JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP..........................0628924768
SEHEMU YA................................246-247

Sura ya: 246

Alvin alinyamaza na kuamuru chopa kuondoka. Walifika kwenye baa upesi sana. Thomas ambaye alikuwa amekaa nje ya baa hiyo kwa muda mrefu, mara moja akasogea huku akiwa ameshika kiuno chake kilichojeruhiwa.

Kutokana na muziki mnene ulioziba masikio, Lisa hata hakuweza kusikia muungurumo wa helkopta. Hazikupita sekunde yeye na wenzake walijikongoja kutoka kwenye baa huku wakiwa wamekumbatiana mabega Kwa kuangalia midomo yao iliyokuwa ikipepesuka, ilidhihirisha walikuwa wamekunywa pombe nyingi.

“Bado sijatosheka, tuendeleeni kunywa, naweza kumaliza kreti zima peke yangu.” Pamela aliinua mikono yake juu hewani. "Sitarudi nyumbani hadi nilewe."

"Wacha tule nyama kwanza." Charity alikuwa amefurahi sana.

Lisa alishauri, "Tunaweza kwenda kuendelea kunywa katika nyumba yangu ya kifahari hadi alfajiri."

"Kweli! Sisi ni utatu mtakatifu, wote ni ma-single dadaz. Wanaume ni sh*t! Waache waende zao!" Charity akakubali kwa furaha.

"Sh*t! Wanaume ni nyoko!" Pamela akakandamizia kwa hasira.

Uso wa Alvin ulijawa na mawingu, Lisa hata alimdhihaki mbele ya marafiki zake? Akasogea kumvuta Lisa mikononi mwake. "Twende nyumbani haraka."

Hapo awali alikuwa ameridhika akae nje kwa muda kwa kuhofia kwamba angemdhuru, lakini ilionekana wazi kuwa asingeweza kufanya hivyo.

“Wewe ni nani na unafikiri unafanya nini?” Lisa aliinua kichwa chake akiwa ameduwaa. Baada ya kuutazama vizuri uso wake, lile tukio la Maurine akiwa amemlalia akimfanyia masaji lilimjia kichwani. Ghafla alihisi kichefuchefu na kumtapikia Alvin nguo zake zote na chini.

"Lisa Jones!" Alvin aliita jina lake herufi kwa herufi. Alitamani angemchuna ngozi akiwa hai hapohapo.

"Bwana Kimaro." Maurine alikimbia kwenda kumfuta uchafu ule mwilini
Mwake.

Baada ya kuona hivyo Pamela alikimbia mbele mara moja na kumpiga Maurine kichwani na mkoba wake. “Wewe b*tch, kwanini usitafute mwanaume wako? Umepanga kuharibu ndoa ya Lisa?”

Maurine aliugulia maumivu, Lisa alifurahi sana kuona hivyo, akasogea mbele akijifanya kumsaidia. “Pamela, usifanye hivi…”

Licha ya maneno yake hayo ya upole, Lisa alinyoosha mguu na kumpakaza Maurine kwenye matapishi yaliyokuwa chini, akasogea mbele kumkanyaga mara kadhaa. Maurine alilia kwa maumivu makali huku akishika pindo la suruali ya Alvin. “Bwana Mkubwa, nisaidie…”

“Inatosha.” Alvin alimsaidia Maurine kusimama kabla hajawatizama wale wanawake wawili, “Pamela kweli hujaelimika, Lisa, jiangalie vizuri ulevi wako, nilikuambia ujiepushe na Charity, umekaidi na kuamua kunywa pamoja naye. Kwanini husikii?”

Lisa alipapasa masikio yake na kujibu kwa dharau, “Unasema upuuzi gani, sikuelewi.”

Pamela alicheka. "Lisa, si unajua? Sisi hatujaelimika kuliko wao, kwa hivyo hatuwezi kuwa sawa nao."

“Uko sawa.” Lisa alikubali, “Twende.”

Alvin alikasirishwa kwa kupuuzwa na yule mwanamke, “Simama hapo hapo wewe ni mke wangu, nakuagiza twende nyumbani sasa hivi. Alvin alishika mkono wake tena, lakini wakati huu, nia ya hatari iliangaza macho yake yenye huzuni. “Usinifanye nipitilize kikomo cha uvumilivu wangu.”

