JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP..........................0628924768
SEHEMU YA................................256-257
Sura ya: 256
Alvin aliibana miguu yake na kuguna kabla ya kumfuata ghorofani. Alipofika ghorofani, alimkuta Lisa akijiandaa kwenda kuoga. Alifungua kabati na kugundua nguo nyingi za kiume na hata chupi za kiume ndani.
Kichwa chake kilikuwa na maumivu kutokana na hasira. "Alvin, ni nani aliyekuruhusu kuweka nguo zako hapa?!"
''Sikuwa na nguo za kubadili tangu nimehamia hapa. Kwa hiyo niliamua kuleta chache." Alvin alisimama nyuma yake na kusema kama jambo la kweli.
Lisa alichukua nguo zake akitaka kuzitupa chini. Hapo hapo, Alvin alisema bila kujali, “Unaweza kuzitupa nje kabisa. Nitamwomba Hans alete nguo mpya kesho.”
Lisa ilibidi kujisalimisha kwa tabia yake isiyo na aibu. "Sawa, ninakubali kukuruhusu ukae hapa. Lakini utakaa kwenye chumba cha wageni."
"Hapana." Alvin akapepesa macho yake meusi. “Sababu ya mimi kuhamia hapa ni kulala chumba kimoja na wewe. Kwanini unataka nihamie kwenye chumba kingine? Mimi si mjinga.”
Lisa alizidi kuchanganyikiwa. Yeye ndiye aliyevamia nyumba yake, lakini alikuwa akijifanya kana kwamba ndiye mmiliki wa nyumba hiyo. Lisa aliogopa kwamba angekufa kwa hasira ikiwa angendelea kuzungumza naye, kwa hiyo akaenda kuoga.
Alipotoka kuoga alimuona Alvin akiwa ameshika mop. Alikuwa anasafisha sebule ya kulia chakula. Mwendo wake ulikuwa wa kusuasua kiasi kwamba ilionekana kana kwamba alikuwa ameshika mop kwa mara ya kwanza.
Lisa alificha mkanganyiko aliokuwa nao moyoni. Aligeuka na kuweka nguo kwenye mashine ya kufulia kwenye chumba cha kufulia. Alipomaliza, alimuona Alvin akiwa anadeki sebuleni sasa.
Dakika kumi baadaye, Lisa alishuka kwenda kuchukua mtindi kutoka kwenye friji. Aliporudi alimwona Alvin akisafisha tena sebule ya kulia chakula.
Lisa alikunja uso. "Inatosha. Unataka kubandua sakafu? Sio lazima uendelee kudeki sehemu ya kulia chakula mara zote hizo.”
"Ni saa ngapi nilideki sebule ya kulia?" Alvin alizuia huzuni yake na kusema, "Bado sijasafisha chumba cha kulia chakula."
"Alvin, acha kujifanya hujui unachokifanya!" Lisa alikosa la kusema.
“Nimesema nini kibaya?” Alvin alionekana kuwa na huzuni.
Lisa hakumwelewa kabisa Alvin, alikuwa anajaribu kumuigizia makusudi au alikuwa na tatizo? Lisa alitulia na kujaribu sana kumchunguza kwa makini. Ilionekana kana kwamba hakuwa anajifanya. Wakati huo, alikumbuka alipomuuliza kuhusu Lina hapo awali. Hakuweza hata kukumbuka alichomfanya hapo awali. Pia alishangazwa na kuumwa kwake na kichwa na kuzimia, mbona hakuwa na dalili hizo hapo awali? Moyo wake uliruka mapigo.
"Sawa, chukulia sijasema chochote." Lisa aligeuka na kwenda juu. Hata alifunga mlango kwa makusudi.
Haikupita hata nusu saa, Alvin alifungua mlango kwa urahisi na kuingia ndani. Lisa ambaye alikuwa amevua nguo zake zote alikuwa anajipaka mafuta. Aliposikia kelele za mlango kufunguliwa, alipiga kelele na kuvuta nguo zake mara moja. Hata hivyo, hakuweza kuchukua nguo kwa wakati kwa kuwa alikuwa amechanganyikiwa sana. Maeneo makubwa ya mwili wake bado yalikuwa wazi.
Alvin mwanzoni hakuwa na mawazo yoyote, lakini kuona Lisa alivyokuwa amenona maeneo fulani ilimfanya ahisi joto.
"Kwanini umefunika huko?" Alvin alienda mbele na kumshika bega lake lililokuwa wazi kwa mkono mmoja huku akiitoa mikono yake iliyofumika chini ya kitovu kwa mkono mwingine.
Lisa, ambaye hatimaye alifanikiwa kujizungushia shuka maeneo yake nyeti, aliona macho ya Alvin yakianza kuwaka kwa uchu wa kingono. Alikuwa na aibu na hasira. "Alvin, umeingiaje chumbani kwangu wakati niliufunga kwa funguo?"
“Hii…” Alvin akamuonyesha ufunguo mkononi mwake. "Huu ni ufunguo ambao unaweza kufungua kila kitu."
Lisa alikuwa karibu kuzimia. Kitu cha aina hiyo kweli kilikuwepo! Lisa alitaka kumpokonya, lakini Alvin alikuwa na kasi zaidi na haraka akawahi kuuweka mbali. Hakuweza kuwahi kasi yake na akaanguka kifuani mwake.
"Njoo tulale." Alvin akamkumbatia.
Lisa alijitahidi kutoka kwenye kumbatio lake lakini alishindwa. Bila kufikiria, alimuuma sana begani.
Alvin hakuhisi maumivu yoyote na akamtazama tu kama kawaida. “Endelea kuuma. Hukuwahi kunaimbia kuwa kumng’ata mtu ni ishara ya upendo? Uking’ata sana ndivyo unavyonipenda sana.”
Lisa karibu azibe mdomo kwa mshangao. Hiyo ilikuwa zamani sana, lakini bado aliikumbuka. Sasa kwanini muda mfupi uliopita alikuwa akipoteza kumbukumbu?
“Mbona hauumi tena? Unaogopa kuniumiza?” Alvin aligusa masikio yake kama mtoto wa paka, sauti yake ilikuwa nyororo yenye nguvu ya sumaku. "Ni sawa, we ng’ata tu, siogopi maumivu."
Lisa alikuwa ameshuka moyo kabisa sasa. Ikiwa angemng'ata, ilikuwa ishara ya mapenzi, lakini ikiwa asingemng’ata, basi ilimaanisha kuwa aliogopa kumuumiza. Alikuwa mwathirika wa ule usemi wa ‘ukinipiga umenionea, ukiniacha umeniogopa!’ Hakukuwa na jinsi angeweza kushinda dhidi yake.
"Twende tukalale." Alvin alimkumbatia na kuzima taa kabla ya kulala. Muda si mrefu alilala baada ya kupumbazwa na harufu yake nzuri.
Lakini, Lisa hakuweza kulala. Alikuwa anapata njaa kutokana na mawazo. Alikula sana wakati wa chakula cha jioni na Charity, lakini alikuwa na njaa tena kabla haijafika hata saa tano usiku. Ni lini hamu yake ya kula iliongezeka kiasi hicho?
Siku inayofuata, Lisa alipozinduka, tayari ilikuwa saa tatu asubuhi. Ilikuwa ni mara ya kwanza kuamka akiwa amechelewa sana. Alishuka haraka haraka, Alvin aliyekuwa amekaa kwenye sofa akisoma gazeti, mara akainuka. "Nimekuandalia kiamsha kinywa, kwa hivyo-"
"Alvin Kimaro, ulizima kengele yangu?" Lisa alimkatisha kwa hasira.
"Kengele yako ililia kwa muda mrefu lakini ulikuwa bado umelala kama nguruwe mdogo, kwa hivyo niliizima."
"Hiyo haiwezekani. Kawaida mimi huamka kwa sauti ndogo tu.” Lisa alishtuka, akakataa kukubali kwamba alikuwa amelala sana.
Macho yake yalikuwa yamemtoka pande zote, na nywele zake zilikuwa zimechanganyikana alipoamka tu.
Alvin alicheka tu. “Nilijua kwamba ungenilaumu Kwa bahati nzuri, nilirekodi video kama uthibitisho.”
Alicheza video hiyo. Kwenye skrini, Lisa alikuwa amelala fofofo juu ya mkono wake huku kengele ikilia kwa nguvu. Alikunja uso tu na kuvuta blanketi kabla ya kuendelea kulala.
Kama asingeona hiyo kwa macho yake mwenyewe, asingejua kuwa alilala hivyo. Hata alitumia mkono wake kama mto. Ilikuwaje, mbona hakuwa na mazoea ya kulala sana?
“Kuwa mvumilivu. Kifungua kinywa kiko kwenye jiko. Kitakuwa tayari muda si mrefu.” Alvin aliutazama uso wake uliopooza na kutabasamu. Kisha, akaenda jikoni kupika.
Hapo awali Lisa alitaka kusema 'Sitaki kula', lakini tumbo lake liliguna ghafla, hivyo hakuweza kusema maneno hayo. Hata hivyo, yeye ndiye aliyempikia kabla. Ilikuwa wakati wake wa kumlipa.
Dakika tatu baadaye, bakuli la tambi lilitolewa. Lisa alionja na kupata ladha isiyo ya kawaida. “Hukuweka chumvi?”
"Hiyo haiwezekani. Nakumbuka niliweka.” Alvin alionja na kugundua kuwa kweli hakuweka chumvi.
"Leta chumvi.” Lisa akaamuru.
Alvin alinyanyuka kufuata chumvi. Lisa alimtazama akitembea kuelekea sehemu tofauti kabisa. “Subiri, chumvi iko jikoni. Kwanini unaenda chooni?”
Alvin aliduwaa kana kwamba ameamka kutoka kwenye ndoto na kubadili njia kuelekea jikoni.
Nyuma yake, uso wa Lisa uliongezeka kuwa na mshangao zaidi. Alikuwa akiigiza kama bibi yake ambaye alipata shida ya akili, lakini Alvin alikuwa bado mdogo sana…
Ghafla, kengele ya mlango ililia. Alifungua geti na Hans akaingia kwa haraka huku akiwa amekunja sura nzito. “Bibi mdogo, nilipata mtu wa kuchunguza jambo hilo jana usiku. Lina Jones alitoroka miezi michache iliyopita.”
Sura ya: 257
Kama ilivyotarajiwa… Lisa alikuwa na uhakika zaidi wa jibu moyoni mwake sasa.
Hata hivyo, uso wa Alvin ukabadilika kwa hasira. “Mjinga wewe! Ungewezaje kumruhusu atoroke hata baada ya kumpeleka kwenye kijiji hicho cha mbali kabisa?”
Hans alikasirika lakini akajizuia. "Mzee huyo alisema kuwa kuna gari lilimchukua alipokuwa akimkimbiza."
“Ni vigumu kuamini kwamba Lina Jones bado ana marafiki wowote. Nenda ukafuatilie gari hilo,” Alvin aliamuru kwa ukali.
“Sawa.” Hans alinyamaza na hakuweza kujizuia kuuliza, “Bibi mdogo, uliniuliza ghafla nimchunguze Lina Jones jana. Je! unafahamu kitu chochote?"
Alvin naye alimtazama Lisa kwa kuchanganyikiwa.
“Siwezi kukuambia sasa hivi.” Lisa alitazama pembeni. Alvin pengine asingemwamini kama angesema kwamba Maurine Langa anaweza kuwa Lina Jones. Angeweza hata kumlaumu kwa kutumia mbinu chafu kumpakazia Maurine.
"Niambie. Sipendi unaponificha mambo.” Alvin alimvuta begani kwa ubabe.
Lisa alikosa la kusema. “Basi kwanini hukufikiria jinsi nilivyohisi ulipoweka Maurine Langa kama muuguzi wako huku ukinificha ukweli?”
Alvin akafunga breki ya mdomo kuhusu hilo, akageuza mada. "Kula. Tambi kabla hazijapoa.” Hakuthubutu kuuliza chochote zaidi kwani aliogopa kumchukiza.
Lisa aliinama tena kuendelea kula kifungua kinywa chake. Lakini alipoonja tu tena akahisi kukasirika. "Alvin, chumvi yangu iko wapi?"
“Hii hapa.” Alvin akamkabidhi ile chumvi huku akionyesha mbwembwe.
Hans alikosa la kusema kabisa baada ya kutazama tukio hilo. Hakutarajia kamwe kama Alvin alikuwa ni mtu wa utani kiasi hicho.
Jina lake la WhatsApp pia lilikuwa limebadilishwa na kuwa jina la utani kama 'Ni Wako Pekee', na kufanya kila mtu afikiri kwamba akaunti yake ilikuwa imedukuliwa.
“Enhee! Hans, si ulisema kuna mkataba wa ugavi nilipaswa kusaini jana? Umekuja nayo leo?" Alvin aliuliza ghafla.
Hans alishangaa. “Bwana Mkubwa, tayari ulitia saini jana, hukumbuki?”
Alvin alikunja uso na kutaka kukumbuka zaidi, lakini kichwa kilimuuma tena na uso ukawa umekunjamana kwa maumivu.
“Bwana Kimaro, twende hospitali. Unahitaji dripu ya IV." Hans alimtazama Lisa kwa kumsihi. “Bibi mdogo, unaweza kumpeleka? Gari langu liliharibika na nilichukua teksi kuja hapa. Bibi Mdogo, Bwana Mkubwa anahitaji kupata dripu ya IV kila siku. Lazima aende.”
Lisa alikosa la kusema. Hakuwa tayari kabisa kuamini hilo. Ilikuwaje Alvin akawa mgonjwa sana?
"Ngoja nimalize mlo wangu." Alichukua tena uma wake. Alvin alimpiga Hans kwa siri sura ya kufurahisha kwa kazi nzuri ya kumshawishi Lisa ampeleke hospitali.
Dakika 15 baadaye, Lisa alitoa BMW mpya kutoka karakana. Kabla ya Alvin kuingia ndani, aligeuka na kumwambia Hans, “kalete gari mpya nililomnunulia majuzi.”
Lisa ghafla akakumbuka kuwa gari alilompa lilikuwa na plate namba ya '4EVA. Lilikuwa gari pekee la aina yake nchini, hivyo alifurahi sana alipolipokea. Hata hivyo, hakuwa na haja malo tena.
"Hakuna haja, silipendi tena." Baada ya kumaliza kuzungumza, aliongeza, “Alvin, unapaswa kuacha tabia yako ya kutumia namba kutangaza mapenzi yako kwa wengine. Ninaogopa nitachukizwa ikiwa nitaingia ndani ya gari hilo.” 4EVA? Upuuzi gani. Kufikiria tu kulimfanya atamani kutapika.
Uso wa Alvin uliingia simanzi mara moja. "Sikufikiria kulipua fataki saa mbili usiku kila siku ya Ijumaa. Ilikuwa wazo la Rodney—”
“Ndiyo, Bi Kimaro. Ninaweza kuthibitisha hilo,” Hans alisema kwa umakini.
Lisa alitabasamu na kutikisa kichwa. “Oh, najua. Jina la Alvinarah pia halikupendekezwa na wewe, lakini lilikuwa wazo la Chester. Pia haukuwa na wazo la kuita jina la Sarah katika ndoto yako. Alikuwa ni Sarah ambaye alikukumbuka kutoka kwenye ulimwengu mwingine."
Alvin akaishia kuguna tu tena. Kama wakili, ilikuwa mara ya kwanza kupata hisia za kushindwa kujitetea.
Baada ya gari kufika hospitali, Lisa alisema bila kujali, “Nimekufikisha hospitali. Lazima niende ofisini kwa ajili ya mkutano.". Lisa akawasha gari na kuondoka. Hakutaka kuwa na moyo wa huruma kwa sababu tu Alvin alikuwa akionyesha huruma. Ni nani ambaye alimhurumia alipokuwa na huzuni na kuteseka?
Wakati anaondoka, ghafla akamwona Maurine Langa akiwa amevalia nguo ndefu ya maua ya bluu. Nywele zake ndefu zilipepea huku akiwa ameshikilia rundo la maua mkononi mwake.
Lisa ghafla akaahirisha kuondoka na kumpigia simu Hans. “Upo wodi gani?”
"Bibi mdogo, unakuja?" Hans alishangaa sana.
“Ndiyo.”
"Ghorofa ya 5, wodi ya VIP6."
Baada ya Hans kumalizia simu pale juu, aligeuka na kuona macho ya Alvin yakiwa yanawaka moto wa furaha. “Anakuja?”
“Ndiyo.” Hans alicheka. "Inaonekana anakupenda. Ingawa maneno yake ni makali, bado hawezi kukuacha utoke moyoni mwake."
Alvin alitabasamu na papo hapo akamgeukia muuguzi, “Fanya hivi baadaye…” Alvin akautoa mkono wake ghafla. “Nidunge sindano ukisikia mlango unagongwa, lakini uchome vibaya ili damu itoke zaidi. Kadiri itakavyoonekana kutisha zaidi, ndivyo nitakavyokupa pesa nyingi zaidi.”
Nesi alipigwa na butwaa. Hakuwahi kufikiria kwamba Alvin angetumia mbinu ya kitoto ya kujidhuru ili kupata huruma ya mwanamke. Ilibadilisha kabisa mtazamo wake kwake.
Dakika tano baadaye, hodi ikasikika. Nesi akashtuka na kumchoma sindano vibaya Alvin na kusababisha damu kutoka. Alvin aliuma mdomo wake uliopauka kidogo. Mwonekano dhaifu ulifunuliwa kwenye uso wake mzuri na maridadi. Ingawa alikuwa na maumivu, bado alionekana kuvutia.
Moyo wa nesi ulikaribia kuyeyuka. Alvin alikuwa mwigizaji mzuri sana. Angeweza kuiba mioyo ya wasichana wadogo na hata wanawake wazee. Angeweza kuwafanya wasitake chochote zaidi ya kumlinda mikononi mwao.
Wakati huo, Hans alifungua mlango na Maurine, ambaye aliingia na maua safi, mara moja akageuka sura. "Bwana Kimaro, kwanini unavuja damu nyingi?"
Uso wa Alvin haukuweza kujizuia kuwa mkali. Maurine alikimbia na kumsukuma nesi, akimshutumu kwa maneno makali, “Unajua hata kufanya kazi yako? Unawezaje kumuumiza mgonjwa namna hii?”
Nesi akagugumia, “Mimi...” “Bwana Kimaro, alisema...” Maurine haraka alichukua usufi wa pamba kutoka kwenye trei ili kukandamiza jeraha lake linalovuja damu.
Alvin alitaka kumzuia, lakini Maurine alimng'ang'ania. “ Bwana Kimaro, usiogope. Tukiacha hivi itavimba. Inauma? Nitakupuliza…”
Lisa aliingia ndani wakati huo. Hapo awali hakutaka kukasirika, lakini mara baada ya kuingia, alimuona nesi akiwa amesimama pembeni huku Maurine akiwa amemshika mkono Alvin. Midomo yake ilikuwa karibu kugusana na mkono wa Alvin.
Alipofikiria jinsi alivyokaribia kuamini kuwa hakukuwa na kitu kati yake na Maurine, Lisa hakutaka kitu zaidi ya kujipiga makofi mawili......ITAENDELEA....
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
