JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP..........................0628924768
SEHEMU YA................................279-280

Sura ya: 279

Lisa alimtazama Jack kwa hisia tofauti. Ilikuwa ni muda tangu alipokuwa na fikra tofauti kuhusu yeye. Jack alimkazia macho huku akionyesha safu ya meno meupe.
Baada ya kuona vitendo vyao vya kuteteana, uso wa Alvin ukaingia simanzi.
Sarah kisha akasema kwa upole, “Matibabu yako yamekamilika kwa leo, Alvinic. Unaweza kumpeleka mkeo nyumbani kwanza.”
“Sawa.” Alvin akaitikia kwa kichwa. Ilimtia wasiwasi kuwaona Lisa na Jack wakirudi pamoja. Kwa upande wa Sara, alikuwa na hakika kwamba alikuwa na uwezo wa kuendesha gari peke yake kwenda nyumbani.
Lisa alipofika mlangoni aligeuka nyuma na kumtazama Sarah. “Dokta Nyasia, natumai unaweza kumfuata Alvin nyumbani ikiwa unataka kuendelea kumtibu. Samahani kwa kuwa na wivu, kwani wewe ni mrembo na pia ni ex wa Alvin huku mimi ni mjamzito tu. Kwa kuzingatia kuwa wewe ni mwanamke pia, nina uhakika unaelewa hisia zangu.”
“Naelewa." Sarah akaitikia kwa tabasamu hafifu.
Sarah alipogundua kuwa Alvin ameondoka bila kuangalia nyuma, uso wake mzuri ulibadilika ghafla. Kweli Alvin alimuacha peke yake pale? Ingekuwa zamani, asingefanya hivyo kabisa. Kwa mwonekano wa mambo, alionekana kujali umuhimu wa mwanamke huyo mbaya usoni mwake. Ilibidi alishughulikie suala hilo kwa mbinu nyingine.
Jack alitoka nje ya hoteli na alikuwa karibu kuondoka. Ghafla, Lisa akamwita, “Asante kwa leo Jack. Nitakununulia chakula cha jioni kukushukuru.” Ilikuwa ni muda mrefu tangu atoke nje. Harufu ya nyama choma kando yake ikaingia puani na kumfanya atamani kula nyama choma ghafla.
"Wewe ni mjamzito na unataka kula nyama choma?" Alvin alikunja uso kwa nguvu sana mpaka uso wake mzuri ukawa unachukiaza. “Twende nyumbani.”
“Najua hutakubali ndiyo maana sikuomba hata ruhusa yako. Ikiwa unataka kwenda nyumbani, unaweza kutangulia peke yako." Lisa alimpa Jack ishara kwa macho. Baada ya hapo, wote wawili walitembea hadi upande mwingine. Kulikuwa na baa ya kawaida pale na ilikuwa imechangamka sana.
Alipomwona Alvin aliyechanganyikiwa nyuma yake, Jack ghafla aliinua uso wake kwa majivuno. ‘Afadhali! Ingawa sina uwezo wa kutosha kushindana nawe kazini, angalau naweza kukutesa kidogo kupitia mke wako' Jack alijiwazia.
Alvin alipandwa na hasira. “Lisa, nisingekuwa na shida na wewe kula nyama za mitaani kabla ya kuwa mimba. Lakini kwa kuwa sasa una mimba, huwezi kuwahatarisha watoto wetu!”
“Haya, kaka, umekosea kusema hivyo. Nani amesema wajawazito hawawezi kula nyama choma? Ni sawa ilimradi atumie kidogo,” Jack alicheka na kusema huku akikonyeza macho.
Lisa alikubali kabisa kwa kichwa. Ikiwa asingekuwa na mimba wakati huo, alitamani hata kupata chupa chache za divai. “Nimekuwa nikila chakula cha wapishi wa Kimaro kila siku. Hakina ladha. Wewe mwenyewe hukujali hata kunitoa nje, lakini unathubutu vipi kunizuia sasa? sijali. Lazima nipate nyama choma leo." Harufu ya nyama ilimfanya Lisa adondoshe udenda.
