JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP..........................0628924768
SEHEMU YA................................244-245

Sura ya: 244

Nairobi Square Garden, ni eneo linalojumuisha mabangalow na majengo ya kifahari, ni eneo lililo nje kidogo ya jiji la Nairobi. Pia kuna na malls, viituo vya michezo, na maeneo mengine muhimu.

Muuzaji aliwazungusha Lisa na Pamela kwenye ziara mchana mzima. Waliporudi kwenye kitengo cha mauzo, meneja alishtuka baada ya kumtambua Lisa, na mara moja akamjulisha bosi wake. Bosi akampigia simu Hans haraka na kumfikishia Alvin ujumbe ule. "Bwana Kimaro, Bi Jones anatazamia kununua nyumba."

Alvin aliyekuwa akisoma nyaraka za kazi ofisini kwake alikunja uso. “Anajaribu kumaanisha nini? Kwamba hana mpango wa kurudi nyumbani tena?”

Hans alijua anapaswa kumfariji Alvin badala ya kumpanikisha zaidi.
“Labda… Anataka kufanya uwekezaji? Wanawake wengi matajiri wanafanya vivyo hivyo siku hizi.”

Alvin akalegeza uso wake uliokuwa umekakamaa kwa hasira. Baada ya kufikiria kwa ufupi, alisema, “Kwa vile mke wangu anapanga kununua nyumba, waambie wampe punguzo bora zaidi. Hmm, punguzo la 90%.”

Hans alitetemeka hadi moyoni. "Lakini Bwana Kimaro, Bibi mdogo bila shaka atakuwa na shaka ikiwa utafanya hivyo. Anaweza hata kubadili mawazo yake kuhusu kuinunua.”

Alvin alimtupia jicho la kuudhi. "Basi 70%. Hawawezi kwenda chini zaidi ya hii."

“Um… sawa.” Hans alikosa la kusema. Hii ilikuwa mara yake ya kwanza kuona bosi wake akijaribu kumpa mteja punguzo zaidi ya inavyopaswa.

Lisa na Pamela waliridhika sana baada ya ziara hiyo. Kitu pekee kilichomchelewesha ni bei kwa sababu ilikuwa nje kidogo ya bajeti yake. Jumba la bei rahisi zaidi pale lingegharimu angalau mamia ya mamilioni ya shilingi.

“Tafadhali nifanyie bei nzuri zaidi. Nitahitaji siku chache kufikiria hili,” Lisa alisema mwishoni.

"Hakika, ngoja nicheki na bosi wangu." Muuzaji huyo alipotea kwa dakika tano kabla ya kutokea tena kwa furaha. "Bi Jones, habari njema! Utakuwa mteja wetu wa 1000 ukiweka amana leo. Bosi wetu amesema nyumba yoyote utakayochagua utapewa punguzo la 50%, na unaweza hata kupata nafasi ya kujiunga na droo yetu maalum ya bahati nasibu. Baadhi ya zawadi hizo ni pamoja na punguzo zaidi la bei, jokofu na vifaa vya nyumbani bila malipo, zawadi za kifahari zenye thamani ya dola laki moja, na kadhalika.”

Lisa alizidiwa na taarifa hizo za ghafla. Pamela alipiga kelele kutokana na msisimko. “Umeshinda bahati nasibu! Haraka na ulipienyumba sasa. Hakuna haja ya kuchelewa zaidi."

"Hiyo ni sawa. Ni mteja wetu wa 1000 pekee ndiye anayeweza kupata bahati kama hii. Inastahili pesa hizo hata ukinunua nyumba na kuisahau
baadaye,” muuzaji alikariri kwa kutia chumvi.

Mwishowe, Lisa alilipa pesa na kujaribu bahati yake kwenye droo. Muuzaji aliitazama na kuziba mdomo huku akipiga kelele kwa sauti. “Mungu wangu, wewe ndiye mtu mwenye bahati zaidi duniani! Umejishindia zawadi ya punguzo zaidi. Unapata punguzo zaidi la 20% juu ya 50% ya hapo awali. Kwa maneno mengine, utapata punguzo la 70%! Unaweza kuwa na nyumba ya kifahari iliyokarabatiwa kikamilifu ambayo kwa kawaida inagharimu dola milioni mbili kwa bei ya dola laki moja na nusu tu! Inashangaza!”

Lisa hakuwa na neno. Alihisi kana kwamba uchawi wa bahati ulikuwa umetupwa juu yake. Je, hatma yake ingebadilika na kuwa bora baada ya kuachana na Alvin? Alitoka nje ya kitengo cha mauzo akiwa ameduwaa.

Pamela alikuwa na mawazo tofauti na yeye. "Sidhani kama hii ni bahati tu. Haudhani inawezekana kwamba mkono wa Alvin unafanya kazi kwa siri?”

“Hapana, kwanini aniwazie mimi? Pengine anafurahia wakati wake na Maurine muda huu. Kitu pekee anachofikiria juu yangu labda ni kunifungia tena." Lisa alipuuzia kabisa mawazo ya Pamela.

“Uko sahihi. Labda hata Mungu alikuhurumia. Hebu turudi hotelini na tupakie vitu vyetu. Tunatakiwa kwenda kwenye baa usiku wa leo kusherehekea bahati yako!”

Pamela alizungusha mkono wake mabegani mwa Lisa.

Lisa hakukataa. Baada ya yote, ilikuwa imepita muda mrefu tangu aende baa pamoja na Pamela.

Saa tatu usiku wawili hao waliingia ndani ya baa pamoja. Lisa hakuwa katika mazingira kama hayo kwa muda mrefu sana. Kuwa baa kulimkumbusha maisha rahisi na ya kujiachia kabla ya kuolewa.

Hata hivyo, muda si mrefu baada ya kuanza kunywa pombe, walifikiwa na jamaa mmoja aliyevalia shati la maua. "Pamela, ni bahati njema kama nini tunakutana tena." Mwanaume huyo aliubembeleza uso wa Pamela kwa tabasamu la kejeli.

Uso wa Pamela ulizama mara moja na kuusukuma mkono wake mbali. “Thomas Njau, nimekwambia wazi kuwa sina shida na wewe. Peleka sura yako mbali na mimi.”

Lisa alishtuka kusikia mtu huyo alikuwa kaka mkubwa wa Sarah Langa.

“Usiseme hivyo. Nipe nafasi hata mara moja. Huenda usiweze kujizuia mara tu utakapoona jinsi nilivyo mtamu kitandani.” Aliendelea kumsumbua huku akiwa na tabasamu baya usoni mwake. "Ni heshima kwako kuwa mwanamke wangu. Mimi ni handsome, kwa kawaida wanawake huwa wananipapatikia..."

"Thomas, nitampigia dada yako au polisi ikiwa utaendelea na kutusumbua." Lisa alijiweka mbele ya Pamela.

“Kaa kushoto na sura yako mbaya wewe. Unafikiri wewe ni nani?” Alimtazama kwa sekunde kadhaa kabla ya kucheka ghafla. “Oh, wewe ni mke wa Alvin. Si ajabu unakuwa na kiburi sana.”

Lisa alikunja uso, lakini Pamela aliinua kichwa chake mbele kutoka nyuma. "Hiyo ni sawa. Lisa ni mke wa Bwana Kimaro, na mimi ni rafiki yake mkubwa. Kuninyanyasa ni sawa na kumnyanyasa.”

Thomas alicheka kwa sauti baada ya kusikia hivyo. “Ningeogopa ikiwa Alvin angekuwa hapa, lakini huyu ni mke wake tu. Kusema kweli, hata kama ningelala na mke wake usiku wa leo, kikubwa atakachonifanyia ni kunipiga ngumi za usoni tu. Unaniamini?"

Lisa alihisi moyo wake kuzama kwa kuona sura yake ya kiburi, lakini, ilimbidi akubali kwamba labda alikuwa sahihi. Mtu huyu alikuwa kaka wa damu wa Sarah Langa. Alvin asingemfanya lolote hata angeangamiza dunia nzima.

Thomas alimpandisha juu na chini kama anamfanyia tathmini fulani. “Tsk, wewe ni mbaya sana na hakuna kitu ukilinganisha na dada yangu. Usingeolewa na Alvin kama si kwa bahati ya kifo.”

“Ondoka!” Pamela hakuweza kuvumilia kwa muda mrefu zaidi, mikono yake iligonga meza kwa hasira. “Sijali mdogo wako ni nani, lakini kwa kaka kama wewe, nahisi atakuwa ni takataka tu kulinganisha na Lisa wangu.”

“Wewe mwanamke mjinga. Nisipokupelekea moto usiku wa leo, labda mimi siyo Tom!” Kwa uso uliopinda, Thomas alinyoosha mikono yake kushika mabega ya Pamela.

Mara mkono mzuri uliibuka ghafla kana kwamba umetoka hewani na kumshika mkono Thomas.

“Nani tena…” Alitazama juu ya mabega yake na kuganda mara moja alipoona sura ya Charity iliyofura kwa hasira.

"Nakumbuka nilikuambia uache kumsumbua Pamela." Charity alimtazama bila kujali.

Donge la chuki likaangaza ghafla machoni pake lakini likatoweka haraka kama lilivyoibuka. "Charity, unadhani wewe ni nani wa kuingilia mambo yangu?"

"Kwa hivyo nikuruhusu uendelee kufanya fujo na kuleta aibu kwa familia?" Charity alimminya zaidi kwenye kifundo cha mkono wake.

“Lo… Inauma!” Thomas aliinama na kukunja uso kwa uchungu lakini hakuweza kujinasua kutoka kwenye mkono wa Charity hata baada ya kufurukuta sana. “Niache niende, Charity. Wewe si lolotei. Familia ya Njau inasambaratika kwa sababu umemkosea Bwana Kimaro. Yote ni makosa yako!”

Charity akakunja uso. Thomas alitabasamu kwa hasira baada ya kuona hivyo. “Ngoja nikupe neno la ushauri. Alvin atakusamehe tu mara tu utakapoikabidhi New Era Advertisings kwangu. Au ungependa kuona kampuni hiyo ikikufia mikononi mwako?

Sura ya: 245

“Nyamaza. New Era Advertisings ingekufa siku moja tu chini ya uongozi wako.” Charity alimshika Thomas bega na kumpindua juu. Thomas alianguka chini bila huruma machoni pa watu.

Wote Lisa na Pamela walipigwa na butwaa. Hata hivyo, Pamela alikuwa wa kwanza kuvunja ukimya kwa kupiga makofi kwa sauti kubwa. "Wewe ni mzuri sana, Charity!"

Thomas alikasirika kwa kukosewa heshima na kuaibishwa mbele ya umati. "Charity, sitaacha hili lipite hivihivi, nakuapia." Kisha, akasimama na kutoka nje ya baa.

"Asante." Lisa alimimina glasi mbili za wine nyekundu na kumkabidhi Charity moja. Alikuwa na hisia nzuri tangu mwanzo na mwanamke huyo. Usiku huo, alimvutia sana.

“Usijali. Nilikuwa napita tu. Mmiliki wa baa aliniambia Thomas alikuwa akiwanyanyasa wanawake tena, kwa hivyo nilikuja kutazama." Charity akanywa mvinyo.

"Asante, dada!" Pamela akampa dole gumba. "Hakika ningekupa wewe kama ungekuwa mwanaume."

“Si vyema kwa wanawake kuwa dhaifu kiasi hicho," Charity alitania na kucheka. "Mimi ndiye ninayepaswa kuwaombeni msamaha ..."

"Yeye sio ndugu yako wa tumbo moja, kwa hivyo usijisumbue sana." Lisa alikokota kiti kutoka kwenye meza iliyofuata. “Unataka kujiunga nasi?”

Charity alikunja uso na kusita kwa muda. "Ningependa, lakini sisi si wa ulimwengu mmoja. Ikiwa Alvin atajua kuhusu hili…”

“Nimetengana naye,” Lisa alimkatiza. "Nimehama kutoka kwake. Sitaki kuwa mjinga tena.”

Uamuzi wa Lisa ulimshangaza Charity. “Unaweza kumwacha Alvin kweli?”

"Hasara kidogo ni bora kuliko majuto ya milele." Lisa alitabasamu kwa uchungu. “Kwa kweli, nimejua kuhusu Sarah zamani sana. Nilidhani haina tatizo kwa sababu Sarah ni marehemu kwa sasa. Lakini, Alvin ameamua kutafuta mbadala wake kwa kumleta Maurine, ni kama vile anaishi na mzimu wa Sarah. Mimi sioni umuhimu wa kushindana na mbadala wake.”

“Hiyo ni sawa. Kuna samaki wengi baharini,” Pamela alikubali. “Alvin ni tajiri, lakini ili iweje? Wewe mwenyewe una pesa zako pia."

“Inatosha.” Macho ya Charity yalimetameta kwa uzuri. "Ikiwa ni hivyo, tunapaswa kuwa na furaha usiku wa leo."

Wanawake hao watatu walikuwa na umri sawa, na juu ya ushawishi wa pombe, maongezi yalienda vizuri sana. Baada ya kunywa kwa muda, watatu hao walianza kucheza kwenye jukwaa. Lisa hakuwahi kujisikia huru zaidi ya alivyokuwa muda huo. Maisha yake yalikuwa yakimzunguka Alvin kwa muda mrefu. Kwa kweli, aliishi siku zake kwa mafadhaiko na bila uhuru. Sasa, hata akapata rafiki mpya. Labda huu ulikuwa mwanzo wa kitu kizuri.

Baa hiyo ilitembelewa tu na watu matajiri na mashuhuri zaidi. Mmoja wao kati ya umati wa watu alikuwa mwimbaji mwenye wafuasi wengi sana. Alitupia klipu ya video kwenye chaneli yake ya Youtube akichezana kila Lisa.

Maoni mengi kutoka kwa wafuasi wake yalitiririka.

[Nikicheza kwenye baa baada ya kugongana na malaika watatu kutoka mbinguni. Tonight's really worth it.]

[Wasichana ni warembo sana. Mmoja anaonekana kama mtoto mchanga wa rangi mchanganyiko, na mwingine ana sifa za urembo wa kawaida. Ni aibu kwamba aliyesimama katikati ana kovu usoni, lakini umbo lake ni la kushangaza.]

[Wow, ni mimi tu, au aliye katikati anafanana na mke wa Alvin Kimaro?]


[Lazima awe yeye.]


Baadaye, hashtag #Kimaro’sWifelnPub ilisambaa kwa kasi mtandaoni. Video hiyo hata ilipata kutazamwa mara nyingi chini ya nusu saa.

Alvin alikuwa ametoka kuoga wakati Maurine alipomwendea akiwa na glasi ya maziwa. "Bwana Kimaro, ngoja nikuchane nywele zako."

Alijaribu kunyoosha mkono lakini Alvin alikwepa haraka. "Hakuna haja ya hilo." Alikunywa glasi ya maziwa na kusema kwa upole, “Shuka chini. nitakuita nikikuhitaji.”

“Lakini…” Hakuweza kuficha wasiwasi machoni mwake. “Hupaswi kuachwa peke yako katika hali hii. Ninaweza kuweka kitanda changu pembeni…”

“Hapana.” Alikunja uso kabla ya kusema, “Hiki ndicho chumba ninacholala na mke wangu. Sipendi wanawake wengine kukaa hapa.”

“Samahani. Sikuwa nimefikiria kuhusu hilo.” Maurine akatingisha kichwa. Baada ya kutoka chumbani, aliuma midomo kwa kuudhika.

Alvin hakuvutiwa naye licha ya sura yake kuwa sawa na ya Sarah Langa Njau. Ni vile tu alitaka kutumia taswira ya Sarah ili aweze kupona ugonjwa wake. Hata hivyo, haikujalisha. Alikuwa katikati ya lengo lake hata hivyo.

Alvin alitabasamu huku akitazama glasi ya maziwa. Baada ya Maurine kuondoka, Alvin alirudi kitandani kuangalia WhatsApp. Hakukuwa na ujumbe wala taarifa mpya kutoka kwa Lisa au mitandao yake ya kijamii.

Mwanamke msumbufu huyu. Je, kweli alilamua kuondoka nyumbani na kumpuuza kwa sababu tu ya ugomvi mdogo? Alikuwa ameahidi kutumia maisha yake yote pamoja naye, lakini sasa, alimwacha peke yake nyumbani. Angewezaje? Alihisi uzito wa ghafla katika kifua chake.

Ili kujizuia kuangazia hilo, alifungua kurasa zake za mitandao ya kijamii. Uso wake mzuri ulianguka baada ya kuona hashtag hiyo maarufu, #Kimaro’sMastersWifelnPub. Kisha akabofya play kwenye klipu iliyokuwa ikivuma sana.

Ndani ya baa hiyo ya kupendeza, Lisa aliwekwa kati ya Pamela na Charity huku wakisakata dansi la kufa mtu jukwaani. Alikuwa amefunga shati lake kiunoni, akifunua kiuno chake kidogo na kitufe cha tumbo. Alionekana kama video-vixen mdogo.

Alvin alikuwa amekasirika sana hata akakaribia kumwaga damu. Lisa angeacha lini kufanya mambo kama hayo? Ilikuwa imepita siku moja tu tangu aondoke, kisha akaibuka akiwa anacheza dansi kwenye baa.
Ndo maana aliamua kumfungia ndani ya chumba cha upweke ili asitoke nje na kufanya mambo ya ajabu. Mapigo ya moyo wake yaliongezeka ndani ya sekunde chache.

Ghafla, simu yake iliita na kuiona namba ilitoka kwa Thomas Langa Njau. “Bwana Kimaro, lazima unisaidie. Dharau zake zimevuka mipaka safari hii. Alinipiga hadharani na kuniaibisha sana.”

Alvin alihisi kukereka, lakini alizuia hisia zake haraka. “Hilo lilitokea wapi?”

"Kwenye baa," Thomas alifoka. “Hata sikumfanya chochote, nilimkuta na mkeo wakimsengenya Sarah kuwa ni tapeli. Sikuweza kuvumilia zaidi kuhusu hilo, kwa hiyo nikaanza kubishana naye. Hapo ndipo aliponipiga.”

Alvin alikodoa macho. Charity kwa hakika alikuwa akitamani kifo chake. Kisha, Thomas akasema kwa sauti ya chini, “Kuna jambo lingine… sina uhakika kama niseme hivi, lakini Charity anamharibu mke wako. Yuko pamoja naye wanakunywa pombe usiku wa leo. Kweli, kwa kile ninachoweza kusema, Charity alikuwa akijaribu…”

“Inatosha. Niaifahamu vyema hiyo baa. Nitakuwepo hapo mara moja.”
Alvin akacheka kwa kujidharau. Hakutarajia kwamba Charity angejaribu kujenga urafiki na Lisa baada ya kushindwa kumsamehe. Hata hivyo, asingemsamehe kwa kumtumia mke wake kufikia malengo yake.

Alvin aliagiza helkopta imfuate haraka. Mara baada ya kubadilisha nguo, alishuka ngazi.

“Bwana Mkubwa, unaenda wapi?” Maurine alimuuliza.

“Nje.” Alitoka nje na kusubiri kwa dakika kadhaa kabla ya kusikia muunguro mzito wa helkopta angani. Helkopta ikatua kwenye uwanja mkubwa.

Alipoingia kwenye helkopta, aligundua kuwa Maurine alikuwa amejwahi kupanda kabla yake. Akaamuru kwa kukunja uso, “Teremka!”

“Hapana. Ni lazima niende nawe kutokana na hali yako kutokuwa shwari.” Maurine alitabasamu kwa uchungu. "Nina hakika unaweza kushindwa kujidhibiti."........ITAENDELEA...

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.