“Kikomo? Una kikomo gani?" Lisa alicheka baada ya kumuona Thomas akiwa amesimama nyuma ya Alvin. “Kwa nini umemleta hapa? Ili kumtetea tena?”

Mara Thomas aliugulia maumivu. “Bi. Kimaro, kwa kweli unapaswa kukaa mbali na Charity. Ana kusudi la kufanya urafiki na wewe kwa nia mbaya."

“Thomas, ninajuta sana kwamba sikukupiga vya kutosha muda ule.” Charity akayafumba macho yake mazuri.

Thomas aliogopa sana na mara moja akajificha nyuma ya Alvin. “Bwana Mkubwa, tazama jinsi anavyo nitisha mbele yako.”

"Charity, inaonekana nimekuwa mkarimu sana kwako." Uso wa Alvin ulikuwa umekunjamana kwa hasira. “Nakuonya sasa ukae mbali na mke wangu. Vinginevyo, utasahau kama uliwahi kuwa mkurugenzi wa New Era Advertisings.”

Uso mzuri wa Charity ulibadilika na kupoa ghafla kama maji mtungini. Hata hivyo, Lisa alimshika mkono na kumtazama Alvin akiwa ameinamisha kichwa. “Hahitaji kufanya urafiki nami. Kuanzia sasa na kuendelea, mimi ndiye nitakayefanya urafiki naye. Yeye ndiye rafiki wa kwanza mzuri ambaye nimempata hapa Nairobi.”

Alvin alikasirika sana. “Lisa, ngoja nikukumbushe tena kuwa huyu mwanamke ni mjanja mjanja na mlaghai, lakini bado unataka kuwa rafiki yake. Wewe ni mjinga sana kutokuona hivyo?"

"Ndio, mimi ni mjinga sana ndo maana nilikupenda." Lisa alicheka kwa kebehi. “Huwezi kujua ni nani mjanja na nani mjinga? Charity hakunidanganya. Kinyume chake wewe na marafiki zako ndiyo mnanidanganya. Najua kwamba mume wangu ameweka mwanamke ambaye anaonekana kama mpenzi wake wa zamani karibu naye ili ajisikie vizuri. Je, huu ndio upendo unaoendelea kuuzungumzia? Unachukiza.”

Akiwa amepigwa na butwaa, mchanganyiko wa mshangao na aibu ukatanda usoni mwa Alvin. Hata hivyo, ilipita kwa sekunde chache tu kabla hajamkodolea macho Charity. “Ulimwambia kuhusu hili?”

Charity alikosa la kusema, mara Lisa akajiweka mbele yake kumtetea. “Angethubutu vipi kuniambia wakati unamtishia kuiangusha New Era Advertings? Uhusiano wako na Sarah ulikuwa maarufu sana hivi kwamba kila mtu hapa Nairobi anajua. Isitoshe, huenda sikuwahi kukuambia, lakini huwa unaliita jina la Sara usingizini. Hata jina la Alvinarah mchanganyiko wa maneno ya jina lako na lake. Nilijua hilo zamani. Oh, nini kingine? Ulijenga bustani ya kushangaza ili kumchumbia. Fataki bado hulipuka kila saa 8:3o usiku kama tamko la upendo wako. Mpaka hapo, mimi ninani ukilinganisha na Sarah?”

"Ni kweli. Lakini yote hayo yamepita…” Alvin hakujua la kufanya.”Huwezi kumwonea wivu mtu aliyekufa.”

Hakujua kamwe kuwa aliita jina la Sarah katika ndoto zake. Kwanini hakuweza kukumbuka lolote kati ya hayo? Alinyoosha mkono kuushika mkono wa Lisa, lakini aliutupa kwa ukali. Lisa alimtazama kwa mchanganyiko wa chuki, kukatishwa tamaa, na hasira.

"Hata mimi nilijua yamepita pia, lakini uamuzi wako wa kumweka Maurine karibu nawe unaniambia kuwa sitakuwa bora zaidi ya kumbukumbu ya mzimu, au hata kumkaribia tu." Lisa alimnyooshea Maurine kidole kinachotetemeka. “Ni mambo mangapi ya kuchukiza umefanya naye kitandani kwangu nikiwa sipo kila siku? Je, hakuna chumba kingine ndani ya nyumba? Toka Maurine aingine ndani kwetu hata hisia zangu huzijali tena. Kila anachokuambia unafuata tu.”

"Bi. Kimaro, unazungumza nini?" Akiwa na huzuni, Maurine alisema, “Wewe pekee ndiye Alvin anakujali.”

"Nyamaza! Hakuna mtu anayeweza kujifanya zaidi yako. Uliwadanganya wanaume wote na kufanya kila kitu kionekane kama ni kosa langu.” Lisa akashusha pumzi ndefu. “Lakini haijalishi. Unaweza kuwa na Alvin ukitaka kwa sababu mimi sijali tena.”

"Ikiwa hunijali, basi unamjali nani?" Alvin alimkandamiza mabega. Mwili wake ulimuuma kana kwamba anakosa hewa. “Sijafanya chochote na Maurine. Ninamweka karibu tu… kwa sababu… kwa sababu yeye ni binamu ya Sarah, na nilifikiri ni lazima nimtunze. Sivutiwi naye hata kidogo.”

"Sawa, kumtunza vipi huko mpaka kwenye kitanda chetu pia?" Lisa alicheka.

'Sikufanya hivyo.” Alvin alifoka kwa ukali, “Mbona huniamini?”

“Kwa sababu hustahili kuaminika.” Lisa akatikisa kichwa. Alihisi amani zaidi baada ya kutoa hisia zake alizozivumilia kwa muda mrefu. “Kwa sababu ya Sarah umeamua kulala chumbani kwetu na binamu yake. Kwa sababu ya Sarah umeamua kumtetea na kumlinda kaka yake. Kwa sababu ya Sarah umeamua kumchukia Charity na kuikandamiza kampuni yake. Ni nini kingine kitafuata katika siku zijazo?"

