JINA LA SIMULIZI............................LISA
AUTHOR...........................JOMBA WAJO
SPONSORED BY......SIMULIZI ZA DULLY
WHATSAPP..........................0628924768
SEHEMU YA................................226-227
Sura ya: 226
Lisa alimkumbatia mara moja na kumnong'oneza sikioni, “Ninakuahidi kwamba sitaondoka. Ukiamka nitakuandalia nyama choma ya nguruwe.”
Macho ya Alvin yakalegea taratibu. Alianguka na kupoteza fahamu na kuonekana kama mtoto ambaye alikuwa amelala fofofo. Hakuna mtu ambaye angeweza kufikiria kwamba alikuwa mgonjwa ambaye alipandisha wazimu muda mfupi uliopita.
Lea alikaa chini baada ya kuokolewa. Hata baada ya muda mrefu kupita, amani haikurudi usoni mwake.
Jack alimkimbilia na kumsaidia kuinuka. "Mama, tayari nimewasiliana na hospitali ya magonjwa ya akili. Watatuma gari kumchukua Alvin.” Lea alipigwa na butwaa.
Lisa alimkazia macho. “Nani alikuambia upige simu hiyo?”
Jack alisema kwa ukali, “Kama hatutampeleka kwa matibabu, kwa hali yake ya sasa, je, unatfikiri ataishije na watu?”
“Yuko sahihi. Alvin alikuwa katika hali ya kutisha sana sasa hivi.” Mason alishika mikono ya Lea na kusema kwa woga, “Niliogopa sana. Bado kidogo tu angekusukuma chini. Ni Lea wakati huu, lakini ugonjwa wake utakapomrudia, nani atafuata?”
Aliongea kwa kusitasita, lakini Lea alimwelewa na kumuunga mkono. “Ni bora kumpeleka hospitali kwa matibabu. Siyo jambo geni, hata zamani aliwahi kutibiwa pia…”
Lisa hakutaka kusikia tena. “Si umesikia alichosema Alvin sasa hivi? Ukweli kwamba ulimdanganya na kumpeleka hospitali ya magonjwa ya akili siku za nyuma tayari umeacha kovu juu yake. Kama mama, unajua kipi kingine cha kumsaidia zaidi ya kumsukumia hospitali? Hustahili kuwa mama hata kidogo.” Aibu na haya vilitanda kwenye uso wa Lea.
Jack alikunja uso na kuongea kwa hasira. "Unajua nini? Ikiwa hatutamfunga, ataumiza mtu mwingine tena. Anaweza hata kukuumiza wewe mwenyewe.”
“Hiyo ni juu yangu.” Lisa alihisi hasira kali kwa ajili ya Alvin. “Jack, ni rahisi kwako kusema hivi kwa sababu si wewe uliyekuwa umefungwa hospitalini. Tangu utotoni, umekuwa na upendo wa wazazi wako. Hata baada ya kukua, mama yako bado anafikiria njia nyingi za kukusaidia, na sasa anapanga kukukabidhi biashara na familia ya Kimaro mikononi mwako. Lakini vipi kuhusu Alvin? Kwanini alikua mgonjwa wa akili? Ni kwa sababu alikuwa amefungiwa kwenye chumba peke yake wakati nyinyi watatu mkiwa na familia yenye furaha. Wazazi wako walipokupeleka kusafiri kote ulimwenguni, Alvin alinyimwa chakula na joto kwa sababu ya unyanyasaji wa yaya wake. Ni sawa ikiwa mnahisi hamna hatia na hamna makosa hata kidogo, lakini je, mnaweza kumhurumia japo kwa muda mfupi tu?”
Jack alijihisi vibaya kutokana na kukemewa, na rangi zote zikatoka usoni mwa Lea.
Lisa alidhihaki, "Hata uliniambia mwanzo kwamba mimi na Alvin tuna hatima sawa. Inafurahisha sasa ninapofikiria juu yake. Wewe ni mroho usiyetosheka. Una kila kitu lakini bado ulitaka kunyakua KIM International ambayo ilikuwa kitu pekee ambacho Alvin alikuwa nacho. Alipata tu mapenzi kutoka kwa familia ya Kimaro kupitia msaada wa KIM International. Anawajali ninyi, lakini ninyi ni kundi la watu mnaomuumiza kila mara.”
“Umemaliza kututukana?” Jack aliuma meno na kukunja ngumi kwa hasira.
Lisa akawatupia jicho la chuki. “Kuhusu ugonjwa wa akili wa Alvin kufichuliwa, hakuna mtu mwingine anayeweza kuwa nyuma ya hili isipokuwa nyie familia ya Kimaro. Tutawafanya mlipe deni hili."
Alimtazama Chester baada ya kumaliza kuongea. “Hebu mchukue Alvin tuondoke.”
Chester alimtazama Lisa kwa kumshangaa na kutikisa kichwa. Akambeba Alvin na kushuka chini.
“Nyie…” Jack alitaka kuwafuata, lakini Lea akamvuta nyuma. Akatikisa kichwa chake na kumwambia. “Achana nao…”
Mason alikuwa na hali ya wasiwasi. “Lakini…”
“Ninapaswa kuwajibika kwa ugonjwa wa Alvin.” Lea alikuwa na hisia tofauti. Alikuwa hajapenda kuwepo kwa Alvin muda wote. Ilikuwa ni kwa sababu yake ilimbidi aolewe na mtu ambaye hakumpenda. Mara ya mwisho alipohisi hatia kwa Alvin ni wakati ugonjwa wake ulipomshika alipokuwa na umri wa miaka minane.Lakini, wakati huo, Lea alikuwa na kazi yake, familia yake, na Jack wa kumlea, akampeleka Alvin akalelewe hospitali ya vichaa. Hatimaye Alvin alirudi baada ya kukaa katika hospitali ya wagonjwa wa akili kwa miaka michache na tayari alipata nafuu. Aligeuka kuwa mwenye hasira na mkatili baada ya kupona, na kumfanya azidi kumdharau.
Tukio lililotokea siku hiyo lilimfanya Lea akumbuke baadhi ya mambo ya muda mrefu uliopita. Alikuwa amemwachia Alvin majeraha mengi. Hakika alidharau uwepo wa Alvin, lakini Alvin alimchukia kwa kumzaa pia.
“Jack, ngoja nikuulize hivi, Wewe ndiye uliyesambaza picha hizo?” Lea alikunja uso na kuuliza, “Mkutano wa wanahabari na kampuni ya Alvinarah kuhusu cement yao mpya unafanyika kesho. Bila shaka picha hizi zimetolewa makusudi ili kuvuruga tukio hilo. Mtu anayeshukiwa zaidi katika familia ya Kimaro ni mam’dogo wako, na anayefuata ni wewe."
"Mama, mimi sikufanya." Jack alikasirika. "Hata iweje, bado nina uhusiano naye wa damu. Alikuwa mgonjwa tangu mwanzo, na hata iweje nisingefikia hatua ya kumdhalilisha kwa kutumia ugonjwa wake.”
Lea alipapasa paji la uso wake. Alikuwa anaumwa na kichwa. Alijua mtoto wake alikuwa na utu gani. Je, ni kweli Valerie ndiye aliyefanya hivyo?
"Mama, baada ya hili la Alvin, katika hali hii, mkutano wa waandishi wa habari wa kesho bado unaweza kufanywa?" Jack aliuliza kwa kusitasita.
Lea alimkazia macho na kuondoka zake. Alikuwa anaenda kumfuata Valerie.
•••
Chester alimpeleka Alvin moja kwa moja hadi kwenye hospitali binafsi kwa ajili ya kumfanyia uchunguzi na kumtwisha dripu iliyokuwa na dawa za kutuliza. Wakiwa wodini, Lisa alimshika mkono Alvin kimyakimya.
Aliona tu upande wake wa kiburi, jeuri, na ukatili katika siku za nyuma. Siku hiyo, alikuwa ameona upande wake dhaifu. Moyo wake bado ulimuuma.
"Kusema kweli, nilipojua kwa mara ya kwanza kwamba wewe na Alvin mmekutana, nilifikiri kuwa haukuwa mzuri kwake." Chester alitabasamu. “Lakini sasa, ninaona aibu kuwa na mawazo hayo. Unastahili kuthaminiwa na Alvin.”
Lisa hakushangaa. Alvin na marafiki zake walikuwa ni watu ambao walikuwa wamesimama juu ya ufahari wa Kenya, kwa hiyo ilikuwa kawaida kwamba wangemdharau. Aliachana na mada hiyo na kumuuliza swali tofauti. "Dokta Choka, unaweza kuniambia jinsi Alvin alivyopata jeraha kwenye mkono wake sasa?"
Chester alitabasamu kwa uchungu. "Unaweza kuwa umekisia tayari, lakini ndio, wakati wowote Alvin anapokaribia kushindwa kuthibiti hasira zake, huwa anajikata kwa kisu. Ilitokea mara mbili, na mara zote mbili zilihusiana na wewe." Lisa alishtuka. Aliinua kichwa na kumtazama.
"Mara ya kwanza uligombana naye asubuhi. Baada ya kuondoka alijiumiza ndani ya gari. Mara ya pili ilikuwa njiani kuja hospitali baada ya kukuokoa kutoka kwenye jela ya familia ya Kimaro.”
Lisa alikumbuka hili. Asubuhi hiyo, alisema kuwa hampendi na kisha akaondoka kwa hasira. Kwa mara ya pili, ghafla alisema kwamba anataka kutoka kwenye gari. Alidhani alichukizwa na harufu ya uvundo kwenye mwili wake. Kumbe aliondoka kwenda kujiumiza mwenyewe. Alijuta sana.
"Wewe na Lea ndio watu pekee mnaoweza kumfanya ashindwe kujidhibiti kwa sababu anawajali ninyi wawili." Chester alimtazama na kumwambia moja kwa moja.
Moyo wa Lisa ulitetemeka. “Nitamsaidiaje?”
"Kaa naye," Chester alisema, "Hawezi kufanya kazi katika hali hii sasa. Alvin ana jumba lake Mombasa kando ya bahari. Napendekeza nyie mngeenda huko. Fuatana naye ili kupata hewa safi na kumpa joto na upendo.”
“Sawa.” Lisa aliitikia bila kuchelewa.
“Naamini hutamchukua tena baada ya kuujua ukweli wake.” Chester aliinua macho yake kwa udadisi. “Si uliendelea kumlaumu kwa kutumia mbinu za siri kuwatenganisha wewe na Kelvin? Na Alvin alichangia pia kwa wewe kuharibika sura?"
Sura ya: 227
Lisa alihisi uchungu. "Ndio, ilikuwa ni lazima nimchukie. Nilipaswa kumchukia kwa kutoniamini huko Dar es Salaam, kwa kunidhalilisha tena na tena, na kwa kuniumiza. Baada ya kusema hivyo, sikuweza kujizuia kuwa na wasiwasi juu yake nilipogundua kwamba kuna jambo lililompata. Niliumia sana kufahamu kuhusu maisha yake magumu ya utotoni. Nilijidanganya kwa kuamini kwamba nimeacha kuwa na hisia naye, lakini siwezi kuudanganya moyo wangu. Kadiri ninavyoelewana naye, ndivyo ninavyozidi kumpenda.”
Alimtazama kwa upendo yule mtu aliyekuwa amepoteza fahamu pale kitandani. Aliamua kuacha yaliyopita yawe yamepita. Kuanzia siku hiyo na kuendelea, alitaka kuwa mzuri kwake. Sasa Joel alikuwa hajitambui kitandani, Alvin ndiye alikuwa mwanafamilia pekee aliyebaki kwake, ilibidi amthamini kwa kila hali.
Chester alifurahishwa na hali hiyo, lakini Hans aliyekuwa kando yake alionekana kuwa na wasiwasi. "Ikiwa Bwana Kimaro hawezi kufanya kazi, mkutano wa waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa cement mpya utafanyika vipi? Zaidi ya hayo, habari kuhusu hali ya akili ya Bwana Kimaro inaenea kama moto wa nyika. Ni lazima tupunguze zogo.”
Lisa alipigwa na butwaa. "Je, hakuna mtu mwingine yeyote anayeweza kuchukua jukumu la kampuni ya Alvinarah wakati kama huu?"
"Kunao, lakini tayari imetangazwa kuwa Bwana Alvin Kimaro ndiye atakayehudhuria mkutano huo. Ninahofia kwamba kutokuwepo kwake kwa dharura kutasababisha ghasia na kuathiri vibaya maendeleo ya Alvinarah ya siku za usoni.”
Lisa alikunja uso na kufikiria kwa nusu dakika kabla ya kusimama ghafla. “Nitahudhuria kwa niaba yake. Kama mke wake, nitawajibika kwa hilo.”
Hans na Chester wote walishangaa. "Lakini hakika kutakuwa na wanahabari wengi watakaokuuliza maswali kuhusu hali ya Bwana Mkubwa Kimaro wakati wa mkutano huo..."
'”Nitajibu maswali ya waandishi." Lisa alielekeza macho yake makali kwa Hans. “Nisaidie kukusanya taarifa. Nataka umma ujue kuwa Alvin si kichaa.”
Hans aliyekuwa anatetemeka ghafla aliguswa na ujasiri wake. Angalau kulikuwa na mtu ambaye alimjali bosi wake katika maisha yake.
Siku iliyofuata, Jumba la Alvin lililokuwa huko Mombasa likitazamana na Bahari ya Hindi, lilivamiwa na wageni wa ghafla. Vuli ilikuwa imefika na maua yalikuwa yamechanua kabisa.
Baada ya kupoteza fahamu kwa usiku mmoja, Alvin aliyekuwa kitandani alifumbua macho na kuketi. Kwa kasi alikimbilia mlangoni bila kuvaa nguo zake. Hapo hapo mlango ukasukumwa. Hans aliingia ndani huku akionekana kushangaa. “Umeamka, bosi…”
Alvin alimsukuma na kuelekea chini. Baada ya kuangaza-angaza, alimvuta Hans kwenye shati lake kwa macho yenye muwako wa damu. "Yuko wapi? Ameenda wapi?”
Hans akapata fahamu. "Bi Jones -"
"Aliondoka, sivyo?" Alvin akamkatisha sentensi yake na kuunguruma, “Amenidanganya! Aliahidi kukaa karibu nami wakati wa matibabu yangu na kuniandalia nyama choma ya nguruwe. Wote ni uongo.”
"Bwana Mkubwa, umemwelewa vibaya." Akihofia kwamba Alvin angeshindwa kujidhibiti tena, Hans mara moja alisema, "Bi Mdogo ameenda kuhudhuria mkutano wa waandishi wa habari na Alvinarah kwa niaba yako."
"Nini?" Alvin alikodoa macho.
"Dokta Choka alisema kuwa hautoweza kutoka nje, lakini kashfa nyingi zaidi kuhusu wewe zinaenea huko na ni ngumu kuzizuia. Waandishi hao tayari wamejazana kwenye ukumbi wa mkutano tangu jana usiku. Kwa sababu hiyo, Bi Jones aliamua kuhudhuria mkutano huo badala yako na kwenda kufafanua kuhusu hali yako pia.”
Alvin alimtazama Hans kwa hasira. "Je, viongozi wa juu wa kampuni wamekufa? Pia, unawezaje kumruhusu ashughulike na wanahabari hao wakatili? Hapana, hawezi kushughulikia. Lazima niharakishe huko…”
“Bwana Mkubwa, huwezi kwenda huko.” Hans akamzuia.
"Niondokee. Wewe ni msaidizi wangu tu. Unathubutuje kunizuia?!" Alvin alipandwa na hasira.
"Hans anakuzuia kwa faida yako mwenyewe." Chester aliingia ghafla. Hakuwahi kuwa mkali hivi hapo awali. “Jiangalie. Unajua wazi kwamba waandishi watakuuliza maswali ya kutisha, una uhakika 100% kwamba hutaathiriwa na maswali yao na hutapoteza udhibiti?"
Koo la Alvin likakaza, na vidole vyake vitano vilijikunja na kuwa ngumi.
Chester aliendelea kusema, "Ugonjwa wako ukitokea mbele ya kamera, Alvinarah itakuwa imetupwa majini na maisha yako yatakwisha."
"Acha kunitisha!" Macho ya Alvin yalimtoka kwa huzuni.
“Uwe na imani na Lisa. Yeye si dhaifu kiasi hicho.” Chester akatoa simu yake na kubofya programu iliyokuwa ikitangaza mkutano huo moja kwa moja. "Sasa, wacha tuone jinsi anavyofanya."
Mtiririko wa moja kwa moja wa matukio ya mkutano wa kampuni ya Alvinarah na waandishi wa habari uliofanyika usiku huo ulipata watazamaji zaidi ya milioni moja kutoka ndani na nje ya Kenya. Lisa akiwa amevalia gauni jeusi alikuwa akitoa hotuba jukwaani.
Ilikuwa ni mara ya kwanza kuonekana hadharani kama mke wa Alvin.
Wale ambao hawakuwahi kumuona walikuwa wakidhani kwamba alikuwa mrembo mkubwa, ikizingatiwa kwamba Alvin Kimaro, tajiri mkubwa zaidi nchini Kenya alimpenda sana. Lakini, dakika ambayo alionekana hadharani, kila mtu alipigwa na butwaa.
Alvin hata aligundua kuwa watazamaji wengi waliendelea kujaza ukurasa wa maoni.
[Inawezaje kuwa yeye? She's so ugly.]
[Damn! Nini kilitokea kwa uso wake? Ni mbaya sana.]
[Je, inawezekana kwamba kuna kitu kilienda vibaya kwa macho ya Bwana Kimaro tangu alipokuwa na ugonjwa wa akili?]
Akiwa ameshtuka, Chester alifunga mara moja ukurasa wa maoni.
Hata hivyo, Alvin tayari alishaona maoni hayo na kulipuka kwa hasira.
“Hawa watu wamerukwa na akili nini? Je, wana nia ya kutazama mkutano au wanawake warembo?”
Kwa kujisikia vibaya, Hans alibadilisha mada haraka. “Bwana Kimaro, tazama. Bi. Jones ameanza kuongea. Ana sauti ya mamlaka na ushawishi.”
Alvin alimkazia macho. Hakuhitaji Hans kumkumbusha kwani aliweza kuona kwa macho yake. Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kumuona Lisa akiwa amesimama mbele ya waandishi wa habari. Mkutano wa usiku huo ulikuwa umevuta hisia za makampuni mengi ya ndani na nje ya Kenya.
Wakati wa mkutano huo kuanza, Lisa aliinua kipaza sauti kwa utulivu. Aligonga kipaza sauti ili kukijaribu kabla ya kuanza kuzungumza, “Habarini nyote. Mimi ni mke wa Alvin Kimaro, Lisa Jones. Niko hapa kukaribisha mkutano na waandishi wa habari kuhusu Alvinarah's Oceanic Cement. Hii ni brand ya kwanza ya cement bora zaidi zinazozalishwa nchini Kenya. Mwanzilishi wa cement hiyo, Alvin Kimaro, alipaswa kutambulisha bidhaa hiyo ana kwa ana, lakini Bw. Kimaro hakuweza kuja kwa sababu za kibinafsi—”
Kabla hajamaliza kuzungumza, ripota kutoka Nairobi Financial Times alikatiza hotuba yake, “Je! ni kwa sababu ugonjwa wake wa akili umemshika tena? Ni kweli alimuua yaya aliyekuwa akimtunza tangu akiwa mdogo? Si lazima aende jela baada ya kumuua kwa sababu ya kosa la jinai, sivyo? Au ni kwa sababu ya hadhi yake ya juu ndiyo maana hajafungwa?”
Mara baada ya ripota huyo kuanzisha somo, waandishi wengine wengi walianza kumuuliza maswali mfululizo juu ya Alvin.
"Tulisikia kwamba ambulensi kutoka hospitali ya wagonjwa wa akili ilikwenda nyumbani kwa mama yake jana. Ugonjwa wake ulianza tena?"
“Mbona bado hajapelekwa hospitali ya magonjwa ya akili? Je, kama ataumiza wengine wakati ujao?”
"Je, watu wenye matatizo ya akili kama yeye wanaweza kuiongoza vizuri Alvinarah? Je, kunaweza kuwa na tatizo na cement?"
“Sasa unaishi na Alvin huogopi? Amewahi kukuumiza?”
"Sio tu kwamba kuna tatizo kwenye akili ya Alvin, lakini pia ana matatizo ya macho pia . Vinginevyo, kwanini alikuchagua wewe kuwa mke wake?”
Lisa aliulizwa maswali mengi mabaya kutoka kwa waandishi wa habari waliokuwa chini ya jukwaa. Mimuliko ya mara kwa mara ya kamera iliumiza macho yake pia. Hata hivyo, aliendelea kuvaa tabasamu la upole na la adabu. Dakika tano baadaye, waandishi walikuwa wamechoka kuuliza maswali. Walipoanza kunyamaza, Lisa alifungua mdomo wake. “Mmemaliza kuuliza maswali?”........ ITAENDELEA.....
Unafikiri nini kitafuata hapo, maana simulizi inazidi kuwa tamu kila siku lakini sina budi kuhitimisha kipande hiki ila niwasihi tukutane katika episode zijazo ili kujua nini kitafuata kwenye mkasa huu wa kusisimua na kuelimisha unaokwenda kwa jina la LISA