"Kaka, unaweza kutangulia nyumbani ikiwa hutaki kula." Jack alimfuata Lisa huku akitabasamu.
Alvin alihisi hamu kubwa ya kumkanyaga Jack usoni. Hatimaye, alivuta uso mrefu na kuwafuata. Baada ya kupata viti vyao kwenye klabu ile ya usiku, kelele za jirani na mazingira mabaya yalimfanya Alvin kukunja uso.
Kila mtu aligiza nyama choma za kutosha, isipokuwa Alvin.
Alvin alishindwa cha kusema. Kwa fikra zake aliona hata bia tu zinazouzwa hapo hazina kiwango cha yeye kutumia, sembuse chakula? Thubutu! Mara ya mwisho alilazimishwa na Lisa kula nyama za kuku huko Coco Beach katika mazingira kama hayo, na alisumbuliwa na kinyaa cha mdomoni kwa wiki nzima.
Hata hivyo, hakuweza kuruhusu watoto wake wateseke. Aliinuka na kuelekea kwenye jiko la nyama choma. "Bwana, umeosha vyombo vyako?"
“Mke wangu ameosha vyombo hivi mara kadhaa. Vipo safi bosi wangu,” mchoma nyama alijibu huku akitabasamu.
Alvin hakuamini hata kidogo. "Hiyo haiwezekani. Nilisikia kwenye mitandao kuwa huwa mnafutafuta sahani zenu, na hata nyama wakati mwingine mnachoma zilizoharibika."
Mchoma nyama alikosa la kusema. “Bosi, kama unaona nyama zetu hazifai, kanunue sehemu nyingine.”

'Sawa, mimi binafsi nitaosha vyombo ambavyo mke wangu atatumia." Alvin alichukua sahani kadhaa na kuelekea bombani.Mchoma nyama alishindwa hata kusema, kwa miaka kumi ya uzoefu wake wa kuchoma nyama kwenye baa hiyo, hakuwahi kuona mtu wa dizaini kama hiyo.
Lisa alitingisha mdomo bila kusema, kisha akagusa tumbo lake, "Watoto wangu wana bahati iliyoje."
Jack alicheka. "Jack unachekea nini? Funga domo lako!" Alvin alionya kwa mshtuko.
"Nimekosea? Bdo unaendelea kunishangaza sana broo. Kwanza, badala ya kutibiwa hospitalini, unatibiwa kwenye chumba cha hoteli na ex wako. Haha, sijawahi kusikia kuhusu mtaalamu yeyote anayetibu hivi. Jiangalie, broo,” Jack alijibu bila kujali.
“Kwanini unaendelea kukazia fikira jambo hili? Kila mwanasaikolojia ana njia yake mwenyewe ya kuwatibu wagonjwa.” Sura ya papara ilivuka uso wa Alvin,
"Sawa, unaweza kuwa huna nia mbaya, lakini una uhakika gani kwamba Sarah hana hisia na wewe?" Jack alishtuka, “Kama haya yangetokea nyuma, nisingepata tabu kukukumbusha, hakika mimi ni mhuni, mimi pia si mtu mzuri. Lakini kama ningekuwa kwenye viatu vyako na mke wangu ni mjamzito, bila shaka ningejiweka mbali na wanawake wengine, sembuse ex wangu. Sababu inayonifanya niseme hivyo ni kwamba sitaki kuona wapwa zangu wakikua katika familia isiyokamilika. Ninaweza kuelewa aina hii ya maumivu, sawa?"
Sura ya Alvin ikabadilika, Lisa alimtazama Jack kwa kumshangaa, alikiri kuwa alikuwa na kinyongo dhidi yake, lakini kilitoweka wakati huo,
Jack na Alvin waliendelea kubishana wao kwa wao kwa muda mrefu. Baada ya kuona tukio hilo, tabasamu mwanana lilienea usoni mwa Lisa,
“Unatabasamu nini?” Jack aliuliza.
“Ni nadra sana kuwaona nyinyi wawili mkiongea kama hivi” Lisa akasema kwa ghafula, “Kwa kweli, nyinyi watu mnaweza kukubaliana, kusaidiana, na kusikilizana.”
Jack alisema, “Ni nani anaweza kuelewana na kichaa huyu?"
Alvin pia alisema, "Siwezi kuvumilia hata kusikia sauti yake."
Lisa alikosa la kusema. Baada ya yote walikuwa ni ndugu. Baada ya kumaliza kula nyama choma zaoi, wale watatu walirudi kwenye nyumba ya ya Mzee Kimaro.
Punde tu baada ya kuingia chumbani, ghafla Alvin alipokea simu kutoka kwa Rodney. "Alvin, ungewezaje kumuacha Sarah peke yake? Ungemrudisha nyumbani angalau. Wakati anaelekea nyumbani peke yake sasa hivi, mwendesha bodaboda alimpora na kumjeruhi."
Alvin alipigwa na butwaa, na uso wake ukakunjamana. “Sarah si ana gari?”
"Angekuwa na wakati gani wa kupata gari wakati ndo kwanza amerudi Nairobi?" Rodney aliongea kwa hasira, “Pia alikuwa amelowa nguo zote, nilipomuuliza kilichotokea alikataa kuniambia. Broo, umeenda mbali sana.”

Sura ya: 280

Alvin alikunja midomo yake kwa kuudhika. "Mtunze."
Baada ya simu kukatika, Lisa aligeuza kichwa na kumtazama Alvin. "Nini tatizo? Kuna kitu kilimpata Sarah?"
“Umesikia kila kitu?” Macho ya Alvin yaliangaza. Alikuwa amerekebisha sauti hadi kiwango cha chini kabisa, hivyo alishangaa kwamba kweli Lisa alisikia.
Hakusikia chochote, kwa kweli. Ilikuwa tu kwamba angeweza kufahamu mbinu za Sarah. Hakika, mwanamke huyo hakuwa rahisi.
Lisa alikoroma. “Siyo tu kwamba nilikisia kwa usahihi kwamba kuna jambo limemtokea, lakini pia nina uhakika kwamba Rodney ndiye aliyepiga simu hiyo. Rodney alikulaumu kwa kutompeleka Sarah nyumbani na alishangaa kwanini alikuwa amelowa, lakini Sarah hakumwambia ukweli.”
Alvin alipigwa na bumbuwazi hata akakaribia kutilia shaka kama masikio ya Lisa yalikuwa na kinasa sauti. Alikuwa amepunguza sauti hadi yeye mwenyewe akawa anasikia kwa shida, Lisa alisikiaje?
“Umejuaje?”
Lisa alikunja midomo yake. Kama ilivyotarajiwa, hisia zake zilikuwa sahihi. "Hata Lina alitumia mbinu kama hizo hapo awali. Sioni tofauti kati ya wasichana hawa wawili."
Alvin aliposikia hivyo alikunja uso.
Lisa alishtuka. “Kwanza kabisa, utaingiwa na huruma kwa vile kuna jambo limemtokea. Pili, hakumwambia Rodney kuwa ni mimi niliyemwagia mvinyo hivyo utamuona ni mwanamke muelewa. Kwa kawaida wanawake hujifanya wavumilivu ili kumvutia umakini wa mwanamume.”
Alvin akalipapasa paji la uso wake na kusema. “Lisa, najua humpendi Sarah, lakini humjui vya kutosha—”
“Sawa. Najua yeye ni mkarimu. Huenda umemfahamu kwa zaidi ya miaka kumi, wakati mimi ndiyo nimemuona kwa mara ya kwanza usiku wa leo. Hutajisikia vizuri kwamba ninamkashifu mpenzi wako wa kwanza ambaye hukuweza kumsahau milele.” Lisa aliitikisa kichwa. “Lakini samahani. Kwa macho yangu, yeye ni mwanamke ambaye anaweza kumpokonya mume wangu na kuharibu familia ya watoto wangu.”
“Kwanini huniamini?” Alvin alikuwa akichemka kwa hasira. "Kwa maana hiyo mimi ni mtu asiyewajibika kwako?"
"Uaminifu unapatikana kwa kujengwa tu. Umefanya nini ili kuujenga? Ilikuwa Maurine hapo awali na Sarah sasa.” Lisa hakuweza kujizuia kuongeza, “Ulienda naye hotelini jana, na nimekukuta naye pia hotelini leo. Ninyi wawili mmekuwa mkitumia muda mwingi pamoja na huwa hurudi nyumbani. Nitajisikiaje?”
Alvin alipigwa na butwaa. “Umejuaje…”
“Watu wengi waliwaona mkijachia tu. Walituma hata picha zenu kwenye simu yangu. Niambie jinsi ninavyopaswa kujisikia ikiwa kila mtu huko mtaani anajua mpenzi wako amerudi na kisha wanakuona ukibadilisha naye tu viwanja kula bata.” Lisa alijifuta machozi usoni mwake. “Mimi ni mwanamke mjamzito. Kwanini huwezi kunifanya nijisikie salama zaidi? Unajua nilivyofadhaika nilipoziona hizo picha? Mbaya zaidi sikuweza kukupata hata kwenye simu.”
“Nilikuwa tu nikijadiliana naye kuhusu hali ya ugonjwa wangu pale hotelini asubuhi hiyo. Hatukufanya lolote lingine.” Alvin alinyoosha mikono kumkumbatia huku akiwa na hofu kubwa.
Hata hivyo, Lisa alimsukuma mbali. “Usinishike. Nasikia harufu ya mwanamke mwingine juu yako. Inanichukiza.”
"Nilianza lini kunuka harufu ya mwanamke mwingine?" Alvin aliinamisha kichwa chini na kunusa mwili wake. Papo hapo aligundua harufu yake hafifu, sura yake ilibadilika kidogo. “Nitaenda kuoga.”
Lisa aligeuza uso wake mbali naye, hakujisumbua kumtazama tena. Haikuwa nia yake kumwaga machozi. Hata hivyo, Alvin alihisi kana kwamba Lisa alikuwa amebadilika na kuwa mtu tofauti tangu alipopata mimba. Alianza kuwa na wasiwasi juu ya kila kitu hata kama ni kidogo tu.
Alvin akahema. Moja kwa moja akavua nguo zake mbele yake.
"Unafanya nini?" Lisa alipigwa na butwaa. Uso wake ulijawa na hasira na aibu. Ingawa walikuwa wanandoa, hakuweza kuvumilia kumwona uchi chini ya mwanga mkali.
“Unaweza kuangalia mwili wangu ili kuona kama kuna dalili zozote za kulala na mwanamke. Mimi sina hatia.” Alvin akanyoosha mikono yake na kugeuka mbele ya Lisa.
Lisa hakuweza kuendelea kumtazama. Alisimama kwa haraka na kumsukuma mbali.

“Acha kulia mpenzi wangu. Ukilia utaniliza na mimi.” Alvin alichukua nafasi hiyo kumvuta mikononi mwake na kumkanda busu usoni mwake. Baada ya hapo, alisema bila aibu, "Kila mara unanituhumu bila kupata ukweli wako. Sarah alikuwa ni mpenzi wangu, lakini kwa sasa anajua nina mke. Ana wajibu wa kunitibu tu kwa sasa.”
"Alvin, nachukia tabia yako hii." Lisa aliinua mikono yake na kumpiga. Hakujisikia vizuri. Badala yake, alihisi huzuni zaidi na kulia kwa uchungu zaidi. “Sikubali kukutana na Sarah."
"Hilo haliwezekani, mpenzi." Tabasamu la uchungu likaangaza usoni mwa Alvin. "Ninahofia ni yeye pekee anayeweza kutibu ugonjwa wangu. Unataka niugue ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu nikiwa na umri mdogo na kukusahau wewe na watoto wetu?”
Lisa aliuma mdomo kwa uchungu. “Siwezi kuvumilia nyinyi mkitumia muda mwingi pamoja kila wakati. La sivyo… bora umuoe tu nijue moja, nami nitaangalia ustaarabu mwingine.”
Alvin alibana mashavu yake kwa nguvu. “Wewe ni mke king’ang’anizi kiasi gani? Sikutambua hilo mapema.”
Lisa alimkazia macho. "Alvin, unahitaji kuelewa kuwa nisingekujali kama sio watoto."
"Unamaanisha nini?" Macho ya Alvin yalimkazia. "Kwa hiyo umekaa nami kwa sababu ya watoto tu?"
“Fikiria ulichofanya. Mwanzoni, ulimweka Maurine kando yako, na sasa una Sarah pamoja nawe. Ninahisi kuchoka. Sijui mapenzi yangu kwako yatadumu kwa muda gani,” Lisa alisema ukweli wake kwa uchungu.
Alvin alisikitika sana. Hakutarajia kwamba Sarah angegeuka kuwa mwanasaikolojia wake pia.
Baada ya kusema hivyo, kwa kweli hakuwa na nia ya kurudiana na Sarah. “Nimekuelewa, babe.” Kisha akaelekea bafuni.
Wakati Alvin anatoka bafuni, Lisa alikuwa tayari amejilaza kitandani. Aliendelea kujirusha huku na kule huku akipata shida kupata usingizi.
Alvin akajilaza kitandani na kumzungushia mikono yake. “Sitalala nje ya chumba hiki leo. Nataka kulala na wewe.” Lisa aligeuza mwili wake na kumpuuza. "Ninashuku kuwa tumekuwa tukigombana siku hizi hasa kwa sababu tunalala tofauti sasa. Kama wanandoa, tunahitaji kuwa karibu ili kuboresha uhusiano wetu.” Kwa hayo, Alvin akambusu usoni.
Hapo awali, alipanga tu kumpa busu. Hata hivyo, aliishia kumbusu kwa muda mrefu kuliko alivyopanga, labda kwa sababu hakuwa na uhusiano wa karibu sana naye kwa muda mrefu sana.
Lisa aliduwaa huku akimbusu. Nusu ya moyo wake ilimkataa huku nusu nyingine ikienda pamoja naye. Kwa hayo, Alvin akanogewa. Kweli, walikuwa wamegombana lakini walikuwa wakibiringishana kwa mahaba mazito pale kitandani kama wapenzi waliokamiana kwa muda mrefu.
Siku iliyofuata, hatimaye Lisa alikuwa akijisikia vizuri baada ya kulala vizuri. Hakika, Sarah alikuwa amekuja, na alionekana kumhitaji Alvin. Ilipokuja suala la kushughulika na mwanamke wa aina hii, Lisa alipaswa kuwa jeurikuliko yeye.
Ikiwa hilo lingetokea mapema, Lisa angeweza kuachana na uhusiano huo usio na utulivu. Sasa kwa kuwa alikuwa mjamzito, ilimbidi ailinde familia yake. Hakuwa na la kufanya zaidi ya kumpambania Alvin wake.
Baada ya kutafakari kwa muda, aligeuza mwili wake na kumwambia Alvin, “Kuanzia leo na kuendelea, nitatembelea ofisi kwako mara kwa mara. Kila siku nafungiwa humu ndani, sina pa kwenda na huwa nafikiria kupita kiasi, jambo ambalo linanisababishia mfadhaiko. Naweza kuwaathiri watoto waliomo tumboni.”
Alvin alikunja uso na alikuwa na wasiwasi juu yake. “Lakini—”
“Nimechoshwa na kufikiria juu yako kila wakati. Ulipokosa kurudi siku zile, nilijiuliza labda umeangukia kwamwanamke mwingine, au labda hunipendi kwa kuwa mimi ni mjamzito, na hunipendi kwa kuwa na wivu. Itaendelea kuishi katika mazingira kama hayo tena.” Lisa alikatisha sentensi yake. Sauti yake ilijaa dhiki.
Alvin akashusha pumzi. Baada ya kufikiria migogoro waliyokuwa nayo kwa siku kadhaa, hakutaka kupingana naye. “Sawa.”......ITAENDELEA....

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.