JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP..........................0628924768
SEHEMU YA................................232-233
Sura ya: 232
“Nini?” Jerome alipiga kelele kwa hasira, "Nimewekeza sana katika uzalishaji wake na sasa unataka nipate hasara kubwa?"
“Hasara gani kubwa? Hamjavuna faida ya kutosha kabla ya hili?” Jack alisugua kichwa chake. "Isitoshe, niambie ukweli, je, familia ya Campos ilivujisha picha za maisha ya Alvin?"
“Una wazimu kumuamini Lisa? Mtu wa nje kama mimi angewezaje kupata picha hizo?" Jerome alishangaa.
Jack alikaa kimya huku taswira ya baba yake ikiingia kichwani mwake. Lakini kwa mawazo ya pili, ilionekana kuwa haiwezekani kwamba Mason Campos ambaye siku zote alikuwa hajali mambo hayo angefanya kitu kama hicho. “Hata hivyo, kila mtu katika familia ya Kimaro anashuku kuwa mimi ndiye niliyesababisha haya. Alvin ataniangamiza mara tu atakapopata tena ushindi wa juu.”
“Usijali. Utapata hisa za mama yako mwishoni kwa njia fulani. Jerome alikata simu hii na kupiga nyingine baada ya hapo. "Mpango haukufaulu." “Hmm, nilidharau ujasiri wa Alvin na Mzee Kimaro. Sembuse huyo mwanamke Lisa.”
Jerome alikaza macho yake. Alikuwa ameangalia historia ya Lisa hapo awali. Mwanamke huyu aliibuka hivi karibuni tu kuwa mwenyekiti wa Mawenzi Investments. Alikuwa binti mdogo tu kutoka Tanzania. Hata hivyo, wakati wa kipindi cha moja kwa moja cha jana yake, mwanamke huyo alidumisha utulivu wakati akizungumza na taifa zima la Kenya—bila kusahau mawazo yake makali na ya kufikirisha huku akiipa changamoto familia yenye nguvu zaidi ya Kimaro.
Haikuwa makosa kusema kwamba Lisa alikuwa ameongoza kampuni ya Alvinarah kupitia shida hii wakati Alvin akiwa mgonjwa. Kwa sababu fulani, ilimkumbusha kuhusu mchumba wake, Melanie. Walikuwa dada wa kambo kutoka kwa baba mmoja lakini Melanie alikuwa kama mjinga.
“Kwa hiyo, nini kinachofuata?” Jerome aliuliza.
"Kwa bahati nzuri, nina mpango mbadala. Ni wakati wa kumpeleka kwenye uwanja wa vita." Mtu yule kwenye simu alijibu.
“Sawa. Nina imani na wewe kabisa.” Jerome alijibu kwa unyenyekevu. Alisikiliza mawazo ya kimkakati ya huyo mtu mwingine kwenye simu. Bila shaka, familia ya Campos ingekuwa familia yenye nguvu zaidi nchini Kenya kwa muda mfupi. Enzi ya familia ya Kimaro… ilikuwa inakaribia mwisho.
•••
Siku iliyofuata, Bibi Kimaro alimpelekea Alvin fomu ya uhamisho wa umiliki wa hisa kwenye jumba lake la kifahari ufukweni mwa bahari huko mombasa. Alipoingia ndani ya nyumba hiyo, aliona hakuna mtu mwingine ndani ya nyumba hiyo isipokuwa Aunty Yasmine ambaye alikuwa akisafisha sakafu.
“Alvin yuko wapi? Ametoka?”
"Bwana Mkubwa na Mkewe wameenda kununua mboga kwenye duka kubwa lililo jirani." Shangazi Yasmine alipiga goti ili kumsalimia yule kikongwe.
"Kununua mboga?" Maneno yale yalimponyoka kinywani Bibi Kimaro bila kujijua. Asingeweza kuamini kuwa mjukuu wake alikuwa ameenda kununua mboga ikiwa asingesikia kwa masikio yake mwenyewe.
"Alikuwa na matatizo ya ugonjwa siku mbili tu zilizopita. Anapaswa kupumzika nyumbani. Kwanini hukumzuia kutoka nje?”
“Usijali Bi Mkubwa. Bwana Kimaro hana tatizo kabisa na huchangamka sana anapokuwa na mkewe.” Kabla sauti yake haijakatika, vicheko vya furaha vilisikika kutoka nje.
Bibi Kimaro alitazama kupitia dirishani. Wanandoa wachanga walioshikana mikono walikuwa wakitembea kuelekea nyumbani. Nywele ndefu za Lisa zilining'inia mabegani mwake. Umbo lake zuri liliweza kuonekana licha ya suruali ya jeans ya mguu mpana na fulana nyeusi aliyokuwa amevaa. Pia alikuwa amevalia jozi ya viatu vyeupe vya turubai. Alionekana nadhifu na mchangamfu.
Karibu naye, Alvin alionekana mtanashati na mwenye furaha akiwa amevalia mavazi meupe ya kawaida. Alikuwa ameshika mifuko miwili ya shopping huku uso wake ukiwa na tabasamu la kupendeza. Wenzi hao walionekana kama watu waliooana hivi karibuni. Hasa, hakuonekana kama mtu ambaye alikuwa na tatizo lolote la akili.
Yule kikongwe alipigwa na butwaa kabisa kumuona. Ilikuwa ni muda mrefu sana kwamba hakuweza kukumbuka mara ya mwisho alipomwona akiwa na furaha hivi.
Bibi Kimaro alikuwa amejitayarisha hata kwa ukichaa wa Alvin akiwa njiani kwenda kwake. Hakika ilikuwa ni kutokana na matarajio yake kumuona katika hali hii ya utulivu na uchangamfu.
Wenzi hao wachanga walipomwona yule mwanamke mzee walipoingia ndani ya nyumba, mara tabasamu usoni mwa Alvin likatoweka. Macho yake yalionyesha uhasama na kujihami. Bibi Kimaro alihisi kana kwamba sindano imeuchoma moyo wake.
“Habari, Bibi,” Lisa alimsalimia mwanamke huyo mzee kwa upole kana kwamba hakuna jambo lolote baya lililokuwa limetokea kati yao hapo awali.
Bibi Kimaro alimpa tu mtazamo wa kijeuri, akikataa kujibu salamu yake.
Hasira ikawaka usoni mwa Alvin. “Kama umekuja kumkosea heshima mke wangu, tafadhali ondoka.”
“Wewe...” Bibi Kimaro aligugumia kwa hasira. “Mimi ni bibi yako. Utafurahi tu baada ya mimi kufa?"
“Ninachojua ni familia ya Kimaro ndiyo iliyonimwagia chumvi kwenye kidonda changu. Ningekuwa nimenaswa kwa nguvu katika hospitali ya magonjwa ya akili kama si Lisa.” Alvin alitabasamu kwa uchungu. "Ikiwa nyote bado mnaniona kama familia, basi kitu kidogo kabisa mnachoweza kufanya ni kumwonyesha heshima."
Bibi Kimaro alionekana kuchanganyikiwa. Lisa alisema kwa upole alipoona hivyo, “Bibi, mimi ndiye ninayepaswa kuwa na hasira kwa sababu uso wangu umeharibika kutokana na familia yako. Je, ninastahili mambo yote mabaya kwa sababu sitoki katika malezi yenye nguvu kama familia ya Kimaro?”
Bibi Kimaro alipasua midomo yake kutaka kusema kitu lakini Alvin alimkatisha kabla hajapata nafasi. “Mimi ndiye nimekuwa nikimsumbua tangu mwanzo hivyo acha kudhani kuwa ni mwanamke mlaghai. Hakuwa anajua mimi ni nani alipokutana nami mara ya kwanza. Pia nilichumbiana na Melanie baadaye ili tu kumfanya aone wivu.”
“Unawezaje kumfanyia hivyo Melanie?” Sauti ya kikongwe ilidhihirisha kutofurahishwa kwake.
"Ikiwa unampenda sana, basi mchukue kama mjukuu wako." Macho ya Alvin yalionekana kuwa makali kama moto. “Nilifanya mambo hayo kwa kukuridhisha tu. Melanie ni msichana mzuri—”
“Na Lisa je?” Bibi Kimaro alimkatiza bila subira kwa sauti ya ukali, “Wote wawili ni mabinti wa Joel Ngosha.”
“Lisa alikosea nini?” Alvin alidakia. “Je, alichagua familia aliyozaliwa? Hakuwahi kukumbana na mapenzi ya baba yake tangu akiwa mdogo lakini sasa kwa vile hatimaye ameungana na baba yake, kila mtu anamdharau. Kwa kweli, yeye ni mkubwa kuliko Melanie na mama yake ndiye aliyeachwa na Joel. Yeye ndiye mwathirika wa kweli hapa."
Bibi Kimaro hakuwa na maneno ya kubishana naye.
Alipohisi hali ya mvutano ikizidi kushamiri, Lisa alipendekeza, “Inakaribia saa sita mchana. Nyie wawili mnapaswa kuelewana nami nitaelekea jikoni kuandaa chakula cha mchana. Bibi, tafadhali kaa kwa chakula cha mchana.”
"Ikiwa unabaki tu ili uendelee kumshambulia mke wangu, basi ni bora ungeondoka tu," Alvin alisema kwa upole.
Bibi Kimaro aliona aibu sana kwa sauti ile. “Unadhani L-”
“Alvin, si rahisi kwa Bibi kufanya safari ndefu hivyo kuja hapa katika umri wake. Afadhali ukae kimya,” Lisa alifoka, na kufanya mambo yasiwe magumu kwa yule mzee. Alvin alikoroma, na Bibi Kimaro naye akakaa kimya.
Baada ya Lisa kutokomea jikoni, Bibi Kimaro alimuagiza mwanasheria atoe fomu ya kuhamisha umiliki wa hisa. “Hii imetoka kwa babu yako. Utakuwa na udhibiti kamili wa KIM International baada ya kusaini hii. Mimi na babu yako hatutaingilia mambo ya kampuni kuanzia hapo.”
Alvin akasaini karatasi bila kusita. “Siyo tu kwamba mam’dogo Valerie hajaboresha biashara ya KIM Insurance tangu achukue kitengo hicho, lakini mauzo yameshuka kiwango cha chini zaidi. Anapaswa kustaafu mapema, kuketi, na kufurahia bonasi za kila mwaka nyumbani.”
Bibi Kimaro alionekana kushtuka kabla ya kupiga kelele, “Unafanya hivi kumlipishia kisasi kwa sababu alisababisha Lisa kuharibika usoni…”
“Kwa hivyo itakuwaje kama hiyo ni kweli? Unamvumilia hata baada ya kusababisha madhara kwa mtu mwingine kwa sababu tu ni binti yako? Lakini yeye si binti yangu,” Alvin alijibu bila kujali.
“Lakini yeye ni mam’dogo wako, hata hivyo…” Bibi Kimaro akashusha pumzi ndefu. "Mbali na hilo, mauzo yake yaliimarika mwezi uliopita…”
Sura ya: 233
'Hiyo ni kwa sababu Nina Mahewa aliwekeza shilingi bilioni kadhaa." Macho ya Alvin yalidhihirisha dhamira ya hatari. “Ikiwa nilikisia kwa usahihi, alifanya hivyo baada ya mam’dogo Valerie kukubali kuharibu uso wa Lisa. Anadanganya takwimu za mauzo." Akiwa amepigwa na butwaa, Bibi Kimaro akakosa cha kusema.
“Bibi, unapaswa kushukuru. Nisingemuacha hai kama si wewe na babu.”
Alvin akainuka. “Angalia mwanao Spencer na binti zako. Mmoja wao anajali tu kusaidia familia ya mumewe, mwingine anadanganya mauzo. Mwanao pekee wa kiume ni dhaifu na hana uwezo. Unafikiri wewe na babu mngeweza kufurahia uzee wenu kwa mali mlizonazo sasa kama si mimi?” Bibi Kimaro alionekana kuwa mzee kwa miaka michache zaidi baada ya kusikia hivyo.
Saa sita kamili mchana, Lisa alitokea tena jikoni baada ya kuandaa chakula cha mchana lakini mvutano kati ya Alvin na bibi yake ulionekana kuongezeka. Alitenga chakula na kumkaribisha Bibi Kimaro mezani.
Mwisho bibi yule alionekana kushangazwa na vyakula vilivyowekwa mbele yake. Kila mlo haukuwa mzuri tu bali ulikuwa na ladha ya kupikwa nyumbani kuliko vile vya wapishi wa familia ya Kimaro. Aligundua kwamba Alvin, ambaye hakuwahi kufurahia chakula, alikuwa akila kila chakula—hasa nyama ya nguruwe.
Bibi alijaribu kipande kidogo cha nyama ya nguruwe. Walahi alitamani aachiwe sahani zote peke yake. Bakuli la nyama lilikuwa karibu kuisha alipofikia kipande cha pili.
“Usimalize yote. Bibi bado hajala vya kutosha.” Lisa akasogeza bakuli la nyama ya nguruwe kuelekea kwa Bibi Kimaro.
Alvin alikunja uso. “Kwanini hukujitayarisha nyingi?”
"Ulikula jana usiku na unataka tena mchana huu? Si afya kula nyama ya nguruwe kupita kiasi.” Aliweka mbogamboga badala yake kwenye sahani yake. “Ni muhimu kuwa na lishe bora na sio kuchagua. Ukiendeleza tabia hiyo mbaya, basi sitakupikia tena.” Lisa alimuonya.
“Sawa, nimekusikia.”
Chini ya macho ya Bibi Kimaro, mjukuu wake alianza kula mbogamboga. Mtu ambaye alikula vijiko vichache vya chakula kwa siku alikuwa akila sahani nzima wakati huu. Hata yule kikongwe alikuwa na hamu ya kula alipomwona mjukuu wake akila kwa hamu vile. Mwishowe, chakula cha mchana kilichotosha watu sita kilimalizwa na wale watatu.
Baada ya chakula cha mchana, Lisa alitenga majagi mawili ya mtindi kwenye meza. Aunty Yasmine alisema huku akitabasamu. “Hii pia imetengenezwa kwa mikono na Bi. Jones. Ni mtindi na asali na jamu safi ya strawberry ambayo aliiandaa polepole kwa masaa mawili. Alisema kunywa glasi ya mtindi baada ya mlo ni vizuri kwa usagaji chakula na kusafisha matumbo.”
Bibi Kimaro alionja kidogo kisha akanongewa tena. Mtindi ulikuwa mtamu sana. Alijisikia kuongeza glasi nyingine! lakini alikuwa na aibu sana kuomba kuongezewa.
Hata hivyo, Alvin hakuona aibu hata kidogo kuomba huduma nyingine mara baada ya hapo. Ombi lake lilikataliwa na Lisa. "Huwezi kunywa mtindi mwingi au unaweza kuvimbiwa."
"Una shida gani?" Alikunja uso lakini hakuzungumza zaidi.
Ingawa hakumpenda sana Lisa, Bibi Kimaro ilibidi akubali kwamba binti huyo alikuwa amembadilisha Alvin kuwa bora. Labda ugonjwa wa Alvin ungeimarika, kama hapo awali…
Baada ya chakula, Bibi Kimaro alisimama na kuaga ili kuondoka. “Asante kwa chakula wajukuu zangu, nimekula, nimefurahia na nimeshiba. Ni wakati wa mimi kuondoka.”
"Unaweza kukaa kwa siku chache zaidi. Kutembea na kupunga upepo baharini kunastarehesha kweli,” Lisa alisema kwa tabasamu hafifu.
Bibi Kimaro alijisikia vibaya kuona jinsi mwanamke huyo alivyoharibika usoni. “Ni sawa. Babu yako hajazoea kuwa mbali na mimi.” Baada ya kutulia kwa sekunde chache, aliendelea kusema, “Asante kwa ukarimu wako leo.”
Lisa alishangaa kusikia hivyo. Bado alikuwa akitabasamu hata baada ya yule kikongwe kuondoka zake.
Alvin alimkumbatia kwa upendo. “Bibi yangu alikutendea vibaya lakini bado ulijaribu sana kumfurahisha kwa chakula cha mchana na mtindi. Anafikiri kukushukuru mara moja ni fidia ya kutosha?"
“Ni kwa sababu yeye ni bibi yako.” Aligeuka na kuifunga mikono yake shingoni. “Ulimwambia maneno makali lakini bado najua unawajali sana babu na babi yako. Vinginevyo, usingeichukua KIM International tena. Una wasiwasi kwamba wanandoa hawa ambao wameishi maisha ya kitajiri wakati wote wangedhihakiwa na wengine katika uzee wao ikiwa KIM itaanguka?"
Alvin aliinua nmacho yake kinyonge. Hakuna mtu aliyemjua vizuri kuliko yeye.
“Alvlisa, nilikuwa na bibi pia. Ni pale tu alipotangulia mbele ya haki ndipo nilijuta kutotumia muda mwingi kuwa naye. Familia ni damu halisi na ni ngumu sana kuiondoa. Kwa sababu yako, ninaweza kujaribu kuwavumilia na kuwasamehe. Ilimradi utafurahi.” Kwa macho makali, Lisa alimtazama Alvin usoni.
Alvin alimsukuma ukutani. Hisia ambazo zilikuwa zimelala ndani ya moyo wake zililipuka kama volkano. Aliinamisha kichwa chake ili kumbusu kwa mahaba kwenye midomo. "Samahani, Lisa. Kwa ajili ya familia yangu kukuumiza.”
Uso wake uliharibiwa na familia ya Kimaro lakini bado aliwavumilia kwa ajili yake. Hata hivyo haikuwa imepita hivihivi tu. Aliahidi kuwalipa kwa yale waliyomfanyia.
"Siku moja, tutatapa mtu wa kutibu uso wako. Nitakupenda maisha yangu yote.”
Lisa alifunga macho yake karibu. Wakati huo huo, alihisi nguvu na utulivu. Haijalishi uso wake ulikuwa umeharibika vipi, kilichokuwa muhimu ni kwamba hakujali.
Siku iliyofuata, Lisa akaenda kufanya kazi katika kampuni yake. Alikuwa akitoka Mombasa hadi Nairobi na kurudi kwa ndege kila alipotaka kwenda ofisini kwake.
Alipotoka tu, Hans alijitokeza nyumbani kwa Alvin akiwa na wauguzi wachache. Kulikuwa na sura ya wasiwasi usoni mwake aliposema, "Bwana Kimaro, hawa ni wauguzi waliochaguliwa na mkurugenzi wa hospitali."
Alvin aliyekuwa anasoma kitabu cha hadithi za Jomba Wajo aliinua kichwa chake. Ugonjwa wake wa akili haukuwa kitu ambacho kingeweza kuponywa kwa siku kadhaa. Lisa alikuwa na kazi yake mwenyewe ya kufanya, kwa hivyo asingeweza kumtunza kila wakati. Ili kumzuia asipatwe tena na ugonjwa huo, ilikuwa vizuri kuwa na muuguzi aliyezoezwa ifaavyo nyumbani ili kumtazama.
Hata hivyo, alionekana kuchanganyikiwa wakati macho yake yalipotua kwenye uso mzuri sana. "Jina lako nani?"
Mwanamke huyo alionekana kushtuka chini ya macho yake kabla ya kujibu kwa sauti nyororo, "Jina langu ni Maurine Langa."
“Langa?” Alvin akashtuka kusikia jina hilo. "Una uhusiano gani na Sarah Njau Langa?"
"Yeye ni binamu yangu." Maurine alipepesa macho na kumtazama Alvin. “Unamfahamu binamu yangu?”
“Ni zaidi ya kumjua.” Alvin alihema ndani kwa ndani. "Wewe bado ni Langa, angalau. Kwanini uliishia kuwa nesi? Hii si kazi rahisi.”
"Langa sio kama tulivyokuwa hapo awali. Lakini ni sawa, angalau tuna cha kupeleka matumboni mwetu na paa juu ya vichwa vyetu.” Aliinua macho yake na kutabasamu kwa shukrani. "Pengine kuchukua kwangu taaluma hii kuna uhusiano na binamu yangu. Sisi wawili tulizoea kuwa karibu sana tulipokuwa wadogo lakini alipelekwa katika hospitali ya magonjwa ya akili. Nilijisikia vibaya sana kwake. Mpango wangu wa awali ulikuwa kuwa mwanasaikolojia aliyeidhinishwa lakini sikufanikiwa. Kwa kweli niko katika maandalizi ya kufanya mtihani tena.”
Alvin alichanganyikiwa tena aliposikia hivyo. Swali la Hans lilimrudisha kwenye ukweli. "Bwana Mkubwa, ungependa kumwajiri nani?"
"Maurine Langa, ndiyo." Alvin akachukua kitabu chake tena na kuendelea kusoma.
Tabasamu kubwa lilienea usoni mwake. “Asante, Bwana Kimaro. Nitafanya kila niwezalo kukusaidia kupona.”
Hans alionekana kushangaa. Mara tu Maurine alipoondoka kwenda nyumbani kuchukua vitu vyake, Alvin alimtazama Hans na kuagiza, “Mchunguze mwanamke huyu.”
"Bwana Mkubwa, unashuku kwamba-"
"Fanya nilichokuagiza!"
Katika muda usiozidi nusu siku, Hans alirudi na baadhi ya matokeo. “Maurine Langa hakika ni binamu wa Sarah Langa. Alikuwa akisoma nje ya nchi na hivi karibuni alirudi nyumbani. Tangu kifo cha mama yake, familia ya Langa imekuwa ikinyanyaswa sana na familia ya Njau. Maurine anabaguliwa nyumbani na hospitalini pia na kila mara hupewa jukumu la kuwaangalia wagonjwa wenye jeuri na fujo. Lakini, utendaji wake hospitalini umekuwa mzuri sana. Sio tu kwamba yeye ni mvumilivu bali pia ana mawazo yenye nguvu ya kuvumilia magumu.”......ITAENDELEA...
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA
