JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP..........................0628924768
SEHEMU YA................................276-278
Sura ya: 276
Huyo ndiye mwanamke ambaye Alvin alimfikiria hata katika ndoto zake.
Charity alikuwa amemuonya hapo awali kwamba Sarah alikuwa ni mwanamke mwenye nguvu sana kwa Alvin. Lisa asingekuwa na nafasi ikiwa Sarah angalikuwa hai.
Sawa, Charity pia alisema ‘ajihadhari’ jana yake. Alikuwa anamaanisha ajihadhari na Sarah Njau? Lisa alitetemeka. Alikuwa katika mshtuko mkubwa. Charity alikuwa akimwonya kujihadhari na Sarah Njau. Kwa hiyo, tayari alijua kwamba Sara alikuwa angali hai. Nini kingine alijua?
Mbali na hilo, Jack pia alikuwa amemkumbusha Lisa jana yake usiku. Kila mtu alijua juu ya hilo isipokuwa yeye mwenyewe. Je, Alvin angerudiana na Sarah?
Moyo ulimdunda huku akiligusa tumbo lake bila kujua. Hapana! Hakujali jinsi alivyokuwa zamani, lakini alikuwa baba wa watoto sasa. Walihitaji familia kamili. Hakutaka watoto wake walelewe na single mother. Hapo hapo akashika simu yake kumpigia Alvin.
"Samahani, nambari unayopiga haipatikani." Alikuwa anafanya nini hata akashindwa kupokea simu yake? Inawezekana kwamba alikuwa pamoja na Sara?
Hakuweza kuizuia akili yake kuendelea na mawazo hayo na haraka akampigia simu Hans. “Mbona Alvin hapokei simu zangu?”
Hans, ambaye alikuwa akifanya kazi kwa muda wa ziada ofisini, alishikwa na mshangao. “Bwana Kimaro anapatiwa matibabu ya kisaikolojia hivi sasa. Daktari anasema hatakiwi kusumbuliwa.”
“Matibabu? Unamaanisha Dk. Nyasia?”
"Ndiyo, daktari alisema ni muhimu kuanza kumtibu haraka iwezekanavyo.” Hans alikuwa na wasiwasi. Alitumai Alvin angeweza kupona haraka. Ingekuwa balaa endapo Lisa angegundua kuwa Nyasia ni Sarah Njau aliyefariki dunia.
Lisa aliuliza baada ya ukimya wa muda mrefu, "Analala huko New Metropolis Park?"
“Ndiyo.”
Lisa alitamani angeweza kwenda kumngoja kwenye nyumba hiyo ya New Metropolis Park, lakini, alijua asingeweza kuruhusiwa kuondoka katika familia ya Kimaro. Alizidiwa na majuto kwa kukubali kuhamia katika nyumba ya familia ya Kimaro hapo mwanzo.
•••
Saa mbili na nusu usiku, Alvin aliingia kwenye baa ya hoteli ya Peninsula iliyokuwa ikicheza wimbo wa jazz. Alimwona Sarah ambaye alikuwa amekaa baa mara ya kwanza. Usiku huo alikuwa amevalia gauni refu jeupe. Alionekana kama ua la thamani ambalo lilichanua tu usiku.
“Si ulisema tuna ratiba ya kutibu ugonjwa wangu usiku huu? Kwanini tunakutana hapa?" Akamsogelea na kuketi karibu yake.
"Ungependa kwenda hospitali ya kuchosha au kliniki ya wagonjwa wa akili?" Sarah alitabasamu.
Alvin akaminya midomo yake. Hakika, hakutaka kukutana katika mojawapo ya sehemu hizo.
“Hapa ndio mahali pazuri zaidi. Hakuna kelele wala ghasia nyingi.” Saraha alimwambia kwa utulivu.
Kwa mshangao wake, mhudumu wa baa alikuja na vinywaji viwili. Akampa kila mmoja cha kwake.
“Tunakunywa pia?” Alvin akakunja uso.
"Unataka kutibiwa katika hali hii ya wasiwasi?" Sarah alielekeza mkono kwenye moyo wake na kisha kichwa chake. "Mwanasaikolojia hufanya nini? Tunashughulikia maeneo haya mawili. Kunywa tembe hakusaidii ugonjwa wa moyo wala akili.” Alvin alichukua pombe hiyo kimya kimya.
Sarah alimtazama Alvin. Ingawa alikuwa ameketi katika eneo lenye giza, sifa zake za kupendeza zilibaki za kuvutia. Alihisi haja ya kuushinda moyo wake. “Alvinic unaweza kunifanyia upendeleo? Unaweza kuiacha New Era Advertisings?”
“Unataka kuichukua, huh?”
"Hapana. Nina shughuli nyingi za kutosha kwa hiyo sina muda wa kusimamia kampuni.” Sarah alitoa kicheko cha uchungu. “Baba yangu ameanguka tena huku Charity akiwa gerezani. Baba yangu anachojali zaidi ni kampuni yake. Ninahofia hataweza kuendelea bila kampuni yake.”
Chembe ya upole ikaangaza machoni mwa Alvin. “Wewe bado ni yule yule. Hata hivyo, usisahau jinsi baba yako alivyokutendea ulipokuwa ukitangatanga huko ulaya kwa miaka hii.”
“Hiyo ni hadithi nyingine. Ninafanya tu kile ninachopaswa kuwa kama binti. Angalau nina dhamiri safi.” Sarah akahema. “Zaidi ya hayo, kaka yangu hana kazi licha ya kwamba tayari ni mtu mzima. Ninapaswa kumsaidia kugeuza ukurasa mpya ili asiwe mtu mbaya kama hapo awali.”
Kwa kutajwa kwa Thomas, Alvin alifunua sura ya kuchukiza. "Ni wakati wa kubadilika."
Sarah alimcheka ghafla. “Nilifikiri ningehitaji kuweka jitihada fulani ili kukushawishi. Sikutarajia kwamba ungekubali kwa urahisi.”
"Nina deni kwako," Alvin alisema.
"Hapana. Huna deni kwangu,” Sarah alijibu huku akiinamisha kichwa chini na kutazama mvinyo iliyokuwa mezani.
Nusu saa baadaye, wote wawili walipanda ghorofani pamoja.
Kelvin alitokezea kwenye kona yenye giza na kuchukua picha za wawili wale. Alitabasamu baada ya kuona picha iliyokuwa mkononi mwake. Alipokuwa akifanya kazi ofisini kwake mchana huo, ghafla alipokea ujumbe wa ajabu kutoka kwa Melanie ambao ulimwambia atembelee hoteli hiyo kuchukua udaku wa Alvin.
[Lisa, inaonekana uko hatarini.] Kelvin alimtumia Lisa picha hiyo kupitia WhatsApp. [Niliona haya nilipokuwa na rafiki yangu kwenye Hotel ya Peninsula usiku huu. Wote wawili waliingia katika chumba cha faragha ghorofani. Nilisikia una mimba. Afadhali uendelee kulea mimba yako peke yako. Unaweza kuja kwangu muda wowote ikiwa unahitaji msaada.]
•••
Wakati Lisa alipopokea picha hiyo, moyo wake ulibadilika kuwa wa baridi. Ilionekana kana kwamba shimo lilikuwa limetobolewa moyoni mwake.
Jana yake, Melanie aliwanasa wakitoka kwenye chumba cha hoteli hiyo. Siku hiyo, walionekana tena pamoja. Alimaanisha nini kwenda kutibiwa? Alimaanisha nini kwa kujishughulisha na kazi? Haya yote yalikuwa ni uongo. Alitaka tu kumweka Sarah karibu yake. Vipi kuhusu yeye na watoto wachanga tumboni mwake?
Lisa alilipuka kwa hasira kwani alishindwa kuvumilia tena. Ilibidi aondoke kwenye nyumba ya Kimaro na kwenda kumtafuta Alvin, lakini alidhani kwamba hakuna mtu ambaye angekubali kumruhusu. Baada ya kuwaza, akatafuta namba ya simu ya Jack na kumpigia.
“Ni nadra kwamba unanipigia simu kwa hiari yako mwenyewe," Jack alisema kwa mshangao.
“Jack, tafadhali nitoe kwenye nyumba hii. Nina jambo la dharura la kushughulikia.” Baada ya kufikiria kidogo, aligundua kwamba Jack alikuwa mtu pekee katika familia ya Kimaro ambaye angeweza kumwomba msaada.
Jack alipasuka kwa mshangao. “Ni usiku sana sasa. Ni nini muhimu sana ambacho unahitaji kushughulikia? Ikiwa bibi na babu yangu watajua kuhusu hilo, hakika watanizika nikiwa hai. Pia, Alvin…”
“Sifanyi chochote cha hatari. Ninahitaji tu kushughulikia mambo kadhaa ya haraka. Nitakuwa na uhakika wa kujitunza mimi na watoto wangu.” Lisa alimhimiza kwa utulivu. “Jack, usisahau uliahidi kunisidia baada ya kunikasirisha. Kama bado una hatia kuhusu hilo…”
“Sawa, sawa. Umeshinda. Nitakutoa. Njoo chini kwa siri. Usiruhusu mtu yeyote ajue.” Jack akashusha pumzi.
Dakika kumi baadaye, Lisa aliingia kisiri kwenye gari la Jack. Mlinzi alipogundua kuwa ni gari la Jack, hakulizuia gari hilo na kuliruhusu litoke nje ya nyumba ile.
"Unaenda wapi?" Jack alipomkazia macho, akajikuta bado amevaa nguo za kulalia. Alishangaa ni jambo gani la dharura lililomkurupua kiasi hicho.
"Peninsula Hotel."
"Mbona unaelekea hotel saa hizi?" Wasiwasi ulikzidi kuongezeka kwa Jack. Alijua kabisa kwamba familia ya Kimaro ilikuwa na wasiwasi sana juu ya watoto wa tumbo la Lisa.
"Ili kuangalia ikiwa Alvin yuko kitandani na mtu mwingine." Jack alifunga breki. Lisa aliongeza bila kujali, “Jack, tayari unajua kwamba Sarah bado yuko hai na Alvin amekutana naye hivi karibuni? Ulinikumbusha kuwa wanaume wanavutiwa kirahisi na wanawake wakati wake zao wakiwa wajawazito. Ulikuwa unamaanisha niwe makini na Sarah, sivyo?"
Sura ya: 278
Jack alipapasa paji la uso wake. Wakati mwingine, wanawake walikuwa na machale sana hivi kwamba ilionekana kana kwamba walikuwa na antena. “Kwa kweli, nilisikia tu kwamba Alvin, Rodney, na genge lake wamekutana pamoja na Sarah hivi majuzi. Sina uhakika na mambo mengine.”
"Badala ya kujitenga na mpenzi wake wa zamani, anafuatana naye na kuzurura naye badala yake. Je, hii haimaanishi kwamba atanisaliti mapema au baadaye?” Lisa aliuma mdomo, akihisi uvimbe kwenye koo lake. "Sitaki watoto wangu wakue bila baba."
“Sawa.” Jack aliendelea kuendesha.
Dakika 40 baadaye, gari lilikuwa limeegeshwa mbele ya Peninsula Hotel. Lisa aliufungua mlango wa gari na kutoka nje.
"Nisubiri." Akiwa na wasiwasi kwamba kuna kitu kingetokea kwa watoto wachanga tumboni mwake, Jack alimfuata haraka.
Lisa alipanda ngazi na kuusukuma mlango wa kila chumba cha faragha. Aliposukuma mlango wa chumba cha nne, aliona mwanamume na mwanamke wakiwa wamekumbatiana kwenye kochi. Mwanaume mrefu na mzuri alikuwa Alvin. Wakati huo huo, Sarah alikuwa akigusa kichwa chake kwa upole, kilichokuwa kimeegemea kifua chake.
Mlango uliposukumwa kwa nguvu, Sarah alishikwa na butwaa. Lisa alitazama eneo la tukio huku akiwa amejikita mahali hapo. Hisia nyingi zilimtawala sana. Alihisi kutapika. Kweli alijisikia kutapika.
Huyu ndiye mwanaume ambaye alikuwa akimpenda sana, lakini alikuwa ameegemea kifua cha mwanamke mwingine, tena alionekana kuzama kabisa kwenye hisia nzito kiasi cha kutojitambua. Kwa mtazamo huu mbele yake, alikiri kwamba hakuwahi kumshinda Sara. Angeweza kuchagua kutompenda Lisa, lakini angalau alipaswa kuzingatia watoto wake. Akilipuka kwa hasira, akaongeza mwendo wake kuelekea kwao.
Sarah alimsukuma Alvin kwa haraka. “Wewe ni mke wa Alvinic? Sio jinsi inavyoonekana…”
Lisa alichukua glasi ya mvinyo kutoka mezani na kummwagia Sarah usoni.
“Ah!” Sarah alipiga kelele.
Bado kichwa cha Alvin kilikuwa kinamuuma sana akiwa amejiinamia kwenye kochi. Sarah alipokuwa akimpatia matibabu muda ule, alitumia mbinu za kisaikolojia zinazojulikana kama Hypnosis, kumfanya akumbuke kumbukumbu zake mbaya za utotoni ili aweze kuzibadilisha kwa kumbukumbu nzuri badala yake. Katikati ya kukata tamaa na kutokuwa na uwezo, aliamshwa na kelele.
Mara tu maono yake yalipoonekana wazi, aligundua kuwa Sarah alikuwa amelowa na katika hali ya kusikitisha huku Lisa akiwa ameshikilia glasi ya divai kwa hasira.
"Unafanya nini?" Alvin akaruka na kusimama ghafla na kumtazama Lisa.
Sarah akamshika mkono mara moja. “Usikasirike, Alvinic. Yeye hakuwa na maana mbaya juu yangu. Nadhani alituelewa vibaya.” Macho ya Lisa yakatua kwenye mkono wa Sarah ulioshika kwenye mkono wa Alvin. Alipoona tukio hilo lisilopendeza, machozi yalianza kumtoka. Ni kutokuelewana? 'Alvinic' lilikuwa jina la utani la kupendeza.
"Wewe ni Sarah, sivyo?" Lisa alimtazama bila kujali, macho yake yalionyesha ukali. “Nilihisi kwamba upendo wa kwanza wa mume wangu ulikuwa safi na wa kipekee. Inatokea kwamba wewe huna tofauti na wale wanawake ambao wanafeki kuwa na huruma na kupanga njama za siri dhidi ya watu wengine.”
Uso mzuri wa Sarah ulipauka ghafla. “Kwa kweli ni kutokuelewana. Nilikuwa nikimtibu Alvin tu.”
“Kutibu?” Lisa alitoa kicheko. “Ni tiba gani hii? Chumba cha hoteli kimegeuka kuwa wodi ya wagonjwa, na pombe ndiyo dawa, na tiba ni mahaba?”
“Inatosha.” Alvin alikemea huku akionekana kulegea. Huku akiumwa na kichwa, aliendelea kumsikia Lisa akipiga kelele sana. Kichwa chake kilizidi kuwa na hali mbaya na akaruka kwa hasira. “Lisa nilikuambia utunze ujauzito wako nyumbani, lakini ulikuja hapa kumshambulia Sarah kwa maneno makali saa hizi. Unatafuta nini?”
Hali ya kutoamini ikapita usoni mwa Lisa. Yeye ndiye aliyekuwa akifanya mambo yasiyostahili na mwanamke mwingine. Hata hivyo, hakuwa na aibu wala wasiwasi hata kidogo. Badala yake, alikuwa akimlaumu.
“Kwa hivyo unanilaumu kwa kukukatisha starehe zako na mpenzi wako wa zamani?” Lisa alimkejeli Alvin katikati ya kwikwi zake.
"Nilisema sijafanya chochote, kwa hivyo inamaanisha hakuna kitu kinaendelea kati yetu. Kwanini huwa unawadhalilisha watu kabla ya kujua ukweli? Omba msamaha kwa Sarah sasa hivi,” Alvin alimuamuru kwa huzuni.
“Kuomba msamaha?” Lisa aliuliza kana kwamba alikuwa ametoka tu kusikia mzaha wa kuchekesha zaidi duniani.
“Ni sawa, Alvinic," Sarah alizungumza naye mara moja. “Bora uondoke na mkeo sasa. Ah-choo.” Sarah alipiga chafya na kujikunyata kitandani.
Hisia za kuchanganyikiwa zilimtawala Lisa ghafla. Wakati Maurine, ambaye alikuwa amefanana tu na Sarah alipotokea hapo awali, Lisa na Alvin walikuwa na mzozo mkali na walikuwa kwenye hatihati ya talaka. Sasa Sarah mwenyewe alikuwepo, je Lisa bado angekuwa na matumaini ya kumshinda? Macho ya Lisa yalitoa hali ya kuchanganyikiwa.
Aliyesimama mlangoni alikuwa Jack ambaye alikuwa akijizuia kuingilia suala hilo. Hata hivyo, alipoitazama sura ya Lisa inayotetemeka na upweke, alishindwa kuvumilia hali hiyo tena. Alisema licha ya nafsi yake, “Umeenda mbali sana, Alvin. Baada ya yote, yeye ni mke wako. Tayari umeoa, lakini unafanya mambo ya faragha na mwanamke mwingine kwenye chumba cha faragha usiku namna hii. Umewahi kufikiria hisia za Lisa?”
"Kwani nimefanya nini na Sarah?" Alvin alimtazama Lisa kwa hasira na kusema, “Jack ndiye aliyekuleta hapa? Umesha sahau alichokufanyia mara ya mwisho? Anajaribu tu kutusambaratisha. Kwanini kila mara huwa na watu wenye nia potovu?”
“Nani ana shida ya kuwatenganisha nyie? Lazima utakuwa umerukwa na akili.” Jack alishindwa kujizuia.
“Sawa. Twende zetu.” Lisa alimkokota Jack. Alikuwa amechoka. Hakupaswa kwenda.
"Ni nani aliyekuruhusu kumshika mkono?" Alvin alimsogelea Lisa na kumvuta kwake. "Jack, bora ukae mbali naye."
Baada ya kuona tukio hilo, sura ya Sarah iliganda. Alikunja ngumi kwa siri, na macho yake yalikuwa mazito kwa wivu.
"Unataka Jack akae mbali nami, lakini wewe kwanini hutaki kukaa mbali na Sarah?" Lisa alijitenga na Alvin na kumdhihaki. "Unaweza kufanya kitu kama hicho, lakini huruhusu watu wengine kufanya vivyo hivyo, sivyo? Alvin, kama unataka kurudiana pamoja na Sarah, unaweza kuniambia moja kwa moja. Sikuomba uwe nami. Ulidai kuwa unahitaji kufanya kazi ya ziada na kwenda kutibiwa, lakini kumbe unanidanganya. Unajua jinsi nilivyojihisi nilipokuona umeegemea kifua chake sasa hivi?”
Alvin alipigwa na butwaa, na uso wake ulikuwa umekunjamana. Hakujua kama alikuwa amemwegemea Sarah kifuani.
Wakati huo, Sarah alimsogelea Lisa. "Alvinic, ngoja nimuelezee." Kwa hayo, Sarah akamkabidhi kadi ya biashara. "Bi. Kimaro, mimi ni Nyasia, mwanasaikolojia ambaye anahusika na matibabu ya ugonjwa wa Alvin. Nilikuwa namtibu kweli sasa hivi. Nilijaribu kumfanya akumbuke kumbukumbu zake za utoto ili kumsaidia kushinda kiwewe chake, lakini alishindwa kujizuia. Basi nikamkumbatia ili kumtuliza, ndipo nyie mkaingia.”
Baada ya kupokea kadi, Lisa alipigwa na butwaa. Kamwe hangeweza kutarajia kwamba Sarah alikuwa yule Daktari anayeitwa mwanasaikolojia, Nyasia, ambaye Chester alikuwa amemtaja kuwa mwenye kipaji na asiyeeleweka.
Kwa wazi, mwanamke huyu hakuwa rahisi. Ikiwa angemtibu ugonjwa wa Alvin kila siku, angeweza kumnasa kwa mbinu za hila.
“Kweli, alikuwa akinitibu sasa hivi. Sababu iliyonifanya nisikuambie ni kwamba niliogopa utatuelewa vibaya na kufikiria mambo kupita kiasi kama sasa,” Alvin alisema.
Lisa aliinua kichwa chake bila huruma na kudhihaki, "Kwa hiyo mnataka niwaombe msamaha kwa hilo?"
Ikiwa Alvin angekuwa na ujasiri wa kumfanya aombe msamaha kwa Sarah, uhusiano wao bila shaka ungeharibika. Alvin alikosa la kusema.
Jack alisema kwa namna ya mzaha, “Kwanini aombe msamaha? Huu ni uonevu. Sarah ni ex wako, na kwa kweli mko peke yenu katika chumba cha faragha. Ulimfokea mkeo mjamzito dakika tu ulipomwona. Ni kawaida kwa mwanamke kuingiwa na wivu kwa kumkuta mumewe akiwa katika hali kama hiyo, hata kama ingekuwa ni wewe.”.....ITAENDELEA...
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
