JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP..........................0628924768
SEHEMU YA................................230-231

Sura ya 230

Hata hivyo, Lisa hakuwa na haya kama alivyokuwa wakati huo. “Acha. Nitafua mwenyewe.” Alimsogelea na kumfukuza.

"Hapana. Nataka nipate mateso ambayo mke wangu alipitia hapo awali,” Alvin alijibu kwa mzaha baada ya kuona uso wake ukiwa umekunjamana.

"Hujui jinsi ya kufua." Lisa aliingiwa na aibu na kero. “Huwezi kuisugua hivi. Usiiharibu.”

“Basi, nifundishe.” Alvin aliinua uso wake na kujifanya kama mtoto mzuri ambaye alikuwa tayari kujifunza.

Kwa mara ya kwanza, Lisa alijua maana ya kujipalia makaa yeye mwenyewe. Aliuanzisha mchezo lakini Alvin akawa mchezaji mzuri kuliko yeye.

"Harakisha." Alvin alimhimiza.

Akiwa hoi, Lisa aliketi kando yake na kumuongoza. “Isugue ndani nje…”
Baada ya Lisa kumwangalia mwanamume huyo akiosha chupi yake kwa uangalifu chini ya uongozi wake, kila aina ya hisia zilimjaa akilini.

Baada ya kuanika chupi hiyo, Alvin aligeuka nyuma na kuyaona macho ya mwanamke huyo ambayo yalitoa hisia kali za huba. Ilikuwa ya kufurahisha na kuudhi kwa wakati mmoja. “Umefurahi?”

“Bila shaka. Ni kwa sababu kuna mtu alinifulia nguo kwa mara ya kwanza.” Mdomo wa Lisa ulitetemeka. Ingawa alikuwa katika uhusiano na Ethan kwa miaka kadhaa nyuma, wawili hao hawakuwa wamewahi kuwa wa karibu namna hiyo.

Kabla ya hili, Lisa alikuwa amesikia tu wanawake kwenye mtandao wakijisifu kuhusu wapenzi wao wanaofua chupi zao. Alipokutana na Alvin, hakutarajia kabisa kwamba mwanaume mwenye kiburi kama yeye siku moja angefua nguo zake za ndani.

"Umewahi kupata wanaume wangapi wa kufua nguo zako za ndani?" Alvin alimbeba juu juu na kumuweka kitandani. Kisha akamuonya, “Unatakiwa kujisikia mwenye bahati kwamba hukuruhusu Ethan na Kelvin kufua nguo zako za ndani. Vinginevyo, ningeikata mikono yao.”

“Hakika nisingewaruhusu wanifulie nguo yangu ya ndani. Ninakupenda wewe tu.” Lisa akauzungusha mkono wake shingoni na kuchukua hatua ya kumbusu kwenye midomo. "Nakupenda, Alvilisa."

Akiwa amekabiliana na utani wake, wimbi la hisia lilimkumba Alvin ndani kabisa. Akaunyoosha mkono wake na kumbana pua yake. "Una uhakika?"

“Ni lini sikuwa serious?” Lisa aligeuka kuwa mnyonge. Kwa kweli, alikuwa akikiri mapenzi yake kwake.

"Zamani?" Macho ya Alvin yalitiwa giza. "Uliniambia kila wakati jinsi ulivyokuwa unanipenda kabla ya hii. Lakini kumbe yote yalikuwa uwongo." Lisa alijisikia vibaya. "Bado siwezi kujua wakati unasema ukweli na wakati unasema uongo. Afadhali kuwa mkweli na mimi. Ulianza kunipenda lini?” Alvin alimtazama kwa hasira. "Afadhali uniambie ukweli."

Lisa aligusa pua yake kwa aibu. "Huwezi kuwa na hasira baada ya kukuambia, sawa?"

“Ndio. Nimejipanga kiakili.” Alvin alionekana kutojali.

“Pengine… muda ulioniokoa nilipokuwa karibu kujeruhiwa kwenye eneo la ujenzi…”

“Kwa hiyo mambo yote uliyoniambia kabla ya hapo yalikuwa ya uwongo?” Alvin alishindwa kujizuia. Kwa kweli alikuwa amemdanganya kwa muda mrefu sana na kumchukulia kama mpumbavu.

“Lo… Hapana. Acha nifikirie tena. Pengine ilikuwa wakati uliniokoa kutoka kwenye jumba letu la ukoo…” Lisa aliingiwa na hofu kuuona uso wake uliopauka. “Oh, hapana. Labda ilikuwa wakati ulipoingia hotelini ili kuniokoa baada ya kunyweshwa dawa…”

“Ilikuwa lini hasa, mbona unanichanganya?” Alvin alishindwa kumvumilia sasa. Alianza kujisikia hasira. "Afadhali usianzishe ugonjwa wangu."

Lisa akaizungushia mikono yake mwilini mara mwake moja. “Hata mimi sina uhakika. Labda upendo wangu kwako ni kama nukuu hii kutoka kwenye kipande cha muvi ya ‘WHEN HARRY MET SALLY’--‘Unapogundua kuwa unataka kutumia maisha yako yote na mtu, unataka maisha yako yote yaliyobaki yaanze haraka iwezekanavyo'.”

Alvin alitabasamu. "Kazi nzuri. Umejifunza nukuu nyingi kutoka kwenye sinema za mapenzi, huh? Tulipokutana kwa mara ya kwanza, ulinichezea kimapenzi kwa nukuu tamutamu, 'Siwezi kujizuia kujisikia furaha kwa kuwa nimekutana na mpenzi wa maisha yangu'. Niambie nini kingine unajua. Jaribu na uniambie sasa hivi.” Kumbukumbu yake kali ilimwacha Lisa hoi. Yeye mwenyewe alikuwa kisha sahau kama aliwahi kumwambia Alvin maneno hayo.

Hatimaye, alijihisi mnyonge na akaizungushia mikono yake shingoni mwake kwa shauku. “Samahani, mume. Hata hivyo, sisemi uwongo kwa sasa. Sasa kwa kuwa unataka nikuambie nilipoanza kukupenda, siwezi kubainisha kwa wakati maalum. Pengine ilikuwa katika moja ya siku hizo tulipokaa pamoja. Inaweza pia kuwa wakati uliniokoa kishujaa tena na tena. Kufikia wakati nilipopata fahamu, tayari nilishaanza kukupenda.”

Maneno yake yaliyeyusha moyo wa Alvin. “Kweli?”

“Ndio. Kwa kweli, nilipokutana na wewe kwa mara ya kwanza, nilifikiri kwamba wewe ndiye mwanamume mzuri zaidi ambaye sijawahi kukutana naye katika maisha yangu, lakini hukuwa na moyo wa kimapenzi. Siku zote ulinitendea kwa dharau na hata kunifanya nilie kwa hasira mara kadhaa. Vinginevyo, ningekuangukia mapema zaidi. Kwa kweli, ilikuwa rahisi kwako." Lisa alishika mashavu yake yenye kupendeza. Uso wake ulionekana katika macho yake.

Alvin alimbusu kwa mahaba kwenye midomo. “Unajivunia sana kutaniana na wanaume. Ulishawahi kuwachezea wanaume wangapi hapo awali?"

"Wewe tu. Utakuwa peke yako pia." Lisa alimkumbatia kwa nguvu.
Koo la Alvin likasogea, na sauti yake ikageuka kuwa ya kishindo. “Vizuri. Unanifanya nijisikie kuwa na mtoto na wewe.”

Uso wa Lisa ulikuwa unawayawaya. Akiwa anasitasita kuitikia kwa kichwa, simu ya Alvin ikaita ghafla. Baada ya kuitazama simu yake, alikunja uso na kuiweka pembeni ya sikio. Sauti ya hasira ya Mzee Kimaro ilisikika.

“Wewe mwanaharamu, endelea kumtazama mwanamke wako! Kwa hakika anaomba kurejeshewa hakimiliki za bidhaa za KIM International. Inaonekana anajiamini kupita kiasi kuliko uwezo wake.”

Lisa aliinua kichwa chake. Alvin alimtazama huku akitabasamu, lakini sauti yake ilikuwa na jeuri. “Nakubaliana na mke wangu.”

"Alvin, unajaribu kuifanya damu yangu ichemke?" Sauti ya Mzee Kimaro ilitetemeka.

“Babu, mwanzoni sikupanga kufanya unyama kama huu, lakini nyie ni wakatili sana,” Alvin alijibu bila huruma.

“Alvin, sijawahi kufikiria kukushambulia kwa hizo picha. Kwani wewe ni mjukuu wa familia ya Kimaro.” Sauti ya Mzee Kimaro ilijaa unyonge. “Unajua vizuri njia zangu. Hata kama ningepanga kukufanyia ubaya, nisingetumia mbinu za siri kama hizi.”

“Hiyo haimaanishi kwamba watoto na wajukuu zako wengine hawatafanya hivyo,” Alvin alijibu kwa upole, “Kama unavyojua, mimi ndiye wakili mahiri zaidi hapa nchini na sijawahi kupoteza kesi yoyote. KIM International pia haiwezi kunishinda hata kama mtaenda mahakamani.”

Kulikuwa na muda wa kimya kimya upande wa pili wa simu. Mzee Kimaro aliuliza kwa unyonge, “Unataka nifanyeje ili uachane na harakati hizi? Niambie masharti yako.”

“Ni rahisi. Nataka tu mamlaka na hisa zako. Ninataka kuiongoza KIM International katika siku zijazo. Pia, msinisumbue kuhusu ndoa yangu na mke wangu.” Alvin alisema kwa upole, "Ninaamini tayari unafahamu kwamba cement ya Alvinarah Corporation imezalisha mauzo ya zaidi ya shilingi bilioni moja nchini kote ndani ya masaa matatu tu baada ya kuzinduliwa. Zaidi ya hayo, tumetia saini makubaliano na makampuni mengi ya kigeni kufanya kazi pamoja. Bila hakimiliki ya Oceanic Cement, KIM International italazimika kukoma kuendesha biashara yake ya saruji nchini kote. Nyinyi watu mnahitaji kuajiri timu nyingine ili kuvumbua cement mpya, ambayo itachukua angalau miaka miwili ya utafiti. Miaka miwili baadaye, je KIM International bado itashikilia nafasi ya kwanza?"

Kwa muda mrefu, Mzee Kimaro hakutoa neno lolote.

KIM International ilihusika katika nyanja mbalimbali, ikiwa ni pamoja na fedha, bima, mawasiliano na ujenzi. Kwa sababu ya ushindani mkali, hata hivyo, ilichukua asilimia 20 tu ya soko. Zaidi ya hayo, watu kama Spencer na Valerie walikuwa na uwezo mdogo wa kuendesha biashara. Familia zingine zingeweza kuipiku familia ya Kimaro kwa urahisi katika nusu mwaka, chini ya miaka miwili.

'Kama unamtarajia mama yangu…” Alvin alicheka ghafla na kusema, “babu, kwa kusema kweli, huoni kwamba Jack na mama yake wanapendelea familia ya Campos kupita kiasi? Miaka 20 iliyopita, mali ya familia ya Campos ilikuwa na thamani ya dola milioni kumi pekee.

Sasa, wameweza kuingia katika familia tatu tajiri zaidi nchini Kenya. Hata mama yangu hakuenda mbali katika kukuza kampuni yake.”

Sura ya: 231

“Tatu bora? Hilo haliwezekani.” Mzee Kimaro alishikwa na butwaa.

"Unaweza kuangalia taarifa ya kifedha ya familia ya Campos kwa mwaka huu. Familia ya Campos kwa kawaida hawana biashara, wao huwekeza hisa kwenye makampuni makubwa. Baada ya Jack kuanza kusimamia kampuni, alisaini makubaliano na familia ya Campos ambayo hutoa faida ya asilimia tano kwao. Kana kwamba familia ya Campos haina nguvu za kutosha.” Taarifa hizo zilikuja kuwa pigo kwa Mzee Kimaro.

"Mara tu familia ya Kimaro itakapozama, familia ya Campos ina uhakika wa kuwa ya kwanza ambapo hawawezi kusubiri kuchukua usimamizi wa kampuni hiyo. Ikiwa nitamiliki KIM International, hadhi ya familia ya Kimaro haitabadilika kamwe. Hata hivyo, ni juu yako. Hata kama huna mpango wa kuniruhusu kuchukua kampuni, bado ninaweza kulinda hadhi yangu nchini Kenya kwa njia zangu mwenyewe. Katika hali hiyo, hali ya familia ya Kimaro haitakuwa na uhusiano wowote na mimi…”

“Lakini ugonjwa wako…” Mzee Kimaro alikuwa na wasiwasi.

“Kama huniamini, ni sawa. Niko bize, na ni lazima nikate simu sasa…”
Kwa hayo, Alvin alikuwa karibu kukata simu.

Hapo hapo, Mzee Kimaro akajibu mara moja, “Sawa, mimi tayari ni mzee. Siwezi kushindana na vijana. Nitakuruhusu uchukue KIM International, lakini ninatumai kuwa utaisimamia vyema. Mam’mdogo wako… Amekukosea, na sitarajii umlipishie kisasi. Baada ya kusema hivyo, usiende mbali sana. Baada ya yote, sisi ni familia."

"Babu, mimi hufuata kanuni ya jicho kwa jicho na jino kwa jino." Alvin alisisitiza.

“Wewe…” Mzee Kimaro alikosa la kusema.

“Huna uwezo wa kujadiliana nami tena.” Baada ya Alvin kukata simu, macho yake yalidhihirisha kupuuzia aliyoyaongea.

Lisa hakupenda maneno yake yaliyoashiria visasi. Alianguka mikononi mwake na kumkumbatia kwa nguvu. Kisha, alibadilisha mada. Je! ni kweli familia ya Campos ilifanikiwa kuwa kati ha familia tatu tajiri zaidi nchini Kenya na mali zao?"

"Nini unadhani, huniamini?" Macho ya Alvin yalififia polepole.

“Hilo haliaminiki kabisa. Familia ya Campos daima imekuwa na hadhi ya chini. Nilikuwa na fikra kwamba itakuwa familia ya Choka na familia ya Shangwe ndizo ambazo zinaweza kuingia kwenye tatu bora.”

“Ndio. Familia ya Campos imekuwa ikijificha vizuri sana. Kama isingekuwa kwa ajili ya harusi ya Jerome wakati huu, nisingechunguza historia ya familia yake,” Alvin alisema “Familia ya Campos ni tata. Ninaogopa kwamba baba yangu wa kambo si rahisi kama anavyoonekana.”

Lisa alipigwa na butwaa. “Nimemwona Mason mara mbili. Ananipa hisia kwamba yeye ni mpole na mwenye urafiki. Uvumi unadai kwamba amekuwa akijishughulisha na sanaa na muziki na havutiwi kabisa na mali na mamlaka ya familia yake.”

"Nilikuwa nikifikiria hivyo pia, lakini Mason Campos ni mtu wa chinichini sana. Nadhani anajaribu kutumia njia hizo kugeuza mawazo yetu mbali naye.” Alvin alijaribu kufikiria.

Lisa aliuliza. "Kwa kuwa ni familia ya Campos iliyopanga njama ya picha dhidi yako, jambo hili linaweza kuhusishwa na Mason?"

“Labda…” Moyoni, Alvin alifadhaika kidogo. Aliinamisha kichwa chake na kumbusu kwenye midomo mara moja. "Nitaweka dhiki zote nyuma yangu kwa sasa. Hebu tufanye jambo la kufurahisha…”

“Aa…”
•••
Katika makazi ya familia ya Kimaro, Mzee Kimaro alishika simu huku akiwa amekaa kwenye kiti cha mbao, macho yake yakionyesha hisia tata.

“Kwa hiyo mazungumzo yako na Alvin yalikwendaje?” Bibi Kimaro akammiminia kikombe cha kahawa.

“Kwa kweli, hakuna maana kubishana kuhusu hilo. Yeye ni mjukuu wa familia ya Kimaro, hata hivyo. Nilipotazama video ya kuhojiwa yaya wake, nilihuzunika. Tuna deni kubwa kwake. Zaidi ya hayo, ni familia yetu wenyewe iliyofichua picha hizo…”

“Unafikiri ni nani alifanya hivyo?” Bibi Kimaro aliuliza.

"Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Lisa alidai kwamba ilikuwa familia ya Campos, kwa hivyo nadhani atakuwa ... Jack." Mzee Kimaro alihema kwa kukata tamaa. "Alvin aliniambia kuwa familia ya Campos imefanikiwa kuingia katika familia tatu tajiri zaidi nchini Kenya."

Bibi Kimaro alishikwa na butwaa. “Inawezekanaje?”

“Bado unakumbuka familia ya Campos ilivyokuwa miaka 20 iliyopita? Nilimdharau Mason enzi hizo. Ingawa ana talanta ya muziki, hawakuwa na kitu kabisa enzi hizo. Baadaye, Lea alisisitiza kuisaidia familia ya Campos, na mimi nilifumbia macho. Ikiwa hii ni kweli, hufikirii kwamba familia ya Campos imekuwa ikituhujumu kwa kujificha vizuri?” Mzee Kimaro alieleza wasiwasi wake.

“Ndio. Wakati wa harusi ya Lea nakumbuka Mama Campos alivyokuwa akinung'unika jinsi biashara yao ilivyokuwa mbaya. Alitumaini kwamba tungeweza kusaidia familia yake.” Bibi Kimaro alijawa na huzuni.

“Nilikuwa namchukia Alvin kwa kuniharibia heshima ndiyo maana nilimuachia Jack kusimamia KIM International. Lakini nikiendelea kumwacha aisaidie familia ya Campos, familia ya Kimaro itapoteza sifa ya kuwa familia bora zaidi hivi karibuni.” Mzee Kimaro alimpigia simu moja kwa moja wakili wake. "Njoo hapa."

Katika muda usiozidi saa 12, habari kwamba Mzee Kimaro alihamisha hisa na mamlaka yake yote kwa Alvin zilikuwa zimesambaa Nairobi nzima. Wazao wa familia ya Kimaro ndio walikuwa wa kwanza kumtafuta Mzee Kimaro.

Valerie alikuwa wa kwanza kupinga kati yao. “Baba, una akili? Unawezaje kumruhusu Alvin kuchukua nafasi ya mwenyekiti wa KIM International? Hukumbuki jinsi alivyotufanyia hapo awali?”

"Umesemaje, sina akili?" Mzee Kimaro alikasirika sana hadi akahisi kutaka kumpiga makofi hadi kufa.

“Baba naogopa Alvin atanilenga baada ya kuchukua kampuni kwani ananichukia.” Valerie alizungusha mikono yake kwenye mguu wa Mzee Kimaro kwa mshtuko. “Kaka, Dada, ongeeni na baba, Alvin ataniua!”

Mdomo wa Spencer ulitetemeka. “Sina mgogoro na Alvin hata hivyo. KIM International itakuwa imekufa majini ikiwa hatutamruhusu kusimamia kampuni. Kila mtu huko nje anaichukulia familia yetu kama kituko kwa sasa. Wanasubiri tu kutuona tukianguka.”

“Vipi wewe?! Wewe ni mtoto wa pekee wa kiume kwa baba na mama. ulitakiwa uwe na nguvu kuliko wajukuu, lakini huna uwezo sana,” Valerie alimtukana.

"Nyamaza!" Mzee Kimaro alielekeza macho yake kwa Jack bila subira. “Unafikiri nini Jack?”

Jack alikunja ngumi. Alikuwa amejitahidi sana kabla ya kupata nafasi yake ya uenyekiti katika kampuni. Lakini, ikawa kwamba Alvin angechukua tena nafasi hiyo muhimu katika siku chache. Ilikuwa haiwezekani kwa Jack kuwa sawa na hilo. “Babu ni sawa na wewe kutishiwa na Alvin namna hii? Amekuwa akikukosea heshima waziwazi. Mara tu atakapopata nafasi ya kuongoza, ninaogopa atakudharau zaidi. Zaidi ya hayo, karibu amuue mama yake mzazi siku chache zilizopita. Ugonjwa wake umerejea.”

“Hasa. Mtu mwenye ugonjwa wa akili anawezaje kuchukua jukumu la KIM International?" Valerie akaongeza haraka.

"Kabla sijafikia uamuzi huu, mna suluhisho gani?" Mzee Kimaro alimkazia macho Jack. "Nilikupa nafasi, lakini ulichagua kufichua ugonjwa wa akili wa Alvin kwa umma badala ya kushughulikia mambo ya kampuni."

Jack ghafla alitazama juu kwa macho mekundu. “Sikufanya hivyo babu. Kuna mtu ananifanyia njama.”

“Unafikiria nini, Mason?” Mzee Kimaro alielekeza macho yake makali kwa mkwewe ghafla.

Mason alipigwa na butwaa kwa muda. Kisha akanung’unika, “Sina uhakika sana kuhusu hilo…”

Lea hakuweza kujizuia kusema, “Baba, Mason kwa kawaida hutumia wakati wake kutunga muziki. Hata hajali kinachoendelea kati ya familia ya Kimaro na familia ya Campos. Je, angewezaje kujua lolote kuhusu hili? Pia, Jack ni mwanangu na ninaelewa tabia yake. Nina hakika ni mtu mwingine aliyevujisha picha."

“Kwa hali hii…” Mzee Kimaro alichukua kikombe cha kahawa na kunywa kidogo kabla hajaendelea. “nilivyoamua imetosha. Hakuna haja ya kujaribu kunishauri tena. Machoni mwangu, hakuna kitu muhimu zaidi kuliko kulinda nafasi ya familia ya Kimaro kama familia bora zaidi nchini Kenya.” Mzee Kimaro alisimamia msimamo wake. Hakuna mtu aliyekuwa na ujasiri wa kuzungumza upuuzi tena.

Mishipa iliyovimba ilionekana kwenye ngumi za Jack. Baada ya Jack kutoka nyumbani, alipiga mlango wa gari kwa nguvu. Akatoa simu yake na kumpigia Jerome. "Kuanzia sasa na kuendelea, Alvin ndiye mtoa maamuzi mkuu katika kampuni. Atakaporejea kwenye kampuni, ninahofia anaweza kufuta makubaliano kati ya familia ya Kimaro na familia ya Campos, na kufanya aslimia tano za faida kuwa batili......ITAENDELEA...

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA