JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP..........................0628924768
SEHEMU YA.................................274-275

Sura ya: 274

Usiku huo, Mzee Kimaro ghafla alimuuliza Alvin, “Mama yako anaendeleaje kwenye kampuni siku hizi?
“Nina muda sijamuona” Alvin alijibu.
Mzee Kimaro alikoroma kwa sauti nzito. “Bado anamsaidia Mason? Ananichukiza sana.”
Alvin alikataa kutoa maoni yake. Alimjua Lea, alimpenda na kumwamini Mason kupita kiasi.
“Wow, mnakula chakula cha jioni.” Willie na Jack ghafla wakaingia “Babu, Bibi, mnadhani nilikutana na nani kwenye baa usiku huu? Niligongana na Sa—’”
Ghafla aliganda baada ya kuwaona Lisa na Alvin kwenye meza ya kulia chakula. Rangi zote zilimtoka usoni papo hapo. Hawakutegemea kuwakuta kwenye makazi ya familia Kimaro.
Jack, kwa upande mwingine, alimtazama Alvin kwa utulivu kabla ya kujiweka karibu na Mzee Kimaro.
“Uligongana na nani, mbona umekatisha ghafla?” Mzee Kimaro aliuliza.
Willie alivuta pumzi kwa kina kabla ya kujibu, “Um… hakuna mtu. Nahisi njaa. Shangazi Yasmine, tafadhali unaweza kunipitishia sahani?”
Mzee Kimaro alimkazia macho na kutoa mkoromo wa dharau. "Unajua tu jinsi ya kubarizi kwenye baa, lakini kwenye majukumu ya kazi,walaa! Kwanini nyinyi wawili hamwezi kujifunza kitu kutoka kwa Alvin? Angalia jinsi anavyosimamia vyema KIM International.”
Uso wa Jack ulianguka na akakunja ndita ghafla. Babu yake asingeweza kamwe kutambua kazi nzuri aliyoifanya hata iweje.
Kwa upande mwingine, Willie hakuonekana kuwa na wasiwasi hata kidogo. "Babu, sio kila mtu ana talanta kama yeye. Kenya inaweza kuwa na mtu mmoja tu tajiri zaidi."
“Uko sawa.” Bibi Kimaro alisema. Aligeuka ghafla na kulitazama tumbo la Lisa na kutabasamu. “Lakini watoto walio tumboni mwa Lisa hakika watarithi akili za baba yao.”
Alvin akakipapasa kichwa cha Lisa taratibu. "Sijali kitu kingine chochote mradi tu wawe na afya."
"Hiyo ni sawa." Hisia ngumu ilijidhihirisha katika moyo wa Jack alipoona hivyo.
“Sawa, Jack, Alvin atakuja kuwa baba hivi karibuni. Wewe ni lini utatafuta mchumba uoe?” Bibi Kimaro ghafla alibadilisha mtazamo wake kwa mjukuu wake mwingine. “Nimefikiria juu yako na kuona binti kutoka kwa familia ya—”
“Bibi, tafadhali acha kunitambulisha kwa wasichana wa ajabu.” Jack aliziba masikio yake. "Familia ya Campos ilinipendekeza kwa hafla ya kuchagua mchumba siku chache zijazo na ninakaribia kupoteza akili."
Bibi Kimaro alikunja uso. “Wanakutambulisha kwa nani?”
"Binti kutoka kwa familia ya Ngugi, binti wa mwanahisa mwingine katika Kampuni ya Campos."
"kwa hiyo wewe unafikiria nini?" bibi mzee aliuliza.
Jack alihisi kutetemeka hadi kwenye uti wa mgongo wake. "Bado sifikirii kuoa."
"Hmm, kumbuka kuwa wewe ni Kimaro. Hatukukulea ili uwe chombo cha familia ya Campos,” Mzee Kimaro alimkumbusha kwa upole, “Familia ya Campos pia haitamruhusu mtu wa nje kujipenyeza ndani ya biashara zao.”
Jack aliinamisha kichwa chake kula chakula chake taratibu. Kwa kweli, alikuwa amefikiria kujaribu bahati yake katika Kampuni ya Campos kwani hakuthaminiwa kwenye kampuni ya KIM International. Lakini, Jerome Campos alikuwa tayari akifirikiwa kukabidhiwa mikoba ya Campos Ltd. Labda nafasi yake ingekuwa ya chini zaidi katika familia ya Campos kuliko akiwa na familia ya Kimaro. Kwa kweli alihisi kama hafai popote.
Baada ya chakula cha jioni, Mzee Kimaro alisimama na kusema. “Alvin, twende maktaba pamoja nami, nina jambo la kuzngumza na wewe.”
Alvin alikunja uso kabla ya kumgeukia Lisa. “Unaweza kwenda kupumzika kwanza. Nitaungana nawe baadaye.”
"Sio lazima." Lisa alitembea kuelekea mlangoni bila kujali.
Ndani ya maktaba, Mzee Kimaro alipumua kwa muda mrefu kabla hajaanza kuongea. "Familia ya Campos haijaribu hata kuficha tamaa zao mbaya sasa. Wanataka kumtumia Jack kama zana ya kujipenyeza kwa familia za matajiri kupitia ndoa. Umemsikia Jack sasa hivi, nini maoni yako kuhusu hilo?”
"Sijali mradi tu watu wa familia ya Kimaro hawaniangusha." Mzee Kimaro alikosa la kusema.

Baada ya chakula, Lisa alienda kupumzika kwenye bustani. Shangazi Yasmine alikuwa ameondoka kwenda kumtafutia blanketi. Mahali alipokuwa ameketi kulimpa mtazamo mzuri wa Mlima wa Sherman wakati wa usiku huo wa mbaramwezi. Harufu hafifu ya majira ya kiangazi ilimkumba huku upepo wa usiku ukivuma.
"Hongera kwa ujauzito wako." Jack akamsogelea taratibu. Lisa hakumtazama hata kidogo.
“Haya, bado unanikasirikia? Wewe ni mke wa mtu tajiri zaidi Kenya.” Akaketi karibu yake. “Unapaswa kunishukuru. Bado ungekuwa mpenzi wa kisirisiri kama nisingekuwa mimi."
Lisa akamkazia macho, akakosa la kusema. Hakuwahi kukutana na mtu asiye na aibu zaidi yake. Kwa kweli, hakumkasirikia tena kwa kumfanyia njama chafu mara ya mwisho. Mambo mengi sana yalikuwa yametokea baada ya hapo na kulikuwa na watu wengi sana ambao alikuwa amekasirishwa nao.
Jack alimwambia baada ya kuona utulivu wake. “Um… nimekuja kukuambia ujihadhari...”
“Huh? Nijihadhari na nini?”
"Juu ya Alvin. Nilisikia wanaume wanavutiwa kirahisi na wanawake wengine pindi wake zao wakiwa wajamzito, hivyo inabidi umuangalie, haha,” alisema kwa nusu-utani. “Um… Inabidi niondoke hapa, kuna baridi sana. Hupaswi pia kukaa hapa kwa muda mrefu utapata nimonia.” Jack alipunga mkono na kugeuka ili kuondoka na kumwacha Lisa akiwa amekunja uso.
Lisa alijiwazia kwanini Jack alimfuata kumwambia hivyo? Alikuwa mtu wa pili siku hiyo aliyempa onyo kama hilo. Charity alikuwa amesema vivyo hivyo, lakini alipaswa kuwa makini na nani?
“Jack amekuambia nini?” Alvin alimwona Jack akiwa anaishilizia wakati yeye alipofika kwa Lisa akitokea ndani. uso wake ulikunjamana kwa hasira.
“Hakuna kitu.” Lisa aliangalia upande mwingine.
“Usiamini neno lolote analosema. Bado hafurahii kupoteza nafasi ya kuongoza kampuni. Anajua wewe ni udhaifu wangu hivyo atajaribu kuzua mafarakano kati yetu.” Kisha kumwambia hayo, akamchukua mikononi mwake. “Umekaa hapa kwa muda wa kutosha. Turudi ndani kutazama sinema.”
"Hapana." Lisa aliinamisha kichwa chini, akihisi kupasuka. Hakutaka kukaa chumbani peke yake lakini pia hakuweza kumsamehe kwa kumtelekeza kwa muda wa siku kadhaa.
"Wanawake huwa wanasema kinyume na kile wanachotaka." Alipokumbuka maneno hayo ya Daktari, Alvin alimbeba hadi kwenye chumba cha sinema.
Alikuwa amekaa kwenye nyumba hiyo kwa muda sasa lakini hii ilikuwa mara ya kwanza walikuwa wakitazama sinema kwa pamoja. Kufikiria jambo hilo kulimhuzunisha. "Alvin, lazima uwe umetazama sinema nyingi hapa na marafiki au wapenzi wako."
“Si…” Alikuwa karibu kukataa lakini akakumbuka kwamba alikuwa ametazama sinema na Melanie mara ya kwanza Lisa alipotembelea jumba hilo. Mwanamke huyo kweli alikuwa na wivu. Lisa alichaia tabasamu la kichefuchefu kabla hajageuzia uso wake pembeni.
Alvin aliurejesha uso wake ili kumpa busu kwenye midomo. “Usiwe na wivu, sikutazama sinema na Melanie mara ya mwisho. Nilikuwa kwenye simu yangu na sikujua sinema yake hata inahusu nini.”
“Sikuwa na wivu. Niache.” Ghafla aliona aibu baada ya kuona tabasamu lake la uvivu.
"Siendi popote. Chagua filamu unayopenda tutazame. Nimekuandalia korosho za kutafuna. Ni nzuri kwa ukuaji wa ubongo wa watoto."
Alimtazama na kisha akachukua korosho kabla ya kutikisa kichwa kukubali. “Nafikiri hivyo pia. Itakuwa balaa ikiwa watoto wangu watakuwa na akili ya polepole kama baba yao.” Mwishowe, alichagua filamu ya James Bond, ambayo iligeuka kuwa nzuri sana.
Alvin alimlisha korosho kimahaba mara kwa mara wakati filamu inaendelea. Lisa hakuwa na hamu ya kula korosho hizo lakini akajikuta zinamnogea. Aliishia kula takriban pakiti tano peke yake.

Sura ya: 275

Wakati filamu ikiwa imekolea, simu ya Alvin iliita ghafla. Akaitoa mfukoni. Lisa aliiba kwa kuitazama na kugundua mtu anayeitwa Nyasia alikuwa akimpigia simu.
“Nitaenda nje kupokea." Alitoka chumbani na kuitikia simu kwa sauti ya chini. “Kuna nini?”
“Siwezi kukupigia simu mpaka niwe na sababu?” Sauti ya Sarah ya kukata tamaa ilisikika kutoka upande wa pili.
'Siyo kwamba…mimi…” Alvin akajikanyagakanyaga.
Mwanamke kwa upande mwingine alicheka. “Pole kwa kukusumbua. Nilifanya utafiti kuhusu hali yako wakati wa mchana na nikaja na mpango wa matibabu. Hebu tuanze matibabu usiku wa leo.”
“Leo usiku?” Alvin alishangaa.
“Uh-ha. Nimeandaa mipango 30 ya matibabu kwa sasa na itafanywa kwa nyakati tofauti za siku. Muda mzuri zaidi ni usiku na nadhani mwili wa mwanadamu ndio huwa umetulia zaidi kwa wakati huu, kwa hivyo itakuwa rahisi kwako kuungana na hisia zako za kweli. Kando na hilo, ni vigumu kutibu hali yako kadiri tunavyoahirisha kwa muda mrefu. Usiku wa leo ni wakati mzuri zaidi.”
Alvin alikunja uso na kusema baada ya kusitasita kwa muda mfupi, “Samahani lakini nina shughuli nyingi kwa sasa…”
“Naona. Najua utakuwa umebanwa na mkeo! Samahani kwa hilo…” Sarah alisikika akifadhaika. "Karibu nilisahau kuwa wewe ni mume wa mtu sasa."
“Ni sawa. Vipi kesho usiku?” Alvin aliuliza.
“Hakika.” Alitabasamu kwa uchungu. "Nina wivu sana na mke wako."
Hili lilimshangaza. Hisia ngumu ikatokea moyoni mwake. Ikiwa mambo yangeenda kulingana na mipango, Sara angekuwa mke wake sasa.
Wakati akiwaza ni kitu gani cha kumwambia, tayari mtu wa upande wa pili wa simu aliaga na kukata simu. Alisimama pale kwa sekunde chache kabla ya kuingia tena kwenye chumba cha sinema.
Lisa aliinua macho yake kumtazama. “Mmempata mwanasaikolojia Nyasia?”
"Ndio. Inaonekana kuna nafasi naweza kupona kabisa.” Akamkumbatia Lisa kwa furaha.
"Ni mwanaume au mwanamke?" Lisa alihoji baada ya kusitasita kwa muda mfupi.
“Una wivu tena?” Alvin aliinua macho yake. "Babe, lazima uamini kuwa ninakujali wewe na watoto tu kwa sasa." Bila kumpa nafasi ya kujibu, alibana midomo yake juu ya lips zake.
Lisa alitaka kukataa lakini ilikuwa imepita muda mrefu sana tangu wapeane busu kwa mahaba. Kwa sekunde kadhaa, akili yake ilipotea kabisa. Hatimaye, alimvuta mikononi mwake alipokuwa karibu kukosa pumzi.
Filamu ilipoisha, alimbeba juu hadi chumbani. Alvin alikaa kitandani huku akiwasomea vitabu vya hadithi watoto waliokuwa tumboni mwa mama yao. Sauti yake ya sumaku ilituliza masikio ya Lisa. Hatimaye, alilala kwa kubembelezwa na sauti hiyo. Alikuwa akisumbuliwa na kukosa usingizi kwa siku kadhaa. Muda mrefu ulikuwa umepita tangu apate usingizi mzuri.
Asubuhi iliyofuata. Alvin alipokea simu kutoka kwa Rodney baada ya kuzinduka. "Alvin, Sarah alilewa jana usiku na nikamrudisha nyumbani."
“Sawa…” Alvin aliitikia kwa mkato.
“Nafikiri alitoka kunywa pombe kwa sababu yako,” Rodney alilalamika kwa kufadhaika, “aliendelea kunung’unika kuhusu kukosa nafasi kwako na hata kulia.”
Alvin alisugua kichwa chake. Alikuwa amehisi sauti yake isiyo ya kawaida wakati wa mazungumzo yao jana yake usiku. “Rodney, nimeoa. Kweli…Ikiwa unampenda, unapaswa kuwa naye badala ya kumpa mtu mwingine.”
Hilo lilimshangaza Rodney. Aliweza kuonja uchungu mdomoni mwake. "Siku zote amekuwa akinichukulia kama rafiki na shemeji yake."
“Utajuaje kama hutajaribu? Nitakuwa baba hivi karibuni. Hii sio haki kwake pia,” Alvin alishauri. Kulikuwa na ukimya wa muda mrefu upande wa pili wa simu.
Alvin alivaa kabla ya kwenda kumtazama Lisa. Aliandamana naye wakati wote wa kifungua kinywa kabla ya kuondoka kwenda kazini.
Aunty Yasmine alimtania Lisa baada ya kuona mwanga wa furaha usoni mwake. "Inaonekana kama Bwana Kimaro ndiye tiba yako."
Lisa aliona haya na kuuma mdomo. Alichukia kwamba ujinga wao umepelekea madhara kwa Charity na Pamela. Hata hivyo, hakuweza kujizuia kutamani penzi la Alvin sasa akiwa mjamzito.

Alvin alimpigia simu ilipofika usiku. "Ninafanya kazi ya ziada usiku wa leo, kwa hivyo sitakuwa nyumbani kwa chakula cha jioni. Pia nina mkutano wa kijamii baadaye na sijui huo utaisha lini. Nitalala katika nyumba ya New Metropolis Park.”
“Sawa.” Ghafla Lisa akakumbuka ukumbusho wa Jack baada ya simu. Akiwa amechanganyikiwa, alishika kichwa chake kwa mikono yake yote miwili. Alitamani angemuuliza Jack vizuri alimaanisha nini alipomwambia awe makini na Alvin. Maurine alikuwa amekufa. Pengine ni Nyasia ndiye alikuwa changamoto nyingine muda huo?
Saa mbili usiku ujumbe uliingia kwenye simu yake wakati anakaribia kuoga. Alipokea picha iliyotumwa na nambari isiyojulikana kwenye whatsapp.
Alibofya kwenye picha. Alvin alikuwa akitembea kwenye korido ya hoteli ya nyota tano na mwanamke aliyevalia nguo ndefu. Mwanamke huyo alikuwa amevaa mtandio na mikunjo yake mirefu ilikuwa imening'inia kwenye pande za mabega yake kiasili. Wawili hao walionekana wakamilifu kana kwamba mwanamke katokea kwenye ubavu wa mwanamume.
Lisa alishtushwa na ukweli kwamba mwanamke huyo alifanana sana na yule kwenye picha ambayo Kelvin aliwahi kumuonyesha.
Alikuwa akifikiri kwamba Maurine anafanana sana na mwanamke huyo lakini sifa zake hazikuwa zikiendana sawia kama yule aliyekuwa kwenye picha. Mwanamke huyu alikuwa hata zaidi ya kufanana. Hapana, alifanana kabisa na Sara. Hata Alvin alikuwa akimwangalia kwa upole.
Lisa aliangalia tarehe chini ya picha. Ilichukuliwa jana saa tatu asubuhi. Ilikuwa wakati alipokuwa akikimbilia mahakamani. Alvin alikuwa akifanya nini hotelini na mwanamke huyu? Alikuwa nani?
Alihisi baridi kali ikipenya hadi kwenye uti wa mgongo wake. Alihisi presha zaidi kuliko alipopata habari kuhusu Maurine. Maurine hakuwa amemtisha kiasi hiki hapo awali.
Mara simu yake ikaita. Ilitoka kwa nambari ile ile iliyotuma picha hizo. Mara moja akaipokea. Kicheko cha furaha cha Melanie kilisikika. “Dada yangu kipenzi, umeiona picha? Umezipenda?"
“Zinakuhusu nini wewe?…” Lisa alisema kwa utulivu huku akijaribu kila awezalo kuzuia hisia zake.
Melanie alicheka. "Sawa, labda bado hujui kuhusu hili lakini mwanamke kwenye picha ni Sarah Njau. Hajafa.”
“Ni ujinga gani huo?” Lisa alikunja uso. Hilo lingewezekanaje? Sara alikuwa amekufa kwa muda mrefu.
“Ninasema ukweli. Nimemwona Sarah ana kwa ana hapo awali na hakika huyo ni yeye. Mbali na hilo, nimefuatilia. Sarah hakufa nje ya nchi wakati huo. Alirudi nyumbani siku chache zilizopita kwa ajili ya mazishi ya Maurine. Alvin, Rodney, na Chester wanakula bata pamoja naye kila siku, wakimchukulia kama binti wa kifalme. Kweli, niliona kwa macho yangu kwamba alikuwa akitoka naye kwenye chumba cha hoteli jana asubuhi. Unafikiri wapenzi wa zamani wangefanya nini katika chumba cha hoteli?”
Kweli, binadamu anaweza kukunyima neno la hekima litakalokusaidia, lakini umbea? Atakupa bila gharama yoyote. Mkono wa Lisa uliokuwa umeshika simu ulianza kutetemeka. Miguu yake ilikuwa ikizidiwa na udhaifu. Taswira ya Alvin kuwa kitandani na mwanamke mwingine ilipeleka maumivu makali kwenye moyo wake.
"Nina hakika kwamba lazima utaumia sana na kuogopa sasa." Melanie alicheka kwa furaha. “Najisikia vibaya sana kwako. Ingawa wewe ni mjamzito, mume wako anakutana kwa siri na mpenzi wake wa zamani. Naona hukuwa na wazo kuhusu hili. Habari hii nitakupa bure maana mimi ni dada mzuri sana.” Alikata simu baada ya hapo.
Lisa akaketi kitandani. Sarah alikuwa hai? Hilo liliwezekanaje?
Hakutaka kuamini, lakini picha ilikuwa uthibitisho......ITAENDELEA...

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.