Sura ya: 247

“Lisa, acha. Twende nyumbani.” Alvin akazidi kufadhaika jinsi Lisa alivyokuwa mkali.
Hata hivyo, Lisa alibakia kusimama kama ameota mizizi chini. Alimwangalia na kummwagia tabasamu la kejeli. “Kwa sababu ya mpenzi wako wa zamani, siwezi kuwa rafiki na Charity. Oa tu Maurine ikiwa huwezi kuacha kumfikiria mwanamke huyo. Nipo radhi tupeane talaka.”
“Umemaliza? Wewe ndiye mtu ninayekupenda sasa." Kichwa chake kilikuwa kinamuuma sana. Kwa kweli hakujua ni nini kingine angeweza kusema ili kumshawishi.
"Ndio, unanipenda, lakini sio kama unavyompenda Sarah." Lisa alihema kwa uchungu. “Ikiwa Maurine, ambaye anafanana na Sarah, anaweza kuchukua nafasi yangu leo, basi inakuwaje mtu mwingine anayefanana naye zaidi atakapotokea siku moja? Mimi ni mtu ambaye anaweza kubadilishwa wakati wowote, na sitaki kuendelea na uhusiano wa aina hii tena. Samahani. Labda nisiseme hivi kwa sababu ya hali yako, lakini siwezi kukaa kando yako. Jitunze.”
“Hapana, Lisa, wewe ni wa kipekee na hakuna anayeweza kuchukua nafasi yako. Usiniache.” Alvin alimkumbatia kwa nguvu huku akiingiwa na hofu mithili ya mtoto anayekaribia kupoteza mali yake aipendayo.
Alikuwa amepitia upweke na uchangamfu wa upendo, lakini Lisa ni mwanamke pekee aliyebaki kando yake. Angewezaje kuishi ikiwa angeondoka?
"Acha. Mimi sio muhimu sana kwako. Baada ya yote, marafiki zako wanaweza kunifokea na wewe unawaangalia tu, na unaweza kunifungia wakati wowote upendao. Na nikihitaji marafiki mpaka nipate idhini yako… Sahau.” Lisa alijaribu kuunyoosha mkono wake kutoka kwake, lakini Alvin alikataa kuuachia.
“Usiende. Siwezi kuishi bila wewe. Nitamruhusu Maurine aondoke, sawa? Kisha tunaweza kurejea jinsi tulivyokuwa tunaishi hapo awali.” Alvin aliogopa sana. Hakuwahi kufikiria kuwa hivyo ndivyo itakavyoisha kwa Lisa.Kwanini watengane kwa sababu ya mabishano madogo?
"Bwana mkubwa naomba umwachie aende." Charity akasogea mbele kumsaidia Lisa.
"Charity, yote ni kwa sababu yako, sawa?" Akamtazama kwa chuki. "Unanichukia kwa kuibania kampuni yako nafasi ya ushirikiano na Alvinarah, kwa hivyo unalipiza kisasi kwa njia hii, sivyo?"
“Bwana Mkubwa, unawaza mambo kupita kiasi. Lisa sasa ni rafiki yangu. Kama marafiki yake, naweza kusema kwamba wewe na marafiki zako mmekuwa mkimtendea isivyo haki.” Charity alijibu kabla ya kumuongoza Lisa.
Pamela alifuata mara moja. Kisha wote watatu wakaingia kwenye gari na kuondoka.
Moyo wa Alvin ulipasuka sana huku akilitazama gari lile likipotea kwa mbali. Alitamani sana kuikimbia lakini ghafla, kichwa chake kilikuwa na maumivu makali, akaaanguka chini na kuzimia!
•••
Katika klabu ya usiku, Pamela aliagiza vinywaji vingine kumi na mbili, na wote watatu wakaagiza chakula.
Ingawa walikuwa wamezungumza mambo mengi, Lisa hakuweza kuacha kunywa pombe akijaribu kusahau kuhusu mateso ya Alvin. “Charity, naweza kukuuliza swali? Kwanini Alvin na marafiki zake wanakuchukia sana? Nimekufahamu kwa muda mfupi tu, lakini naweza kusema kwamba wewe ni mtu mzuri.”
"Ndio, umechukua maneno mdomoni mwangu Hata mimi nilitaka kumuuliza hivyohivyo." Pamela alitikisa kichwa.
Charity alionekana mwenye huzuni. "Labda ina uhusiano fulani na Sarah. Mama yangu alipoanza uhusiano na Langa Njau wakati huo, walimwona mama yangu kama mvurugaji tu wa familia ya Langa na hata kuwafanya wengine wanichukie pia nilipozaliwa. Nilipokuwa binti nilikutana na Chester nikiwa shule ya sekondari tukawa wapenzi, lakini haikuchukua muda tukaachana. Wote watatu walifikiri kwamba mimi nilikuwa sababu ya Sarah kukosa raha. Waliamini kwamba niliondoa ushirika na upendo wa baba ambao ulikuwa haki yake na kaka yake. Lakini siku zote nimekuwa nikitegemea juhudi zangu na uwezo wangu kufikia hapa nilipo leo.”
Lisa alipata picha halisi. “Nimegundua kitu, Alvin anawachukia sana watoto wa nje ya familia. Anaamini ni chanzo cha kuvuruga furaha ya familia. Kwa hiyo na wewe anakuchukia mpaka kwenye damu yake kwa sababu anaamini uliharibu furaha ya Sarah.” Kwa namna fulani, hii ilimkumbusha Lisa kuhusu Alvin na Jack na ndiyo maana hawakupatana maisha yao yote.

Baada ya sekunde chache, Charity alisema, "Hiyo ndiyo sababu kubwa. Alvin alimpenda sana Sarah na aliwachukia wote waliomuudhi. Kama Sarah atafufuka leo, hakika Alvin atachagua kurudi kwake na kukuacha wewe." Lisa alisikiliza maneno hayo huku akinywa bia kimya kimya.
•••
Katika hospitali. Alvin akarejewa na fahamu.
Mkono wake ulikuwa umeunganishwa na dripu. Akapepesa macho mara kadhaa. Aliweza kusikia sauti ya Rodney kutoka chumba kingine.
“Nimesema tangu mwanzo kwamba Lisa si mtu mzuri. Alvin tayari ni mgonjwa sana, lakini bado anasisitiza kutaka talaka. Hamjali hata kidogo.”
“Punguza sauti yako. Je, akiamka na kukusikia?” Chester alimtahadharisha.
“Nimekosea? Hana shukrani kwa kila kitu ambacho amempa, na bado anajaribu kushindana na mtu aliyekufa?” Rodney alizidi kulalamika.
“Bwana mkubwa, umeamka." Maurine, ambaye alikuwa ameketi kando yake, alipiga kelele alipomwona Alvin anafungua macho yake.
Mazungumzo ya koridoni yalisimama. Dakika kadhaa baadaye, Rodney na Chester waliingia chumbani kwa fujo.
"Nionyeshe hizo hati za talaka." Alvin alinyoosha mkono wake.
Rodney almkabidhi baada ya kusitasita. Alvin aliichunguza hati hiyo, ambayo ilisema kwamba Lisa hataki chochote. Alikuwa tayari kuacha ndoa bila chochote ilimradi tu akubali kusaini karatasi hizo. Vidole vyake vilishika karatasi hizo na kuzichanachana mara moja.
Kila mtu alichukulia jambo hilo kwa njia tofauti, lakini Maurine alijaribu kumfariji. “Bwana Mkubwa, usijali. Bi. Mdogo anafanya hivi kwa hasira tu. Atajuta baada ya kutulia.”
“Unatakiwa kuondoka.” Sauti ya Maurine ilimpa maumivu makali ya kichwa.
Rodney alisimama kumtetea kwa hasira. “Alvin, unasemaje? Lisa hata hajaja kukuangalia baada ya kuzimia. Ni Maurine ndiye aliyekuleta hapa.”
"Kwa hiyo? Unataka nimuoe yeye badala yake?” Alvin akanyanyua macho yake kwa jeuri. “Kwanini usimuoe wewe kwa kuwa unapenda kumtetea sana?” Rodney alishindwa cha kusema.
Machozi yalitiririka mashavuni mwa Maurine aliposema katikati ya kwikwi, “Bwana Shangwe, tafadhali acha kubishana naye. Najisikia vibaya sana. Bwana Mkubwa asingeingia kwenye vita hivi na mke wake kama si mimi. Ni bora niondoke tu." Maurine akatoka nje.
Alvin alishika midomo yake bila kutoa neno zaidi.
"Maurine, nisubiri." Rodney alipumua, kisha akamkimbilia Maurine.
Chester alisugua kichwa chake kama ishara ya kukosa cha kusema. "Utafanya nini?"
“Sitamruhusu Lisa aondoke upande wangu. Nina hakika kwamba yeye ndiye mtu ninayempenda.” Alvin aliweka msimamo.
Matukio ya kabla ya kuzimia yalimjaa akilini, na kumfanya kuchanganyikiwa. "Ni kosa langu. Labda… Sikupaswa kumruhusu Maurine abaki. Lakini sikufikiria kwamba Lisa angeniwazia mabaya zaidi. Anadai alinikuta kitandani na Maurine, lakini si kweli.”
"Labda Charity alikuwa akimpotosha." Chester alikunja uso.
“Charity Njau…” Alvin alikunja ngumi. “Sitakuwa mwema kwake tena. Nitahakikisha familia ya Njau inafilisika ndani ya mwezi mmoja.”
“Sikubaliani. Lisa atakuchukia zaidi akijua,” Chester alisema. "Familia ya Njau tayari iko mwisho wa wakati wao, itajifia yenyewe tu. We achana nayo."
“Sawa.” Alvin alihisi kichwa chake kuanza kumuuma tena. “Wewe ni mzoefu zaidi katika hili. Niambie jinsi ninavyopaswa kumrudisha.”
"Subiri, nitakutumia vidokezo vichache vya siri." Chester alimtumia mafaili machache kwenye simu. Alvin aliyapitia siku nzima......ITAENDELEA....

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.