JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP..........................0628924768
SEHEMU YA................................262-263
Sura ya: 262
Valerie alimchukia Lisa. Aliamini yote ni sababu yake kwamba Alvin alimuondoa kwenye wadhifa wa mkurugenzi wa kitengo cha Bima cha kampuni ya KIM International baada ya kushika wadhifa wa kuongoza kampuni tena, na kumfanya adharaulike na kuwa mtu asiye na maana. Moyo ulimuuma kwa chuki kila alipokuwa akimfikiria Lisa Jones.
“Aunty, kwanini nisiwe hapa? Mimi ni mke wa Alvin.” Lisa aliinua uso na kutabasamu.
“Koma, usiniite ‘Aunty’! Hufai. Unanitia kichefuchefu tu.” Valerie alifadhaika.
“Ndio hivyo, wewe ni binti wa haramu. Hatukutambui hata kidogo.” Queen naye alimdharau.
“Usiniudhi,” Lisa alisema kwa sauti ya chini, bila ya kutishika hata kidogo.
Valerie alicheka kwa hilo. “Kwa hiyo nikikuudhi itakuwaje? Vipi ikiwa nitakupiga kabisa?" Aliinua mkono wake wakati akisema, lakini Queen haraka akamshika. “Mama, Bibi…”
Valerie alisimama na kugeuka kutazama, na kumwona Bibi Kimaro akitembea kuelekea kwao. Alikuwa mbali sana, kwa hiyo Valerie hakujali hata kidogo. "Kwa hivyo ikiwa bibi yako anakuja? Hata yeye pia hampendi b*tch huyu asiye na haya.” Alitupa mkono wake chini alipomaliza kuzungumza, lakini Lisa aliushika. Valerie alimtikisa kwa nguvu, na Lisa akarudi nyuma hatua chache.
Bibi Kimaro, ambaye hakuwa mbali sasa, alipatwa na hofu. "Mtoto wangu mpendwa, uko sawa?" Bibi Kimaro alikuwa na wasiwasi na haraka akakimbia.
Valerie alitabasamu. “Mama, sijambo…”
Kabla hajamaliza, Bibi Kimaro alimshika mkono Lisa kwa wasiwasi huku akiwa anahofia kwamba Lisa angedhurika kwa kuguswa na Varelia.
“Bibi, wewe...” Queenie alifungua mdomo kwa kutoamini kile kilichokuwa kikitokea mbele ya macho yake. Bibi Kimaro kweli alimuita Lisa 'mtoto wake kipenzi'. Ni kweli au alikuwa anaota?
“Bibi, sijambo.” Uso wa Lisa ulionekana kukunjamana vibaya huku akigusa tumbo lake. "Lakini nina wasiwasi kwamba sitaweza kujifungua salama ikiwa nitaendelea kuishi hapa."
“Una mimba?” Valerie alipigwa na butwaa.
"Nyamaza!" Bibi Kimaro alimkazia macho kwa hasira. “Unaltaka kuleta shida tena hata nyumbani8? Nimezaaje binti asiyefaa kama wewe? Jambo lolote likitokea kwa vitukuu wangu wa thamani, sitakusamehe kamwe.”
Valerie alikanyaga miguu yake kwa hasira. "Mama, mimba yake inaweza kuwa feki. Nani amedhibitisha kuwa ni kweli ana mimba? Pia alikuwa na mpenzi hapo awali. Huenda mtoto hata asiwe wa Alvin.”
Lisa ghafla alimtazama kwa macho ya hasira. “Aunty, samahani, si wewe unayelala na mimi. Alvin si mjinga kiasi cha kutojua kama ujauzito ni wake ama si wake. Lakini sikuelewi kabisa. Mimi ni mgeni tu niliyekuja Nairobi na hakuna baya nililokufanyia, lakini wewe una chuki ngumu dhidi yangu sijui kwanini. Mara ya kwanza, kwa makusudi ulitafuta mtu wa kunipeleka kwenye chemchemi ya maji moto ambayo Willie Kimaro alikuwa akizama ndani yake kwa lengo la kunitengenezea kashfa ili sifa yangu iharibike. Mara ya pili, hata umeniharibu sura yangu. Tayari nimekusamehe, lakini wewe bado unanichukia tu. Nimewahi kukufanyia nini?”
Bibi Kimaro alishtuka. Haishangazi Lisa alipotea mara ya kwanza alipoenda kwenye makazi hayo. Wakati huo, hata alikuwa amemlaumu Lisa kwa kukimbia, lakini hakujua kwamba yote yalikuwa njama ya Valerie.
"Valerie, umekuwa mbaya sana na hutaki kukubali makosa yako." Bibi Kimaro alikatishwa sana tamaa na yeye.
“Mama usisahau kuwa ni kosa lake Alvin kuniondoa kwenye nafasi yangu ya ukurugenzi na kunifanya nidharaulike. Hapo awali, nilikuwa nikiheshimiwa, lakini sasa, kila mtu ananiona lofa, hata Nina hanijali tena,” Valerie alilalamika.
"Alvin alikufukuza katika nafasi yako kwa sababu huna sifa." Bibi Kimaro alikatishwa tamaa kabisa na watoto wake baada ya Alvin kumfunulia ukweli mara ya mwisho. "Hata unamruhusu Nina Mahewa kukusaidia kughushi kazi zako. Ikiwa angekuacha uendelee kufanya kazi, ungeharibu tu kampuni.”
"Mama, unamtetea tu kwa sababu ni mjamzito." Macho ya Valerie yalikuwa mekundu kwa hasira.
Bibi Kimaro akatikisa kichwa. “Inatosha, huna hata aibu. Unachojua ni kukosea tu lakini si kujutia makosa yako. Sio tu kwamba haukubali makosa yako, lakini bado una nia ya kumdhuru Lisa. Ninaweza kusema kuwa moyo wako ni mbaya. Kosa langu ni kukudekeza tangu utoto. Sasa kwa kuwa Lisa atakuwa analea ujauzito wake hapa, huruhusiwi kuja hapa bila idhini yangu kuanzia leo.”
Valerie alipigwa na butwaa. "Mama, hapa ni nyumbani kwetu..."
Queenie pia aliingiwa na wasiwasi. “Bibi, msamehe mama. Hakukusudia—”
“Babu yako na mimi tumezeeka. Tunataka tu kuishi maisha ya amani, si vurugu kila siku. Hatuwezi kuvumilia tena tabia zenu mbaya. Queenie, kama na wewe una tabia za mama yako, basi si utaondoka naye.”
Bibi Kimaro alikuwa amechoka sana. Alipunga mkono na kuwaambia walinzi kuwatoa nje.
“Bibi, samahani...” Lisa alionekana kuomba msamaha.
“Usiombe msamaha. Niliona wazi kuwa yeye ndiye alikuwa anakuchokoza. Ni kweli kwamba sikupendi kiasi hicho, lakini bado ninaweza kutofautisha kati ya mema na mabaya.” Bibi Kimaro alinyooka sana.
Lisa hakuhisi kukasirika. Kinyume chake, tabia ya bibi huyo ilimfanya ahisi raha zaidi.
“Ikiwa mtu yeyote atakunyanyasa, niambie tu. Wewe pia ni mke wa Alvin. Katika siku zijazo, utakuwa msimamizi wa familia hii kwa hiyo unastahili kuishi kama kwako.”
Lisa aliganda. Kwa hiyo Bibi Kimaro alikuwa amekubali? Hata hivyo, bado haikujulikana ikiwa Alvin na yeye wangeweza kutembea hadi mwisho kutokana na jinsi walivyokuwa wakati huo.
Bibi Kimaro alipomuona amenyamaza, alimtazama usoni na kupata utulivu moyoni. Kisha akageuka na kuondoka na mfanyakazi wa nyumbani.
•••
Jioni, Lisa alimpigia simu Pamela. "Iliendaje?"
"Usijali, Dar es Salaam ni jiji la familia ya Masanja. Ni mchezo wa kitoto kupata nywele za Jones kutoka jela,” Pamela alisema, “Tayari nimewaambia watu wangu wafanye haraka. Tutapata matokeo baada ya siku mbili.”
“Basi nitakuachia jambo hili.”
“Haya, sisi kimsingi ni ndugu, usiwe na wasiwasi . Afadhali uwatunze mapacha wangu. Nataka kuwa godmother wao.”
"Ndio, hakika utakuwa godmother wao. Hutaweza kuepuka hili.” Lisa alikata simu na kuiweka pembeni wakati mlango wa chumba ulipofunguliwa ghafla. Alvin akiwa amevalia vazi la bluu bahari aliingia huku akiwa ameshikilia vitabu vichache. "Nani anataka kuwa godmother wa mapacha wangu? Pamela au Charity?"
Sauti ya ghafla na mwonekano wa Alvin uliufanya mwili wa Lisa kuruka kwa hofu. “Alvin, umeingiaje humu? Si bibi alikuambia ulale jirani? Kwanini unakuja kwenye chumba changu?"
"Nimezoea kulala na wewe." Alvin kama kawaida alinyanyua blanketi na kuketi kitandani.
Lisa alichukia sana. Hata hivyo, ilionekana kwamba popote alipokaa, hakuna kitu kingeweza kumzuia asije kumtafuta. “Ondoka mara moja, au nitamwambia Bibi…”
Sura ya: 263
“Jaribu. Bibi ameshazima simu yake saa hii ili alale." Alvin kwa nguvu alimnyanyua, na mkono wake wa kushoto ukapapasa tumbo lake. "Acha nione ikiwa watoto wetu wawili wamekua kidogo leo."
"Wana mwezi mmoja tu sasa. Hakutakuwa na mabadiliko yoyote." Lisa aliusukumia mkono wake mbali bila kujali. “Ondoka. Nataka kulala."
“Hujajibu swali langu.” Alvin alimkazia macho. "Nani anataka kuwa godmother wa watoto wangu? Ikiwa ni Pamela Masanja, sikubaliani kwa sababu IQ yake inatia wasiwasi. Ikiwa ni Charity Njau, sikubaliani zaidi…”
“Alvin, daktari alisema natakiwa kupumzika kwa muda mrefu, mbona unakuja katikati ya usiku ili kunisumbua, huwapendi watoto wako?” Lisa alikasirika na kumpiga na mto. “Watoto ni wangu. Ni uamuzi wangu juu ya nani atakuwa godmother wao. Usipoacha kunisumbua, sitawazaa.”
"Umesema nini?" Uso wa Alvin ukakunjamana ghafla. "Lisa Jones, fikiria kabla ya kuzungumza. Usifikiri kwamba watoto hawataelewa unachosema kwa sababu tu wamo tumboni sasa. Umefikiria juu ya hisia zao?"
Lisa alikuwa mjamzito, kwa hiyo hisia zake zilifadhaika kwa urahisi. Kwa maudhi machache tu, macho yake yakawa mekundu kwa manung'uniko. “Wewe ndio umenitia hasira. Nakwambia ukitaka turudiane lazima ukubali marafiki zangu pia.”
Alvin aliingiwa na hofu alipoanza kulia. “Sawa, usilie basi.”
Lisa hakulia tu, bali machozi pia yalimtoka kwa wingi na kupiga kelele zaidi. “Zaidi ya hayo, unathubutuje kuwadharau marafiki zangu?! Je, Rodney Shangwe ni bora kiasi hicho? Nadhani yeye ni mjinga kuliko nguruwe. Kuhusu Chester Choka, yeye ni mchafu kuliko mbwa. Wote ni bure.”
Alvin ghafla alipigwa na butwaa kwa lawama zake. Kimantiki, alipaswa kukasirika kwasababu alikuwa akiwadhihaki marafiki zake. Hata hivyo, alipoona machozi yake, moyo wake ulimuuma kana kwamba unayeyuka kutokana na maumivu. “Usilie. Kulia si vizuri kwa watoto walio tumboni.”
“Wacha nilie tu kwa sababu unanikera sana. Nataka nipumzike lakini unanisumbua tu.” Lisa alishindwa kabisa kujizuia. Maumivu aliyokuwa akiyavumilia moyoni yalimtoka ghafla.
Hata Shangazi Zara, ambaye alikuwa akimilinda Alvin katika mlango wa chumba kidogo cha jirani, alishtushwa na kelele hizo na akaingia ndani mara moja.
"Bwana Kimaro, umeingiaje?" Zara mara moja alimkaripia Alvin. “Bibi Kimaro aliniambia nikuchunge mlangoni kwako. Mke wako sasa anapitia kipindi muhimu, kwa hiyo hamwezi kulala pamoja. Kwanini umeingilia dirishani na kuja kumsumbua? Fanya haraka utoke nje.”
Ilikuwa sawa kama angekuwa mtumishi wa kawaida tu, lakini Shangazi Zara alikuwa na bibi huyo mzee kwa makumi ya miaka. Ingawa Alvin hakuthubutu kumbishia chochote, lakini bado alijisikia huzuni sana.
"Nilikuja tu kuwasimulia watoto hadithi." Alvin alijitetea kijinga.
Lisa aliyapapasa macho yake na kubanwa na hasira. “Ulikuja…? Usitake kunikasirisha zaidi. Ondoka!”
"Bwana Kimaro, tafadhali ondoka haraka." Shangazi Zara akamtoa nje kwa haraka.
Mpaka kila mtu alipoondoka ndipo Lisa aliachia machozi yake taratibu, lakini moyo wake ulikuwa bado umekasirika. Alipoamka siku iliyofuata, alikuwa na uvimbe mwepesi chini ya macho yake.
Wakati wa kifungua kinywa, wazee wale wawili waligundua kuhusu tukio la jana yake usiku na Mzee Kimaro alishindwa kujizuia papo hapo. “Unawapenda kweli watoto wako? Una umri gani sasa? Huna akili hata kidogo!”
Bibi Kimaro naye alikasirika. "Kibaraza kitafungwa kuanzia leo. Usimruhusu apate nafasi ya kuingia chumbani kwa mjamzito tena mpuuzi huyu asiye na nidhamu!”
Alvin, ambaye uso wake uliangukia kwenye karipio lao, aliupapasa kwa mguu wake mguu wa Lisa kwa upole. “Mpenzi…”
Lisa alitazama pembeni na kumpuuza kabisa.
•••
Siku mbili baadaye huko Dar es Salaam, Pamela alipokea simu kutoka hospitali alikopeleka nywele za Maurine na Jones kwa uchunguzi, na mara moja akakimbia kuelekea huko. Pamela akaipata ripoti hiyo haraka na kuona maneno makubwa 'positive match' juu yake. Mara moja alimlaani Lina Jones na mababu zake wote.
Alipiga namba ya Lisa, akisema, "Ulikuwa sahihi! Maurine Langa kweli ni binti wa damu wa Jones. Yeye ni Lina Jones."
Lisa alipapasa paji la uso wake. Kwa kweli hakutaka matokeo yawe ya kweli. Hata hivyo, katika hali ya ugonjwa wa Alvin ulivyozidi kuwa mbaya na dawa na maziwa ambayo Maurine alikuwa akimpa Alvin kila siku… Je, hiyo ilikuwa dawa ya kawaida? Ghafla alishtuka.
“Nitachukua picha na kukutumia. Fanya haraka ukamwambie Alvin.” Pamela alimwambia na kukata simu.
“Pamela Masanja, ni wewe!” Mara Pamela akashtuliwa ghafla baada ya kukata simu, uso wa Linda Sheba uliyajaza macho yake. Alionekana mwenye furaha sana kumuona Pamela.
Linda alienda pale hospitali kumpeleka Patrick Jackson, ambaye tangu apigwe kibuti na Pamela huko Nairobi aligeuka kuwa mlevi wa kupindukia hivyo alikuwa akisumbuliwa na afya mbovu.
Hata hivyo, Pamela alitaka kutapika damu mara tu alipomuona Patrick. Alirudi tu Dar es Salaam kwa siku chache lakini akaishia kukutana na mtu aliyemchukia zaidi.
Linda alikunja uso ghafla na kuuliza. "Pamela, kwanini umerudi Dar es Salaam? Nilisikia kwamba umepata mpenzi mpya huko Nairobi. Ungewezaje kumfanyia hivi Patrick?”
“Hilo halikuhusu. Hebu nipishe niondoke zangu.” Sauti ya Pamela ilikuwa imejaa papara.
Macho ya Linda yalikuwa mekundu kwa kuzidiwa huzuni. “Samahani! Naomba msamaha kwa niaba yake, anateseka sana Patrick, hana hata hamu ya kula siku hizi, kutwa anakunywa pombe tu ili kujisahaulisha mawazo yako. Hata ufanisi wake wa kazi umepungua sana. Nashukuru sana kukuona hapa vinginevyo nilipanga kukufuata Nairobi ili kumuombea msamaha!”
Patrick alionekana mnyonge sana. Umbo lake refu sasa lilikuwa limeinama kidogo, na uso wake wa kupendeza sasa ulionekana kupauka kama kipande cha muhogo. Macho yake yalikuwa yamepoa kama mtu aliyekosa matumaini ya kuishi. Alionekana kujichokea kabisa.
Pamela aliweza kuhisi mara moja kuwa Patrick hakuwa vizuri. Moyo wake ulijikaza, lakini alishusha haraka wasiwasi moyoni mwake. Tayari walikuwa wameachana. Haikuwa ikimhusu tena hata kama alikuwa hajisikii vizuri. Zaidi ya hayo, ilikuwa bado ni kama zamani. Iwe alikuwa anaumwa au la, ishu ni kwamba, Linda alikuwa kando yake.
Patrick alimtazama moja kwa moja. Pamela alikuwa amejipodoa kidogo tu lakini uso wake ulikuwa bado mzuri. Patrick hakuwahi kuacha kumfikiria tangu walipoachana. Mara nyingi hakuweza kudhibiti hisia zake zilizomuumiza moyo. Hapo awali alikuwa hapendi kunywa pombe, lakini sasa marafiki zake walipomtaka aende kujumuika nao, hakuweza kuwakatalia.Mara alianza kuumwa kwa sababu alikunywa pombe kupita kiasi na hakuzingatia kula, na hatimaye aliishia kuumiza tumbo lake.
Linda alimuona Patrick akimkazia macho Pamela naye akauzuia wivu moyoni mwake kabla ya kulazimisha tabasamu. “Pamela kwanini usirudishe moyowakokwa Patrick? Ulikuwa karibu mara ya mwisho ku…
Alikuwa karibu mara ya mwisho kufanya nini? Pamela alikunja uso. Maneno hayo yalionekana kuwa na maana iliyofichwa. Alikuwa karibu mara ya mwisho kuolewa naye, ama?
Hata hivyo, tayari alishakata tamaa na Patrick Jackson na hakuwa na mpango wa kwenda sambamba na mawazo ya Linda.
"Una fikra mbaya. Hatuna tena chochote cha kufanya kati yetu. Niko bize, kwa hiyo nitaondoka sasa hivi.” Pamela akawaacha na kuondoka.
Patrick alihisi maumivu ya moyo wake yakizidi kuwa makali, karibu kuufanya mwili wake utetemeke kwa uchungu. Hapo awali, Pamela alikuwa na wasiwasi mwingi juu yake. Kila alipohisi kuumwa hata kidogo, Pamela angemhudumia hadiapone. Angekaa naye usiku kucha ili tu kumhudumia. Sasa, hakutoa hata neno la kufariji.
"Patrick, twende." Linda alimshika Patrick na kumuongoza kwenye idara ya vipimo.
Baada ya Patrick kuingia kwenye chumba cha daktari, Linda alibaki akimsubiri nje kwenye mabenchi ya kupumzikia. Aliyakumbuka vizuri maongezi aliyomfumania Pamela akiongea na Lisa. Alichukua simu yake na kupiga namba za Lina. “Lina, otea nimemwona nani hospitali sasa hivi?”
“Nani?”
“Pamela Masanja, alikuwa kwenye ofisi za uchunguzi wa vinasaba. Kama sikumsikia vibaya alimtajia Lisa jina lako huku akisema kwamba matokea yameonyesha kufafana kwako na Jones Masawe. Ina maana Lisa alikuwa haamini kama wewe ni mtoto wa Jones?”.....ITAENDELEA....
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA
