JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP..........................0628924768
SEHEMU YA................................258-259

Sura ya: 258

"Lisa, usielewe vibaya." Alvin alimsukuma Maurine bila fahamu. “Aliuona mkono wangu ukivuja damu, kwa hiyo—”
“Sawa, lakini muuguzi si yuko hapa? Ina uhusiano gani naye?" Lisa alimkatisha kwa hasira. “Kwa kuwa huwezi kuvumilia kumuacha kiasi hiki, mbona bado unanisumbua? Unaona raha nikishuhudia mahaba yenu?”
Uso mzuri wa Alvin mara moja ukageuka kuwa mbaya kama mzimu. Haikujulikana ikiwa ni kwa sababu alikuwa amepoteza damu nyingi au kwa sababu alichomwa na maneno ya Lisa.
Maurine alieleza kwa haraka, “Bibi Mdogo, Maneno ya Bwana Kimaro yote ni ya kweli. Angalia mkono wake, bado unavuja damu…”
“Funga mdomo wako.” Lisa alimfokea. “Maurine Langa, nimekuvumilia kwa muda mrefu sana. Unafikiri mimi ni boya siyo?” Ghafla alikimbia na kushika nywele ndefu za Maurine na kuzivuta kwa nguvu, kisha akamchapa makofi kwenye mashavu yote mawili.
“Ahhhh! Bibi mdogo, usinipige! Bwana Kimaro, nisaidie!” Maurine alilia na kuhangaika huku akiburutwa pembeni na Lisa.
“Lisa, tulia. Mwache aende zake." Alvin alikimbia kumvuta Lisa.
Hata hivyo, Lisa alikataa kuachia nywele za Maurine, na kumfanya mwanamke huyo apige kelele kubwa kwa maumivu.
"Lisa Jones, unapibu kifo?" Rodney, aliyeingia ghafla aliona tukio hili na mara moja akamwangusha Lisa chini. Alikuwa na nguvu nyingi, hivyo Lisa alijibamiza chini na kuumia vibaya.
Maumivu yale yalisababisha mwili wake kuhisi kusambaratika. Hata hivyo, suala kubwa zaidi ni kwamba alihisi kitu kikimtoka sehemu za siri. Ghafla, muuguzi alimnyooshea kidole na kupiga kelele, “Unavuja damu!”
Lisa alitazama chini na kuona damu ikichuruzika kutoka chini alipokuwa amekaa. Aliigusa kwa mkono wake. Bado kulikuwa na mchuruziko mwingi. Akili yake ilimtoka.
Alvin alimnyanyua kwa woga. “Muite daktari haraka!” Alipiga kelele na kukimbilia chumba cha dharura huku akiwa amembeba Lisa. Kwa haraka daktari akampeleka Lisa kwa uchunguzi wa mwili.
Mlango ulipofungwa, Alvin alikuwa akisubiri nje kwa hamu. Maurine alikuja huku akilia. “Bwana Kimaro, samahani. Yote ni makosa yangu. Bibi Mdogo kanielewa vibaya tena.”
Alvin alimtazama kwa macho yaliyojaa hasira. Mwanzoni, aliamua tu kumwacha Maurine lakini hakuridhika naye. Wakati huo, hata hivyo, hisia kali za chuki zilimpanda alipokumbuka kuona Lisa akivuja damu.
“Si nilikuambia uondoke? Nani alikuambia uje?”
Rodney alisimama mbele ya Maurine. “Maurine alikuja tu kukutembelea kwa nia njema. Lisa Jones ndiye aliyempiga bila sababu yoyote.”
“Ni mke wangu. Hukupaswa kumsukuma.” Kifua cha Alvin kilijawa na hasira kali.
Rodney alikasirika. “Nilimsukuma tu, kwani nilijua kama angeanguka? Labda ni kipindi chake cha kuingia mwezini. Usifadhaike kwa hilo.”
"Afadhali uombe jambo baya lisimfike." Alvin hakuweza kuhangaika kuzungumza naye upuuzi kwa kuhofia kukasirishwa. Hata hivyo, pia alitumaini kwamba Lisa alikuwa tu kwenye kipindi chake.
Nusu saa baadaye, daktari alitoka na Alvin akamfuata. "Daktari, vipi hali yake?"
“Bwana Kimaro, ujauzito aliobeba mke wako umetikisika na mwili wa mkeo unaonyesha dalili za kuharibika kwa mimba. Inabidi abaki hospitalini ili kuzuia hali hiyo.”
“Ana mimba?” Alvin aliganda mwili mzima.
“Ndiyo, ni zaidi ya mwezi mmoja. Ni mapacha wa kufanana.”
“Mapacha wa kufanana?” Mwili wa Alvin ukazidi kutetemeka kwa mshtuko.
“Ndiyo, mapacha, lakini ni kwa sababu ni mapacha ndiyo maana hata ameweza kuathirika kwa urahisi,” daktari alisema kwa hasira, “Ninyi ni watu wazima mnahitaji kuwa makini zaidi. Ikiwa ajali hii ingetokea nje ya hospitalini leo na asingepata matibabu kwa wakati, basi vitoto vingekuwa vimepotea. Ikiwa kuharibika kwa mimba kwake kunaweza kuzuiwa au la itategemea jinsi mambo yanavyoendelea baadaye.”
“Asante daktari.” Alvin ghafla alihisi kupasuka kwa hofu.

Yeye na Lisa walikuwa tayari kupata mtoto pamoja, lakini hakuna kitu kilichotokea kati yao tangu Maurine atokee. Zaidi ya hayo, daktari huko Dar es Salaam pia alikuwa amesema kwamba ingekuwa vigumu kwake kupata mimba kutokana na hali ya mwili wake, kwa hiyo hakuwahi kufikiria sana jambo hilo. Lakini, alikuwa amebeba watoto wake sasa. Walikuwa mapacha. Jambo la kusikitisha ni kwamba watoto wangeweza kupotea. Alihisi kama ameanguka kutoka mbinguni hadi duniani.
"Rodney Shangwe!" Alvin alimpiga Rodney ngumi ya uso kwa hasira.
“Ningejuaje kuwa ana mimba?” Rodney pia alikasirika kidogo lakini alikataa kukiri kosa lake. "Lilikuwa kosa lake kutogundua kuwa ana mimba na kuzunguka na kuwapiga watu wengine kama mwanamke mwendawazimu. Ni kosa lake mwenyewe!”
“Ondoka nje!” Alvin alimpiga teke kali. "Chukua Maurine wako mpotee! Nakuonya usije tena hospitali kuniona, sawa?”
Baada ya yote, walikuwa marafiki kwa miaka mingi. Hakutaka wafukuzwe hospitalini.
“Sawa, hatutakuja tena. Maurine wende zetu.” Rodney alimvuta Maurine na kuondoka.
Maurine aliinamisha kichwa chake huku sura ya kero ikimulika machoni mwake. Hakutarajia Lisa kuwa mjamzito, na mapacha pia. Kwanini alikuwa na bahati sana? Watoto hao hawakupaswa kuruhusiwa kuwepo!
Lisa aliposukumwa nje ya chumba cha dharura, bado alikuwa amechanganyikiwa. Alipataje mimba? Alikuwa hata amebeba mapacha. Kama ingekuwa zamani, angekuwa na furaha, lakini sasa… alikuwa na hisia tofauti moyoni mwake. Baada ya yote, walikuwa mwili na damu yake mwenyewe—watoto wake. Alipenda na kutaka, lakini hii ingemfanya ashikwe zaidi na Alvin.
“Lisa, usijali. Watoto wetu wataokolewa.” Uso wa Alvin uliokuwa umefadhaika mara moja ukatokea mbele yake. Wakati huo, uso wake ulikuwa umejaa furaha. “Unashangaza sana. Ni mara ya kwanza na unanipa mapacha. Mtoto, wewe nikupendeje8?"
“Unaweza kuondoka? Naudhika kwa kukutazama tu.” Lisa alijisikia vibaya na alikuwa mwepesi wa kukasirika.
“Siwezi. Wewe ni mama wa watoto wangu, kwa hiyo ni lazima nikutunze vizuri.” Alvin hakuwa na hasira hata kidogo. “Nesi, tafadhali mlete kwenye wodi yangu. Nitamtunza mwenyewe.”
“Sitaki.” Lisa alimkazia macho. "Isipokuwa unataka kunikasirisha hadi kuharibika kwa mimba."
Daktari hakuweza kujizuia kumkumbusha, “Bwana Kimaro, hupaswi kuwasumbua wanawake wajawazito. Jambo muhimu kwa sasa ni kumwacha awe mtulivu. Kuwa mwenye busara na makini na na zingatia lishe yake. Mwache alee vijitoto kwa amani ya akili.”
“Sawa, basi muweke kwenye wodi iliyo karibu na yangu. Siwezi kuvumilia kuwa mbali na yeye.” Alvin aliwaza na kuongea.
Lisa hakutaka chochote zaidi ya kukaa mbali naye kadiri awezavyo, lakini kila mtu hospitalini alimsikiliza kwa utiifu Alvin, hivyo upesi akapangiwa wodi namba 6 VIP.
Aunty Yasmine naye alipangwa kumhudumia. "Bibi mdogo, hongera! Mimi ni mzuri katika kupika vyakula vyenye lishe. Nitahakikisha unajifungua watoto wawili wenye afya njema, Bi.Kimaro.”
"Lo, ni bora ikiwa ni mvulana na msichana, lakini hata wasichana wawili itakuwa poa tu." Alvin alitabasamu kwa furaha. "Napenda mabinti zaidi. Lakini wote ni sawa, watoto ni watoto tu!"
"Hahah, pamoja na sura zenu zilivyo za kuvutia, haijalishi kama ni wavulana au wasichana, wataonekana wazuri sana," Aunty Yasmine aliunga mkono.
"Ndio, nafikiri hivyo pia." Akiwasikiliza wakizungumza, Lisa alishindwa kuvumilia na kusema, “Alvin Kimaro, unaweza kutoka? Si unatakiwa kuwekewa dripu ya IV?”

Sura ya: 259

Alvin alikwenda kitandani na kumtazama kwa macho ya upole. “Lisa, kwa kweli hakuna kinachoendelea kati yangu na Maurine. Yule nesi aliyenichoma sindano hiyo alisababisha mkono wangu utokwe na damu, na Maurine akamsukuma nesi alipoona damu ikivuja kwa wingi. Ndio maana ulikiona ulichokiona hapo awali. Usikasirike. Wewe ni mama sasa."
Lisa alicheka. Alikuwa akimlaumu kwa kuwa na akili ndogo hata baada ya kuwa mama. Alikuwa akimtwika lawama sasa. “Shangazi Yasmine, unaweza kuniletea simu yangu?” Hakutaka kuzungumza naye.
Aunty Yasmine akamkabidhi simu. Lisa alituma ujumbe kwa Pamela na kuanza kucheza mchezo bila kumwangalia Alvin hata kidogo. Alvin alikaa kwa muda hadi alipotolewa na daktari kwenda chumba cha pili kuwekewa dripu ya IV.
Hans aliingia na rundo la nyaraka, lakini Alvin akazifyagilia mbali. “Siko katika hali ya kusoma hizi sasa. Nenda uninunulie vitabu vya mwongozo wa kulea wanawake wajawazito.”
Hans alikuwa anaumwa na kichwa sasa. "Hapana, hati hizi ni za muhimu sana -"
"Ni za muhimu zaidi kuliko watoto wangu?" Macho ya Alvin yalikuwa makali.
Hans hakuwa na lakusema tena.
Mchana, Pamela aliingia na kumuona Lisa akinywa uji wa lishe akiwa amelala kwenye kitanda cha hospitali. Alipumua, akisema, "Inaonekana hautaweza kutoroka kamwe kwenye mikono ya Alvin Kimaro maishani mwako."
Lisa alihisi kuchanganyikiwa. Pia alikuwa amelifikiria tatizo hili. Hakuweza kufikiria kuwatoa watoto hao, lakini ikiwa angewazaz, bila shaka angenaswa na Alvin. Familia ya Kimaro isingeruhusu damu yao ipotee nje, na ilikuwa vigumu zaidi kwake kuwaacha watoto baada ya kuwazaa.
“Tusilizungumzie hilo. Njoo hapa nikuambie kitu." Lisa alimpungia mkono. Pamela akaenda, na Lisa akaweka mkono mfukoni mwa Pamela.
Pamela akaingiza mkono mfukoni kwa kuchanganyikiwa. "Unanipa bahasha ya nini?"
Lisa akamvuta karibu na kusema kwa sauti ya chini, “Nywele za Maurine Langa zimo ndani ya bahasha hiyo. Nenda omba likizo na urudi Dar es Salaam na nywele hizi. Chukua nywele za Jones Masawe na Salome Masawe kutoka gerezani ili kufanya kipimo cha DNA. Kumbuka kuiweka siri. Hakuna anayetakiwa kujua kuhusu jambo hili. Unatakiwa kuwa makini.”
Kila mtu alifikiri kwamba alikuwa ameshika nywele za Maurine kwa sababu alikuwa na wivu na hasira, lakini sababu yake halisi ilikuwa kupata nywele za Maurine. Ilibidi awe na kisingizio halali. Vinginevyo, Maurine angekuwa na shaka.
Macho ya Pamela yalimtoka. “Hilo haliwezekani…”
“Inawezekana sana. Lina hajulikani alipo, na Maurine huyu ananipa hisia ninazozifahamu sana,” Lisa alisema, “Ikiwa Maurine Langa ni Lina Jones, lazima kuwe na nguvu zinazomuunga mkono. Mtu aliye nyuma yake lazima awe anamlenga Alvin. Hili si jambo ambalo tunaweza kulishughulikia kwa nguvu za kikatili.”
“Si ungemwambia Alvin?” Pamela akabanwa na mate.
“Ataniamini? Halafu Alvin si mtulivu, hata kama tanaiamin anaweza kulishughulikia kwa papara”
Pamela akanyamaza kimya. Alvin kweli angeweza asimwamini. "Kwa hali hiyo, nitarudi Dar es Salaam kesho saa sita mchana."
Muda si mrefu baada ya kuondoka, Hans aliingia na baadhi ya nyaraka huku akiwa na tabasamu usoni mwake. Baada ya yote, Lisa alikuwa na ujauzito wa watoto wa Alvin, hivyo nafasi yake ingeimarika zaidi na Mawenzi ingekuwa na maisha mazuri ya baadaye. Alijua alikuwa akimtumikia mtu sahihi.
"Bi. Jones, Meneja Mkuu alinipa hizi nyaraka na kusema kwamba itabidi uzichunguze wewe binafsi."
Lisa alichukua nyaraka hizo wakati Alvin alipoingia ghafla. Uso wake ulisinyaa alipoziona zile nyaraka. “Daktari alisema kwamba hawezi kufanya kazi sasa. Ni nani aliyekuruhusu kuleta vitu hivi ili kumsumbua wakati amebeba watoto wangu?”
Hans alikasirika kidogo na Lisa hakufurahishwa. “Unasemaje? Kwa hiyo nisisimamie kampuni kwa sababu tu nimelbeba watoto wako? Siwezi kukaa na kumtegemea mwanamume ambaye anaweza kuanzisha uhusiano usio na utata na mwanamke mwingine wakati wowote. Ninaweza hata kutupwa ghafla siku moja na kuachwa bila chochote.”
Kichwa cha Alvin kilikufa ganzi. “Sitaweza—”

“Hutaweza? Tulipooana mara ya kwanza uliniambia wazi kwamba sitapata hata senti moja tukiachana.” Lisa alicheka.
Hans alishtuka na kumtazama kwa siri Alvin. Alifikiri kwamba Alvin alikuwa mpenzi wa ajabu tu, lakini kumbe ni mjinga mtakatifu pia! Aligundua kuwa alikuwa mbaya zaidi kuliko alivyomfikiria. Alikuwa mtu tajiri zaidi nchini lakini hivyo ndivyo alivyosema kwa mke wake wa ndoa?
Alvin alihisi dharau ya Lisa kwake na sura yake ikaingia simanzi mara moja. Akatoa pochi yake kwenye mfuko wake wa nyuma na kumrushia. “Sawa, nitakupa pesa zangu zote kuanzia sasa, sawa?”
