumrudisha. Baada ya kumsikiliza Cindy, inawezekana Lisa alikatisha mawasiliano na Cindy baada ya kupata mafanikio?
Lisa hakujali Chester alifikiria nini juu yake na alisema moja kwa moja, “Hujui kwanini niliacha kuwasiliana nawe?”
“Hiyo ni sawa." Sauti ya Sam ilisikika. “Nakukumbuka huko Dar es Salaam, mara nyingi alijichanganya na kundi la wanawake wa kawaida kama Janet Kileo. Ndio, hata tuliwahi kuwakuta wakiwafanyia fujo Lisa na Pamela kwenye mgahawa. Alvin, unakumbuka?"
Alvin akauchuna tu. Angewezaje kusema kwa sauti kwamba alikuwa amesahau mambo mengi? Lakini, kulingana na kile Sam alichosema, alikumbuka mwanamke huyo hakika hakuwa mzuri.
"Chester, kwanini una’date na mwanamke kama huyu?" Alvin alikunja uso. Hakuficha chukizo machoni pake.
Uso wa Cindy ulipauka kidogo, na macho yake yakaangaza machozi kutokana na aibu. "Bwana Harrison, nilikuwa mwimbaji mdogo wakati huo. Janet na wengine walikuwa wakijaribu kuniunga mkono. Lisa, najua unanidharau, lakini mimi sina nguvu kama wewe. Lazima nijitegemee mara nyingi na kuwa mwangalifu sana. Nitaharibikiwa nikimkosa mtu kama Chester.” Alimshika mkono Chester huku akitetemeka. "Chester, unapaswa kujua kuhusu maisha yangu ya zamani."
"Wacha yaliyopita yawe ya zamani." Chester aliinua tabasamu la kustaajabisha huku akipigapiga nyuma ya mkono wake. "Nenda ukaketi."
“Chester, huyu ndiye mpenzi wako mpya? Yeye ni mrembo sana.” Wakati huo, Sarah na Rodney walirudi.
Sarah alimsogelea Cindy huku akitabasamu na kumshika mkono. "Inapendeza usiku wa leo kwani nimepata kampani ya wanawake wenzangu pia. Hey, kwa nini unalia?"
“Hakuna kitu…” Cindy aliinamisha kichwa chake na kufuta machozi yake kwa haraka.
Sura ya: 292
Sarah mara moja akahisi damu yake ikiendana na Cindy. Alijihisi faraja kuwa naye utadhani alikuwa rafiki yake wa siku nyingi. "Twende tukaimbe nyimbo kadhaa."
Lisa aliwatazama wale wanawake wawili bila la kusema. Walionekana kuendana kabisa kitabia. Walikuwa ni pea iliyotengenezwa mbinguni. Laiti angejua, bora asingeenda.
Muda si muda, muziki ulianza kuchezwa katika chumba cha faragha. Lisa aliutambua wimbo huo mara moja. Ulikuwa wa Bruno Mars' 'Count On Me'.
“Oh-oh
Ukijikuta umekwama katikati ya bahari
nitasafiri duniani kukutafuta
Ukijikuta umepotea gizani na huoni
nitakuwa nuru ya kukuongoza…”
Pamela Lisa na Cindy mara nyingi waliimba wimbo huo pamoja hapo awali kwa hivyo ulimgusa sana Lisa.
Wakati huo, Cindy alichukua kipaza sauti na kusema, “Lisa, nyanyuka tuimbe pamoja. Tuliwahi kuimba wimbo huu zamani tulipokuwa marafiki. Najua nilifanya makosa kadhaa hapo awali na sijui niseme nini zaidi ya samahani. Lakini nimeu’miss urafiki wetu. Isingekuwa kwa kunitia moyo, nisingefika hapa nilipo katika tasnia ya burudani. Nimekukumbuka sana. Ni kweli..”
Aliposema maneno matatu ya mwisho, alisisitiza kidogo. Lisa alikuwa ameduwaa kwa muda, lakini haraka akaona ni jambo la kuchekesha.
Cindy hakuwa hata na aibu? Alikuwa amefanya mambo mengi sana ambayo yalimzidishia uchungu kwenye jeraha lake wakati huo.
“Cindy, unataka kuigiza, lakini sina hamu na drama zako,” Lisa alimdhihaki.
Chester akaweka glasi yake chini. Kidokezo cha chuki kiliangaza machoni pake. Rodney hakuweza kumvumilia tena na akasema, “Lisa, Cindy anakuomba msamaha kwa dhati. Kwanini unakuwa hivi? Unadhani wewe ni mzuri sana kwa sababu tu wewe ni mke wa Alvin?”
Sarah akasema. “Kwa kweli, ninaelewa hisia za kutoelewana na rafiki yako. Lakini baada ya kuwa na urafiki mzuri wa miaka mingi, ni vyema kusahau maudhi machache aliyokufanyia na kurejesha furaha yenu ya zamani. Ninauonea wivu sana urafiki ambao ulianzisha wakati wa shule ya msingi hadi sekondari. Msiruhusu urafiki huo upotee kwa sababu ya changamoto chache tu za maisha.”
Lisa alikosa la kusema. Maneno ya Sarah yalikuwa na maana nzito ndani yake. wengine wasingeelewa kwa urahisi alichokuwa akimaanisha. Alimaanisha kuwa urafiki wake na Alvin ambao ulianza miaka ishirini huko nyuma na baadaye kuzaa mapenzi kati yao haukutakiwa uachwe upotee hivihivi kwa sababu ya changamoto ya Lisa.
Kila mmoja wa watu waliokuwepo hapo alikuwa akimtazama Lisa kwa sura ya kuchukiza kana kwamba ni mtu mwenye fikra finyu na mbaya.
Baada ya muda mfupi, Lisa alicheka. “Hii ni mara yangu ya kwanza kujua kuwa mtu aliyetendewa ubaya ataonekana na makosa kwa kutosamehe wengine hata kama walimuumiza vibaya hapo awali. Cindy sasa ananiomba msamaha wa kinafiki kwa sababu anajua nipo juu zaidi yake. Nilipokuwa naporomoka miezi kadhaa nyuma alimuunga mkono Lina kuninyanyasa kwa kila nafasi waliyoyapata. Msamaha wake utakuwa na maana gani kwangu?" Lisa akaweka chini fimbo ya kuchezea pool. “Sichezi tena. Naona sistahili kuendelea kuwepo hapa nisije nikaharibu hisia za watu wengine.” Aligeuka na kuondoka baada ya kusema hayo.
Alvin akamshika mkono kwa haraka. “Lisa…”
“Alvin, mwache aondoke. Tumeshoshwa kabisana mke wako. Amekuwa msumbufu sana tangu alipotokea. Kila mtu alikuwa ametulia hapa kabla hajaja.” Rodney alisema kwa sauti ya ukali.
Lisa alitazama nyuma na kumpiga jicho la chuki. "Kusema kweli, kukaa na watu wasio na akili kama nyinyi pia inanichosha sana.”
Wakati huo, uso wa Chester ulibadilika pia. Alisema kwa ukali kuliko alivyowahi hapo kabla, “Alvin, mwondoe na usije naye tena siku nyingine.”
“Vizuri tu. Sina mpango wa kujiunga na nyie tena pia.” Lisa alitupa mkono wa Alvin na kuondoka. Alvin aliwatazama Chester na Rodney kwa hasira kabla ya kumfuata.
Baada ya wawili hao kuondoka, Cindy alionekana kuwa na sura ya wasiwasi na majuto. "Ni kosa langu. Kama nisingemwomba Lisa msamaha, hili lisingetokea.”
“Sio kosa lako. Lisa ndiye mwenye kiburi na jeuri.” Rodney alisema.
“Clank!” Sam ghafla akatupa imbo ya pool table kwenye meza. “Nyie endeleeni kufurahi, mimi naondoka.”
“Unaondoka kwanini?” Rodney aliuliza kwa mshangao, "si tumekuja hapa kukukaribisha wewe usiku wa leo?"
"Hakuna maana." Sam aliweka mikono mfukoni na kuuendea mlango. Aligeuka nyuma ghafla na kumtazama Cindy. “Alichosema Lisa kilikuwa sahihi. Hii ni mara yangu ya kwanza kuona kwamba msamaha wa kinafiki unaweza kufanywa kwa njia hii. Rodney na Chester hawakuwa Dar es Salaam wakati huo. Hawaelewi tabia yako hata kidogo. Ingekuwa mimi, nisingekusamehe kwa mambo uliyofanya pia. Chester, umefanya uamuzi mbaya wakati huu.” Aliondoka mara baada ya kuongea.
Chester aliachwa akiwa kama haelewi kinachoendelea. Cindy naye alianza kuhisi msisimko wa aibu.
Baada ya kutoka nje ya jumba hilo, Lisa alishusha pumzi ndefu. Kama ilivyotarajiwa, kila alipokuwa akikabiliana na marafiki wa Alvin, aliishia kugombana nao tu.
Lisa aligusa tumbo lake na kusema. “Samahani watoto wangu. Niliahidi sitakasirika lakini sikuweza kujizuia tena.”
"Lisa, nitakurudisha nyumbani." Alvin alimshika mkono. "Nitamwambia dereva aendeshe gari." Lisa alikaa kimya.
Akiwa njiani kurudi nyumbani, hakuzungumza neno lolote pia.
Alvin aliusoma uso wake kwa wiziwizi. Macho yake yalionekana kuchoka. "Samahani. Sikutakiwa kukupeleka huko leo. Alichosema Rodney kilikuwa kibaya mno.”
“Uko sahihi. Sitaki tena unipeleke kwa marafiki zako wakati mwingine,” Lisa alijibu kwa utulivu.
Kwa kweli, bado alihisi kukata tamaa moyoni mwake. Kila alipokuwa akikabiliana na kundi la marafiki wa Alvin, kila mara alijihisi kuwa anapambana nao peke yake. Alvin hakuwahi hata siku moja kuchukua upande wake kwa msimamo thabiti. Hakuweza hata kukumbuka ni mara ngapi hali kama hiyo ilikuwa imetokea.
Gari iliposimama, Lisa alishuka kwenye gari mara moja, kimyakimya.
“Mpenzi wangu, babe…”Alvin alimwita kwa nyuma, lakini Lisa hakutazama nyuma. Hatua kwa hatua, Alvin alianza kuwa na hasira pia. “Unataka nini? Utanionyesha tabia hii hadi lini?”
Lisa alisimama na kugeuza kichwa chake. "Labda nitaacha utakapoacha kujumuika na Rodney na wengine."
Alvin akachoka ghafla. Ingawa hakufurahishwa na Rodney na Chester, alikuwa amewajua kwa miaka 20. Walikuwa wameongozana naye kwa njia panda na nyembamba. Haikuwa kutia chumvi kusema kwamba walikuwa ni ndugu walioapishwa.
"Nilijua hautakuwa tayari." Lisa alitoa tabasamu la kujidharau kisha akageuka nyuma kuondoka.
Kwa kusema ukweli, alielewa kuwa ndege wafananao huruka pamoja. Rodney na Chester walikuwa wamekwisha kabisa kwa wale wanawake wawili hata waliwachukulia kama mabinti wa kifalme. Mapema au baadaye, Alvin angekuwa hivyo pia. Hakutaka kuwa kama Sarah na Cindy.
Kuanzia siku hiyo, Lisa hakumtafuta tena Alvin. Si hivyo tu, Makazi ya familia ya Kimaro yalichukua eneo kubwa sana hivi kwamba wangeweza kukaa hata wiki bila kuonana. Alvin alikuwa na hasira nyingi sana ndani yake, lakini hakuwa na pa kuzitolea.
Ilikuwa siku ya jumapili. Sarah alifika nyumbani kwa Mzee Kimaro kama kawaida kwa matibabu ya Alvin. Alipoingia ndani alimsikia Alvin akishindwa kujizuia. "Lisa yuko wapi? Yeye ndiye alitaka nipatiwe matibabu kyangu hapa nyumbani. Dr Nyasia anakuja lakini bado sioni hata kivuli chake.”
"Bibi Mdogo anatembea mara nyingi na Bibi Kimaro," Shangazi Yasmine alisema kwa uso wa uchungu, "Alisema yeye si daktari na hatakuwa na msaada mkubwa, kwa hivyo hataki kuwasumbua ninyi wawili."
Kichwa cha Alvin kilikuwa katika maumivu ya hasira. Maneno ya aina gani hayo? Yeye ndiye aliyekuwa akimhofia kuwa na uhusiano wa kimapenzi kana kwamba anajihadhari na mwizi, lakini ghafla akaacha kabisa kumfuatilia. Alimaanisha nini?
Sarah aliumia ndani kwa ndani kisiri. Hakutarajia hisia za Alvin kwa Lisa zingekuwa za ndani sana. Ilikuwa ni muda mrefu sana tangu arudi lakini bado uhusiano wake na Alvin haukua karibu zaidi, badala yake ulikua ukizidi kuwa wa mbali zaidi. Hiyo ina maana, asingekutana naye tena baada ya ugonjwa wake kupona kabisa? Ilionekana kana kwamba angelazimika kutumia nafasi ya ugonjwa wake kuendelea kumsogeza karibu.
"Alvinic." Sarah alitembea na kuuliza kwa wasiwasi, "Lisa bado ana hasira kuhusu kile kilichotokea mara ya mwisho?"
Alvin alikosa jibu. Hakuweza kuelewa Lisa alichokuwa anawaza hata kidogo. Wakati fulani, alishuku kwamba alikuwa na unyogovu kabla ya kuzaa, lakini kulingana na Shani, aliishi vizuri na washiriki wengine wa familia ya Kimaro. Ilikuwa tu wakati alipokuwa akikabiliana naye. Lisa alianza lini hata kukataa kuzungumza naye?.....ITAENDELEA......
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
