JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP..........................0628924768
SEHEMU YA................................272-273
Sura ya: 272
Katika chumba cha kifahari kwenye hoteli ya nyota tano, Sarah alikuwa akisoma rekodi ya ugonjwa wa Alvin kwenye kochi. Alvin akaweka kikombe cha kahawa mbele yake.
Alikunywa haraka kabla ya kutabasamu. "Bado unakumbuka kuwa napenda Americo Coffee?”
"Ndiyo, sio wanawake wengi wanaopenda kahawa chungu." Alvin alikaa kwenye kochi lililo mkabala na Sarah. Ghafla alikumbushwa juu ya mwanamke nyumbani, Lisa, ambaye alipenda kahawa tamu. Kila mara alikunywa kahawa yake yenye sukari nyingi na cream.
Sarah aliona namna alivyokuwa amepotea kwenye mawazo. Mwanaume huyu alikuwa amekaa mbele yake lakini alikuwa amesafiri maili mia kadhaa kimawazo. Ni wazi kwamba alikuwa akimfikiria mwanamke mwingine. Asingefanya hivyo zamani. Moyo wake ukafadhaika, na kabla hajalifunga lile faili, alitabasamu. "Nina uhakika 80% kwamba ninaweza kutibu hali yako kabisa na kuzuia kujirudi tena kwa ugonjwa wako kwa siku zijazo."
Mwale wa mwanga ulionekana machoni mwa Alvin. Alipasua midomo yake kusema kitu wakati Shani alipompigia ghafla. "Bwana Kimaro, Bibi Mdogo ameondoka kuelekea mahakamani."
Uso wake ulianguka papo hapo. "Sikukuambia kwamba haruhusiwi kuondoka kwenye nyumba hiyo kwa sasa?"
"Samahani, lakini Bibi Mdogo alitishia maisha ya watoto ..." alielezea bila kusita.
"Vizuri sana." Kwa hasira, karibu aitupe simu yake. Mwanamke huyo alikuwa akitumia hata maisha yake na ya watoto kumtishia sasa. Hivi kweli aliwajali hata hao watoto kweli? Ina maana mapacha hao hawakuwa muhimu kwake kuliko Charity? Alihisi hasira na kukata tamaa kwa wakati mmoja.
Alvin akanyanyuka ghafla. “Tutaendelea siku nyingine. Ninahitaji kuwa mahali pengine sasa."
"Kweli, lakini ni bora kutoiahirisha au uwezekano wa kupona utakuwa mdogo." Sarah akaingiza simu yake kwenye mkoba wake. Wawili hao wakaelekea chini pamoja.
Melanie, ambaye alikuwa akitoka kwenye korido iliyokuwa karibu, aliwaona na harakaharaka akajongea kwenye kona ili kupiga picha.
"Melanie, kwanini umejificha hapa?" Jerome alimfuata na kuweka mkono juu ya kiuno chake.
"Tazama hii." Alimuonyesha picha. “Ni Sarah Njau! Hajafa!” Akafinya macho. "Huyu ndiye Sarah, tofauti na yule Maurine ambaye anafanana naye tu. Tsk, unafikiri wenzi hao walikuwa wakifanya nini pamoja kwenye chumba cha hoteli?” Melanie alifurahishwa na kitendo hicho. “Unadhani Lisa atazipokeaje picha hizi?”
Jerome alishtuka. “Nilisikia anakaa kwa Mzee Kimaro kutokana na ujauzito wake. Nina hakika kwamba atapoteza watoto wake ikiwa atagundua kuwa mume wake anachafuana na mpenzi wake wa zamani.”
“Uko sawa.” Alitabasamu kwa ndani. “Lisa alidhani alishinda kwa sababu aliolewa na Alvin, lakini inavyoonekana ataachwa hivi karibuni.”
•••
Mahakama ya Nairobi.
Kesi ilikuwa inaishilizia wakati Lisa na Pamela walipoingia eneo la tukio. Charity alikuwa amesimama kizimbani. Ilikuwa ni muda tangu walipokutana mara ya mwisho. Mwanamke huyo aliyekuwa mrembo na mzuri alikuwa akionekana dhaifu na amechoka, nywele zake zikiwa kavu na zilizotimkatimka.
“Sikufanya hivyo. sikuua mtu yeyote.” Alikanusha vikali licha ya ushahidi wote ulioelekezwa kwake. "Nimetengenezewa njama tu."
Bw. Shea alisema kwa uthabiti, “Si lazima ukubali lakini inasalia kuwa kweli kwamba uliwakodisha watu kumuua Maurine Langa katika moto wa kikatili. Kinachochukiza zaidi ni kwamba hata hujutii matendo yako!”
Jaji kiongozi alikunja uso kabla ya kutangaza hukumu ya mwisho, “Mshtakiwa Charity Njau amepatikana na hatia ya mauaji. Kutokana na ukaidi wake na kutoonyesha dalili za kujutia kitendo chake, mshtakiwa anahukumiwa kifungo cha maisha jela na kunyimwa haki za rufaa mara moja.”
"Hapana, binti yangu hakuua mtu yeyote!" Jennifer alisimama kwa nguvu, uso wake ukiwa na machozi. Askari wa usalama walijaribu kumzuia kuondoka eneo lililotengwa.
Macho ya Charity yalimtoka machozi. Ingawa alitazamia hili kutokea, hakuweza kujizuia kuhisi kukata tamaa wakati hatimaye ulipofika.
“Charity…” Lisa alimtazama kwa huzuni. “Samahani…” Lisa alihisi hatia. Charity asingeingia kwenye matatizo hayo kama Lisa asingefanya kipimo cha DNA.
"Sikutarajia nyinyi wawili mngekuja." Midomo ya Charity ilitetemeka. Ilikuwa ni ukweli kwamba walikuwa hawajafahamiana kwa muda mrefu.
"Tunaamini kuwa huna hatia." Mashavu ya Pamela tayari yalikuwa yamelowa kwa machozi. “Bila shaka tutakata rufaa dhidi ya kesi hiyo na kuwatunza wazazi wako.”
"Asanteni. Lakini ikiwezekana, tafadhali wasaidieni wazazi wangu waondoke Nairobi haraka iwezekanavyo...” Kabla hajamaliza maneno yake, maafisa wa kutekeleza sheria walikuja kumburuta. Alitazama nyuma kwa mara ya mwisho na kusema. “Jihadhari na Sarah Njau…”
Kwa sababu ya umbali huo na sauti yake iliyochoka, Lisa aliona tu midomo yake ikicheza lakini hakuweza kusikia alichosema. “Anasema nini? Anasema tujihadhari na nini?"
“Hata mimi sijasikia vizuri.” Pamela alijaribu kufikiria jinsi Charity alivyotamka. “Jihadharini na nani sijui…”
Lisa alichanganyikiwa. Hakuweza kutafakari sana kwa sababu Jennifer Musyoka nusura azimie kwa kulia sana. Wawili hao walimshika mkono haraka mwanamke huyo aliyekuwa amehuzunika. “Anti Jennifer, usijali. Bado kuna matumaini maadamu Charity yuko hai. Tutamtoa hata ikichukua mwaka, miaka miwili au mitatu.”
“Asanteni.” Jennifer alithamini msaada huo.
"Lakini wewe na mumeo mnapaswa kuondoka Nairobi hivi karibuni," Lisa alisema kwa sauti ya wasiwasi. “Charity alipendekeza kwamba ninyi wawili muondoke hapa mara moja. Nadhani amegundua kuwa kuna kitu kibaya, kwa hivyo anadhani ninyi wawili mnaweza kuwa hatarini.”
Sura ya kuchanganyikiwa iliosha uso wa Jennifer. "Mimi na Boris hatukumchukiza mtu yeyote."
"Lakini nadhani Charity yuko makini kuhusu hili, hata mimi nahisi wasiwasi sana," Pamela alisema, "Naweza kuwapeleka Dar es Salaam. Familia yangu itawapokea huko. Ninaweza kumwomba kaka yangu mkubwa awatunze.”
“Asante, kwa kweli.” Sauti ya Jennifer ilidhihirisha shukrani ya kweli.
“Unapaswa kuondoka sasa hivi kwenda kufungasha. Charity atakuwa na utulivu zaidi ikiwa mtaondoka hivi karibuni," Lisa alihimiza.
Baada ya Jennifer kuondoka, Pamela alishusha pumzi ndefu. "Familia ya Njau ilikuwa moja ya familia tajiri hapa Nairobi hapo awali. Sikutarajia wangeangukia katika hali hii katika siku chache.”
“Hakika,” Lisa alijibu.
"Angalia matatizo uliyonayo kwa sasa. Nitaondokaje na kukuacha ukiwa hivi?" Pamela alisikitika.
"Unaondoka?" Lisa alishangaa.
"Ndio. Ninafuatiliwa na Rodney kwa sasa, kwa hivyo kaka yangu alipendekeza kwamba niondoke nchini kwa muda.” Alishusha macho yake chini kwa huzuni. "Siwezi kukusaidia wewe au Charity kwa kukaa hapa. Nataka kuwa na nguvu zaidi. Siku moja, ninataka kutengua uamuzi wa kesi yake.”
Lisa alishtuka. “Uko sahihi. Hatuna uwezo sana.”
Hakuwa na nguvu hata ya kuweza kuondoka kwenye nyumba ya Kimaro siku hiyo ikiwa asingetumia maisha ya watoto kama tishio. Alitaka kuwa na nguvu zaidi, lakini kwa wakati huo, hakuwa na uhuru wa kibinafsi.
"Pamela, unapaswa kwenda." Alimtazama sana rafiki yake. “Nimeelewa matumaini yako. Nitajitahidi kuwa na nguvu pia baada ya kujifungua watoto. Sisi bado ni marafiki hata kama tuko katika nchi tofauti. Unapanga kuondoka lini?"
“Bado sijafikiria juu yake. Labda mwezi ujao.”
"Sawa, nijulishe mapema na nitakufanyia party ya kukuaga." Lisa alimkumbatia rafiki yake kwa nguvu. Pamela ndiye rafiki pekee ambaye angeweza kumtegemea katika jiji hilo lakini naye alikuwa anaondoka tena. Angekuwa peke yake tena kwa muda usiojulikana. Pamela alianza kulia kwa mara nyingine.
Wakati huo huo, gari jeusi la kifahari likasimama pembeni yao na Alvin akatoka ndani yake kwa hatua kubwa. Alionekana kuogofya, na kwa ujasiri, Pamela alimkinga Lisa nyuma yake.
“Sogea!” Macho yake yalidhihirisha dhamira ya hatari. "Pamela Masanja, nasema pisha njia! Nimekuwa nikikuvumilia kwa muda mrefu sasa."
Sura ya: 273
“Alvin, nimekuwa nikikuvumilia kwa muda mrefu pia. Lisa ana mimba ya watoto wako. Kwanini bado una mnyanyasa? Kwanini umtelekeze tu kwa bibi yako kisha upotee? Anahitaji mtu ambaye anaweza kumjali na kumtegemea,” Pamela alifoka kwa hasira, “Lini utaacha kuwa na hali ya kubadilika-badilika na kukasirisha? Yeye pia ni mtu mwenye mipaka.”
"Nyamaza! Huna haki ya kuingilia mambo yetu.” Alvin alimsukuma na kumsukumia Lisa kwenye gari.
Lisa alifumba macho. Kusema kweli, alikasirishwa sana na jinsi Alvin alivyokuwa mkorofi kwa Pamela.
"Kuna nini hutaki hata kuhangaika kunitazama sasa?” Alvin alikibana kidevu chake. "Fungua macho yako."
Lisa alihisi uchovu umeenea mwilini mwake. Uso wake wa kifahari ulionekana mara tu alipofungua macho yake tena. Bado ulikuwa uso ule ule, lakini moyo wake ulimuuma kwa kutokujua. "Alvin, Pamela yuko sahihi. Lini utaacha kuwa na tabia mbaya na dharau? Unakuwa mtu asiyeeleweka muda wote. Unaweza kunipa nyota wakati uko katika hali nzuri lakini utanifungia kwenye friji wakati una hasira mbaya. Nimechoka kuishi hivi.”
“Unadhani mimi napenda kufanya hivyo? Kwanini hutaki kuwa mke mwema? Unajua kuwa namchukia Charity lakini ulinitishia watoto ili tu kukutana naye.” Macho yake yalikuwa yamejaa hasira. "Ina maana watoto wetu sio muhimu kwako kuliko Charity kwamba uko tayari kuwatumia ili kunitishia?"
Lisa akadhihaki. “Unadhani nilikuwa na chaguo jingine? Mimi pia ni binadamu lakini unanifungia kwenye banda kama ndege. Nimepoteza uhuru wangu wote. Nisingebeba watoto wako kama ningejua haya yangekuwa maisha yangu baada ya kunioa.” Mwili wake ulitetemeka.
Muda mrefu baadaye, macho yake ya chuki yalikata tamaa. "Lisa, hustahili kuwa mama." Alidhihaki.
Lisa alihisi kana kwamba kuna kitu kimeingia ndani yake na akamfokea kwa mbwembwe, “Nitaliki ikiwa hufikirii kuwa ninastahili kuwa mama! Nenda katafute mtu ambaye anaweza kufanana nawe!”
Alikunja ngumi kuwa mipira huku akihisi moyo wake ukizidiwa na mapigo. "Hans, mrudishe kwa bibi."
"Hapana, sitarudi kwenye nyumba hiyo."
“Huna chaguo,” alisema huku akimkazia macho.
Lisa alipasua midomo yake lakini hakuna neno lililotoka. Badala yake, machozi yalianza kutiririka mashavuni mwake huku akimpiga ngumi za mgongoni. “Alvin kwanini unanifanyia hivi? Niambie nilikosa nini! Nimepoteza kila kitu, uso wangu, uhuru wangu…”
Hata wale marafiki wawili ambao walimjali sana. Mmoja alifungwa na mwingine alikuwa anaondoka hivi karibuni. Mwanaume pekee aliyempenda alikuwa hamjali pia.
“Umerukwa na akili…” Alvin alifoka na muda huohuoi Lisa alianguka chini kwa mfadhaiko. Alimnyanyua mara moja lakini tayari alikuwa ameshazimia.
“Hospitali,” Alvin aliagiza kwa hasira. Hans akatekeleza haraka.
•••
Katika hospitali.
Baada ya uchunguzi mfululizo, daktari alisema bila kujali, "Bwana Kimaro, nilikuambia hapo awali kwamba ujauzito wa mke wako bado haujatulia kwa hivyo hupaswi kumfadhaisha."
“Ni nini hasa kilimtokea?” Alvin aliuliza kwa wasiwasi.
“Nadhani amekuwa akivumilia hasira na huzuni nyingi hivi karibuni, bila kusahau kwamba mabadiliko ya homoni katika mwili wake yanamfanya apate hisia tofauti. Unapaswa kuwa mwangalifu na kumjali zaidi ili awe katika hali nzuri kila wakati. Kama mume wake, unapaswa kujaribu kutomkasirisha mara kwa mara.” Daktari akashusha pumzi. “Nimeona wanawake wengi wajawazito wakianguka katika mfadhaiko. Wao ndio walio hatarini zaidi kihisia katika hatua hii. Tumia wakati mwingi pamoja naye.”
Akakunja uso. "Haitaji kampani yangu."
Daktari akatabasamu. “Bila shaka anafanya hivyo. Mimi mwenyewe ni mwanamke na nimejifungua pia. Licha ya kile anachosema, kila mwanamke bado anatamani sana urafiki wa mume wake wakati na baada ya ujauzito.”
Alvin alionekana kushtuka. Baada ya daktari kuondoka, Alvin aliburuta kiti karibu na kitanda, akihisi uchovu. Ni lini mara ya mwisho alimtazama Lisa kwa ukaribu hivyo? Kwa muda sasa, wangeishia kwenye mabishano kila mara walipokutana. Ghafla aligundua kuwa alikuwa amepungua uzito na alionekana dhaifu kuliko hapo awali. Alipaswa kuongeza uzito wakati wa ujauzito.
Baada ya kusitasita kwa muda mfupi, Shani, ambaye alikuwa amesimama karibu, hakuweza kupinga kusema, “Bwana Kimaro, kwa kweli, nadhani umekuwa mkali sana kwa Bibi Mdogo hivi karibuni—”
Alvin alimtupia jicho baridi kabla hajamaliza sentensi yake.
“Um… Ninaelewa sababu yako ya kutotaka Bibi Mdogo kukutana na marafiki zake ili kumzuia kuwaza kupita kiasi. Lakini amekuwa akichoshwa na upweke kukaa ndani muda wote. Hurudi nyumbani wala hauulizi habari zake. Anaonekana mwenye huzuni sana akisimama karibu na dirisha kila siku kutazama ulimwengu wa nje…”
Alvin alijisikia vibaya kusikia hivyo. Watu walidhani kuwa mke wake anatia huruma? "Sikujibu simu zake kwa sababu kila mara anataka kubishana nami kuhusu Charity."
“Lakini Bibi Mdogo hajui hilo. Anafikiria tu kwamba umemchoka,” Shani alinong'ona.
Alvin alikaa kwenye ukimya mzito baada ya kusikia hivyo. Dakika 20 hivi baadaye, Lisa alifungua macho yake taratibu. Mara tu alipogundua mahali alipokuwa, mikono yake ilirukia tumboni haraka. “Watoto wangu…”
“Usijali, watoto wako salama.” Alvin alisema kwa upole huku akimshika mikono.
Sura ya mshangao ilienea usoni mwa Lisa. Kwa sekunde moja, alifikiria kuwa bado anaota.
“Mbona unanitazama?” Alipiga kichwa chake kwa upole na kuweka mikono yake karibu na midomo yake. “Lisa, nakiri nilikuwa na makosa. Badala ya kukaa na wewe na kukubaliana na wewe ukiwa mjamzito, niliendelea kugombana na wewe. Sikukusudia lakini mambo mengi sana yametokea hivi karibuni. Nipe muda. Upo tayari tusafiri nje ya nchi hali yangu itakapoimarika? Hatujasafiri pamoja hapo awali.”
Baada ya kimya kifupi, hakuweza kujizuia kusema, “Utanijali tena kwa siku chache kabla ya kunibadilikia tena? Naona huo ndiyo utaratibu wako siku hizi.”
Alvin alitabasamu kwa uchungu. "Ni lazima tuingie katika hali hii kwa sababu ya Charity? Fikiria kuhusu watoto. Unataka wakue bila wazazi?"
Machozi yakaanza kumtoka Lisa. Alikua bila wazazi, kwa hivyo hakutamani watoto wake wawe hivyo.
“Nimekuwa nikipuuza simu zako kwa sababu sikutaka kukuumiza. Upendo wangu kwako haujabadilika.” Alimshika mkono kwa nguvu kabla ya kumpa busu nyuma yake. "Nitajaribu niwezavyo kumaliza kazi mapema na kurudi nyumbani haraka, sawa?"
“Sitaki kuongea na wewe.” Lisa aligeuza na uso wake nyuma yake.
Kwa kweli, alikuwa amechanika kwa ndani. Hakuweza kukubali kutojali kwake lakini pia hakuweza kusamehe ukweli kwamba walikuwa wamempeleka Charity gerezani.
Baada ya Lisa kumaliza kuingizwa dripu, Alvin alimpeleka nyumbani kwa bibi yake.
Bibi Kimaro hakujua kwamba alikuwa amezimia bali alifurahi kuwaona wanandoa hao wakirudi pamoja. Aliwaamuru wasaidizi wa jikoni kupika chakula kizuri sana.....ITAENDELEA.....
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