"Hapana Asante. Kuna wanaume wachache tu ambao huweka pesa zao kwenye pochi siku hizi. Wengi wao huhifadhi pesa zao kwenye miradi” Lisa hata hakumtazama.
Alvin hakuweza kushindana naye, ikabidi tu kumwambia Hans, "Nipe hati hizo, nitazishughulikia.”
Hans alijikongoja aliposikia maneno hayo. Ilimshangaza na kumchekesha. Alvin alisema hakuwa na muda wa kushughulika na masuala ya kampuni yake, hata hivyo alikuwa na muda wote wa kuingilia masuala ya kampuni nyingine. Alvin alichukua zile nyaraka na kutafuta sehemu kwenye sofa ili kuzisoma kwa makini.
Shangazi Yasmine aliingia akiwa na matunda na kushangaa. “Bwana Kimaro, umemaliza kuchukua dripu ya IV? Kwa kawaida huchukua angalau saa nne.”
Hans alisema kwa unyonge, "Bwana Kimaro alitumia sindano kubwa zaidi na kuimaliza kwa saa mbili tu ili aje kukaa na Bi. Mdogo."
Shangazi Yasmine alipigwa na butwaa.
Lisa kimya kimya alitazama kasi ya dripu yake ya IV. Sindano yake ilikuwa ndogo tu, lakini maumivu yake yalikuwa hayawezi kuvumilika. Ikiwa angetumia sindano kubwa zaidi, maumivu yake yangekuweje? Hakupata picha!
Kutokana na hali ya kutisha ya Alvin, kila mtu alitoka wodini kimyakimya kumkwepa.
Dakika kumi baadaye, Lisa aliusogeza mwili wake na kujiandaa kutoka kitandani. Mara Alvin akanyanyuka. “Usinyanyuke. Daktari alisema unapaswa kukaa kitandani."
"Naenda kujisaidia." Lisa alifoka. "Daktari hakunizuia kwenda chooni."
“Usijali. Nitakubeba kama unataka kwenda.” Alvin hakuzungumza zaidi na kumnyanyua. Alimuweka chini kwenye choo na kumvua gauni lake kwa nguvu.
Uso mzima wa Lisa ulikakamaa kwa hasira. “Ondoka, nataka nibaki peke yangu.”
“Daktari alisema tunapaswa kukuhudumia kwa uangalifu…”
“Samahani, lakini siwezi kujisaidia ukiwa karibu.”
“Kuwa mpole. Wataalamu wanasema kwamba mwanamke anapokuwa mjamzito, baba mtarajiwa anapaswa kumtunza mke wake na kumfariji. Nikikuacha peke yako, hakika utakuwa na mawazo yasiyofaa.” Alvin alimbembeleza kwa upole na subira.
"Inatosha. Sitafanya kitu kama hicho.”
"Wataalamu wanasema kwamba wanawake hawamaanishi wanachosema."
Lisa alikuwa karibu kufa kutokana na maneno yake ya ajabu. Ni aina gani ya wataalamu wa kijinga walikuwa wakimshauri? "Simama nje au sitaweza kujisaidia." Alvin alitoka nje na kusubiri mlangoni.
Lisa alipoinuka, aligundua kuwa pedi ilikuwa imechafuka sana na alihitaji kubadilisha, lakini pedi mpya zote zilikuwa nje. Aliuma mdomo na kumwambia Alvin aliyekuwa nje kwa sauti ya chini, “Alvin, nisaidie pedi. Au unaweza kumwambia Aunty Yasmine aniletee.”
"Hakuna haja."Alvin akafungua droo na kuchukua pedi. Alifungua moja na kuisoma kwa muda. Haraka akagundua njia sahihi ya kuitumia.
Baada ya kufungua mlango, Lisa alitoa mkono wake nje.
"Simama. Nitakuwekea,” Alvin alisema, “Hutakiwi kuinama. Watoto walioko tumboni wataumia."
“Jamani, ina maana nisiiname kisa ujauzito?” Lisa alihisi mateso sasa.....ITAENDELEA....

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.