JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP..........................0628924768
SEHEMU YA....................................264-265

Sura ya: 264

“Uchunguzi wa vinasaba?” Sauti ya Lina upande wa pili wa simu ilionyesha mshangao. “Ina maana Pamela amerudi Dar es Salaam?”
“Hata mimi nimeshangaa kwanini karudi Dar ghafla,” Linda aliongea kwa wasiwasi. “Isije kuwa anataka kurudiana na Patrick! Sitamwacha afanikiwe kwa hilo—”
“Linda, tutaongea zaidi baadaye,” Lina alimkatisha ghafla. “Kuna dharura imejitokeza ghafla.” Lina alikata simu na ghafla akahisi kuwa kichwa chake kinamuuma. Alikuwa amepoteza sehemu kubwa ya nywele wakati Lisa alipomvuta nywele hapo awali.
Moyo wa Lina ukadunda kwa hofu. Hapo hapo akapiga namba ya siri na kusema, “Rafiki wa Lisa Pamela alionekana kwenye idara ya uchunguzi wa DNA kwenye hospitali ya Golden Life huko Dar es Salaa. Nahisi Lisa ameshanishtukia.Atakuwa alinyofoa nywele zangu na kumpa rafiki yake akafanye uchunguzi wa ili kuhakikisha kama ni Lina.”
“Nitalishughulikia hilo kikamilifu.” Sauti ya ajabu kutoka kwenye simu ilisikika.
Lina aliingiwa na wasiwasi. “Sasa nifanyeje bosi? Ikiwa Alvin na genge lake watagundua kuwa mimi ni Maurine Langa feki, bila shaka wataniua."
“Usijali. Maadamu unatufanyia kazi, sitakuacha ufe.” Sauti hiyo ilimtoa wasiwasi.
•••
Lisa alizipokea zile nyaraka kutoka kwa Pamela kwa njia ya whatsapp na moja kwa moja akaenda maktaba kumtafuta Alvin. Alvin mara chache alienda ofisini kwa siku hizo na kwa kawaida alifanyia kazi zake katika chumba cha maktaba. Aliusukuma mlango na kuingia ndani.
Macho ya Alvin yalimtoka alipomuona. Aliona nia ajabu sana. Kwa siku kadhaa, Lisa hakuwa amejisumbua hata kumtafuta. “Umenimiss?
Lisa alikwenda moja kwa moja kwenye pointi. Aliwasha simu yake, na kumuonyesha kile cheti cha matokeo ya uchunguzi wa DNA.
Wakati Alvin alipoona ripoti ya uchunguzi wa DNA kati ya Jones Masawe na Maurine Langa, uso wake wote ukaganda. “Hiyo ina maana gani? Wao ni baba na binti?” Alipigwa na butwaa kidogo. Maurine alikuwa binamu wa Sarah Langa. Kwanini ghafla akawa binamu wa Lisa? "Hapana, Maurine Langa halisi hawezi kuwa binti wa Jones Msawe.” Alvin alibisha.
“Ni kwa sababu Maurine Langa wa sasa ni feki. Yeye ni Lina Jones baada ya kufanyiwa upasuaji wa plastiki.” Lisa alimwambia.
Alvin aliganda kabisa. Baada ya muda mrefu, alimtazama Lisa kwa macho tata. “Lisa, najua humpendi Maurine. lakini si vyema kumzushia jambo kubwa kama hili—”
“Hapana, siwezi kumzushia, huu ni ushahidi tosha.” Lisa alimshawishi Alvin. “Sikuwahi kufikiri hivyo hapo kabla. Nilishangaa Maurine alikuwa amenifahamu vipi mara ya kwanza nilipokutana naye, lakini sikufikiria sana jambo hilo wakati huo. Kisha, nilikwenda kwenye spa na Charity nikamwona Maurine pale. Charity alisema kuwa Maurine halisi alipata ajali alipokuwa mdogo ambayo ilimpa kovu kubwa chini ya shingo yake lakini hakuona kovu hilo kwenye shingo la Maurine huyu. Isitoshe, tabia yake ni tofauti kabisa na Maurine anayemjua yeye. Ndiyo maana nilivuta nywele zake pale hospitalini na kuzifanyia uchunguzi kwa kulinganisha na nywele za Jones Masawe. Imetokea kwamba wao ni baba na binti wa damu.”
Lisa alimtazama Alvin kwa umakini. “Je, hukumbuki kwamba Lina Jones alichukuliwa na watu wasiojulikana huko kijijini mlikompeleka?”
"Lakini nilimwomba Hans achunguze maisha ya zamani ya Maurine na hakupata chochote cha kutilia shaka..."
"Alichopata kinaweza kuwa cha juu juu tu. Je! unamfahamu Maurine Langa halisi? Unajua tabia yake? Unajua aliko?" Lisa aliendelea, “Fikiria kwa makini. Marafiki zako wanaendelea kusema kwamba kumbukumbu yako inazidi kuwa mbaya kwa sababu nilikukasirisha, lakini lazima ulihuzunika sana pia Sarah Langa alipokufa. Je, hili lilikutokea wakati ule? Tangu Maurine Langa alipoanza kukuhudumia, kwanini umekuwa ukisahau kumbukumbu zako?”
Uso wa Alvin ukawa mweupe kama karatasi. Kwa hakika, ilikuwa tangu Maurine aanze kumhudumia tu ndipo alianza kupata maumivu ya kichwa mara kwa mara na alipata shida ya kumbukumbu.

"Nina uhakika 100% kuwa yeye ni Lina Jones. Kusudi lake ni nini kwa kutokea ghafla karibu nawe? Je, alikuongezea chochote kwenye maziwa na dawa ambazo huwa anakuandalia? Umewahi kufikiria kuhusu hilo?” Macho ya Lisa yalikuwa na huzuni. "Unadungwa dripu na kunywa dawa kila siku, na ulikuwa na uwezo wa kupata nafuu hapo awali. Mbona zimekuwa bure sasa?”
Alvin alikosa la kusema. Pia alianza kuamini maneno yake.
"Unaweza kumwambia mtu kumshika Maurine mara moja na kumpeleka kwa uchunguzi wa uzazi? Nina uhakika kwamba yeye ni Lina Jones.” Lisa alikumbusha kwa dhati, “Chukua hatua sasa kabla hawajashtukia. Pia, aliyemtorosha Lina ndiye aliyepanga haya yote. Mtu aliye nyuma ya Lina lazima awe na nia mbaya na wewe!”
“Ndiyo.” Mara Alvin akampigia simu Hans. "Mteke Maurine Langa mara moja. Ninataka kupata ripoti ya uchunguzi wa uzazi kuhusu Maurine na Alex Langa Njau ndani ya saa 24."
Lisa alihisi kufarijika kidogo. Mwishowe, bado hakuamini kwamba ripoti hiyo haikuwa ya kweli, lakini ilimbidi aithibitishe yeye binafsi kabla ya kuwa na uhakika. Hata hivyo, haikujalisha. Alichosema aliamini kuwa ni kweli.
•••
Saa nane za usiku, Alvin ghafla alipokea simu kutoka kwa Hans. “Bwana Mkubwa, kuna habari mbaya. Maurine Langa amekufa.”
"Nini kimetokea?" Alvin alikaa ghafla.
"Nilimfungia ndani ya nyumba moja nje kidogo ya jiji. Usiku wa manane, walinzi walimfumania mtu akijaribu kumwokoa Maurine na kuanza kumkimbiza, lakini waliporudi, walikuta walinzi wengine wawili wakiwa wamepoteza fahamu na nyumba inawaka moto. Maurine aliteketea na moto hadi kufa.” Hans alisema kwa huzuni, “Nadhani hawakuwa watu waliojaribu kumwokoa Maurine. Walikuwa wakitaka kumteketeza.”
“Nakuja sasa hivi.” Alvin akakata simu na kuliendesha kwa haraka hadi eneo lilipotokea tukio hilo.
