JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP..........................0628924768
SEHEMU YA................................270-271
Sura ya: 270
Sarah alikunja midomo yake kwa uchungu bila kutamka neno lolote.
“Ni sawa, Rodney. Sarah lazima awe na sababu zake,” Chester aliingilia kati. Rodney alimtazama Sarah kwa huzuni na hatimaye akahema.
“Mbona umerudi ghafla?” Alvin aliyekuwa kimya ghafla aliongea.
Moyo wa Sarah uliumia macho yake yalipotua kwenye uso alioufahamu mzuri. Aligeuza macho yake polepole kwenye picha ya Maurine nyuma yake. “Ni kwa sababu sikutarajia kifo cha Maurine. Kwa kuzingatia kwamba yeye ni binamu yangu mpendwa, bado ninapaswa kutoa heshima zangu za mwisho kwake.” Kila mtu alinyamaza.
Alex Langa alitembea ghafla kuelekea kwa Sarah. Akamkumbatia na kububujikwa na machozi. “Sarah mbona umerudi sasa hivi? Kifo cha Maurine kilikuwa cha kuhuzunisha na kisichokuwa cha haki.”
"Mjomba, Maurine alikufa vipi?" Sarah aliuliza huku akibubujikwa na machozi.
Hapo hapo Alex alimkazia macho Alvin. "Ilikuwa haswa ni sababu ya mke wake akishirikiana na Charity."
Sura ya Sarah ikawa ngumu kidogo, na uso wake ukabadilika polepole. Alipepesa macho na kuelekeza kwa Alvin. “Alvinic…”
Alvin alikwepa macho yake. “Ni Charity…”
“Alvin, acha kuwa upande wa Lisa,” Rodney alisema kwa hasira, “nimetamani sana kusema kwamba Lisa hastahili kuwa nawe kwa vile amejaa nia mbaya. Sasa kwa vile Sarah amerudi, unaweza kuachana na Lisa na kurudi kwa Sarah?”
Alvin akakunja uso wake. Alipokaribia kujibu, Sarah alisema kwa haraka, “Rodney, acha kuzungumza upuuzi. Alvinic tayari ana mke. Unawezaje kumshawishi aachane naye? Zaidi ya hayo, siwezi kuwa na Alvinic tena…”
“Kwanini? Daima hajawahi kukusahau. Au nii kwa sababu hupendi—”
“Inatosha,” Alvin alikatiza sentensi yake kwa sura ya kufoka, “Rodney, ninafurahi kwamba Sarah amerudi, lakini tayari nina mke”
“Acheni ubishi. Kurudi kwa Sarah ni tukio la furaha. Tunapaswa kusherehekea usiku wa leo,” Chester alisema.
Sarah aliinua kichwa na kusema. "Asante. Mnaweza kuondoka kwanza. Ninataka nipate muda wa utulivu pamoja na mjomba na shangazi yangu.” Wanaume watatu walitoka nje ya chumba.
Rodney alihisi kuongezeka kwa furaha kutoka ndani ya moyo wake. Ni Alvin na Chester pekee ndio walikuwa wamekunja uso kwa undani. Haikuwa wazi ni nini kilikuwa akilini mwao.
"Sikutarajia kamwe kuwa Sarah angekuwa bado yuko hai."
Baada ya muda, Chester akahema. "Kwa bahati mbaya, hakurudi kwa wakati. Inawezekana akamkosa Alvin."
“Shukrani kwa mtu huyu mwenye mawazo kigeugeu. Ikiwa ungesubiri nusu mwaka zaidi, ungekutana na Sarah tena.” Rodney alifoka.
Alvin aliwasha sigara yake huku akimpuuza Rodney.
•••
Saa mbili na nusu usiku, Sarah alifika kwa kuchelewa kwenye chumba cha faragha cha hoteli kilichoandaliwa kwa ajili ya mapokezi yake na kina Rodney. “Samahani kwa kuchelewa. Baada ya Maurine kuzikwa, mjomba na shangazi yangu walilia sana, hivyo ilibidi nikae nao muda mrefu nikiwaliwadha.”
'Ni sawa. Tunaelewa." Chester aliinua mkono wake. "Keti chini."
Wanaume watatu walikuwa wameketi mbalimbali na kila mmoja kwenye kochi refu. Chester alikaa katikati, ambapo Alvin na Rodney walikaa pande tofauti. Baada ya kusitasita kwa muda, Sarah alikaa karibu na Rodney.
"Sarah, kwa kuwa sisi watatu tuko hapa, unaweza kutuambia ilikuweje hadi leo tukuone ukiwa hai wakati tunajua ulikuwa umekufa?" Chester alimkazia macho. “Sisi ni marafiki zako. Tuliumia sana moyoni tulipojua kuwa umekufa. Je, huoni kwamba unapaswa kutupa maelezo?”
"Sarah aliinamisha macho yake. Akiwa katika hali ya hofu, alichukua glasi ya mvinyo mwekundu uliokuwa juu ya meza. Kisha, akalazimisha tabasamu lililojaa uchungu na woga. "Pengine mnafahamu kwamba tulitekwa nyara na Al-Shabaab nilipokuwa na rafiki yangu katika utafiti huko kwenye msitu wa Garisa baada ya kumaliza masomo yangu ya chuo kikuu nje ya nchi."
“Ndio. Alvin alitumia nusu mwaka kukutafuta huko. Baadaye, maiti iliyooza ilipatikana karibu na hifadhi ya msitu huo. Ilikuwa ni mwanamke, na sote tulidhani ni wewe,” Rodney alisema kwa huzuni.
Sarah alichezea glasi ya divai mkononi mwake. “Hapana, haikuwa mimi!”
Alvin, Chester, na Rodney walishangaa sana. Mkono wa Alvin ulitetemeka huku akishika glasi ya mvinyo. Akainua macho na kumtazama Sarah kwa mshtuko.
"Sitaeleza ilivyokuwa. Nimevumilia mateso mengi sana. Ilikuwa inauma sana kuishi kwenye kambi ya magaidi huko Somalia baada ya kutekwa.” Sarah alikunja midomo yake na kuinywa mvinyo. “Niliteswa tena na tena. Baada ya muda, nilifanikiwa kutoroka na kuzamia meli hadi ulaya. Nilifanikiwa kwenda Ujerumani ambako nilipata kazi ya kulea wazee kwenye kituo cha kukulelea wazee. Sikuwa na visa, kwa hivyo sikuweza kurudi. Nilijaribu kuwasiliana na familia ya Njau, lakini hawakunijali kabisa. Waliniambia moja kwa moja kwamba huku kila mtu anajua kuwa mimi ni marehemu hivyo nisijisumbue hata kurudi."
“Walienda mbali sana. Hawa watu ni binadamu kweli?” Rodney alitupa glasi ya mvinyo na kusimama kwa hasira.
"Nilifikiria kuhusu kuwasiliana na Alvinic, lakini ... sikustahili hata kuwa naye." Sarah akapepesa macho, machozi yakimtoka. “Yeye ni mwanamume mwenye mustakabali mzuri mbele yake, ilhali mimi tayari nilikuwa na mwili mchafu zaidi. Wale magaidi wa Al-Shabaab walikuwa wakitubaka kwa zamu kila siku. Hata usichana wangu niliokuwa nimemtunzia Alvinic ulitolewa kinyama na wale magaidi wasio na huruma. Nilitumaini angeweza kupata mwanamke bora baada ya mimi kuondoka kwenye maisha yake.”
Alvin alifumba macho. Moyo wake ulikuwa ukiwaka kwa maumivu. Hakuwazia mateso ambayo Sara alikuwa amepitia huku akihisi kwamba amekufa. Ikiwa angewahi kurudi kabla hajakutana na Lisa, angemuoa Sarah bila kusita. Sasa kwa kuwa Lisa alikuwa na ujauzito wa watoto wake, hisia zake kwake zilikuwa zimebadilika.
“Sawa, usilie.” Chester akamkabidhi Sarah kipande cha tishu.
Rodney alihisi kana kwamba kisu kilikuwa kikimpasua moyoni. “Usijali Sarah. Haijalishi umepitia unyanyasaji kiasi gani, hatutawahi kukudharau. Wewe ndiye mwanamke safi kila wakati mioyoni mwetu."
“Asante.” Sarah alitabasamu huku machozi yakimtoka. "Kwa kweli, kuna sababu nyingine iliyonifanya nirudi tena kwa wakati huu." Pamoja na hayo, aliwakabidhi kadi tatu za biashara.
Alvin alipigwa na butwaa baada ya kuona kadi ya biashara mkononi mwake. "Wewe ndiye mwanasaikolojia maarufu kimataifa, Dokta Nyasia?"
“Ni jambo la kustaajabisha kusema kwamba ninajulikana kimataifa. Baada ya kusema hivyo, mimi nina ujuzi kabisa katika kutibu aina hizi za kesi. Kituo cha wazee huko Munich Ujerumani ambacho nilikifanyia kazi kwa muda mrefu kilinigharamia masomo yangu ya ‘psychiatrist’ hadi ngazi ya PhD. Nilisomea Saikolojia ili kuwasaidia zaidi wazee wenye matatizo hayo.” Tabasamu tamu lilienea kwenye uso wa Sarah. Alinyoosha mkono wake kwake. "Bwana Kimaro, nimekuja kukusaidia."
Kwa hisia tofauti, Alvin alipeana naye mikono.
Rodney alisema, “Sarah, wewe ni mzuri. Ni kama Mungu alikuwa anakuandaa ili uje kumsaidia Alvin.”
“Sikutarajia angerudia tena hali yake,” Sarah alisema huku akitabasamu.
'Yote ni kwa sababu--"
"Kunywa pombe yako." Alvin alitumia glasi ya mvinyo kusimamisha mdomo wa Rodney.
Sarah alicheka kuona hali ile. “By the way, nataka kumtembelea Charity…”
“Kwanini unataka kumtembelea? Alikunyanyasa sana wakati huo.” Chester alikunja uso.
“Hasa. Hata alikuzuia usirudi. Utasema yeye ni ndugu yako kweli?”
"Pamoja na hayo, yeye ni dada yangu wa kambo. Zaidi ya hayo, sijui hukumu yake itakuwa ya muda gani wakati huu. Labda sitamwona tena. Natumai atajifunza kutokana na makosa yake.” Sarah alitoa kicheko cha uchungu.
•••
Siku inayofuata. Katika kituo cha Polisi, Charity alikaa kimya kwenye kona. Kulikuwa na michubuko mwili mzima na usoni. Hakuna sehemu hata moja ya mwili wake iliyoachwa bila kujeruhiwa.
Kundi la wahalifu wakatili walikuwa wakimtazama. Kama asingekuwa na ujuzi wa msingi wa karate, angekuwa tayari ameteswa hadi kufa.
"Charity, kuna mtu alikuja kukutembelea." Kelele ilisikika kutoka nje.
Charity alijitahidi kuinuka na kusimama. Hakuna mtu aliyekuja kumtembelea katika kipindi chote alichoswekwa ndani, hata wazazi wake. Ni wazi, mtu fulani alikuwa amezuia asitembelewe na watu. Kwa wakati huo ni nani angeweza kumtembelea?.
Sura ya: 271
Charity akatoka. Alipomtazama vizuri yule mwanamke, macho yalimtoka ghafla. "Sarah, bado uko hai?"
“Naam, niko hai. Nimerudi, Charity.” Macho ya Sarah yalimtiririka. “Hata hivyo, sikutarajia kwamba ungeishia hivi. Tsk, una harufu mbaya."
“Kwanini umerudi?” Charity alimtazama kwa hasira. Kila mara mwanamke huyu alipokuwa karibu, watu wa karibu na Charity walikuwa wakiishia kuumizwa tu. Charity alikuwa na hisia kwamba Mungu alikuwa ameondoa maisha ya Sara. Hakutarajia kwamba Sara alikuwa amerudi.
“Niko hapa ili kurudisha kila kitu changu kilichopotea,” Sarah alikunja midomo yake na kusema kwa furaha, “Kwa kuzingatia kwamba mama yako aliharibu familia yangu, unafikiri nifanye nini ili kumlipisha kisasi?”
“Unapanga kufanya nini?” Charity akamtazama. “Sarah, mama yangu hajawahi kukutesa. Alikutendea mema kuliko mimi.”
“Hiyo ni kwa sababu alikuwa anajaribu kumbembeleza baba yangu. Vinginevyo, ungewezaje kuchukua kampuni ya New Era Advertisings? Wewe na mama yako mmekuwa mkipanga na kula njama. Haha, kwa kuwa sasa baba amepoteza fahamu hospitalini baada ya kupata mshtuko wa moyo, Jennifer hana mtu wa kumtegemea. Nitamlipa pole pole kwa mateso yote ambayo mama yangu amevumilia. Nitayafanya maisha yake kuwa mabaya zaidi ya kuzimu.”
“Baba hakumtaliki mama yako. Alikuwa na tabia mbaya ya kuwatongoza wanaume wengine huko nje…”
“Nyamaza!” Sarah alikatiza sentensi yake ghafula kwa maneno makali, “Unawezaje kuthubutu kunijibu katika hali kama hii?”
"Sarah, ikiwa chochote kitatokea kwa mama yangu, utajuta kwanini uliamua kufufuka." Kwa macho mekundu ya damu, Charity alimtazama huku akiwa ameshika vyuma vya dirisha vilivyokuwa mbele yake.
“Haha, usijali. Nimefufuka ili nije kukushughulikia.” Akiwa amefunika mdomo wake, Sarah alicheka kwa dharau. “Kumbe nimesikia unaelewana na mke wa Alvin.” Wimbi la kufadhaika lilimkumba Charity. “Sasa nimerudi, ni wakati wake wa kupotea,” Sarah alisema kwa msisitizo na kukunja midomo yake.
"Endelea kuota. Alvin anampenda Lisa,” Charity alisema bila huruma, “Tayari wameoana. Huwezi kufananishwa naye.”
“Kweli? Lakini Alvin amekuwa akitumia muda na mimi kila siku. Hataki hata kurudi kwa anayeitwa mke wake. Unapaswa kujua kuwa uhusiano wangu na Alvin hauna mpinzani.”
Kwa hayo Sarah akageuka taratibu. “Kwaheri. Huenda hatutaweza kukutana tena katika siku zijazo kwa sababu utafia jela." Macho ya Charity yalifichua dokezo la kuchanganyikiwa.
Alipoona hali ya kutoamini usoni mwa Charity, Sarah alitabasamu na kusema, “Pengine hujui kwamba wakili anayewakilisha familia ya Langa wakati huu ni Bw. Shea. Chester Choka ndiye aliyechonga naye na kumwomba ahakikishe unafungwa milele.”
"Chester Choka?" Aliposikia jina hilo, Charity alihisi kana kwamba moyo wake ulikuwa unawaka moto. Hakukuwa na mtu katili zaidi kuliko mpenzi wake huyo wa kwanza.
“Kwa kuzingatia kwamba utafia jela, nitakuambia jambo fulani kwa hisani. Hapo awali, Chester alikubali kuwa na uhusiano na wewe sio kwa sababu alikuwa akikupenda. Alikuwa akinipenda mimi, na ilimbidi kuwa na wewe kwa sababu alitaka kuniumiza mimi kwa kumkatalia. Kwa hivyo ulipompanulia tu mapaja yako ukiwa na miaka 17, akaishia kukutolea usichana wako na kukuacha.”
Sarah aligundua kuwa macho meusi ya Charity yalikuwa yamelegea ghafla. Huku akijisikia fahari, aliondoa miguu yake iliyovalia viatu vya visigino virefu.
Mwili wa Charity ukateleza chini taratibu. Kisha akachuchumaa na kukaa chini. Ilimchukua muda mrefu kujinyanyua pale. Alichukia jinsi alivyokuwa mjinga wakati huo. Kwanini alimwangukia mtu ambaye alionekana kuwa mpole kwa nje lakini kwa kweli alikuwa mkatili sana?
Njia pekee ambayo angeweza kujilinda ilikuwa ni kuyapotezea maneno ya Sarah na kuvumilia. Matone makubwa ya machozi yalianguka sakafuni.
Chester Choka, Sarah Langa, Rodney Shangwe, Alvin Kimaro: Charity aliapa kwamba asingewasamehe hadi siku atakapokufa.
•••
Akiwa katika makazi ya familia ya Kimaro, Lisa alijihisi kama ndege wa kufugwa. Angeweza tu kuzunguka ndani ya uzio na hakuwa na mahali pengine pa kwenda. Ilikuwa imepita wiki moja tangu alipomuona mara ya mwisho Alvin.
Alijihesabu kuwa mwanaume huyo tayari amesahau kuhusu ujauzito wake. Alikuwa ameshuka moyo kabisa na kupoteza hata hamu ya kula. Jambo hili liliwatia wasiwasi sana Mzee Kimaro na Bibi Kimaro.
"Mpigie Alvin," Bibi Kimaro alimwagiza mfanyakazi wa nyumba wakati wa chakula cha jioni. “Hawezi kumpuuza mke wake na watoto hata awe na shughuli nyingi kiasi gani. Nilitaka walale vyumba tofauti lakini sikumuamuru amtupe mke wake kando.”
Mlinzi wa nyumba akapiga simu mara moja. "Bwana Kimaro alisema anafanya kazi za ziada ofisini kwake."
“Kwa hiyo hana hata muda wa kupumzika! Anafikiria nini?!" Mzee Kimaro alipiga ngumi kwenye meza.
"Tusimlaumu sana labda kweli amezidiwa na kazi, ukizingatia kwa sasa anashughulika pia na kampuni ya Lisa." Bibi Kimaro akamtupia jicho mzee huyo na kuonesha ishara kuelekea upande wa Lisa kwa kutumia kidevu chake.
Mzee Kimaro alikuwa na wasiwasi. Alvin alimfanya Lisa kuwa mke wake lakini sasa alikuwa amemtelekeza. Je, inawezekana kwamba alikuwa na mabadiliko yoyote kwenye moyo wake? Mzee huyo hakumpenda Lisa sana lakini hakuweza kujizuia kumuonea huruma mwanadada huyo ambaye sasa alionekana kuwa dhaifu na amechoka.
“Babu, Bibi, hakuna haja ya kumpigia simu. Tuligombana sisi wawili, kwa hiyo huenda hataki kuniona kwa sasa.” Lisa aliinua kichwa chake kwa utulivu. "Nimechoka sana kukaa ndani ya nyumba kila siku. Naweza kwenda nje kesho kumuona rafiki yangu?”
“Mh, sawa basi. Lakini unapaswa kuwa waangalifu. Aunty Yasmine atakwenda nawe,” Bibi Kimaro alisema bila kusita.
Hata hivyo, siku iliyofuata Lisa alipopanga kuondoka nyumbani, Shani alijaribu kumzuia. "Bibi mdogo, samahani lakini Bwana Kimaro ametoa amri kwamba hairuhusiwi kuondoka kwenye nyumba hii."
“Anapanga kunifungia milele?” Lisa alimtazama mlinzi wake kwa masikitiko. Mwanamume huyo angewezaje kumtendea unyama hivyo?
Maneno ya kinyonge yalienea kwenye uso wa Shani. “Najua unataka kwenda kortini kwa ajili ya kesi ya Charity Njau lakini hili litamkasirisha Bwana Kimaro…”
“Kwa hiyo siruhusiwi hata kumuona rafiki yangu kwa mara ya mwisho?” Lisa alipiga hatua chache kuelekea kwa Shani. "Mwambie kwamba ikiwa sitaondoka kwenye nyumba hii leo, nita ...." Kisha, akaonyesha ishara mbaya kwenye tumbo lake.
Shani alishtuka. "Bibi mdogo, tafadhali tulia."
“Siwezi kutulia. Mimi ni mwanamke mjamzito lakini ninaishi kama mfungwa. Nini kinampa haki ya kunifungia? Mimi ni binadamu! Ni afadhali nikate tamaa ya watoto ikiwa haya ndiyo maisha ninayopaswa kuvumilia milele.” Macho yake yalikuwa yakimtoka machozi, hata mikono yake ilikuwa inatetemeka muda huo.
Shani aliogopa sana kwamba Lisa alitishia kuwadhuru watoto, kwa hivyo alikubali upesi na kutabasamu kwa uchungu. “Hakika, tafadhali nenda. Nitampigia simu Bwana Kimaro baadaye.
Mara Lisa akapiga hatua kubwa kuelekea lango kuu. Alikuwa tayari anachelewa. Labda kupoteza sekunde nyingine kungemfanya akose kesi.......ITAENDELEA...
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
