JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP..........................0628924768
SEHEMU YA................................234-235
Sura ya: 234
Nuru ilizimika machoni mwa Alvin kwa sauti hiyo. "Inaweza kuwa ni bahati tu kwamba yuko hapa leo?"
"Inaonekana. Mabinti waliopendekezwa na wasimamizi wa hospitali hiyo ndio wauguzi wanaofanya vizuri zaidi kwa sasa.”
Aliitikia kwa kichwa baada ya kusikia hivyo, kigugumizi kwenye moyo wake kikatoweka. "Nani mkuu wa familia ya Njau sasa?"
"Charity Njau." Hans alijibu.
“Hakikisha KIM International na Alvinarah Media Network zinavunja mikataba yote ya ushirikiano na kampuni ya New Era Advertisings. Tutaona watapeleka wapi matangazo ya wateja wao. Nataka kumfunza somo Charity Njau kwa kuinyanyasa familia ya Langa.
Hans alikubali kwa utii na hakuongeza neno lolote.
Saa kumi na moja jioni Lisa aliondoka kazini mapema kuliko siku nyingine yoyote. Alisikia kelele kutoka kwa uwanja wa mpira wa vikapu mara tu aliposhuka kutoka kwenye gari.
Alitembea kwa wakati na kumuona Alvin akiinua mikono yake kutumbukiza mpira kwenye pete kufunga goli. Hakujua ni muda gani alikuwa akicheza mpira huo wa kikapu. Nyuma ya fulana yake nyeupe kulikuwa na unyevunyevu kidogo lakini uso wake ulionyesha hali ya jua.
Kumwona katika hali hiyo kulichukua pumzi yake. Alipokuwa bado shuleni, Ethan alikuwa mchezaji pekee wa mpira wa kikapu ambaye alisifiwa sana, lakini, akimtazama Alvin kwa wakati huo, aliona haiba ya kweli ya mwanamichezo.
“Naam!” Mfululizo wa makofi ya pongezi ulisikika kutoka upande wa pili wa uwanja. Hapo ndipo alipomwona yule mwanamke aliyelingana naye kiumri akiwa amevalia suruali ya jeans na top nyeupe. Nywele zake nyeusi zilizometa zilikuwa juu kwenye mkia wa farasi.
“Inavutia, Bwana Kimaro." Mwanamke huyo alitembea na chupa ya maji na kipande cha taulo. "Umecheza kwa dakika 40. Ni wakati wa kupumzika.”
“Sawa.” Alvin aliipokea ile chupa na kuanza kumeza vilivyomo ndani yake.
Miale ya jua la machweo iliwamulika wote wawili. Tukio hilo la aina fulani lilimchoma macho Lisa.
“Alvlisa…” Lisa aliita kabla ya kwenda haraka.
Alvin alitazama mwelekeo wa sauti hiyo na tabasamu likaenea katika uso wake wa kupendeza. "Baby, umefika nyumbani mapema leo."
"Nilirudi nyumbani mapema kwa kuhofia kuwa ungekuwa mpweke nyumbani peke yako." Alimtazama kwa karibu yule mwanamke mwingine. Alikuwa mrembo lakini hakuwa na kitu cha ajabu ikilinganishwa na yeye alivyokuwa zamani. Hata Melanie alikuwa mrembo zaidi ukilinganisha naye. Lisa alijisikia ahueni.
“Halo, Bi. Jones Mimi ndiye nesi niliyetumwa na hospitali kumuangalia Bwana Kimaro,” Maurine alijitambulisha huku akitabasamu.
“Oh, habari.” Lisa alishikwa na butwaa. Kwa sababu fulani, alihisi kana kwamba aliyaona macho hayo hapo awali lakini hakuweza kukumbuka ni wapi na lini.
“Ni heshima yangu kumwangalia Bwana Kimaro. Natumai atapona haraka iwezekanavyo.” Maurine alijieleza kitaaluma.
“Twende, naelekea ghorofani kuoga.” Alvin aliweka mkono begani kwa Lisa.
"Bwana Kimaro, unapaswa kupumzika kwa nusu saa baada ya kufanya mazoezi kabla ya kuoga," Maurine alimkumbusha.
“Sawa…” Alisita kabla ya kukubali.
Lisa alishangaa sana. Aliondoa fulana yake baada ya kupanda ghorofani. Alichukua taulo na kumpigapiga mgongoni. "Vipi mbona umeanza kucheza mpira wa kikapu ghafla?"
"Maurine Langa alisema kiasi kinachofaa cha mazoezi kinaweza kusaidia kupona kwa haraka na pia kuboresha ubora wa usingizi usiku."
“Maurine Langa?” Kitetemeshi kilipita kwenye uti wa mgongo wake.
Ni sadfa iliyoje! Aliwahi kuwa na mpenzi wa zamani mwenye jina la kati Langa pia. Sarah Langa!
“Ndio, kuna nini?” Akageuka kumtazama.
Lisa alichanganyikiwa sana. Hakuweza kusema kwamba alishituka kwa sababu jina la mwisho la nesi lilikuwa Langa. Hata hivyo, haikuwa sawa kujifanya kuwa mkarimu. “Sikutarajia ungemsikiliza msichana huyo kwa utiifu,” alisema huku akihema.
Alvin aliinua macho yake kabla ya kuinama ili kunusa midomo yake. "Hmm, nasikia harufu ya wivu."
“Nipo serious.” Akampiga kofi la mgongoni kwa utani.
Aliushika mkono wake mara moja na kuutoa kidogo. "Nisiingekuwa mtiifu hapo zamani na hata nisingekubali wazo la kuajiri muuguzi kutoka hospitali ya magonjwa ya akili. Hata hivyo, ninapenda nipone mapema kwa ajili yako, kwa hivyo ninahitaji kufanya kazi na mpango wa matibabu. Sitaki kufanya jambo lolote litakalokuumiza tena. Unaelewa?"
Aliuma midomo yake, ghafla akajisikia vibaya kwa kuwa na wivu sana. “Nimeelewa, lakini kwa nini usiajiri mtu ambaye ni mkubwa kidogo au labda nesi wa kiume? Nitakuwa nikifanya kazi ofisini na kukuacha peke yako nyumbani na msichana kweli?!”
Alvin alitabasamu kabla ya kuinua kichwa chake na macho yao yakagongana. “Una wivu kweli?”
“Alvin Kimaro!” Alimtazama kwa macho makavu.
“Usiwe na wivu bwana.” Alvin alimshusha wasiwasi. “Sekretari au mfanyakazi yeyote katika kampuni yangu ni mrembo kuliko yeye. Usingekuwa na nafasi ya kuwa Bi. Kimaro kama ningekuwa zoazoa fagio la chuma.” Alvin alijibu huku akitabasamu. “Sikuona ukiwa na wivu hivyo nilipokuwa na Melanie. Ulikuwa umekaa kimya kuhusu hilo.”
Aibu ilitanda usoni mwake alipofichua ukweli. “Siwezi kuwa na wasiwasi na hili. Naelekea chini kuandaa chakula cha jioni.” Akamtupia taulo na kuelekea kwenye ngazi.
Mara tu alipoingia jikoni, Maurine alimwendea na mpango wa lishe. "Bi. Mdogo, huu ni mpango wa lishe iliyoundwa mahsusi kwa ajili ya Bwana Kimaro. Kwa kuzingatia ugonjwa wake, ninapendekeza milo yake mikuu izingatie maelekezo haya.”
“Sawa, asante.” Lisa alipokea mpango wa chakula kabla hajauliza, "Je, tumewahi kukutana hapo awali?"
Maurine alionekana kushtuka lakini haraka akabadilisha mshangao huo na kutabasamu. "Sidhani. Hata hivyo ni mara yangu ya kwanza kukutana nawe, Bi. Kimaro. Lakini watu wengi wamesema kwamba wanaonekana kunifahamu.”
“Labda.” Lisa aliitikia kwa kichwa.
Lisa alitokea tena jikoni baada ya kupika chakula cha jioni, alimuona Alvin akiwa amekaa kwenye kochi huku Maurine akiwa amejiinamia kiunoni akijadiliana naye jambo kwa upole.
"Wakati wa chakula cha jioni," Lisa alimkumbusha.
Alvin akanyanyuka na kabla hajajonge mezani akatangaza, “Maurine na Shangazi Yasmine, kwa nini msijiunge nasi kwa mlo wa jioni wa leo?”
Hilo lilimshangaza Maurine. “Asante…” Alijibu huku akisitasita.
“Ni sawa. Usione haya wala woga. Kila mtu ni sawa katika zama za leo, na zaidi ya hayo, imekuwa ndefu kwako pia,” Lisa alisema kabla ya kugeuka kumwangalia Alvin.
Kwa kweli chakula cha jioni kilichangamka zaidi huku watu wale wanne wakiwa mezani. Hata hivyo, Lisa alikosa amani Maurine alipoendelea kumkumbusha Alvin ale nyama kidogo bali mboga na dagaa zaidi. Baada ya yote, yeye ndiye alikuwa na wajibu wa kusema maneno hayo. Kwa hivyo, ilikuwa ni ajabu sasa kwamba mtu mwingine alikuwa amechukua majukumu yake. Kwa kweli alijiona anazidi kuwa na wivu mkali.
Baada ya chakula cha jioni, yeye na Alvin walitembea ufukweni ili chakula kishuke vizuri tumboni. Waliporudi nyumbani, wote wawili walifanya kazi zao za ziada katika maktaba yao. Kwa kuwa Lisa alimaliza kazi yake mapema, alienda kuoga.
Alipotoka bafuni, aligundua kwamba Alvin alikuwa akinywa kitu kwenye glasi. Maurine alikuwa akimwangalia kwa makini pembeni. Mwanga wa taa ya manjano ulimulika juu yao kutoka darini kwa juu. Kuona jambo hilo kulimuumiza macho.
"Unakunywa nini?" Akasogea kuchungulia kwenye glasi yake. Kioevu cheupe kilionekana ndani yake, labda kilikuwa ni maziwa.
Maurine alieleza kwa upole, “Kunywa glasi ya maziwa kabla ya kulala huboresha ubora wa usingizi.”
“Asante, lakini hili ni jukumu langu,” Lisa alijibu kwa tabasamu hafifu.
Maurine alishikwa na butwaa kiasi kwamba uso wake ulipauka ghafla. Akiwa amechanganyikiwa, alitikisa kichwa kwa aibu. "Ndio, nitawaacha nyie wawili sasa."
Sura ya: 235
Maurine alimtazama Lisa kwa tahadhari kabla ya kufunga mlango nyuma yake.
Alvin alisema kwa kucheka, “Umemuogopesha binti huyo.”
Lisa alishindwa cha kusema. “Nilifanya nini cha kumuogopesha? Nilisema maneno hayo kwa uso wa kirafiki.”
"Hmm, lakini pia kwa sauti ya wivu sana." Alvin aliitikia kwa kichwa huku uso wake ukionekana kutojiweza. “Ni glasi tu ya maziwa. Hutakiwi kuwa na wivu juu yake.”
Maneno ya Alvin yalimfanya ajione kuwa ni mwanamke mwenye fikra finyu. Lisa alishusha pumzi ndefu huku akihisi mshangao mwingi ukimuandama.
“Acha kuwaza kupita kiasi. Ngoja nikukaushe nywele zako.” Alvin akachukua mashine ya kukaushia nywele.
Mara tu nywele zake zilipokauka, alipanda kitandani na uso wenye haya. Tangu wapatane, alikuwa na shauku kubwa ya kufanya mapenzi kitandani, lakini bado aliona aibu kila alipojiwazia. Hata hivyo, alijilaza tu kitandani kwa utulivu baada ya kuzima taa usiku huo. Hamu yake iliyofichika haikuwa ya kawaida. Lisa akaanza uchokozi wa makusudi. Akageuka juu juu juu na kumkandamiza Alvin na makalio yake.
"Tulia basi tulale." Alvin aliyekuwa amegeuziwa makalio na kumkandamiza ipasavyo kwenye ikulu yake akampigapiga tu mgongoni na kumpoza kwa sauti yake ya upole.
Lisa hakuamini masikio yake. Aliuma midomo yake na kuizungushia mikono yake shingoni mwake. “Alvlisa…” Lisa aliita taratibu. Ukiacha sauti yake iliyotetema kwa huba, uso wake wote ulikuwa ukizungumza mapenzi tu. Kwa bahati nzuri, Alvin hakuweza kuuona kwa sababu taa zilikuwa zimezimwa.
Hili lilimshangaza sana Alvin. Mshawasha ukatekenya kunako makao makuu yake, lakini alizuia shauku yake mara moja. “Maurine alinikumbusha kwamba dawa ninazotumia haziniruhusu nifanye hivyo kwa sasa. Ni bora tusitishe jambo hili kwa sasa.” Unyonge ulionekana katika sauti yake.
Lisa alionekana kushtuka. “Lakini kabla… Sote tulikuwa wazuri. Sio lazima, sivyo?"
“Unanitaka sana hivyo?” ghafla alisema kwa mahaba mazito.
Lisa aligeuka tu bila kujibu. Alitaka ndiyo lakini hakutaka kujirahisha sana, alihitaji kudumisha kiburi chake pia. Alitaka abembelezwe kwanza ndipo atoe!
Alvin akamkumbatia kwa nyuma. “Kuwa mvumilivu. Siwezi kufanya chochote ambacho kinaweza kunisisimua kupita kiasi kwa sasa. Ninaogopa nitafanya kitu nje ya udhibiti wangu ambacho kinaweza kukuumiza. Kama mara ya mwisho."
Lisa aliuma midomo yake, alikasirika, na mwishowe akanung'unika "sawa" baada ya muda mrefu. Usiku ule hakupata usingizi huku Alvin akipitiwa na usingizi mzito. Mawazo yake yalikuwa yakimshawishi kwamba labda nadharia ya Maurine ilikuwa sahihi. Baada ya yote, alikuwa akisumbuliwa na usingizi tangu aanze kupandisha wazimu. Muda ulikuwa umepita tangu amwone amelala vizuri sana.
Siku iliyofuata, Lisa alipokea simu kutoka hospitalini. Inavyoonekana, daktari bingwa wa mfumo wa neva, Daktari Angelo kutoka nje ya nchi alikuwa amefika kumtibu Joel. Bila kupoteza muda, alieelekea hospitali mara moja. Bibi na Babu Ngosha walikuwa tayari wameshafika.
Dk. Angelo alikuwa amemaliza uchunguzi wa Joel. "Ninahitaji kumtibu kwa kudhibiti mishipa yake kwa muda mrefu. Bado kuna matumaini kwamba Bw. Ngosha atatoka katika hali ya kukosa fahamu, lakini huenda ikawa ni safari ndefu. Muda mfupi zaidi labda utakuwa nusu mwaka hadi mwaka mzima.
"Asante sana." Lisa alishukuru.
“Usijali. Wewe ni rafiki wa Chester, kwa hiyo nitafanya kila niwezalo kukusaidia.” Dk. Angelo alisema.
Baada ya kutafakari kwa ufupi, Lisa aliomba, “Dokta Angelo, ikiwa mtu atakuja kuuliza kuhusu hali yake, tafadhali mwambie kwamba Bw. Ngosha atarudiwa na fahamu ndani ya mwezi mmoja.”
Daktari alisita kwa sekunde kadhaa kabla ya kutikisa kichwa. “Hakika.”
Baada ya daktari kuondoka, Mzee Ngosha hakuweza kupinga kuuliza, “Unajaribu kuchunguza kama kuna mtu alipanga kumuua baba yako?”
"Babu, unadhani ni nani anayeweza kuwa mhusika?" Aliuliza.
Mzee alikaa kimya kwa muda. Uchunguzi wa maiti ya dereva wa lori ulionyesha kwamba alikuwa alisinzia kwa sababu ya matumizi ya dawa za kulevya. Hata hivyo, mwanamume huyo hakuwa mraibu na alikuwa ametumia tu dawa hiyo kimakosa. Kwa wazi, hili lilikuwa tendo la makusudi.
“Nina uhakika ni Nina.” Mzee Ngosha alifoka kwa hasira. "Baada tu ya ajali amemwingiza Melanie kufanya kazi katika Kampuni ya Ngosha."
Lisa alikubali kwa kichwa. “Ikiwa ni hivyo, atahakikisha kwamba baba yangu hataamka kamwe. Kwa sababu hiyo ndiyo njia pekee itakayomwezesha kurithi kila kitu alichoacha nyuma. Kando na hilo, ikiwa mtu mwingine yuko nyuma ya hili, mtu huyo bila shaka atajaribu kuchukua udhibiti wa Ngosha Corporation ndani ya mwezi huu. Nina hakika mhalifu atafichua asili yake hivi karibuni.”
Mzee Ngosha na Bibi Ngosha walishangaa kusikia hivyo. Kwa mara ya kwanza, walimtazama mjukuu huyo wa kike mwenye mawazo ya kuvutia kwa umakini.
"Kitu kimoja zaidi. Usimwambie mtu yeyote nilichokuambia leo, pamoja na Bam’dogo Damien.” Lisa alitoa angalizo.
Mzee alishtuka. "Unamaanisha nini? Kwamba tunapaswa kumshuku Damien pia?”
"Hawezi kuwa Damien." Bibi Ngosha akatikisa kichwa mara moja. "Hali ya miguu yake imemfanya kuwa dhaifu na mgonjwa tangu utoto.”
“Umenielewa vibaya. Ninaogopa kwamba Bam’dogo Damien anaweza kudanganywa kwa urahisi kwa sababu ya madhaifu yake ya kuzaliwa. Kadiri watu wachache wanavyojua kuhusu hili, ndivyo itakavyokuwa bora zaidi,” Lisa alisema huku akitabasamu.
Kielelezo cha wasiwasi kwenye uso wa wanandoa hao wazee hatimaye kilipungua. Waliitikia kwa kichwa kuafiki kabla ya kuondoka hospitalini.
Shani, ambaye alikuwa akimlinda Lisa pembeni, hakuweza kujizuia kuuliza, “Kwanini hukuwaambia kwamba unamshuku pia Damien Ngosha?”
“Hawataniamini. Isitoshe, mimi ni mjukuu wao tu, na Damien ni mwana wao. Ninahitaji kuwaonyesha ukweli badala ya kuwashawishi kwa maneno matupu.” Kisha, akaingia kwenye gari.
Shani alishtuka alipotazama umakini wa mwanamke huyo. Ikamjia akilini kwamba Lisa alizidi kufana na Alvin kitabia.
Punde Nina akasikia habari za Joel akitibiwa na Dk. Angelo. Alikaribia kupoteza akili aliposikia hilo. Mara moja, alipiga namba ambayo haikuseviwa kwenye simu yake. "Joel atapata fahamu ndani ya mwezi mmoja."
"Tulia. Huenda huu ukawa mtego wa Lisa.”
“Lakini Daktari Angelo ana uwezo kwelikweli. Amesaidia wagonjwa kadhaa kutoka katika hali ya kukosa fahamu,” alisema huku akifadhaika. "Joel hakika atanishuku mara tu atakapoamka, na atanitaliki. Huenda nisipate hata senti kama hilo likitokea.”
“Usijali. Nitajitahidi niwezavyo kuchukua kampuni ya Ngosha ndani ya mwezi huu.”
"Kwa hivyo utafanya nini? Sitapewa senti hata moja ya kampuni.” Nina aliuma meno. “Kwanini hukumuua?”
"Usijali ... atakufa."
“Naweza tu kuweka imani yangu kwako. Yote haya ni kwa ajili ya msichana wetu kipenzi, Mel.” Nina ghafla akasitisha maneno yake..
Alipokata simu tu, mlango ukafunguliwa. Melanie alikuwa amesimama kando ya mlango, uso wake ukiwa umepauka kama mzimu. “Mama, nani alikuwa kwenye simu? Unajaribu kumuua nani? Baba?”
Uso wa Nina ulibadilika ghafla. “Usiingize pua yako katika hili. Sasa ni saa ngapi? Mbona haupo ofisini?”
“Mama acha kujaribu kubadilisha mada. Nilisikia yote.” Melanie alimtazama mama yake kwa hofu. “Ni kweli wewe ulikodi mtu kusababisha ajali ya baba? Mama, ungewezaje kufanya hivyo? Yeye ni mume wako. Pia, unamaanisha nini unaposema 'msichana wetu kipenzi Mel'? Mimi si binti wa baba?”
“Nyamaza. Yeye si mume wangu.” Nina alijua hakuna haja ya kuweka siri hii tena. "Hiyo ni sawa. Yeye si baba yako.”
Melanie alishtuka sana. "Hiyo haiwezekani. Hapana. Joel Ngosha ni baba yangu!
“Melanie, sikiliza. Baba yako alitaka kunitaliki muda si mrefu uliopita. Alikuwa anaenda kukupa 5% tu ya hisa za Ngosha Corporation, lakini 35% kwa Lisa. Nimefanya haya yote kwa ajili yako,” Nina alifoka huku machozi yakimtoka na kumshika bintiye mabegani.
Macho ya Melanie yalijaa chuki. “Baba yangu… Kwanini? Kwanini anifanyie hivyo?”
"Kweli," Nina alisema kwa huzuni. "Sote wawili hatungekuwa na nafasi katika jumuiya ya matajir ya Nairobi ukiwa na 5% tu ya hisa. Hata Jerome angebadili mawazo yake kuhusu kuwa na wewe.”
Melanie aliuma midomo yake. Hakutaka kupata uchungu wa kuachwa tena. "Mama, kwa nini kila mtu ana upendeleo kwa Lisa? Je, mimi si binti wa baba kweli? Kwa hiyo baba yangu ni nani?"
“Acha kulia. Baba yako anakupigania upate kampuni ya Ngosha." Nina alimkumbatia bintiye karibu. "Utajua ukweli hivi karibuni.".....ITAENDELEA....
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA
