JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP..........................0628924768
SEHEMU YA................................254-255
Sura ya: 254
“Usiwe mjinga. Ikiwa familia ya Campos inapanga kwenda mahakamani na Alvin, hakuna nafasi kabisa ya kushinda. Alvin ni mtaalamu wa sheria. Hakuna mtu anayeweza kumshinda.” Lea akakabidhi kadi mkononi mwake. "Ninaendesha kampuni pia. Ninajua jinsi mzunguko wa pesa wa kampuni ya Campos Ltd. ulivyo mkubwa. Unaweza kunirudishia pesa hii pale tu kampuni itakapokuwa na mtaji wa kutosha.”
"Asante." Mason alimkumbatia. Lea akatabasamu.
Wakati huo huo, Mzee Kimaro alimpigia ghafla. “Uko wapi? Nina jambo la kujadili na wewe. Rudi nyumbani kwangu mara moja."
“Sawa…”
“Uje peke yako.” Mzee Kimaro alisisitiza. Lea alipigwa na butwaa.
Saa moja baadaye, Lea aliingia sebuleni. “Baba, kwanini umeniita hapa?”
"Hebu nikuulize, una pesa ngapi benki?" Mzee Kimaro alimtazama kwa ukali.
Lea alibana midomo yake pamoja bila kuelezeka. “Sina salio kubwa. Niliwekeza sehemu.”
Mzee Kimaro alisimama taratibu. “Niweke wazi kuhusu kiasi gani ulicho nacho na uliwekeza kiasi gani. Usiniambie kwamba ulimkopesha Mason pesa hizo?”
Lea aliuma meno yake na kusema, “Baba, Alvin alidai shilingi bilioni 80 kutoka kwa Campos Ltd kwa ghafla. Familia ya Campos inaweza kupata wapi pesa nyingi hivyo—”
“Kwa hiyo umempa kweli?” Bibi Kimaro aliuliza kwa kutetemeka.
“Ndiyo.” Lea akaitikia kwa kichwa.
Alipomaliza, Mzee Kimaro alimpiga kofi usoni. “Mjinga wewe!”
“Baba…” Lea alikuwa ameduwaa kutokana na kupigwa. Tangu alipokuwa mchanga, hakupokea chochote ila sifa kutoka kwa Mzee Kimaro- isipokuwa kwa wakati aliposisitiza kuolewa na Mason.
"Nilidhani ulikuwa na akili hapo awali, lakini kwanini shimo kwenye ubongo wako linakua kubwa unapoanza kuzeeka?" Mzee Kimaro alitupa hati usoni mwake. “Tazama mwenyewe. Huu ni uchunguzi wangu wa hivi karibuni kuhusu familia ya Campos. Campos Ltd ina thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 900. Kwa kweli, nyingi zilitumika kwa uwekezaji, lakini bado kuna angalau dola bilioni 100 kwenye akaunti ya kampuni.”
Lea alishtuka baada ya kuziona zile nyaraka. Wakwe zake walikuwa wakimwambia kila mara kwamba familia ya Campos ilikuwa na matatizo ya ya pesa hivyo alijitutumua kuwasaidia. “Hii… Sikujua kwamba wakwe zangu walikuwa wajanja sana, lakini hii hakika haina uhusiano wowote na Mason. Mawazo yake yote ni kutunga muziki na mara nyingi husafiri. Hausiki kabisa kusimamia kampuni. Hasimamii Kampuni ya Campos hata kidogo…”
Mzee Kimaro akatikisa kichwa kwa kukatishwa tamaa. “Kama wakwe zako wangekuwa werevu kiasi hicho, hawangekuwa masikini na waliofeli kwenye maisha. Kampuni ya Campos imekuwa ikijiendesha kwa ujanja ujanja sana miaka hii yote. Kuna mtu anafanya hila nyuma ya pazia.”
"Baba, usitake kusema kwamba mtu huyu ni Mason, sawa?" Lea hakuamini hata kidogo. “Nimelala naye kitanda kimoja kwa miaka makumi kadhaa. Hakuna anayemuelewa kuliko mimi.”
Bibi Kimaro alisema kwa unyonge, “Babu yako tayari amechunguza. Jack na Valerie siyo walioeneza picha kuhusu ugonjwa wa akili wa Alvin. Kuna watu wengi tu katika familia ya Kimaro, unadhani angekuwa nani kama si yeye?”
Lea alishtuka. Hakutaka kuwa na mashaka, lakini kama hilo lilifanywa na Mason…
“Na…” Mzee Kimaro alisema, “Unajua kuhusu ndoa kati ya familia ya Campos na familia ya Ngosha sivyo? Ilipaswa kuwa tukio la furaha, lakini tangu Joel alipoingia kwenye ajali, familia za Campos na Ngosha sasa zinaunganisha nguvu na pesa kuingia katika sekta ya fedha, vifaa, na biashara ya mtandaoni. Tayari wana kampuni tanzu. KIM International imezingirwa na iko katika hali ngumu.”
Bibi Kimaro alisema, "Ndiyo maana Alvin anataka Campos Ltd kufidia shilingi bilioni 80 ili kupunguza mzunguko wao wa mtaji na kufanya mipango yao kuwa bure. Lakini wewe…”
Lea alijilaza kwenye kiti. Alihisi baridi pande zote.
"Imekuwa bahati tuna Alvin, tungeendelea kukuachia kampuni mikononi wako, muda si mrefu tungeisahau KIM International." Mzee Kimaro alitaka kumpiga kofi. “Potelea mbali, sitaki kukuona.”
Lea hakujua alitokaje kutoka kwa nyumba ya familia ya Kimaro. Alikuwa ametumia pesa zake alizochuma kwa bidii kusaidia familia ya Campos, kumbe alikuwa anaisaidia kuiba biashara ya familia ya Kimaro? Hapana, ilibidi arudishiwe pesa yake hata iweje!
Aliporudi kwenye fahamu zake, akamwpigia simu Mason kwa haraka. "Mason, unaweza kunirudishia zile bilioni 60? Usijali, tayari nimezungumza kuhusu hilo na baba yangu. Alisema atamzuia Alvin—”
“Oooh! Pole, mpenzi wangu. Tayari nimempa Jerome pesa hizo,” Mason alisema kwa unyonge, “Jerome tayari amehamisha pesa hizo kwenye akaunti ya KIM International.”
Uso wa Lea ulikuwa mweupe kama karatasi. Alihisi kana kwamba kuna kitu kinamzuia kooni.
“Ni sawa, mpenzi. Unaweza kumwomba Alvin akupe pesa,” Mason alisema kwa furaha, “Asante kwa kuwa msaada mkubwa kwa familia ya Campos. Nakupenda."
Kama ingekuwa zamani, Lea angeguswa, lakini kwa muda huo, mwili wake wote ulihisi baridi. "Mason, nijuavyo, biashara ya familia ya Campos imekuwa ikifanya vizuri miaka hii michache. Je, akaunti yake haina shilingi bilioni 80?”
"Mpenzi, wazazi wangu walisema hakuna pesa. Nadhani hawawezi kunidanganya.”
Lea alifarijika kidogo. Familia ya Campos lazima ilimdanganya Mason pia. Haikuwezekana kwamba Mason angemdanganya.
•••
Katika ofisi kwenye ghorofa ya juu. Baada ya Mason kukata simu, uso wake wa kiungwana ulibadilishwa na sura kejeli na dharau, akaitupa simu yake pembeni.
Jerome alitabasamu kwa furaha. “Uncle, Lea ni mjinga sana. Nilikuwa nasita kumpa Alvin pesa hizo, lakini mama yake katoa bilioni 60 kirahisi kabisa. Hahah, Alvin labda atakufa kwa kufadhaika ikiwa angejua tulichukua pesa za mama yake na kumlipa yeye.”
"Mwanamke huyu anaanza kuwa na shaka," Mason alisema kwa utulivu.
“Haijalishi, lakini, hakuna mtu anayeweza kuzuia kunyanyuka kwa familia ya Campos sasa.” Jerome alitabasamu. “Uncle, unashangaza. Umeinyanyua familia ya Campos peke yako hadi kufikia kiwango hiki?”.
“Ndiyo maana nataka umuoe Melanie haraka iwezekanavyo. Ndoa pekee ndiyo inaweza kufunga familia mbili kwa nguvu kwenye mashua moja.”
“Nitafanya. Baada ya hapo, nitaimeza Ngosha Corporation hatua kwa hatua. Kufikia wakati huo, familia ya Campos ndiyo itakuwa juu ya utukufu wa Kenya.” Jerome alizidi kufurahi huku akiwaza juu yake.
"Sawa, Alvin hapaswi kututawala kwa muda mrefu pia." Mason alikodoa macho.
•••
Usiku huohuo. Katika spa.
Nusu ya mwili wa Lisa ulikuwa umezama kwenye sinki la maziwa. “Mahali hapa ni pazuri sana. Ni mara yangu ya kwanza kuja hapa.” Baada ya kuongea alikodoa macho na kumtazama Charity aliyekuwa anaingia kuoga. "Wow, unaonekana mwembamba lakini una mwili mzuri."
Aibu hafifu ilionekana kwenye uso wa Charity, ambaye ilikuwa nadra kwake kutokeea akiwa uchi kwa wanawake wenzake. Lisa alimtazama kwa husuda. Wakati huo, sauti ya mwanamke ilisikika kutoka upande wa pili wa ukuta.
“Maurine, nilisikia kwamba bei za hapa ni za juu sana. Una pesa gani ya kutuleta hapa?"
"Najua, lazima ni Alvin Kimaro ambaye alikupa pesa, sivyo?"
Maurine alisema kwa aibu, “Bwana Kimaro ni mkarimu sana. Ingawa simhudumii tena, alinipa kadi hii ya benki. Alisema naweza kuitumia nipendavyo.”
“Wow, nina wivu sana. Bwana Kimaro lazima awe amekupenda."
“Mh! Kwa mhudumu kama wewe, hata mtawaanaweza kuvunja nadhiri yake. Inaonekana kama Alvin kakupenda. Ukiniuliza, ningesema unaonekana mrembo zaidi kuliko huyo Lisa. Nani anajua? Unaweza kuwa Bi. Kimaro katika siku zijazo.”
Sura ya: 255
Masikio ya Charity yalihisi kuziba baada ya kusikia maneno hayo. Alikuwa karibu kusimama na kuwafuata, lakini Lisa alikandamiza mabega yake chini.
"Utamwacha aende hivihivi tu?" Charity akamtazama.
“Usiwe na haraka. Hebu tumalize kuoga kwanza.” Lisa akatikisa kichwa na kufumba macho.
Dakika 20 baadaye, Maurine na wanawake wengine watatu walitoka kwenye chumba cha kubadilishia nguo wakiwa wamevaa nguo za kuogea. Mara wakawaona Lisa na Charity wakiwazuia njia.
"Bi Kimaro, unataka kufanya nini? Bila shaka hutanipiga tena, sivyo?” Maurine alikuwa na hofu kwenye uso wake.
Mwanamke mrefu, aliyekonda nyuma yake alikuja mbele na kusema, "Madam Kimaro, hakuna haja ya wewe kumalizia hasira yako kwa mwanamke asiye na hatia. Wakati mwingine wanaume wanapokusaliti, lazima ujitafakari. Baada ya yote, inachukua vidole viwili ili kuvunja chawa.”
Macho ya Charity yakageuka kuwa ya kutisha. “Si ajabu nyie mnapatana. Inaonekana kama ndege wafananao huruka pamoja.”
Lisa alicheka. “Maurine, nataka tu unipatie kadi ya benki uliyo nayo sasa hivi. Alvin na mimi ni mume na mke, mali yake ni mali yetu ya pamoja. Nina haki ya kurudisha pesa alizokupa.”
“Bibi mdogo sijui unaongea nini. Pesa zangu natafuta kwa jasho langu mwenyewe,” Maurine alisema kwa huzuni.
"Kwa kazi ya kuuza mwili wako kwa Alvin?" Charity alimdhihaki, “Maurine, umekuwaje hivi? Nakumbuka ulikuwa mwaminifu sana enzi hizo. Katika siku yako ya kuzaliwa ya kutimiza miaka 18, ulikataa mkufu wa almasi ambao Sarah alikupa kwa sababu ulikuwa wa bei ghali, mbona umekuwa tofauti sana sasa hivi?”
"Charity, sijawahi kubadilika." Macho ya Maurine yalikuwa yakilengwa machozi.
Macho ya Charity yakaangaza kwa kutoamini.
"Sawa, ikiwa hautaitoa, nitaita polisi." Lisa akatoa simu yake kwa hasira. “Kama bado utaikatalia kadi yenye jina la mume wangu mpaka polisi watakapokuja, nitasema wewe ni mwizi na utasema uliipata wapi. Kwa kweli, ikiwa una uwezo, unaweza kumpigia simu Alvin aje."
Alipoona karibu mambo yanakuwa mazito, Maurine aliuma mdomo wake na kutoa kadi mfukoni mwake. “Unaweza kupiga simu polisi, lzkini kadi hii nilipewa na Rodney. Ninaweza kumwita aje na kuhakikisha jambo hili.”
Marafiki zake walipigwa na butwaa. "Maurine, si ulisema sasa hivi kwamba ni Alvin aliyekupa?"
Uso wa Maurine ulikuwa mdogo kwa aibu. Aliongea kwa kigugumizi, “Kadi ambayo Alvin niliisahau nyumbani…”
Charity alimdhihaki, “Kwanini wote wawili Alvin na Rodney walikupa kadi ya benki? Nilisikia kwamba matajiri wanapenda kushea wanawake wao na marafiki zao. Kumbe ni kweli?"
Jinsi marafiki wa Maurine walivyomchukuia ilikuwa tofauti ghafla. Macho yao sasa yalikuwa yamejaa dharau na kebehi.
"Charity, twende." Lisa alimshika Charity mkono na kuondoka zao. Kwa kuwa kadi ambayo Maurine alikuwa nayo ilikuwa ya Rodney, hakuwa na haki ya kuendeleza jambo hilo zaidi.
Charity alimtazama tena Maurine na kunong'ona, "Maurine huyu ni wa ajabu."
“Ndiyo, ni mtu anayejua kujirahisisha…”
“Hapana, Maurine binamu wa Sarah ninayemfahamu mimi ni tofauti na huyu. Mara nyingi alikuja nyumbani kwetu kucheza. Nilikutana naye mara nyingi wakati huo. Kutokana na kile ninachokumbuka, Maurine alikuwa mtu mwaminifu na mwenye tabia njema. Nilimjaribu sana kipindi hicho lakini hakuwa na tamaa hata kidogo. Katika siku yake ya kuzaliwa ya 18, Sarah alimpa zawadi ya mkufu wa almasi, lakini aliukataa kabisa…”
Moyo wa Lisa ulidunda kwa nguvu. "Unataka kusema kwamba Maurine huyu ni feki?"
Charity akaitikia kwa kichwa. "Si hivyo tu, Maurine aligonga lori kwa bahati mbaya siku za nyuma alipokuwa akiendesha baiskeli kurudi nyumbani akitoka shule. Vipande vya chuma kwenye lori viliacha jeraha kubwa kwenye shingo yake, na kovu likabaki milele. Hata hivyo, shingo ya Maurine huyu haina kovu lolote sasa hivi….”
Hatua za Lisa zilisimama. Kichwa chake kilikuwa karibu kulipuka. Ikiwa Maurine huyo alikuwa feki, ni nani aliyekuwa anajifanya Maurine na nia yake ilikuwa nini?
Kweli, alipokutana na Maurine kwa mara ya kwanza, alifikiri kwamba macho na sauti yake ilikuwa ya kawaida sana. Tabia yake ilimfanya amfikirie… Lina. Ubaridi uliuvaa ghafla mwili wake.
“Charity, sitaendelea kukaa hapa kwenye spa tena. Nilikumbuka tu kwamba nina kikao cha kuhudhuria. Nitaondoka kwanza.” Lisa alibadili nguo haraka haraka na kurudi nyumbani kwa kasi.
Aliposukuma mlango wa nyumba yake ya kifahari, alimwona Alvin akiwa amekaa kwenye sofa mle ndani akifanya kazi zake.
“Lisa si ulisema unaenda spa? Mbona umerudi mapema." Alvin akaweka laptop yake chini na kusimama. “Umekula—”
“Alvin, hebu nikuulize, ulikutana na Lina ulipokuwa bado Dar es Salaam baada ya kila kitu kutokea?” Lisa alimkatisha.
"Kwanini unauliza kuhusu Lina?" Macho ya Alvin yakawa ya kutisha.
“Baada ya Jones na mkewe kwenda jela, Lina alitoweka ghafla. Ulikuwa na uhusiano wowote na kutoweka kwake?" Lisa alimkazia macho.
Alvin alikunja uso. "Ni kweli. Nilimpa somo dogo. Yeye…” Ghafla alisikia maumivu makali kichwani mwake. “Nilimfanya nini? Kwanini sikumbuki?”
Moyo wa Lisa ulifadhaika. Alidhani kumbukumbu ya Alvin ilikuwa nzuri wakati wote. “Mpigie Hans umuulize. Hakika anajua.” Alvin alisema na kumshangaza sana Lisa.
Lisa alimpigia simu Hans. "Unakumbuka Alvin almfanya nini na Lina Jones? Usiwe na wasiwasi, ni yeye aliyesema nikuulize."
“Bwana Mkubwa, si uliniambia nimpeleke Lina kwenye kijiji cha ukiwa na kumuozesha kwa yule mzee?” Hans alishangaa.
Lisa akamwuliza harakaharaka. “Kijiji hicho kiko wapi?”
“Usijali Bi Mdogo. Lina lazima atakuwa anateseka sana kwa sasa. Hawezi kamwe kutoroka kutoka hapo kwa maisha yake yote,” Hans alisema kwa uhakika.
"Fuatilia kujua kama bado yupo huko au la…" Alvin aliamuru.
“Bibi mdogo…”
“Fanya kama nalivyosema,” Lisa aliongea kwa sauti thabiti.
“Sawa.” Hans alikubali tu.
Baada ya simu kukatika, Alvin aliuliza kwa sauti ya kutoridhishwa, “Kwanini umerudi ghafla na kuuliza kuhusu Lina?”
“Mimi ndiye ninayepaswa kukuuliza. Kwanini hukumbuki mambo uliyofanya hapo awali?” Lisa alimkazia macho. "Na maumivu ya kichwa chako yanatokana na nini?"
“Una wasiwasi na mimi?” Macho ya Alvin yakaangaza. Alinyoosha mikono yake na kumkumbatia. "Nilijua. Bado unanijali.”
“Alvin, acha kuekti ujinga. Nani anakujali wewe…” Wakati Lisa akihangaika kumsukuma, alishangaa kuona alama za sindano nyuma ya mkono wake. Alikumbuka Hans akisema kwamba Alvin alikuwa amezimia siku chache zilizopita.
“Mbona umeacha kuongea?” Alvin alizika uso wake kwenye shingo yake, na akasikia harufu ya kushangaza. “Lisa, una harufu ya maziwa mwilini mwako. Una harufu nzuri…” Lisa aliona haya. Alinukia vizuri kwa sababu alikuwa ameoga maziwa.
Hata hivyo, bado walikuwa katika ugomvi. Angewezaje kutaka kustarehe naye? Alikuwa anaota! Alimsukuma na kupiga hatua chache nyuma.
“Maurine wako ana harufu hii ya maziwa pia. Nilikutana naye na marafiki zake ambao kwa bahati walikuwa wakioga jirani kwenye spa. Alijitapa kuwa ulimpa kadi ya benki ya kutumia atakavyo.”
Alvin alikunja uso akiwa hafahamu chochote kuhusu hilo. "Sijawahi kumpa kadi ya benki. Maurine anawezaje kusema mambo kama hayo?”
"Unamaanisha nini? Unafikiri ninamsingizia?” Lisa karibu kufa kutokana na kuchanganyikiwa.
Alvin alijikaza. Kwa kawaida, kwa hadhi yake, alikuwa akiongea tu bila kuficha. Hata hivyo, alijionea kwamba kuzungumza ovyo kungeleta shida tu. “Sawa, hukumsingizia. Yote ni makosa yangu.”
“Kwa hiyo ulimpa kweli?” Lisa alimpiga teke kwa hasira na kwenda juu kwa hasira......ITAENDELEA....
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