Aliposhuka kwenye gari, alimuona Rodney akiwa amesimama mbele ya begi lenye mabaki ya mwili wa Maurine. Macho yake yalikuwa mekundu, alipomuona Alvin, alimkimbilia ili kumpiga ngumi.
"Tulia." Alvin akaishika ngumi yake.
“Nitawezaje kuwa mtulivu? Kwanini umemfungia Maurine? Amekufa. Umemuua!” Rodney alimlalamikia. “Najua hawezi kufananishwa na Lisa Jones, lakini bado ni binamu wa Sarah. Yeye ni msichana asiye na hatia."
"Huenda asiwe Maurine Langa," Alvin alisema kwa upole.
Rodney alicheka kwa hasira. “Mimi si kipofu. Ni nusu tu ya uso wake ulichomwa moto. Bado niliweza kumtambua.”
"Lisa alimfanyia uchunguzi wa uzazi. Yeye ni Lina Jones, lakini alifanyiwa upasuaji wa plastiki ili kufanana na Maurine.” Alvin alikunja uso. "Nilimteka ili kujua aliyepanga haya yote ni nani."
“Unasema nini?” Rodney alionyesha kuwa na mashaka.
“Kwanini nikudanganye?” Alvin alipomaliza kuzungumza, ghafla Hans aliingia na kuzungumza, “Bwana Mkubwa, idara ya uchunguzi imetoka na matokeo. Ripoti inaonyesha kuwa Maurine na Alex Langa wana uhusiano wa damu.”
"Alvin Kimaro, wewe b*stard!" Rodney alimpiga kweli ngumi ya uso safari hii.
Alvin alirudi hatua chache nyuma na kushindwa kurejesha usawa wake. Uso wake wote ulikuwa na huzuni. "Una uhakika hakuna kosa lolote?" Alvin alipigwa na butwaa.

Sura ya: 265

“Ni hospitali ya Dokta Choka, kwa hivyo hawezi kuwa amekosea. Baadaye, daktari wa uchunguzi atachukua mwili kwa ajili ya uchunguzi . Itafahamika kama alikuwa amefanyiwa upasuaji wa plastiki au la.”
“Sawa.” Alvin akasugua kichwa chake. "Tafuta ni nani aliyetuma watu hapa jana usiku."
“Kuna nini cha kuchunguza tena? Ni wazi Lisa Jones ndiye aliyefanya haya. Bado unamsikiliza yule mwanamke?!” Rodney alipiga kelele kwa huzuni, “Yule mwanamke ni mkatili sana! Maurine hakuwahi kamwe kufikiria kukutongoza, lakini Lisa bado alijaribu kumuua Maurine kwa kila njia na hatimaye amefaulu.”
"Lisa sio mtu wa aina hiyo." Alvin alikanusha. "Lazima alidanganywa."
"Hata kama alidanganywa, ni kwa sababu ya mawazo yake finyu. Ni mjinga sana huyo mwanamke”
"Rodney Shangwe, umemaliza?" Alvin alishindwa kuvumilia tena.
“Hapana, sijamaliza. Nimemvumilia muda wote huu kwa sababu ni mkeo, sasa sitaweza kumvumilia tena.” Rodney alifoka.
“Acheni kugombana!” Chester alishuka kwenye gari na kusikia sauti zao za ugomvi.
“Sijali. Sitaacha jambo hili lipite hivi hivi. Hata kama Alvin atachagua kumlinda mke wake, sitamsamehe kamwe.” Rodney aligeuka na kuondoka baada ya onyo hilo.
"Nini mwazo yako, ?" Chester alienda kwa Alvin.
"Lisa anamwonea wivu Maurine, lakini sidhani kama angekuwa mkatili kiasi hiki." Alvin akasugua kichwa chake. “Kama Charity Njau asingesema kwamba Maurine huyu ni feki, Lisa asingemshuku…”
“Charity Njau.” Chester alikunja uso. "Ni yeye tena." Baada ya kutulia, alisema kwa upole, “Afadhali awe hana uhusiano na hili. La sivyo, nitahakikisha kwamba ameozea jela.”
Mchana, matokeo ya uchunguzi wa maiti yalitumwa kwa Alvin.
"Bwana Kimaro, mtu aliyeteketea kwenye eneo la tukio imebainishwa kuwa ni Maurine Langa. Wazazi wake pia wamefanyiwa ulinganisho kamili wa vinasaba na kuthibitisha hilo.”
Hans alipomaliza kuongea, alimuona Alvin akiwa ameshika kichwa chake kwa mikono yote miwili huku mwili ukimtetemeka kwa maumivu.
“Bwana Kimaro…”
“Wazazi wa Maurine wanasemaje?” Alvin alivumilia maumivu na kuuliza kwa sauti ya kuchoka.
“Walikuwa wakilia bila kukoma. Unafikiri wangewezaje kupokea taarifa kama hizo? Wanataka haki itendeke.” Hans alipumua.
"Lifanyie kazi hilo."
“Kuna jambo moja zaidi.” Hans aliongeza. “Aliyewahadaa walinzi jana usiku na aliyewasha moto wamenaswa. Wana…wanahusiana na Charity Njau. Ni watu ambao wamekuwa wakifanya kazi na Charity nyuma ya pazia.”
“Charity Njau, kwa hivyo alikuwa ni yeye…” Alvin aligonga meza kwa ukali na kusimama, uso wake mzuri ukiwa umejawa na hasira ya kutisha.
"Rodney aliwapigia polisi na wamepeleka maafisa wao kwa familia ya Njau kumkamata." Hans alisema.
“Waambie polisi wampe mwanamke huyo adhabu nzito zaidi. Sitaki aachiliwe maisha yake yote.” Alvin aliuma meno yake na kuamuru neno baada ya neno
“Imeeleweka.”

•••
Katika makazi ya familia ya Njau, hakuna aliyekuwa anajua kilichokuwa kikiendelea. Boris Langa Njau, Baba wa Charity alikuwa akifanya kazi zake sebuleni kwa utulivu wote huku mkewe, Jennifer Musyoka, akiketi kimya jikoni akimtengenezea chai.
Charity akatoka akiwa amevalia mavazi ya ofisini, alikutanisha macho yake na baba yake aliyekuwa ametulia sebuleni.
"Charity, unaenda ofisini?" Bwana Langa alimwona na kumpungia mkono binti yake kipenzi.
“Baba.” Charity akatembea kuelekea kwake. “Hali ya kampuni si nzuri kwa sasa—”
“Usijali. Usiwaze sana kuhusu hilo. Ikiwa familia ya Kimaro inataka kweli kutufilisi, basi hatuwezi kuwazuia.” Boris alimtazama na kusema kwa utulivu, "Ikiwa kampuni itanyanyuka, basi itanyanyuka tu. Ikibidi tutaiuza tu na kuanzisha kampuni ya mambo mengine. Haijalishi hata kama tutalazimika kuhama jiji la Nairobi, mradi tu familia yetu ya watu watatu iwe na furaha. Wakati fulani, ninapomwona msichana kama wewe akifanya kazi kwa bidii sana kiasi kwamba hapati hata wakati wa kupumzika, mimi na mama yako huumia moyo sana.”
Jennifer aliitikia kwa kichwa na kusema kwa sauti ya upole, “Baba yako na mimi tumezeeka. Hatujali ni pesa ngapi unapata. Cha muhimu ni kuwa uko salama na mwenye furaha.”

"Asanteni." Moyo wa Charity ukapata faraja. “Nitajaribu kwa mara nyingine kumbembeleza Alvin. Ikiwa nitashindwa kupata nafasi kwenye mtandao wake, basi nitaiuza kampuni. Baada ya hapo, familia yetu inaweza kuondoka Nairobi…”
Alipomaliza tu kuzungumza, kundi kubwa la polisi liliingia ghafla. “Bi. Njau, polisi wamepata ushahidi wa kuhusika kwako katika kesi ya mauaji. Uko chini ya ulinzi.” Afisa mmoja akamfunga pingu mara moja.
Charity alipigwa na butwaa. “Kesi gani ya mauaji? Sijui unazungumzia nini.”
“Maurine Langa amekufa. Uliwaambia Shaka na Solo wamchome moto. Tayari wamekiri hilo kwenye maelezo yao polisi.”
Akili ya Charity ikaganda ghafla. "Hiyo haiwezekani. Shaka na Solo ni watu wangu sawa, lakini sikuwahi kuwaambia wafanye hivyo.”
"Hakuna mhalifu anayekubaligi kosa lake, lakini tayari tuna uthibitisho wa uhakika." Bila kusema neno jingine, afisa huyo alimsukuma Charity nje ya mlango.
"Hiyo haiwezekani. Binti yangu hajawahi kuua mtu kamwe!” Boris Njau alikimbia na kumvuta polisi huyo.
Mwanaume huyo alimsukumiwa mbali. "Sio tu kwamba binti yako aliua mtu, lakini pia ana rekodi mbaya za kihalifu. Ataozea jela maisha yake yote.”
Boris alianguka chini. Mwili wake wote ukakamaa na kuzimia kwa mshtuko mara moja.
“Mpenzi amka!” Jennifer alichanganyikiwa na kupiga simu kwa haraka kuita ambulance kwa hofu.
Familia ya Njau ilikuwa ikiporomoka. Watumishi walitazama kwa macho yao wenyewe wakati familia ya Njau, ambayo ilikuwa juu kwa miaka kadhaa, ikitoweka kama moshi.
Moyo wa Lisa haukutulia. Ulikuwa ukitetemeka kwa siku mbili mfululizo. Alikuwa amepata ushahidi kwamba Maurine Langa alikuwa ni Lina, kwa hiyo lazima Alvin angekuwa anachunguza jambo hilo. Lakini tangu alipozipata taarifa hizo, hakuwa amerudi nyumbani na hakuweza kumpata kwenye simu pia. Zaidi ya hayo, hakuweza kuipata hata simu ya Charity pia. Hisia ya hofu na wasiwasi ilizidi kuwa na nguvu moyoni mwake.
Wakati huo, Pamela alimpigia simu. “Jamani, nitakufa kwa hasira! Kwa kweli Rodney Shangwe alimwambia meneja mkuu wa Osher anifukuze kazi. Yeye ni mwendawazimu kabisa. Kichwa chake lazima kimejaa mavi tu!"
"Nini kimetokea? Si ulitia saini mkataba?”
Ndio, nilitia saini mkataba wa miaka mitano lakini wamenifukuza bila maelezo yoyote wala kunilipa fidia yoyote, na hata wameniweka kwenye orodha ya blacklist, sitaweza kuajiriwa na kampuni yoyote nchini Kenya… sijui nilifanya kosa gani.” Pamela aliongea kwa masikitiko.
Lisa alishtuka. Halikuwa tatizo kubwa kwa Pamela kufukuzwa kazi, lakini kumworodhesha kwenye blacklist hakika ilikuwa ni kumwangamiza. Rodney Shangwe alikuwa na chuki gani kubwa na Pamela hadia kaamua kumfanyia hivyo?
“Usijali. Nitamuuliza Alvin kuhusu hali hiyo,” Lisa alisema kwa wasiwasi.”Si wazo zuri kukuajiri kwenye kampuni yangu, lakini ikibidi nitafanya hivyo, usiwaze sana.”
“Sawa. Je, umeweza kuwasiliana na Charity hivi karibunii? Nilitaka kumpigia nipate kinywaji naye lakini sikuweza kumpata.” Pamela alisema kwa sauti ya huzuni.
“Hujaweza kumpata pia? Hata mimi nimejaribu kumtafuta sijampata”
"Ndio, kunaweza kuwa na kitu kimemtokea?" Pamela aliuliza kwa jazba.
"Nenda kwa familia ya Njau na ujaribu kuulizia." Lisa alizidi kuwa na wasiwasi
Pamela alifukuzwa kazi na kuwekwa kwenye blacklist, na simu ya Charity haikuweza kupatikana. Nini kilikuwa kinaendelea?.....ITAENDELEA.....

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA