JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP..........................0628924768
SEHEMU YA................................228-229

Sura ya: 228

Swali la Lisa lilipita kimya.

“Naam, hatimaye naweza kuzungumza sasa.” Lisa akaanza. “Kuhusu ugonjwa wa Alvin, ni kweli, lakini nashangaa hakuna hata mwandishi mmoja aliyeuliza chanzo cha ugonjwa wake, wote mmeishia kumtuhumu na kumjaji kana kwamba ni mhalifu mkubwa. Kila mtu ana matatizo. Kama ilivyo kwa binadamu wengine, Alvin naye ana matatizo yake. Hakumuumiza yaya wake kwa kupenda wala bila sababu. Hii hapa ni ripoti ya matibabu kuhusu matibabu ya Alvin alipokuwa na umri wa miaka minane. Aligundulika kuwa na msongo wa mawazo na kiwewe baada ya mfadhaiko kwa sababu alikuwa akiteseka kutokana na unyanyasaji kwa muda mrefu. Ni ukweli kwamba alikuwa amenyanyaswa kwa muda mrefu na yaya wake.”

Lisa alitazama nyuma ya jukwaa, na video ya zamani ilionyeshwa kwenye skrini kubwa. Katika video hiyo, afisa wa polisi alionekana akimhoji mwanamke wa makamo mwenye nywele chafu na mikunjo usoni.

"Ulimfanya nini huyu mtoto wakati analia?"

“Nilimvua nguo zake na kumfungia chumbani."

“Ulimfungia kwa muda gani?”

"Kwa kawaida siku moja hadi mbili. Familia ya Kimaro haikuwa ikimjali, kwa hivyo hakuna mtu aliyejua. Asingekufa baada ya kutokula kwa siku mbili hata hivyo, siku ya tatu ndipo nilimfungulia na kumpa chakula kidogo.”

Afisa wa polisi alikasirika. "Je, ulifanya hivyo wakati wa baridi pia?"

“Ndiyo. Nilipoona kwamba angezimia nyakati fulani kutokana na baridi kali, mara moja nilimtoa nje na kuiambia familia ya Kimaro kwamba alikuwa na homa. Familia ya Kimaro iliniamini. Zaidi ya hayo, ukizingatia jinsi Alvin alikuwa mbali na kila mtu, wote walimchukia.”

Baada ya video ya dakika tano kumalizika, kimya kilitanda kwenye ukumbi huo. Waandishi wengi wa kike walikasirika. Lisa akashusha pumzi ndefu, na macho yake yalikuwa mekundu kidogo. “Ninachojaribu kusema ni kwamba hakumuua yaya. Alimchoma kisu tu kwa sababu alishindwa kujizuia na akajitetea dhidi yake baada ya kufungwa kwa siku tatu ngumu. Baadaye, alikaa katika hospitali ya magonjwa ya akili kwa miaka mitatu. Daktari alisema kwamba mara chache angerudia tena hali hii, kwa hivyo almiruhusu Alvin kurudi nyumbani.

“Hata hivyo, habari kuhusu hali yake na picha zake za zamani zilianza kusambaa jana. Hakika, ilipangwa kwa makusudi siku moja kabla ya mkutano huu wa waandishi wa habari ili kuvuruga tukio hili. Nilipotoka nyumbani leo, bado alikuwa amepoteza fahamu. Mkutano wa waandishi wa habari ulikaribia kusitishwa hivyo nikaamua nije mimi."

Ghafla macho ya Lisa yalizidi kuwa makali. "Ni wazi kwamba mtu ambaye alisambaza picha hizo kwa nia mbaya alikuwa anajaribu kuongeza jeraha kwenye moyo wa Alvin ambao tayari unavidonda. Tunaweza kushindana kama biashara, lakini hatuwezi kuvuka msingi wa maadili. Katika miaka hii yote, Alvin ametoa shilingi bilioni 200 kwa hisani, ameunda nafasi nyingi za kazi, na kusaidia familia nyingi. Amefanya kosa gani? Amewahi kuwaumiza nyie?"

Kila mtu aliyekuwepo kwenye mkutano huo alinyamaza. Mwanahabari aliyeanzisha mjadala huo hatimaye aliomba msamaha, “Ninaomba msamaha kwa Bwana Kimaro kwa kuuliza swali hili, sikuwa na nia mbaya ila nilitaka tu kujua. Samahani sana. Swali langu linaweza kuwa limekwenda mbali sana."

“Ni sawa.” Lisa aliinua midomo yake na kutabasamu kwa unyonge. Macho yake yakatua kwa mwandishi huyo wa Nairobi Financial Times. "Ikiwa nakumbuka vizuri, lilikuwa ni gazeti lako ambalo ilichapisha habari kuhusu hali ya Alvin na picha zake. Wewe pia ulikuwa wa kwanza kuanzisha mada hiyo hapa leo. Alvin amewakosea?”

Ripota kutoka Nairobi Financial Times alishuka. "Ninatimiza tu majukumu ya mwandishi."

“Kweli? Kama ripota wa habari za fedha, unaonekana kutaka kuchimba mambo ya kibinafsi badala ya kuniuliza maswali yanayohusiana na maendeleo ya kampuni na masuala ya kifedha,” Lisa alimdhihaki huku akicheka, “Familia ya Campos ilikulipa kiasi gani kutimiza jukumu hili?”

“Familia ya Campos?” Zogo lilizuka ukumbini hapo. “Familia ya Campos inahusikaje?"

“Chukueni hii kwa faida yenu.” Lisa alijiweka sawa. “Familia ya Campos ni familia ya baba wa Jack, na Jack ni mwenyekiti wa KIM International ambayo kwa sasa ina ushirikiano wa kibiashara na familia ya Campos. Familia ya Campos wanamdidimiza Alvin ili kudumisha nafasi ya Jack kama mwenyekiti wa KIM International na kulinda maslahi yao kwenye kampuni. Ni wazi, tukio hili linahusiana na familia ya Kimaro na familia ya Campos. Msisahau kwamba Alvinarah Company na KIM International sasa ni washindani wa biashara.”

“Jamani. Alvin ni wa familia ya Kimaro pia. Hawana aibu?"

"Kama wangekuwa na aibu yoyote, Alvin angenyanyaswa na yaya katika umri mdogo?"

"Kuna nini?! Wanafamilia ya Kimaro ni watu wa aina gani?"

Katikati ya mjadala mkali, ripota yule kutoka Nairobi Financial Times alijibu kwa haraka, “Familia ya Campos? Sielewi hata kidogo unachokisema.”

“Ni sawa. Utaelewa baada ya muda mfupi. Ukiwa mwakilishi wa chombo cha habari, ulieneza harakaharaka picha za faragha za Alvin mtandaoni na kumsababishia madhara kiakili. Nimeripoti suala hilo kwa polisi, kwa hivyo unaweza kwenda kujieleza huko hizo picha ulizipata wapi.” Lisa alisema kwa moyo mwepesi, “Tafadhali mchukueni, walinzi. Polisi wanasubiri nje.” Maneno yake yalimtia hofu mwandishi huyo. Wanausalama walimchukua bila kumpa nafasi ya kuongea.

Kwa jinsi Lisa alivyokuwa akishughulikia suala hilo bila huruma, waandishi wote waliokuwa pale ukumbini hawakuwa na ujasiri wa kuongea kizembe tena. Kila mtu alimtazama yule mwanamke aliyevalia mavazi meusi kama hakimu jukwaani. Aliweka uso usio na wasiwasi na alionyesha haiba ya kipekee na ya kiburi, ambayo ilimwacha kila mtu katika hofu.

Lakini, Lisa bado alitabasamu wakati huo. "Suala la kibinafsi limetatuliwa, kwa hivyo turudi kwenye japo husika lililotukutanisha hapa, Oceanic Cement. Baadhi ya watu wanashangaa kama teknolojia ya cement hii ilivumbuliwa na KIM International. Kwa kweli, haikuwa hivyo. Ilikuwa Team Simon iliyovumbua cement hii, na Alvin anamiliki hakimiliki yake. Kwa kuwa sasa Alvin ameondoka KIM International, ataomba kurejeshewa hakimiliki kwenye prototype ya bidhaa zote ambazo Team Simon ilivumbua ikiwa kwenye kampuni hiyo.”

Hili lilikuja kama pigo jingine kwa KIM International. Ikiwa hii ingetokea kweli, hakuna kampuni yoyote ambayo ingekuwa na ujasiri wa kufanya kazi na KIM International, ikizingatiwa kuwa kampuni hiyo isingekuwa na bidhaa yake yenyewe ambayo ni halisi.

Waandishi waliuliza kwa mshtuko, “Ina maana kwamba Bwana Kimaro anaingia kwenye vita na KIM International?”

"Hakutakuwa na vita vya aina yoyote. Kampuni ya Alvinarah inataka tu kurudisha mali zake.” Lisa alijibu kwa kujiamini. Hakukuwa na swali tena kutoka kwa waandishi, na zogo likatulia.

Tabasamu likatanda usoni mwa Lisa. "Acha niwajulishe nyote kuhusu undani wa Oceanic cement."
•••
Katika jumba la kifahari lililo kando ya bahari, Alvin alikuwa akimtazama yule mwanamke mrembo, aliyejiamini, akizungumza kupitia mtiririko wa moja kwa moja. Hakuweza kujizuia kuachia mshangao wake kwa kiburi. Hakika huyu ndiye mwanamke ambaye alikuwa amemtamani sana. Alijiuliza ni lini yule mwanamke mnyonge na mwenye aibu ameanza kukua na kuwa jasiri vile. Alikuwa na ujasiri na busara zaidi. Hapo zamani, Alvin alilazimika kumuokoa na kumlinda kila wakati kutokana na uzembe wake.
Sasa, alikuwa bora kama yeye!

Kutazama video hiyo, Chester alihisi utulivu. “Lisa ananiumiza vichwa vya watu. Nina kiwango kipya kabisa cha heshima kwake. Yeye ni mzuri. Anazungumza kitaalamu zaidi kuliko wataalamu.”

“Usiongee kama hujui huyo mwanamke ni wa nani.” Midomo ya Alvin haikuweza kuficha kiburi chake.

Chester alikosa la kusema. Je, ni kweli huyu ndiye mtu ambaye alikataa katakata kumwamini Lisa kabla ya hapo?

Hans alicheka na kusema, "Bi. Jones alitumia usiku mzima kukariri data. Alikuwa na wasiwasi kwamba waandishi wangemuuliza kuhusu maswala kuhusu teknolojia yake, kwa hivyo alipitia habari zote muhimu.

Sura ya huzuni ilivuka kwenye uso wa Alvin. Kwanini alilazimika kuhangaika sana? Alvin alimtazama Hans. "Mwanamke wangu alifanya karibu kila kitu. Kuna faida gani mimi kuwaweka nyie kwenye kampuni na kuwalipa pesa nyingi sana?”

Aliposikia shutuma hizo, uso wa Hans ukageuka kuwa jivu. Akiwa hana msaada, Chester alimtetea, "Jana usiku, Hans alikuwa na shughuli nyingi akitafuta video ya kukiri kwa yaya baada ya kukamatwa wakati huo."

"Lilikuwa wazo lako kupata video kuhusu kuhojiwa?" Alvin aliuliza huku akiwa ameinua kichwa chake.

Hans alijibu kwa kusitasita, “…Lilikuwa wazo la Lisa.”

"Ha, nilijua tu." Alvin hakuweza kuficha kejeli katika sauti yake. Hans hakuwa mjinga. Alijua kabisa kuwa kejeli ile ilikuwa inaelekezwa kwake.
Chester alikosa la kuongea. “Kusema kweli video ilirekodiwa miaka mingi iliyopita. Haikuwa rahisi kwa Hans kuipata.”

Sura ya: 229

Alvin alitoa sura ya kutoridhika. “Umenifanyia kazi kwa muda mrefu. Lakini kwanini hukuweza kushughulikia hili? Hupaswi hata kuitwa msaidizi wangu.”

Hans na Chester walibaki midomo wazi. Ilionekana kuwa mchango wao haukuthaminika na ni mke wake tu ndiye aliyeonekana kuwa mpambanaji zaidi. Aliupiga mwingi kiasi kwamba hakuna mtu angeweza kulinganishwa naye.

Mkutano na waandishi wa habari uliendelea kwa saa tatu. Baada ya kumalizika, Lisa alirudi kwenye jumba lao la ufukweni.

Dereva alipofungua mlango wa gari, Lisa alitoka na kumuona Alvin akiwa amesimama kwenye kingo kandokando ya bwawa la kuogelea. Alivaa suruali laini ya kitambaa na shati ambalo halikuchokewa ndani ya suruali yake kama kawaida. Alionekana akiwa amepumzika na kujisahau kabisa.

Upepo wa baharini ulipita nyuma ya shati lake na kulipeperusha taratibu.
Kwa mtazamo wa haraka haraka, alionekana kuwa mdogo kwa miaka kumi kuliko alivyokuwa. Alionekana kama mwanafunzi wa chuo kikuu, akionekana mpole na mtulivu. Hata hivyo, ngozi yake ilikuwa imepauka sana.

Lisa alitembea taratibu kuelekea kwa Alvin na kudhibiti mapigo yake ya moyo kabla ya kusema kwa tahadhari. “Nisamehe kwa kukiri ugonjwa wako hadharani. Utanilaumu kwa hilo?”

Alvin alipitisha mkono wake kwenye nywele zake na kumkumbatia. "Umefanya vizuri zaidi ya nilivyotegemea mke wangu."

"Hujachukia?" Lisa alishikwa na butwaa. “Nilifikiri ungekasirika kwa kukubali hadharani kuhusu ugonjwa wako?”

"Sitajali endapo utakuwa karibu nami." Alvin aliukunjua uso wake kwa tabasamu na kumkazia macho yake meusi. "Uko tayari kuwa karibu nami wakati wa matibabu yangu?"

“Ndiyo.” Lisa alikubali kwa kichwa na sauti.

“Lakini sina uhakika ni lini nitapona ugonjwa wangu. Pengine nisiweze kupona kamwe. Zaidi ya hayo, nimekuumiza mara nyingi. Ninahofia kwamba huenda nikapoteza tena udhibiti wakati fulani.” Macho ya Alvin yalidhihirisha wasiwasi na taabu.

"Alvlisa, mradi uko tayari kutibiwa ugonjwa wako, sitakuacha." Lisa aliuma mdomo kana kwamba amedhamiria. "Wacha tupate mtoto pamoja."

Alvin alishtuka. "Lakini hukutaka kuwa na mtoto hapo awali."

“Nimejadili hali yako na Dokta Choka, Alvlisa. Moyoni mwako unatamani kuwa na familia. Familia yetu sisi wawili itakuwa kamili tukiwa na mtoto." Lisa aliinua macho ya upole. "Ninaamini utaweza kusahau polepole kumbukumbu hizo chungu za utoto wako baada ya kupata mtoto pamoja."

“Asante, babe.” Alvin alimkumbatia Lisa kwa nguvu, macho yake yakamtoka. "Kwa hivyo ... twende tukatafute mtoto sasa?"

Kwa aibu, Lisa alimkandamiza kiunoni. “Ni mchana sasa. Huna aibu kwenda kujifungia chumbani na jua lote hili? Sijapata hata chakula changu cha mchana. Tutafanya baadaye, sawa?”

"Tutafanya baada ya chakula cha mchana, basi?"

“Alvlisa, hunihurumii? Nimekesha usiku wote wa jana kukariri data za mradi wako. Nimechoka eti!” Lisa alijifanya kuwa na hasira na kumkodolea macho.

“Nashukuru kwa bidii yako mpenzi,” Alvin alijibu kwa huruma.

“Hakuna maana kusema tu. Utanikanda mabega yangu baada ya kumaliza chakula changu cha mchana,” Lisa alimuamuru kabla hajaingia kwenye jumba hilo.

“Umesema nini?” Alvin alitilia shaka sana ikiwa alisikia vibaya.
‘Huyu mwanamke anathubutu vipi kuniamuru nimfanyie masaji?!’

“Hutanifanyia?” Lisa alimuuliza kwa sura iliyoshuka. “Kwa sababu yako, sikulala usiku kucha. Data nyingi nilizokariri bado zinaniumiza kichwa.”

Alvin alipoona sura yake ikiwa imepooza, alinyamaza kwa muda.

Baada ya kubadilisha slippers za nyumbani, Lisa aliingia kwenye chumba cha chakula. Shangazi Yasmine alimtengea chakua baada ya kukipasha moto.

Lisa aligeuza kichwa chake na kumtazama Alvin. "Nipakulie wali."

Alvin alimtazama kwa macho meusi. "Mimi ni mgonjwa sasa, sitakiwi kusumbuliwa."

"Kwani mikono na miguu yako imelemaa?" Lisa alipepesa macho na kumtazama juu chini.

"Hapana." Alvin alitilia shaka sana iwapo Lisa alikuwa akijaribu kumlipa kwa yale aliyomfanyia hapo awali.

"Ngoja nikupakulie, Bibi mdogo." Shangazi Yasmine hakujua ni nini kilikuwa kinaendelea kati yao. Aligeuka kuchukua hotpot la wali.

“Hapana, Shangazi Yasmine. Huu ni utani wa kimapenzi kati yetu.” Lisa alimnong’oneza Aunty Yasmine na kuegemeza kidevu chake kwenye mikono yake. Macho yake makubwa yenye kung'aa yalitua kwa Alvin kwa fujo. Macho yake yaliyeyusha moyo wa Alvin mara moja.

“Sawa, nitafanya hivyo.” Alvin alifungua hotpot na kuanza kupakua wali.

Kwa tabasamu, Lisa alimvuta pembeni Aunty Yasmine na kumnong’oneza kwa sauti ambayo Alvin hakusikia, “Ninajua kuhusu hali yake, lakini nadhani ni bora kumchukulia kama mtu wa kawaida katika maisha yetu ya kila siku. Kadiri tunavyokuwa wachangamfu kwake, ndivyo atakavyohisi hisia za kupendwa zaidi.”

Aunty Yasmine hatimaye alielewa. "Wewe ni mzuri, Bibi mdogo. Unajua Bwana Kimaro hajala. Lazima umshawishi ale baadaye."

Punde, Alvin alijaza sahani ya wali. “Mbona hujipakulii chakula?” Lisa alimuuliza.

“Nimekula kidogo. Sihisi njaa." Alvin aliweka sahani ya wali mbele yake.
“Unadanganya. Shangazi Yasmine aliniambia kuwa hujala chochote, kwa hivyo unahitaji kula kitu. Lisa akamlazimisha kuketi. "Lazima ule kidogo."

“Sijisikii kula…”

“Ngoja nikulishe.” Lisa alichota kijiko cha wali uliomwagiwa njegere na kumwekea mdomoni. Alipotafuna akamlisha na kipande cha nyama ya kuku. Alikuwa akiona ladha ya wali kuwa mbaya sana hapo awali, lakini kwanini ladha hiyo ilipendeza ghafla alipolishwa na Lisa?

“Nilishe zaidi,” Alvin aliendelea kumwagiza baada ya kunogewa.

"Jaribu na kula peke yako." Lisa alimwekea kijiko mkononi mwake.

"Hapana. Sijisikii kula.” Alvin alitazama pembeni, akionyesha uso wa kukaidi.

Lisa alikuwa hoi. Hakuonekana hivyo alipomlisha mara ya kwanza. Je, ni kwa sababu chakula alichomlisha kilikuwa na ladha tofauti? Alihisi ni madeko tu ya Alvin. Hata hivyo, asingeweza kumwacha na njaa. Bila kuwa na chaguo lingine, Lisa alimlisha na kula chakula chake kwa wakati mmoja. Bila yeye kutambua, Alvin alikuwa amekula sahani mbili za wali wakati yeye alikuwa na sahani moja tu.

Sura ya mshangao iliosha uso wa Aunty Yasmine. “Ni muda umepita tangu Bwana Kimaro kula wali mwingi kiasi hiki. Inaonekana anahitaji wewe umlishe, Bibi Mdogo.”

Lisa alikosa maneno, alijiuliza kwanini hakutambua upande huu wa kitoto wa Alvin enzi hizo.

Ghafla, alihisi kubanwa mabegani mwake. Aligeuza kichwa chake na kukutana na macho machachari ya Alvin. "Uliniambia nikufanyie masaji baada ya chakula cha mchana, sivyo?"

“Ndio.” Lisa alifarijika kidogo. Angalau jitihada zake za kumlisha hazikuwa bure. Muda mfupi baadaye, alipiga kelele kwa uchungu, “Fanya taratibu basi! Unaniumiza!"

"Mbona nafanya taratibu sana?"

“Hapana, tafadhali usinikande mabega yangu tena. We unafanya utadhani ukanda unga wa chapati? Inauma sana.” Lisa aliikwepa upesi mikono yake kama shetani. “Nifanyie kitu kingine badala yake. Nisaidie kufua nguo zangu kwa mikono baada ya kuoga."

"Nini?" Alvin aliuma meno. “Lisa, unajaribu kunilipiza kwa ajili ya kazi nilizokufanyisha wakati huo? Kama vile kufua nguo na kusafisha nyumba?”

“Uko sahihi. Hiyo ni kwa sababu ulinitesa hivyohivyo hapo awali.” Lisa alitoa ulimi wake nje kwa namna ya kucheza. "Nataka upate machungu ya mambo uliyonifanyia hapo awali."

Kwa kicheko kibaya, Alvin alimbeba na kuelekea juu. “Sawa, ngoja nikakuogeshe.”

"Hapana. Niache mara moja, wewe mpuuzi!” Kicheko kitamu cha wanandoa hao wachanga kilisikika kutoka juu.

Kwa hayo, ahueni ikamshinda Aunty Yasmine. Ilikuwa ni busara sana kwa Lisa kukabiliana na hali ya Alvin kwa njia hiyo. Aunty Yasmine hakutarajia kuwa Alvin angeweza kupata furaha nyingi kiasi hicho.

Dakika 40 baadaye, Lisa alitoka bafuni baada ya kuoga vizuri. Alikaa mbele ya dressing table akikausha nywele zake. Baada ya kukausha nywele, alirudi bafuni.

Alvin alikuwa amekaa bafuni, akimsaidia kusugua… chupi yake.

“Lisa ulikuwa umelowa ndani ya sekunde chache tu?” Alvin alimtania huku akipekecha chupi yake sehemu ya katikati. Lisa hakuwa na tabia ya kufua chupi. mara zote alivaa chupi na sidiria zake mara moja tu kama pedi. Hata hivyo siku hiyo aliamua tu kumfanya Alvin afue kama utani wa kimapenzi tu.

Katika muda usiozidi nusu siku, Hans alirudi na baadhi ya matokeo. “Maurine Langa hakika ni binamu wa Sarah Nelson Langa. Alikuwa akisoma nje ya nchi na hivi karibuni alirudi nyumbani. Tangu kifo cha mama yake, familia ya Langa imekuwa haifanyi vyema chini ya unyanyasi wa familia ya Nelson. Maurine anabaguliwa hospitalini pia na kila mara hupewa jukumu la kuwaangalia wagonjwa wenye jeuri na fujo. Lakini, utendaji wake hospitalini umekuwa mzuri sana. Sio tu kwamba yeye ni mvumilivu bali pia ana mawazo yenye nguvu ya kuvumilia magumu.”....ITAENDELEA....

Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA