JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP..........................0628924768
SEHEMU YA................................236-237
Sura ya: 236
Hans akamkabidhi Lisa taarifa alizozikusanya kwenye kampuni ya Ngosha Corporation. “Kwa siku za karibuni, Damien amekuwa akitumia muda mwingi kushawishi wanahisa kumpa nafasi na Joel. Hata alimfukuza msaidizi aliyemwamini Joel kwa kisingizio cha uongo. Ndani ya kipindi cha nusu mwezi, alikuwa amechukua udhibiti kamili wa kampuni ya Ngosha Corporation.”
Lisa alizama katika mawazo ghafla baada ya kumsikiliza kwa makini.
“Bi Jones, hivi ndivyo ulivyotabiri. Wafanyabiashara wote wameshtushwa na Damien, yule mtu mlemavu, kwa kuanza kupigania madaraka ya kampuni wakati kaka yake akiwa hajitambui hospitalini.” Hans alivutiwa sana na Lisa. Machale ya mwanamke yanaweza kuwa ya kutisha sana wakati mwingine.
“Vipi kuhusu Melanie?” Lisa aliuliza ghafla.
“Kwa sasa yeye ni Makamu Mkurugenzi. Damien alimpa nafasi hiyo mara baada ya kuchukua udhibiti wa kampuni siku chache zilizopita. Inavyoonekana, wakati wa mikutano michache iliyopita ya wanahisa, Damien alitumia muda mwingi kuwashawishi wanahisa kumpatia nafasi hiyo Melanie.”
Lisa alianguka katika mawazo mazito. “Damien ana uhusiano gani hasa na Melani, kwanini amchukulie kwa uzito hivyo? Hata alimpa jukumu la kusimamia kampuni kubwa kama Ngosha Corporation! Kando na hilo, familia ya Ngosha na familia ya Campos wanapanga ushirikiano kwa njia ya ndoa, kuna nini ndani yake?”
Aliinua kichwa chake. “Hans, nifanyie umafia kidogo. Unaweza kupata nywele za Damien na Melanie kwa kipimo cha DNA?”
Hili lilimshangaza kidogo Hans. "Unashuku kwamba ... haiwezi kuwa hivyo. Nasikia jogoo wa Damien hapandi mtungi."
“Huoni ajabu? Kwanini Damien amuumize kaka yake wa damu ili kumpigania Nina na Melanie? Kwanini amjali sana binti wa kaka yake?”
Maneno yake yalimshawishi Hans. "Hakika, nitafuatilia hili mara moja."
Ilikuwa tayari saa sita mchana wakati Hans alipoondoka na kumwacha Lisa ofisini. Aliongea na Alvin kwa furaha kwenye simu. "Hubby, umekula chakula cha mchana?"
"Bado. Nilikuwa karibu kukupigia simu nikwambie kitu. Rodney alinialika tukale kwenye jumba lake jipya la kifahari,” alisema kwa upole. "Ninaweza kulala huko pia."
"Nina wasiwasi kuhusu wewe kukaa usiku kucha mbali na nyumbani peke yako." Lisa alikuwa na wasiwasi kweli.
“Usihofu, sitakuwa peke yangu. Rodney, Chester, na Maurine watakuwapo kunitunza.” Alvin akacheka. "Mwambie Shani akulete hapa mchana ikiwa utani’miss."
“Hakika,” Lisa alikubali bila kusita. Alionekana kushtuka lakini haraka akabadilisha mshangao na mawazo ya kutaniana. "Kwa kweli siwezi kuvumilia kuwa mbali nawe hata sekunde moja."
Maneno yake yalimfanya akose la kusema. “Sawa, siwezi kuvumilia kuwa mbali na wewe pia. Njoo baada ya kazi, sawa?"
Lisa alihisi kuchanganyikiwa sana baada ya kukata simu. Kwa kweli, haikuwa kwamba hakuweza kuvumilia kuwa mbali naye, bali alikuwa na wivu. Kila siku baada ya kuondoka kwenda kazini, Maurine alikuwa akiandamana naye siku nzima. Sasa, alikuwa akimtoa out mwanamke huyo ili kujumuika na marafiki zake. Ingawa lilikuwa jambo la kawaida, Lisa hakuweza kujizuia kuhisi wasiwasi kuhusu hilo.
•••
Saa 12:30 jioni, gari moja la kifahari lilipita kwenye lango na kuingia kwenye nyumba kubwa ya kifahari. Rodney na Chester walikuwa wamengoja mlangoni kwa muda mrefu. Hata hivyo, Maurine alipotoka kwenye kiti cha nyuma cha gari, wote wawili walishangaa. Rodney hasa alikodoa macho kumtazama mwanamke huyo.
“Anaitwa Maurine Langa.” Alvin alimtambulisha haraka haraka bila kufafanua zaidi.
“Maurine Langa, Sarah… Sarah Langa unamfahamu?” Rodney aliuliza kwa msisimko baada ya kusikia jina hilo.
“Unamfahamu pia Sarah? Mimi ni binamu ya Sarah.” Maurine alitabasamu na kufunua vishimo kwenye mashavu yake.
Machozi yalianza kumtoka Rodney, lakini aliyazuia kwa haraka. "Binamu ya Sarah ni binamu yangu pia."
“Ni nini kinaendelea?” Chester akamgeukia Alvin. “Kwanini unaambatana na binamu wa Sarah?”
“Yeye ndiye muuguzi aliyependekezwa na hospitali ya wagonjwa wa akili kwa jukumu la kunitunza,” Alvin alieleza kwa uthabiti.
“Sikujua.” Chester akaitikia kwa kichwa. "Anakuhudumiaje, Umekuwa ukijisikia vizuri?”
Hapo, Maurine aliyarudisha macho yake kumtazama Alvin kwa woga.
“Usijali,” Rodney alisema huku akimpigapiga kichwani. "Sitamruhusu akubadilishe."
Maurine alinyanyua kichwa na kutabasamu kinyonge na kumtazama Rodney. "Kama nikionekana sifai lazima nibadilishwe. Hakuna kisingizio cha kuvuruga matibabu ya Bwana Kimaro."
"Yupo vizuri." Alvin alimjibu kwa haraka kabla hajatangulia kuingia ndani.
Chester alimuuliza kwa sauti ya chini, “Haya, ulimchagua yeye kwa sababu hujamsahau Sarah?”
“Usiwaze kupita kiasi.” Alvin akatabasamu. “Unakumbuka jinsi nilivyopona maradhi yangu mara ya mwisho? Daktari alisema ugonjwa wangu ulitokana na kiwewe cha mfadhaiko wa utotoni, na Sarah ndiye pekee aliyekuwa chanzo cha furaha yangu katika kipindi hicho. Labda hisia za kwamba nipo karibu na Sarah zitanisaidia kupona mapema. Kwa kweli, tangu aje nimekuwa nikijisikia vizuri sana.”
"Lakini huna wasiwasi kwamba Lisa akiju ..."
"Hawezi kujua ikiwa nyinyi wawili hamtasema." Alimkodolea macho rafiki yake kama onyo. "Mkumbushe Rodney kukaa kimya kuhusu hili."
Chester alikunja uso lakini hakuzungumza zaidi kwani Sarah alikuwa ameshaaga dunia. Akaamua kubadili mada. “Alvin, nimesikia umeamua kufanya mambo kuwa magumu sana kwa Charity Njau, kwanini?”
“Si mbaya sana, nataka tu niifundishe familia ya Njau somo rahisi. Vipi kwani, bado unampenda?” Alvin alimuuliza kwa utani.
“Aaahaah!” Chester akaruka maili sita. “Ninachojutia zaidi ni kushea mapenzi na mwanamke msaliti kama yule. Mfunze kabisa adabu yake mbwa yule.”
“Basi mwache aisome namba safari hii.” Alvin alisema na kupotezea mada.
•••
Saa kumi na nusu jioni, Lisa alikuwa njiani kuelekea kwenye jumba hilo la kifahari la Rodney. Katikati ya safari, aliona Range Rover nyeupe ikiwa imekwama kwenye matope. Binti mmoja wa makamo kama yake alikuwa amesimama kando ya barabara. Alikuwa amevalia gauni refu jekundu chini ya koti jeusi, ambalo lilimpongeza umbo lake refu na lililopinda.
"Paki pembeni," Lisa alimwambia Shani.
Shani alikunja uso baada ya kumtupia jicho huyo binti. "Bi Jones, hatupaswi kuingilia mambo ya watu."
'Jua linazama na giza litaingia sasa hivi. Si salama kumwacha mwanamke mwenzetu amekwama barabarani peke yake.” Lisa akausukuma mlango na kutoka nje ya gari. “Unahitaji msaada?”
Binti huyo aligeuka, na alishangaa macho yao yalipokutana. Lisa naye alishtuka. Binti aliyekuwa mbele yake alikuwa amefunga nywele zake ndefu kwenye fundo, akionyesha shingo yake nyembamba na ngozi yake nzuri. Sio tu kwamba alikuwa na sura nzuri, lakini umbo lake maridadi pia lilikuwa nzuri. Alionekana kuvutia hata kwa wanawake wenzake.
“Wewe ni mrembo sana,” Lisa alimpongeza kwa dhati.
"Ni heshima kusifiwa na Bi. Kimaro." Tabasamu hafifu lilienea usoni mwa binti huyo.
“Unanifahamu?” Lisa alishangaa. "Kweli, watu wengi wameniona kupitia mkutano wa waandishi wa habari. Ni ngumu kusahau sura hii."
Yule binti alikunja uso kwa huzuni. "Nadhani uzuri wa ndani hushinda mwonekano wa mwili."
“Haha, nimekubali.” Lisa alicheka. “Ilikuweje ukazama hapa?”
"Gari langu lilikuwa karibu na ukingo nilipokuwa nikipita gari lingine sasa hivi na kwa bahati mbaya likazama kwenye matope. Nimejaribu mara kadhaa kuliondoa lakini bado nimeshindwa.” Alilazimisha tabasamu la uchungu.
Lisa akasogea ili aangalie kwa karibu. “Nadhani naweza kusaidia. Nipe funguo zako.” Yule binti alipitisha funguo zake kwa mashaka.
Lisa akaweka jiwe kubwa chini ya tairi kabla hajaingia ndani ya gari. Aliwasha gari, akaweka ‘four wheel drive’ na kukanyaga moto, na gari likatoka kwenye matope ndani ya sekunde chache.
“Sikujua Bi Kimaro kuwa ni mtaalamu wa magari. Asante." Dokezo la shukrani lilipita mbele ya macho ya binti huyo.
“Usijali, sisi ni wanawake lazima tusaidiane.” Lisa aligeuka kurudi kwenye gari lake. Shani haraka aliwasha gari na kuondoka.
Hata hivyo, wazo la ajabu likamjia kichwani Lisa. Shani alikuwa kando yake akimlinda tangu siku ya kwanza, lakini siku hiyo alibaki ndani ya gari bila wasiwasi. “Shani, unamfahamu huyo binti?”
“Ndiyo,” Shani alijibu baada ya kusitasita kwa muda mfupi. “Bi Mdogo, huyo binti si kama unavyofikiria. Ana sifa mbaya sana huko Nairobi. Ni bora ukijiweka mbali naye kabisa kuepusha matatizo.”
“Kweli?” Lisa hakukubali. Maneno ya watu si ya kukubali wakati mwingine. Mbali na hilo, tofauti na wanawake wengine matajiri huko Nairobi, binti huyo hakujitambulisha au kujaribu kujipendekeza kwa Lisa hata kama alijua kuhusu utambulisho wake kama mke wa Alvin. Huenda alikuwa na kiburi kidogo, lakini alikuwa na adabu. Watu kama yeye labda walipakaziwa sifa mbaya kwa sababu ya tabia zao za kipekee za kujitegemea.
Sura ya: 237
Ilikuwa yapata saa kumi na mbili jioni wakati Lisa alipofika kwenye jumba la kifahari la Rodney. Alitoka kwenye gari na kuelekea kwenye banda lililo karibu na bwawa la kuogelea. Akiwa njiani, alisikia wahudumu aliopishana nao wakinong'ona.
"Kile ambacho kilipaswa kuwa karamu ya vyakula vya Kizungu kimebadilishwa ghafla kuwa karamu ya nyama choma. Ni uharibifu ulioje wa vyakula ambavyo vilisafirishwa kutoka Ulaya?”
"Hasa, na karibu nusu ya chakula cha jioni kilikuwa tayari kimepikwa pia. Kwa kweli siwaelewi hawa matajiri.”
“Sawa, hatuna chaguo. Yote ni kwa sababu mgeni wa Alvin Kimaro, Bi Langa, anataka karamu ya nyama choma.”
“Anamdekeza kweli. Lakini nilifikiri Bwana Kimaro anampenda sana mke wake.”
“Pengine ni kwa ajili ya kujifurahisha tu na msichana mrembo. Hukuona mkewe alivyoharibika usoni?”
“Uko sahihi. Baada ya kuwatumikia matajiri hawa kwa muda mrefu, tumeona michepuko yao mingi sana.”
Upepo wa majira ya joto ulimpiga Lisa. Hata hivyo, alihisi baridi kali kuanzia kichwani hadi miguuni baada ya kusikia maneno yale ya wahudumu. Kama asingejua kuwa kuwa Alvin alikuwa pale, labda angefikiria wahudumu wale walikuwa wanajadili mtu mwingine.
Hata hivyo, kwanini mambo yalikuwa hivyo? Ingawa Alvin alikuwa ameweka nafasi moyoni mwake kwa ajili ya Sarah, bado alimpenda Lisa. Ukweli kwamba Sarah aliwahi kuwa mpenzi wake hakikuwa kitu ambacho kinaweza kubadilishwa. Lakini kwanini avutiwe na Maurine hata watu wahisi kuwa ni mchepuko wake? Au ni kwa sababu yeye aliharibika sura?
Simu ya mkononi ya Lisa ililia kwa sauti ya juu na kumtoa kwenyemawazo yakeake. Jina la Alvin lilikuwa likiangaza kwenye skrini. Lisa alilitazama jina la Alvin, moyo wake ukamwenda mbio sana. Alipoitikia simu hiyo, sauti ya kupendeza ya Alvin ilisikika. “Mbona bado haujafika?”
“Nitakuwa hapo baada ya dakika moja.” Lisa akajibu kifupi.
“Sawa.”
Mara baada ya Alvin kukata simu, Lisa alitulia na kujitahidi sana kupotezea mawazo yaliyokuwa yakimsumbua kichwani kuhusu Maurine. Labda ni wahudumu ambao hawakuelewa hali hiyo. Kwa kuzingatia kuwa alipitia mengi na Alvin, alipaswa kumwamini zaidi.
Dakika tatu baadaye, alimuona Alvin akiwa anamsubiri uwanjani. Kulikuwa na watu wanne kwa jumla - wanaume watatu na mwanamke mmoja.
Maurine, ambaye hakujitokeza katika umati hapo awali, sasa alikuwa amevaa nguo zilizompendeza sana, kana kwamba alikuwa amebadilika kutoka kuwa mtumwa hadi kuwa malkia.
Maurine na Alvin walikuwa wamesimama mbele ya jiko la nyama choma sambamba na Rodney aliyekuwa akiongea kwa furaha karibu nao. Kwa upande mwingine, Chester alikuwa ameshika glasi ya mvinyo huku akitabasamu upande wa pili wa jiko hilo, akigeuzageuza nyama kwenye moto.
Ghafla, Lisa alishikwa na mshangao. Ingawa Alvin alikuwa mume wake, na ukiachana na Sam, Lisa hakuwahi kuwa karibu sana na marafiki zake wengine. Akiwa mke aliyempenda mume wake sana, alitamani angechanganyika na marafiki wa mume wake.
Hata hivyo, Maurine alionekana kuzoeana na marafiki zake mapema kuliko yeye. Maurine alikuwa nani? Alikuwa tu muuguzi ambaye alikuwa akimhudumia Alvin kwa muda au kuna zaidi ya hilo? Lisa alishindwa kujua. Lisa alihisi kana kwamba kuna kitu alikuwa hakijui, na jambo hilo lilimfanya akose raha sana.
“Lisa…” Akiwa wa kwanza kati yao kumwona, Chester alimpungia mkono. Alvin akageuza kichwa chake na kumpungia mkono pia.
Kwa kulazimisha tabasamu, Lisa alimsogelea Alvin na kumshika mkono. "Kwa nini mlifikiria kuwa na karamu ya nyama choma usiku wa leo?"
"Unaipenda?" Alvin aliuliza bila mpangilio huku akitabasamu.
"Utabadilisha ikiwa nitakataa?" Lisa alikodoa macho na kumtazama. Alionekana kutania, lakini moyoni mwake alikuwa serious. Ni kwa sababu tu alisikia kutoka kwa wahudumu kuwa Maurine ndiye aliyependekeza karamu hiyo.
Alvin hapo awali alikuwa amebadilisha karamu ya vyakula vya kizungu kuwa ya choma nyama. Ikiwa angebadilisha tena. ..
Alvin alipapasa kichwa chake kwa kukosa maamuzi. Kabla hajajibu, Rodney alisema, “Tayari tumetayarisha kila kitu. Utakuwa ni usumbufu sana tukiibadilisha tena."
"Ikiwa unataka kitu tofauti, mjulishe tu mpishi. Atakuandalia” Alvin alibana kidole chake na kusema kwa sauti ya kuhimiza, “Rodney ameajiri wapishi bora kabisa nchini Kenya. Wanaweza kupika chochote.”
"Nilikuwa natania." Lisa alicheka. “Nitakula nyama choma ya mbuzi. Wewe unataka kula nini? Samaki ni sawa? Lakini nguruwe ndiyo favorite yako."
Alvin alisita kwa muda, lakini alipokuwa karibu kujibu, Rodney alisema,
“Ni sawa. Maurine tayari ametayarisha nyama ya nguruwe kwa ajili ya Alvin.”
Lisa alielekeza macho yake kwa Maurine, ambaye alikuwa ameshikilia vipande vya nyama ya nguruwe, nyama iliyokuwa ni kipenzi cha Alvin.
Lisa alihisi kuishiwa pozi. Mtazamo wa woga ukajidhihirisha juu ya uso wa Maurine. Alikuwa mwishoni mwa akili zake. “Pole, Bi. Kimaro. Sikujua ungefika mapema. Nitakuacha uendelee kumwandalia mumeo.”
Rodney hakuridhika na pendekezo la Maurine. “Siyo ishu kubwa Lisa, usichukie. Ni nyama tu ya nguruwe, sivyo? Maurine ndiye anayesimamia kumtunza Alvin. Hakuna haja ya kuchukia kuhusu hilo.”
"Kwani mimi nimechukia?" Lisa alimkazia macho Rodney kwa hasira. Siku zote alikuwa akimchukia, lakini alimchukia zaidi siku hiyo.
Mtazamo wake ulimfanya Rodney kuudhika. "Umekuwa ukimwangalia Maurine kwa hasira, na ikasababisha aingiwe na hofu."
"Hapana, Rodney," Maurine alisema mara moja kwa upole. "Bi. Kimaro hata hajanikasirikia. Mbona huwa tunaelewana vizuri tu."
Rodney alikoroma, “Kwanini unamuogopa sana?”
"Mimi simuogopi bwana!" Maurine aliongeza kwa tahadhari. "Ninaonyesha heshima yangu kwake."
"Heshima? Wewe ni muuguzi, na unalipwa kutekeleza majukumu yako.” Rodney aliendelea kumtetea Maurine.
Lisa alipandwa na hasira. "Bwana Shangwe, maneno yako yananifanya nionekane kama sijakaribishwa mahali hapa. Sijawahi kumtendea vibaya Maurine, tafadhali.”
“Bi. Mdogo, Bwana Shangwe, nyinyi…” Maurine alijibu kwa haraka, lakini Lisa akamkatisha kabla hajamaliza kuzungumza, “Kwa vile tunamlipa kufanya kazi, si ni jambo la busara kwake kuwa na heshima? Unawalipa wasaidizi wako wa nyumbani na walinzi pia kutunza nyumba yako, kwa hiyo ina maana wanaweza kukukosea heshima?”
Rodney alishindwa kujizuia pia. “Lisa, umemaliza? Nimekukosea? Kwanini unaendelea kunirushia maneno? Acha nikuambie kwamba Maurine ni tofauti na watu wengine…”
“Rodney.” Alvin akakatisha sentensi yake kwa sauti nzito. “Lisa ni mke wangu. Uwe na adabu kwa shemeji yako."
Lisa alikunja uso huku akiwaza Rodney alikuwa anapanga kusema nini tena. Tofauti na watu wengine? Maurine alikuwa tofauti vipi?
Rodney akajibu kwa uchungu, “Unapaswa kumdhibiti, basi. Ikiwa ana jambo la kusema, aseme tu badala ya kuwa mbishi sana.”
"Nilifikiri nimezungumza moja kwa moja na wala sikutia mafumbo hata kidogo," Lisa alibishana bila kujali.
“Wewe…” Rodney akakomea njiani baada ya kukosa cha kusema.
“Lisa, nichomee nyama.” Alvin alimvuta ghafla Lisa. “Twende huku.”
".. Sawa." Baada ya yote, Lisa alifikiria kuwa Rodney alikuwa rafiki wa Alvin. Ikiwa angeanzisha ugomvi kuhusu jambo hilo, isingemsaidia kitu. Kwa hivyo, alitikisa kichwa na kuelekea kwenye jiko la nyama choma upande mwingine.
Lakini, bado alikuwa katika hali mbaya. Hakusema lolote tangu alipofika, lakini Rodney alionekana kama amempania kwa namna fulani. Ghafla ilimwingia kichwani Lisa kwamba tabia ya Maurine ilijaa unafiki, ambao ulimkumbusha Lina.
"Nyama itaungua usipo igeuza," Alvin alimkumbusha. “Bado umekasirika?”
"Hapana. Nilikuwa nikifikiria jambo lingine.”
“Ulikuwa unafikiria nini? Unawezaje kutengwa wakati uko pamoja nami?" Alvin aliinua uso wake na kumtazama machoni.
“Nilikuwa najiuliza… Je, wauguzi siku hizi ni matajiri sana?” Lisa aliuliza ghafla. “Ameeweza kumudu mavazi ya gharama hivi kuanzia unyayoni hadi utosini, kwa hesabu ya haraka haraka hapo anaweza kuwa ametupia milioni na ushee, ukijumlisha na nywele.”
Alvin akamjibu bila kuwaza. "Tulipoenda kuvua samaki alasiri hii, Maurine alianguka majini kwa bahati mbaya. Rodney ndiye aliyemnunulia nguo hizo za kubadilisha.”
Lisa akiwa ameduwaa, midomo yake ikatengana kidogo.
“Angalia…” Alvin alicheka bila kujizuia. “Huniamini tu, huh? Una wivu kwa sababu ya Maurine. Angalia jinsi ulivyomtisha.”
Lisa alishindwa cha kusema. Ni saa ngapi alimtisha Maurine? Maurine alionekana kutojiamini ingawa Lisa hakusema neno. Je! lilikuwa kosa lake?
“Hata wewe unafikiri nilimtisha?” Lisa aliuliza baada ya kimya cha muda.”Labda anaogopa sura yangu mbaya.”
"Lisa, sahau kuhusu hilo." Alvin alimshika tena mikono. "Ninajua kuwa hujiamini, lakini hujui hisia zangu kwako?"
Baada ya kuelewa ujumbe wake, Lisa alirudia swali lake. “Unadhani hata mimi ninamuogopa?”
"Tunaweza kuacha mada hii?" Alvin alifungua chupa ya mvinyo na kumkabidhi. "Yeye ni muuguzi, hana maana yoyote kwenye moyo wangu."
Lisa alichukua mvinyo kimya kimya. "Rodney anavutiwa na Maurine?"
"Labda. Sina uhakika.” Alvin alibadilisha mada. "Ninahisi kula ndizi."
“Sawa.” Lisa alichukua ndizi akazimenya na kuziweka kwenye grill.
Muda mfupi baadaye, Chester alikuja na sahani ya nyama ya ngurwe iliyochomwa. Alisema kwa namna ya kutania, “Shemeji naomba nipate kibali chako. Alvin anaweza kula nyama ambayo mwanamke mwingine alichoma?”
"Hapana. Anaweza kula tu nyama nitakayomchomea,” Lisa alijibu kwa ukali......ITAENDELEA....
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA.
